Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

STAND UNITED WAFANYA ZIARA KUONA CHAMPIONI LINAVYOANDALIWA

$
0
0

PICHA YA PAMOJA YA WAFANYAKAZI WA CHAMPIONI NA WALE WA STAND UNITED WALIPOTEMBELEA KWENYE OFISI ZA GLOBAL PUBLISHERS, BAMAGA JIJINI DAR NA KUJIFUNZA NAMNA GAZETI HILO LINAVYOANDALIWA. STAND WANAODHAMINIWA NA MATAIRI YA VEE RUBBER KUTOKA KAMPUNI YA BIN SLUM WAKO JIJINI DAR KUWAVAA SIMBA KESHO KWENYE UWANJA WA TAIFA.

SIFAEL PAUL 'BABA IJUMAA WIKIENDA' (KULIA) AKIFAFANUA JAMBO HUKU AKISIKILIZWA NA MWANDISHI WA CHAMPIONI, MARTHA MBONA NA WACHEZAJI NA VIONGOZI WA STAND UNITED.

WAANDISHI WA CHAMPIONI WAKITAMBULISHWA NA MHARIRI WA CHAMPIONI JUMATANO, PHILLIP NKINI.

MKUU WA KITENGO CHA IT CHA GLOBAL PUBLISHERS, CLARENCE MULISA MAARUFU KAMA KIGOGO AKIFAFANUA JAMBO.

BOSI MTOTO, ERICK EVARIST NAYE AKIFAFANUA JAMBO KWA WAGENI WAKE.


KOCHA WA STANDA, MASSAWE (KUSHOTO) AKIZUNGUMZA NA BOSI MKUBWA WA CHAMPIONI, SALEH ALLY. 


MWANDISHI MARTHA MBOMA AKIFAFANUA JAMBO HUKU MTAALAMU WA IT, NICO 'INJINIA' AKIFAFANUA JAMBO.

MHARIRI WA CHAMPIONI JUMAMOSI, SHABANI MBEGU AKIFAFANUA JAMBO.


MHARIRI WA CHAMPIONI JUMATANO, PHILLIP NKINI AKIWATAMBULISHA STAND KWA MHARIRI WA CHAMPIONI JUMATATU, EZEKIEL KITULA. 'EEEHH' .

KOCHA MSAIDIZI, BILLO, MKURUGENZI WA UFUNDI KANU NA DAKTARI, CHUMA WA STAND UNITED WAKILISOMA GAZETI LA CHAMPIONI.

KUMBE ARSENAL ILIMKOSA MESSI SABABU YA SUALA LA UHAMIAJI

$
0
0
MESSI (ALIYEVAA KINYAGO) AKIWA KWENYE KIKOSI CHA WATOTO CHA BARCELONA PAMOJA NA GERRARD PIQUE NA CESC FABREGAS (WALIOZUNGUSHIWA DUARA).

Kocha Arsene Wenger amesema alifanya kila juhudi kumsajili mshambuliaji Lionel Messi akiwa na umri wa miaka 16.

Anasema makubaliano na Barcelona yalikuwa safi kabisa, lakini tatizo likawa ni uhamiaji.
Uhamiaji ya England iliweka ugumu, hiyo ilikuwa mwaka 2003.
Hali hiyo ilitokana na Messi kutokuwa na uraia wan chi yoyote ya Ulaya. Hali hiyo ikasumbua kibali cha kufanyia kazi nchini England licha ya kwamba alikuwa tayari kwenda kufanya kazi London.
Mwaka 2006, Messi ndiye akawa raia wa Hispania, huenda ingekuwa lahisi kwake kujiunga na Arseb,nal.

Wakati huo, Messi alikuwa kwenye kikosi cha vijana pamoja na Cesc Fabregas na Gerard Pique.

A JOURNALIST IS BACK (MWANDISHI AMERUDI) - 09

$
0
0






Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

Mchanga mwingi wa ufukweni ndio ambao ulimfanya kutokukimbia kwa kasi. Mbwa watano walizidi kumsogelea zaidi na zaidi, ni umbali wa hatua kumi tu ndizo ambazo walikuwa wamebakiza kabla ya kumkamata Dominik ambaye alionekana kuchoka kutokana na mchanga mwingi uliokuwa pale ufukweni ambao ulimfanya kutokumbia kwa kasi.
“Kama kunikamata…acha tu wanikamate…sina ujanja” Dominick alijisemea huku kasi yake ikianza kupungua Tayari alikuwa amekwishakata tamaa kabisa. Aikuwa tayari kukamatwa na mbwa wale, kuumwa na hatimae mtu yule aliyemmulika tochi kumfikia.
                                                               *******
Walinzi  wanne walikuwa wakiendelea na ulinzi katika nyumba ya balozi wa Marekani Bwana Brown Poll. Mbwa wakali ambao walikuwa wamepewa mafunzo ya kutoshwa walikuwa mikononi mwao, tochi pamoja na bunduki zilikuwa mikonon mwao.

Wawili walikuwa wakizunguka zunguka katika eneo la nyumba lile huku wengine wakiwa getini wakipiga stori lakini huku wakiwa makini kwa kila kitu ambacho kingeweza kutokea mahali hapo. Huku wakiwa katika maongezi yao, gari moja aina ya VX likapita kwa kasi mahali hapo kiasi ambacho kila mtu akabaki akishangaa.
Mbwa wakaanza kubweka kuashiria kitu cha hatari kilikuwa kinakwenda kutoke. Walinzi wote wakaonekana kupuuzia, wakabaki wakiendelea na stori zao. Wala hazikupita dakika nyingi, moto mkali ukaanza kuonekana kwa mbali.
Wote wakaonekana kushtuka. Moto ule ukaonekana kuwashtua kupita kiasi. Kwanza ilikuwa usiku sana kukutana na kitu kama kile. Kule baharini hakukuwa na mtu yeyote katika kipindi kile, sasa kwa nini kulikuwa na mwanga mkali wa moto.
Wakaandaa tochi zao na kuanza kusogea kule huku wakikimbia. Tayari walikwishaona kulikuwa na hatari ambayo ilisababisha moto ule kuwaka, walitaka kutoa msaada wa haraka katika kuuzima kutokana na maji kuwa karibu.
Kwa mbali wakaanza kumuona mtu akiwa amesimama pembeni, mlinzi mmoja akammulika kwa tochi aliyokuwa nayo, mara Dominick akaanza kukimbia hali ambayo iliwafanya kuwaachia mbwa wote watano waliokuwa nao mikononi kumkimbiza Dominick.
“Shiiiikaaaaa…shiiiiikaaaaa……” Mlinzi mmoja alisikika na kisha mbwa wale kuanza kumkimbiza Dominick ambaye akaanza kukimbia.
“Kumbe ni gari. Mungu wangu…!” Mlinzi mmoja alisema huku akishangaa.
Hawakutaka kuliona gari lile likizidi kuteketea, wakaanza kuchukua maji kutoka baharini kwa kutumia madumu mawili ambayo yalikuwepo mahali pale na kujaribu kulizima gari lile. Kazi haikuwa rahisi kabisa, kadri upepo ulivyozidi kuvuma na ndivyo ambavyo mot ule ulivyozidi kuchochewa.

Mpaka moto unazimika, tayari gari lile lilikuwa limeteketea kwa ailimia kubwa. Wakasubiri kwanza mpaka bati lipoe na ndipo wakaingia ndani. Miili miwili ndio ambayo ilikuwa imepatikana huku ikiwa imeteketezwa vibaya na moto ule ambao ulikuwa umeteketeza gari lile.
“Wewe si unajua kidogo kizungu..nenda kule waamshe watoto wa bosi waje huku kutoa msaada” Mlinzi mmoja alimwambia mwenzake ambaye akaanza kuondoka mahali hapo na kuelekea katika nyumba ile ya balozi wa Marekani.
Mara baada ya kufika kule, mlinzi akaanza kuugonga mlango ambako baada ya muda mtoto mmoja wa balozi akatokea na kisha kuanza kumuelezea kile ambacho kilikuwa kimetokea ufukweni. Kwa haraka sana kijana yule akachukua gari pamoja na yule mlanzi na kuanza kuelekea kule katika ufukwe.
Mara baada ya kuitoa miili ile, wakaipakiza katika gari lile na safari ya kuelekea hospitalini kuanza. Miili ilikuwa imeteketea vibaya kiasi ambacho ilikuwa ni vigumu kumjua huyu ni nani na yule ni nani.
“Mbwa wako wapi?” Mlinzi mmoja kati ya wale waliobaki aliuliza.
“Kumbe bado hawajarudi? Ebu twende tukaangalie, watakuwa wamemkamata na kuanza kumshambulia kiasi ambacho wamejisahau kurudi” Mlinzi mwingine alimwambia mwenzake huku wakianza kuelekea kule Dominick alipokimbizwa na mbwa.
                                                             ********
Kijasho kilikuwa kikimtoka, alikuwa akikimbia kwa mwendo wa kasi kuifuata taksi moja ambayo ilikuwa katika eneo la hospitali ya taifa. Mara baada ya kuchukua taksi na kulipia gharama zote, safari ya kuelekea huko alipookuwa akitaka kuelekea kuanza.
Mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda mbio kutokana na kitu ambacho alikuwa amekiona. Aliliona gari likiendeshwa taratibu sana kiasi ambacho alimwambia dereva aendeshe kwa mwendo wa kasi. Bado moyo wake ulikuwa na hamu moja ya kufikisha taarifa juu ya kile ambacho alikuwa amekiona.
Taksi ikapaki katika eneo la kupakia magari ya klabu ya usiku ya Rapinho. Kwa haraka haraka kijana yule akateremka na kuanza kuelekea ndani ya klabu ile. Akaanza kumtafuta baunsa ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni kulinda usalama katika klabu ile.
“Vipi tena Steve?” Dickson aliuliza huku akimwangalia Steve ambaye alikuwa akionekana kuwa na kiu ambacho alitaka kumwambia.
“Nimetokea Muhimbili” Steve alimwambia Dickson.
“Kwa hiyo?”
“Nimekutana na kitu ambacho kimenishtua sana” Steve alimwambia Dickson ambaye nae akaonekana kushtuka.
“Kitu gani tena?”
Steve hakujibu kitu, akabaki kimya kwa muda, akaanza kuyapeleka macho yake huku na kule hali ambayo ilionyesha kama alikuwa akimtafuta mtu fulani mahali pale. Alipoona hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akimtafuta, akayarudisha macho yake usoni mwa Dickson.
“Mama yuko wapi?”
“Mama gani?”
“Mke wa Mheshimiwa”
“Kama kawaida yake, kuna kijana kutoka Tanga alikuja mahali hapa, wakatamaniana, akaondoka nae” Dickson alimwamba Steve ambaye akaonekana kushtuka.
“Na binti yake?”
“Nani? Sara? Nae amemfuata alipokwenda” Dickson alijibu.
Steve akaonekana kushtuka zaidi. Mwili wote ukamlegea, us wake ukaonekana kujawa na majonzi. Dickson akaonekana kuhisi kitu, hali aliyokuwa ameionyesha Steve mbele yake tayari ikaonekana kumpa wasiwasi na kuona kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kimetokea.
Steve akaanza kupiga hatua kuelekea katika kaunta na kutulia. Bado alionekana kuwa na huzuni usoni mwake. Dickson akaanza kumfuata, tayari nae akahisi kwamba kulikuwa na kitu kimetokea ambacho Steve hakutaka kukiongea.
“Kuna nini lakini?”
“Ajali. Ajali ya moto” Steve alimwambia Dickson.
“Nyumba imeungua?”
“Hapana. Nafikiri mke wa mheshimiwa alichomwa moto pamoja na binti yake” Steve alimwambia Dickson.
Dickson akahisi mwili wake ukianza kupoteza nguvu, magoti yake yakalainika kiasi ambacho kikamfanya kuchuchumaa. Hakuamini kutokana na maneno ambayo alikuwa ameyasikia kutoka kwa Steve, akamwangalia mara mbili mbili huku akionekana kutokumuamini kabisa.
“Umesemaje?” Dickson aliuliza huku akionekana kutokuamini kibisa.
“Ndio hivyo”
“Umejuaje kama ni wao?”Dickson aliuliza.
“Nilikuwa hospitalini pale kumpeleka mke wangu, si unajua anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo, wakati nimemfikisha na kuanza kuondoka, nikakuta gari moja likiingia, nafikiri ni la balozi fulani kwani hata namba zake zilikuwa si za raia wa kawaida” Steve alimwambia Dickson an kuendelea.
“Nikaonekana kuvutiwa kuangalia ni mtu gani ambaye angeteremka, mara mzungu mmoja na kijana mwingine mweusi wakateremka na machela kuletwa haraka haraka. Miili ya watu wawili iliyoonekana kuungua vibaya na moto ikateremshwa. Nikaiangalia vizuri. Nikamgundua Sara kwa kuwa sura yake haikuwa imeungua sana, lakini kwa Bi Magdalena, sijui kama utaweza kumjua kama ukionyeshewa” Steve alimwambia Dickson.
Dickson akachoka zaidi na zaidi. Steve akaanza kuwaambia na watu wengine juu ya tkio lile hali ambayo ikawafanya watu wengi kutoka nje ya ukumbi kuona kama gari lake lao lilikuwa mahali pale. Gari halikuwepo, kila mmoja akajua kwamba kile ambacho alikuwa amekiongea Steve kilikuwa na ukweli.
Kila mtu mahali pale akaanza kuongea lake, kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo idadi ya watu ikazidi kuongezeka zaidi na zaidi. Kila mtu alikuwa akionyesha kuhuzunika, taarifa ile ilionekana kumshtua kila mtu, hakukuonekana kuwa na haja ya kurudi ndani ya klabu na kuburudika.
Wala hazikupita dakika nyingi, mzee akafika mahali hapo, akateremka kutoka garini na kuanza kuwafuata watu wale waliokusanyika huku uso wake ukionekana kuwa na mashaka.
“Kuna nini jamani” Mzee Ombeni aliuliza huku akionekana kuwa na wasiwasi.
                                                                           *********
   Dominick alikuwa amechoka kupita kiasi, alibaki akiwa amesimama tu huku akiwasubiria mbwa ambao walikuwa wakimfuata kwa kasi huku wakibweka. Ghafla, akili ikamjia kichwani mwake. Akaanza kuiangalia bahari ambayo ilkuwa imetawaliwa na mawimbi mengi makubwa.
 Akili ambayo ilimjia kwa wakati huo ni kukimbilia na kwenda kujiingiza katika bahari ile. Wala hakutaka kuchelewa, moja kwa moja akaanza kukimbia tena kuifuata bahari ile na kuingia. Kutokana na mawimbi makubwa ambayo yalikuwepo baharini, mbwa wale wakashindwa kuingia, wakabaki pembezoni mwa bahari huku wakiendelea kubweka.
 Walinzi wa nyumba ya barozi wakafika mahali pale, wakawaona mbwa wao wakiendelea kubweka huku wakiangalia baharini hali iliyowafanya kujua kwamba mtu ambaye walikuwa wakimkimbiza alikuwa amekimbilia baharini. Wakajaribu kuangalia anglia baharini lakini hawakuona mtu yeyote.
Dominick alikuwa akiendelea kupiga mbizi kuelekea katika upande mwingine. Mawimbi makubwa ya bahari ile yalionekana kumchosha zaidi lakini hakutaka kuacha kupiga mbizi. Moyo wake ulikuwa na furaha kila alipofikiria kuwa tayari alikuwa ameiteketeza familia ya waziri Ombeni..
Alipiga mbizi na kutokea katika sehemu nyingine ya mbali. Akaanza kutoka na kuelekea katika barabara ambayo wala haikuwa na magari mengi katika muda huo. Akaangalia macho yake katika kila upande, akaziona bajaji kadhaa zikiwa zimepaki nje ya ukumbi wa sinema wa 3D Movie.
Akakodi bajaj moja na kuanza kurudi nayo hotelini, La Vista Inn. Muda wote Dominick alikuwa akionekana kuwa na furaha, alijiona kuwa shujaa kuliko hata mwanajeshi ambaye alikuwa ametoka kupigana vita na kushinda.
“Mmmmh! Mbona hela yenyewe imeloa broo?” Dereva wa bajaji aliuliza huku akiigeuza geuza noti ya shilingi elfu kumi aliyopewa.
“Si unajua nilitumbukia kwane bwawa la kuogelea. Ila usijali, chukua yote tu” Dominick aimwambia dereva ambaye alionekana kushukuru.
Dominick akaanza kupiga hatua kuelekea katika ngazi za hoteli ile ambako akapanda mpaka katika ghorofa aliyoitaka na kuanza kutembea hadi katika chumba chake. Akajilaza kitandani, uso wake ulikuwa ukionyesha tabasamu pana. Akachukua rimoti ya televisheni yake na kisha kuiwasha tv huku akiwa na hamu ya kutaka kuangalia kile ambacho kilikuwa kimeajili kwa wakati huo.
                                                                    *************
Mpelelezi Bugabu alikuwa akijiandaa kuanza kufanya kazi ambayo alikuwa amekabidhiwa na serikali ya kumtafuta muuaji ambaye alikuwa ameiteketeza familia ya waziri Boniface. Kitu cha kwanza ambacho alikifanya ni kwenda katika kituo cha polisi cha Osterybay nawa lengo la kutaka kuonana na Mrisho, dereva aliyekuwa akiendesha gari la waziri Boniface.
Kutokana na umaarufu wake pamoja na cheo chake, hakukuwa na polisi yeyote ambaye alimzuia, kwa haraka sana akapelekwa katika chumba cha mahojiano ambapo baada ya muda wa dakika chache, Mrisho akaletwa mahali hapo.
Hali ya afya yake ilikuwa imeanza kubadilika, muda wote alikuwa akionekana mpweke, unyonge ulionekana kumjaa. Akakaa kitini na kuanza kumwangalia mpelelezi Bugabu. Akili yake ikaanza kurudi nyuma huku akianza kufikiria kama alikwishawahi kumuona mtu huyo katika maisha yake, jibu alilolipata, lilikuwa ‘hapana’  
“Karibu” Bugabu alimkaribisha Mrisho mahali pale. Mrisho hakuongea kitu chochote kile, alibaki akimwangalia mpelelezi Bugabu huku akionekana kuchoshwa na maisha ya pale.
“Unataka nikusaidie nini?” Mrisho aliuliza.
“Nataka kumfahamu huyu muuaji. Najua utakuwa umemuona tu. Nataka uniambie huyu muuaji ni nani” Mpelelezi Bugabu alimuuliza Mrisho ambaye bado alikuwa akimwangalia Bugabu kwa macho yaliyokuwa na hasira.
“Simfahamu mtu huyu”
“Haumfahamu? Acha utani. Kwenye maelezo yako ulipoingia katika kituo hiki ulisema alikuteka garini, ukaenda nae mpaka kwako, sasa kwa nini unasema haumfahamu? Yaani hata rangi ya ngozi yake?” Bugabu aliuliza huku akionekana kuanza kupata hasira.
“Ningemfahamu vipi kama mtu mwenyewe muda wote alikuwa amevaa kofia? Toka aliponiteka mpaka kuniacha, hakuitoa kofia yake kichwani” Mrisho alimwambia Bugabu.
“Kwa hiyo haufahamu kitu chochote kile?”
“Sifahamu”
“Ila si alikuja na gari lake?”
“Ndio”
“Nalo pia haulifahamu?”
“Nalifahamu. Ilikuwa chesser mayai nyeusi”
“Namba za gari?”
“Nilichanganyikiwa sana kiasi ambacho sikuweza hata kuangalia namba za gari” Mrisho alimwambia Bugabu.
“Nashukuru kwa ushirikiano wako” Bugabu alimwambia.
Buganu akainuka kutoka kitini, hakuona kama Mrisho angeweza kumsaidia katika kile ambacho alikuwa akikihitaji kwa wakati huo. Akaondoka na moja kwa moja kuelekea nje ya kituo kile abako akachukua gari lake na kuanza kuelekea nyumbani kwake.
Hakujua aanze wapi, kazi kwake ilikuwa ikionekana kuwa rahisi katika kipindi cha nyuma lakini kwa wakati huo tayari akaanza kuiona ngumu. Ila pamoja na mambo hayo yote, hakutaka kukata tamaa, dhamira ya kutaka kumkamata muuaji ilikuwa ikiendelea kubaki moyoni mwake.
                                                              ***************
Mzee Ombeni hakuonekana kuamini kile ambacho alikuwa ameambiwa, hakuamini kabisa kama ndoto ile ambayo alikuwa ameiota kuhusiana nakuchomwa moto kwa familia yake ndicho ambacho kilikuwa kimetokea. Akanyong’onyea na kuchuchumaa chini.
Kila mtu akabaki akimwangalia mheshimiwa Ombeni kwa jinsi ambavyo alivyochanganyikiwa. Hakuamini kama kwa wakati huo alikuwa ameipoteza familia yake kama jinsi ambavyo Bwana Boniface alivyoipoteza familia yake. Mauaji ya kuteketezwa kwa moto ndio ambayo yalionekana kumchanganya zaidi.
Akainuka na kuanza kukimbia kulifuata gari lake ambalo alikuwa amelipaki katika maegesho ya magari mahali pale. Akapanda na moja kwa moja safari ya kuelekea katika hospitali ya Muhimbili kuanza. Muda wote alikuwa amechanganyikiwa, machozi yalikuwa yameanza kumtoka, hakuamini kama siku hiyo ndio ilikuwa siku ya kuipoteza familia yake.
Kutokana na namba za gari lake kuonyesha kwamba alikuwa mtu kubwa Serikalini, geti likafunguliwa na moja kwa moja kuliingiza gari ndani ya eneo la hospitali ile. Akatereka huku akionekana kuchanganyikiwa
“Mheshimiwa….” Aliisikia sauti ikimuita.
Akageuka nyuma, macho yake yakatua kwa daktari ambaye alikuwa amevaa koti refu jeupe huku akiwa na msichana ambaye alikuwa na gauni refu jeupe. Akaanza kupiga hatua kuwafuata watu hao.
“Niambie daktari” Bwana Ombeni alimwambia dokta hata kabla ya salamu.
“Nikuambie nini?”
“Kuhusu mke wangu na binti yangu”
“Njoo ofisini”
                                                              ************
   Muda wote Bwana Ombeni alikuwa akilia, hakuami kama kweli alikuwa ameipoteza familia yake. Maisha yake akayaona kuanza kubadilika, kuishi pasipo familia yake lilikuwa jambo ambalo hakuwahi kuliwaza katika maisha yake.
Kwenye msiba, muda wote alikuwa akilia tu kama mtoto, familia yake ilikuwa kila kitu maishani mwake. Akajiona kupoteza kitu cha maana sana katika maisha yake yaliybakia. Hakujua ni kitu gani ambacho angemfanya yule ambaye alikuwa amehusika katika kuiteketeza familia yake, moyo ulimuuma kupita kiasi.
Magazeti mitaani yalikuwa na habari juu ya mauaji hayo. Kila mtu aliyeisoma alibaki kuwa na mshangao. Wala haukupita hata muda mrefu tangu Bwana Boniface alipoondokewa na familia yake, tena kwa kuteketezwa na moto namna ile, tukio jingine lilikuwa limetokea.
Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akifahamu chanzo cha muuaji kuziteketeza familia hizo, tena kwa moto katika magari yao. Mapolisi walibaki wakiwa wamechaganyikiwa kupita kawaida. Mt ambaye alikuwa amevaa kofia kubwa aina ya Malboro ndiye ambaye alikuwa akihusishwa katika matukio yae.
Kila mtu alikuwa akijiuliza juu ya muuaji huyo ambaye alikuwa akipenda kuvaa kofia ya aina hiyo. Viongozi wengine wakaanza kupatwa na wasiwasi juu ya matukio hayo ambayo yalikuwa yametokea. Hakukuwa na kiongozi ambaye alikuwa akiishi kwa furaha, kila mmoja alikuwa akiishi kwa wasiwasi huku ulinzi wa familia yake ukizidi kuongezeka.
“Mmmmh! Au atakuwa Dominick?” Bwana Boniface alimuliza Bwana Tumaini.
“Hakuna. Yule kwa sasa ni maiti, amekwishazikwa muda mrefu uliopita”  Bwana Tumaini alijibu.
Hakukuwa na mt ambaye alikuwa akimfikiria Dominick kuhusika katika mauaji yale, bado kitendawili kilikuwa mioyoni mwao juu ya muuaji ambaye alikuwa ameziteketeza familia zile. Kila siku waandishi wa habari walikuwa wakitoa taarifa kuhusu matukio hayo ambayo yalionekana kuitikisa Serikali.
“Au vyama pinzani wanataka kuchukua majimbo yetu?” Bwana Boniface aliuliza.
“Hilo linawezekana. Si unajua kwa jinsi tunavyochukiwa! Ni lazima watakuwa wapinzani, katika hili yatupasa kujiandaa”  Bwana Tumaini alijibu.
                                                                    **************
Katika maisha yake hakuwahi kupata mtoto. Kila siku haya ndio yalikuwa maombi yake kwa Mungu, alitamani kupata mtoto katika maisha yake kuliko kitu chochote. Aliiona ndoa yake kutokukamilika kabisa, ni kweli alimpenda sana mumewe lakini tatizo lilikuwa mtoto.
Aliangaika kwenda sehemu zote lakini hakupata suluhisho la tatizo lake. Alibaki nyumbani akilia, mumewe ndiye alikuwa mtu ambaye alikuwa akimbembeleza kila siku. Alimtumaini Mungu kwa kuamini kwake Yeye hakuna ambacho kilishindikana.
Kila siku alikuwa akimuomba Mungu pamoja na mumewe lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote yale. Kwa kuwa mumewe alikuwa na fedha nyingi, wakaamua kusafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutafuta suluhisho lakini bado tatizo lilikuwa vilevile tu, mtoto hakupatikana.
Suala la kutokupata mtoto ndio likaonekana kuwa tatizo kubwa katika ndoa yao. Ingawa alikuwa ameridhiana na mumewe lakini tatizo kubwa lilikuwa kwa ndugu wa mume. Kila siku walikuwa wakiongea yao, kila siku malalamiko yalikuwa hayaishi nyumbani.
Maisha ya msichana Edith yakapoteza kitu muhimu sana katika maisha yake, furaha. Kila alipokuwa akiongea na mumewe, bado alikuwa akijiona kuumia kupita kiasi, alihitaji kuitwa mama, alihitaji kunyonyesha kama wanawake wengine walivyokuwa wakinyonyesha.
Kila alipokuwa akiondoka nyumbani asubuhi kuelekea kazini, basi alipokuwa amerudi, nyumba haikuwa na mabadiliko hata kidogo. Kama aliacha vitambaa vya makochi vikiwa makochini, alivikuta hivyo hivyo. Alitamani apate mtoto ambaye angeweza kuvirusharusha vitambaa vile na kuifanya nyumba kutokuwa na mvuto.
Kila siku ndoto zake zilikuwa ni kupata mtoto, hata mtoto mmoja kwake ilikuwa tosha kwani aliamini ni lazima angewanyamazisha ndugu ambao walikuwa wakiendelea kulalamika. Mumewe hakutaka kumuacha, kila siku alikuwa akiongea nae huku akimfariji, aliamini kila kitu kilichokuwa kinatokea, kilikuwa katika mipango ya Mungu.
Kilio kiliendelea kila siku, Mungu akakisikia kilio chake, Edith akapata ujauzito ambao ulionekana kuleta matumaini katika maisha yake. Furaha ilikuwa kubwa katika maisha yake. Mapenzi yakaongezeka katika familia hiyo, ndugu ambao kazi yao ilikuwa ni kulalamika kila siku wakawa wamefungwa midomo, hawakuwa na la kuongea.
Kila siku mumewe alikuwa akitumia kiasi kikubwa cha fedha kwa kununua vitu mbalimbali na kuvileta nyumbani kwa mkewe, Edith. Ndoto zake zilioekana kutimia, hasa kila alipokuwa akiliona tumbo la mkewe likizid kuongezeka kila siku.
“Ni mwanaume” Edith alimwambia mumewe katika kipindi ambacho walikuwa sebuleni.
“Mwanaume! Mungu wangu! Ataitwa Brian…ataitwa Brian” Mumewe alimwambia huku akiishika shika tumbo lile.
Furaha ilikuwa ikiongezeka kila siku, ujauzito ule ukaonekana kuleta furaha kubwa na mabadiliko makubwa maishani mwao. Mumewe akawa akirudi mapema tofauti na zamani. Hakutaka kuwa mbali na mkewe kwani aliona kwamba alikuwa akihitajika kuliko mtu yeyote kwa mwanamke huyo.
Huyu ndiye alikuwa Bwana Tumaini, mlengwa ambaye familia yake ilikuwa ikihitajika kuliko kitu kingine na Dominick. Taarifa za ujauzito wa mke wa waziri kijana zilipokuwa zikitolewa gazetini, kila mtu alijisikia kuwa na furaha lakini kwa Dominick hali ilikuwa ni tofauti kabisa, moyo wake ulikuwa ukitaka kumuua Edith kama kulipa kisasi kwa kile ambacho alifanyiwa na mawaziri hao.
Mipango yake ilikuwa ikiendelea kila siku. Akaifuatilia ratiba nzima ya muda ambao Edith alikuwa akitoka nyumbani na kuelekea kliniki. Ratiba nzima alikuwa nayo, hakujali kuhusu ujauzito ambao alikuwa nao,kitu ambacho alikuwa akikijali kwa wakati huo ni kumuua Edith, msichana ambaye wala hakuwahi kumuona hata kwa sura zaidi ya kumsikia katika vyombo mbalimbali vya habari akitangazwa.
“Ni lazima nimuue. Mumewe si aliiangamiza familia yangu! Na yeye ni lazima afe kwa ajili ya mumewe, ni lazima nilipe kisasi” Dominick alijisemea.
ITAENDELEA KESHOOOOOOOOO
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

USIKU WA KIGODORO - 9

$
0
0

Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

ILIPOISHIA: Alimwalia James kwa macho yaliyojaa furaha, akamkumbatia na kumsogeza kifuani pake kisha kuanza kumpa mabusu mfululizo.
SHUKA NAYO MWENYEWE…
“Mbona umeonekana kuwa na furaha ghafla, vipi kwani?” aliuliza James baada ya kumwona Lina akihema kwa nguvu na kumvutia kwake kumpa mabusu mfululizo…
“Hamna mume wangu jamani, siku hazilingani hata siku moja, nikoje kwani mume wangu?” Sasa Lina alipata hata muda wa kusema neno ‘mume wangu.’
“Uko happy ghafla.”
“Aaah jamani baby. Lina alizidi kumbusu James mpaka wakajikuta wamezama kwenye ulingo mwingine kabisa wa mahaba mazito juu ya kitanda.
Lina siku hiyo alimfanyia mambo makubwa ya kimapenzi James kama siku yao ya kwanza kukutana ilivyokuwa.
Kila hatua, Lina alihakikisha anatoa kilio cha mahaba huku akimsifia James kwamba ni mwanaume bora kwake licha ya kwamba alijua furaha yake inaweza kuwa ya muda mfupi kuliko kilio kitakachofuata mbele yake siku chache zijazo.
Lina alilala kwa furaha siku hiyo, usiku alipata hata muda wa kuchati na mumewe, Semi kwani James aliwahi kulala akijua ana safari ya kumpeleka stendi Lina asubuhi kwa safari ya kwao, Korogwe.
Kulikucha salama, Lina alijiandaa kwa safari, akapakizwa kwenye gari na James hadi Ubungo.
“Baby mpe pole sana mama, mwambie nampenda panapo majaliwa nitamuona siku moja na Mungu atamsaidia afya njema,” alisema James wakati Lina akijiandaa kupanda basi ndani ya stendi ya Ubungo.
Walipeana mabusu ya nguvu ndani, gari lilikuwa na vioo visivyoonwa ndani yaani ‘tintedi.’
Walipanda wote ndani ya basi baada ya kukata tiketi, Lina akakaa kwenye siti yake huku James akisimama pembeni akizidi kumwombea dua njema kwa safari yake. Baada ya dereva kuingia na kuingiza gia, James alimbusu Lina mbele za watu, akashuka.
Cha kwanza baada ya James kushuka, Lina aliingiza mkono kwenye mkoba wake na kutoa kitita cha pesa alizopewa na James kikiwa ndani ya bahasha. Alihesabu mpaka alipoweka kituo, tayari alishajua amepewa shilingi milioni moja na laki tano.
“Mh!” aliguna Lina, akaangalia juu ya gari kisha akawaangalia abiria wenzake na kuwaona hawana maana, maskini wakubwa.
Basi liliondoka Ubungo, likashika Barabara ya Morogoro na kusogelea mataa ya Ubungo. Mungu ibariki, taa zikaruhusu magari kupita, dereva alivusha gari na kuishika njia ya kwenda Kimara…
Ah! Konda samahani, mzigo niliokuwa nakwenda nao Korogwe nimeusahau nyumbani jamani,” alisema kwa sauti Lina huku akiwa ameshasimama na kutembea kwa kasi kuelekea mlango mkubwa.
Abiria wengine walimpa pole wengine walimshangaa kwa kuhoji iweje mtu asafari mpaka ndani ya basi kumbe anachokipeleka amekiacha nyumbani? Waliona ni usanii mtupu.
“Shusha konda, samahani sana,” alisema Lina.
Dereva akaweka gari pembeni maeneo ya Kimara-Rombo, Lina akashuka huku konda akimkazia macho kuamini kwamba huenda atadai nauli lakini wala!
Akiwa chini ya sasa, Lina aliangaza pembeni na kuona Bajaj…
“Tafadhali nipeleke Kijitonyama.”
Lina alipofika nyunbani kwake, yaani kwake na Semi, alizama ndani akiwa haamini kilichotokea. Alishika simu na kumtwangia Eg kumpa mkasa wote, Eg alishangaa sana. Hakuamini kile alichokuwa anasimuliwa na Lina.
“Sasa mpendwa wangu, ukimwambia umefika si atataka kuzungumza na mama?” aliuliza Eg.
“Nitamwambia hawezi kuongea kwani si nimemwambia mama anaumwa, sijasema anafanyiwa bethidei!”
“Hapo sawa. Kwa hiyo sasa upo nyumbani?”
“Nimejaa tele, nabadili nguo nakwenda kazini.”
Ghafla Lina akakumbuka kwamba, James huwa anakwenda sana kazini kwake na ndiko walikokutania, itakuaje akifika na kumkuta?
Alifikiria kutuma udhuru kwa mabosi wake lakini akaona kwamba ataonekana mvivu maana siku mbili tatu zilizopita alishatoa udhuru mwingine.
“Mh! Sasa itakuaje? Hapa mawili, nitoe udhuru au niende. Lakini nikienda akitokea James nimeumbuka,” alisema moyoni Lina.
Muda huohuo meseji ikaingia kwenye simu yake, akajua ni James lakini sivyo, alikuwa bosi wake…
“Lina hakikisha unafika kazini leo, kuna kazi nyingi sana zimelala. Usikose.”
Lina alijishika kichwani, akajikuna kidogo, akahema…
“Nahisi nimepatikana leo, sina ujanja. Miongoni mwa hizo kazi nyingi anazosema bosi ni pamoja na za James,” alisema moyoni Lina huku akikosa amani ya moyo.
Lina alibadili nguo, akaondoka kuelekea kazini. Ile anaingia tu ndani ya geti, James anapaki gari nje…
“Mungu wangu ndiyo mambo niliyoyakataa haya,” alisema Lina akikimbilia ndani, akaenda kuingia kwenye chumba cha kuchemshia chai ambako mchemsha chai alimshangaa…
“Lina vipi tena, unakimbizwa?”
“We acha tu! Naomba utoke, mfuatilie kaka mmoja anaingia, naamini atakuwa ameshika brifkesi, jua anaingia wapi, anatoka muda gani,” aliagiza Lina.
“Pole na kuumwa mama?”
“Aaa…santé saa…na.”
“Basi sawa mama, we pumzika tutawasiliana tena baadaye.”
“Ha…haya…aa.”
Lina aliipokea simu na kuangua kicheko ambapo mwanamke huyo naye aliungana naye kwa usanii walioufanya.
“Daa! Jamani! Ama kweli dunia tambara bovu,” alisema mama mpika chai…
“Umeona ee?”
“Nimeona Lina.”
“Sasa mama wewe utanisaidiaje katika hili?”
“Hili suala ni gumu sana mwanangu, tena gumu kwelikweli. Ila cha kufanya wewe kuwa muwazi kwa James, mwambie ukweli wako.”
“Hee! Si atanipeleka polisi?”
“Akupeleke polisi kwa kosa gani?”
“Nimemtapeli.”
“Sasa unadhani nini kitafuata katika maisha hayo ya kukwepakwepa, kujifichaficha? Kwanza unaelewa kuwa huyo James karibu kila baada ya siku mbili anakuja hapa ofisini…”
“Ndiyo hapo  sasa mama.”
“Ndiyo maana nimekwambia hivyo au we una mawazo gani Lina?”
Lina alitulia kidogo kisha akamkodolea macho mama mpika chai na kumwambia…
“Nimuue mmoja.”
“Eti?” alishtuka mama mpika chai.
“Bila hivyo hili suala haliwezi kumalizika kirahisi hata siku moja, mi najua.”
“Sasa unataka kumuua nani kati ya James na Semi?”
“Hapo ndipo penye mtihani mkubwa.”
“Mh! Lakini hilo wazo umelitoa wapi wewe binti?”
“Mimi mwenyewe nimewaza hivyo. Unajua hii ni kesi kama nitaamua kumuweka wazi James na ni kweli ndiye anayetakiwa kuwekwa wazi…”
“Basi kama ni hivyo hata kumuua muue yeye,” mpika chai alisema.
Lina alionekana kusita kukubaliana na maneno ya mama huyo kwamba kama ni kufa afe James…
“Lakini mama, unajua mimi nahisi kama mapenzi yangu makubwa yapo kwa James na si Semi…”
“Una kichaa?”
“Kwa nini?”
“Sasa huo si ndiyo usaliti! Unampenda mwanaume wa pembeni zaidi kuliko mumeo? Ndiyo maana ndoa zinawashinda siku hizi.”
Lina alirudi kwenye meza yake bila kupata mwafaka wa namna ya kumaliza utapeli wake kwa James huku kichwa kikiwa kimejaa mawazo…
“Ukweli pale nimejibu sivyo, lakini ndiyo uhalisia wenyewe. Lazima mwanaume mmoja afe ndipo mimi niweze kuwa huru na si vinginevyo. Nani atanielewa siku ikijulikana nini kilitokea? Nitaonekana mwanamke wa ajabu sana mimi.”
***
Mchana wa siku hiyo, James alikutana na Kindaundau mjini, yule mwanaume aliyekwenda kuchukua mzigo ofisini kwa Lina ulioachwa na mume wa Lina, Semi…
“Bwana leo afadhali tumeonana, nataka tuzungumze,” alisema Kindaundau…
“Hebu tukakae kwenye mgahawa wa maana,” alisema James. Kila mmoja aliingia kwenye gari lake na kwenda kwenye mgahawa mmoja maarufu kwa jina la Mashefa!
“Kwanza nina swali lilelile la siku zile,” alianza kusema Kindaundau…
“Lipi?”
“Kuhusu mwanamke uliyemuoa…”
“Kwani Kindaundau unataka kujua nini zaidi rafiki yangu?”
“Nina wasiwasi na jambo fulani.”
“Kuhusu mke wangu?”
“Ndiyo…”
“Kuwa..?”
“Unasema anaitwa Lina si ndiyo?”
“Ndiyo! Anaitwa Lina Joseph Ambakucha, ni mzaliwa na  Kijiji cha Kilole, Korogwe mkoani Tanga…”
“Sasa sikia James, mimi nina rafiki yangu anaitwa Semi…”
“Semi?” alihoji kwa mshtuko James…
“Ndiyo, Semi.”
James akakumbuka aliona jina la Bro Semi kwenye simu ya Lina…
“Enhe, kafanyaje?”
“Semi ana mke, anaitwa Lina Joseph Ambakucha. Mimi sijawahi kumwona ila kuna wakati Semi alikuwa anafukuzia mkopo mkubwa benki, Lina alikuwa mmoja wa watu wanaotakiwa kutia sahihi kwenye fomu. Kwa sababu tulikuwa tukienda benki kila siku nikalizoea hilo jina.
“Halafu juzi nadhani, nilikwenda kuchukua mzigo wangu ofisini kwa huyo Lina aliuacha mumewe, huyo Semi…”
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

ITAENDELEA SIKU YA KESHO

UNANG'ANG'ANIA KUPENDA USIKOPENDEKA ILI IWEJE? - 2

$
0
0

WIKI iliyopita tuliianza mada hii ambayo inatufundisha juu ya kutong’ang’ania kupenda pasipopendeka. Unampenda mtu wakati yeye moyo wake haupo kwako, utateseka bure wakati mwenzako wala hayajui mateso unayopitia.
 
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

Utaambulia maumivu yatakayokugharimu kwa kiasi kikubwa usipokuwa makini, leo tumalizie mada hii kwa kutazama madhara ya kung’ang’ania penzi hilo.
TUENDELEE…

Uking’ang’ania kupenda sehemu usiyopendwa kitakachofuata hapo ni kuanza kujiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu.
Yawezekana alikuwa akikupa moyo kutokana na majibu yake na kukufanya uendelee kuwa karibu yake kwa muda mrefu lakini kuna wakati utachoka, utaanza kujijengea maswali yasiyokuwa na majibu.
Utajiuliza kwamba, inamaana muda wote ule niliokuwa niko naye alikuwa akicheza na akili yangu? Kwa nini lakini akufanyie hivyo? Utawaza kwamba ni bora angekukataa mapema kuliko kuendelea kukufurahia machoni wakati moyoni anakung’ong’a.
Kipindi hicho ndicho ambacho mtu ni rahisi kusikia amefanya maamuzi ambayo yanaweza kumgharimu. Wapo wanaoamua kujiua au kumuua yule aliyempenda eti kwa sababu tu ametendwa kitu ambacho si sahihi. Ni vyema kila mmoja akatambua umuhimu wa kupenda pale unapopendwa ili kuepusha maumivu mazito mwishoni.
 

 Wakati wa kufanya uchaguzi, wakati wa kumtafuta mchumba ndiyo wakati ambao watu wanapaswa kuwa makini. Ni vigumu kuzizuia hisia lakini tunapaswa kuzidhibiti. Macho yanaona, yanapeleka ujumbe katika moyo kwamba hapa nimependa na akili inaamua kwamba ngoja nirushe ndoano.
Unarusha ndoano, unakutana na kisiki. Japo mara nyingi kwa desturi za Kiafrika mwanaume ndiye anakuwa wa kwanza kumpenda mwanamke na kuthubutu kumwambia kisha baadaye mwanamke naye anapokea na kuzama penzini lakini si kila utakayempenda naye atakupenda pia. 
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

Kuna athari nyingi za kung’ang’ania kupenda sehemu ambayo hupendwi. Hapa chini nitakuonesha baadhi ya athari ambazo mtu huzipata pale anapopenda sehemu ambayo hapendwi.
Kuishi kwa hofu

Mtu anapompenda mtu na kuweka asilimia zake nyingi kwamba atafanikiwa, akikosa huwa anatawaliwa na hofu. Hofu huwa kubwa, anakuwa mtu wa kujishtukia, anajihisi ana kasoro kumbe kiuhalisia wala hana tatizo lolote.
Kitendo cha kukataliwa kwake hugeuka kuwa hofu, inamtesa. Tena hofu huongezeka hususan kama mhusika aliyemkataa wanaonana naye mara kwa mara.
Pasipokuwa na sababu, hofu hiyo inaweza kudumu kwenye akili yake kwa muda mrefu. Baadhi ya watu wamekuwa wakibadilisha hata njia kumkwepa yule ambaye alimkataa. Anahisi atamdharau. Kumbe mwenzake wakati huo anakuwa ameshasahau kama aliwahi kutamkiwa kuwa anapendwa, haoni hata haja ya kuliwaza
suala hilo maana halipo akilini mwake. Akili na mawazo yake yote huwa yanakuwa kwa mpenzi wake.
Kuharibu majukumu

Hii pia ni athari nyingine ya mtu kupenda asipopendwa. Akili yake inakufa kwa kutokubaliana na jibu kwamba hapendwi. Kama ni mfanyakazi, mwanachuo au hata mfanyabiashara, mambo hayaendi tena sawa wakati huo.
Ndiyo wakati ambao kama ni bosi ofisini, utendaji wa kazi utashuka. Ni rahisi hata wafanyakazi wake kuathirika na jambo hilo. Mambo yote yatakwenda ovyoovyo eti kisa tu amekataliwa na mtu.
Kukonda

Mawazo yanapokuwa mengi, kinachofuata huwa ni mtu kukonda. Pasipokuwa na sababu za msingi, unaanza kudhoofu mwili kwa sababu ya kukataliwa. Akili yako inaamini kwamba umpendaye ndiye huyo na hakuna mwingine unayeweza kumpenda.
Nini cha kujifunza?

Unapaswa kukubaliana na matokeo hususan pale unapoona hakuna muelekeo wa unayemtaka kukuelewa. Uvumilivu unatakiwa wakati unamsaka mchumba lakini upande wa pili unapaswa kukubaliana na matokeo kwamba yawezekana ukapenda lakini usikubaliwe.
Mtu anakukataa kwa vigezo vyake, yawezekana anaye anayempenda. Kelele zako zote za kumshawishi zitakuwa kazi bure. Yawezekana hamuendani kisura, tabia na vitu vingine, usilazimishe!
Mwisho.

 Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

LULU AFUNGUKA UKARIBU WAKE NA KADINDA

$
0
0

Mtotomzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa na Martin Kadinda.
MTOTO mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefafanua ukaribu wake na Martin Kadinda kwa kudai ni rafiki yake wa karibu na hakuna cha ziada.
Akipiga stori na paparazi wetu, Lulu alisema yeye na Kadinda ni marafiki wa kweli na amekuwa akiinjoi maisha yao kwa kushauriana masuala mbalimbali ya kimaisha tofauti na wengine wanavyojiongeza. 
Mtotomzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
“Kadinda ni mtu wangu wa nguvu hakuna kingine zaidi ya urafiki wa kawaida, manenomaneno ni kawaida kwa wanadamu,” alisema Lulu.Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

UTAPELI MZITO: WABONGO WALIZWA 'MIKOPO YA OBAMA, JK'

$
0
0
 
Stori: Harun Sanchawa na Hamida Hassan
Utapeli mzito umeshamiri Bongo ambapo imebainika kuna taasisi iliyojipachika jina la Tanzania Loan Society inayojieleza kuwa inafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wa Serikali ya Marekani huku ikiwarubuni watu kuwa inatoa mikopo bila riba.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Ipo kimtandao zaidi
Taasisi hiyo iliyoanzishwa muda mrefu ikapotea, sasa imeibuka upya na inawaliza wengi ambapo inaendesha shughuli zake kimtandao na wahusika hutumia utundu kuingilia mawasiliano katika akaunti za watu katika facebook na kuweka ushuhuda kuwa wamiliki wamefanikiwa kupata mkopo bila riba tena kwa masharti rahisi.
Mtandao umegundulikaje?
Mmoja wa wasomaji wa gazeti hili aliyefahamika kwa jina la Lulu, hivi karibuni alileta malalamiko yake akieleza jinsi wahusika wa utapeli huo walivyoingilia mawasiliano yake ya Facebook, wakamlisha maneno kuwa aliomba mkopo wa shilingi milioni 3 baada ya kutoa shilingi 95,000 kwa ajili ya uanachama na akapewa fasta.
Kwenye ukurasa wa Facebook wa Lulu, kulikuwa na maelezo ya kupika kuwa, Tanzania Loan Society ni taasisi iliyo chini ya Rais Jakaya Kikwete kwa msaada wa Rais wa Marekani Barack Obama huku watendaji wakuu wakiwa ni Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda na Mbunge wa Chalinze, Mhe.
Ridhiwani Kikwete.
Ikadaiwa eti muweka hazina wa taasisi hiyo ni Zainabu Kikwete huku namba zake za simu zikitajwa kuwa ni 0767 602 518  na 0713 009 819, lengo la mpango huo likiwa ni kuhakikisha Watanzania wanaondokana na umaskini kwa kupewa mikopo kwa masharti nafuu.
Chini ya maelezo hayo kuna linki ya kuingia kwenye mtandao wa taasisi hiyo feki (ambapo ukiufungua unakuta nembo ya serikali ya Tanzania na maelezo yanayomshawishi mtu yeyote kuamini kuwa siyo ishu ya kitapeli.
Kinachomsukuma mtu kuingia mtegoni ni kwamba, kwanza wanahusishwa viongozi wakubwa, pili matapeli hao wanaeleza kuwa makao makuu ya taasisi hiyo ni Posta jijini Dar kwenye jengo la Utumishi, ghorofa ya 5, chumba namba 30 na anayehitaji mkopo kuanzia laki moja hadi milioni 50 anatuma 95,000 kupitia namba za muweka hazina (Zainabu Kikwete feki).
Risasi laingia kazini
Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo, Septemba 28, mwaka huu, waandishi walianza uchunguzi kwa kuthibitisha kama namba za Zainabu zimesajiwa kwa jina gani ambapo ilionekana imesajiliwa kwa jina la Zainabu Kikwete.
Kisha mwandishi wetu alimpigia Zainabu, alipopokea na kuulizwa kuhusiana na taasisi hiyo alisema ni kweli ipo na maelezo yote yapo kwenye mtandao wao huku akimsisitiza mwandishi kutuma pesa ili atumiwe mkopo.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Rais Barack Obama wa Marekani .
Waandishi watinga Jengo la Utumishi
Baada ya kujiridhisha, waandishi wetu walimpigia tena Zainabu na kumtaarifu kuwa wapo njiani kuelekea ofisini kwao, kwa kujiamini alisema hakuna shida na kama ni mkopo upo unawasubiria.
Baada ya waandishi wetu kufika kwenye jengo la Utumishi, walimpigia tena simu Zainabu kumjulisha kuwa wameshafika ambapo alidai wametoka kidogo ofisini (eti wameenda kukusanya madeni sugu) na kwamba wakutane kesho yake.
Waandishi wetu wakiwa nje ya jengo hilo, waliongea na mmoja wa walinzi na kumuuliza juu ya uwepo wa taasisi hiyo ambapo alieleza kuwa, haipo na wengi wamekuwa wakifika hapo baada ya kutapeliwa.
Ili kupata taarifa rasmi, waandishi walifika kwenye ofisi ya mmoja wa maafisa habari wa Ofisi ya Rais, Menejimenti na Utumishi wa Umma, Florence Laurence ambaye alikiri taasisi hiyo ya kitapeli kuhusisha jengo lao na walishatoa tahadhari kwa wananchi.
Msako wafanyika
Licha ya majibu yaliyotolewa na afisa habari huyo, waandishi wetu walifika katika Ofisi ya Polisi, Kanda Maalum ya Dar, Kitengo cha Intelijensi na kutoa taarifa ambapo walichukua taarifa kuhusiana na mtandao huo na kuahidi kudili nao.
Septemba 30, mwaka huu ofisi hiyo ilitoa polisi wawili ambao waliongozana na waandishi wetu mpaka katika jengo la Utumishi na mhusika alipopigiwa simu alidai siku hiyo pia walikuwa bize kukusanya madeni sugu na kwamba waende tena kesho yake.
Kutokana na kuchengachenga kwa wahusika, polisi walishauri waachwe wafanye kazi yao na kwamba kwa mbinu zao za kiintelijensia watawanasa wahusika. Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, mtandao huu umewaliza wengi hivyo ni vyema watu wakawa makini. 
(CREDIT: GLOBAL PUBLISHERS)

BETHIDEI YA DIAMOND, WEMA AWA GUMZO!

$
0
0

NI Gumzo! Hiyo ndiyo kauli pekee inayoweza kuakisi pati ya kuzaliwa ya supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ametimiza umri wa miaka 25, iliyofanyika usiku wa kuamikia jana kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Tower (PSPF), Posta jijini Dar, Risasi Jumamosi lilikuwepo ndani ya nyumba.
 
Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake, Wema Isaac Sepetu ‘Onyinye’.
Ubavu wa Diamond, Wema Isaac Sepetu ‘Onyinye’ ndiye aliyekuwa gumzo katika sherehe hiyo baada ya watu wengi kuwa na shauku ya kuona kama atafika au la.
Wengi walitaka kujua kama atafika, ataingia kwa staili gani kutokana na minong’ono iliyokuwa ikiendelea kuwa huenda Wema asitokee kwenye sherehe hiyo kutokana na madai kuwa Diamond alikasirika baada ya kukuta mpenzi wake huyo amezawadiwa ndinga aina ya BMW 454i na Martin Kadinda hivyo kuhoji uhalali wake.
 
Diamond Platnumz, ubavu wake, Wema Sepetu na Bi mkubwa wake wakipiga picha ya pamoja.
Katika hali isiyotegemewa, Diamond na Wema waliingia pamoja huku wakiwa wameshikana mikono.
Wema alivaa gauni lenye mpasuo wa aina yake, kila mmoja alimfuatilia hatua kwa hatua kutaka kujua atasababisha tukio gani.
Watu kibao waliohudhuria ukumbini hapo, walipiga shagwe za kutosha kwa Wema huku wakidai ndiye mke halali wa Diamond hivyo kumshangilia kila alipokuwa akiinuka kufanya tukio.Kwenye ukumbi huo, kila kitu kilikuwa kimeshalipiwa hivyo waalikwa wote walikunywa, kula na kucheza kwa gharama za Diamond.
Diamond Platnumz na Wema Sepetu wakiwa wamepozi.
Pia kulikuwa na bendi mbalimbali zilizotumbuiza hasa Ya Moto Band na wasanii mmojammoja au kundi huku kukiwa na mastaa wengi wa filamu na muziki Bongo ambao walibaki midomo wazi kutokana na namna shuguli hiyo ilivyokuwa kubwa.
Mapaparazi wetu; Shani Ramadhani, Denis Mtima, Mayasa Mariwata na Mpiga Picha Mkuu, Richard Bukos walikuwepo ukumbini hapo kuhakikisha wananasa kila tukio lililotokea na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa;
 
Wema Sepetu akimuweka sawa mpenzi wake.
Saa 3:30 USIKUBUKOS AZINGUA
Risasi Jumamosi: Bukos naamini utakuwa umeshafika ukumbini, nini kinaendelea hapo?
Bukos: Kiongozi wangu nipe dakika 20 nitakuwa nimeshafika hapo.
Risasi Jumamosi: Bukos unazingua, ngoja nimcheki Shani ameniambia ameshafika. Shani kama unanisikia, nini kinaendelea ukumbini hapo?
 
Baadhi warembo waliohudhuria sherehe hiyo ya Bethidei.
SAA 4:00 USIKUBIA ZAMWAGWA
Shani: Kiongozi hapa naona wageni waalikwa tayari wameanza kutembezewa bia za kumwaga, bia zinamwagika kama vile bomba la mvua.
Risasi Jumamosi: Mh! Mapema yote hiyo, si watazima hao? Enhe, nini kinaendelea?
Shani: Kiongozi namuona Vanessa Mdee ‘V-Money’ kaingia hapa, amevaa kivazi cha ajabu kweli. Cheni ya kiunoni njenje.Risasi Jumamosi: Mh! Mtoto ana balaa huyo, poa piga kazi Shani, ngoja nimcheki Denis.
 
Mc wa shughuli hiyo, Sauda Mwilima na 'Chid Benz' wakiwa jukwaani.
SAA 5:00 USIKUSHILOLE, NUH FULL MAHABA
Denis: Kiongozi nawaona Shilole na Nuh Mziwanda wameongazana wanakwenda kuketi lakini hapa full mahaba au mahaba nikongorowe, kila mmoja anamdekeza mwenzake.Risasi Jumamosi: Safi, hayo ndiyo mahabati, hebu ngoja nimpe nafasi Mayasa naona anasumbua kweli.
SAA 5:45 USIKUDIAMOND, WEMA WATINGA
Mayasa: Mkuu Diamond na ubavu wake, Wema au Madam ndiyo wanaingia kwa staili ya kumbikumbi. Pembeni yao namuona mama Diamond naye anawapa kampani. Duh! Tayari Diamond amefikia kufungua shampeni, waalikwa full kelele.
 
Nuh Mziwanda na mpenzi wake Shilole wamehudhuria sherehe hiyo.
Risasi Jumamosi: Mayasa acha mbwembwe, kwanza niambie keki zipo ngapi na shampeni?
Mayasa: Keki kubwa zipo tatu, shampeni zipo zaidi ya kumi. Keki ndogo ndiyo zipo za kumwaga, hazina idadi.
SAA 6:20 USIKUNGOMA ZA ASILI
Denis: Sasa ni zamu ya ngoma za asili zinapigwa…Duh! Mzuka umempanda Diamond ameinuka ameanza kucheza na Wema. Waalikwa full kushangilia, wanaonesha kuzirudi ngoma za asili hatari.
 
Wageni waalikwa wakizidi kuingia ukumbini.
Hapa wasanii kibao wameanza kutoa shangwe, namuona Vincent Kigosi ‘Ray’, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Queen Darlin, Petit Man, Chegge, Temba, Yamoto Band, Jacob Steven ‘JB’ na Aunt Ezekiel wanakula bata.
Risasi Jumamosi: Enhee…Denis: Mama Diamond naye kaingia kucheza…
SAA 7:00 USIKU KEKI YAKATWA
Bukos: Keki ndiyo inakatwa, Diamond amekata, anaanza kuwalisha wageni mbalimbali. Ameanza mama Diamond, amefuata Wema sasa.
 
Keki ya Bethidei ya Diamond.
Analishwa kwa staili ya njiwa. Anamalizia na wageni mbalimbali wakiwemo waliozaliwa siku moja nay eye ambao siyo mastaa.Risasi Jumamosi: Bukos muda umekwenda, yaweke matukio yote kwa pamoja utupe uhondo mzima.
Baada ya nusu saa…
Bukos: Kimsingi rekodi imeandikwa. Bethidei hii watu wamekunywa, wamekula, bendi mbalimbali zimetumbuiza. Kubwa zaidi, Diamond amepewa gari aina ya BMW kama lile la Wema na menegimenti yake ya Wasafi. 
 Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
(CREDIT: GPL)

MKONGO WA WOLPER, HUSNA: NAMTAKA LULU KWA GHARAMA YOYOTE!

$
0
0


Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwami inayosaidia watu wasiojiweza na yatima, inayofanya kazi nchi za Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mwami Rajabu ‘Mkongo’ ameibuka na madai mazito kwamba baada ya ‘kumalizana’ na mastaa wa Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe na Husna Maulid, kwa sasa anamtaka mwigizaji Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ kwa gharama yoyote.
 
Mwami Rajabu ‘Mkongo’.
Akizoza na gazeti hili ndani ya Hoteli ya Double Tree iliyopo Masaki, Dar, mapema wiki hii, Mwami ambaye ni raia wa nchi ya Kongo alifunguka kwamba, amewahi kudaiwa kutoka na wasichana kibao Bongo lakini yeye ni mume wa mtu anayejiheshimu na hao wanawake aliotajiwa kutoka nao aliwahi kuwa nao karibu kwa lengo la kutaka kufanya nao kazi tu na si vinginevyo.
“Unajua watu wamenitajia eti nimetoka na Wolper, Husna mara Wema, si kweli, hawa watu mimi niliwahi kukutana nao Nairobi (Kenya) kwa lengo la kufanya nao biashara lakini mwanamke ambaye ananilaza macho na hata nikimpata siwezi kuficha penzi ni Lulu,” alisema Mwami bila soni.
 
Mwigizaji Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Jamaa huyo ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 na kuendelea huku akiwa na mke na watoto sita alisema kwamba, akipatikana mtu wa kumuunganisha na Lulu kwa gharama yoyote atafurahi kwani ni mwanamke wa ndoto zake.
“Wote siwataki lakini nikimpata Lulu simwachi nampenda sana tena sana,” alisema jamaa huyo kwa nyodo akionekana ni mtu ambaye fedha zimemtembelea.
Jitihada za kumpata Lulu ili kusikia analichukuliaje suala hilo hazikuzaa matunda kwani simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na hata alipofuatwa nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar, hakuwepo hivyo juhudi za kumpata zinaendelea.

NICOLE FRANKLYN SARAKIKYA NDIYE REDD'S MISS TANZANIA TALENT 2014

$
0
0

Nicole Franklyn Sarakikya ambaye ni mwakilishi kutoka Shinyanga 2014  usiku wa kuamkia leo alifanikiwa kuwabagwa warembo wenzake 26 kati ya 30 wanao wania taji la Miss Tanzania mwaka huu na kufanikiwa kuwa mrembo wa 3 kuingia Nusu Fainali ya Mashindano hayo baada ya kutwaa taji la miss talent. Shindano hili limefanyika New Maisha Club jijini Dar es Salaam. (Picha na Pamoja Blog)
Tano bora ilikuwa hii


 Ommy Dimpoz akiwa kwenye red carpet
 Msami akitoa burudani ya nguvu ndani ya Maisha club jijini Dar
  Mambo yalikuwa hivyo kwa baadhi ya washiriki
Mardha John akifanya vitu vyake


 Huyu ni balaaaa
 Elizabeth Eliud akikizungusha kiuno chake
Dorice Molel akifanya ya kwake kwenye stage
  Kwa Naomi Kisaka ilikuwa ni shidaaaaaa
 Huyu alikuja kiivi
 Sabina Thomas  alitoka kivyake vyake
  Weeeeee hii ni shida 
 Maureen Godfrey akishake kwenye stage
 Majaji wakifuatilia shindano hilo kwa makini
 Nicole Franklyn Sarakikya akiimba kwa hisia kali
Ni mwendo wa furaha tu
 Camilla John aliimba kwa hisia 
 Hii ni kikwetu kwetu
Happy Sosy alikuja kama Beyonce 
Queen Latifa Hamisi yeye aliamua kukata nyonga 
Ni mwendo wa mauno
 Ni furaha tu
 Ngoma ziliamia India kwa muda
 Mc wa mashindano ya Redds  Miss Tanzania Talent, Hypeman Hk akifanya ya kwake kwenye jukwaa la New Maisha Club.
Ommy Dimpoz akitoa burudani kwenye stage ya Tanzania Miss Talent iliyofanyika ndani ya New Maisha Club Dar es salaam.
Kazi inaendelea hapa 

 Majaji wakijadiliana jambo
 
Ommy Dimpoz (kulia) akiimba pamoja na Christian Bella waimbo wa mama ulioleta amasa kwa mashabiki wake.
 Majaji wakiongozwa na Chief jaji Martin Kadinda wakitoa maoni juu ya washiriki walioonesha vipaji vyao
  Chief Jaji Martin Kadinda akitangaza washindi
Baadhi ya mashabiki wakifuatilia kwa makini tukio lililokuwa likiendelea

HAPPY BIRTHDAY ZAMARADI MKETEMA

$
0
0
 

Hosti wa Program ya Take One kupitia Clouds TV, Zamaradi Mketema.

HOST wa Program ya Take One kupitia Clouds TV na mwigizaji, Zamaradi leo ni siku yake ya kuzaliwa. Global Publishers tunakutakia maisha marefu.

WAKAZI WA SINGIDA WAKUNWA TAMASHA LA FIESTA...PICHA ZIPO HAPA

$
0
0

 Baadhi ya mwashabiki wa tamasha la Fiesta 2014 wakishangilia kwa hisia,wakati shoo ikiendelea jukwaani ndani uwanja wa Namfua mjini Singida.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kampuni ya No Fake Zone,Lina Sanga ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Oletemba,akiimba jukwaani mbele ya umati wa watu wakati wa tamasha la Fiesta lililofanyika jana katika uwanja wa Namfua,kulia ni mmoja wa wacheza shoo wake akiwajibika jukwaani.
 Kundi mahiri la muziki wa kizazi kipya litambulikalo kwa jina la Makomando wakilishambulia jukwaa la Fiesta hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
 Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta ndani ya Uwanja wa Namfua hapo jana mjini Singida.
 Mmoja wa mashabiki akishangilia huku akiwa amebebwa
 Msanii wa muziki wa bongofleva,Mr Blue a.k.a Kabyssal akiimba mbele ya umati wa wakazi wa mji wa singida waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua.
 Sehemu ya umati wa watu ndani ya tamasha la Fiesta mjini Singida hapo jana katika uwanja wa Namfua
 Ilikuwa ni shangwe tu ndani ya uwanja wa Namfua wakati tamasha la Fiesta likiendelea.
 Msaniii mwingine anaefanya vyema katika anga ya muziki wa bongofleva,kupitia kundi la WEUSI,Niki wa Pili akiwaimbisha mashabiki wake
 Shabiki kapagawa na yaliyokuwa yakijiri jukwaani.
 Badala ya kuwa watazamaji tu,nao pia walikuwa wakijimwaya mwaya taratiibu.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nyumba ya vipaji ya THT,Rachael akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani),wakati wa tamasha la Fiesta likendelea ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
 Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes anaetamba na wimbo wake wa Togola akiwaimbisha mashabiki wake,kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
 Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kizazi kipya atambulikae kwa jina kisanii Mwana-FA akiimba mbele ya umati wa wakazi wa Singida waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta 2014,lililofanyika jana ndani ya uwanja wa Namfua.
 Msanii Mwana-FA na Linah wakiimba kwa pamoja jukwaani,huku miluzi na makelele ya mashabiki yakiwa yametawala kila kona ya uwanja wakati wa tamasha la Fiesta likiendelea.
 Mashabiki wakishangilia
 Wasanii mahiri wa muziki wa Bongofleva,Ney wa Mitego na Stamina wakilishambulia jukwaa kwa pamoja kupitia wimbo wao unajojulikana kwa jina la Huko kweni Vipi,ndani ya tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Singida wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya tamasha la Fiesta.PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA.

JK ATEMBELEA CHUO CHA SAYANSI YA AFYA UDOM

$
0
0

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shaaban Mlacha na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (tai nyekundu) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya  Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianzi kazi rasmi hivi karibuni.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali na  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dododma Profesa Shaaban Mlacha (mbele) na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (kulia) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianzi kazi rasmi hivi karibuni.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo kwa  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shaaban Mlacha na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (tai nyekundu) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianzi kazi rasmi hivi karibuni.
Jengo kuu la  Chuo  cha Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha Chuo Kikuu cha Dodoma  mjini Dodoma 
 Sehemu ya majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu ya UDOM
 Sehemu ya barabara ya lami ya kutoka na kuelekea vyuo mbalimbali vya UDOM
 Mhe. Baraka Konisaga, ambaye ni Mjumbe wa Kikao cha kazi cha viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini akitoa rais binafsi muda mfupi kabla Rais Jakaya Mrisho Kikwete hajafunga rasmi kikao hicho cha siku tatu kilichojumuisha wajumbe zaidi ya 900 kuzungumzia sekta ya elimu ili  kupanga mikakati na kutatua changamoto zinazoikabili, katuika ukumbi wa Chimwaga katika Cho Kikuu cha Dodoma mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunga rasmi Kikao cha kazi cha viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini katuika ukumbi wa Chimwaga katika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dodoma.

SIMBA YABANWA MBAVU NA STAND UNITED, YATOKA 1-1

$
0
0

 Mshambiliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (kushoto)  akijaribu kuwatoka wachezaji wa Stand United.

SIMBA SC imelazimishwa sare ya tatu mfululizo nyumbani baada ya kufungana bao 1-1 na Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hadi mapumziko, tayari timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1, Simba SC wakitangulia kupitia kwa Shaban Kisiga dakika ya 35 kabla ya Stand United kusawazisha dakika 10 baadaye.
Wafungaji  ni Shaban Kisiga kwa Simba SC na Kheri Mohamed wa Stand United.

Kikosi cha Simba SC: Hussein Sharrif ‘Cassilas’, Miraj Adam, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Joram Mgeveke, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’/Said Ndemla dk46, Shaban Kisiga ‘Malone’/Amri Kiemba dk84, Emmanuel Okwi na Ibrahim Hajibu/Elias Maguri dk68.

Kikosi cha Stand United:John Mwenda, Swaleh Abdallah, Yassin Mustafa, Iddi Mobby, Peter Mutabuzi, Omar Mtaki, Mussa Said, Reyna Mungira, Kheri Mohamed, Soud Mohammed/Salum Kamana dk70 na Suleiman Jingo.


 Wachezaji wa Stand United wakishangilia baada ya kusawazisha bao kipindi cha kwanza

 Kikosi cha Stand United kilichoanza dhidi ya Simba.
  
Kikosi cha Simba SC kiichoanza mechi dhidi ya Stand United na kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kipa wa STAND United.

LAVEDA AFUNIKA UFUNGUZI WA BIG BROTHER HOTSHOTS

$
0
0

Irene 'Laveda' akionyesha ufundi wa kutumia saxophone wakati akitoa shoo kwenye ufunguzi wa Big Brother Hotshots.
MSHIRIKI wa shinadano la Big Brother Hotshots kutoka Tanzania, Irene 'Laveda' amefunika vilivyo katika shoo ya ufunguzi wa shindano hilo usiku huu nchini Afrka Kusini.
Laveda ameongoza kwa kura zilizopigwa na watu waliokuwa mjengoni akipata asilimia 85 kutokana na shoo yake kali aliyotoa akicharaza vilivyo saxophone na kuwafunika washiriki wengine 25 kutoka mataifa mengine ya Afrika.
Kwa ushindi huo, Laveda hatakuwemo katika orodha ya washiriki watakaopigiwa kura kwa ajili ya kutolewa mjengoni kuanzia wiki ijayo.

SEMINA YA FURSA YAWAONYESHA NJIA WAKAZI WA DODOMA

$
0
0

 
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group, Ruge Mutahabaakiongea na baaddhi ya wakazi wa Dodoma mjini waliyohudhuria kwenye Semina ya Kamata Fursa ndani ya Ukumbi wa Royal Villege mapema leo,ambapo aliweze kuongea nao na kuwapatia mbinu mbalimbali za kujikwamua kupitia lasilimali zilizopo kwenye mazo yapatikanayo ndani ya mkoa huo.
 
Msemaji kutoka G5 One, Pius Mikongoti akiwalezea wakazi wa Dodoma namna ya kunufaika kupitia huduma zitolewazo na GS One hasa katika kutumia Barcode.
 
Msanii wa kughani Mashairi, Mrisho Mpoto naye akijaribu kuwapa historia yake ya mafanikio na namna alivyoweza kutumia fursa hadi kufikia hapo alipo kwa sasa.
 
Afisa Utekelezaji na mipango wa NSSF, Ally Mkulemba akitoa semina kwa wakazi wa Dodoma huku akiwapa mbinu za kutumia fursa katika kusongesha mafanikio kupitia mikopo mbalimbali itolewayo na Shirika hilo mapema leo ndani ya Ukumbi wa Royal Villege.
 
Mrisho Mpoto akimkabidhi kifaa cha kupimia magari mmoja wakazi wa Dodoma Beatrice Chilewa (kulia), muda mfupi baada ya kujishindia moja ya swali lililoulizwa na msemaji wa GS One Pius Mikongoti, ambalo lilikuwa likimtaka ataje nchi tatu za Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazotoa Barcode na namba za utambulisho wa nchi hizo, wa kwanza kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Josekazi Auto Garage ambaye ndiye mimiliki wa kifaa hicho cha kupimia magari.
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Josekazi Auto Garage, Joseph Mgaya akiwaeleza wakazi wa Dodoma namna alivyotumia fursa na kumnya aweze kumiliki kampuni hiyo inayojishugurisha na huduma za kutengeneza A/C za magari na Ndege na nanamna alivyo wekeza hadi leo anakifaa kinachoweza kupima magari yote na kujua matizo yote kwa halaka.
 
Baadhi ya wakazi wa Dodoma waliyojitokeza kusikiliza mafunzo mbalimbali kwenye Semina ya Kamata Fursa iliyokuwa ikifanyika ndani ya Ukumbi wa Royol Villege.
 
Msanii wa Bongo Fleva Mwasiti Almasi akijaribu kuwaonyesha wakazi wa Dodoma namna alivyotumia Fursa iliyopo kwenye muziki na kufanikiwa kuwekeza baadhi ya vitu kupitia mafao mbalimbali yatolewayo na Shirika la NSSF.
 
Sehemu ya watu waliyojitokeza kwenye Semina ya Kamata Fursa iliyokuwa ikifanyika ndani ya Ukumbi wa Royal Village.
 
Mmoja wa wanasemina hao akiuliza swali lililotokana na mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na wasemaji mbalimbali wa Semina ya Kamata Fursa muda mfupi kabla ya kumalizika kwa semina hiyo.
 
Mtangazaji wa Kipindi cha Leo tena, Gea Habib akizungumza jambo kwenye semina ya Kamata Fursa.
 
Meza kuu ya watoa mada ya Kamata Fursa wakijadiliana baadhi ya mambo yaliyokuwa yakiendelea mahali hapo.
Habari/Picha: Musa Mateja/ GPL/Dodoma

FALCAO, DI MARIA MASHUJAA MAN UNITED IKIITUNGUA EVERTON 2-1

$
0
0
FALCAO AKISHANGILIA BAADA YA KUFUNGA BAO LA USHINDI DHIDI YA EVERTON.
Manchester United: De Gea 8, Da Silva 7, McNair 6.5, Rojo 6, Shaw 5.5 (Blackett 71, 7), Blind 7, Valencia 5 (Fellaini 78, 5.5), Di Maria 7.5, Mata 5.5, Falcao 6 (Wilson 73, 6), van Persie 5.5
Substitutes not used: Januzaj, Lindegaard, Fletcher, Thorpe
Scorers: Di Maria 27; Falcao 62

Booked: Van Persie, Blind, Valencia, Wilson 
Everton: Howard 6, Hibbert 6.5 (Browning 77, 6), Stones 7, Jagielka 6, Baines 6.5, Barry 6, Besic 6, Pienaar 6 (Oviedo 63, 6), Naismith 7, McGeady 5.5 (Osman 77, 6), Lukaku 6
Substitutes not used: Robles, Gibson, Eto'o, Alcaraz
Scorer: Naismith 55 
Booked:  Besic, Pienaar, Howard
Referee: Kevin Friend (Leicestershire)
Attendance: 75,294 




















CHELSEA WAITUNGUA ARSENAL 2-0, HAZARD, COSTA KAMA KAWA

$
0
0



Chelsea imeichapa Arsenal mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu England iliyomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London.

Mechi hiyo ilijaa vituko kibao ikiwa ni pamoja na kuchelewa kuanza kwa dakika 15, pia makocha Jose Mourinho na Arsene Wenger kukwidana.
Lakini ndai ya uwanja ushindani ulikuwa juu na Eden Hazard na Diego Costa walikuwa mashujaa kwa kufunga mabao hayo mawili.
Hazard alianza kwa mkwaju wa penalti baada ya kuangushwa, kabla ya Costa kumaliza kazi akiwazidi ujanja mabeki na kipa wa Arsenal.
Sasa Chelsea imekwea kileleni mwa Premier League huku Costa akizidi kupaa kwa wafungaji bora akiwa na mabao tisa.
Chelsea:
Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; Matic, Fabregas; Schurrle, Oscar, Hazard; Costa
Arsenal:
Szczesny, Chambers, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Wilshere, Flamini, Cazorla, Ozil, Alexis, Welbeck.









MMILIKI WA CHELSEA, ROMAN ABRAMOVICH AKISHANGILIA BAO LA COSTA.

MOURINHO, WENGER NUSURA WAZICHAPE KAVUKAVU UWANJANI

$
0
0



Makocha Jose Mourinho na mgeni wake Arsene Wenger siku ya jana nusura wazichape kavukavu uwanjani.
Wawili hao walitaka kuzichapa wakati Chelsea ikipambana na Arsenal.

Haijajulikana tatizo lilikuwa ni nini ingawa inawezekana Mourinho alisema jambo lililomuudhi Wenger.
Kutokana na hasira, Wenger alimfuata Mourinho na kumkwida, wakaanza kuvutana.
Baadaye mwamuzi aliwaita na kuwaonya akionekana anasisitiza wakirudia, watakwenda jukwaani.

YANGA YAILZA JKT 2-1

$
0
0

Wachezaji wa Young Africans wakimpongeza Kelvin Yondani baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza katika mchezo dhidi ya JKT Ruvu, Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 2-1

Kikosi cha timu ya Young Africans chini ya kocha mbrazil Marcio Maximo leo kimeendeleza wimbi la ushindi katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya maafande wa jeshi la Kujenga Taifa nchini  JKT Ruvu mchezo uliofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijin Dar es salaam.

Young Africans iliingia uwanjani leo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi  wa mabao 2-1 dhidi ya maafande wa jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons iliyoupata mwishoni mwa wiki na ikatumia chachu hiyo hiyo kupata ushindi kama huo katika mchezo wa leo.

Mlinzi wa kati wa timu ya Young Africans Kelvin Yondani "Cotton" aliipatia timu yake bao la kwanza dakika ya 32 ya mchezo kwa shuti kali akiitumia vizuri pasi nzuri ya kiungo Haruna Niyonzima aliyewatoka walinzi wa JKT Ruvu na kumpasia Yondani ambaye pia ndiye alianzisha mashambulizi ya bao hilo toka langoni mwa Yanga na kufunga bao lake la kwanza ndani ya klabu ya Young Africans.

Washambuliaji wa Young Africans wakiongozwa na Geilson Santos "Jajaj", Saimon Msuva na Andrey Coutinho walikshindwa kuzitumia nafasi walizozipata kutokana na kutokua makini na mipira kuokolewa na walinzi wa JKT.

JKT Ruvu walicharuka na kucheza kwa nguvu kwa kukamia na kukuta wachezaj wake wakipewa kadi za njano baada ya kuwachezae vibaya wachezaji wa Young Africans wakiwemo Jaja, Niyonzima na Msuva.

Kipindi cha pili kilianz akwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo Young Africans iliwaangiza Mrisho Ngasa, Nizar Khalfani na Salum Telela waliochukua nafasi za Andrey Coutinho, Haruna Niyonzima na Edward Charles aliyeumia mabadilko ambayo yalileta tija kwa kikosi cha Maximo.

Dakika ya 73 ya mchezo kiungo Haruna Niyonzima aliipatia Young Africans bao la pili kwa mpira wa adhabu kufuatia kiungo Hassan Dilunga kuchezewa madhambi nje kidogo ya eneo la hatari na Niyonzima kupiga mpira uliojaa moja kwa moja wavuni na kumuacha mlinda lango wa JKT Ruvu Chove akiduwaa.

Young Africans iliendelea kulishabulia lango la JKT kwa mpira wa speed kupitia kwa Msuva na Ngasa lakini mipira yao ya mwisho haikuwa na madhara na kukuta harakati zao zikiishia mikononi mwa golikipa Chove wa JKT Ruvu.

Dakika ya 88 ya mchezo kiungo wa Jabir Aziz aliipatia timu yake ya JKT Ruvu bao la kufutia machozi kwa shuti kali baada ya kuitumia vyema pasi ya Amos Mgisa aliyewazidi ujanja walinzi wa Young Africans na kumkuta mfungaji alipiga shuti kali na kumuacha golikioa Dida akiruka bila mafanikio.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 2 - 1 JKT Ruvu Stars, matokeo ambayo yanaipeleka timu ya Young Africans mpaka kwenye nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015.

Young Africans: 1. Deo Munish "Dida", 2. Juma Abdul, 3.Edward Charles/Salum Telela, 4. Nadir Haroub "Cananavao" (C), 5.Kelvin Yondani, 6.Mbuyu Twite 7.Hassan Dilunga, 8.Haruna Niyonzima/Nizar Khalfani 9.Geilson Santos "Jaja" 10.Andrey Coutinho/Mrisho Ngasa 11.Saimon Msuva
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>