Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

Kim Kardashian atoboa siri ya kutompigia kura Donald Trump

$
0
0
WAKATI joto la uchaguzi mkuu wa rais Marekani unaotarajiwa kufanyika Novemba 8, mwaka huu likizidi kupamba moto, mwanadada mwenye jina kubwa duniani, ambaye pia ni mke wa Mwanamuziki Kanye West, Kim Kardashian amefunguka kuwa kura yake hawezi kumpa mwanasiasa anayewakilisha Chama cha Republican, Donald Trump kwa sababu si aina ya kiongozi ambaye dunia inamhitaji kwa sasa.

Kuhusu nani atampigia kura, Kim alisema baada ya kufanya uchunguzi wake kwa muda akiwafuatilia wanasiasa wote ambao wamejitokeza kuwania kiti cha urais na kupima sifa zao ikiwemo kusikiliza sera wanazozitoa,  amegundua kuwa Hillary Clinton ndiye mtu sahihi ambaye atampigia kura yake.

 “Linapokuja suala la kitaifa kama hili sihitaji kufikiria kuhusu mimi mwenyewe, nahitaji kuwaza kuhusu watoto wangu, matumizi mabovu ya silaha, kulinda haki za akina mama na maendeleo kwa ujumla ambapo nina uhakika basi la Hillary linanifaa sana kupanda,” alisema Kim. Hata hivyo, mbali na kauli hiyo, Kim na mumewe Kanye West wamewahi kuonekana kwenye mkutano wa Hillary Clinton uliofanyikia katika Ukumbi wa Scooter Braun’s Los Angeles Home, hapohapo Marekani jambo lililovifanya vyombo vya habari kuripoti kuwa wanamsapoti Hillary Clinton.

Meneja wa Diamond Athibitisha Diamond Kanunua Nyumba Afrika Kusini

$
0
0
Kuna nyumba ilikuwa sokoni inayofanana na ile Diamond amedai kuinunua South, zinafanana tu ama ni ile ile? Hilo ni swali ambalo hadi sasa wengi wamekuwa wakijiuliza, lakini sasa Bongo5 ina jibu la uhakika.

Wiki iliyopita Diamond Platnumz alitengeneza vichwa vya habari baada ya kupost kwenye Instagram picha ya nyumba anayodai ameinunua nchini Afrika Kusini itakayotumiwa na mchumba wake Zari.

Picha hiyo aliisindikiza na maelezo mazito yaliyowalenga wale aliowaelezea kama wanaopenda kujisifia ni matajiri na kumuita yeye maskini ilhali watoto wao bado wanaishi kwenye nyumba za kupanga. Wengi walitafsiri kuwa dongo hilo lilimlenga ex wa Zari, Ivan anayefahamika kwa kuishi maisha ya kifahari.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya Diamond kuweka picha hiyo, wametokea watu ambao wamesambaza picha ya nyumba nyingine inayofanana kwa karibu asilimia 100 na nyumba ile iliyowekwa kwenye mtandao wa privateproperty.co.za na hivyo kuzusha minong’ono mingi.

Kwa mujibu wa meneja wa Diamond, Sallam, nyumba hiyo imelipiwa Alhamis iliyopita na tayari ni mali ya muimbaji huyo wa Salome na amefafanua kwanini bado haijatolewa kwenye tovuti hiyo.

“Nyumba imelipiwa thursday haiwezi toka muda huo huo kwenye website mpaka agency amalizane na mwenye nyumba then process zote zikamilike ndio inatolewa kwenye site,” Sallam ameiambia Bongo5.

Nyumba hiyo ipo Moreleta Park, mjini Pretoria.


Ina vyumba vitano, lounge 3, mabafu matatu, bwawa la kuogelea, balcony, gereji mbili na nyumba ya pembeni ya kuishi wafanyakazi.

Ipo kwenye eneo lenye ukubwa wa mita za mraba, 1068.


Bei yake si haba, ilikuwa inauzwa kwa Rand 2,480,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 396 za Kitanzania.

Kuhusu anachokisema Diamond baada ya watu kudhani kawapiga changa la macho watanzania, Sallam amejibu, “Anachukulia kawaida, ni mengi kila siku yanasemwa.”

Hiyo ni sababu kubwa staa huyo ameamua kujizawadia mapumziko mahsusi visiwani Zanzibar mwishoni mwa wiki.

UPDATES:

Kibao cha ‘SOLD’ kimeshaweka kwenye nyumba aliyonunua Diamond, Pretoria, Afrika Kusini na tayari imeshatolewa kwenye listings za mtandao wa http://www.privateproperty.co.za. Na sasa ni mali yao halali..

Picha za Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange zinazokimbiza katika mitandao!

$
0
0

  Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’.











Mdahalo Wagombea Urais Marekani Watawaliwa Na Kejeli Na Vijembe

$
0
0


Donald Trump na Hillary Clinton kabla ya kuanza kwa mdahalo huo.
NEW YORK , MAREKANI: Homa kubwa nchini Marekani kwasasa ni uchaguzi mkuu wa rais wa nchi hiyo unaotarajia kufanyika Novemba 4, 2016.
Homa hiyo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na wagombea wa pande zote mbili, mwanamama Hillary Clinton wa Chama Cha Democratic na Donald Trump wa Chama Cha Republican ambao kura za maoni zinaonesha wanakabana koo kuwania nafasi hiyo muhimu.
Usiku wa kuamkia leo wagombea hao wamepambana vikali katika mdahalo wa kwanza wa televisheni ambapo wamepingana katika masuala mbali mbali ikiwemo masuala ya sera, kodi, ajira na uchumi.trump….Wagombea hao wakiwa kwenye mdahalo huo.
Vilevile wote wamezungumzia kuhusu Vita vya Iraq na juhudi za kukabiliana na kundi linalojiita Islamic State ambalo inadaiwa chimbuko lake kubwa ni kutokana na vita hivyo.
Msimamizi wa mdahalo huo, Lester Holt alimwuliza Donald Trump mbona hadi kufikia sasa bado hajaweka wazi taarifa zake za ulipaji kodi.
Mwanamama Hillary Clinton amemshutumu mpinzani wake akisema amekuwa akikwepa kulipa kodi na kudokeza kwamba hilo lina maana kwamba bwana Donald Trump hawezi kuwa na wanajeshi imara, pesa za kulipa wanajeshi waliostaafu pamoja na kufadhili elimu na huduma ya afya.
Lakini tajiri huyo kutoka New York amejibu kwa kusema kwamba atatoa hadharani taarifa hizo iwapo Bi Clinton naye atakubali kutoa barua pepe 33,000 ambazo zilifutwa kutoka kwa akaunti yake wakati wa uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba alitumia barua pepe ya kibinafsi kwa kazi rasmi alipokuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani.
Bi Clinton amekubali lawama kuhusu kosa hilo na kusema hakuwezi kuwa na “kisingizio”.
Kadhalika, Donald Trump amemlaumu mpinzani huyo wake kuhusu kupotea kwa ajira akisema nafasi za kazi “zinaikimbia nchi” na akalaumu mikataba duni ya kibiashara.
Amesema Hillary Clinton amekuwa mtu wa “maneno mengi, bila vitendo”.
Bi Clinton ameahidi kuongeza uwekezaji na kuahidi kuunda nafasi takriban 10 milioni za kazi.
Mdahalo huo ulioandaliwa jijini New York huenda ukawa mdahala uliotazamwa na watu wengi zaidi katika historia ambapo watu 100 milioni inakadiriwa walitazama mdahalo huo.
Kura za maoni zinaonyesha wawili hao wanakaribiana sana katika uungwaji mkono.
Mambo mengine makuu yaliyoibuka kwenye madahalo:
Trump amesema hata jeshi linajua yeye anafaa kuwa Amiri Jeshi Mkuu, ISIS ni Wadukuzi na jeshi limemuidhinisha kuwa yeye ni mtu thabiti kuwa Amiri Jeshi Mkuu.
Bwana Trump pia amewashutumu Rais Obama na Hillary Clinton kwa kuweka nafasi katika nchi zenye migogoro kama Libya na Syria jambo lililoruhusu kumea kwa makundi kama ISIS na pia kuondoa majeshi mapema nchini Iraq ndiko kumepelekea kuimarika kwa ugaidi wa ISIS.
“Umekuwa ukikabiliana na ISIS maisha yako yote,” Bwana Trump amemkejeli Bi Clinton
Pia amemzungumzia Bi Clinton na kusema hana uwezo wa kudhibiti ukali wa kumuwezesha kuwa rais. Anadai mwanamama huyo ni mpole sana.
Trump amesema Wamarekani Weusi wanaishi “katika jehanamu” nchini Marekani, kwa sababu maisha yao yamekuwa hatari sana.
Akijibu kupigwa risasi kwa watu weusi, bwana Trump amesema suluhu ni kurejesha utawala wa sheria.
Bi Clinton amesema akichaguliwa kuwa rais atatekeleza mageuzi katika mfumo wa sheria kwa sababu “suala la asili limekuwa likiamua masuala  mengi ya muhimu”.
Hillary Clinton “Trump anajenga urafiki na viongozi wa mataifa wahasimu kama Russia, China na Iran na kwamba Rais Putin wa Russia ameruhusu mashambulizi ya mtandaoni kutoka Moscow.”
Pia mwanamama huyo amesema ana wasiwasi na urafiki wa Donald Trump na Vladmir Putin na kwamba Trump hafai kukaa White House.
Baada ya mdahalo kumalizika wagombea wote wamekubaliana kuheshimu matokeo.
Bado midahalo miwili itakayofanyika kabla ya uchaguzi mkuu wa Novemba 4, 2016.

Wabunge EU wamuunga mkono Magufuli

$
0
0

WAKATI Rais John Magufuli wa Tanzania akishikilia msimamo kuwa nchi yake haitasaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) na Umoja wa Ulaya (EU) mpaka dosari kadhaa zitakaporekebishwa, baadhi ya wabunge wa EU wamemuunga mkono na kutahadharisha mkataba wa sasa utaua viwanda vya ndani.
Siku kadhaa zilizopita, msimamo wa Tanzania na Burundi ulilazimisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kukubaliana kusogeza mbele makubaliano ya ama zote zisaini mkataba huo au la ili kuruhusu uchambuzi zaidi.
Tayari nchi za Kenya, Uganda na Rwanda zimekubaliana na mkataba huo wa EPA huku Tanzania na Burundi zikitoa sababu nzito za kiuchumi, zinazolenga kuhakikisha kuwa kabla ya kusaini mkataba huo, ni vyema suala la ulinzi wa viwanda vya ndani likazingatiwa.
Mkataba huo unapaswa kusainiwa na nchi zote ili uanze kutumika katika ukanda mzima.
Chini ya mkataba huo ambao majadiliano yake yalianza tangu mwaka 2007, EU inaahidi kuzipatia bidhaa kutoka ukanda wa Afrika Mashariki soko kwa kutotozwa kodi zinapopelekwa kwa nchi wanachama wa Ulaya, lakini na yenyewe italeta bidhaa zake katika soko la ukanda bila kutozwa kodi. Hata hivyo, msimamo wa Tanzania umesimama katika ulinzi wa viwanda vya ndani, hasa wakati huu Serikali ikijikita zaidi katika uchumi wa viwanda.
Msimamo huo sasa unaungwa mkono na wabunge wawili wa EU, Marie Arena na Julie Ward, ambao wanashauri Afrika Mashariki isisaini mkataba huo wa ubia kwa namna ulivyo sasa.
Katika mahojiano yao maalumu na mwandishi wa mtandao wa jarida mashuhuri la The New Times, wabunge hao wanasema bayana kuwa uamuzi wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki wa kuahirisha kusaini ubia huo hadi mwakani ili watafakari zaidi uko sahihi.
“Tunaamini mkataba huu kwa namna ulivyo sasa hauko sawa. Ulaya inaitumia Kenya ambayo ndiyo yenye maslahi zaidi katika mkataba huu kuwa kama ngao yao. Wakati Kenya ilishaendelea kiviwanda, hali sio kama hivyo kwa Tanzania, Uganda na Burundi ambazo hazitafaidika.
“Iwapo bidhaa za Ulaya zitaruhusiwa kuingia tu katika ukanda wa Afrika Mashariki italeta ushindani usio wa haki na zaidi nchi hizo zitapoteza kodi katika baadhi ya bidhaa na pia baadhi ya viwanda vitashindwa ushindani na kufa,” wanasema wabunge hao.
Wabunge hao wananukuliwa wakisisitiza kuwa kutokana na hali hiyo, wamejitolea kuzisaidia nchi kama Tanzania na Afrika kwa ujumla kwa kuzishinikiza nchi za Ulaya zipitie upya ubia huo na kuanzisha mfumo mpya wenye manufaa kwa pande zote.
“Tunadhani nchi hizi zinapaswa kusubiri mpaka zote zitakapoingia katika uchumi wa kipato cha kati ndipo zinaweza kuingia mikataba kama hii yenye kuleta ushindani wa kibiashara. Kwa Rwanda na nchi nyingine za EAC sisi tunaona kwa sasa wangeimarisha kwanza soko lao la ndani katika ukanda huo,” wanaongeza wabunge hao.
Wabunge hao wanafafanua kuwa kwa sasa Kenya, ambayo imeshaingia katika uchumi wa kipato cha kati inaweza kufaidika, lakini wanaonya nchi nyingine hazitafaidika na EPA mpaka hapo watakapofikia uchumi wa kati. Walipoulizwa ni kwa nini wakiwa wabunge wa Ulaya, bado wanapingana na mkataba huo utakaoipa faida za kiuchumi jumuiya yao, wabunge hao walijibu:
“Hoja yetu sio kupinga biashara na Afrika Mashariki, tunachotaka ni kuona ubia huu unanufaisha pande zote. Tunazo taarifa nyingi za kitafiti hata kutoka Kituo cha Kimataifa cha Biashara zinazoonesha kuwa mkataba huu utakuwa na hasara kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.”
Wabunge hao wanazidi kufafanua kuwa mikataba mibovu inayoingiwa na Ulaya na Afrika inaathari nyingi ikiwemo kusababisha umasikini Afrika na matokeo yake kuleta athari mbaya kwa Ulaya ikiwemo kuongezeka kwa wahamiaji haramu.

SITALIA TENA - 02

$
0
0

NYEMO CHILONGANI
Saida alikuwa kwenye wakati mgumu, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya. Ni kweli alikuwa kwenye mahusiano mazito na mwanaume ambaye hakuwahi kuonana naye, walijuana kwenye mitandao na kuweka uhusiano mkubwa, ukaribu uliokuwa ambao ulimfanya kila mmoja kuwa karibu na mwenzake.
Akaombwa kuwa mpenzi wake na hivyo kuolewa lakini bado kwake kulikuwa na mtihani mgumu. Alimpenda Kareem zaidi ya mwanaume mwingine yeyote yule, na hakuwa radhi kumuona akiondoka mikononi mwake lakini suala la kumkubalia na kuwa wapenzi, kwake ulikuwa mtihani mwingine mgumu.
Alikaa na kujifikiria kwa kipindi cha siku mbili na ndipo akamwambia Kareem kwamba alikubali kuwa mpenzi wake. Huo ndiyo ukawa mwanzo wa uhusiano wa kimapenzi baina ya watu wawili hao.
Mawasiliano yakachanganya na kila mmoja akamuona mwenzake kuwa muhimu katika maisha yake. Siku zikakatika huku mapenzi ya mtandaoni yakiendelea kunoga. Baada ya miezi sita mingine, Kareem akamwambia Saida kwamba alitaka kumfuata nchini Tanzania, aende akajitambulishe kwa wazazi wa msichana huyo.
Hilo halikuwa tatizo, Saida akawaambia wazazi wake. Kwanza wakashtuka, walishangaa, hawakuamini kile walichoambiwa na binti yao. Ilikuwa vigumu kumwamini mwanaume huyo kwani kulikwishawahi kutokea wanaume wengi ambao walianzisha uhusiano wa kimapenzi na wasichana kwenye mitandao lakini mwisho wa siku, kulikuwa na mambo mabaya yaliyowatokea.
“Una uhakika huyu ni mtu mwema?” aliuliza baba yake.
“Baba! Siwezi kulijibu swali hilo, ila nahisi ni mtu mwema kwani kwa jinsi tunavyowasiliana, anaonekana ni mtu mzuri sana,” alijibu Saida.
“Halafu yeye akija atataka na wewe uende kwao, ndiyo?” aliuliza mama yake.
“Ndiyo mama! Tumelizungumzia hilo pia. Ananipenda na ninaomba mumkubali,” alisema Saida.
“Mmh!”
“Nawaombeni jamani! Nataka niolewe na Kareem,” alisema Saida.
Kwa jinsi alivyokuwa akizungumza, machozi yalikuwa yakimlenga, moyo wake ulimpenda sana mwanaume huyo na hakuwa radhi kumuona akiondoka mikononi mwake.
Wazazi wake hawakuwa na jinsi, binti yao alipenda, tena kitu kizuri ni kwamba alimpenda mwanaume wa dini yake hivyo suala la kuoana halikuwa tatizo kabisa. Wakamkubalia na kumwambia kwamba huyo Kareem alikaribishwa kwenda Tanzania na kujitambulisha.
“Nashukuru sana,” alisema Saida.


“Usijali binti yetu. Ila utatakiwa kuwa makini! Hutakiwi kumwamini kila mtu kwenye mtandao,” alisema baba yake.
Saida akamwambia Kareem kilichokuwa kimetokea, ilikuwa ni furaha kwake na alimuahidi kwamba ndani ya wiki moja angekuwa nchini Tanzania. Hilo ndilo likafanyika, kama utani, Kareem akatua nchini Tanzania.
Kitendo cha kumuona Saida uwanja wa ndege kilimfurahisha, akamfuata na kisha kukumbatiana. Huyo ndiye alikuwa msichana wake, aliyempenda kwa moyo wa dhati na ndiye aliyemfanya kusafiri kutoka nchini Oman mpaka Tanzania kwa ajili yake.
“Karibu mpenzi! Siamini kama umekuja kuniona,” alisema Saida, alishindwa kuyazuia machozi yake.
“Nimekuja kwa ajili yako! Nyumbani wazima lakini?”
“Wazima!”
Wakaondoka na kwenda hotelini. Wakafika katika Hoteli ya Nyota Tano ya Caspean iliyokuwa Mikocheni B na kutulia huko. Wahudumu wa hoteli hiyo walipomuona Kareem, hawakuamini kama kwenye dunia hii kulikuwa na mwanaume aliyekuwa na sura nzuri kama alivyokuwa mwanaume huyo.
Kila mmoja alimpenda, walimuonea wivu Saida na kuona kama alikuwa mwanamke mwenye bahati kubwa, kuwa na mwanaume kama Kareem halikuwa jambo la kawaida hata kidogo.
Kareem akaenda kuoga huku akimwacha Saida chumbani. Alipomaliza, akatoka, akajifuta maji, baada ya dakika kadhaa, wote wakajikuta wakiwa watupu kitandani na ni sauti za mahaba ndizo zilizokuwa zikisikika chumbani humo.
Sauti hizo zilisikika kwa saa moja, wote wakainuka na kuelekea bafuni kuoga, baada ya hapo wakaondoka na kuelekea nyumbani kwa kina Saida.
“Ninatamani kuwaona wazazi wako, inaelekea ni watu wazuri sana mpenzi,” alisema Kareem huku wakiwa ndani ya teksi.
“Bila shaka utawafurahia, wao wenyewe wanatamani sana kukuona,” alisema Saida, hakutaka kuutoa mkono wake kwa Kareem.
Safari hiyo iliwachukua dakika thelathini, wakafika Magomeni Mapipa ambapo wakateremka na kuelekea ndani. Siku hiyo hata majirani walikwenda kwao kwani waliambiwa kuhusu Kareem, hivyo kila mmoja alitaka kumuona.
Kitendo cha kuingia tu, kila mmoja akaanza kupiga makofi. Kareem hakulizoea hilo, alishangaa lakini moyo wake ulikuwa na furaha mno kwani hakuamini kama angepokewa kiasi hicho.
Wazazi wakamfahamu siku hiyo, wakamkaribisha na kutoa baraka zote kwamba binti yao awe na mwanaume huyo. Kwa kuwa familia ya Saida haikuwa ya kitajiri na nyumba waliyokuwa wakiishi haikuwa nzuri, baada ya wiki moja kukaa nchini Tanzania, alichokifanya Kareem ni kuwanunulia nyumba nyingine iliyokuwa Mbezi Beach, nyumba kubwa na ya kifahari.
“Nitataka mke wangu aishi humu kwa sababu ni mkwe wa bilionea mkubwa,” alisema Kareem.
Ilikuwa ni bahati kubwa, maisha yake hayakuwa na mbele wala nyuma lakini ghafla yakabadilika na kuwa ya mtu fulani mwenye pesa nyingi. Kareem alipanga kuibadilisha familia hiyo kwa sababu tu alimpenda mno Saida.
Familia ikapewa hela nyingi na kufungua biashara. Wakatoka Magomeni Mapipa na kuelekea Mbezi Beach huku wakiyaendesha maisha yao huko. Kwa familia nzima, hawakuamini kilichokuwa kikiendelea, wakati mwingine walihisi kama maigizo ambapo baadaye ‘scenes’ zao zingeisha na kurudi Magomeni au kwenye ndoto ndefu nzuri na ya kusisimua na baadaye wangeamka na kujikuta wakiwa vitandani. Hiyo haikuwa filamu, haikuwa ndoto bali kilikuwa kitu halisi kilichokuwa kikiendelea.
Baada ya kukaa nchini Tanzania kwa wiki mbili, Kareem akaondoka na kurudi nchini Oman. Wakati huu baba yake hakutaka arudi na ndege ya abiria ila alichokifanya ni kumtumia ndege binafsi na kurudi nyumbani kwao.
Njiani, mawazo yake yalikuwa kwa Saida, alitokea kumpenda mno msichana huyo. Aliwahi kuwa kwenye uhusiano na wasichana wengine lakini kwa Saida, alikuwa tofauti, alikuwa msichana mwenye furaha mno, tabasamu pana ambaye alimjali kupita kawaida.
Hakutaka kuondoka, alitamani aendelee kubaki nchini Tanzania kwa kipindi chote kwani kuwa mbali na msichana huyo tayari ikaonekana kuwa kama mateso makubwa. Ndani ya ndege, kazi yake ilikuwa ni kuwasiliana na mpenzi wake kupitia WhatsApp. Kila mmoja alikuwa akimuonyeshea mwenzake jinsi alivyokuwa akimpenda.
“Hakika nitaishi na wewe mpaka kifo kitakapotutenganisha, na siku ya kufa, nitataka nife nikiwa mikononi mwako,” aliandika Kareem.
“Kama Romeo na Juliet...”
“Ndiyo mpenzi! Nitakupenda hata zaidi ya Romeo alivyompenda Juliet. Wewe ni mama wa watoto wangu, nisingependa kuona ukiteseka, katika maisha yako yote, nitakuwa nawe bega kwa bega. Nakupenda mpenzi,” aliandika Kareem.
Waliwasiliana mpaka ndege ilipotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muscat nchini Oman ambapo akapanda ndani ya gari lililokuja kumchukua na kwenda nyumbani kwao.
Baada ya kulala siku hiyo, siku iliyofuata, Kareem akawaambia wazazi wake juu ya safari yake, aliwaambia namna alivyokutana na msichana huyo huko, alivyopokelewa mpaka kurudi nchini Oman.
Wazazi wake wakawa na furaha mno hivyo walichokihitaji ni msichana huyo afunge safari na kwenda Oman. Hilo halikuwa tatizo kabisa, baada ya wiki kadhaa, Saida akatumiwa tiketi na hivyo kupanda ndege kwa mara ya kwanza na kuelekea nchini Oman.
Alivaa kiheshima, juba jeusi huku kichwani akiwa amevaa ushungi uliozifunika nywele zake. Miguu yake hakuiacha wazi, alivalia soksi kwani alizijua sheria kali za nchi hiyo jinsi walivyokuwa wakikemea mwanamke kutokujisitiri.
Baada ya saa kumi na tano, akafika huko. Alipomuona mpenzi wake, Kareem, akamsogelea na kisha kusalimiana naye kwani alijua kabisa kwamba sheria za kidini za nchi hiyo zilikemea mambo mengi mpaka pale watu walipokuwa wameoana.
Kama alivyopokelewa Kareem nchini Tanzania ndivyo alivyopokelewa yeye nchini Oman. Wazazi wa mwanaume wake walifurahi kumuona na walimkaribisha kwa mikono miwili.
Kutokana na nchi hiyo kutotaka watu kujihusisha na mambo ya kimapenzi kwa kuishi pamoja na wakati hawakuwa wameoana, ilichokifanya familia hiyo ni kumtambulisha Saida kama mfanyakazi kutoka Afrika.
“Ila utatakiwa kuwa makini!” alisema baba yake Kareem.
“Hakuna tatizo baba!”
“Hutakiwi kufanya mapenzi na huyu msichana, si unajua unaweza kumpa mimba kwa bahati mbaya! Ukiona umempa mimba, jua kwamba atauawa kwa kupigwa mawe kama sheria yetu inavyosema,” alisema baba yake.


“Hicho kitu hakiwezi kutokea, siwezi kumpa mimba Saida.”
“Basi sawa. Nashukuru.”
Hicho ndicho alichokijua kwamba asingeweza kufanya mapenzi na Saida hivyo asingeweza kumpa mimba msichana huyo. Ukaribuni wao wa kimahaba ulikuwa ndani ya nyumba tu na wageni walipokuwa wakifika, ilikuwa ni vigumu kugundua kwamba watu hao walikuwa wapenzi kwa namna ambavyo walivyokuwa wakiishi, Saida alionekana kama mfanyakazi wa ndani nyumbani hapo.
Siku zikakatika na hatimaye wiki ya kwanza ikatimia. Hakukuwa na mabadiliko yoyote yale lakini kipindi hicho mwili wa Kareem ukaanza kumuhitaji msichana huyo. Alikuwa mpenzi wake na alikataliwa kufanya naye mapenzi, hakutaka kukubali tena kwani kila alipokuwa naye faragha, msichana huyo alimtamanisha kupita kawaida.
Alichokifanya ni kuanza kuelekea chumbani kwa Saida kila siku usiku. Hakukuwa na mtu yeyote aliyeligundua hilo, huko, walikuwa wakikumbatiana mpaka saa kumi alfajiri ambapo alikuwa akitoka na kwenda msikitini.
Hayo yakawa maisha yao, hakukuwa na siku ambayo Kareem hakuwa akitoka chumbani kwake, walifanya sana mapenzi kisiri, wazazi hawakugundua kitu chochote kile, hawakujua kwamba kila siku watu hao walikuwa wakikutana chumbani kitandani na kufanya mapenzi walivyotaka.
Baada ya mwezi mmoja kutimia tangu Kareem aanze kuelekea chumbani humo, hali ya Saida ikaanza kubadilika. Mwili wake ukaanza kuchoka, kichefuchefu kikamshika na hatimaye kuanza kutapika.
Mara ya kwanza walichukulia ni tatizo la kawaida ila baada ya kuendelea kutokea mara kwa mara Kareem akahisi kwamba mpenzi wake alikuwa na mimba. Akamchukua na kuanza kuzungumza nayye pembeni, alitaka kujua ukweli juu ya kile kilichokuwa kikiendelea.
“Unasemaje?” aliuliza Kareem kana kwamba hakusikia aliambiwa nini.
“Nina mimba mpenzi! Mimba imeanza,” alisema Saida, hapohapo Kareem akakaa chini. Hakuamini alichoambiwa.
“Unasema kweli?”
“Ndiyo!”
“Mungu wangu! Tumekwisha..” alisema Kareem huku kijasho chembamba kikianza kumtoka.
Aliikumbuka vilivyo adhabu ya kifo waliyokuwa wakihukumiwa watu wengine mara baada ya kupewa mimba. Hakutaka kuona hilo likitokea kwa msichana aliyekuwa akimpenda, tena aliyekuwa na mtoto wake tumboni.
Ilikuwa ni rahisi kumwambia Saida aondoke na kurudi nchini Tanzania lakini ugumu uliokuwepo ni kwamba kulikuwa na sheria ya kuwapima mimba watu wote waliokuwa wakitaka kuondoka nchini humo kwani kabla ya hapo, wengi walikimbia nchi hiyo baada ya kuona kwamba walikuwa wajawazito kwani mbali na kupima, kwa wale waliokuwa wameolewa, walitakiwa kuonyesha vyeti vyao vya ndoa kujua kama walikuwa ndani ya ndoa.
“Kwa hiyo?” aliuliza Saida huku akionekana kuogopa.
“Sijajua! Saida, ninachohofia ni kwamba utauawa kwa kupigwa mawe tu,” alisema Kareem huku akionekana kuwa na hofu moyoni mwake.
“Haiwezekani! Ni lazima niitoe.”
“Utaitoaje? Ukienda hospitali, daktari haruhusiwi, na akijua una mimba, kitu cha kwanza kitakuwa ni kuitaarifu serikali. Saida, nimechanganyikiwa,” alisema Kareem maneno yaliyomfanya Saida kukata tamaa ya kurudi nchini Tanzania, iwe isiwe ilikuwa ni lazima kuuawa kwa kupigwa mawe.

Je nini kitaendelea?

Vanessa Mdee na Trey Songz wana mahusiano? Vanessa Afunguka hapa!

$
0
0
Kuna tetesi, picha na video zimesambaa mtandaoni zinazoonesha ukaribu kati ya nyota wa muziki wa R&B nchini Marekani, Trey Songz na Vanessa Mdee, zinazotafsiriwa kuwa huenda wakawa wameenda hatua ya juu zaidi ya kile walichokuwa wakikifanya Nairobi, Kenya.
ctsm9-wwaaagjb_
Wiki iliyopita, Vanessa pamoja na wasanii wengine takriban 9 wa Afrika, waliingia studio na Trey Songz kurekodi wimbo kwaajili ya msimu mpya wa kipindi cha Coke Studio Afrika. Hata hivyo Trey alionekana kuwa karibu zaidi na Vee Money kiasi cha kuzusha tetesi kuwa huenda Jux akawa amesalitiwa.
cti1p1iwcaaxwya
Anasema picha na video hizo zinatafsiriwa vibaya na kwamba yeye na Trey wamewahi kukutana kabla ya hapo na siku zote amekuwa karibu naye.
“Me and J are 100,” Vanessa ameiambia Bongo5 baada ya kuulizwa kuhusu minong’ono hiyo.
“The video and pictures going around are misinterpreted, I worked for MTV and had met Trey before, we were cool then and are cool now,” amesisitiza.
“I respect him [Trey Songz], Juma and all our fans.”
“Being a female artist in Africa, people are always waiting for any opportunity to tarnish ones image , and disregard years of handwork and success. Watch this space am about to give them more. Kazi tu,” ameongeza.
ctfs1prwgaapu31
Kwa upande mwingine Vanessa amedai kuwa watu wasubirie kusikia jinsi wasanii wa Afrika walichokifanya na mshindi huyo wa tuzo za Grammy.
“I can’t wait for you and everyone to hear what we worked on with Trey.”

List Ya Vyuo Vilivyotoa Selection Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo Vikuu Mbalimbali 2016/2017

$
0
0

Kuona Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Chuo Kikuu 2016/2017,
 
==>Chuo  Kikuu Cha Mwalimu Nyerere  <<bonyeza Hapa>> 

==>Chuo  Kikuu Cha  Udsm,duce Na Muce   <<bonyeza Hapa>> 

==>Chuo  Kikuu Cha  Tumaini Makumira    <<Bonyeza Hapa>>   

==>Chuo  Kikuu Cha Udom  <<bonyeza Hapa>>

 ==>Chuo  Kikuu Cha Ifm <<bonyeza Hapa>>

==>Chuo Kikuu Marian << Bonyeza Hapa>>

 ==>Chuo Kikuu Cbe        << Bonyeza Hapa>>

==>Tumaini-mbeya     << Bonyeza Hapa>>& <<hapa>>

 ==>Chuo Kikuu Mum         << Bonyeza Hapa>>

==>Chuo Mum(Diploma) <<Bonyeza Hapa>>

 ==>Chuo- Stella Maris  << Bonyeza Hapa>>

 ==>Chuo- Kampala-kiu  << Bonyeza Hapa>>

Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam Degree-2016/2017

$
0
0

The following applicants have been selected to join various undergraduate degree programmes for the 2016/2017 academic year. 
The selected applicants should report at the Mwl. J.K. Nyerere Mlimani Campus on Saturday 8th October 2016 for the orientation week which will start on Monday 10th October 2016. 
Applicants selected for admission into Dar es Salaam University College of Education (DUCE) and Mkwawa University College of Education (MUCE) should report directly to the college's campuses in Chang'ombe and Iringa respectively on the same dates. 
Joining instructions and admission letters should be collected at the University campuses where one is admitted. Joining instructions and other important information can also be downloaded from the University website.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba na Katibu wa Mkoa Watumbuliwa na Rais

$
0
0

Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Steven Makonda baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia maafa iitwayo "Kamati Maafa Kagera" kwa lengo la kujipatia fedha.

Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Simbaufoo Swai kutokana na kuhusika katika njama hizo.

Taarifa hiyo  iliyotolewa na Waziri Mkuu, Majaliwa muda mfupi baada ya kupokea hundi ya msaada kutoka kwa Waziri Mkuu wa India imeeleza kuwa pamoja na kutengua uteuzi huo Rais Magufuli ameagiza vyombo vya dola vichukue hatua dhidi ya wote waliohusika katika njama za kufungua akaunti hiyo.

Kadhalika Rais Magufuli leo amepokea msaada wa Shilingi Milioni 545milioni kutoka kwa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kwa ajili ya kusaidia wananchi wa Mkoa wa Kagera waliopatwa na maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 10 Septemba, 2016.

MKE WA BILIONEA MSUYA AENDELEA KUSOTA RUMANDE

$
0
0





KESI nayomkabili mke wa Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revovatus Muyela ambayo ilikuwa isikilizwe leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar, imeahirishwa, hivyo watuhumiwa hao wataendelea kusota rumande.

Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Magreth Bankika alisema kesi hiyo itasikilizwa Oktoba 10 mwaka huu.

Wiki iliyopita wakili wa washtakiwa, Peter Kibatala aliwasilisha maombi ya wateja wake katika mahakama hiyo, kwa kile alichodai kuwa hati ya mashtaka ilikuwa ina mapungufu kwa kuwa haioneshi kama washitakiwa hao walikuwa wana nia ovu.

Akijibu hoja hiyo ya Kibatala mahakamani hapo, wakili wa serikali, Diana Lukundo alisema hoja zote walizoziwasilisha na upande wa washtakiwa haziko kisheria na kuna aina mbalimbali za kuwasilisha mashtaka.

Baada ya upande huo wa Jamhuri kujibu hoja hizo za upande wa washtakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkazi Mkuu, Bankika, mahakama hiyo ilitarajia kutoa uamuzi wa hoja hiyo leo, hata hivyo, ameahirisha hadi Oktoba 10, mwaka huu.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mnamo Mei 25, mwaka huu maeneo ya Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam, Miriam Mrita na Revocatus Muyela, walimuua kwa kumchinja dada wa bilionea Msuya, Anathe Msuya.



Ibrahim Lipumba Afukuzwa uanachama CUF kuanzia leo

$
0
0

MAAZIMIO NA MAAMUZI YA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LILILOKUTANA KWENYE MAKAO MAKUU YA CHAMA, MJINI ZANZIBAR
TAREHE 27 SEPTEMBA, 2016
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) limekutana leo, Jumanne, tarehe 27 Septemba, 2016 katika kikao cha dharura kilichofanyika Makao Makuu ya Chama, mjini Zanzibar na ambacho kiliitishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa kwa mujibu wa Katiba ya Chama ya 1992 (Toleo la 2014), Ibara ya 80 (1). Wajumbe 43 kati ya wajumbe 53 wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa walihudhuria kikao hicho.
Agenda tatu zilizotayarishwa na kuwasilishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa zilijadiliwa na kufanyiwa maamuzi ambazo ni:
1. Kujadili barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya tarehe 23/09/2016;
2. Kupokea na kujadili mashtaka dhidi ya Prof. Ibrahim Lipumba kutokana na hujuma alizozifanya tarehe 24/09/2016 Afisi Kuu ya Chama, Buguruni, Dar es Salaam;
3. Kumjadili na Kumhoji Prof. Ibrahim Lipumba mbele ya kikao na kumchukulia hatua za kinidhamu.
Baada ya mjadala wa kina wa agenda hizo, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio na maamuzi yafuatayo:
KUHUSU BARUA YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA YA TAREHE 23/09/2016:
1. Baraza Kuu limeukataa ushauri, msimamo na mwongozo wa Msajili wa Vyama vya Siasa alioutoa kupitia barua yake ya tarehe 23/09/2016 kwa sababu Sheria ya Vyama vya Siasa (Political Parties Act, No. 5 of 1992) – Sura ya 258 haimpi mamlaka wala uwezo wowote kutoa ushauri, msimamo au mwongozo kwa vyama vya siasa kuhusiana na maamuzi ya vikao vya Chama na kwa kulitambua hilo ndiyo maana katika matamko yake yote aliyoyatoa, Msajili huyo ameshindwa kutaja kifungu gani cha sheria hiyo kinampa uwezo huo.
2. Baraza Kuu limesikitishwa sana na kitendo cha Jaji Francis Mutungi kujishushia hadhi, kujifedhehesha na kujivunjia heshima mbele ya macho ya jamii ndani na nje ya nchi, yeye na Ofisi anayoiongoza kwa kuvunja sheria na kudharau maamuzi ya Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia UAMUZI wa tarehe 9/5/2005 wa Jaji T.B. Mihayo katika kesi ya Emmanuel Nyenyemela na Magnus Msambila v/s Registrar of Political Parties & Others (Civil Case No. 6 of 2003) ambapo Jaji Mihayo aliamua kwamba:
“… I do not see anywhere in the Political Parties Act where the Registrar has power to bless or condemn meetings of political parties or decisions that they make.”
Tafsiri yake ikiwa ni kwamba, “… Sioni popote katika Sheria ya Vyama vya Siasa ambapo Msajili ana madaraka ya kubariki au kupinga vikao vya vyama vya siasa ay maamuzi ambayo vikao hivyo vinafanya.”
3. Baraza Kuu limemuagiza Katibu Mkuu wa Chama kumjibu kwa maandishi na kwa kina Msajili wa Vyama vya Siasa na kumueleza maamuzi ya Baraza hilo ambalo kikatiba ndilo lenye madaraka ya kusimamia uendeshaji wa Chama kwamba halitambui ushauri, msimamo na mwongozo huo na limeutupilia mbali kwa kukosa kwake mantiki, hoja na pia kukosa nguvu za kisheria.
4. Baraza Kuu linamtanabahisha Msajili wa Vyama vya Siasa kwamba atabeba dhamana kwa yote yaliyofanywa na yatakayofanywa na Prof. Ibrahim Lipumba na kikundi chake cha wahuni ambacho kilivamia Ofisi Kuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam tarehe 24 Septemba, 2016 na kupiga watu na kufanya uharibifu wa mali kutokana na tamko lake hilo ambalo halina msingi wa kisheria.
KUHUSU MASHTAKA DHIDI YA PROF. IBRAHIM LIPUMBA KUTOKANA NA HUJUMA ALIZOZIFANYA TAREHE 24/09/2016 AFISI KUU YA CHAMA, BUGURUNI, DAR ES SALAAM:
1. Baraza Kuu limepokea mashtaka dhidi ya Prof. Ibrahim Lipumba yaliyoandaliwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa ambayo kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 108 (1) ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia nidhamu ya Chama katika ngazi ya Taifa na kuyawasilisha mapendekezo yake mbele ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.
2. Baraza Kuu limeridhika kwamba Kamati ya Utendaji ya Taifa imefuata masharti yote ya Katiba ya Chama ya 1992 (Toleo la 2014) katika kuanda mashtaka hayo kutokana na mtuhumiwa, Prof. Ibrahim Lipumba, kuvunja Katiba ya Chama, Ibara ya 12 inayohusu ‘Wajibu wa Mwanachama” hasa Ibara ndogo za 12 (6), 12(7) na 12(16).
KUHUSU KUMJADILI NA KUMHOJI PROF. IBRAHIM LIPUMBA MBELE YA KIKAO NA KUMCHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU:
1. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limeridhika kwamba Kamati ya Utendaji ya Taifa ilimfikishia mtuhumiwa, Prof. Ibrahim Lipumba, barua ya wito (Kumb. Nam. CUFHQ/OKM/WM/2016/Vol.1/49 ya tarehe 24/09/2016) ambayo pia ilikuwa na maelezo ya tuhuma na kumtaka afike mbele ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kilichofanyika leo, tarehe 27 Septemba, 2016, mjini Zanzibar kuja kujieleza na kujitetea kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Katiba ya Chama kwa kuvunja masharti yanayohusu “Wajibu wa Mwanachama” Ibara ya 12(6), 12(7) na 12(16).
2. Baraza Kuu limesikitishwa na dharau iliyooneshwa na Prof. Ibrahim Lipumba dhidi ya kikao hiki ambacho ni chombo cha juu chenye mamlaka ya kusimamia uongozi wa Chama pamoja na kupelekewa wito wa kumtaka afike mbele yake. Kitendo hicho cha dharau kinaonesha tu jinsi gani heshima na uaminifu wa Prof. Ibrahim Lipumba kwa Chama ulivyoshuka.
3. Baraza Kuu limeridhika kwamba kwa kuwa Prof. Ibrahim Lipumba akiwa mtuhumiwa alichagua mwenyewe kudharau wito wa kufika kujieleza na kujitetea ambayo ni haki yake kama mwanachama kwa mujibu wa Ibara ya 11(6) ya Katiba ya Chama, halikuwa na sababu ya kutoendelea kumjadili na kuchukua hatua dhidi yake.
4. Baraza Kuu limeridhika na mashtaka dhidi ya Prof. Ibrahim Lipumba kwamba kwa kitendo chake cha kuongoza na kusimamia kikundi cha wahuni kuvamia Ofisi Kuu ya Chama, Buguruni, Dar es Salaam, siku ya Jumamosi, tarehe 24 Septemba, 2016 na watu hao aliowaongoza na kuwasimamia kupiga walinzi waliokuwepo, kuvunja na kuharibu mali za Chama na hivyo kuharibu heshima na taswira ya Chama mbele ya jamii ndani na nje kwamba amtenda makosa kinyume na “Wajibu wa Mwanachama” kama ilivyoelezwa kwenye Ibara ya 12(6), 12(7) na 12(16) za Katiba ya Chama.
5. Baada ya kuridhika na mashtaka hayo, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limeamua kwa kutumia uwezo wake kwa mujibu wa Ibara ya 10 (1) (c) na kwa kura zote 43 za wajumbe wake waliohudhuria kumfukuza uanachama Prof. Ibrahim Lipumba, kuanzia tarehe ya leo, Jumanne, tarehe 27 Septemba, 2016.
6. Kwa maamuzi haya, Baraza Kuu linaweka bayana kwa wanachama wa CUF, Watanzania na mamlaka zote nchini kwamba kuanzia tarehe ya leo, Prof. Ibrahim Lipumba hana haki ya kujihusisha kwa namna yoyote ile na shughuli zozote za Chama.
MWISHO:
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linawapa pole wanachama wa CUF walioathirika kutokana hatua ya Msajili kuingilia mambo ya Chama kinyume na uwezo alio nao na pia kwa matendo ya kihuni yaliyofanywa na Prof. Ibrahim Lipumba na kikundi chake kuvamia Ofisi Kuu ya Chama. Wakati huo huo, Baraza Kuu linawapongeza wanachama wote kwa kusimama imara kukilinda Chama chao na linawahakikishia litasimamia wajibu wake wa kikatiba kukiongoza na kukilinda Chama hiki dhidi ya njama za maadui wa ndani na nje.
HAKI SAWA KWA WOTE
BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA
THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi)
27 Septemba, 2016

Ndege Ya Pili Ya Serikali Yawasili Dar

$
0
0
magufuli-plane-6 Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ikitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kufanyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
magufuli-001
magufuli-plane-8-001
Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ikipata Saluti ya maji (Water Canon Salutation) mara tu baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
magufuli-plane-2-001Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ikiegeshwa karibu na pacha wake iliyofika wiki moja uliopita  katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
magufuli-plane-13-001Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard  Chamriho na viongozi wengine wakielekea kwenye Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ilipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
magufuli-plane-10Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard  Chamriho  akisalimiana na nahoda wa  John Kuipers aliyeeendesha Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) na kuiwasilisha salama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwakuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
magufuli-plane-4Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard  Chamriho  akikagua  Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara ilipotua  katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.
magufuli-plane-11Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard  Chamriho akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi pamoja na maafisa wengine wakiwa katika Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara ilipotua  katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.
magufuli-plane-5Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard  Chamriho na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi wakitelemka baada ya kuikagua Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara ilipotua  katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.
magufuli-plane-9Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard  Chamriho  akimpa pongezi   nahoda wa  John Kuipers aliyeendesha aliyeendesha Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara ilipotua  katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.
magufuli-plane-3Nahoda  John Kuipers na Nahodha Owen Davies walioendesha Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) wakifurahia mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.
 PICHA NA IKULU

Kilichoandikwa Leo Septemba 28, 2016 Katika Magazeti ya Tanzania

AUNT: WEMA ATAJIJUA KISA KUWA KARIBU NA ZARI

$
0
0
 
KAMA ni noma na iwe noma! Mwigizaji Aunt Ezekiel amesema kama kitendo cha yeye kuwa karibu na mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kama kitapokelewa vibaya na shosti wake muigizaji Wema Sepetu ‘Madam’, hatajali, atajijua mwenyewe maana hana jinsi. Kauli hiyo imekuja ikiwa ni baada ya Aunt kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mpenzi huyo wa Diamond, iliyofanyika visiwani Zanzibar na picha za Aunt akiwa ameshikilia tumbo la Zari kuvuja mitandaoni. Baada ya picha hizo kuvuja, watu mbalimbali walianza kuchangia kwenye mitandao ya kijamii kwa kusema kitendo hicho hakitamfurahisha Madam huku wengine wakimpongeza Aunt kwa kuonesha anamsapoti kwanza ‘ubavu’ wake halafu marafiki baadaye.

Mara baada ya kuona maoni hayo mitandaoni, R i s a s i Mchanganyiko, lilimvutia waya Aunt na kutaka k u m u u l i z a k w a m b a haoni kitendo hicho kinaweza k u p o k e l e w a tofauti na
Madam ndipo mrembo huyo alipofunguka: “Mimi sioni kama ni tatizo, kupiga picha na Zari na kuwa naye karibu maana anapaswa pia atambue mimi kuwa karibu na yule au Diamond kuna sababu. Mtu wangu mimi (Moses Iyobo) anafanya kazi chini ya Diamond, Zari ni mtu wa karibu wa Diamond sasa wakinialika shughuli yao lazima niende. “Kwanza namuunga mkono mume wangu mtarajiwa Iyobo, lakini pia si vibaya mimi nikiwa karibu na Zari maana namuunga mkono Diamond ambaye ni bosi wa Iyobo.

Naanzaje kumchukia mtu anayesababisha sisi tupate mkate wa kila siku? Kama yeye (Wema) atanichukia kwa hili kwa kweli atajiju maana sina jinsi lakini naamini hawezi kufanya hivyo maana hata yeye ni muelewa,” alisema Aunt. Urafiki wa Wema na Aunt ulikuwa mkubwa sana kipindi cha nyuma lakini katika kipindi cha hivi karibuni, u n a o n e k a n a k u l e g a l e g a hivyo kitendo cha Aunt kuonekana yupo karibu na Zari, k i m e z u a gumzo na kuongeza hisia za watu kuamini kwamba ushosti wao umekufa kabisa!

Jokate Asaka Msusi Bora Mkoa Wa Dar

$
0
0




Mwanamitindo, Jokate Mwigelo kupitia kampuni yake ya kidoti ameandaa shindano la kusaka msusi bora alilolipa jina la msusi wao lengo ni kuwaamsha wasusi wasiokuwa na ofisi na kuwafanya wakitambue kipaji chao.


Akiongea na waandishi wa Habari, Escape One Jokate jana alisema kuwa alikaa na kuona kuwa kundi la wasusi ni watu muhimu  katika masuala ya urembo ndio akaamua kuandaa shindano ambalo litawapa fursa ya kujiendeleza zaidi na kuitambua nafasi yao.


“Unajua siku moja nilitafuta msusi nikaletewa nyumbani dada mmoja ambaye hana ofisi ambaye alinisuka vizuri lakini nilipomuhoji anakazi gani inayompa kipato hakuwa na kazi, ndipo niliona ipo haja ya kuwakuza wasusi wetu ikiwa sehemu ya kutoa ajira na kuwafanya wajitambue,” alisema Jokate.


Jokate alimtaja mshindi wa kwanza kuwa atapata nywele za Kidoti zenye gharama ya shilingi milioni 1.5 Pesa shilingi laki tatu na Draya, wa pili atapata nywele za gharama ya shilingi milioni 1.2 na laki mbili na Draya na wa tatu atapata milioni moja na laki mbili na nusu pamoja na draya.


Washindi watatafutwa kila wilaya ya ambapo kutakuwa na fomu za kujaza ili kuwatambua vema na wanaohusika ni wale tu wasiokuwa na ofisi.

Mahiga: Jumuiya ya kimataifa isaidie kukabili rushwa

$
0
0
ANZANIA imebainisha kuwa juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kukabiliana na vitendo vya rushwa, hazitafanikiwa endapo hazitaungwa mkono na Jumuiya ya kimataifa.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga

Aidha, imezitaka nchi zilizoendelea kuwawajibisha wawekezaji wao, zikiwemo kampuni za mafuta ili zilipe kodi. 

Hayo yalisemwa jijini New York nchini Marekani jana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga alipozungumza katika Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la 71 la Umoja wa Mataifa. Alitumia fursa hiyo kuelezea vipaumbele vya Serikali ya Tanzania.

Alisema lengo namba 16 la Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGS) linatambua kuwa, rushwa inakandamiza juhudi za kupambana na umaskini na usawa wa jinsia, inazuia fursa na inakuwa na kama kodi kwa familia maskini pale wanapotafuta haki.

Balozi huyo alisema Tanzania imeamua kuanzisha vita dhidi ya rushwa kwa kuhuisha uwazi, uwajibikaji na usahihi katika utoaji wa huduma kwenye taasisi za umma.

Alisisitiza kuwa serikali imeweka misingi mizuri ya uwajibikaji, inayomtaka mtumishi wa umma kutambua kwamba wajibu wake wa kwanza ni kutoa huduma bora na kwa wakati kwa umma.

“Juhudi hizi za serikali za kupambana na rushwa hazitaweza kuzaa matunda bila ya kuungwa mkono wa jumuiya ya kimataifa. Nchi zilizoendelea zinatakiwa kuwawajibisha wawekezaji wao pamoja na kampuni za mafuta ili ziweze kulipa kodi stahiki. Ni lazima wawe tayari kurudisha mali na fedha zilizoibwa kutoka nchi zinazoendelea na kuzificha katika nchi zao ili mali na fedha hizo ziweze kusaidia maendeleo yetu,” alisema Balozi Mahiga.

Akizungumzia fursa za jinsia na uwezeshwaji wa wanawake, Waziri Mahinga alisema juhudi mbalimbali zimefanywa na serikali katika kuwawezesha wanawake ikiwemo kushika ngazi za juu za maamuzi kuanzia serikali kuu hadi bunge na uwezeshwaji wa kiuchumi.

Katika kuthibitisha kuwa Tanzania inazingatia usawa wa jinsia katika uteuzi wa ngazi mbalimbali za maamuzi, alisema kwa mara ya kwanza wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Rais John Magufuli aliteua mwanamke kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wa vijana, waziri huyo alisema serikali imeanzisha mfuko wa maendeleo wa vijana ambao hadi kufikia Machi mwaka huu jumla ya Sh bilioni 1.6 zilipelekwa kwa vikundi 284 vya vijana.
Akizungumzia elimu, alisema serikali inatekeleza bila kuchoka kuhakikisha kwamba watoto wote wa kike na wa kiume, wanapata elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari, ikiwa ni pamoja na kuboresha mitaala yake kwa kuzingatia mahitaji ya karne ya 21.

“Alipoingia madarakani, Mheshimiwa Dk Magufuli alitangaza kuwa kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari itakuwa bure. Serikali imetenga zaidi ya Sh bilioni 263 ili kuhakikisha elimu inatolewa bure kwa wote,” alisisitiza Balozi Mahiga.

Aliainisha vipaumbele vingine vya Tanzania mbele ya mkutano huo kuwa ni pamoja na mikakati ambayo serikali imejiwekea katika utekelezaji wa mkataba wa mabadiliano ya tabia nchi, utekelezaji wa malengo ya SDGs, mapambano dhidi ya dawa haramu za kulevya na kukabiliana na ugaidi.

Kwa upande wa migogoro inayoendelea katika nchi za Burundi na Sudan Kusini, Mahiga alizitaka pande zote zinazopingana, kutambua kwamba majadiliano ambayo ni jumuishi kwa pande zote ndiyo njia sahihi ya kutatua matatizo ya nchi yao.

Alifafanua kuwa Tanzania ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, iliitisha kikao kwa ajili kuzungumzia hali ya kisiasa ya Burundi na Sudan Kusini.

CHANZO; HABARI LEO

Picha za siku na Hamisa Hassan Mobeto

$
0
0
 Mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Hassan Mobeto.

Bond: Watoto Wa Wastara Hawakupenda Aolewe

$
0
0

wastaranabondStaa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma akiwa na Bond Suleiman.
SIKU chache baada ya kuripotiwa kupika na kupakua na staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, Bond Suleiman ameibuka na kusema watoto wa mke huyo wa zamani wa Mbunge wa Donge, Sadifa Juma, hawakupenda mama yao aolewe na mtu mwingine zaidi yake.
WASTARA-X
Mbunge wa Donge, Sadifa Juma alipofunga ndoa na Wastara.
Akipiga stori na Za Motomoto News, Bond alisema alipokuwa kwenye ndoa, watoto hao walimfuata na kumwambia kuwa hawakufurahishwa mama yao kuolewa na mtu mwingine kwa sababu ya mapenzi ya dhati aliyokuwa akimuonesha mama yao enzi za uhusiano wao.
wastara (1)
Wastara Juma.
“Upendo wangu ndiyo uliomrudisha Wastara maana niliamua kubadilika na kuachana na pombe kwa ajili yake, nawaomba wanawake wanaonisumbua kunitaka kimapenzi waache kwani ninaye Wastara, mwanamke wa maisha yangu, siwezi kumsaliti tena, ndani ya mwaka huu tutafunga ndoa,” alisema Bond ambaye pia ni muigizaji.

Deni La Bil. 7 Lamziba Mdomo Madam Rita

$
0
0
DAR ES SALAAM: Habari zilizozagaa wiki iliyopita kuhusu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuidai shilingi bilioni 7 Kampuni ya Benchmark Production inayomilikiwa na mjasiriamali, Ritha Paulsen ‘Madam Rita’, zimesababisha mwanamama huyo kuziba mdomo wake kwa kukataa kuzungumzia sakata hilo.

Gazeti hili lilimtafuta mdau huyo mkubwa wa burudani ambaye pia huendesha shindano la kila mwaka la Bongo Star Search (BSS) kutaka kusikia maoni yake kuhusiana na habari hizo zilizotikisa wiki iliyopita, lakini akawa na jibu fupi;


“No comment kwa sasa, nitatoa taarifa hivi karibuni juu ya jambo hilo, lakini siyo leo, muda muafaka ukifika nitafanya hivyo,” alisema Madam Rita.


Wiki iliyopita, TRA ilitoa muda wa siku 14 kwa kampuni hiyo kuwa imelipa deni hilo linalotajwa kuwa ni la kuanzia mwaka 2009, kupitia kwa meneja msaidizi wa madeni wa mamlaka hiyo, Mkoa wa Kodi wa Kinondoni, Sylever Rutagwelera aliyekuwa ameambatana na Kampuni ya Udalali ya Yono.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Yono, Scholastica Kevela, alisema wameifungia kampuni hiyo na kuanzia sasa walinzi wa Yono watalinda na baada ya muda wa siku 14, waliopewa kulipa deni hilo ukipita, watachukua hatua nyingine kisheria ya kuuza mali za kampuni hiyo kwa mnada.


Alisema deni hilo ni kubwa kwa sababu ni muda mrefu umepita bila kodi ya serikali kulipwa na kuwashauri Watanzania kuacha tabia ya kulimbikiza kodi kwa sababu deni litakuwa kubwa ila likilipwa kwa wakati linaondoa usumbufu usio wa lazima.


“Yono tumepewa kazi ya kukusanya madeni ya serikali na tutaendelea kuwakamata wale wote tunaopewa kuwafuatilia, lengo sio kuwaumiza ni kuhakikisha kodi ya serikali inakombolewa kwa manufaa ya nchi yetu, kwa maana tunamuunga mkono Rais Dk John Magufuli kuhakikisha taifa letu linaendelea kwa kukusanya mapato stahiki,” alisema Kevela.
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>