Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

JUVE YAITWANGA DINAMO BAO 4-0 KWAO LIGI YA MABINGWA ULAYA

$
0
0


Dinamo Zagreb: Semper; Situm; Sigali; Schildenfeld; Pivaric; Antolic (Machado 72); Benkovic; Gomes de Sousa (Fiolic 48); Soudani; Fernandes (Hodzic 58); Pavicic
Subs not used: Livakovic; Peric; Henriquez; Gojak
Scorers:
Booked: 

Juventus: Buffon; Barzagli (Muscat 68); Bonucci; Chiellini; Alves; Khedira; Hernanes; Pjanic (Cuadrado 45); Evra; Dybala; Higuain (Mandzukic 71)
Subs not used: Neto; Sandro; Lemina; Sturaro
Scorers: Pjanic 24; Higuain 31; Dybala 57; Alves 85
Booked: 







Simba yavuruga kambi ya Yanga Pemba

$
0
0


KASI ya ushindi kwenye mechi za Ligi Kuu Bara wanayoendelea nayo Simba, imezua hofu kwenye  kambi ya Yanga waliyoweka huko Pemba kujiandaa na mchezo wa watani wa jadi utakaopigwa Jumamosi wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga iliingia kambini huko Pemba juzi Jumatatu mchana wakitokea Shinyanga kuvaana na Stand United, katika mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo ilimalizika kwa kufungwa bao 1-0.


Simba hadi hivi sasa imecheza michezo sita ikishinda mitano huku mmoja wakitoka suluhu na JKT Ruvu wakati Yanga yenyewe imecheza mitano ikishinda mitatu, ikitoa suluhu na Ndanda FC huku ikifungwa mmoja na Stand United.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo limezipata Championi Jumatano kutoka ndani ya kambi hiyo, hofu kubwa imetanda ya kupoteza mechi hiyo kutokana na mwenendo mzuri wa matokeo wanayoendelea kuyapata Simba.


Mtoa taarifa huyo alisema, presha imeongezeka zaidi mara baada ya kipigo walichokipata dhidi ya Stand United hali inayosababisha kuzuka hofu kubwa ya kufungwa katika mchezo huo.


“Tupo kambini Pemba, lakini presha imeongezeka kwa kiwango kikubwa kutokana na matokeo mazuri ya ushindi wanayoendelea kuyapata watani wetu Simba.


“Kiukweli kabisa, wachezaji wetu wanahitaji somo la saikolojia ili kurejesha morali ya timu iliyopotea baada ya kufungwa na Stand, tunajua siyo kazi rahisi lakini tutahakikisha tunafanikisha hilo.


“Uongozi umepanga kukutana na wachezaji siku moja kabla ya mechi kwa ajili ya kuzungumza nao na kikubwa kutuliza presha ya mechi hiyo ili tushinde na hilo linawezekana kutokana na ubora wa kikosi chetu,”alisema mtoa taarifa huyo.


Alipotafutwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Mholanzi, Hans van Der Pluijm kuzungumzia hali hiyo, alisema kuwa: “Siku zote zinapokaribia mechi za watani wa jadi presha inakuwa kubwa kwenye timu kwa kuanzia viongozi, kocha hadi wachezaji, lakini nikwambie kitu tu, wao (Simba) wenyewe wanatuogopa sisi.”

TFF yapata buku mbili mgao Ligi Kuu Bara

$
0
0

HIVI karibuni Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilipigwa na butwaa baada ya kupata mgao wa Sh 2,000 tu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliozikutanisha African Lyon na Mbao FC, Uwanja wa Uhuru, Dar.


Habari za kuaminika kutoka ndani ya TFF, zilidai kuwa katika mchezo huo uliopigwa Septemba 12, mwaka huu na Lyon kuibuka na ushindi kwa bao 3-1, mapato yaliyopatikana yalikuwa ni chini ya Sh 50,000.
“Baada ya kufanyika kwa mgawanyo wa mapato ambao ulifanyika kwa kukata asilimia 18 ya Vat zilibakia fedha kidogo ambazo pia ziligawanywa pande zote zilizokuwa zikihusika na mchezo huo.


“Asilimia 15 ya fedha hizo zilizokua zimebakia baada ya kukatwa Vat, zililipia uwanja, asilimia nane zililipia gharama ya mchezo, asilimia tano zilienda TFF, asilimia tisa zilienda Bodi ya Ligi, asilimia tatu zilienda FA, asilimia 40 ya fedha hizo ilichukuliwa na African Lyon na asilimia 20 ilichukuliwa Mbao FC.


“Kutokana na mgawanyo huo TFF iliambulia shilingi 2,000 tu, huku Mbao FC wakiondoka na fedha kiduchu ambayo haizidi hata Sh 10,000,” kilisema chanzo hicho cha habari.


Alipoulizwa kuhusiana na suala hilo Ofisa Habari wa TFF, Alfred  Lucas alisema: “Ni kweli katika mchezo huo mapato yalikuwa kidogo sana lakini hizo zote ni changamoto ambazo tumekuwa tukikumbana nazo, hivyo viongozi wetu wanaposema shirikisho halina fedha inabidi tukubaliane na ukweli.”

Kuiona Yanga vs Simba buku saba

$
0
0
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Simba unaotarajiwa kupigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo kiingilio cha chini ni Sh 7,000.

Mchezo huo ambao rasmi mashabiki wa soka wataanza kutumia tiketi za elektroniki, utakuwa na viingilio vya aina tatu huku kadi maalum za mfumo huo mpya zikitarajiwa kuanza kutolewa bure leo Jumatano mpaka siku ya mchezo wenyewe.


Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema: “Viingilio vitakuwa ni Sh 30,000 kwa viti vya V.I.P A, V.I.P B na C ni Sh 20,000 na mzunguko ambapo ni viti vya rangi ya bluu kijani na chungwa ni Sh 7,000.


“Tumewaondolea mzigo mashabiki wa soka kwani zile kadi za elektroniki kwa kawaida zinauzwa Sh 3,000, lakini kwa sasa watazipata bure kwenye mawakala mbalimbali wa Selcom, unachotakiwa ni kulipia kiingilio chako kati ya hivyo vitatu, kisha utapewa kadi yako bila ya gharama zingine.”


Wakati huohuo, Meneja Miradi wa Kampuni ya Selcom ambayo inasimamia mchakato huo wa tiketi za elektroniki, Gallus Runyeta, alitaja sehemu zitakazopatikana kadi hizo kuwa ni vituo vyote vya mafuta vya Total, Village Supermarket iliyopo Mbezi Beach, vituo vya mafuta vya Puma na katika matawi yote ya Samaki Samaki. Hiyo ni kwa wakazi wa Dar pekee.


Lakini pia alitaja sehemu zote zenye mawakala wa Selcom Tanzania zinapatikana kadi hizo, ambapo baadhi yake ni Buguruni Sheli, Ilala Bungoni, Vingunguti, Tandika, Buza, Kiwalani na Sinza Afrika Sana.

MAONYESHO YA FILAMU ZA BEIJING 2016 CHACHU KWA UKUAJI WA SANAA NCHINI

$
0
0

 Washindi wa kwanza hadi wa tatu wa mashindano ya sauti waliopatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China wakionesha tuzo baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Washiriki 10 walishinda mashindano hayo. Kutoka kushoto ni Hilda Malecela, Safiya Ahmed na Sadiq Kututwa.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akisalimiana na mmoja wa washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti, Abraham Richard, ambao watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes jijini Beijing, China wakati wa hafla fupi ya Maonyesho ya Matangazo ya Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing 2016.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Anastazia Wambura akizungumza na washindi hao.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,. Anastazia Wambura akiwasisitizia jambo mshindi wa kwanza hadi wa tatu baada ya kuwakabidhi tuzo zao.
 Washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti, Abraham Richard, ambao watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes jijini Beijing, China wakiwa katika picha ya pamoja na kutoka (kushoto) Muwakilishi wa Mamlaka ya Halmashauri ya Beijing, Yang Peili,  Meneja Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa, Dk. Ayoub Riyoba, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, Muwakilishi wa Ubalozi wa China nchini,  Guo HaoDong, Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes,  Guo ZiQi na Kansela wa Utamaduni katika Ubalozi wa China nchini Tanzania, Gao Wei wakati wa hafla fupi ya Maonyesho ya Matangazo ya Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing 2016.
 Washindi hao 10 wakifurahia baada ya kukabidhiwa  tuzo.

Na Dotto Mwaibale

STARTIMES  imefanya Maonyesho ya Michezo ya Kuigiza ya Runinga na Filamu za Beijing ya mwaka 2016 kwa mara ya pili jijini Dar es Salaam kwa lengo lakuendelea kukuza ushirikiano wa iutamaduni baina ya China na Tanzania.

Akizungumza wakati wa maonyesho hayo yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam leo asubuhi, mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura amesema kuwa kwa muda mrefu serikali ya China na Tanzania zimekuwa na mahusiano mazuri katika Nyanja za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.

“Mahusiano mazuri ya kiutamaduni ndiyo yaliyopelekea serikali hizi mbili kuendelea kushirikiana na kuwa marafiki mpaka hivi leo. Uhusiano huo si tu unatunufaisha katika masuala ya kiuchumi bali pia kijamii. 

Kupitia kazi za sanaa kam vile tamthiliya za michezo ya kuigiza na filamu watu huweza kujua na kujifunza tamaduni za kila upande. 

Nawapongeza StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kutuletea maonyesho haya ambayo nina hakika yatakuwa na manufaa makubwa kwa tasnia yetu.” Alisema . Wambura

“Pia ningependa kuwapongeza StarTimes kwa juhudi zao za dhati katika kukuza utamaduni wetu kuipa nafasi lugha ya Kiswahili kuwa mojawapo inayotumika kutafsiri filamu na tamthiliya hizi za 
michezo ya kuigiza. Nimesikia mlifanya shindano la vipaji vya sauti ambapo watanzania kumi walipatikana na watakwenda kufanya kazi katika makao yenu makuu yaliyopo Beijing. 

Hii ni hatua nzuri na jambo la kuigwa kwa kukipa Kiswahili nafasi kubwa. Ninegependa kumalizia kwa kutoa wito kwa washindi waliopatikana kwenda huko China kutuwakilisha vema kama mabalozi wetu na kukifanya Kiswahili kiendelee kutambulika zaidi.” alisema Wambura

Akielezea umuhimu wa maonyesho hayo Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes,. Guo ZiQi amebainisha kuwa kihistoria China imedumisha kwa dhati urafiki na mataifa ya Afrika na kushirikisha tamaduni ndio njia madhubuti itakayoenzi mahusiano hayo.

‘’Utofauti ndio unaofanya dunia pawe mahala pazuri pa kuishi na China na Tanzania kwa muda mrefu zimedumisha utamaduni wao unaovutia zaidi. Katika kilele cha mkutano wa jukwaa la ushirikiano baina ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2015, Rais wa Jamhuri ya watu wa China, 

 Xi Jinping alionesha nia ya kujizatiti katika kudumisha mahusiano mazuri ya kiutamaduni, kuimarish mafunzo baina ya China na Afrika ili kusonga mbele kwa pamoja na vilevile kuhakikisha mustakabali wa ukuaji wa urafiki baina ya China na Afrika.’’Alisema  ZiQi

‘’Kwa kuendelea kukua kwa mahusiano ya maingiliano ya kiutamaduni baina ya watu wa China na Waafrika, michezo ya kuigiza ya runinga na filamu za Kichina imezidi kujizolea umaarufu na kuwa kichocheo muhimu katika kujenga mahusiano baina ya pande hizo mbili. Kwa hivi sasa Beijing inaongoza China katika uzalishaji wa michezo ya kuigiza ya runinga na filamu. 

Mpaka hivi sasa ina taasisi takribani 3,400 zilizojikita katika uzalishaji wa filamu na vipindi vya uninga na uendeshaji, vikiwa tayari vimekwishazalisha zaidi ya mfululizo wa vipindi vya runinga 3,000 na karibuni filamu 300 kwa mwaka.’’ alisema ZiQi

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Teknolojia na Ufundi ambaye alizungumza kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Wang Xiabo alisema kuwa,‘’mnamo mwaka 2014, Halmashauri ya Mamlaka ya Uandishi wa Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Runinga ya Beijing ilishirikiana na StarTimes kuzindua msimu wa Maonyesho ya Michezo ya Kuigiza ya Runinga na Filamu za Beijing katika nchi za Kiafrika. Lengo kubwa lilikuwa ni kuleta simulizi nyingi za Kichina barani Afrika na kukuza uhusiano katika tasnia za filamu na runinga baina ya pande mbili.’’

‘’Maonyesho haya yamefanyika kwa mafanikio makubwa kwa miaka ya 2014 na 2015 mfululizo. Filamu maarufu za Kichina na mfululizo wa michezo ya kuigiza ya runinga  ambayo imeingizwa sauti kwa lugha ya Kiingereza, Kifaransa na lugha nyinginezo tano za Kiafrika zilionyeshwa na StarTimes kwa miaka hiyo iliyopita,’’ alisema Wang Xiabo kuwa,‘’Katika kipindi hiko tamthiliya kama zilipata mapokezi makubwa sana kutoka kwa hadhira ya barani Afrika.

Meneja Mkuu wa Shirika la Utangazaji waTaifa (TBC),  Ayoub Riyoba, ambao ni washirika wa kampuni ya StarTimes katika urushaji wa matangazo ya dijitali nchini Tanzania amebainisha umuhimu wa filamu hizo hususani katika ukuzaji wa tamaduni baina ya nchi hizo mbili.

‘’Tanzania na China zina historia ndefu ya mahusiano tangu enzi hizo za waasisi wa mataifa haya. Nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Sisi kama chombo cha habari cha taifa tumekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa tunasaidia jitihada za 
serikali kukuza na kuutangaza utamaduni wetu hususani lugha ya Kiswahili. Kwa takribani miaka miwili iliyopita TBC imekuwa ikionyesha tamthiliya za Kichina zilizoingiziwa sauti kwa lugha ya Kiswahili. 

Kwa kufanya hivyo hivyo tamthiliya hizo zimeonyesha kupokewa vizuri na kupendwa sana na watanzania kwani wamekuwa wakielewa kinachoonekana.’’ alisema Riyoba

‘’Mbali na kukuza lugha yetu ya Kiswahili nchini na nje yanchi, hii pia ni fursa kwa tasnia yetu ya filamu kujifunza kutoka kwa wenzetu ambao wamepiga hatua zaidi. Tasnia yetu bado ni change na inahitaji mengi ya kujifunza ili kusonga mbele na kufikia pale walipo wenzetu na kuwa inazalisha kazi nyingi zaidi za sanaa. 

Ningependa kuchukua fursa hii kuipongeza na kuishukuru serikali ya China kwa jitihada zao wanazozionyesha katika kukuza filamu na lugha yetu ya Kiswahili. Na ningependa kuwaahidi kutokana na ushirikiano huu watazamaji wa TBC wataendelea kupata burudani ya tamthiliya 

na filamu nzuri zaidi ya zilizopita.’’  alisema Meneja Mkuuwa TBC katika maonyesho hayo Ubalozi wa China nchini Tanzania pia ulikabidhi mfano wa hati za makubaliano ya kwenda kufanya kazi jijini Beijing kwa washindi 10 waliopatikana katika shindano la vipaji vya sauti lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Washindi hao 10 waliopatikana ni; Hilda Malecela(DSM), Safiya Ahmed(ZNZ), Saiq Kututwa(ZNZ), Mathew Philip Mgeni(Arusha), Maisala Abdul(DSM), Rukia Hamdan(ZNZ), Richard Rusasa (DSM), Happiness Stanslaus - Nyamayao (DSM), Jamila Hassan(DSM) na Abraham Richard (DSM).

DORTMUND YAILAZIMISHA MADRID SARE YA BAO 2-2 LIGI YA MABINGWA ULAYA

$
0
0


Mechi ya Real Madrid dhidi ya wenyeji Borussia Dortmund imeisha kwa sare ya mabao 2-2.

Mechi hiyo ilikuwa kali baada ya wenyeji kulazimika kusawazisha mara mbili dhidi ya mabingwa hao wa Ulaya.


Cristiano Ronaldo ndiye alianza kufunga kwa upande wa Madrid, PierreAubameyang akasawazisha dakika ya 43. 

Kipindi cha pili Raphael Varane akaifungia Madrid tena dakika ya 68 lakini ‘jioni’ kabisa katika dakika ya 87, Andre Schuerrle akaifungia Dortmund bao la kusawazisha.

VIDEO: WEMA SEPETU APOSTIWA NA CHIBU DANGOTE AKIIMBA WIMBO 'SALOME'

SITALIA TENA- 03

$
0
0

NYEMO CHILONGANI
Kareem alimpenda Saida, hakutaka kuona akimpoteza msichana huyo ambaye kwake alikuwa kila kitu, kubwa zaidi ni kwamba alikuwa na mimba yake, hivyo kwa namna moja ama nyingine ilikuwa ni lazima amuokoe kutoka katika mkono wa kifo.
Alikuwa chumbani, hakutulia, alikuwa akizunguka huku na kule akifikiria ni kitu gani alitakiwa kufanya. Alihitaji msaada kipindi hicho, akaanza kuwafikiria marafiki zake ambao aliamini kwamba wangemsaidia kumnasua mpenzi wake katika kifo kilichokuwa kikimsogelea.
Alikuwa na marafiki wengi ambao aliamini kwamba wangeweza kumsaidia lakini wakati akiwafikiria hao wote, kichwani mwake alikuja mmoja ambaye alikuwa na uhakika asilimia mia moja kwamba angemsaidia kumtorosha msichana huyo nchini humo.
Tafiki yake huyo alikuwa Al Khalid, mtu ambaye alikua naye tangu akiwa mtoto mpaka kipindi hicho. Alichokifanya ni kuchukua simu yake na kuanza kulitafuta jina lake, alipolipata, hakutaka kuchelewa, harakaharaka akampigia simu.
Simu iliita pasipo kupokelewa, iliendelea kuita mpaka ilipokatika. Hakutaka kukoma, alichokifanya ni kupiga tena kwani mtu huyo alikuwa muhimu sana, alikuwa mtu pekee ambaye angeweza kumuokoa kutoka katika tatizo kubwa alilokuwa nalo kipindi hicho.
“Al Khalid! Can we meet somewhere! (Al Khalid! Tunaweza kuonana sehemu?) aliuliza Kareem mara baada ya simu kupokelewa, hata salamu hakutaka kutoa.
“What is it?” (kuna nini?)
“There is something I want you to help me,” (kuna jambo nataka unisaidie mara moja!) alijibu Kareem.
Hilo lilikuwa jambo dogo kwa Al Khalid, mara kwa mara walikuwa wakipigiana simu na Kareem kuomba kusaidiana katika mambo mengi ambayo kwa namna moja au nyingine yaliufanya urafiki wao kuendelea kukomaa zaidi.
Alimjua Kareem, alikuwa mtu wa kupenda kuyafanya mambo mengi kivyakevyake na kama kulikuwa na kitu alichokuwa akihitaji msaada, basi kitu hicho kilikuwa kikubwa ambacho kwa namna moja au nyingine alikwama kabisa kukifanya.
“Lipi? Baadaye nitakwenda Masjeed, unataka nikusaidie katika lipi?” aliuliza Al Khalid kwenye simu.
“Naomba tuonane kwanza.”
“Ila si unajua kwamba leo tunasubiri mwezi uandame ndiyo tuanze kufunga?”
“Najua! Ila naomba tuonane kwanza.”
Al Khalid na Kareem walikuwa marafiki wakubwa huku wote wakiwa watoto wa mabilionea wakubwa nchini Oman. Waliaminiana kwa kila kitu, walipendana ila tofauti yao ilikuwa moja tu.
Al Khalid alikuwa mtu wa dini haswa, alikuwa mtu wa swala tano, hakutaka kusikia adhana akiwa nje ya msikiti, katika maisha yake yote, alimpenda Mungu na hakutaka kufanya dhambi kabisa.
Kwa Kareem ilikuwa tofauti, hakuwa mtu wa swala, wakati mwingine aliombea misikiti yote ya Oman ibomolewe na kujengwe klabu kwa ajili ya kula bata usiku kama ilivyokuwa Dubai, Qatar na nchi nyingine zilizokuwa katika muunganiko wa Emirates.
Wawili hao wakaonana katika Mgahawa wa Ya Sadeek uliokuwa katikati ya Jiji la Muscat. Wakaonana hapo na kuanza kuzungumza mambo mengine kabisa. Kichwani mwa Kareem kulikuwa na mambo mengi, alikuwa akijiuliza kama lilikuwa jambo sahihi kumuomba msaada Al Khalid au amuache na kuomba msaada sehemu nyingine.
“Nina kitu nahitaji unisaidie,” alisema Kareem.
“Kuhusu nini rafiki?”
Kareem akamwambia ukweli Al Khalid kilichokuwa kimetokea, hakutaka kumficha kitu chochote kile, alikuwa rafiki yake wa dhati, akamuweka wazi kwamba alimpa mimba msichana ambaye alikuwa mfanyakazi wa ndani hivyo alihitaji msaada wa kuweza kumtorosha kutoka nchini humo.
Al Khalid alishangaa, hakuamini alichokisikia kutoka kwa Kareem. Alishangaa kwani lilikuwa jambo lisilo la kawaida kwa Mwarabu kufanya kitu kama hicho, kumpa mimba msichana na wakati alijua fika kwamba adhabu kubwa kwa msichana ilikuwa ni kunyongwa.
“Unanitania Kareem,” alisema Al Khalid.
“Ni kweli! Naomba unisaidie. Mpaka nimekwambia hili ni kwamba ninahitaji msaada wako,” alisema Kareem.
“Mmh! Hebu nikajifikirie, nitajua ni kipi tunachotakiwa kufanya,” alisema Al Khalid na kisha kuagana.
Moyo wa Kareem ukarudi kwenye tumaini kubwa, akaona kwamba hatimaye angeweza kusaidiwa na rafiki huyo na kumtorosha Saida nchini humo. Aliporudi nyumbani, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuonana na msichana huyo kisha kuzungumza naye.
Alimwambia mpango aliokuwa ameufanya wa kumtorosha nchini hapo pasipo mtu yeyote kugundua hilo. Saida akashusha pumzi, ni kweli alitamani kuondoka nchini humo lakini kitu kilichomtisha ni kwamba Kareem alilitoa jambo hilo nje ya nyumba yao, akahisi hapo ndipo kulipokuwa na tatizo.
“Kareem, utamuamini vipi rafiki yako?” aliuliza Saida.
“Usijali! Ni rafiki yangu sana, hawezi kufanya kitu chochote kibaya. Naomba umuamini!” alisema Kareem huku akimwangalia Saida.
Walibaki sebuleni wakizungumza, walionekana kama marafiki wa kawaida na hakukuwa na kitu chochote kilichokuwa kikiendelea. Suala hilo bado liliendelea kuwa siri, hakukuwa na mtu yeyote ndani ya nyumba aliyelifahamu zaidi ya wao wawili.
Ilipofika saa moja usiku, wazazi wake Kareem wakarudi nyumbani. Kila mmoja alibaki akisikilizia kuona kama mwezi uliandama au la! Kwa siku hiyo, redio zote nchini Oman zikiwemo TunIn Fm, Hi Fm na nyingine zilitangaza kwamba siku hiyo mwezi haukuwa umeandama hivyo ilikuwa ni lazima siku inayofuata kula ila siku nyingine inayofuata ni kufunga.
“Kesho itatubidi twende kufanya manunuzi sokoni kwa ajili ya futari ya keshokutwa,” alisema mama yake.
“Hakuna tatizo!” alijibu Kareem.
Wakatulia sebuleni lakini muda mwingi Kareem na Saida walikuwa wakiangaliana kwa macho ya kimahaba. Ilipofika saa tatu usiku, wakasikia geti kubwa likigongwa. Kupitia kamera za CCTV zilizofungwa kila kona nyumbani humo, wakaliona gari la polisi likiwa limesimama nje ya geti.
Kila mmoja akashtuka, halikuwa jambo la kawaida kwa polisi kufika nyumbani hapo, tena kwa usiku kama huo. Wakamwambia mlinzi afungue geti kwa rimoti maalumu, geti likafunguliwa na polisi wawili waliokuwa na silaha kuingia ndani.
Wakamuulizia mzee Abdoulaziz, wakaambiwa yupo, wakaufuata mlango na kuingia na kuanza kugonga. Kareem akahisi kitu, harakaharaka akasimama kutoka kitini, akamshtua Saida naye asimame, akafanya hivyo na kuanza kuelekea chumbani.
“Kuna nini?” aliuliza Saida.
“Nina hofu na hawa polisi. Mungu wangu! Al Khalid atakuwa amewaambia polisi,” alisema Kareem huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Unasemaje?”
“Nahisi itakuwa hivyo!”
Wakati wakizungumza hivyo chumbani. Mara mlango wa chumba hicho ukaanza kugongwa. Kareem akajiuliza kama alitakiwa kuufungua au la. Wakati huo, Saida alikuwa akitetemeka mno chumbani humo, alitamani kufumba macho na kufumbua awepo nchini Tanzania.
Wakati akijiuliza, akashtukia mlango ukipigwa teke, polisi wawili wakaingia chumbani humo. Hawakutaka kumkamata Kareem, walichokifanya ni kumchukua Saida.
“Kuna nini?” aliuliza Kareem huku akijaribu kuwazuia wasimchukue mpenzi wake.
“Taarifa zinasema ana mimba.”
“Hapana! Hana mimba!”
“Unabishana na wapelelezi wetu. Tumekuja na daktari kwa ajili ya vipimo,” alisema polisi mmoja.
Wakatoka ndani ya chumba hicho huku wakiwa wamemfunga pingu Saida. Kareem alibaki akitetemeka. Saida alikuwa akilia kwa sauti, hakutaka kutoka ndani ya nyumba hiyo, hakutaka kumuacha mpenzi wake lakini kutokana na kutolewa kinguvu, hakuwa na jinsi.
Wakamchukua na kumuingiza ndani ya gari, alikuwa akilia mno, polisi hao hawakutaka kujali, kwao, sheria ya nchi ilipewa kipaumbele kuliko kitu chochote kile. Gari likawashwa na kuondoka mahali hapo, lilipoelekea, lilikwenda katika kituo kikubwa cha polisi hapo Muscat kwa ajili ya kupelekwa mahakamani kesho asubuhi na mchana adhabu ya kupigwa mawe itolewe na kufanyiwa kazi hata kabla mfungo wa Ramadhani haujaanza.
****
Al Khalid aliondoka katika Mgahawa wa Ya Sadeek. Moyo wake ulimuuma mno mara baada ya kuambiwa na Kareem kilichokuwa kimetokea. Moyoni mwake, kufuata misingi ya dini kilikuwa kitu cha kwanza kabisa, alikipa kipaumbele na ndicho kitu ambacho mara kwa mara aliwaambia wenzake kwamba walitakiwa kukifuata.
Kitendo cha kuambiwa hivyo na Kareem kwamba alikuwa na msichana aliyempa ujauzito, moyo wake ulimuuma mno, aliona katika maono yake kwamba malaika wa shetani wakimfuata, wakamshika na kumuingiza katika shimo la moto kulipokuwa na mateso makubwa kutokana na kushiriki kitu ambacho aliamini ni dhambi kubwa mbele za Mungu.
Hakutaka kukubali, hakutaka kushiriki dhambi hiyo kubwa. Kwake, kudanganya na kusengenya zilionekana kuwa dhambi ndogo ambazo zisingekuingiza motoni kuliko kumpa mimba mwanamke hata kabla ya kuolewa.
Moyo wake ulimfurukuta, akashindwa kula, akashindwa kupumzika, muda wote alikuwa akimfikiria Kareem. Hakutaka kuona akiendelea kushiriki dhambi hiyo, alichokifanya, tena kwa kusukumwa na sauti ambayo aliamini ni ya Mungu, akaenda kituo cha polisi na kutoa taarifa juu ya kilichokuwa kimetokea.
“Una uhakika?” aliuliza polisi huku akimwangalia Al Khalid.
“Ndiyo! Nina uhakika! Nimeamua kuja kuiosha mikono yangu kwa maji masafi, sitaki kushiriki kikombe hiki kilichojaa dhambi,” alisema Al Khalid huku akionekana kumaanisha alichokizungumza.
“Safi sana...ukiwa unafanya hivi, unapata swawabu nyingi kwa Mungu! Tutakwenda huko na atakulinda katika maisha yako yote,” alisema polisi mmoja.
Moyo wake ukawa na amani, hakujisikia mzigo wowote moyoni mwake, hakujihukumu kwani kile alichokifanya aliona kilikuwa kizuri na halikuwa jambo baya. Kareem alikuwa mkosaji kama wakosaji wengine hivyo serikali ilitakiwa kuchukua sheria mkononi kwa kwenda kumkamata msichana huyo, kwa mwanaume, hakutakiwa kukamatwa kwani hakukuwa na uhakika kama kweli mimba ile ilikuwa yake au ya mtu mwingine. Ila kwa mwanamke, hakukuwa na utetezi wowote ule.
Polisi wakafika huko na kumkamata Saida na kuondoka naye huku wakimuacha Kareem akiwa na mawazo tele. Kilichokuja moyoni mwake, ilikuwa ni lazima kumuokoa Saida, hakutaka kuona msichana huyo akifa na wakati alikuwa akimpenda na tumboni alikuwa na mtoto wake.
Je, nini kitaendelea?
Je, Saida atauawa kwa kupigwa mawe?
Je ni nani alisema hatolia tena?
Kwa nini aseme hivyo?
Tukutane

Mahakama Kuu Yaikana Kampuni Iliyomtoa Mbowe

$
0
0
Mahakama Kuu imekana kuitambua kampuni ya Fosters Auctioneers and General Traders iliyohusika kuondoa vitu vya kampuni za Freeman Mbowe kwenye jengo la Shirika la Taifa la Nyumba (NHC).

Hayo yalibainishwa jana na kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema, Peter Kibatala wakati wa usikilizwaji wa maombi yaliyofunguliwa na mlalamikaji huyo kupitia kampuni ya Mbowe Hotels Ltd dhidi ya NHC na kampuni hiyo ya udalali.

Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo jana, pamoja na mambo mengine Mbowe aliiomba Mahakama iliamuru NHC na kampuni hiyo wamrejeshe katika jengo hilo pamoja na vifaa na mali zake zinazoshikiliwa na kampuni hiyo.

Wakili Kibatala aliieleza Mahakama kuwa mteja wake aliondolewa katika jengo hilo kinyume na sheria.

Alidai dalali aliyetumiwa na NHC kuziondoa kampuni za Mbowe katika jengo hilo hajasajiliwa na Mahakama kwa kuwa walimwandikia Msajili wa Mahakama barua kujua kama anatambulika, lakini alijibu kuwa haimtambui.

Kutokana na majibu ya msajilihuyo kupitia barua yake ambayo wameiwasilisha mahakamani kama kielelezo, Kibatala alidai sheria na mchakato mzima uliotumika vilikuwa ni batili.

Mawakili wa NHC, Ipilinga Panya na Aloyce Sekule walidai shirika hilo kabla ya kumtimua Mbowe lilimwandikia notisi ya siku 30 iliyokwisha kisha akaongezewa siku 30 zingine kama sheria inavyotaka ambazo ziliisha na kumpa tena siku 14, lakini hakulipa deni.

Wakili wa kampuni ya Foster Auctioneers and General Traders, Aliko Mwamanenge alidai madai ya kuwa mteja wake ni dalali wa Baraza la Usuluhishi na kwamba anayesajiliwa kama dalali ni mtu binafsi na siyo kampuni, hayana ukweli kwani upande wa mlalamikaji ulipoandika barua kuulizia uhalali wake ulipaswa kuuliza jina la mmiliki kampuni hiyo.

Hata hivyo, wakili wa mlalamikaji Kibatala alidai notisi zinazodaiwa kuandikwa na NHC zilipelekwa mahali pasipohusika kwa kampuni ya Free Media badala ya Mbowe Hotels ambayo ina mkataba na NHC. Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Sivangilwa Mwangesi anayesikiliza kesi hiyo aliiahirisha hadi Oktoba 18, mwaka huu atakapotoa uamuzi wa maombi hayo ya mlalamikaji.

Septemba Mosi, wafanyakazi wa kampuni ya udalali ya Foster Auctioneers and General Traders walifika kwenye ofisi za kampuni ya Free Media na kuondoka vifaa mbalimbali vya kazi, zikiwamo kompyuta na viti kwa madai kwamba mmiliki wake, Mbowe anadaiwa na NHC fedha nyingi za kodi ya pango.

Chanzo: Mwananchi

Jokate Asaka Msusi Bora Mkoa Wa Dar es salaam

$
0
0






Mwanamitindo, Jokate Mwigelo kupitia kampuni yake ya Kidoti ameandaa shindano la kusaka msusi bora alilolipa jina la Msusi Wao, lengo ni kuwaamsha wasusi wasiokuwa na ofisi na kuwafanya wakitambue kipaji chao.

Akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Escape One,  Jokate jana alisema kuwa alikaa na kuona kuwa kundi la wasusi ni watu muhimu  katika masuala ya urembo hivyo akaamua kuandaa shindano ambalo litawapa fursa ya kujiendeleza zaidi na kuitambua nafasi yao.

“Unajua siku moja nilitafuta msusi nikaletewa nyumbani dada mmoja ambaye hana ofisi  na ambaye alinisuka vizuri lakini nilipomhoji ana kazi gani inayompa kipato akasema hakuwa na kazi, ndipo niliona ipo haja ya kuwakuza wasusi wetu ikiwa sehemu ya kutoa ajira na kuwafanya wajitambue,” alisema Jokate.

Jokate alimtaja mshindi wa kwanza kuwa atapata nywele za Kidoti zenye gharama ya shilingi milioni 1.5 na pesa shilingi laki tatu na draya, wa pili atapata nywele za gharama ya shilingi milioni 1.2 na laki mbili na Draya na wa tatu atapata milioni moja na laki mbili na nusu pamoja na draya.

Washindi watatafutwa kila wilaya  ambapo kutakuwa na fomu za kujaza ili kuwatambua vyema na wanaohusika ni wale tu wasiokuwa na ofisi.

Dk.Kigwangalla afanya ziara Hospitali za Wilaya ya Mlele na Mpanda Mkoani Katavi

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mlele na kutembelea Hospitali ya Mlele ya Wilaya hiyo pamoja na Hospitali ya Mpanda iliyopo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi huku akitoa maagizo mbalimbali ya kiutendaji.

Katika ziara yake katika Hospitali ya Mlele, Dk.Kigwangalla amewaagiza viongozi wa Serikali wa Wilaya na ule wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanakamilisha mambo muhimu ikiwemo ujenzi wa chumba cha upasuaji, jengo la kuhifadhia mahiti na vitu vingine huku akitaka ndani ya miezi mitatu view vimekamilika.

Akiwa katika Hospitali hiyo ya Mlele, Dk.Kigwangalla ameweza kutembelea sehemu mbalimbali za hospitali pamoja na kukagua ujenzi wa majengo ya Chumba cha upasuaji, chumba cha kuhifadhia maiti na majengo mengine ambapo amemtaka Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanafanya juhudi wanakamilisha kwa wakati majengo hayo ili wananchi wapate huduma bora.

Kwa upande wa ziara yake hiyo katika Wilaya ya Tanganyika yaliyopo makao makuu ya Mkoa wa Katavi, Dk. Kigwangalla ameweza kutembelea Hospitali ya Mpanda ambayo kwa sasa inahudumia kama Hospitali ya Mkoa ambapo napo ameagiza kufanyiwa marekebisho mbalimbali ikiwemo kuzingatia masuala usafi.

Aidha, ametoa maagizo kuhakikisha wanafunga mfumo wa malipo wa kisasa katika vyanzo vyote vya mapato ili kukusanya pesa nyingi zaidi zitakazoweza kuendesha huduma za Afya ndani ya Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Chifu Kayamba wa Pili wa Kabila la Wakonongo. Wakati wa kupokelewa alipowasili ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Mlele,Mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya viongozi na watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Mkoani Katavi.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Bi.Rachel Kasanda akisoma taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati).
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na watendaji wa Wilaya ya Mlele.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na madaktari wa hospitali ya Mlele.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya vifaa katika chumba cha Maabara ya hospitali ya Mlele.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitembelea katika viunga vya hospitali ya Mlele.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua jengo la chumba cha Upasuaji wa hospitali ya Mlele.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua jengo linalojengwa la chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Mlele
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na watumishi wa Hositali ya Mpanda.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua stoo ya dawa ya hospitali ya Mpanda.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo katika chumba cha Maabara ya Hospitali ya Mpanda.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wananchi (Hawapo pichani) wakati wa ziara yake hiyo katika Hospitali ya Mpanda.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa uongozi wa Hospitali ya Mpanda juu ya kufanyia marekebisho mapungufu yaliyobainika.

Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi azindua maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani Mkoani Tanga

$
0
0


Mgeni Rasmi kwenye Uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande kushoto ambaye alimuwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Makame Mbawara katika maashimidho hayo akiingia kwenye viwanja vya Tangamano kunakofanyika maadhimisho hayo katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra,Gilliard Ngewe kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(Ras)Mhandisi Zena Saidi.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TPA,Focus Mauki kushoto akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande aliyesimama katikati wakati alipolitembelea Banda la Mamlaka ya Bandari (TPA) kunakofanyika maadhimisho ya siku ya Bahari Dunia wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra,Gilliard Ngewe.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),Joseph Msaki kushoto akimueleza jambo Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande wakati alipotembelea Banda lao leo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),Joseph Msaki aksisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande wakati alipotembelea Banda lao leo wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika kushoto akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande wakati alipotembelea Banda lao leo.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika kushoto akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande ambaye hayupo pichani wakati alipotembelea Banda lao leo.
Tug Master Idara ya Marine Bandari ya Tanga,Mkanga Mbwana akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande wakati alipotembelea Banda lao leo katikati ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TPA,Focus Mauki.
Afisa Zimamoto na Usalama wa Bandari ya Tanga (TPA),Athumani Mkubwa akimueleza jambo Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande wakati alipotembelea Banda lao leo katikati ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TPA,Focus Mauki.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Quality Body Product LTD ambayo inajihusisha na Vifaa vya Uvuvi na Malighafi za Vipodozi,Hussein Walt akimuonyesha mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande namna wanayotengeneza bidhaa hizo wakati alipo tembelea Banda lao leo.
Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra) Mussa Mandia kushoto akisoma vipeperusi kuhusiana na mfuko wa Pensheni wa PSPF mara baada ya kulitembelea Banda lao lililopo kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga panako fanyika maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani katikati ni Afisa wa Mfuko huo,Michael Kazimili na kulia aliyekaa ni Afisa Mwandamizi wa mfuko huo Mkoa wa Tanga,Happines Mbuna.
Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra) Mussa Mandia kushoto akisoma vipeperusi kuhusiana na mfuko wa Pensheni wa PSPF mara baada ya kulitembelea Banda lao lililopo kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga panako fanyika maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani katikati ni Afisa wa Mfuko huo,Michael Kazimili na kulia aliyekaa ni Afisa Mwandamizi wa Mkoa wa Tanga,Happines Mbuna.
Afisa Mkaguzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Vyombo vya Majini kutoka Sumatra ,Mhandisi Christopher Mlelwa akimsikiliza mkazi wa Jiji la Tanga ambaye aliitaja kupata ufafanuzi kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusiana na mamlaka hiyo.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Tanga wakifuatilia uzinduzi wa Maonyesho ya Bahari Dunia leo kwenye viwanja vya Tangamano

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA RASMI NDEGE MBILI MPYA ZILIZONUNULIWA NA SERIKALI KWA AJILI YA ATCL JIJINI DAR LEO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles baada ya kukata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiingia kwenye ndege mojawapo baada ya kukata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoka kwenye ndege mojawapo na kuelekea ingine baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza mmoja wa wafanyakazi kwenye ndege mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe akishuka kwenye ndege mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe Isaya Mwita akishuka kwenye ndege mojawapo baada ya Rais Magufuli kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe Isaya Mwita na Meya wa Halmashuri ya Manisapaa ya Temeke Mhe Abdallah Chaurmebo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Sophia Mjema wakijiandaa kupiga picha ya kumbukumbu mara baada ya Rais Magufuli kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wengine waandamizi katika picha ya kumbukumbu na watumishi na viongozi wa ATCL mara baada ya Rais Magufuli kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wengine waandamizi katika picha ya kumbukumbu na Brass band ya Polisi mara baada ya Rais Magufuli kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Mama Janeth Magufuli wakiagana na wafanyakazi wa ATCL baada ya uzinduzi rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016. PICHA NA IKULU

TIKETI ZA YANGA VS SIMBA JUMAMOSI, MFUMO MZIMA WA UNUNUZI NA UNUNUE WAPI, SOMA HAPA..

Wastara Apata Ubalozi wa Simu za KZG, Atalipwa shilingi Milioni Mia Nne Kwa Mwaka

$
0
0




  Wastara (katikati) akisaini mkataba huo.
Meza kuu wakionyesha aina za simu hizo.


Staa wa filamu Bongo, Wastara Juma amepata shavu la kuwa balozi wa Kampuni ya simu ya mkononi ya KZG ambapo leo amekabidhiwa na kusainishwa mkataba rasmi.
Akizungumza katika tukio la kusaini makubaliano ya kuwa balozi wa kampuni hiyo  lililofanyika katika ukumbi wa De Mag Hotel iliyopo Mwananyamala, Dar,  Wastara alisema amefurahi sana kupata shavu hilo kwani kujituma kwake katika biashara ndiko kulikompatia bahati hiyo.
Aliendelea kusema kwamba atahakikisha anafanya vizuri katika ubalozi huo ambao kwa mwaka unampatia shilingi milioni mia nne kutegemea na jinsi kampuni hiyo inavyouza bidhaa zake hizo kwani imempa heshima kubwa ambayo hakuitarajia.
“Nina furaha sana kuwa balozi wa KZG, hii imetokana na kujituma kwangu kwani ninafanya biashara nami ni mwanamke ambaye ninajitambua na najua ninachokifanya, naishukuru kampuni hii kwa kuniona hivyo, naomba mashabiki zangu waniunge mkono,” alisema Wastara.
Katika tukio hilo pia kampuni hiyo ilimzawadia keki Wastara ikiwa ni zawadi ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake kwani ilikuwa jana, hivyo kutokana na nafasi hiyo wakaona ni vyema wampe zawadi hiyo iliyokuwa imechorwa aina mojawapo ya simu za KZG.

Rais Magufuli aumizwa na uzushi wa kwenye mitandao ‘natamani siku moja malaika wazime mitandao’

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amechukizwa na jinsi watu wanavyozusha mambo ya uongo katika mitandao ya kijamii.

Akiongea Jumatano hii wakati wa uzindizi wa ndege mpya mbili za ATCL aina ya Bombardier zilizonunuliwa kwa fedha taslimu za kodi za wananchi kutoka Canada, Rais Magufuli ameshangaa kuona watu katika mitandao ya kijamii wakiandika gharama za manunuzi ya ndege hizo wakati hawajui chochote.
“Mtu mwingine anasema ndege hizo tumezinunua kila ndege dola milioni 61 wakati mimi najua ndege moja haikufika hata nusu ya hiyo bei, na anapost pale anaandika uongo, halafu hata akishajua ukweli wake baadaye wala hatubu. Nilikuwa natamani siku moja malaika washuke waizime hii mitandao yote ili baada ya mwaka mzima itakapokuja kufunguka wakute sisi tumeshatengeza Tanzania yetu mpya, wanapost vitu vingine vya ovyo, wanasema no research no right to speak,” alisema Magufuli.
Pia katika uzinduzi huo, Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuwafukuza kazi mara moja watendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania(ATCL) watakaokwamisha ufanisi wa huduma za kampuni hiyo.

Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Chuo Kikuu Ruaha University- RUCU 2016/2017

Magazeti ya Tanzania Leo Alhamisi ya Septemba 29, 2016

Hainaga Ushemeji Afande Laivu na Mke Wa Mdogo Wake Gesti

$
0
0
DAR ES SALAAM: Wimbo wa msanii wa Singeli, Man Fongo wa Hainaga Ushemeji ndiyo habari ya mjini kwa sasa ambapo mashairi yake hivi karibuni yalitimia kufuatia askari wa Gereza la Ukonga jijini hapa, Kassim Juma kudaiwa kunaswa chumbani gesti akiwa na mke wa mdogo wake aliyejitambulisha kwa jina la Haroub, aitwaye Rukia Clemens, Amani lilidokezwa na kuibukia kwenye tukio. Ishu hiyo yenye viashiria vya kusambaratisha ukoo, ilijiri Septemba 26, mwaka huu kwa maana ya Jumatatu iliyopita, kwenye chumba namba nne cha gesti iliyopo Ukonga ya Majumba 6, Dar. Afande Kassim alikumbwa na kasheshe hilo akiwa tayari chumbani na shemejiye huyo bila kujua kuwa, alikuwa ndani ya bomba ambalo limezibwa kotekote hivyo haikuwa rahisi kutoka.

AMANI LILIPATAJE ISHU?
 Ni wakati gazeti hili likikatiza kuelekea kwenye mihangaiko ya kila siku, ndipo lilipomwona Haroub akiwa ameongozana na askari wawili wa usalama barabarani na kutonywa kuwa, wa
nakwenda kumnasa afande huyo akiwa na shemeji yake. Gazeti hili liliunga msafara huo mpaka kwenye gesti hiyo ili kushuhudia fumanizi hilo likiwa limesimamiwa na maafande hao, huku mume wa Rukia akiwa katika hali ya jazba kali.

AFANDE ALIVYONASWA
Baada ya kufika, mtu mmoja aligonga mlango wa chumba namba nne ambapo mlalamikiwa huyo alipouliza ni nani, alijibiwa kuwa ni mhudumu amepeleka sabuni ya kuogea. Mlalamikiwa huyo alifungua mlango kidogo na kutoa mkono ili kuipokea sabuni hiyo na ndipo waliokuwa nje waliposukuma mlango na kuzama ndani ya
chumba, sambamba na mpigapicha wetu.

AFANDE APIGWA MASWALI
Baada ya kuwa chini ya ulinzi, afande huyo aliulizwa maswali kadhaa kama ifuatavyo: Trafiki: “Habari yako?” Afande Kassim: “Salama afande.” Trafiki: “Unaitwa nani?” Afande Kassim: “Naitwa Kassim Juma.” Trafiki: “Huyo uliyenaye ni nani yako?” Afande Kassim: “Shemeji yangu.” Trafiki: “Na huyu hapa unamjua?” Afande Kassim: “Ndiyo namjua, huyo ni mdogo wangu ambaye huyu ni mkewe.”

 Trafiki: “Sasa mnataka kufanya nini hapa kitandani?” Afande Kassim: “Jamani naomba mnisamehe, siyo amri yangu ni ibilisi tu alinipitia halafu mimi ni poti mwenzenu.” Mlalamikiwa huyo alijitambulisha kuwa, yupo Magereza Ukonga na kusema ana kitambulisho. Katika mbilinge hilo, mume wa Rukia alitaka kwenda mbele zaidi na kumuangushia kipigo kaka yake lakini alidhibitiwa na trafiki hao.

ALICHOAMUA MDOGO MTU Baada ya zoezi hilo kukamilika, Haroub alisema hana sababu ya kumpeleka kaka yake polisi ila anachoomba apewe mkewe arudi naye nyumbani
kwa vile alishamjua mbaya wake ni nani!

HUU NDIYO UDUGU WAO Akizungumza na gazeti hili kuelekeza mazingira ya fumanizi hilo la kaka yake, Haroub alisema: ”Huyu Kassim ni kaka yangu kabisa, mtoto wa mama yangu mdogo. Alitoka kijijini kule Mafia baada ya kumaliza kidato cha nne na kuja hapa Dar ambapo alifikia nyumbani kwetu, Tandika. “Mama yangu mzazi ambaye ni mama yake mkubwa ndiye aliyemfanyia mpango wa kujiunga na mafunzo ya JKT (Jeshi la Kujenga Taifa). Na mimi ndiye niliyempeleka mpaka kwenye vipimo pale Ruvu JKT. “Baada ya kumaliza mafunzo ya JKT  alipata nafasi ya ajira katika Jeshi la Magereza anapofanya sasa hapo Ukonga ambapo anaishi na mkewe. “Kinachoniuma zaidi mimi ndiye niliyemuonesha maeneo mbalimbali hapa Dar, ikiwemo Uwanja wa Taifa, Posta, Feri, Ikulu na maeneo mengine.
Nakumbuka alinishukuru sana. Lakini leo hii ananigeuka? Yaani siamini.”

KUMBE ULIKUWA MTEGO “Iko hivi, siku moja mke wangu Rukia aliniambia kuwa shemeji yake anamtumia meseji ambazo zinavuka mipaka ya ushemeji. “Ingawa mke wangu alimtilia shaka lakini aliendelea kuchati na shemeji yake akimrudishia majibu yaliyopoa lakini kaka alizidi kumtumia vijimeseji vyake. “Siku moja, kaka alimpasulia wazi, mke wangu hakuamini alichoambiwa hivyo alinieleza mimi mumewe na kunionesha meseji zote. Ili kunithibitishia, mke wangu alimpigia simu bro ili nisikie sauti yake. Kweli nilimsikia vizuri sana. Na ndipo tukaandaa mtego wa kumnasa gesti.”

KWA NINI TRAFIKI? Haroub alisema kuwa, baada ya kaka yake na shemejiye kuingia kwenye
gesti hiyo, aliamua kuwafuata trafiki hao waliokuwa eneo la kuongozea magari eneo la Ukonga na kuwaomba kwenda kumsaidia. “Walisema wao hawahusiki na mambo ya fumanizi, lakini nikawaambia kwamba kama hawataki, mimi nakwenda kumfumania mwenyewe, kitakachotokea, kama ni kuua, kumwaga damu au kufanyaje, wao watawajibika kwa sababu nimewaambia wakakataa kunipa msaada, ndipo wakakubali kuongozana na mimi.”

FAMILIA YAPIGWA BUTWAA, HAIAMINI “Kusema ukweli, kila ndugu niliyemwambia hajaamini. Mama haamini pia, kila mtu amepigwa na butwaa. Wanauliza kweli Kassim anaweza kufanya hivi kwa shemeji yake? Awali walijua mke wangu anamsingizia,” alisema Haroub akiwa anaondoka na mkewe kuelekea nyumbani kwake huku akilia na mkewe akimbembeleza.

Lulu Diva amdhalilisha Tiffah wa Diamond

$
0
0

 Video queen matata Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’.

Video queen matata Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ anadaiwa kumdhalilisha mtoto wa Mbongo Fleva anayefanya vizuri kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Latifa ‘Tiffah’ kwa kumuita mbwa wake jina Shikiki, ambalo pia ni jina jingine la utani la mtoto huyo. 

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, mrembo huyo amemuita mbwa wake huyo jina hilo, kitu ambacho kimetafsiriwa na wengi kama ni kumdhalilisha mtoto huyo wa staa mkubwa Bongo. 
 

“Jamani Diva anatafuta matatizo makubwa na D i a m o n d , kwanini kampa mbwa wake jina kama hilo ambalo pia huwa linatumiwa na Tiffah? Ana hatari sana,” kilisema chanzo chetu. 
 Mtoto wa Mbongo Fleva anayefanya vizuri kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Latifa ‘Tiffah’.

Gazeti hili lilipomtafuta Lulu na kumuuliza kuhusu ishu hiyo, alisema ni kweli mbwa wake anaitwa Shikiki lakini hakuwa akijua kwamba mtoto wa Diamond, jina lake lingine ni hilo. 

“Jamani mimi sikuwa najua kabisa kama Tiffah, jina lake lingine ni hilo, mimi nilimpa tu kama watu w e n g i n e wanavyowapa m a j i n a mbwa wao,” alisema Diva.
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live