Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

WEMA, DIAMOND WAZINDUA GARI KWA MAHABA

$
0
0
 
Stori: Richard Bukos
Mahaba nimalize! Mastaa wapendanao, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wamesababisha tukio jipya kama kawaida yao, safari hii wameishtua kadamnasi kwa kuzindua gari jipya kwa mahaba mazito ndani yake, Ijumaa Wikienda lilinyaka mchongo mzima.
 
Mastaa wapendanao, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wakikumbatiana kimahaba.
KAMA MUVI YA MAPENZI
Tukio hilo lililojiri kama muvi ya mapenzi (romantic movie) lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee uliopo Posta jijini Dar wakati Diamond alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na kujizawadia ndinga aina ya BMW X6 ambalo waliligeuza kuwa uwanja wa malovee wakati walipokwenda kukabidhiwa na menejimenti yake ya Wasafi.
SHEREHE ILIVYOANZA
Awali, waalikwa sambamba na mastaa mbalimbali wakusanyika kwenye ukumbi huo na ilipofika saa 5:00 usiku, Diamond akiwa ameambatana na ubavu wake, Wema sambamba na mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’, waliingia na sherehe kuanza.
 
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wakila 'romansi'
TUKIO LA ZAWADI
Baada ya sherehe hiyo kupambwa na matukio mbalimbali zikiwemo bendi za asili na wasanii, ulifika wakati wa zawadi ndipo wageni waalikwa walipoanza kujinadi kupitia kipaza sauti na mwishoni ikawa ni zamu ya menejimenti ya Wasafi ambayo ilitamka kuwa inatoa gari hilo.
CHIEF KIUMBE NDANI
Pedeshee maarufu Bongo ambaye kwa sasa amemrudia Mungu na kuwa mtu wa ibada, Chief Kiumbe hakuwa nyuma katika eneo la zawadi, alifanya kufuru kwa kumrushia Diamond mabunda ya dola za Kimarekani.
 
Mapaparazi wakidaka mchongo mzima laivu.
BABU TALE SASA!
Baada ya kufuru ya kurushiwa ‘madolari’, funga kazi ya zawadi ilimaliziwa na meneja wa msanii huyo, Bab Tale aliyepanda jukwaani na kutangaza kuwa uongozi na familia ya mwanamuziki huyo wamemnunulia gari jipya aina ya BMW X6 na kumtaka ampeleke lilipoegeshwa amkabidhi.
WATU WASHUKA UKUMBINI
Kwa kuwa ukumbi huo upo ghorofani, waalikwa wote sambamba na ‘birthday boy’, Dangote au Chibu, walishuka kwa kutumia lifti za jengo hilo kwenda kuliona gari hilo lililokuwa limeegeshwa katika ‘parking’ maalum.
 
 Wakitoka kwenye ndinga(BMW) kuendelea na sherehe nzima ya bethidei.
MAMA AKABIDHI
Mbwembwe na mikogo ya kimahaba kati ya Diamond na Wema iliendelea hadi pale mama Diamond, Sandra alipomkabidhi mwanaye huyo funguo za gari hilo, wakazama ndani.
MAHABA MAZITO
Kitendo cha wawili hao kuingia ndani ya gari hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 90 za Kitanzania na kufunga milango, kilikuwa ni mwanya mzuri kwao kuanza kuoneshana mahaba motomoto ambapo Diamond alimminia mtoto wa kike mabusu ya kumwaga kisha kugandana kama kumbikumbi.
 
Hili ni gari jipya aina ya BMW X6 ambalo Diamond amezawadiwa katika sherehe ya bethidei yake.
WATUMIA DAKIKA 20
Wapendanao hao walionekana kuzidisha mahaba ambapo walijifungia ndani ya gari hilo kwa zaidi ya dakika 20 na kufanya yao huku watu wapenda ‘ubuyu’ wakiwachungulia kwa dirishani lakini wale waungwana waliamua kutazama pembeni wasione mambo ya chumbani hadharani.
Baada ya kushuka ndani ya gari hilo, wawili hao walikumbatiana tena na kurudi ukumbini ambapo burudani za kula na kunywa ziliendelea.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Hivi karibuni ilifanyika bethidei ya Wema ambapo Diamond alimzawadia mpenzi wake huyo gari aina ya Nissan Murano lenye thamani ya Sh. milioni 36 za madafu huku meneja wa wema, Martin Kadinda akimpa BMW ambalo limeibua mjadala juu ya uhalali wa meneja huyo kuwa na uwezo wa kulinunua.
(CREDIT: GPL)


A JOURNALIST IS BACK (MWANDISHI AMERUDI) - 10

$
0
0

MWANDISHI: NYEMO CHILONGANI
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

“Nitamuua mumeo. Ni lazima nimuue” Dominick alimwambia Edith huku machozi yakitiririka mashavuni mwake.
“Usimuue. Nakuomba usimuue…” Edith alimwambia Dominick.
“Nitamuacha vipi mumeo? Ameiangamiza familia yangu kwa kuichoma na moto ndani ya nyumba yangu. Amebadilisha maisha yangu, nimekuwa mtu wa kutanga tanga. Ameuumiza moyo wangu kwa kunifanya kuwa mpweke katika kipindi chote hiki. Hakuna sababu ya kufanya afurahie maisha Ni lazima nimuue tu” Dominick alimwambia Edith huku akiendelea kulia.
Kadri muda ulivyokuwa ukizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo maisha yake ya nyum yalivyokuwa yakijirudia kichwani mwake kama mkanda wa filamu. Alikumbuka kila kitu, hakuona sababu yoyote ya kumuacha waziri Tumaini hai, ni lazima amuue, tena kwa mkono wake mwenyewe.
“Naomba umsamehe….naomba umsamehe Dominick”  Edith alimwambia Dominick.
“Nitaanzia wapi? Hivi familia yangu itanielewa? Haiwezekani kabisa, kama alivyoiangamiza familia yangu, na yeye nitamuangamiza pia” Dominick alimwambia Edith ambaye alikuwa akilia tu.
Dominick akazunguka nyuma ya Edith na kuanza kuzifungua kamba zile ambazo alikuwa amemfunga pale mtini. Edith bado alikuwa akilia huku akiwa haamini kama Dominick yule mpole ambaye alikuwa pamoja nae shuleni ndiye yule ambaye alikuwa nae mahali pale.
Hakuamini kama mumewe alikuwa amehusika katika mauaji yoyote, uovu wa mumewe ulionekana kumsikitisha kupita kawaida. Alimwangalia Dominick mara mbili mbili, Dominick alionekana kuwa na hasira kupita kiasi, matukio mengi ya nyuma ambayo yalitokea nyuma yake yalionekana kumsikitisha.
“Nitamuua. Nitamuua baada ya kupata msaada mkubwa kutoka kwako”Dominick alimwambia Edith.
“Kupata msaada mkubwa kutoka kwangu? Siwezi Dominick kukusaidia. Siwezi” Edith alimwambia Dominick.
Dominick alimwangalia Edith mara mbili mbili, akaonekana kubadilika zaidi, hasira ambazo alikuwa nazo katika kipindi cha nyuma zikaonekana kuongezeka maradufu. Edith akaonekana kuogopa, hakuwahi kumuona Dominick akiwa katika hali ile hata siku moja.
“Nitakuua. Sitojali chochote kile” Dominick alimwambia Edith ambaye akaanza kutetemeka.
“Naomba unisamehe”
“Nitahitaji msaada wako. Msaada wako ndio utakuwa uhai wako. Kama ukienda kinyume. Nitakuua” Dominick alimwambia Edith.
Dominick akaonekana kubadilika. Tayari hasira zilionekana kumkaba rohoni. Hakuonekana kujali tena kwamba yule aliyekuwa akiongea nae alikuwa Edith au nani, kitu ambacho alikuwa akikitaka kwa kipindi hicho ni kusaidiwa tu.
“Nitakusaidia” Edith alisema.
“Sio kwa maneno. Nitahitaji kwa vitendo” Dominick alimwambia Edith.
“Ingia ndani ya gari” Dominick alimwambia Edith na kisha wote kuanza kuingia garini.
Dominick hakuongea kitu chochote kile, alibaki kimya huku macho yake yakiangaia mbele. Alama za machozi ambayo yalikuwa yakimtoka katika kipindi cha nyuma zilikuwa zikionekana mashavuni mwake. Edith nae alibaki kimya, hakuongea kitu chochte kile kwani aliogopa kumkwaza Dominick.
Safari ile iliishia katika jengo bovu bovu lililokuwa katika uwanja wa Tanganyika Pakers. Giza lilikuwa limeanza kuingia mahali hapo. Hakukuwa na watu wengi mahali pale kitu ambacho wakateremka na kuanza kupiga hatua kuelekea katika jengo lile.
“Mpigie simu mumeo. Mwambie aje mahali hapa, tena akiwa peke yake” Dominick alimwambia Edith.
Edith akachukua simu yake, akawaiwasha na kisha kuanza kumpigia mumewe. Simu ilianza kuita, iliita kwa muda fulani, ikapokelewa. Sauti ya Bwana Tumaini ilisikika kwa wasiwasi, aliongea kama mtu ambaye alikuwa na kigugumizi. Ila baada ya kipindi fulani, ikakaa sawa.
“Umesema uko nae hapo?”
“Ndio. Alitaka kuniua kwa kunichoma moto”
“Mungu wangu! Nakuja sasa hivi” Bwana Tumaini alisema na kisha kukata simu.
Edith alibaki akimwangalia Dominick. Machozi yakaanza kumtoka, alijua fika kwamba kitendo cha mumewe kufika mahali pale basi kingeashiria kwamba angekwenda kuuawa. Alitamani kumuomba Dominick msamaha kwa ajili ya mumewe lakini akaona kuwa ngumu kufanya hivyo.
Dominick akaa kimya. Kadri muda ulivyozidi kwenda na ndivyo ambavyo hasira zake zilivyokuwa zikizidi kuongezeka. Muda aliuona ukienda taratibu sana kuliko siku nyingine, alitamani dakika ziende haraka haraka ili Tumaini afike mahali hapo na kumuua.
                                                                      ***********
Bwana Tumaini alikuwa akitetemeka kwa woga, kitendo cha mke wake kutekwa na mtu mbaye alisadikiwa kuua familia za mawaziri kilionekana kuwa kitendo ambacho kilimuogopesha. Hakutaka kabisa kwenda peke yake huko ambako aliiitwa, kitu alichokitaka ni kwenda pamoja na mapolisi.
Moja kwa moja akaanza kuondoka kuelekea kituo cha polisi. Mapolisi wote wakaonekana kutetemeka mara baada ya kumuona waziri akiingia ndani ya kituo hicho. Bwana Tumaini hakuongea kitu chochote kile, alibaki kimya kwa muda huku akiwaangalia mapolisi ambao walikuwa katika kituo kile.
“Karibu mkuu” polisi mmoja alimkaribisha Tumaini.
“Asante. Nina tatizo na ninahitaji msaada wenu”
“Msaada gani mkuu?”
“Mke wangu ametekwa na mtu ambaye aliua familia za mawaziri wengine” Bwana Tumaini aliwaambia mapolisi ambao walionekana kushtuka.
“Unasemaje?”
“Ndio hivyo. Ameniambia kwamba ni lazima niende Tanganyika Parkers kuonana nae. La si hivyo, atamuua mke wangu” Bwana Tumaini aliwaambia.
Mapolisi wote wakaonekana kuogopa, taarifa ambayo walikuwa wamepewa ilionekana kuwaogopesha kupita kiasi. Walikumbuka baadhi ya mauaji ambayo yalikuwa yamepita katika miezi iliyopita, muuaji hakuonekana kuwa na hurma.
Mapolisi hawakutaka kubaki mahali hapo, moja wa moja wakaingia katika gari lao aina ya Defender na moja kwa moja kuanza safari ya kuelekea katika viwanja vya Tanganyika Parkers. Kila mmoja akaanza bunduki yake vizuri, hawakutakiwa kuuliza kitu chochote mara watakapofika, ni kumkamata muuaji huyo na kumfikisha katika vyombo vya dola.
                                                                   ***********
Muda ulizidi kwenda zaidi na zaidi mpaka giza kuingia. Hakukuwa na mtu yeyote uwanjani pale zaidi ya wao ambao walikuwa wamelipaki gari pembeni. Dakika ziliendelea kwenda mbele, Dominick hakuongea kitu chochote kile zaidi ya kumwangalia Edith ambaye muda wote alikuwa akilia.
Mwanga wa taa ukaanza kuonekana kwa mbali jambo ambalo lilimfanya Dominick kuanza kutabasamu. Sauti ya muungurumo wa gari lile ukaonekana kumshtua. Ingawa muungurumo ule ulikuwa ukisikika kwa mbali lakini alijua vizuri kama gari lile halikuwa lile ambalo alikuwa akiliitaji kufika mahali pale.
Muungurumo ulikuwa mzito, wasiwasi ukaanza kumuingia, akamshika Edith mkono na kuanza kuondoka nae mahali pale. Edith alitamani kukataa lakini kutokana na kuvutwa kwa nguvu, Edith akajikuta akisonga kule ambapo Dominick alitaka waelekee.
Wakasimama katika ukuta karibu kabisa na kutoka nje ya uwanja ule. Macho yao yalikuwa yakielekea kule ambapo gari lao lilipokuwa. Mara wakawaona watu wanne wakiteremka kutoka katika gari lile na moja kwa moja kulifuata gari alilokuja nalo Dominick na Edith.
“Amekuja na mapolisi. Vizuri sana. Sidhani kama ataweza kumuona mkewe tena” Dominick alisema maneno ambayo yalisikika vizuri masikioni mwa Edith.
Akamshika mkono Edith na kuanza kuondoka nae mahali hapo. Tayari Edith akaona kwamba ni lazima Dominick angechukua hatua kali zaidi juu yake kwa ajili ya kumkomoa Tumaini. Kwa haraka haraka akaichukua simu yake na kuanza kumpigia mume wake ambaye alikuwa pamoja na mapolisi kule uwanjani.
“Anataka kuniua…..” Edith alimwambia mumewe kwa sauti iliyojaa wasiwasi.
“Naomba niongee nae” Bwana Tumaini alisema huku akihofia.
Dominick akaichukua simu ile, hata kabla hajaongea kitu, akaanza kumwangalia Edith kwa macho ya chuki. Dominick alionekana kukasirika kupita kawaida. Mapenzi yote ambayo alikuwa nayo juu ya Edith yalionekana kupotea kwa wakati huo.
“Nakuombaaa…nakuomba usimuue mke wangu…” Bwana Tumaini alisema.
“Mjanja wewe. Mjanja wewe kwa kuja na mapolisi. Sasa ninataka kukuonyeshea kwamba mimi ni mjanja zaidi yako. Ni lazima nimuue” Dominick alimwambia Bwana Tumaini.
Bwana Tumaini hakuwa na la kuongea, tayari alitambua kwamba alifanya makosa kuja na mapolisi mahali pale. Akazidi kuomba msamaha zaidi lakini Dominick hakuonekana kuelewa zaidi. Kitu ambacho alikuwa akiking’angania kwa wakati huo ni kumuua Edith tu.
“Niambie nije wapi. Sitokuja na mapolisi” Bwana Tumaini alimwambia Dominick.
“Kama umeshidwa kuja peke yako, utaweza kuja peke yako baadae?” Dominick aliuliza.
“Nitawezaaaa..nitawezaaa…”
“Mimi sio mtoto. Hautoweza. Nakwenda kumchoma moto mkeo” Dominick alimwambia Bwana Tumaini ambaye alionekana kuchanganyikiwa zaidi.
“Nakuomba…nakuo…” Bwana Tumaini alisema lakini hata kabla hajamalizia sentensi yake, simu ikakatika.
Dominick akamchukua Edith na kuanza kuondoka nae. Alipofika nje ya eneo la uwanja ule, akaifuata bajaji moja, akaingia ndani pamoja na Edith na kisha dereva kuwasha bajaji na kuondoka mahali hapo.
Bajaji ilisimama karibu na ufukwe wa Msasani. Wote wakateremka na kuanza kuingia ndani ya ukumbi huo. Hawakutaka kukaa ndani ya ukumbi huo, wakapitiliza nakwenda katika sehemu ambayo ilikuwa na idadi kubwa ya miti.
Dominick akachukua simu ile na kisha kuiwasha. Akampigia simu Bwana Tumaini. Simu ilianza kuita, iliita kwa muda mfupi, ikapokelewa.
“Niambie nije wapi….niambie nije wapiiiii…” Bwana Tumaini alisema.
“Njoo Msasani Club huku kulipokuwa na miti. Mara ya mwisho, kama utakuja pamoja na mapolisi, nitamchoma moto mkeo kama nilivyozichoma moto familia za marafiki zako” Dominick alimwambia Bwana Tumaini.
                                                                         **********
   Bwana Tumaini alikuwa amechanganyikiwa, kitendo cha kumkosa mkewe pamoja na muuaji ambaye wala hakuwa akimfahamu katika kipindi hicho kilionekana kumchanganya kupita kiasi. Simu ambayo alikuwa amepigiwa hakutaka kuidharau hata mara moja, akatoka nje ya kituo cha polisi kimya kimya na kuingia garini mwake.
Safari yake ikaanza ya kuelekea katika ufukwe wa Msasani Club. Moyo wake ulikuwa na wasiwasi kwa kuona kwamba angekuta muuaji amekwishamuua mke wake, Edith. Muda wote alikuwa akisali njiani huku akimtaka Mungu Amnusuru mke wake ambaye alikuwa akimpenda kupita kiasi.
Mara baada ya kuliegesha gari lake, moja kwa moja akaanza kuingia ndani ya eneo la ukumbi ule na moja kwa moja kuteremka na kuanza kupiga hatua kuingia ndani ya ukumbi ule. Macho yake hayakutulia sehemu moja, yalikuwa yakiangalia katika kila kona mahali pale.
Akatka kabisa nje ya ukumbi ule na kuelekea katika michanga mingi pembezoni mwa bahari ya Hindi. Akayapeleka macho yake huku na kule, kwa mbali akauona mwanga wa simu. Hakutaka kujiuliza zaidi, moja kwa moja akaanza kuufuata mwanga ule wa simu huku moyo wake ukia na shauku kubwa ya kutaka kumuona mkewe ambaye alikuwa mjauzito.
Bwana Tumaini akaanza kutabasamu, hakuamini kama angemkuta mkewe mzima mahali pale. Kwa furaha kubwa aliyokuwa nayo, akamfuata na kumkumbatia. Edith alikuwa akilia kwa furaha, tukio la kumuona mumewe mahali hapo, aliona ni jinsi gani alikuwa akimthamini.
“Uliiangamiza familia yangu” Dominick alimwambia Bwana Tumaini.
“Wewe ni nani?” Bwana Tumaini aliuliza huku akijaribu kumwangalia vizuri Dominick usoni.
“Najua unanifahamu. Ulisaidiana na wenzako kuiangamiza familia yangu kwa kuichoma moto ndani ya nyumba yangu. Umeuumiza moyo wangu kupita kawaida”  Dominick alimwambia Bwana Tumaini.
“Dominick…Dominick..naomba unisamehe…”
“Nitaanza vipi kukusamehe. Nitaanzia wapi. Ni lazima nikuangamize wewe pamoja na familia yako” Dominick alimwambia Bwana Tumaini na kuanza kuikoki bunduki yake na kuwanyooshea.
“Naomba unisamehe”
“Haiwezekani. Ni lazima niwaue wote” Dominick aliwaambia.
Tayari alikuwa amekwishaiokoki bunduki yake. Moyo wake ulikuwa ukimuuma kupita kawaida. Tayari mapenzi kati yake na Edith yalikuwa yamekwisha kabisa. Hakuwana kitu kingine cha kufanya zaidi ya kutaka kuiangamiza familia hiyo. Walijitahidi kuomba msamaha lakini Dominick hakuonekana kuelewa.
“Ni lazima niwaue” Dominick alisema.
Ghafla milio ya risasi ikasikika mahali hapo, damu zikaonekana kutapakaa katika michanga ufukweni hapo na ukimya kutawala kwa muda.
                                                                   ********
Damu zilikuwa zimetapakaa chini. Bwana Tumaini pamoja na mkewe Edith walikuwa chini huku wakirusha rusha miguu yao. Risasi zaidi ya nane zilikuwa zimeingia katika miili yao. Vifua vyao vilikuwa vimetobolewa na risasi ambazo zilipigwa kwa haraka sana.
Dominick akawasogelea na kuwaangalia vizuri, alihitaji kufahamu kama watu hao walikuwa wamekufa kama alivyokusudia au la. Wote walikuwa wamekufa pale pale hasa mara baada ya kuacha kurusha rusha miguu yao. Dominick akaachia tabasamu pana, kitendo kile cha kishujaa kilionekana kumfurahisha kupita kiasi.
Moyoni hakuhuzunika hata mara moja mara baada ya kumuua Edith. Ni kweli alimpenda sana mwanamke yule, lakini kwa kipindi kile, alijiona kuwa na uhitaji wa kufaya jambo lile ili mladi tu kutunza siri na kutokujulikana na mtu yeyote.
Mara baada ya kuwaangalia kwa muda, akaanza kuondoka mahali hapo. Alipofika nje ya ukumbi ule wa Msasani Beach, akakodi bajaji nyingine na kisha kuondoka mahali hapo kuelekea katika hoteli ya La Vista Inn ambayo alikuwa amechukua chumba.
Dominick alikaa chumbani kwa muda, kichwa chake kikaanza kuifikiria familia yake ambayo iliteketezwa kwa moto katika kipindi kirefu kilichopita. Moyo ulimuuma sana lakini wakati mwingine alibaki akitabasamu kutokana na kuanza kulipa kisasi kwa wale wote ambao walikuwa wameiteketeza familia yake.
Bado kazi ya kuwaua watu wawili ndio ilikuwa imebaki mbele yake, alitamani kazi hiyo kuifanya haraka iwezekanavyo ili apumzike na kuishi maisha ya amani. Kila siku alikuwa akielekea katika makaburi ya familia yake na kusimama pembeni kama ishara ya kuwakumbuka kwa kuacha maua kadhaa ambayo yalionyesha kuwa tukio kubwa ambalo alikuwa akilifanya maishani mwake kama kuwaenzi.
Hakujua ni wapi pa kuanzia ingawa aliona kuwa ni lazima watu hao wauawe kwa mkono wake mwenyewe. Hakutaka kuwaacha kwani kama angfanya hivyo basi angeonekana kutowatendea haki. Mikono yake aliiona ikiwa imejaa damu lakini bado hakuonekana kuridhika.
Alihitaji kuwaua wote ili kuiridhisha nafsi yake, hakutaka kumuacha yeyote yule ambaye alikuwa amehusika katika mauaji ya familia yake. Kila siku alikuwa akifikiria namna ya kulipiza kisasi hicho kwa watu hao ambao kwake aliwaona kuwa kama wanyama.
Waliuumiza moyo wake na kuuwekea majeraha ambayo hakujua kama ipo siku majeraha hayo yangekuja kupata nafuu. Alihitaji kuyaponya maumivu ya moyo wake na hata kama angeshindwa kuyaponya basi hata kuyapunguzia maumivu.
Kila siku alikuwa akiuma meno yake kwa hasira katika kipindi ambacho alikuwa akiwaona viongozi wale ambao walikuwa wameiangamiza familia yake. Aliwachukia kuliko alivyomchukia shetani ambaye hakuwa akimuona, hakukuwa na kitu chochote ambacho alikuwa akikihitaji katika kipindi hicho zaidi ya kuwaua viongozi hao wawili ambao walikuwa wamebakia.
“Ni lazima niwaue….tena kwa mikono yangu mwenyewe” Dominick alijisemea huku akivuta shuka na kulala.
                                                                  *************
Nchi ya Tanzania ikashtuka kupita kiasi. Mauaji ambayo yalikuwa yametokea katika ufukwe wa Msasani yalionekana kumshtua kila mtu. Viongozi wakakosa amani, kila mmoja akajiona kuwa yuko njiani kumfuata marehemu Tumaini na mkewe.
Mauaji yalitotokea ndani ya miezi michache yalionekana kuwasisimua wattanzania. Muuaji alikuwa hajajulikana mpaka katika kipindi hicho. Maswali kadhaa yalikuwa yakimiminika vichwani mwa Watanzania juu ya polisi ambao bado walionekana kuzembea katika kila kitu.
Miili iliyochukuliwa katika ufukwe ule ikapelekwa mpaka katika chumba cha kuhifadhia maiti huku uchunguzi ukiendelea kufanyika kila siku. Kamanda wa polisi alionekana kuchanganyikiwa, kila siku alikuwa akiongea peke yake kana kwamba pembeni yake kulikuwa na mtu.
Matukio ya mauaji ambayo yalitokea mfululizo tena yote yakiwa yakiwahusu viongozi yalionekana kumchanganya kila mtu. Viongozi walitakiwa kuwa makini katika maisha yao ya kila siku hali iliyowafanya kuwaajili walinzi kwa ajili ya kuwalinda katika maisha yao ya kila siku.
Upelelezi ambao bado ulikuwa ukifanyika haukusaidia kitu chochote kile. Mara kwa mara mpelelezi Bugabu alikuwa akiitwa na kuulizwa juu ya mahali ambapo alifikia katika upelelezi wake. Hakuwa na chochote cha kujibu zaidi ya kuomba muda zaidi kwa kuwa kazi ambayo alikuwa akiifanya ilikuwa ngumu tofauti na jinsi ambavyo aliitarajia kabla.
Kila siku waandishi wa habari walikuwa wakielekea katika ofisi ya kamanda mkuu wa jeshi la polisi, Bwana Ngomale huku lengo lao likiwa ni kutaka kufahamu ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea kuhusu muuaji ambaye bado alikuwa akiendeea kuua viongozi wa Serikali.
Bwana Ngomale hakuwa na cha kuongea zaidi ya kuwataka Watanzania wawe wavumilivu kwa kuwaambia kwamba kila kitu kilikuwa kikiendelea kama kilivyopangwa na baada ya muda fulani basi muuaji angeweza kutiwa nguvuni na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Kila siku Watanzania walikuwa wakiendelea kulalamika katika vyombo vya habari kwa kudai kwamba mapolisi walikuwa wameshindwa kumtia nguvuni mtu huyo ambaye bado alikuwa akiendelea kufanya mauaji kuwaua viongozi.
Magazeti ya udaku hayakuishiwa na habari, kila siku yalikuwa yakiandika habari mbalimbali kuusiana na muuaji huyo, huku hata siku nyingine wakithubutu kusema kwamba muuaji alikuwa akikaribia kujulikana, hiyo yote ilikuwa ni njia mojawapo ambayo iliyafanya magazeti yao kununuliwa kila siku.
Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa akimfahamu muuaji ambaye alikuwa amehusika na mauaji yale ya kutisha. Kila siku tetesi zilikuwa zikiendelea kusikika mitaani lakini kiukweli hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa akiufahamu ukweli.
Mpelelezi Bugabu bado alikuwa akiendelea na upelelezi wake kama kawaida, kila siku alikuwa akihakikisha anaandika kitu chochote kuhusiana na mambo yote ambayo yalikuwa yakiandikwa magazetini na kuongelewa na watu mbalimbali.
Listi yake ya mauaji ambayo yalikuwa yameitikisa nchi ilikuwa katika mikono yake. Hakutaka kuyawekea maanani mauaji megine ambayo alikuwa ameyaandika katika kitabu chake. Akaanza kuangalia mauaji ya familia ya Bwana Boniface, familia ile ilikuwa imeteketezwa kwa kuchomwa na moto katika ufukwe wa Coco.
Mpelelezi Bugabu hakuishia hapo, akazidi kufuatlia mauajia mengine zaidi, kwa sasa akafikia katika mauaji ya familia ya Bwana Ombeni, nayo kama kawaida ilikuwa imeteketezwa kwa moto. Mpelelezi Bugabu akatikisa kichwa chake juu na chini kwa kuona kwamba upelelezi wake ulikuwa ukienda kufanikiwa.
Akaanza kuyafikiria mauaji ya Bwana Tumaini na familia yake. Mauaji ambayo yalikuwa yamefanyika hayakuwa ya kuchomwa moto, bali yalikuwa ni mauaji ya kupigwa risasi za viafuani na kufa. Hakutaka kuyapuuzia mauaji haya japokuwa yalikuwa tofauti na mauaji mengine.
Akafunga kitabu chake kidogo ambacho kilikuwa na matukio mengi ya mauaji. Akabaki kimya kwa muda huku akionekana kujifikiria. Kuna mauaji mengine yakamjia kichwani, haya yalitokea katika kipindi kirefu cha mwaka mmoja uliopita, haya yalikuwa mauaji ya familia ya Mwandishi Dominick ambayo iliteketezwa kwa moto ndani ya nyumba yao.
Bugabu akakohoa kidogo, akaendelea kufikiria zaidi. Alionekana kuyatilia shaka mauaji yale. Alimfahamu vilivyo Dominick kama mwandishi bora ambaye alikuwa akiandika mambo mengi tofauti tofauti ambayo yalikuwa yakifichua maovu mengi.
Familia yake pia ikateketezwa kwa moto huku baadae nae akisadikiwa kuuawa baada ya kutekwa na wauaji. Kuna vitu ambavyo alitamani sana kuvifahamu kuhusiana na mauaji haya yote ambayo yalikuwa yametokea. Kwanza alitaka kufuatilia makaburi ambayo maiti za familia zote zile zilipozikwa hata kabla hajaamua ni hatua gani ambayo ingefuata baada ya hapo.
Bugabu akaanza kuelekea katika makaburia ambayo yalizikiwa miili ya familia za viongozi. Aliyaangalia kwa muda mrefu na kisha kuondoka zake. Akaanza kuelekea katika makaburi ya familia ya Dominick, kidogo Bugabu akapigwa na mshtuko mara baada ya kuona maua yakiwa juu ya makaburi mawili, kaburi la Christina na Ibrahim.
Bugabu hakuishia hapo, aliendelea na uchunguzi wake, moja kwa moja akaelekea katika kaburi la Dominick ambalo wala halikuwa mbali kutoka pale yalipokuwa makaburi yale mawili, alipolifikia, akaanza kuliangalia, hakukuwa na ua lolote jambo ambalo likaanza kumtia mashaka.
“Kuna kitu hapa. Kazi yangu itaanzia hapa”  Bugabu alisema.
                                                                      ************
 Mawaziri wakaonekana kuogopa, matukio ya mauaji ambayo yalikuwa yametokea kwa mawaziri wenzao yalionekana kuwatisha kupita kawaida. Kila waziri akahakikisha kuandaa ulinzi wa kutosha katika maisha yake ya kila siku.
Wasiwasi ukaanza kuwatawala hasa wale mawaziri kutoka katika chama tawala cha Republic. Kila mmoja alikuwa na hofu kubwa, mauaji yalionekana kuwatisha kupita kawaida.
Mawaziri wawili, Bwana Ombeni na Boniface ndio ambao walikuwa na wasiwasi zaidi. Tayari walikuwa na uhakika kuwa Dominick ndiye ambaye alikuwa amehusika katika mauaji yote ambayo yalikuwa yametokea. Kila siku walikuwa wakijiuliza njia ambazo alizitumia Dominick katika kuwatoroka vijana ambao walikuwa wamewatuma.
Tayari Dominick akaonekana kuwa mtu hatari katika maisha yao, hawakutaka kuongea na waandishi wa habari kuhusu habari yoyote ya Dominick kwa kuogopa maswali zaidi. Kila Mtanzania alijua kwamba Dominick alikuwa ameuawa na watu wasiojulikana, ingekuwaje kama wangesema kwamba Dominick aikuwa hai na ndiye ambaye alikuwa amehusika katika mauaji yote?
Jambo lile la kuwaeleza waandishi wa habari likaonekana kuwa gumu kwa upande wao, kitu ambacho walitakiwa kukifanya kwa wakati huo ni kuyalinda maisha yao kwa kuwaita vijana ambao wangekuwa wakiwalinda usiku na mchana.
Waliogopa maswali kutoka kwa Watanzania juu ya Dominick kama tu wangejaribu kuwaambia kwamba mambo yale yote ambayo yalikuwa yakifanyika yalikuwa yakifanywa na Dominick. Walijuaje kama Dominick ndiye ambaye alikuwa akifanya mauaji yale? Na kwa nini alikuwa akiwauwa mawaziri tu na familia zao na si watu wengine?. Kila walipokuwa wakiyafikiria maswali yale, wakaamua kubaki kimya huku wakijihakikishia ulinzi katika maisha yao.
                                                             *************
Ukimya ulikuwa umetawala katika nyumba hii kana kwamba ndani hakukuwa na mtu yeyote yule. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akizunguka zunguka katika eneo la nyumba ile zaidi ya mlinzi ambaye alikuwa na bunduki katika mkono wake wa kulia.
Giza lilikuwa kubwa huku saa zikisoma kwamba tayari ilikuwa imetimia saa saba usiku. Milio ya mbwa kutoka katika nyumba nyingine za jirani ndio ambayo ilikuwa ikisikika kwa wingi mahali hapo. Mara mwanga wa taa ukaanza kuonekana ukimulika, kwa haraka sana mlinzi akaanza kulisogelea geti na kisha kufungua kitundu kidogo kilichokuwa getini.
Gari aina ya Range ilikuwa imesimama nje. Honi mfululizo zikaanza kusikika kutoka katika gari lile. Bwana Boniface akatoka kutoka ndani ya nyumba yake. Mwili wake ulikuwa ukitetemeka kupita kiasi. Alionekana kuwa na shauku ya kutaka kufahamu kitu kimoja mahali hapo.
Akampa mlinzi ishara ya kufungua geti lile. Mlinzi akafanya hivyo, geti likafunguliwa na gari lile kupita. Mwanaume mmoja ambaye alikuwa na mwili uliokuwa umejazia akateremka kutoka garini na moja kwa moja kumfuata Bwana Boniface na kuongea nae kwa sekunde kadhaa.
Mwanaume yule akaufuata mlango wa nyuma wa gari lile na kisha kuufungua. Mwanaume mwingine akateremka kutoka garini. Kichwa chake hakikuwa na nywele kabisa. Ndevu nyingi zilikuwa kidevuni mwake huku akiwa amevaa miwani ya jua.
Alionekana kuwa kama daktari, hii ilitokana na koti refu jeupe ambalo alikuwa amelivaa pamoja na mashine ya kusikilizia mapigo ya moyo. Bwana Boniface akaanza kumwangalia daktari yule kwa macho yaliyokuwa na shauku ya kutaka kufahamu kile ambacho kilikuwa kinatarajiwa kuongea kutoka kwa mtu huyo.
Mara baada ya kusalimiana, akamkaribisha ndani. Mwanaume yule ambaye alijitambulisha kama dokta Pius akaingia ndani pamoja na Bwana Boniface na yule mwanaume ambaye alionekana kuwa mlinzi wa Bwana Boniface.
“Umenishangaza sana” Bwana Boniface alimwambia dokta Pius.
“Huo ndio ukweli. Ni ukweli kabisa ambao wala hautakiwi maswali yoyote yale” Dokta Pius alimwambia.
“Kwa hiyo una uhakika kwamba mtu anayefanya mauaji haya ni Dominick?” Bwana Boniface aliuliza.
“Asilimia mia moja”
“Umejua vipi?”
“Nilisoma nae shuleni. Ninafahamu mambo mengi sana. Alikuwa akiniamini sana mpaka alipoanza kazi. Alinieleza kila kitu kuhusiana na ninyi jinsi mlivyoiteketeza familia yake” Dokta Pius alimwambia.
Bwana Boniface akashusha pumzi ndefu. Hakuonekana kuamini kama kweli kulikuwa na mtu mwingine zaidi ya Dominick ambaye alikuwa akifahamu kila kitu kilichokuwa kimetokea. Tayari aliiona siri ambayo ilikuwa maishani mwao ikiwa imeanza kuvuja.
Alimwangalia dokta Pius mara mbili mbili huku akionekana kutokuamini. Akasimama na kuanza kutembea tembea mahali pale huku akionekana dhahiri kuchanganyikiwa. Tayari hatari ikaonekana kuanza kumnyemelea, akaanza kuwakumbuka waandishi wa habari kwa kuona kwamba ni lazima habari ile ingeenea na hivyo kuitoa katika vyombo vya habari.
“Naomba msaada wako” Bwana Boniface alimwambia dokta Pius.
“Msaada gani?”
“Yaani haujanielewa? Sitaki siri hii ifichuke. Nahitaji iendelee kuwa siri” Bwana Boniface aimwambia dokta Pius.
“Kuna kitu labda unatakiwa kukifanya”
“Kitu gani?”
“Kumuua Dominick. Hilo ndilo suruhisho la mwisho”
“Sawa. Ila nitaweza vipi kumuua? Sipajui sehemu alipojificha. Yaani sifahamu chochote kile”
“Usijali. Nitakusaidia. Anaishi hotelini kwa sasa” Dokta Pius alimwambia Bwana Boniface.
“Unaijua hoteli yenyewe?”
“Naifahamu. Huwa ninawasiliana nae mara kwa mara. Na sasa anataka kukua wewe na kisha kumuua Bwana Ombeni” Dokta Pius alimwambia Bwana Boniface.
“Mungu wangu! Yupo hoteli gani?”
“La Vista Inn pale Magomeni”
“Sawa. Inatubidi twende. Naomba unisaidie kumuua. Ninakuahidi kukupa kiasi chochote ukitakacho” Bwana Boniface alimwambia dokta Pius.
“Sawa. Kajiandae. Nitakusaidia kila hatua” Dokta Pius alimwambia Bwana Boniface ambaye akanyanyuka na kuanza kuelekea chumbani kwake.
Dokta Pius akabaki sebuleni pale huku akionekana kuwa na mawazo. Mara baada ya kutulia kwa sekunde kadhaa, akainuka na kisha kuanza kuelekea ndani ya chumba cha Bwana Boniface ambako alikuwa amekwenda kujiandaa. Dokta Pius alionekana kuwa mtu mwema ambaye alidhamiria kumsaidia Bwana Boniface.
MWANDISHI: NYEMO CHILONGANI
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

UNDANI KIFO CHA MKE WA ALI CHOKI

$
0
0
Majonzi! Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ali Choki amepata pigo kubwa la kufiwa na mkewe, Shuea Hamis ‘Mama Shuu’ baada ya kuugua kwa muda mrefu.
 
Aliyekuwa mke wa Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ali Choki, marehemu Shuea Hamis ‘Mama Shuu’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa masikitiko, Choki alisema kwamba mke wake ameugua kwa muda wa miezi tisa akisumbuliwa na tatizo la mguu.
Alisema kwamba katika jitihada za matibabu, mkewe huyo alitibiwa nchini India ikashindikana, akarudishwa nyumbani mpaka mauti yalipomfika usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita.
“Kweli alikuwa akipata mateso makubwa kwani alikuwa hatembei analala tu ndani hivyo kutoa nafasi kwa magonjwa mengine kumshambulia.
“Ukweli nimeumia kwani alikuwa ni mshauri wangu mkuu na ndiye alikuwa kila kitu kwangu.
“Alikuwa akinisapoti sana kwenye kazi yangu ya muziki lakini ndiyo hivyo Mungu amempenda zaidi sina la kufanya,” alisema Choki kwa majonzi.
 
Ali Choki akiwa kwenye picha ya pamoja na mkewe enzi za uhai wake.
Choki alisema mipango ya mazishi ilifanyika nyumbani kwake Tuangoma, Kigamboni jijini Dar na mazishi ya mkewe yalitarajiwa kufanyika jana Jumapili, saa 10:00 jioni katika Makaburi ya Maduka-Mawili, Chang’ombe, Dar.
Mama Shuu alikuwa mdau mkubwa wa muziki wa dansi Bongo hivyo ni pigo kubwa kwa tasnia hiyo. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.

USIKU WA KIGODORO - 10

$
0
0

Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

ILIPOISHIA :Mimi sijawahi kumwona ila kuna wakati Semi alikuwa anafukuzia mkopo mkubwa benki, Lina alikuwa mmoja wa watu wanaotakiwa kutia sahihi kwenye fomu. Kwa sababu tulikuwa tukienda benki kila siku nikalizoea hilo jina.
“Halafu juzi nadhani, nilikwenda kuchukua mzigo wangu ofisini kwa huyo Lina aliuacha mumewe, huyo Semi…”
JIACHIE SASA…

“Kindaundau,” aliita James akiwa na sura yenye mshangao...
“Naam bosi.”
“Unasema?”

“Ndiyo hivyo, jaribu kuchunguza nini kinaendelea kati yenu.”
James alikuwa kama ameganda kwa muda akiwaza, akaangalia juu, kulia na kushoto kisha akamwangalia Kindaundau…

“Kuna mambo unayasema kama yana ukweli fulani. Mfano, unalitaja jina la Semi, naamini kama ni Lina mke wangu, amemsevu kwa jina la Bro Semi…lakini hebu nikuulize Kindaundau…wewe ndiye ulikwenda kuchukua huo mzigo kazini kwa Lina halafu ulimkuta mlinzi?”
“Ndiyo.”

“Halafu uliongea kwa simu na Lina akiwa hayupo kazini?”
“Ndiyo mimi. We umejuaje kwanza? Halafu umenikumbusha kitu James…baada ya mimi kuongea na Lina tu, wewe ukanipigia simu.”

“Ndiyo! Nilikuwa naye mimi alipomuuliza jina lako mlinzi akalitaja la Kindaundau nikakukumbuka na yeye Lina nilimwambia huyo mtu Kindaundau namjua na namba zake ninazo ndiyo maana nikakupigia.”
“He! Kumbe!”

“Mimi nashukuru sanasana ndugu yangu Kindaundau kwa kunihabarisha hili japokuwa nimeumia sana. Lina! Mke wangu, kumbe  ana mume mwingine? Ina maana mimi si mume halali? Siamini hata kidogo. Da! Nitaua mwaka huu Mungu nasema, siwezi kuwa mwanaume bwege mimi.”
“James acha jazba.”

“No Kindaundau. Mimi ni mtu na pesa zangu. Anapotokea mwanamke anakufanyia hivi unadhani nini kitatokea hapo?”“Ni kweli kinaweza kutokea kikubwa. Lakini mimi nakushauri…”

“Unanishauri nini Kindaundau, we umeshaniambia niachie mimi. Kwanza huyo Lina kaniambia anakwenda kumwona mama yake Korogwe anaumwa. Kuna uwezekano hajasafiri…hebu mpigie huyo Semi muulize kiaina ujue mkewe yuko wapi?”

“Da! Bwana James, unavyodhani inawezekana kweli nikamuuliza swali kama hilo?”
“Naamini ukiongea naye mawili matatu atasema jambo ambalo litakupa mwanga.”
“Sawa, ngoja nijaribu.”
Kindaundau alimpigia simu Semi akiwa ameweka loud speaker…
“Hujambo bwana Semi?”

“Sijambo, vipi Kindaundau? Mzima wewe?”
“Mimi mzima bwana. Uko nyumbani nini? Maana wakubwa kama nyinyi si ajabu uko nyumbani na shemeji mnakula bata tu.”

“Nipo mkoa bwana, maisha haya bila kutafuta huwezi kuyamudu kaka.”
“Shemeji vipi? Umesafiri naye?”
“Hamna, yuko kazini saa hizi.”
“Poa, nilidhani upo Dar nikupe dili, basi ukirudi nitafute tuongee.”
“Sawa mkuu.”

Baada ya kukata simu, Kindaundau na James walitazamana…
“Kazini hayupo maana mimi nimetokea huko,” alisema James…
“Basi atakuwa amesafiri kweli?” alisema Kindaundau…

“Haiwezekani asafiri halafu huyo Semi asijue, ni ngumu.”
“Mh! Mpigie basi umuulize aliko.”
“Hapana, nitamshtua mapema sana. Mimi nataka niende naye polepole hadi aingie kwenye kumi na nane yeye mwenyewe.”

“Na kweli, ni wazo zuri sana. Ukifanya papara unaweza kupoteza ushahidi lakini ukienda naye polepole itafika mahali kila kitu kitakuwa kweupe.”

Baada ya hapo, waliagana lakini James hakutaka kuondoka na kumruhusu Kindaundau kuanza kutoka. Nyuma, James alizama kwenye kumfikiria Lina kama habari alizozipata ni za kweli!

“Mimi nahisi Kindaundau amechanganya majina. Siku hizi majina yanafanana sana. Unaweza kuwapata Lina Joseph Ambakucha hata saba, tatizo liko wapi? Na kama kweli ni Lina mke wangu, kwa nini amsevu mumewe kwa jina la Bro Semi…

“Halafu, mpaka nifunge ndoa na mke wake, yeye Semi alikuwa wapi? Tena ndoa ilitangazwa kwa siku ishirini na moja kanisani. Itakuwa si kweli.”

Hata hivyo, nyuma ya mawazo yake hayo, James alipata mawazo mengine yanayompa ushahidi kuwa ni kweli Lina aliyemsema Kindaundau ndiyo Lina wa Semi.

“Lakini si nilimsikia Lina akizungumza na mlinzi wa kazini kwake na akamtaja Kindaundau? Inawezekana ikawa ni Lina huyu kweli. Hata mahudhurio yake kwenye fungate hayakuwa mazuri, lakini ninavyojua mimi mwanamke akishafunga ndoa kukaa honeymoon ni kazi ndogo, sasa yeye kila siku alikuwa akitoa sababu.”

***
Lina alitoka kazini jioni na kurudi nyumbani kwake kwa Semi lakini huku akiwa na wasiwasi kwamba, endapo James atampigia simu na kutaka kuzungumza na mama yake atampa nani, maana mama mpika chai alikuwa ameshaachana naye.

Pia alishangaa sana kwani James hakumpigia simu kwa muda mrefu wakati si kawaida yake.
Alifika nyumbani kwa Semi na akili moja tu kwamba, James akipiga simu asipokee kesho yake akienda kazini ndiyo atampigia na akitaka kuzungumza na mama yake atampa mama wa chai.
***
Ilikuwa usiku wa saa tano Lina akiwa kitandani kwake na kanga moja tu, James hakumpigia simu. Akaingiwa na wasiwasi, akampigia akiamini kwamba kama atataka kuongea na mama yake atamwambia amashalala. Simu ya James iliita mara nane bila kupokelewa…
“Mh! Kuna kitu,” alisema Lina akianza kuogopa. 
Usiku ulipita lakini Lina hakupata usingizi kwani kila wakati alikuwa akishtuka na kuiangalia simu yake kama ataona missed calls au meseji za James…
“Hivi huyu ana nini? Mbona si kawaida yake?” alijiuliza Lina huku akiwa na mawazo kibao kichwani mwake.
***
Kulikucha,  Lina alitoka kitandani huku mwili ukikataa kwani hakuwa amepata usingizi mzuri usiku uliopita kwa kumuwaza James.
Alijiandaa kwenda kazini huku akili ikimwambia ni siku nyingine ya mpambano ambapo itabidi atumie akili sana kuwepo kazini ili asibambwe na James.
Alipofika kazini tu, alipitiliza hadi kwenye chumba cha mama mpika chai…
“Shikamoo mama nanihi…”
“Marhaba, mbona leo upo kama umechoka sana?”
“Ni kweli kabisa. Yaani sijalala.”
“Kisa?”
“Kisa ni James. Toka jana hajanipigia simu wala kunitumia meseji, nimempigia simu hajapokea. Mpaka kunakucha hajawasiliana na mimi.”
“Unahisi nini?”
“Nahisi kuna kitu.”
“Kitu kama kipi?”
“Nahisi ameambiwa mchezo na mtu.”
“Mchezo gani?”
“Si kunioa mimi wakati nina ndoa nyingine?”
Lina hakutaka kujadili sana na mwanamke huyo, akatoka kwenda kwenye meza yake ambapo alikaa akitupa macho getini. Uzuri wake, meza yake akikaa alikuwa akiliangalia geti kwa mbele hivyo, mtu yeyote aliyeingia ilikuwa lazima amuone.
Aliwasha kompyuta lakini ile anaanza kushika makaratasi tu, James aliingia getini, Lulu akatoka mbio hadi kwenye chumba cha mama mpika chai…
“Kaja…kaja, ndiyo anaingia…”
“Nani?”
“Si James!”
“Kwa hiyo?”
“Naomba uende mama. Mpaka atakapoondoka ndiyo urudi.”
“Chai?”
“Nitapika mimi.”
Mama huyo alitoka, akamkuta James ndiyo anaingia mapokezi…
“Karibu sana.”
“Asante. Za kazi?”
“Kazi nzuri.”
“Naona bibie hajarudi.”
“Ee, bado.”
“Oke. Meneja yupo?”
“Yupo ofisini kwake.”
James alipitiliza hadi ofisini kwa meneja huyo.
Baada ya dakika tano, meneja alitoka peke yake na kwenda hadi kwenye chumba cha jiko…
“Lina yuko huku?” aliuliza akifungua mlango.
“Nipo bosi, nakunywa chai.”
“Leo chai unanywea huku?”
“Nimeona ninywee huku bosi.”
“Kuna mgeni kule kwangu, mletee maziwa ya moto bila sukari wala kitafunwa,” alisema bosi huyo huku akitoka. Lina alitazamana na mwanamke huyo kisha akasema…
“Siri inafichuka sasa. Nifanyaje mama nanihi?”
“Mh! Sijui mwenzangu. Na wageni wa kwa mabosi wewe ndiyo unayetakiwa kuwapelekea mahitaji yao, nikienda mimi si itakuwa balaa? Si unakumbuka siku ile nilipeleka kahawa kwa mhasibu wakaniwakia?”
Lina alianza kulia. Aliandaa maziwa huku machozi yakimchuruzika mashavuni, moyoni aliilaani sana siku ya kwanza kukutana na James ambapo ilikuwa kwenye ofisi hiyohiyo.
Alibeba maziwa hayo yaliyokuwa katika kikombe cha dongo na kukiweka kwenye sinia na kwenda nayo. Alipofika mlangoni alisimama, akasali kwa muda kisha akafungua mlango na kuzama ndani.
James alikuwa ameinama akisoma Gazeti la Daily News ambalo ni pana sana hivyo alilishika pembe ya kulia na kushoto kiasi kwamba hakuinua macho kumwangalia Lina.
Lina aliweka sinia na kutoka haraka sana na wakati anafunga mlango akageuka kumwangalia James, bado alikuwa amezama kwenye kusoma gazeti hilo.
Hakuondoka, akasimama na kuchungulia ndani kupitia tundu za funguo kwenye kitasa, akamwona James akiweka gazeti mezani na kupeleka mkono kwenye kikombe cha maziwa.
“Kwa hiyo ile fedha iliyozidi nikupe wewe au mista Brown?” aliuliza James, Lina akaondoka zake. Aliingia kwenye chumba cha chai na kumkuta mama mpika chai akimsubiri kwa hamu kubwa.
“Enhe? Imekuaje?”
“Huwezi amini, nimeshinda mtihani mmoja, bado wa pili. Nimeingia, nimeweka maziwa, nimetoka James hajaniona. Kainama anasoma gazeti.”
“Kweli?”
“Kweli kabisa, sasa nasubiri kwenye kutoa sinia na kikombe.”
“Kwanza unatakiwa urudi mapokezi, uliona bosi amekuja huku ina maana amekupigia simu sana mapokezi hukupokea.”
“Mh! Huo ni mtihani mwingine,” alisema Lina akionekana ana wasiwasi kupita kawaida.
Baada ya nusu saa akiwa bado kwenye jiko, alisikia simu ya mapokezi inaita…
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
 

ITAENDELEA SIKU YA KESHO

DIAMOND AMKUBALI PETIT MAN

$
0
0

HESHIMA! Tofauti na ilivyokuwa ikifikiriwa na wengi kwamba hamkubali shemeji yake, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameonyesha kumkubali shemeji yake Ahmed Hashimu ‘Petit Man’ hadharani.
 
Shemeji wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Ahmed Hashimu ‘Petit Man’ akiwa na 'waifu tu bi'.
Hivi karibuni uvumi uliibuka kuwa Diamond hakufurahishwa na kitendo cha dada’ke kuolewa na Petit ndipo msanii huyo alipoamua kukata ‘vilimilimi’ kwa kusema uvumi huo hauna ukweli katika sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika Oktoba 2, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Tower, Posta jijini Dar.
“Kwa bahati mbaya dada yangu Esma anaumwa hajafika humu ndani, sasa kwa kuwa sasa hivi ameolewa na mtu ninayemkubali, namuita mumewe, shemeji yangu ninayemkubali, Petit Man aje kula keki badala yake,” alisikika Diamond.

SERENGETI FIESTA 2014 YAFUNIKA DODOMA

$
0
0
 
Msanii wa Bongo Fleva, Baba Levo akitumbuiza kwa staili yake kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2014 Dodoma usiku wa kuamkia leo.
 
Mo Music akitoa burudani kwa wakzi wa Dodoma waliyofulika kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
 
Msanii zao la Serengeti Super Nyota G-Lucky akifanya makamuzi ndani ya uwanja wa Jamhuri Dodoma.
 
Y-Tony akiwajibika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta lililokuwa likifanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
 
Chipukizi wa Bongo Fleva, Baraka Da Prince akiwajibika jukwaani.
 
Msanii zao la nyumba ya kukuza vipaji Tanzania (THT), Kadja Maumivu akipagawisha kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2014, usiku wa kuamkia leo.
 
Young Killer akimwaga mistari ya Hip Hop kwa mashabiki waliyojitokeza kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 lililokuwa likifanyika ndani ya Uwanja wa Jamhuri  mjini Dodoma.
 
Mr Blue akifanya yake jukwaani.
 
Recho akiimba jukwaani huku mmoja wa wanenguaji wake akiwajibika kwa staili kali.
 
Mkongwe wa Bongo Fleva, Dully Sykes akipagawisha jukwaani.
 
Vanessa Mdee katikati akipagawisha kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta ndani ya Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
 
Jux akikamua jukwaani.
(PICHA NA MUSA MATEJA/GPL, DODOMA)

UTEKAJI WATOTO WATIKISA DAR

$
0
0
Stori: Makongoro Oging’
MUNGU wangu! Lile sakata la utekaji na upoteaji wa watoto ambao wengi ni wanafunzi wa shule za msingi katika Jiji la Dar na kudaiwa linafanywa na watu walio kwenye magari aina ya Toyota Noah limeingia katika sura nyingine.
Wanafunzi wa shule ya msingi wakitoka madarasani baada kutokea kwa hali ya vurugu.
Safari hii, gari moja lilitupiwa mawe na dereva nusura kuuawa kufuatia kufika katika Shule za Msingi za Kombo na Mtakuja zilizopo Vingunguti, Dar kwa lengo la kuzungumza na walimu kuhusu mikopo lakini likahofiwa lilikwenda kuteka watoto.
Tukio hilo lilijiri Ijumaa iliyopita na kusababisha vurugu kubwa kati ya wazazi na walimu hali iliyowafanya maafande wa Kituo cha Polisi Buguruni kuwasili katika eneo la tukio ili kutuliza ghasia na kwanusuru walimu.
Mmoja wa walimu akiwa na wanafunzi hao.
UWAZI ENEO LA TUKIO
Gazeti hili lilifika eneo la tukio muda mfupi na kuwakuta walimu wakiwa chini ya ulinzi wa polisi ili wasishambuliwe na wazazi ambao walivamia shule wakidai kwamba watoto watatu walitekwa na watu wenye Noah jeusi.
SABABU YA VURUGU
Vurugu hizo zilizoanza saa nne asubuhi siku hiyo zilitokea baada ya gari moja jeusi aina ya Toyota Noah kufika shuleni hapo na kushambuliwa na wananchi wakidai kwamba ndilo linalotumika kuwatekea watoto wao shuleni hapo.
Baadhi ya wazazi na wananchi wakiwa wametanda eneo la Shule za Kombo na Mtakuja zilizopo Vingunguti, Dar.
Mmoja wa wazazi aliyejitambulisha kwa jina la Huma Selemani alisema Noah hilo la mikopo kwa walimu lililokuwa na vioo vyeusi lilihisiwa ni la utekaji baada ya jana yake (Alhamisi) ambapo gari kama hilo lilifika shuleni hapo na dereva kumuuliza mmoja wa wanafunzi sehemu ambapo mwanafunzi huyo akasema haijui.
Ilidaiwa kuwa, pamoja na denti huyo kusema haijui  sehemu hiyo walimchukua na kumuingiza ndani ya gari hilo ili kuondoka naye lakini mzazi mmoja aliona na kupiga kelele huku akilishambulia kwa mawe gari hilo hadi walipomshusha mwanafunzi huyo na wao kutimka.
Maafande wa Kituo cha Polisi Buguruni wakiwa eneo la tukio kutuliza ghasia.
WANAFUNZI WATOKA MADARASANI
Mayowe hayo yaliwafanya wazazi kuvamia shule hizo na kusababisha wanafunzi kutoka madarasani huku wengine wakiruka ukuta na kukimbilia majumbani na baadhi kwenda kusikojulikana.
Wazazi waliokuwa karibu na shule hizo walifika na kuwachukua watoto wao kisha kwenda nyumbani huku wengine wakitegemea msaada toka polisi ambao walipofika walifyatua risasi hewani kuwatawanya wananchi hao.
Walimu wakipandishwa gari kurudishwa makwao.
MANENO YA WALIMU
Hata hivyo, walimu wakuu wa shule hizo hawakupatikana mara moja lakini mwalimu mmoja ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alisema hakuna utekaji wa watoto shuleni bali baadhi ya watu wamekuwa wakivumisha habari hizo na hivyo kuwatia hofu watoto.
MADAI YA WATU
Baadhi ya watu walioongea na gazeti hili walisema kuwa, wana taarifa mbaya kwamba watekaji hao wakishawapata watoto huenda kuwaua ili kutwaa viungo vyao kwa ajili ya ushirikina wa kupata utajiri.
Baadhi ya walimu wakilindwa na maafande wasishambuliwe na wazazi waliovamie shuleni hapo.
UONGOZI WA MTAA
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kombo, Jastin John Chiganga alipohojiwa alikiri kutokea kwa vurugu hizo hali iliyomfanya awaite polisi kutuliza ghasia lakini alisema kwa upande wa kutekwa watoto na gari aina ya Noah hajawahi kusikia.
“Shule ilibidi ifungwe, watoto waruhusiwe kutawanyika hadi hapo taarifa itakapotolewa. Hata hivyo, wazazi wameniomba kwamba kabla watoto wao hawajarejea shuleni hapo anatakiwa kiongozi wa juu, awe DC (mkuu wa wilaya) au yeyote afike kutoa tamko na kuweka mambo ili kuwatoa hofu wazazi na wanafunzi,” alisema mwenyekiti huyo.
Mwanafunzi Hadija Hansi (10) wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Magomeni, Dar aliyepotea.
Polisi wa Buguruni waliokuwepo kwenye tukio hilo walisema hawana taarifa ya watu waliojeruhiwa au  kukamatwa bali zoezi la kudhibiti amani lilifanyika kwa uangalifu wa hali ya juu.
Wakati huohuo, wazazi wa mwanafunzi Hadija Hansi (10) anayesoma darasa la nne Shule ya Msingi Magomeni, Dar wanahaha kumtafuta mtoto wao huyo ambaye alitoweka katika mazingira ya kutatanisha ikidaiwa alitekwa na Noah.
Mfano wa gari la Noah linaloshukiwa kuhusika na utekaji wa watoto
Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita, Zena Amour ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo alisema mwanaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha Septemba 30, mwaka huu wakati akicheza na wenzake na ameshamtafuta katika vituo vya polisi jijini kikiwemo cha Tandale TAND/RB/1059/2014 na hospitali zote bila mafanikio.

A JOURNALIST IS BACK (MWANDISHI AMERUDI) - 11

$
0
0





MWANDISHI: NYEMO CHILONGANI
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

Nitakusaidia. Anaishi hotelini kwa sasa” Dokta Pius alimwambia Bwana Boniface.
“Unaijua hoteli yenyewe?”
“Naifahamu. Huwa ninawasiliana nae mara kwa mara. Na sasa anataka kukua wewe na kisha kumuua Bwana Ombeni” Dokta Pius alimwambia Bwana Boniface.
“Mungu wangu! Yupo hoteli gani?”
“La Vista Inn pale Magomeni”
“Sawa. Inatubidi twende. Naomba unisaidie kumuua. Ninakuahidi kukupa kiasi chochote ukitakacho” Bwana Boniface alimwambia dokta Pius.
“Sawa. Kajiandae. Nitakusaidia kila hatua” Dokta Pius alimwambia Bwana Boniface ambaye akanyanyuka na kuanza kuelekea chumbani kwake.
Dokta Pius akabaki sebuleni pale huku akionekana kuwa na mawazo. Mara baada ya kutulia kwa sekunde kadhaa, akainuka na kisha kuanza kuelekea ndani ya chumba cha Bwana Boniface ambako alikuwa amekwenda kujiandaa. Dokta Pius alionekana kuwa mtu mwema ambaye alidhamiria kumsaidia Bwana Boniface.

Kila siku Dominick alikuwa akiwaza jinsi ya kufanikisha pango wake wa kuwaangamiza wabaya wake ambao walimpa majeraha moyoni mwake. Hakutaka kuwaacha wakiwa hai, alijiona kukosa amani kila alipokuwa akijifikiria kuwaacha.
Kitu alichokifanya Dominick kwa wakati huo ni kuanza kutafuta urafiki na dokta Silyvester wa zahanati ya St’ Maria iliyokuwa Magomeni. Kila siku alikuwa akifika hospitalini hapo huku akionekana kubadilika kupita kawaida. Kichwa chake hakikuwa na nywele kabisa, alivaa ndevu za bandia ambazo ilikuwa ni jambo gumu sana kumgundua.
Siku ziliendelea kwanda mbele huku ukaribu wake na dokta Silyvester ukizidi kukua kila siku. Ndani ya mwezi mmoja tu, wakawa wamezoeana kana kwamba walikuwa wamefahamiana kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.
Dominick akawa akitumia muda mwingi sana kuonana na dokta Silyvester ambaye alikuwa akimkaribisha sana katika zahanati yake. Hakuwa na hofu kabisa na Dominick na wala hakufahamu kwamba kulikuwa na kitu ambacho Dominick alikuwa akikihitaji kutoka kwake.
Kitu ambacho alikuwa akihitaji Dominick ni mashine ya kusikilizia mapigo ya moyo tu. Hakuwa na shida ya kutafuta koti la daktari kwani aliamini kama angetumia koti lolote la muuza nyama buchani basi ilikuwa ni lazima mtu yeyote afahamu kwamba alikuwa daktari wa hospitali fulani.
“Nataka unifundishe mengi kuhusu udaktari” Dominick alimwambia dokta Silyvester.
“Kama kipi Pius?”
“Kwanza hii mashine. Unajua inaonekana kuwa mashine ya kawaida sana lakini kwa mtu kama mimi inaweza kuwa tofauti na ninavyodhani” Dominick alimwambia dokta Silyvester ambaye akaanza kumulekeza Dominick kuhusiana na mashine ile.
Dominick alijifanya kuwa msikivu wa hali ya juu. Dokta Silyvester aliendelea kumuelekeza kila kitu kuhusiana na mashine ile. Dokta Silyvester hakumfundisha kuhusiana na mashine ile tu bali aliendelea kumfundisha na mambo mengine pia.
“Hivi inauzwa?” Dominick aliuliza.
“Ndio. Hasa katika maduka makubwa ambayo yanauza vifaa mbalimbali vya hospitalini” Dokta Silyvester alimwambia.
Dominick hakuona ugumu wowote ule, tayari akawa na matumaini ya kuweza kuipata mashine ile. Akaulizia kuhusu gharama ya mashine ile na kisha kutaka kufahamu maduka ambayo yalikuwa yakiuza mashine zile. Alipopata maelekezo ya kutosha, kesho yake akapaelekea kununua.
Akarudi katika chumba ambacho alikuwa amepanga na kutulia. Akaanza kuangalia mashine ile pamoja na koti, vitu vyote hivyo alikuwa amevinunua kutoka katika maduka ya vifaa vya madaktari katika duka moja kubwa lililokuwa Mwenge.
Dominick akachukua simu yake ya mkononi na kuchukua line ya simu mpya, akaingiza salio na kisha kupiga namba za Bwana Boniface. Simu ikaanza kuita, iliita kwa zaidi ya dakika moja, wala haikupokelewa. Hakukata tamaa, aliendelea kupiga zaidi na zaidi, baada ya muda, simu ikapokelewa.
“Unasemaje?”
“Ndio hivyo mzee. Yaani nimeshtuka sana aliponiambia” Dominick alimwambia Bwana Boniface.
“Habari zako zimenishtua sana, naomba tuonane ili tuweze kuliongea hili” Bwana Boniface alimwambia huku akionekana kuwa na wasiwasi.
“Haitowezekana kuonana na mimi. Nina majukumu mengi ya kazi. Nimejaribu kukwambia ili tu ujue jinsi gani utaweza kujilinda” Dominick alimwambia Bwana Boniface.
“Nahitaji msaada wako. Najua kutakuwa na mambo mengi unayafahamu. Naomba tuonane. Nakuomba kukuona dokta Pius” bwana Boniface alimwambia Dominick.
“Kila kitu fedha. Kila kitu fedha mzee wangu”
“Nalifahamu hilo. Naomba tuonane, kuhusu fedha si tatizo kwangu. Ninachotaka ni kuonana nawe tu” Bwana Boniface alimwambia Dominick.
“Sawa. Kama kuonana, nitahitaji kuonana nawe usiku, kwa mchana haitowezekana kabisa kutokana na ubize wa kazi” Dominick alimwambia Bwana Boniface.
“Unafanya kazi katika hospitali gani?”
 
 “Amana”
“Sawasawa. Nitamtuma mtu akufuate hapo muda wowote ule”
“Sawa. Mwambie aje saa tatu usiku. Ila atakapofika, hatakiwi kuteremka kutoka garini. Sitohitaji wafanyakazi wanione nikiongozana na mtu kuelekea katika gari lake.Nitakachokifanya nitawasiliana nae, cha msingi nitumie namba yake ya simu” Dominick alimwambia Bwana Boniface.
“Usijali. Nitakutumia sasa hivi” Bwana Boniface alisema na simu kukatika.
Dominick akabaki katika hali ya mawazo. Kwa kiasi fulani akajiona kuanza kupata mafanikio juu ya kile ambacho alikuwa amepanga kukifanya. Akajilaza kitandani huku akianza kufikiria ni kwa jinsi gani angefanikiwa kufanya kile ambacho alikusudia kukifanya.
Kwanza akainuka kutoka kitandani na moja kwa moja kuanza kuelekea katika droo ya kabati na kisha kutoa bunduki yake, akaanza kuiangalia kwa muda fulani na kisha kuirudisha na kwenda kitandani.
                                                         *********
Simu ya Dominick ambaye alikuwa katika eneo a hospitali ya Amana ikaanza kuita. Akitoa simu ile na kuanza kukiangalia kioo cha simu ile, namba ilikuwa ngeni, hivyo akaonekana kumjua mtu ambaye alikuwa akimpigia muda huo.
Alichokifanya ni kuanza kutembea kwa mwendo wa haraka haraka kuelekea nje ya eneo la hospitali ile huku akiwa na koti refu jeupe pamoja na mashine ya kusikilizia mapigo ya moyo ambayo alikuwa ameizungushia shingoni mwake. Mara baada ya sekunde kadhaa, akafika nje ya eneo la hospitali ile.
Akaanza kuangalia huku na kule, gari aina ya Range ilikuwa imepaki pembeni kabisa. Hakuwa na wasiwasi nalo kwani alikuwa na uhakika kwamba gari ile ndilo ambalo alihitajika kuingia kwa wakati huku. Akaanza kupiga hatua za haraka haraka kulifuata.
“Karibu dokta Pius” Mwanaume mmoja ambaye alionekana kuwa na mwili uliojazia alimwambia Dominick huku akimfungulia mlango.
“Asante” Dominick alijibu huku akiingia ndani ya gari lile na safari ya kuelekea katika nyumba ya Bwana Boniface kuanza.
                                                            **************
Dominick akakigusa kitasa cha mlango wa chumba cha Bwana Boniface na kuufungua mlango. Bwana Boniface alikuwa akijiandaa tayari kwa ajili ya kwenda kumuua Dominick ambaye alikuwa katika hoteli ya La vista Inn. Tegemeo lake kubwa kwa wakati huo lilikuwa kwa dokta Pius ambaye alikuwa amemuacha sebuleni.
Kichwa chake kikaguswa na mdomo wa bunduki. Akaonekana kushtuka kupita kiasi, akaanza kugeuka nyuma, macho yake yakatua katika uso wa dokta Pius. Bwana Boniface akabaki akishangaa pasipo kuelewa ni kitu gani kilikuwa kikiendelea mahali hapo.
Alimwangalia dokta Pius usoni, macho yake yalikuwa mekundu huku machozi yakiwa yanamlenga. Bwana Boniface hakuelewa ni kitu gani kilikuwa kinaendelea mpaka dokta Pius kumnyooshea bunduki. Bwana Boniface akabaki akitetemeka tu.
“Dokta! Vipi tena?” Bwana Boniface aliuliza huku akionekana kuhofia.
“Unachokiona ndicho kinachoonekana” Dominick alimwambia Bwana Boniface.
“Kwa nini unataka kufanya hivi?”
“Kwa sababu ya kisasi. Hiki ndicho kitu nilichokuwa nikikihitaji kwa kipindi kirefu” Dominick alimwambia Bwana Boniface.
“Sijakuelewa. Nimekuita hapa kwa sababu ya kunisaidia…lakini kwa nini unataka kunigeuka? Au Dominick amekutuma?” Bwana Boniface aliuliza.
                                                                  *********
Bado Dominick alikuwa akitokwa na machozi, kila alipokuwa akimwangalia Bwana Boniface ndivyo ambavyo mambo mengi ya nyuma yalivyokuwa yakimiminika kichwani mwake. Alikumbuka vilivyo siku ambayo nyumba yake ilikuwa ikiteketezwa kwa moto na mkewe mpendwa pamoja na mtoto wake kuuawa siku hiyo.
Alijiona kuwa na sababu zote za kumuua Bwana Boniface kama kisasi cha familia yake. Hakutaka kumuacha katika usiku huo, hiyo ilionekana kuwa nafasi kubwa katika maisha yake juu ya kuendelea na zoezi lake lile. Aliendelea kumwangalia Bwana Boniface kwa macho yaliyojaa hasira.
“Ninakuua…ninakuua kwa mkono wangu mwenyewe” Dominick alimwambia Bwana Boniface ambaye muda wote alikuwa akishangaa.
“Dokta Pius….mbona unanifanyia hivi?” Bwana Boniface aliuliza.
Dominick akabaki akimwangalia kwa muda, akaitoa miwani yake na kuiweka katika mfuko wa koti lake na kisha kuzitoa zile ndevu za bandia. Bwana Boniface akabaki akimwangalia Dominick, sura yake wala haikuwa ngeni machoni mwake.
“Najua umekwishawahi kuniona kabla ya hapa” Dominick alimwambia Bwana Boniface.
“Hapana. Hii ndio mara ya kwanza kukuona. Sikuwahi kukuona kabla ya hapa” Bwana Boniface alimwambia Dominick.
“Niangalie vizuri. Hauwezi kusema kwamba haunifahamu. Nitazame vizuri” Dominick alimwambia Bwana Boniface.
Bwana Boniface akabaki akimwangalia Dominick. Ni kweli sura yake haikuwa ngeni machoni mwake lakini kila alipojaribu kukumbuka mahali ambapo alikuwa amekwishawahi kuiona sura ile, alikosa jibu.
“Wewe ni nani?” Bwana Bonifac aliuliza.
“Muuaji nisiyekuwa na huruma. Mimi ni mwandishi ambaye nimerudi tena kutoka kaburini” Dominick alimwambia Bwana Boniface.
“Dominick! Mungu wangu! Dominick!”
“Ndio mimi. Nimekuwa nikiisubiri nafasi hii kwa muda mrefu sana. Nimekuwa nikiangaika maishani mwangu. Nilikuwa na furaha katika kipindi chote, mkataka kunipa huzuzni maishani mwangu, nawapongeza kwa kuwa mlifanikiwa kwa asilimia mia moja” Dominick alimwambia Bwana Boniface.
“Dominick. Dominick……” Bwana Boniface alijikuta akiita jina la Dominick pasipo kuongea kitu chochote kile.
Alimwangalia Dominick mara mbili mbili, hakuamini kama Dominick angeweza kutumia njia ile kuingia ndani ya nyumba yake. Alitamani kuleta ubishi ili apate kujiokoa kutoka katika mikono ya Dominick lakini kila alipokuwa akiuangalia mdomo wa bunduki ile akabaki akiogopa kufanya hivyo.
Dominick akaanza upiga hatua mpaka kitandani ambako akauchukua mto wa kulalia na kuuweka mbele ya mdomo wa bunduki ile huku lengo lake kubwa likiwa ni kuuzia mlio wa risasi ile usisikike kwa sauti kubwa.
“Wote mtaelekea kule mlipoipeleka familia yangu” Dominick alimwambia Bwana Boniface.
Wala hazikupita hata sekunde kumi, milio kadhaa ya risasi ikasikika kwa mbali kabisa. Dmu zilikuwa zikimtoka Bwana Boniface. Akabaki chini huku akirusha miguu yake huku na kule. Kifua chake kilikuwa kimetobolewa na risasi kadhaa.
Dominick akaiangalia ile maisti ya Bwana Boniface. Hakuonekana kuridhika kabisa, akaifuata ale chini na kuanza kuiongezea risasi kadhaa. Kila alipokuwa akiiangalia maiti ile na ndivyo ambavyo hasira zilivyozidi kumpanda.
Mara baada ya kuridhika, akairudisha miwani yake pamoja na ndevu zake za bandia na kisha kuanza kupiga hatua kuelekea nje ya chumba kile. Akayafuta macho yake ambayo yalikuwa yakitokwa na machozi na kujiweka katika hali ya kawaida, alipomaliza, akatoka nje ya nyumba ile na kuingia garini.
“Tayari dokta?” Mwanaume yule aliyekuwa na mwili wa kujazia alimuuliza Dominick.
“Tayari. Nirudishe hospitalini” Dominick alimwambia mwanaume yule na kisha kuanza kumudisha hospitalini ambako baada ya kufika Amana akateremka na kumzuga dereva kwamba alikuwa akielekea katika hospitali ile.
Alipoona gari lile limeondoka mahali pale, moja kwa moja akaanza kulifuata garil lake na kisha kuanza kuelekea katika hoteli ya La Vista Inn.
                                                           ********
Hali ya hewa ikachafuka zaidi, viongozi wa Serikali wakachanganyikiwa zaidi, mauaji ambayo yalikuwa yametokea katika usiku uliopita yakaonekana kuwachanganya. Hakukuwa na mtu ambaye aliamini kama Bwana Boniface angeweza kuuawa ndani ya nyumba yake iliyokuwa na ulinzi wa kutosha.
Kitu walichokifanya mapolisi ni kumuita mwanaume yule ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni kumuendesha Bwana Boniface katika gari lake la kifahari aina ya Range. Moja kwa moja mwanaume yule akaingizwa katika chumba zcha mahojiano.
“Unaitwa nani?” Polisi aliuliza.
“Bakari Omari” Mwanaume yule alijibu.
“Ulikuwa wapi katika kipindi ambacho Bwana Boniface alikuwa akiuawa?” Polisi aliuliza.
“Kama ni yule dokta ndiye aliyefanya mauaji hayo, basi naweza kusema kwamba nilikuwa nje ya nyumba yake ila kama si yeye basi sikuwapo katika eneo la nyumba yake” Bakari alijibu.
“Ninahitaji kufahamu mengi kuhusiana na huyo dokta” Polisi alimwambia Bakari.
“Mzee alinipigia simu nyumbani na kunieleza kwamba kuna daktari ambaye nilitakiwa kwenda kumchukua katika hospitali ya Amana ifikapo usiku. Nilichokifanya kwa wakati huo ni kwenda katika hospitali hiyo na kumchukua na kisha kuanza kwenda nae nyumbani kwa marehemu” Bakari alielezea na kukaa kimya.
“Anaitwa nani?”
“Dokta Pius”
“Sawa. Endelea”
“Kwa jinsi nilivyokuwa nikiwaangalia wote kwa pamoja, niliweza kugundua kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba walikuwa wakifahamiana, naweza kusema hivi kwa kuwa muda mwingi walikuwa wakionyesheana tabasamu katika nyuso zao. Mara baada ya muda fulani, wakaingia ndani” Bakari alisema.
“Inamaanisha ulibaki nje?”
“Ndio”
“Kwa nini?”
“Mzee hakutaka niingie kitu ambacho nilijua kwamba walikuwa na kitu cha siri walitaka kuongelea ambacho sikutakiwa kukifahamu” Bakari alielezea.
“Sawa. Endelea”
“Ilichukua muda kama wa dakika ishirini, dokta Pius akatoka ndani ya nyumba ile na kisha moja kwa moja kuingia garini. Alinitaka niondoke mahali hapo na kumrudisha kazini kwake, katika hospitali ya Amana. Nilipomfikisha huko, nikaondoka zangu” Bakari alielezea.
Maelezo yote ambayo alikuwa ameyatoa yalikuwa yameandikwa katika faili maalumu na kisha kuruhusiwa. Walichokifanya mapolisi kwa wakati huo ni kuondoka kituoni hapo na moja kwa moja kuelekea katika hospitali ya Amana.Kitu ambacho walikuwa wakitaka kukifahamu katika wakati huo ni juu ya uwepo wa dokta Pius ambaye hadi muda huo ndiye alikuwa akionekana kuwa muuaji. Mara baada ya dakika kadhaa, wakafika katika hospitali ile na moja kwa moja kuelekea ndani ya jengo lile.
Kitu ambacho walikuwa wakikitaka katika muda huo ni kuonana na dokta mkuu ambaye angewapa maelekezo kuhusiana na dokta Pius ambaye kila mmoja alikuwa na wasiwasi nae. Mara baada ya kuelekezwa mahali ilipokuwa ofisi ya dokta mkuu, wakaanza kuelekea huko.
“Inashangaza sana” Dokta mkuu, Bwana Samuel aliwaaambia mara baada ya kuongea kwa muda.
“Kwa nini?”
“Katika hospitali hii wala hakuna dokta mwenye jina hilo” Dokta Samuel aliwaambia huku akitoa faili ambalo lilikuwa na majina ya wafanyakazi wote wa hospitali ile na kuwagawia.
 Kila mmoja alionekana kuchanganyikiwa, hawakuelewa ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea. Ni kweli kutokana na maelezo ya Bakari, dokta Pius alitoka ndani ya jengo lile la hospitali na kisha kuelekea katika gari lile ambalo alikuja kumpokea, sasa kwa nini dokta yue hakuwa na mmoja wa wafanyakazi katika hospitali ile?
Kila walipokuwa wakifikiria, hawakupata jibu, hai ilionekana kuwashangaza kupita kawaida, hawakuelewa ni kitu gani ambacho kilitakiwa kufanyika kwa wakati huo. Kitu walichokifanya ni kuondoka katika hospitali ile na kuelekea ofisini huku wote wakionekana kukasirika kupita kawaida.
Bado hali haikutulia mitaani, magazeti ambayo yalikuwa yameandika taarifa ya kifo cha Bwana Boniface yalikuwa yakinunuliwa kuliko magazeti yote. Kila mtu kwa wakati huo alitaka kufahamu sababu halisi ambazo zilimfanya Bwana Boniface kuuawa.
Wananchi hawakuelewa juu ya matukio yale ya mauaji kutokea. Kila mtu mitaani alikuwa akisema lake, wengine walidiriki hata kusema kwamba vyama pinzani ndio ambavyo vilikuwa vikifanya mauaji yae.
Matukio haya yaliyofuatana yakatengeza historia kubwa nchini Tanzania ya kuwapoteza viongozi wawili ndani ya miezi kumi na moja tena huku wote wakiwa wameuawa kwa kupigwa risasi. Hakukuwa na amani tena katika maisha ya viongozi, wasiwasi mkubwa ukawa umeongezeka katika maisha yao.
Hawakutakiwa kumuamini mtu yeyote katika maisha yao ya kila siku. Walitakiwa kuishi maisha ya peke yao na familia zao. Mauaji yale yalionekana kuendelea kama mfululizo wa filamu za tamthilia.
   Upelelezi bado ulikuwa ukiendelea kufanyika lakini hakuna kitu ambacho kilipatikana, muuaji hakupatikana japokuwa kila mtu alijua kwamba muuaji huyo alikuwa akiishi miongoni mwao.
                                                                *******
   Bwana Tumaini alikuwa na uhakika asilimia mia moja kwamba Dominick ndiye ambaye alikuwa amehusika na mauaji yote ambayo yalikuwa yametokea. Hakutaka kujiuliza kitu chochote kile, jambo ambalo aikuwa amedhamiria ni kuwaeleza mapolisi kwamba Dominick ndiye ambaye alikuwa amehusika katika kila kitu.
ITAENDELEA SIKU YA KESHO
MWANDISHI: NYEMO CHILONGANI
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com


USIKU WA KIGODORO - 11

$
0
0

Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

ILIPOISHIA:
“Kwanza unatakiwa urudi mapokezi, uliona bosi amekuja huku ina maana amekupigia simu sana mapokezi hukupokea.”
“Mh! Huo ni mtihani mwingine,” alisema Lina akionekana ana wasiwasi kupita kawaida.
Baada ya nusu saa akiwa bado kwenye jiko, alisikia simu ya mapokezi inaita…
SASA JIACHIE…
“Mh! Naitwa sasa,” alisema Lina huku akijishika kifuani kama ishara ya kuogopa.
Alitoka hadi mapokezi, akapokea…
“Haloo bosi.”
“Njoo uchukue vitu vyako.”
Lina alikata simu, akatembea kwenda chumbani huku moyoni akisema…
“Liwalo na liwe tu, sasa nitafanyaje? Kwanza ni afadhali ajue ili hili zigo linitue, nitaishi kama mkimbizi hadi lini sasa?”
Lina aliingia kwenye ofisi ya bosi wake huyo akapata mshtuko kutomuona James…
“Chukua vyombo vyako bwana,” alisema bosi wa Lina huku akiwa ametumbulia macho vyombo hivyo. Lina alitamani sana kumuuliza aliko mgeni, lakini kwa sababu ya cheo alishindwa. Akatoka haraka mpaka jikoni…
“Nikwambie kitu mama angu, sijamwona James kule kwa bosi,” alimwambia mama wa Chai…
“Mh! Ina maana ameondoka au?”
“Sidhani, nahisi amekwenda chooni.”
Dakika tatu mbele wakasikia watu wakitoka huku wanaongea…
“Hao wanatoka sasa,” alisema Lina.
Ni kweli, bosi wa Lina alikuwa akimsindikiza James huku wakiongoea mambo mbalimbali ya biashara.
Lina alipotoka, alisimama mapokezi na kumwona James akiishia na gari lake huku bosi wake akirudi…
“Lina,” aliita bosi huyo.
Lina moyo ukamlipuka lip!
“Abee bosi.”
“Unamfahamu mtu anaitwa James?”
Lina alitaka kuanguka chini, alihisi haja ndogo lakini akajikaza…
“Ni yupi huyo bosi?”
Lina alipojibu hivyo, bosi wake alikaa kwenye kiti cha wageni lakini kabla hajasema neno akasimama akimwambia…“Hebu twende ofisini kwangu kwanza.”
Lina alisimama, bosi wake alitangulia mbele, yeye akafuata nyuma. Alijua ishu imeshasanuka, ameshagundulika ni muongo, tapeli mkubwa.
“Karibu,” alisema bosi huyo.
“Asante.”
Bosi huyo alimwangalia kwa muda Lina kisha akaanza…
“Humjui James?”
“Yupi huyo bosi?”
“We unamjua James yupi?”
“Mimi namjua James kijana mmoja anakujaga hapa.”
“Leo kaja?”
“Sina hakika.”
“Huna hakika? Kwani maziwa ulimletea nani?”
“Bosi, nilipoleta maziwa nilimkuta mgeni anasoma gazeti la Daily News, wala sikumwona sura. Nilipofuata vyombo sikumkuta, labda alikuwa chooni. Kwa hiyo sijamwona.”
“Oke. James huyo unayemsema wewe ni nani yako?”
Lina alikaa kimya kwa muda akijiinamia…
“Bosi ni stori ndefu.”
“Kama ipi Lina? Mbona una hatari wewe msichana?! Yaani na uzuri wako wote unakuwa tapeli wa mapenzi?”
“Nimekosa bosi.”
“Umekosa nini sasa?”
“Nimekuwa mwongo kweli.”
“Mimi nilikuwa sijui lolote, leo ndiyo kaniambia unajua mimi nimefunga ndoa ya Lina? Nikamuuliza Lina gani? Akasema Lina mfanyakazi wako. Nilishtuka sana. Mimi ninavyojua wewe umefunga ndoa na Semi, sasa kusikia umefunga na mwanaume mwingine da..!
“Nikamuuliza unaishi naye? Akasema ndiyo, ila kasafiri kwenda kwao Korogwe, Tanga mama yake ni mgonjwa. Kidogo niseme yupo na nikuite mbele yake lakini nikajua kuna siri imefichwa, ndiyo maana kumbe hukai mapokezi ulimwona akiingia, si ndiyo?”
Lina alikubali kwa kutingisha kichwa juu kwenda chini na kurudi tena juu kuashiria amekubali alichoambiwa.
“Hebu niambie, nini kilitokea?” aliuliza bosi huyo huku akijiweka vizuri.
Lina naye alikaa sawa, akamwangalia bosi wake huyo kisha akaangalia ukutani. Aliporudisha macho kwa bosi wake akafunguka kuanzia mwanzo wa kukutana na James kazini hapo, ndoa hadi siku hiyo ambayo James alimwambia yeye yupo Korogwe...
“Mh! Lina, mbona una hatari wewe halafu mambo yenyewe mazito. Sasa unadhani nini kitatokea mbele?” aliuliza bosi huyo huku akimkazia macho Lina…
“Hata sijui bosi. Lakini nimeamua kukwambia ukweli wote ili kama unaweza kunisaidia ufanye hivyo.”
“Mh! Cha kukusaidia sina Lina, naamini ni wewe kujisalimisha kwa James na kumwambia ukweli maana yeye ndiyo hana ndoa na wewe na si Semi…”
“Je, nikimwita mbele yako nikatubu kwake?”
“Unahisi itawezekana? Hilo ni suala la kijamii zaidi tena kifamilia. Kulizungumzia ofisini si sahihi, mbaya zaidi kitendo hicho kinaichafua kampuni.”
Lina alijiinamia kwa muda akitafakari jambo huku akiwa hana la kusema na bosi wake huyo alikuwa akimwangalia tu huku akipangapanga vitu mezani kwake japokuwa havikuwa katika mpangilio mbaya.
“Unamjua nani katika marafiki wa James?” aliuliza bosi huyo.
“Hakuna.”
“He! Kweli? Mbona ni tatizo kubwa sana. Yeye anamfahamu nani kwenye ukoo wako?”
“Hakuna.”
“Mh!”
Wakati wanaendelea kuzungumza, mara mlango uligongwa, bosi akauliza nani?
“James.”
“Mh!” aliguna kwa mshtuko Lina lakini kwa sababu alishamweleza bosi wake kila kitu ikabidi bosi huyo aamue kwa busara kumchukua Lina na kumwingiza chooni mwake kisha akafungua mlango kumkaribisha James...
“Vipi bwana James?”
“Nimesahau ile kadi ya namba za kule Marekani.”
“Oooh, hii hapa,” alisema bosi huyo akiwa ameufungua mlango kwa uwazi mkubwa, James akaingia kuichukua kadi hiyo, akaondoka lakini safari hii hakusindikizwa.
Bosi alimfuata Lina, akamtoa chooni…
“Unajua kwa nini niliamua kukuingiza chooni ili usionane na James?”
“Naamini hukupenda niumbuke.”
“Hilo ni mojawapo lakini pia sababu kubwa umeniambia kila kitu, nikajua akikuona humu ndani inaweza kuwa balaa zito,” alisema bosi huyo akiwa amekaa.
Lina alikosa amani ya moyo, alijikuta akiwa mdogo kuliko inavyotakuwa kuwa. Aliamini uzuri wake ndiyo kisa cha yote, akajichukia ghafla.
“Nashukuru sana bosi, lakini sijajua nitamalizaje hili tatizo.”
“Mtegemee Mungu litaisha, lakini ikiwa tu kama ndani ya moyo wako utakiri kwamba ulichofanya sicho.”
“Nakiri hata sasa bosi kwamba nilichofanya sicho kabisa.”
“Basi kaendelee na kazi.”
Lina alisimama huku bosi wake akimwangalia kwa macho makavu kabisa, akaenda kwenye eneo lake la kazi, alikaa kwa hali ya wasiwasi, lakini aliamini anaanza kupata mwanga wa tatizo.
“Lakini lazima James atakuwa amejua kitu, haiwezekani asinipigie mpaka kunakucha halafu tena mpaka saa hizi, si kweli, amesikia kitu,” alisema Lina. Mara palepale simu ikaingia, James alipiga…
“Mh! Hatajwi,” alisema…
“Haloo baby?” alipokea Lina…
“Yes d, nimekususa leo.”
“Nimeshangaa, nikasema huyu mume wangu vipi tena,” alisema Lina huku akisimama kwenda jikoni. Alijua lazima atamuulizia mama…
“Vipi mama anaendeleaje?”
“Kidogo nafuu.”
“Nipe nimsalimie.”
Lina alishamminya mama wa chai, akampa simu naye akaigiza. Walizungumza kwa sekunde kama kumi na tano kisha James akaomba kuongea tena na Lina, simu ikarudishwa…
“Sasa unarudi lini, si kazini uliomba ruhusa ya siku chache tu?”
“Nitarudi kesho.”
“Oke, halafu leo nilikwenda kazini kwenu, nikamkuta yule mmamamama, sijui anafanyaga kazi gani?”
“Ee, mama yetu huyu bwana, anapikaga chai,” alisema Lina lakini akashtuka kwamba ameongea kitu cha kujikamatisha kule kusema ‘mama yetu huyu’ wakati yeye yuko mbali na ofisi, angesema ‘mama yetu yule’.
Baada ya kukata simu alimwambia yule mwanamke alichozungumza na James. Pia alimwambia alichomsimulia bosi wao.
***
Lina alikuwa nyumbani kwake usiku, mumewe alisharudi. Wakiwa sebuleni wamekaa, mumewe akasema…
“Yule rafiki yangu Kindaundau anasema ana shida sana na mimi. Sijui ana shida gani maana namuuliza ni nini anasema mpaka tukutane laivu.”
“Mh!” Lina aligunia moyoni, alijua kumekucha sasa…
“Kwani mna dili lolote kwa sasa?” aliuliza Lina akiwa anaangalia chini.
“Hatuna. Halafu yule ana kawaida moja, akiwa na tatizo anasema nashangaa hili anasema si la kuongea kwenye simu.
Kesho yake ilikuwa sikukuu, Lina aliwasiliana na James akamwambia ndiyo anapenda gari Korogwe kurudi Dar, James akamuuliza ataingia saa ngapi ili akampokee…
“Kwenye saa nane,” alidanganya Lina…
“Basi linaitwaje?”
“Burudani.”
“Basi utanikuta stendi Ubungo.”
“Sawa baby.”
***
Saa saba mchana, Semi alimwambia mkewe Lina waende wakale Mlimani City. Lina alitaka kuchomoa lakini akahisi mumewe hatamwelewa kwani ni kawaida yao sikukuu kutoka kwenda kupata lanchi au dina mahali.
Walifika Mlimani City, wakaa kwenye meza ya peke yao kabla hawajasikilizwa, Semi alimpigia simu Kindaundau na kumwambia kama yupo jirani aende hapo. Akamjibu ampe dakika kumi na tano tu.
***
Saa nane kamili, James alifika Ubungo stendi bila kumpigia simu Lina. Alitaka akishafika ndiyo ampigie.
Aliegesha gari mahali, akashuka na kutembeatembea huku sasa simu ikiwa sikioni akimpigia Lina.
Lina akiwa na mumewe, Semi alipata mshtuko mkubwa sana kuona simu ya James, akakumbuka kwamba alimwambia atafika Dar saa nane.
Kwa upande wake, James alishangaa kupiga simu ya Lina mara tatu bila kupokelewa. Mara, akaliona basi la Burudani likiingia, akalifuata. 
ITAENDELEA SIKU YA KESHO

ACHAPWA VIBOKO 120 KWA UUCHAFU, AZIMIA

$
0
0
Stori: Joseph Ngilisho, Arumeru
SHERIA iliyopitishwa na wakazi wa Arumeru mkoani Arusha ya kuwachapa viboko 70 hadi 120 wasichana wanaovaa nusu uchi na wavulana wanaovaa mlegezo, kuvuta bangi, wizi, matusi na ulevi nyakati za kazi imeanza kufanya kazi baada ya kijana Zakayo Leonard (26) kuchapwa viboko 120 kwa makosa mbalimbali likiwemo uchafu wa kutofua nguo zake.

Kijana Zakayo Leonard (26) akitumikia adhabu ya viboko 120.
Kijana huyo mkazi wa Ilboru, alihukumiwa adhabu hiyo kwa kuchapwa viboko 70 akidaiwa kutenda  kosa la  kumshambulia baba yake mzazi  aliyetambulika kwa jina la mzee Ng’uraa na kumng’oa jino moja.
Pia alitandikwa viboko 30 kwa kosa la kumtolea maneno machafu mzee wa kimila (Laigwanani) na baadaye alicharazwa viboko 20 kutokana na tabia ya uchafu wa kutofua nguo zake.
Hata hivyo, mara baada ya adhabu hiyo ya viboko 120 kwa mkupuo, kijana huyo alizimia na kushindwa kuinuka wala kutembea hali iliyolazimika kusaidiwa kwa kubebwa na morani wa Kimasai hadi nyumbani kwake.
 
Zoezi la kumsurubu kijana huyo likiendelea.
Adhabu hiyo ilitekelezwa hadharani mbele ya wazee wawili wa ukoo (Laigwanani) waliokuwa wakishuhudia huku mtuhumiwa akitakiwa kutojigusa popote wakati wa utekelezaji wa adhabu hiyo na kwamba iwapo angejishika popote viboko hivyo alivyochapwa vingefutwa na kurejea upya.
Wazee wa makabila ya Wamasi, Waarusha na Wameru wamejiwekea utaratibu wa kimila bila kujali kama unafuata maadili ya mwanadamu kwa kuwaadhibu wahalifu hadharani bila kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
CREDIT: Global Publishers.

ROSE MUHANDO AFYATUA 'JIWE'

$
0
0
7/10/2014 – Dar es salaam: Msanii maarufu namba moja wa Africa Mashariki wa nyimbo za injili amefyatua  kibao cha pili kingine kilichotengenezwa katika studio za Sony Music Africa, ambapo kibao cha kwanza kiliitwa Wololo kilichobeba albam ya Yesu Kung’uta chini ya usimamizi wa Rock star 4000


Wimbo wa jiwe umetengenezwa na kuchezwa na Rose Muhando ambapo kupangiliwa na kuzalishwa na Yusuph Mayige katika Studio ya Sony Music Afrika na kuendelezwa na  kuongezewa vionjo na  Rockstar 4000.

" Rose Muhando asema wimbo huu unatambulisha kuwa naniataendelea kuitawala hii dunia na kila kilichomo ndaniyake, katika dunia hii ya sasa , tunapoteza uaminifu nakumsahau Mungu katika kutawala kila kitu. Ni miminatakiwa kuweka muda wa kumkumbuka na kumsifuyeye kwa njia ileile tunayotumia katika kusifu nyota zetukwa majina tunayoyajua wenyewe ila mungu wetu nimkuu kuliko majina yote makuu, Mungu Mwamba, “Jiwe”.

Rose Muhando amejulikana kuwa msanii mahiri na wa kwanza Afrika Mashariki na pia amefanikiwa kukutana na viongozi wakubwa wa serikali akiwemo Mheshimiwa Rais wa muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete, Rais mstafu wa Kenya mheshimiwa Daniel Arap Moi na viongozi wengi wa siasa.
Kwa takwimu ya usambazaji wa muziki Rose Mhando amekuwa msanii wa kwanza  kuongoza mauzo ya muziki wa injili Afrika mashariki.
DVD ya albamu yake inatarajiwa kufyatulia msimu wa  krismasi.

BRAND NEW BELLE 9 AND JOH MAKINI

$
0
0
Belle 9 na Joh Makini wanakuletea wimbo wao mpya kabisa uitwao VITAMIN MUSIC.

ARTWORK MPYA YA CPWAA - KATA KITU

BRAND NEW NAVY KENZO - I JUST WANNA LOVE YOU

MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR, OTHMAN MASOUD OTHMAN AFUTWA KAZI

$
0
0
 
Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman.
RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, leo amemfuta kazi Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman na nafasi yake kuchukuliwa na Said Hassan Said.
Rais Shein amefanya uteuzi huo wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 55 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984.
Mhe. Said Hassan Said ameteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na uteuzi huo umeaza rasmi leo 7, Oktoba 2014. Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu.
Uteuzi wa Mhe. Othman Masoud Othman umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1) na 55 (3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.


A JOURNALIST IS BACK (MWANDISHI AMERUDI) - 12

$
0
0

MWANDISHI: NYEMO CHILONGANI
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

 Matukio haya yaliyofuatana yakatengeza historia kubwa nchini Tanzania ya kuwapoteza viongozi wawili ndani ya miezi kumi na moja tena huku wote wakiwa wameuawa kwa kupigwa risasi. Hakukuwa na amani tena katika maisha ya viongozi, wasiwasi mkubwa ukawa umeongezeka katika maisha yao.
Hawakutakiwa kumuamini mtu yeyote katika maisha yao ya kila siku. Walitakiwa kuishi maisha ya peke yao na familia zao. Mauaji yale yalionekana kuendelea kama mfululizo wa filamu za tamthilia.
   Upelelezi bado ulikuwa ukiendelea kufanyika lakini hakuna kitu ambacho kilipatikana, muuaji hakupatikana japokuwa kila mtu alijua kwamba muuaji huyo alikuwa akiishi miongoni mwao.
                                                                *******
   Bwana Tumaini alikuwa na uhakika asilimia mia moja kwamba Dominick ndiye ambaye alikuwa amehusika na mauaji yote ambayo yalikuwa yametokea. Hakutaka kujiuliza kitu chochote kile, jambo ambalo aikuwa amedhamiria ni kuwaeleza mapolisi kwamba Dominick ndiye ambaye alikuwa amehusika katika kila kitu.
11
   Hakujali maswali ambayo angeulizwa baada ya kutoa maelezo yale, kitu ambacho alikuwa akikijali kwa wakati huo ni kuwaeleza mapolisi tu kwani aliona kwamba ilikuwa bora kufanya hivyo kuliko zamu yake ya kuuawa itakapofika.
   Alidhamiria kweli kwenda kuwaeleza mapolisi ukweli wote kwamba kila mauaji ambayo yalikuwa yakitokea yalikuwa kama kisasi kutoka kwa Dominick ambaye waliiteketeza familia yake. Muda wote alikuwa na presha, alitaka mazishi ya Bwana Boniface yamalizike haraka haraka ili aelekee katika kituo cha polisi na kueleza kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea.
   Siku zikaanza kukatika huku mazishi yakiwa yamelizika. Bwana Ombeni akajipanga vilivyo kwenda kuelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea toka siku ile ambayo walikuwa wamewatuma vijana wao kwenda kuiteketeza familia ya Dominick.
   Hakutaka kuuawa kama wengine walivyouawa, alitaka kuinusuru roho yake haraka iwezekanavyo. Moja kwa moja akatoka kutoka ndani ya chumba chake na kuingia garini huku lengo lake likiwa ni kuelekea katika kituo cha polisi cha Oysterbay kwa ajili ya kuelezea kila kitu.
   Garini, akili yake wala haikutulia, muda wote alikuwa akimfikiria Dominick. Alitamani kufika katika kituo cha polisi haraka iwezekanavyo na kuelezea kile ambacho kilikuwa kikimsumbua moyoni mwake. Safari iliendelea kama kawaida mpaka akaanza kuingia katika eneo la kituo cha polisi cha Oysterbay. Kwa haraka haraka akateremka na kuanza kuelekea ndani ya kituo kile.
   “Karibu mzee” Poisi ambaye alikuwa kaunta alimkaribisha.
   “Asante” Bwana Ombeni aliitikia.
   Mapolisi wote ambao walikuwa nje wakaingia ndani kwa ajili kumsikiliza Bwana Ombeni ambaye alikuwa ameingia ndani ya kito kile. Kila mmoja akajua kwamba Bwana Ombeni alikuwa na kitu kizito moyoni ambacho alikuwa akitaka kuielezea polisi.
                                                                *************
      Bwana Ombeni alionekana kuchanganyikiwa. Tayari alikuwa katia kituo cha polisi kwa wakati huo. Hakuwa na nguvu za kuongea kitu chochote kile, alibaki kimya huku akiwaangalia mapolisi tu. Alikuja hapo akiwa na nguvu kabisa za kuwaeleza mapolisi kile ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha yake pamoja na njama zote ambazo alikuwa amezifanya katika kuiteketeza familia ya Dominick na kutaka kumuua Dominick mwenyewe.
   Kwa wakati huo alikuwa akijutia uamuzi ambao alikuwa ameuchukua, alijuta kwa kushirikiana na wenzake katika kutekeleza kile kitu ambacho kwa wakati huo alikiona kuanza kukilipia. Hakutaka tena kujificha, alitamani aendelee kuishi kuliko kuendelea kuficha kitu kile ambacho alikiona ni lazima akilipie kwa yeye mwenyewe kuuawa.
   “Nimekuja……” Bwana Ombeni aliwaambia mapolisi ambao walikuwa kimya wakimwangalia.
   “Ndio mzee. Tumekuja hapa kukusikiliza” Mkuu wa kituo hicho, Hussein alimwambia.
   “Nimekuja kueleza ukweli. Kila kitu na njama zote ambazo nilizifanya katika maisha yangu kushirikiana na wenzangu” Bwana Ombeni aliwaambia.
   “Ndio mzee tunakusikiliza”
   “Nimefanya mambo mabaya sana kwa kushirikiana na wenzangu. Sisi ndio tuliiangamiza familia yake” Bwana Ombeni aliwaambia na kunyamaza kwa muda.
   “Mliiangamiza familia yake? Nani?”
   Bwana Ombeni akabaki kimya kwa muda, akaanza kujifikiria kama ingekuwa vizuri kumtaja Dominick mahali pale. Alijua fika kwamba angewekwa chini ya ulinzi hapo hapo kabla ya mambo mengine kufuata.
   “Nani mheshimiwa?” Hussein aliuliza.
   “Familia ya……” Bwana Ombeni alisema lakini hata kabla hajamaliza sentensi yake, simu yake ya mkononi ikaanza kuita.
   Kwa haraka haraka akaichukua kutoka katika mfuko wake wa suruali na kisha kuangalia kioo cha simu, namba ambayo ilikuwa ikiingia katika muda huo ilikuwa ngeni simuni mwake. Kwa haraka haraka akaipeleka sikioni.
   “Halloooo….” Bwana Ombeni aliita.
   “Hallooo…!” Sauti ya upande wa pili iliitikia.
   “Naongea na nani?” Bwana Ombeni aliuliza.
   “Mwandishi wa habari wa gazeti la Mambo leo”
   “Sawa. Nikusaidie nini?”
   “Tumezipata taarifa zote kuhusu wewe na wenzako ambao mlifanya mauaji kwa kuiangamiza familia ya mwandishi mwenzetu, Dominick. Kila kitu tumeambiwa na ushahidi umekamilika. Hapa ninapoongea na wewe nipo ofisini mwangu nikiandaa gazeti kwa ajili ya kuitoa taarifa hiyo gazetini kesho” Sauti ya upande wa pili ilisikika.
   Bwana Ombeni akaonekana kushtuka kupita kiasi. Akaonekana kuanza kutetemeka huku kijasho chembamba kikianza kumtoka. Hakuamini kama mambo yale ambayo walikuwa wameyafanya na kuwa kama siri tayari yalikuwa yameanza kutapakaa.
   Alijua kwamba kama taarifa ingetolewa gazetini basi ingekuwa hatari zaidi. Wananchi wote wangeshtuka na kuitaka serikali kumchukulia hatua kali kwa kumpa adhabu ya kifungo cha maisha jela au kunyongwa.
   Kwa haraka haraka akatoka pale kaunta alipokuwa na moja kwa moja kuelekea garini mwake huku akionekana kutetemeka. Mapolisi wote wakabaki wakishangaa, hawakuelewa kitu chochote ambacho kilikuwa kikiendelea kwa mzee huyo kwa wakati huo.
   “Umesemaje?” Bwana Ombeni aliuliza mara baada ya kuingia garini.
   “Ndio hivyo mzee. Nilifanya uchunguzi wa muda mrefu. Nimeweza kugundua hayo, na sasa ndio ninaandaa gazeti. Kesho, kila Mtanzania ataweza kugundua uovu wako ulioufanya” Mwandishi yule ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake kiusalama alimwambia.
   “Nimekusikia. Naomba unielewe kitu kimoja. Nikweli nimefanya uovu huo ila kwa sasa ninahitaji sana kitu hiki kutokujulikana. Nakuomba, nakuomba sana kama itawezekana tukutane na kuweza kuinunua habari hiyo kwa kiasi chochote cha fedha” Bwana Ombeni alimwambia mwandishi.
   “Hauwezi kuinunua habari hii. Hivi unajua kuwa kama nikiiweka habari hii gazetini nitaweza kupata zaidi ya milioni ishirini? Hii ni habari yenye fedha sana” Mwandishi wa habari alimwambia Bwana Ombeni.
   “Nakuomba sana. Nitainunua hata kwa milioni hamsini” Bwana Ombeni alimwambia.
   “Haitowezekana kabisa. Ni lazima niiuze kama hautoongeza kiasi kikubwa zaidi” Mwandishi alimwambia.
   “Nimekuelewa. Nitakupa milioni mia moja. Najua ni fedha nyingi sana, ila ninachokitaka ni kwamba kitu hicho kiwe siri kati yangu na wewe tu. Nakuomba unisaidie, nina milioni mia moja mwandishi” Bwana Ombeni alimwambia mwandishi huyo.
   “Sawa. Njoo na fedha hizo hapa Caspian Hotel. Chumba namba 18. Kuwa mwangalifu asikugundue mtu yeyote yule” Mwandishi yule alimwambia.
   “Usijali. Ninakuja na fedha hizo”
   “Kama ukichelewa. Hautonikuta”
   “Usijali, nitafanya haraka iwezekanavyo” Bwana Ombeni alisema na kisha simu kukatwa.
   Hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo tena, moja kwa moja akaliwasha gari lake na safari ya kuelekea benki kuanza. Alihitaji kufanya kila kitu kuhakikisha jambo lile linakuwa siri ambayo hatoweza kuitambua mtu yeyote yule.
   Mara baada ya kufika benki, moja kwa moja akaelezea shida yake na kisha kupelekwa katika chumba maalumu ambako huko akakabidhiwa kiasi cha fedha ambacho alikuwa akikihitaji kwa muda huo na safari ya kuelekea katika hoteli ya Caspian kuanza.
   Garini, kichwa chake hakikutulia kabisa. Muda wote alikuwa akimfikiria mwandishi yule wa habari pamoja na habari ambayo alikuwa nayo juu yake. Ni kweli hakutaka Mtanzania yeyote afahamu juu ya kile ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha yake.
   Hakujali kama alikuwa akilipa kiasi kikubwa cha fedha kwa wakati huo kwa ajili ya kuinunua habari ili, ila kitu ambacho alikuwa akikijali ni kuifanya habari ile kuendelea kuwa siri tu. Hakutaka kupata aibu yoyote ile na hiyo ndio maana alihakikisha kufanya kila kitu kuwa siri.
   Mara baada ya kufika katika eneo la hoteli ya Caspian, moja kwa moja akateremka na kisha kuanza kuelekea sehemu ya mapokezi. Alipofika, akaelekezwa kwenda katika chumba ambacho alitakiwa kwenda na kuanza kwenda kule.
   Mara baada ya kukifikia, akaanza kupiga hodi na kukaribishwa. Mwandishi alikuwa bafuni, hivyo moja kwa moja akatulia kitandani huku brifukesi yake akiiweka pembeni. Bwana Ombeni alibaki kuwa na mawazo mahali pale, alitaka mwandishi yule atoke bafuni na kumkabidhi habari ile haraka iwezekanavyo na yeye kuondoka mahali pale.
   Mlango wa bafuni ukafunguliwa na mwandishi kutoka. Bwana Ombeni akaanza kumwangali mwandishi yule kuona kama alikuwa akimfahamu. Hakuweza kuuona vizuri uso wake kutokana na mwandishi yule kutumia taulo kuufuta uso wake.
   “Mungu wangu! Dominick!” Bwana Ombeni aliita kwa mshtuko mara baada ya kuona uso wa mwandishi yule.
   “Umeshtuka sana?” Dominick alimuuliza Bwana Ombeni huku uso wake ukiwa na tabasamu pana.
   “Usishtuke. Wewe ni rafiki yangu mkubwa sana. Mara zote nilikuwa nikiandika habari zako gazetini. Au umesahau?” Dominick alimuuliza.
   Bwana Ombeni hakujibu kitu chochote kile, alibaki akimwangalia Dominick kwa macho yaliyojaa mshtuko. Hakuamini kama yule mtu ambaye alikuwa akimwangalia mbele yake kwa wakati huo alikuwa Dominick, mwandishi ambaye walikuwa wameiangamiza familia yake.
   “Nataka tuongee tu leo. Wewe ni rafiki yangu mkubwa. Au umesahau hilo?” Dominick aliuliza.
   “Sijasahau” Bwana Ombeni alijibu huku akitetemeka, tayari kijasho kikaanza kumtoka.
   “Kila siku nilikuwa nakufagilia katika magazeti na kukufanya kujulikana zaidi nchini hapa. Unakumbuka hilo?” Dominick aliuliza.
   “Nakumbuka” Bwana Ombeni alijibu.
   “Wewe ni rafiki yangu Ombeni, wala hautakiwi kuogopa lolote. Umekumbuka kuja na fedha zangu?” Dominick alimuuliza.
   Bwana Ombeni akaanza kuliangalia brifukesi lake ambalo alikuja nalo mahali pale na kisha kulichukua na kumkabidhi Dominick ambaye tayari alikuwa ameufunga mlango kwa ufunguo. Dominick akaifungua brifukesi ile na kisha kuanza kuziangalia fedha zile, akatabasamu.
   “Lakini kumbuka kwamba ulinisaliti. Yaani upendo wote ule niliokuonyeshea, malipo yake yakawa ni usaliti. Unakumbuka kama ulinisaliti?” Dominick aliuliza huku tabasamu pana likionekana usoni mwake. Bwana Ombeni hakujibu kitu chochote kile, alibaki kimya huku akimwangalia Dominick.
   “Swali gumu hilo, inaelekea haukumbuki kitu chochote kile” Dominick alimwambia Bwana Ombeni.
   “Nakumbuka” Bwana Ombeni alimwambia Dominick.
   “Safi sana. Unakumbuka kwamba ulinisababishia kidonda kikubwa maishani mwangu?” Dominick aliuliza, tayari uso wake ukabadilika, tabasamu lote ambalo lilikuwa likionekana kabla likapotea.
ITAENDELEA SIKU YA KESHO

USIKU WA KIGODORO - 12

$
0
0

Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

ILIPOISHIA: Lina akiwa na mumewe, Semi alipata mshtuko mkubwa sana kuona simu ya James, akakumbuka kwamba alimwambia atafika Dar saa nane.
Kwa upande wake James, alishangaa kupiga simu ya Lina mara tatu bila kupokelewa. Mara, akaliona basi la Burudani likiingia, akalifuata. 
SASA ENDELEA…
“Jamani wazima?” aliwasalimia wafanyakazi wa basi hilo.
“Hili gari linatokea Korogwe?” aliuliza mara baada ya salamu yake kujibiwa.
“Ndiyo mkubwa.”
Alipopata jibu hilo, alisimama kando na kusubiri abiria washuke akiamini Lina yuko ndani. Lakini aliendelea kupiga simu yake ambayo haikupokelewa.
Mpaka abiria wa mwisho anashuka na begi, hakuwepo Lina!
“Mh! Hii kali! Anamaanisha nini sasa kutokupokea simu yangu? Angepokea aniambie kuna nini! Basi la Burudani ndiyo hili na hayumo!” alisema mwenyewe akiwa anaelekea kwenye gari lake.
Alipata wazo la kwenda Mlimani City kupumzika akipata kinywaji baridi na moyoni aliamua kwamba Lina akimpigia na yeye hatapokea ili kulipa kisasi.
Aliingia Mlimani City kwa kutumia geti la kaskazini, akaegesha gari sambamba na gari la Semi. Alishuka akaingia kwenye maduka ya ndani kwanza kwa ajili ya kuosha macho.
***
Lina alisimama kwenda chooni, Kindaundau naye alikuwa anaingia Mlimani City kwa teksi huku akimpigia simu Semi kumuuliza alikokaa.
“Nimekaa jirani na meza ya Samakisamaki, we uko wapi?” aliuliza Semi…
“Ndiyo napita getini…hebu ngoja nipokee simu ya shemeji yako kwanza,” alisema Kindaundau.
Simu hiyo iliyopigwa na mke wa Kindaundau ilikuwa ikimjulisha kwamba, mtoto ameumia mguu alikuwa akicheza na wenzake. Kindaundau alimwamuru dereva wa teksi kugeuza gari kuwahi nyumbani kwake, Makumbusho huku akimpigia simu Semi…
“Ee bwana, mtoto wangu kaumia, wife amenipigia sasa hivi, ngoja niwahi nimkimbize hospitali,” alisema Kindaundau…
“Da! Pole sana bwana. Basi utaniambia maendeleo huko.”
“Sawa.”
***
Inaweza kuwa ni ajabu lakini kweli, James alikatiza meza na kwenda kukaa meza moja na Semi maana watu walikuwa wengi siku hiyo hivyo nafasi ya kukaa ilikuwa ya kutafuta sana…
“Habari yako ndugu?” James alimsalimia Semi huku akimuuliza kama kwenye kiti alishokishika kina mtu…
“Njema tu kaka, karibu, hakina mtu. Ila hiki hapa kina mtu,” alisema Semi huku akikishika kiti cha Lina.
Lina alitoka chooni huku akijiwekaweka sawa nywele zake. Macho yake yalikuwa kwa wateja mbalimbali waliokuwepo eneo hilo. Hakuwa na habari ya kuangalia alipokaa mume wake na sasa waume zake.
Alikuwa amebakiza hatua chache kufika kwenye meza, alipotupa macho alipata mshtuko kumwona James amekaa na mume wake, akarudi chooni mbio. Baadhi ya watu waliomuona akirudi walimshangaa.
“Mungu wangu! Kwani wanafahamiana? Loo! Nimekwisha mimi Lina, kiranga chote leo ndiyo mwisho,” alisema peke yake kule chooni huku akijishika kifuani. Mapigo ya moyo yalimwenda kwa kasi ya ajabu.
Alikumbuka kitu, alichukua simu yake, akatuma meseji kwa James…
“Nililala baby, uko wapi? Si ndiyo tunaingia stendi Ubungo sasa. Please usiondoke nina mizigo.”
James alisoma meseji hiyo, akasimama haraka sana…
“Ee bwana, ngoja niwahi stendi kuna mgeni ameingia hapo,” alimwambia Semi huku akitoa noti ya shilingi elfu tano na kumpa Semi…
“Hii utanilipia hii juisi na mayai.”
“Poapoa mkubwa,” alijibu Semi bila kujua mchezo wote unachezwa na mke wake.
James alikimbilia kwenye gari huku akipiga simu kwa Lina…
“Haloo, sasa umekuja na basi gani?”
“Burudani, si nilikwambia.”
“Mbona basi la Burudani limefika, wewe sijakuona?”
“Burudani la pili..”
“Poapoa, nakuja.”
Lina alihema kwa kuhisi unafuu. Lakini alijua ana kibarua kimoja bado, James atakapomkosa Ubungo itakuwaje? Si atahisi amechukua usafiri kwenda nyumbani? Je, akifika nyumbani na kukuta hajafika?
James alipoingia Ubungo tu, meseji ya Lina ikaingia…
“Baby simu inazima chaji, sijui itakuwaje?”
Lina alipotuma meseji hiyo, akazima simu na kurudi kukaa kwa mume wake, Semi…
“Sweet, tuondoke, tumbo haliko vizuri ghafla,” alimwambia mume wake…
“Mimi mwenyewe nilitaka kukwambia hivyo.”
Waliondoka eneo hilo, wakiwa njiani, Semi alipokea simu…
“Ee Masua, niambie bosi wangu…eee….wapi? Lini? Aaa, sasa….da! Oke, ngoja nifike nyumbani, nakuja tuondoke.”
Alipokata simu alimgeukia mkewe…
“Baby kuna safari ya Zanzibar saa kumi, inabidi nikuache nyumbani mimi niondoke kwenda uwanja wa ndege.”
“Jamani baby, hizo safari zako bwana,” Lina alijidai hajapenda lakini moyoni alishangilia ile mbaya.
“Si ndiyo kutafuta hela mke wangu.”
“Poa, kurudi lini?”
“Nadhani baada ya siku mbili.”
***
Baada ya mumewe kuondoka, Lina alichukua begi lake aliloondoka nalo kwa James, akaenda kukodi Bajaj hadi sokoni. Alinunua viazi, mkungu wa ndizi, nazi na machungwa. Vitu vyote hivyo akavitia kwenye mfuko wa salfeti na kufungwa kamba.
Safari ikaanza ya kwenda nyumbani kwa James. Ile anafika tu, James naye akaingia na gari...
Je, unajua nini kilitokea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi, Jumamosi ijayo.
Naomba ushauri wako
“Oo! Baby, pole na safari, nilijua utakuwa umeshakuja kivyako maana si uliniambia simu ipo karibu na kuzima chaja!”
“Ndiyo hivyo baby, pole na hapa baba angu?”
“Nimepoa sana mpenzi.”
Walikumbatiana, wakabusiana, wakashikana mkono kuingia ndani maana tayari mlinzi alishafika kumpokea Lina kwenye Bajaj na ule mfuko wake mkubwa.
James alibadili zile hisia kwamba Lina ana mume mwingine zaidi ya yeye, aliamini ni maneno ya Kindaundau tu…
“Mtu awe na mwanaume mwingine wa ndoa kabla yangu halafu afikie kwangu toka safari ya mbali kama Korogwe, haiwezekani, kutakuwa na kitu, tena amekuja na mzigo mkubwa tu,” alisema moyoni James huku picha ya Kindaundau kumdanganya ikimjia kwa mbele walivyokuwa wamekaa siku ile kwenye ule mgahawa kule mjini.
***
Lina, ili ajifanye alikuwa safarini kweli na alimmisi sana mume wake huyo, aliamua usiku huo kumtendea vitu adimu na kumwonesha mapenzi motomoto.
Walipomaliza kula tu aliomba wakaoge, walikwenda chumbani kuoga, Lina ndiye aliyemtaka James waende wakalale kwa kisingizio kuwahi kuamka kesho yake lakini ukweli ni kwamba alitaka wacheze kandanda kitandani.
Walipopanda kitandani tu, Lina alitia hisani, maana alipokumbuka jinsi alivyomwona James pale Mlimani City amekaa na mume wake alisikia huruma sana. Aliamini walikaa jirani kwa sababu viti havikuwa vingi na hakuna aliyekuwa tayari kumjua mwenzake kwa undani.
“Baby, nakupenda sana,” ndivyo alivyoanza kusema Lina akimuweka James kifuani pake…
“Hata mimi nakupenda sweet, nilikumisi sana mke wangu.”
“Kweli, kuliko nilivyokumisi mimi?”
“Hunishindi bwana.”
Mara kulipita ukimya kwani walijikuta wamezama kwenye penzi la upande wa pili, walikuwa ndani ya denda. Miguno tu ndiyo iliashiria kwamba wapo pembeni ya uwanja wakisubiri kuingia kati ili kuanza kusakata soka.
Lina kwa mara ya kwanza alimshika James na kumshusha chini, akamuwekea kiti akae. Halafu akashusha godoro, akalitandika vizuri sana, wakalala hapo…
“Baby leo utanipata kwa staili ya usiku wa kigodoro,” alisema Lina.
Alimvuta James na kumkaribisha kwake huku akimsisitizia kwamba anahitaji mtoto kutoka kwake.
Akili za Lina hapo zilikuwa siyo zenyewe, kwani zilibadilika ghafla na kujikuta eti yuko tayari aachane na Semi kuliko kuachana na James.
Alitumia staili mbalimbali ambazo James hakuwahi kujua kama anazitambua na kila pozi alisisitiza kupewa mimba ndiyo ilikuwa kilio chake kikubwa katika mahaba ya usiku huo.
Kwa sababu walitandika godoro chini, kwa hiyo hata pale mmoja wao alipocheza rafu, hakuna mlio uliotoka. Ilikuwa kimyakimya, sanasana kuhema sana kwa Lina na maneno yenye kubembeleza ndiyo yalisikika kwa mbali lakini.
Lina alimaliza pozi zake zote, sasa akataka kupewa mapozi na James. Naye alikuwa mtaalam, alimuonyesha mapozi ya nguvu, mara wakae wote, mara mmoja asimame mwingine achunge mbuzi, mara mwingine kulia mwingine kushoto lakini bila kuachana.
Lina alianza kupiga kelele na kutangaza ushindi wake alipokalishwa kwenye baskeli kiti cha nyuma halafu dereva akamwangalia lakini wakiwa wanaenda mbele.
Kilio chake kilitoa picha kwamba kweli walikuwa kwenye usiku wa kigodoro…
“Na…na…na mimba nakuhakikishia utapata sweet,” alisema kwa kigugumizi James.
“Mtoto tutamuita Jali dear, yaani mimi na wewe.”
Lina alipomaliza kusema hivyo tu akanyoosha miguu na kusalimu amri akifuatiwa kwa karibu sana na James naye, wakawa wanahema wote!
***
Siku iliyofuata, Lina aliondoka kwenda kazini akimwongopea James anapitia saluni kuosha nywele kwanza maana alipokwenda Korogwe zilichafuka hivyo hakutaka lifti lakini walikubaliana kwamba, jioni waende wakapate dina Mlimani City.
***
Ilikuwa saa kumi na mbili na nusu jioni, Semi alirejea kutoka Zanzibar, akafika nyumbani kwake hakumkuta Lina…
“Uko wapi wewe?” Semi alimtumia meseji mkewe.
“Nipo saluni baby wangu. Vipi hali yako sweet?”
“Sawa, hali yangu mi mzima sana,” alijibu Semi bila kusema amerudi.
Alioga, akavaa akatoka. Safari yake ilikuwa kwenda Mlimani City kwenye ahadi moja ambapo ilimlazimu arejee Dar halafu kesho yake aende tena Zanzibar.
Alikanyaga mafuta hadi Mlimani City. Kwa folenifoleni alijikuta amefika Mlimani City saa moja na dakika kumi giza likiwa limeingia tayari.
Aliegesha gari na kwenda kukaa. Ile anaweka kikao kwenye kiti tu, anasikia sauti ikimsalimia…
“Bro za tangu jana, kama nakukumbuka,” alisema James ambaye kiti alichokaa aliweza kuonana na Semi moja kwa moja wakati kiti alichokaa Lina alimpa mgongo kwa hiyo Semi alimwona kwa nyuma.
Kabla hajaitika salamu ya James, Semi alikaza macho kwa Lina, akashangaa, akasimama na kumfuata…
“Lina,” aliita huku akimwangalia usoni na kumshika begani…

Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

MASTAA WAJIENGUA BONGO MUVI

$
0
0

 Msanii wa filamu Bongo, Halima Yahya ‘Davina’.
HALI bado tete! Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kujiuzulu, upepo mbaya unaendelea kuitafuna klabu hiyo ambapo sasa wasanii wengine watano wamejiengua, Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.

Kutokana na wasanii hao kujitoa, klabu hiyo inaonekana kupoteza muelekeo ambapo kwa sasa wanachama waliobaki kundini wanajipanga upya ili kuisimamisha upya.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wasanii waliojiengua ni Halima Yahya ‘Davina’, Esha Buheti, Kajala Masanja, Flora Mvungi na  Salma Salmini ‘Sandra’ huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni kukithiri kwa vitendo vya ngono na ubaguzi wa kimaslahi.
 
Msanii wa filamu Bongo, Flora Mvungi akipozi.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba, hivi karibuni kulitokea safari ya wasanii kwenda mkoani Tanga lakini baadhi ya viongozi wamedaiwa kujichagua kwa ‘kapo’ bila kujali kuwa wapo wanachama wengine ambao wanatakiwa kwenda huko.
Kikifafanua madai hayo, chanzo hicho kilikwenda mbele zaidi na kuzinadi kapo hizo kama ifuatavyo:
Cloud 112 (Issa Musa) alidaiwa kuongozana na Coletha Raymond, JB (Jacob Steven) na Shamsa Ford, Rose Ndauka na Single Mtambalike (Rich) na wengine.
 
Msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja.
Baada ya madai hayo kutua kwa mapaparazi wetu, walianza kwa kuwatafuta walengwa ambao wamedaiwa kubaguliwa na kuamua kujitoa klabuni hapo. Mambo yalikuwa hivi:
Davina:
“Mimi nimeamua kujitoa kwa sababu naona mambo mazuri wanachaguana mapatna tu sisi tunakumbukwa pasipo mazuri, kwenye pesa wanapeana wao wenyewe, mimi mpaka mume wangu alikuwa akiniuliza kwamba napata faida gani.”
 
Msanii wa filamu Bongo, Salma Salmini ‘Sandra’
Sandra:
“Sijapata faida yoyote Bongo Movie, watu wanapeana mapatna inapotokea suala la safari na pesa.”
Esha Buheti:
“Mimi nimeamua kujitoa kwani watu wamekuwa na ubaguzi, sisi tunaitwa unapotokea msiba tu, nitafanya kazi zangu mdogomdogo, nitatoka tu.”
 
Msanii wa filamu Bongo, Esha Buheti.
Kajala:
“Nimejitoa kwa sababu kule nilikuwa nikimfuata Steve Nyerere, sasa ameshatoka nafuata nini tena?”  
Jitihada za kuwapata wasanii wanaotajwa kuwa ni wabaguzi ziligonga mwamba kwa baadhi ya wasanii lakini alipopatikana Cloud 112, alikanusha taarifa hizo.
“Hakuna kitu kama hicho, sisi tunasafiri kulingana na matakwa ya waandaaji wa safari, waandaaji ndiyo wanaosema wanamtaka nani katika shughuli yao, wanaosema hivyo wamekosa la kuongea,” alisema Cloud 112.

BARUA NZITO: WOLPER JIHESHIMU BWANA

$
0
0
 
Kwako
mtoto mzuri unayekimbiza kwenye anga la filamu Bongo, Jacqueline Massawe Wolper. Bila shaka ni mzima wa afya na unaendelea na majukumu yako ya kila siku.

Binafsi mimi naendelea vizuri mambo yanakwenda kwenye mstari na leo nimekukumbuka kupitia barua nzito.
Nataka kusema na wewe mawili matatu ambayo mimi nimeona si sawa kufanywa na wewe!
Nisichelewe sana wala nini, madhumuni ya barua hii kwanza kabisa ni kutaka kukukumbusha kwamba unapaswa kujiheshimu katika kila sekta kwa kuwa wewe ni kioo cha jamii.
Jamii inakuheshimu, inakufuatilia kila hatua unayopiga maishani.

Wanaokufuatilia ujue wanakupenda ingawa pia hata wale wasiokupenda nao pia wanakufuatilia.
Wanakufuatilia kwenye vyombo vya habari, katika mitandao ya kijamii na hata live mitaani. Kauli yako lazima iwe na staha.

Sababu ya kukwambia jiheshimu ni kauli zako kwenye mitandao ya kijamii. Mara kadhaa nimekuwa nikiona ukiposti lugha ya matusi kwa waliokuudhi.Kwa nini utukane? Kwa mtu anayejiheshimu kama wewe si busara hata kidogo kutukana hata kama umechokozwa.
Akili yako inapaswa kutafakari kwa kina kabla ya kuposti kitu chochote katika mitandao ya kijamii. Unapoposti kitu pia ujue kuna watu ambao watakipenda na ambao hawatakipenda, sasa kwanza kuwajibu wale wasiokipenda unajishushia heshima!
Mfano mzuri ni siku ile ulipoweka aina mpya ya simu katika mtandao wa kijamii. Niliufuatilia mjadala ule, kuna watu walikuponda kwamba aina ya simu hiyo mpya haipo na kwamba ulifanya hivyo ili kujipa sifa.
Mtoto wa kike ukaona bora umtukane, ukaandika tusi zito kabisa kumjibu shabiki huyo. Ukimjibu mjinga unategemea nini? Najua kabisa dhamira yako kuweka simu hiyo ilikuwa ni utani lakini walivyoipokea baadhi ya mashabiki wakakusababisha utukane.
Wewe unaheshimika, kutukana si jambo la busara. Siku hizi teknolojia inakua, ni rahisi mtu kukufuatilia na kukupata na hata kukuchukulia hatua za kisheria.
Kwa nini utukane? Kwanza hata ukiamua kutukana, utatukana wangapi katika mitandao ya kijamii? Si sawa!
Siku hizi mitandao inatumika kama chombo cha biashara, ni vyema ukawa makini na unavyoposti ili ikiwezekana hata ukatumia mitandao hiyo kujiingizia mkwanja kuliko kutukana na watu wanaokuheshimu wakakuona hauna maana.
Usipoteze muda wako kuwajibu watu ambao hawakosi cha kuongea. Utajisumbua tu, fuata mifano ya mastaa wengi ulimwenguni, wanapoweka kitu katika mitandao ya kijamii huwa hawageuki kutazama watu wamekomenti nini baadaye.
Weka kitu chako kisha fumba macho kama huoni vile, si wote watakaokichukulia kitu chako chanya. Kuna wengine wataponda au watakutukana, ukiwajibu watu watakuona wewe mpuuzi kuliko hao waliokuanza!
Kwa leo acha niishie hapo, kuwa makini sana na mitandao ya kijamii.

ROSE MUHANDO ADAIWA KUINGIA MITINI NA MILIONI MOJA

$
0
0

Msanii nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando.
Stori: SHANI RAMADHANIMSANII nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando anadaiwa kuingia mitini na shilingi milioni moja alizolipwa kwa ajili ya kutumbuiza kwenye uzinduzi wa albamu ya Injili ya John Lisu iitwayo Uko Hapa, Jumapili iliyopita.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Rose alimegewa kiasi hicho cha pesa na Kampuni ya Msama Promotion iliyoandaa uzinduzi huo uliofanyika ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar Jumapili iliyopita.
“Rose jamani ana mambo! Mnajua kama amemliza Msama (mkurugenzi wa Msama Promotion) shilingi milioni moja? Alipewa ili atumbuize kwenye uzinduzi wa albamu ya John Lisu lakini akaingia mitini.
“Mbaya zaidi kila alipopigiwa simu kuulizwa kwa nini hajafika Dar ile Jumamosi ili Jumapili awepo ukumbini akawa hapokei simu.
Kikaendeela: “Rose ananishangaza sana, sikuwahi kufikiria kama anaweza kufanya hivyo, kikubwa kinachowaumiza wengi ni kutopokea simu na ingekuwa vizuri kama angetoa taarifa mapema kwa kutohudhuria kwake na sisi tungejua cha kufanya mapema,” kilisema chanzo hicho ambacho kipo ndani ya waandaaji hao.
Chanzo hicho hakikuishia hapo, kiliendelea kuanika kuwa shutuma za aina hiyo zimekuwa zikimuandama sana mwanamuziki huyo kiasi cha kushindwa kuaminika na kudai kuwa hana njaa ya kutokomea na pesa hiyo kwani ni kiasi kidogo sana kwake.
 
Msanii nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando akizungumza jambo.
Risasi Mchanganyiko lilimsaka bosi wa Msama Promotion, Alex Msama ambaye alikiri Rose kutotokea kwenye uzinduzi huo licha ya kulipwa kiasi hicho cha pesa na kilichomuumiza zaidi ni kutopokea simu za wasaidizi wake waliotaka kujua nini kilimpata.
“Aliniangusha sana maana hata yeye nilimtangaza sana kwenye vyombo vya habari kwamba atakuwepo, lakini matokeo yake ikawa kimya, sijui nini kimempata lakini nitatoa tamko siku mbili hizi,” alisema Msama kwa masikitiko makubwa.
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Rose Muhando kupitia simu yake ya kiganjani, alipokea na mambo yalikuwa hivi.
Mwandishi: Habari yako dada Rose?
Rose: Nzuri tu habari yako wewe
Mwandishi: Nzuri, mimi ni (akataja jina lake)
Rose: Hilo jina siyo geni kwangu.
Mwandishi: Mimi ni mwandishi wa Global.
Rose: Ahaaa, subiri kidogo nitoke nje niko benki nitakupigia.
Baada ya kukata simu, Rose alikaa kimya kwa zaidi ya dakika tano. Mwandishi wetu alipopiga tena mara kadhaa simu yake haikupokelewa.
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>