Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

Baada ya kusingiziwa kakamatwa na Madawa nchini Brazil, Aisha Bui aonekana Saluni ya Nisha sinza

$
0
0

Mwigizaji wa filamu za kibongo aliyesemekana kuwa amekatwa nchini brazil akiwa na madawa ya kulevya Aisha Bui ameonekana nchini hivi karibuni akiwa kwenye salooni ya mwanadada mwingine muigizaji Nisha iliyopo maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam.

Mwadada huyo ambaye tayari ameigiza filamu kadhaa na mastaa wenzake alionekana kwenye saloon ya Salma Jabu(Nisha) akiwekwa sawa nywele zake kama anavyoonekana pichani.

CREDIT: BONGO MOVIE

YANGA IKIJIFUA KUJIWINDA YA NANI MTANI JEMBE

MAZISHI YA MANDELA: DUNIA KIMYA

$
0
0

DUNIA ipo kimya wakati maandalizi ya kuupumzisha kaburini mwili wa aliyekuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela yakiendelea katika miji ya Johannesburg, Pretoria na kijijini Qunu, Mkoa wa Mthatha jimboni Eastern Cape atakozikwa kijijini atakakozikwa.

UKIMYA WATANDA KWENYE TELEVISHENI
Ukimya uliendelea kutawala juzi na jana katika miji mbalimbali duniani, watu walikusanyika kwenye televisheni za wazi kufuatilia zoezi la kuuaga mwili huo zilizofanyika katika Jengo la Umoja jijini Pretoria.


Maelfu ya waombolezaji walionesha kuguswa kwa kiasi kikubwa na msiba huo unaotajwa kushika rekondi tangu kuwepo kwa ulimwengu kuwahi kutazamwa na watu wengi zaidi kuliko mingine yote iliyowahi kutokea.
Mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Romani Katoliki Duniani, Papa John Paul wa II unatajwa kushika rekodi ya kwanza hadi Desemba 5 mwaka huu alipokufa Mandela.

PICHA ZA TELEVISHENI ZATAWALIWA NA VIDEO ZA MANDELA
Vituo vingi vya televisheni sehemu mbalimbali ulimwenguni, licha ya kuonesha tukio hilo la kuaga mwili, pia viliweka video ya matukio mbalimbali yaliyowahi kufanywa na kiongozi huyo anayetajwa kama mwanamapinduzi wa kweli, mpigania haki na mwanaharakati aliyeheshimika kuliko mwingine katika karne ya 21.
Baadhi ya matukio hayo ni pamoja na jinsi alivyoshiriki shughuli mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na kupiga picha na wanamichezo, wasanii wengi maarufu, ambao pia walionesha kufurahishwa naye kila alipokutana nao.


SERIKALI SAUZI YASAMBAZA SETI YA TELEVISHENI NCHI NZIMA
Serikali ya Afrika Kusini imesambaza seti ya televisheni zipatazo 90 nchi nzima na kuwekwa katika maeneo mengi ya wazi kwa lengo la kuwawezesha mamilioni ya wananchi wake kuangalia shughuli za kumuaga kiongozi huyo zinavyokwenda.

KIJIJINI QUNU KAMA MJINI
Katika Kijiji cha Qunu alichokulia hayati Mandela, maandalizi ya kaburi atakalozikwa yapo tayari huku kijiji hicho kikijaa watu na kuwa na maisha kama mjini.
Magari ya kila aina yanaingia na kutoka, watu wasiofanana na maisha ya kijijini wanapatikana kwa sasa, wengi wao wakiwa wageni, wakiwemo wa vyombo vya habari, wanaingia na bidhaa zao, hususan chakula.

NDEGE YA KIJESHI KUMPELEKA MANDELA KIJIJINI KWAKE
Serikali ya nchi hiyo imetamka kuwa, mwili wa hayati Mandela utapelekwa kijijini Qunu kwa ndege ya jeshi la nchi hiyo, tayari kwa mazishi yake Jumapili ya Deseamba 15.

WAZEE WA KIMILA WATOA MSIMAMO KUHUSU MAZISHI
Taarifa kutoka kijijini hapo zinasema kuwa jamii ya Kabila la AbaThembu (ndivyo inavyaondikwa), imetaka kukabidhiwa shughuli za mazishi hayo ili shujaa huyo aweze kuzikwa kwa mujibu wa mila za kabila lake.
Kiongozi wa jamii ya Xhosa (lugha ya Waaba Thembu), Nokuzola Mndende alisema kuwa endapo serikali itapuuza matakwa yao ipo hatari ya Mandela kutopokelewa na miungu hivyo roho yake kurejea duniani na kuisumbua familia yake.
“Zitakuwa ni mila na desturi za jadi, serikali inapaswa kutupa nafasi na isituingilie. Ng’ombe dume (fahali) atachinjwa kwa ajili ya kumsindikiza marehemu kaburini,” alisema kiongozi huyo bila kupindisha maneno kinywani.
Aliongeza: “Katika utaratibu huu wa mazishi ya kimila ni familia ya Mandela pekee ndiyo watakaohusika kumwandalia safari njema Madiba.”
Kwa mujibu wa desturi za mazishi za kabila hilo, mtu aliyefariki dunia endapo alikuwa kiongozi, hupewa heshima ya kuchinjiwa ng’ombe dume ili amsindikize ambapo damu yake hunyunyiziwa juu ya kaburi.   

TARATIBU ZA MAZISHI ZA KIKABILA
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, zipo taratibu maalum ambazo ni lazima zifuatwe wakati wa mazishi ya mtu wa kabila moja na mzee Mandela.
Baada ya mtu kufariki dunia, ni jukumu la wanafamilia ya marehemu kutangaza msiba huo kwa ndugu na jamaa ili waweze kukutana na kusaidiana wakati wa mazishi.
Kabla ya ujio wa vyumba vya kisasa vya kuhifadhia maiti (mochwari), Waaba Thembu walikuwa wakimzika mtu siku hiyohiyo kwa kuhofia mwili wake kuharibika.
Kabla ya kufanyika kwa mazishi, taratibu zinasema vyombo vyote vilivyomo ndani ya nyumba hutolewa nje na wanawake wanaohusiana na marehemu ni lazima wafanye usafi katika nyumba aliyokuwa akiishi.
Katika siku za nyuma, kuta za kibanda kikubwa kilichokuwa kikitumiwa na marehemu kulala kilikandikwa udongo, lakini hivi sasa nyumba kubwa kwa kawaida husafishwa na kupakwa rangi upya.
Baada ya usafi huo, mkeka wa kiasili huwekwa katika chumba kikubwa cha kulala ambako mjane wa marehemu hutakiwa kukalia mkeka huo unaowekwa chini ya dirisha.
Uchaguzi wa ng’ombe mnono wa kiume hutegemea na umuhimu wa marehemu na wanaume ndiyo wanaopika nyama hiyo katika vyungu vya kikabila ikichemshwa bila kuwekwa kiungo chochote.
Tukio hili huitwa Umkhapho inayodaiwa kuwa  ni mizimu ya kumsindikiza mtu aliyefariki dunia.

CREDIT: GPL

WEMA Sepetu atibua tena

$
0
0

BEAUTIFUL Onyinye, Wema Sepetu ameendelea ‘kutibua’ hali ya hewa kwa kukiuka maadili ambapo kwa mara nyingine tena ametupia picha mtandaoni zikimuonesha akiwa amevaa mavazi yaliyoacha wazi baadhi ya sehemu nyeti za mwili wake.
Picha hiyo iliyopo kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii inamuonesha Wema akiwa amevaa kiblauzi chenye matundu kiasi cha kuifanya sidiria aliyovaa ionekane huku sehemu nyingine zikiwa wazi.
 
Wakiizungumzia picha hiyo ambayo Wema anaonekana akiwa na rafiki yake, Kajala Masanja, baadhi ya wadau wamesema msanii huyo anaonekana kujisikia raha sana sehemu zake kuwa wazi.

“Mh! Huyu Wema na hivi vivazi vyake vya nusu utupu hajambo, sijui anajisikiaje kuvaa vile…hata kama atasema ni kutokana na hali ya joto lakini hii sasa imezidi, huko ni kuwatega wanaume,” aliandika mdau mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mwanaidi.

Morocco atamba kuipaisha Oljoro

$
0
0
Kikosi cha JKT Oljoro.
Na Amisa Mmbaga
KOCHA wa JKT Oljoro, Hemed Morocco, amesema atahakikisha anakipika vilivyo kikosi chake na kuwa tishio kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Morocco amejiunga na Oljoro kwa mkataba wa mwaka mmoja mara baada ya ajira yake katika timu ya Coastal Union kufikia tamati hivi karibuni.

Morocco ambaye ameanza majukumu mapya katika timu hiyo inayoshika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi, amesema vijana wake wapo vizuri na maandalizi yanaendelea na hakuna mchezaji ambaye ni majeruhi mpaka sasa.

“Wachezaji wapo vizuri kwani nimekaa nao kwa muda wa wiki mbili sasa japo sijawajua vizuri wachezaji wote lakini wanaonyesha muelekeo mzuri na naamini watafanya vizuri.
“Natarajia kukibadilisha kikosi kwa lengo la kufanya vizuri zaidi kwani tulifanya vibaya katika mzunguko wa kwanza,” alisema Morocco ambaye timu yake ina pointi 10 katika mechi 13.

Bahanuzi arudi Bongo kama alivyoondoka

$
0
0

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Said Bahanuzi amemaliza majaribio yake ya wiki moja aliyokwenda kufanya nchini Malaysia katika Klabu za Teregganu na T-Team ambapo amerejea nchini.

Bahanuzi aliondoka nchini Alhamisi iliyopita kuelekea nchini humo kwenda kufanya majaribio ya wiki moja kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa.

Akizungumza  Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema Bahanuzi alifanya majaribio katika timu mbili tofauti alipokuwa Malaysia katika timu za Teregganu na T-Team.
 
“Bahanuzi amemaliza leo (Jumatano) majaribio na usiku ataanza safari ya kurudi Tanzania kwa ajili ya kujiunga na wenzake mara baada ya kuwasili. Timu zote hizo zipo nchini Malaysia zinashiriki Super League lakini majibu ya majaribio bado sijayapata,” alisema Baraka.
CREDIT: GPL

Matuta yaizamisha Kili Stars

$
0
0






TIMU ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars imeikosa nafasi ya tatu katika Michuano ya Chalenji iliyomalizika jana nchini Kenya, baada ya kufungwa na Zambia kwa mikwaju ya penalti 6-5.

Katika mchezo huo uliopigwa majira ya saa 8:00 mchana kwenye Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1, ambapo penalti iliyopigwa na nahodha wa Stars, Kelvin Yondani iliota mbawa na kuipa ushindi Zambia.

Zambia ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 52 kupitia kwa kiungo mshambuliaji, Ronald Kampamba.

Katika dakika ya 60, Kocha Mkuu wa Stars, Kim Poulsen alifanya mabadiliko kwa kuwatoa Hassani Dilunga na Athumani Idd ‘Chuji’ na kuwaingiza Ramadhani Singano ‘Messi’ na Haruna Chanongo.
Kuingia kwa wachezaji hao kulibadilisha mchezo wa Stars ambao walianza kulishambulia goli la wapinzani wao na dakika 64 mshambuliaji wa kimataifa wa TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Samatta, akaisawazishia Stars.

Waliofunga penalti za Stars ni Samatta, Erasto Nyoni, Himid Mao, Amri Kiemba na Singano huku waliokosa ni Chanongo, Mrisho Ngassa na Yondani.
Mpaka gazeti hili linaelekea mitamboni, mechi ya fainali ilikuwa ikiendelea kati ya Kenya dhidi ya Sudan.

Straika Simba asaini Oljoro

$
0
0
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Shija Mkina, amesaini mkataba wa mwaka mmoja wakati huu wa usajili wa dirisha dogo kuichezea JKT Oljoro ya Arusha inayoshiriki Ligi Kuu Bara.
Katibu Mkuu wa Oljoro, Ally Njaidi amesema kuwa lengo ya kumsajili mshambuliaji huyo ni kuiimarisha safu ya ushambuliaji.
“Hadi hivi sasa tumefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Simba, Shija ambaye tumeingia naye mkataba wa mwaka mmoja, kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chetu katika mzunguko wa pili.
“Pia kiungo wa zamani wa African Lyon, Jacob naye tumeingia naye mkataba wa mwaka mmoja kama Shija,” alisema Njaidi.

LOWASSA ANUSURIKA KIFO AJALI YA NDEGE

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa.
ABIRIA kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa wamenusurika kifo, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Arusha mchana mchana huu.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Precision aina ya ATR ilipata ajali hiyo wakati ikitua. Matairi yote manne ya nyuma yamepasuka na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria.
 "Yaani Mungu ni mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi chetu Lowassa...Mungu atamlinda jamani...siamini" alisikika akisema mama mmoja miongoni mwa abiria hao wakati akishuka.
Lowassa ni miongoni mwa wana CCM wanaotajwa kuwania urais 2015 na amekuwa na nguvu kubwa katika harakati hizo.

STARS WALIVYOTUA DAR KUTOKA CHALLENGE KENYA

SPEECH YA KIKWETE KWA KISWAHILI ILIVYOFAGILIWA KENYA‏

AIRTEL YAMPOKEA ANDY COLE

$
0
0
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole akiwa sehemu ya VIP kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku mara tu baada ya kuwasili kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kulia) akimkaribisha Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) mara tu baada ya kuwasili nchini kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania . Kati kati ni Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner.  Picha na Mpiga picha wetu.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole akikabidhiwa maua mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania . Picha na Mpiga picha wetu.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kushoto) akimuongoza Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (katikati) kuelekea sehemu ya VIP kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)mara tu baada ya kuwasili nchini jana usiku.  Picha na Mpiga picha wetu.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole akiwa sehemu ya VIP kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku mara tu baada ya kuwasili kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania . Picha na Mpiga picha wetu.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) pamoja na Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner (kulia) wakikamilisha taratibu zakupata hati ya kuingia nchini kwenye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku mara tu baada ya kuwasili kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania . Picha na Mpiga picha wetu.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole akiongea na waandishi wa habari kwenye sehemu ya VIP , Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku mara tu baada ya kuwasili kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania . Picha na Mpiga picha wetu.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kulia) akitete jambo na Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner (kushoto) mara tu baada ya kuwasili kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania . Picha na Mpiga picha wetu.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kulia) akimuelekeza jambo Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner (katika) mara tu baada ya kuwasili kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania . Kushoto ni  Picha na Mpiga picha wetu. Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole. Picha na Mpiga picha wetu.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (mbele) akitoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwelekea hotelini alipofikia mara bada ya kuwasili nchini jana usiku. Nyuma yake ni mwenyeji waka ambaye ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando . Picha na Mpiga Picha wetu.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole akiwa kwenye gari tayari kuelekea hotelini mara baada ya kuwasili nchini jana usiku. Anatarajia kufanya mkutano na waandishi wa habari leo asubuhi. Picha na Mpiga Picha wetu..

MACHO YOTE LEO NI GURUMO 53 TCC CLUB CHANG’OMBE

$
0
0
HATIMAYE ile siku iliyokuwa inasubiriwa na wengi, imewadia, ni GURUMO 53 ndani ya viwanja vya TCC Club, Chang’ombe leo Jumamosi Disemba 14. Kama tangazo linavyojionyesha, ni tamasha kubwa la muziki wa dansi la kustaafu kwa gwiji Muhidin Maalim Gurumo aliyeitumikia fani hiyo kwa miaka 53 mfululizo. Gurumo ataimba angalau wimbo mmoja au zaidi wa kila bendi aliyopitia katika safari yake ndefu kimuziki.
Hadi kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro Chacha, Rufiji Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS – Ndekule, alikuwa ni kiongozi na mmoja wa wamiliki wa Msondo Ngoma ambayo hapo awali ilijulikana kwa majina ya NUTTA, Juwata na OTTU. Gurumo ameitumika Msondo katika majina yote ya nyuma.
Ama kwa hakika ni burudani ya kukata na shoka, bendi kibao, wasanii kibao – ni burudani mwanzo mwisho kuanzia saa 12 jioni mpaka majogoo.

ARSENAL YAKUTANA NA KIPIGO KILALI

$
0
0


Vinara wa Ligi Kuu ya England, Arsenal wamekutana na kipigo kikali kutoka kwa Manchester City cha mabao 6-3 katika mechi iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Etihad jijini Manchester.
Kutokana na kipigo hicho Man City imefikisha pointi 32 wakati Arsenal imebaki kileleni ikiwa na pointi 35.
 Mabao ya Man City yamefungwa na Sergio Agüero katika dakika ya 14, Álvaro Negredo (39), Fernandinho (50 na 88) na David Silva (66).
Theo Walcott aliifungia Arsenal mabao mawili katika dakika ya 31 na 63 kisha Per Mertesacker akaongeza la tatu katika dakika ya 90.

KIJIJI CHA QUNU CHAMPOKEA MANDELA

$
0
0
 Mwili wa hayati Nelson Mandela umepelekwa katika mkoa wa Eastern Cape kwa safari ya mwisho kabla ya kuzikwa siku ya Jumapili kijijini Qunu.
Idadi kubwa ya watu walifurika barabara angalau kumtupia jicho shujaa wao na kutoa heshima zao za mwisho.Mandela aliyefariki tarehe tano Disemba atafanyiwa maziko ya kitaifa siku ya Jumapili,
Mandela's funeral procession drives toward the Union Buildings on December 12. Each morning his remains were transported from the mortuary to the government buildings.
Takriban watu 100,000 walitoa heshima zao za mwisho kwa Mandela mjini Pretoria siku ya Ijumaa kabla ya mamia ya wengine kukosa fursa hiyo pale walipokatazwa kumuona Mandela kutokana na ufupi wa mda.
Kijiji cha Qunu.
People queue to catch a bus to see the remains of Nelson Mandela at the Union Buildings on December 12.
Kijiji cha Qunu ambako atazikwa Hayati Nelson Mandela, kinaomboleza kifo cha shujaa aliyetoka katika kijiji hicho Nelson Mandela.
Mazingira hapa ni ya kipekee, mchanganyiko wa nyumba za kisasa na za kitamduni ambazo mfano wake ni mizinga ya Nyuki.
Visima vya maji anavyovikumbuka Mandela bila shaka hawezi kuviona sasa. Lakini viwanja vya kijiji hiki viko chini ya majabali ambayo yeye na rafiki zake walikesha wakichezea.
Ni viwanja hivi ambapo Madiba alijifunza kuwinda Ndege , kuchukua asali misituni na matunda ya misitu ambayo ilikuwa inaliwa wakati huo.
Alipokuwa na umri wa miaka 5, Mandela aliandika kumbukumbu zake kuhusu safari yake alivyopigania uhuru wa Afrika Kusini, pia alijifunza kuchunga Ng’ombe, na kupitia kwa kazi hiyo alijifunza uhusiano uliopo kati ya watu wa kabila la AbaTembu na Ng’ombe wao.
Alisomea hapa Qunu, lakini kijiji alichokiacha kwa huzuni wakati alimzika babake kimebadilika. Lakini aliporejea hapa mwaka 1990 alipokuja kutembelea kaburi la mamake , alisema aliona umasikini mkubwa machoni mwa watu wa Qubu, viwanja visafi alivyovikumbuka havikuwepo tena, vilikuwa vimejaa takataka kitu ambacho hakuwahi kukiona tangu alipokuwa mtoto.

Hata hivyo Kijiji cha Qunu bila shaka kimebadilika pakubwa, ni kisafi kikubwa na kina dalili za maendeleo, wala sio taswira aliyoitoa Mandela katika kumbukumbu zake kuhusu nyumbani.

Na sababu moja ya hilo ni kuwa alijenga nyumba hapa pamoja na shule, alilemaji, umeme, pamoja na mapato kwa watu wa eneo hili kutokana na makavazi aliyojengewa Mandela ambako atazikwa.


NELSON MANDELA LAID TO REST; WATCH LIVE STREAM OF FUNERAL

DAR LIVE ILIVYOWAKA MOTO JANA‏

$
0
0


Mwimbaji wa bendi ya Five Star Taarabu Ali Jay akikonga nyoyo za mashabiki waliofurika katika Tamasha  la muziki huo lililoandaliwa na Redio ya Times Fm   katika ukumbi wa Dar live Mbagala.
Mwimbaji wa bendi ya Five Star Taarab ,Aisha Mgonjela akiimba kwa hisia kali wakati wa Tamasha liliofanyika Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam,Tamasha hilo liliandaliwa na Redio ya Times FM.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Redio Times Fm ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha la muziki wa taarabu uliofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala hapo jana na kudhaminiwa.
Mkongwe wa muziki wa Taarab Malkia Khadija Kopa akiwapagawisha mashabiki wa muziki huo waliofurika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala  jijini Dar es Salaam,kwenye Tamasha maalumu lililoandaliwa na kituo cha Redio Times FM.

RASI KIKWETE AHUTUBIA KATIKA MAZISHI YA MANDELA

$
0
0

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amehutubia kwenye shughuli ya mwisho ya kumuaga Nelson Mandela katika Kijiji Cha Qunu ambapo ndipo maziko yanapofanyika hapo baadaye.
Rais Kikwete amesimulia uhusiano wa karibu uliokuwepo enzi za utawala wa Mandela na Mwalimu Nyerere.
Mwili wa hayati Mandela utazikwa kwa tamaduni za Xhosa, ambapo ng’ombe dume atachinjwa na jeneza la Mandela kufungwa kwa ngozi ya Chui.

OKWI ATUA YANGA SC

$
0
0
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es SalaamKLABU ya Yanga SC ya Dar es Salaam imemsajili mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Emmanuel Arnold Okwi raia wa Uganda kwa Mkataba wa mia miwili na nusu. Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb amesema jioni hii mjini Dar es Salaam kwamba wamemsajili Okwi na ataanza kuichezea timu hiyo mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara na michuano ya Afrika.
 
Etoile du Sahel ya Tunisia ilimnunua Okwi kutoka Simba SC Januari mwaka huu kwa dola za Kimarekani 300,000, lakini mchezaji huyo akaamua kuachana na klabu hiyo na kurejea kupumzika kwao Uganda, kwa madai hakulipwa mishahara kwa miezi mitatu. 
Wakati huo huo, Etoile hadi sasa haijailipa Simba SC fedha zake za kumnunua mchezaji huyo na sakata lake limefikishwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).Baada ya Okwi kukaa bila kucheza kwa miezi sita, Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA) lilimpigania aruhusiwe kurejea nyumbani kuichezea SC Villa ya huko ili kunusuru kiwango chake.  
Hata hivyo, baada ya kung’ara na timu ya taifa ya Uganda ‘The Ceanes’ nchini Kenya kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwezi huu , Okwi anasajiliwa Yanga SC. 
Bin Kleb amesema kwamba walimsajili Okwi tarkiban siku sita zilizopita, lakini Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) imepatikana leo na ndiyo maana wameamua kumtangaza. 
“Amesaini mkataba kiasi cha siku sita zilizopita, ila taratibu za uhamisho zimekamilika leo. Atakuwa nasi kwa misimu miwili na nusu ijayo,”alisema Bin Kleb. 
Alipoulizwa kuhusu utata wa sakata lake ambalo limefika hadi FIFA, Kleb alisema; “Tumefuatilia kote, hadi kwa wanasheria, na tumefanikiwa kupata hadi ITC yake, nawaambia mashabiki wa Yanga wajue viongozi wao wanafanya kazi, hatuna stori nyingi, sisi tunafanya vitendo, tunafanya kazi kwa siri sana,”. 
“Na tumepitia sehemu zote, tumeona kabisa tuko sahihi katika kumsajili mchezaji huyu na hakutakuwa na tatizo lolote upande wetu,”alisema.  
Bin Kleb alisema lengo la Yanga SC ni kufanya vizuri katika Ligi ya Mbingwa Afrika mwakani na ndiyo maana wameamua kuimarisha timu kwa kusajili wachezaji wazuri.

Diamond Platnumz - BTM (Double Date 5), Coke Studio Africa, Season 1

Viewing all 12768 articles
Browse latest View live