Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

Azam: Ndanda walipata bahati tu

$
0
0
MARA baada ya Azam kupokea kichapo cha pili katika ligi mbele ya Ndanda ya Mtwara, uongozi wa timu hiyo umeibuka na kudai kwamba hakuna wa kumlaumu kutokana na
kichapo hicho kwa sababu wapinzani wao waliwazidi bahati tu ambayo ndiyo iliwasaidia kupata ushindi huo.
 
Azam chini ya kocha wake, Mhispania, Zeben Hernandez, juzi Jumamosi ilijikuta ikiendeleza rekodi yake ya kupoteza katika Uwanja wa Nang’wanda Sijaona, Mtwara
mara baada ya kuchapwa mabao 2-1 mbele ya wenyeji wao Ndanda ya mkoani humo.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Msemaji wa Azam, Jaffar Idd, alisema kwamba licha ya wao kupambana kwa ajili ya kusaka ushindi kwenye pambano hilo, bahati haikuwa ya kwao kutokana
na nafasi nyingi za mabao walizozitengeneza kuishia mikono mwa kipa wa Ndanda na nyingine kuokolewa na mabeki.

 “Kiukweli hatuna wa kumlaumu kutokana na kipigo hiki cha Ndanda kwa sababu sisi tulikuwa bora zaidi ya wapinzani wetu ambao muda mwingi tulikuwa tunawashambulia lakini ndiyo hivyo, mwisho wao wameibuka vinara kwa kutufunga kibahati kwa sababu tuliwazidi kwa kila
kitu. “Bado hatuna wasiwasi wowote juu ya kufanya vizuri licha ya kwamba tumepoteza mechi mbili mpaka sasa kwa sababu kuna mechi nyingi zimebaki na kocha Zeben ameshayachukua mambo yote ambayo yamesababisha sisi kupoteza mechi hizi na ametuhakikishia kwamba tutaibuka washindi katika mchezo ujao,” alisema Idd

Omog: Kwa beki hii Tambwe, Ngoma watapita...

$
0
0
 HIVI karibuni Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, alikuwa na kazi kubwa ya kuwafua mabeki wake hususan wale wa kati ili waweze kuwa fiti tayari kwa kukabiliana na washambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma. Washambuliaji hao walikuwa wakimkosesha usingizi kocha huyo kila alipokuwa akiifikiria kazi yao wanapokuwa uwanjani wakifosi kupata ushindi.

Hali hiyo lilimfanya achukue jukumu la kuwafua vilivyo mabeki wake ili wawe tayari kukabiliana na washambuliaji hao Jumamosi hii, jambo ambalo amedai kuwa limefanikiwa kwa kiwango cha juu. 

Akizungumza Omog alisema kuwa hana tena hofu yoyote kuhusiana na washambuliaji hao baada ya kuridhishwa na uwezo mkubwa wa mabeki wake ambao wamekuwa wakiuonyesha mazoezini tangu alipoanza kuwafua kwa ajili ya mchezo huo lakini pia mechi nyingine za ligi kuu. “Sina hofu yoyote tena juuya washambuliaji hao kwani hivi sasa nawaamini vilivyo mabeki wangu kutokana na uwezo wao mkubwa ambao wamekuwa wakiuonyesha mazoezini. 


“Wameiva vilivyo na wapo vizuri na wapo tayari kukabiliana na washambuliaji hao kwa mpira wa aina yoyote ile, iwe kwa mipira ya juu au chini. Hakuna njia ya kupita kirahisi,” alisema Omog na kuongeza kuwa katika harakati zake hizo za kuwafua mabeki wake hao, amevutiwa zaidi na kiwango cha Mganda, Juuko Murshid, hivyo anaweza akamtumia katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi na mashabiki wa soka hapa nchini. 

Endapo Juuko atafanikiwa kuwa katika kikosi cha kwanza cha Simba siku hiyo, basi itakuwa ni mara yake ya pili tangu ligi hiyo ilipoanza kutimua vumbi msimu huu ambapo mara yake ya kwanza kuanza kuwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo ilikuwa juzi Jumamosi dhidi ya Majimaji FC. Mabeki ambao mara kwa mara wamekuwa wakiongoza Simba msimu huu ni Mzimbabwe mwenye asili ya Tanzania, Method Mwanjale na Novaty Lufunga.

Aibu! Stand yaimaliza Yanga SC

$
0
0
HATIMAYE mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, wamesimamishwa. Yanga ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa jana dhidi ya Stand United, walijikuta wakifungwa mchezo wao wa kwanza baada ya Stand kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga 
 
Huu ni mchezo wa kwanza Yanga wanapoteza kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kucheza michezo mitano, ukiwa ni wa mwisho kabla ya kuvaana na watani wao wa jadi Simba, Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa. Haikuwa kazi ndogo kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo, kwa kuwa Yanga walipanga kikosi imara na kucheza kipindi cha kwanza vizuri, lakini makosa ya mabeki wake Vincent Bossou, na Haji Mwinyi, yalitosha kuwapa Stand bao safi katika dakika ya 58. 

Mshambuliaji wa Stand ambayo haijafungwa hata mchezo mmoja, Pastory Athanas, alitumia uzembe wa mabeki hao alipita katikati yao na kuifungia timu yake bao safi kwa shuti kali na kuifungia timu yake bao safi kwa shuti kali. Ushindi huu umewafanya Stand ambao wanafundishwa na kocha Mfaransa, Patrick Liewig, kukwea hadi nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, wakiwa na pointi 12 ambazo ni nne nyuma ya vinara Simba. Hata hivyo, Stand walionekana kuwa imara sana kwenye nafasi ya kiungo na ulinzi ambapo walitawala kwa sehemu kubwa sana huku wakicheza kwa nidhamu ya hali ya juu. Hii ina maana kuwa Yanga watakuwa wamepoteza mchezo mmoja mkoani, wametoka sare mmoja na kufungwa mmoja. Katika mchezo dhidi ya Ndanda

Simba SC yakwepa hujuma za Yanga SC

$
0
0
UONGOZI wa Simba upo makini kuelekea mchezo wao ujao dhidi ya Yanga baada ya kuwadhibiti wachezaji wao vilivyo ili wasiingie kwenye mtego wa kuhujumiwa na wapinzani wao hao. Simba wamekuwa na kawaida ya kila wakimaliza mechi kuwaruhusu wachezaji wao kwenda kusalimia familia zao, lakini juzi Jumamosi haikuwa hivyo, kwani baada ya mchezo wao dhidi ya Majimaji, moja kwa moja wakaenda kambini Ndege Beach. Simba ambayo juzi Jumamosi iliichapa Majimaji mabao 4-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara
 

uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar, Jumamosi hii itacheza dhidi ya Yanga uwanjani hapo. Katika maandalizi yao kuelekea mchezo huo, jana Jumapili kikosi hicho kiliondoka kwa basi kuelekea mkoani Morogoro huku kikitarajiwa kurudi siku moja kabla ya kuwavaa Yanga. Mmoja wa watu wa benchi la ufundi la timu hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, ameliambia gazeti hili kuwa, baada ya mchezo wao wa juzi, walijifungia kwenye vyumba vya uwanja huo na kuwa na kikao kizito na viongozi wao ambacho kilidumu kwa takriban nusu saa.
“Jana (juzi) tulikuwa na kikao na viongozi ambapo leo (jana) tumesafiri kwenda Morogoro kuweka kambi ambapo tunatarajia kurudi siku moja kabla ya mchezo wetu huo. “Hii ni vita na lazima tujipange kwa mashambulizi, ndiyo maana utaona wachezaji hawakupewa hata ruhusa za kwenda kuaga familia zao kwa kuhofia kuhujumiwa kwani unajua mchezaji anaweza akapewa nafasi hiyo, wapinzani wetu nao wakautumia mwanya huo kutuhujumu. Hatutaki itokee hivyo na mpaka sasa vita hiyo tumeishinda,” alisema mtu huyo.

Mshindi Chemsha Bongo Na Amani Apewa Zawadi Yake

$
0
0


Mshindi wa tatu wa Chemsha Bongo na Amani, Jimmy Kisanga akiwa ameshikilia zawadi yake ya Sh. 500, 000 mara baada ya kukabidhiwa.
amani-mshindi
Mshindi wa tatu wa Chemsha Bongo na Amani, Jimmy Kisanga (kushoto) akikabidhiwa zawadi yake ya Sh. 500,000 na wakala wa Global jijini Mwanza, Alex Mabula. Makabidhiano hayo yalifanyika Jumamosi iliyopita katika ofisi za Global.
Na Idd Mumba, Mwanza
MSHINDI wa tatu wa Chemsha Bongo ya kwenda Dubai inayotolewa na Gazeti la Amani, Jimmy Kisanga mkazi wa Igoma jijini hapa, amekabidhiwa zawadi yake, Sh.500,000.
Akizungumza na mtandao huu mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake hiyo, Jimmy alianza kwa kuishukuru Kampuni ya Global kwa kuweza kuwajali wasomaji wake kwani amekuwa mshiriki na shuhuda wa zawadi nyingi zitolewazo katika chemsha bongo mbalimbali.
“Kwanza namshukuru Mungu kwa zawadi hii na pili niishukuru Global kwa kweli, hii ni mara ya tatu tangu nimeanza kushiriki chemsha bongo hii hivyo kila toleo nilikuwa nasoma swali na kulijibu huku nikisubiri huenda nami nikashinda. Kweli Mungu ameonesha njia na leo hii (Jumamosi iliyopita) nimeshinda na kukabidhiwa zawadi yangu ya shilingi 500,000.
“Kiukweli najiona ni mtu mwenye bahati ya hali ya juu, ujue haipiti siku bila kusoma haya magazeti ya Global yaliojaa hadithi na habari mbalimbali za kufunza. Niwaombe wale wengine ambao hawajashiriki ama wamekata tamaa, wasikate tamaa na wala wasiwe na imani kwamba zawadi hizi zina watu wake maalum wanaowajua wao, hapana!” alisema Jimmy ambaye pia ni mfanyakazi Bodi ya Pamba kitengo cha kuendeleza zao la pamba jijini hapa.
Jimmy aliongeza kuwa zawadi hiyo aliyoshinda imemsaidia kwa kiasi kikubwa kumalizia ada ya mtoto wake aliyokuwa akidaiwa.
“Nina mke na watoto watatu, mmoja yupo darasa la kwanza mwingine la tatu na wa mwisho hasomi. Sasa huyu wa darasa la tatu anasoma shule ya Olimpio na alikuwa akidaiwa ada, niwe mkweli zawadi hii imekuja muda muafaka,” alimaliza Jimmy.
Jimmy anakuwa mshindi wa tatu wa chemsha bongo hii baada ya awali kuwapata wawili, Godwin Deodath Katiali mkazi wa Njia Panda Machame, Moshi na mwingine, Bakari Omar Omunga mkazi wa Manzese jijini Dar.
Chemsha Bongo hii bado inaendelea katika Gazeti la Amani. Kushiriki ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kununua gazeti lako la Amani kila Alhamisi na kujibu swali kiufasaha linalopatikana ukurasa wa pili. Kumbuka mshindi pia anaweza kupata safari ya kwenda kwenye jiji la maraha duniani, Dubai kula bata kwa siku tatu.

Mbunge Bonnah Kaluwa Achangisha Milioni 13.7 Ujenzi Kituo cha Yatima

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa akinadi vitu mbalimbali katika harambee hiyo kuchangisha fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC), chini ya Mchungaji Jehu Mkono. Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa akizungumza katika harambee hiyo kuchangisha fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC), chini ya Mchungaji Jehu Mkono.

 MBUNGE wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa ameongoza harambee ya uchangishaji wa fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC), chini ya Mchungaji Jehu Mkono. Harambee hiyo ilifanyika katika Kanisa la Deliverance Centre Victorius Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam, ambapo Bonnah Kaluwa alikuwa mgeni rasmi na kufanikiwa kukusanya fedha shilingi 13,730,000 ambazo zilipatikana kwa michango ya waumini, wageni waalikwa na kufanyika kwa mnada ulionadi vitu anuai.

 Katika harambee hizo Mbunge, Kaluwa alitoa shilingi milioni mbili yeye pamoja na mumewe huku akiendesha mnada uliotunisha mfuko wa ujenzi wa kituo hicho. Awali akizungumza katika harambee hiyo Mwenyekiti wa umoja wa akinamama wa kanisa la CVC, Rose Haji Mwalimu alisema harambee hiyo itawezesha kupatikana kwa fedha za ujenzi wa kituo pamoja na upanuzi wa kanisa la CVC eneo la Tegeta mradi unaotarajia kutumia shilingi milioni 40.
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (wa tatu kulia) akikata keki kuashiria uzinduzi wa harambee hiyo iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius. Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (wa pili kulia) akipeana mkono na Mwenyekiti wa umoja wa akinamama katika Kanisa la Deliverance Centre Victorius, Rose Haji Mwalimu (kulia) mara baada kukabidhi risala ya ujenzi wa kituo hicho. Kushoto ni Hoyce Temu, ambaye ni mwanakamati wa harambee hiyo. Meza kuu ikimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (hayupo pichani akizungumza) katika harambee ya uchangishaji wa fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC). Askofu Fedrick Ndonde (kushoto) ambaye ni rafiki wa karibu wa Kiongozi Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius, Mchungaji Jehu Mkono akizungumza katika hafla hiyo. Hoyce Temu (kushoto) ambaye ni mwanakamati wa harambee ya uchangishaji wa fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa na mgeni rasmi katika hafla hiyo. Kiongozi Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius, Mchungaji Jehu Mkono (kulia) akishusha maombi kabla ya kuanza kwa harambee hiyo ya uchangishaji wa fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta. Baadhi ya wageni waalikwa katika harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC), chini ya Mchungaji Jehu Mkono wakiwa katika harambee hiyo. Mwimbaji wa muziki wa injili, Edson Mwasabwite (kulia) akitumbuiza katika hafla hiyo ya uchangishaji fedha huku akiungwa mkono na Mbunge, Bonnah Kaluwa na viongozi wengine. Baadhi ya waumini wa Kanisa la Deliverance Centre Victorius Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam, wakiwa katika harambee hiyo. Kutoka kushoto ni Askofu Fedrick Ndonde, mwanakamati wa harambee hiyo, Hoyce Temu pamoja na Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa wakiwa katika harambee hiyo. Kiongozi Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius, Mchungaji Jehu Mkono (katikati) akiahidi kuchangia shilingi milioni moja katika mradi huo.

Watanzania wang’ara Rock City Marathon 2016,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza awa kivutio, akimbia km 5

$
0
0

Chacha Masinde kutoka mkoani Mara akimaliza Rock City Marathon na kuwa mshindi wa kwanza kwenye mbio hizo zilizofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana . Chacha alitumia muda wa saa 01:03:00 kumaliza mbio hizo akifuatiwa na mshiriki kutoka nchini Kenya David Kilimo aliyetumia muda wa saa 01:04:40.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Bw John Mongella sambamba na maofisa kutoka benki ya NMB wakishiriki mbio  za za km 5.
Washiriki wa mbio za km 21 wakiondoka Uwanja wa CCM Kirumba kuanza safari ndefu.
Ushindani ulikuwa ni mkubwa!
Washiriki kutoka pande tofauti za Dunia washiriki.
Ilikuwa ni furaha tupu kwa washiriki
Watoto nao hawakuwa nyuma…mbio zilihusisha watu kutoka rika zote kwa kuzingatia vigezo na mashariti.
Suala la usalama kwa washiriki ilikuwa miongoni mwa agenda za msingi kwenye mbio hizo.
Watu wenye ulemavu wa ngozi walishiriki mbio za km 5.
Mwandishi wetu, Mwanza


Chacha Masinde kutoka mkoani Mara ameibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jana jijini Mwanza baada ya kumaliza kwa muda wa saa 01:03:00, akifuatiwa na mshiriki kutoka nchini Kenya David Kilimo aliyetumia muda wa saa 01:04:40


Mbio hizo za kilomita 21 zilianzia Uwanja wa CCM Kirumba kupitia Barabara ya ikulu ndogo hadi mzunguko wa samaki na kuelekea Buzuruga kisha kutokea barabara ya pasiansi na kumalizikia uwanjani Kirumba huku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella akishiriki kukimbia mbio za km 5 sambamba na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.


Nafasi ya tatu upande wa wanaume ilichukuliwa na Mkenya Moris Mosima aliyetumia muda wa saa 01:04:57, ikiwa sekunde chache nyuma ya mpinzani wake.


Akizungumzia siri ya ushindi wake, Chacha siri ya mafanikio hayo ni kujituma kwake zaidi katika kufanya mazoezi maalum kwa ajili ya mashindano hayo ili kuhakikisha kwamba mwaka huu mshindi wa kwanza katika mbio hizo anatoka nchini Tanzania tofauti na miaka ya nyuma ambapo washindi walikuwa wakitoka nchini Kenya.


 “Niliweka nadhiri nikasema mwaka huu lazima mshindi atoke Tanzania zaidi niwe mimi na ninashukuru nimetimiza adhama yangu. Pamoja na hilo maandalizi ya mwaka huu yamekuwa mazuri zaidi mahitaji yote muhimu yakiwemo maji tukiwa njiani yamesaidia mafanakinio hayo licha ya washiriki kuwa zaidi mwaka huu hatua ambayo iliongeza changamoto kwetu zaidi,’’ alisema.


Upande wa wanawake mshindi wa kwanza ni Mtanzania pia Faimina Abdi kutoka mkoani Arusha aliyetumia muda wa saa 01:13:12 akifuatiwa na mwenzake  kutoka mkoani Arusha Angelina Daniel aliyetumia saa 01:14:38 huku Mkenya Dorifine Omary akishika nafasi ya tatu akitumia saa 01:16:54


Washindi wa kwanza katika mbio hizo zilizofanyika kwa mara ya nane jijini Mwanza  waliibuka na kitita cha Sh1.5 milioni kila mmoja, washindi wa pili Sh900,000 na washindi watatu Sh700,000.


Mashindano hayo ya kila mwaka yaliyokatika kalenda ya RT yaliandaliwa na Kampuni ya Capital Plus kwa udhamini kampuni za Freidkin Conservation Fund na African Wildlife Trust, Benki ya NMB,  New Mwanza Hotel, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Real PR Solutions, kampuni ya Fabec, Tiper, Puma Energies, Clouds Fm, Jembe Fm, Barmedas Tv na EF Out Door.


Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi kwa washindi na washiriki wa wa mbio hizo Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Bw John Mongella ambae pia alishiriki mbio hizo kwa kukimbia mbio za km 5 alisema mbio hizo ni nyenzo muhimu ya kuwaandaa wanariadha nchini kuwa katika nafasi ya kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa na kuirudishia nchi heshima yake katika mchezo huo.


“Ndio maana tumekuwa tukisisitiza wadhamini waendelee kujitokeza kusaidia mbio hizi ili ziendelee kuwa bora zaidi,’’ aliongeza.


Akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio hizo kwenye uwanja wa CCM Kirumba kwa niaba ya Katibu tawala jana, Afisa michezo mkoa waMwanza James William alisema mbio hizo ni nyenzo muhimu ya kuwaandaa wanariadha wetu nchini kuwa katika nafasi ya kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa na kuirudishia nchi yetu heshima ya kipekee katika mchezo huo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.


Alisema: “Tanzania inaweza kurejea katika ramani ya dunia kwenye michezo kama tukijikita katika maandalizi mazuri ya kuibua na kuviendeleza vipaji vya vijana wetu nchini hasa kuanzia ngazi ya shule za msingi.”


Naye Mbunge wa jimbo la Ilemema ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Ntumba na Maendeleo ya Makazi Bi Angelina Mabula alipongeza waandaaji wambio hizo na kutoa wito kwa washiriki walioshindwa kufanya vizuri kwenye mbio hizo kutokata tama bali wajiandae na mashindano yajayo ili waweze kufanya vizuri.


Naye Makamu Mwenyekiti wa mbio hizo Bw Zenno Ngowi alisema mbio hizo zimeweza kufanyika kwa mafaniko makubwa na ushirikiano walioupata kutoka uongozi wa mkoa wa Mwanza na mikoa jirani huku pongezi pia zikielekezwa  kwa jeshi la polisi kwa kuhakikisha kila kitu kinaisha kwa usalama

BEKI KISIKI WA PSG AHUKUMIWA KWENDA JELA, KISA KUMSHAMBULIA ASKARI

$
0
0
Beki wa kulia wa Paris St Germain, Serge Aurier ambaye ni raia wa Ivory Coast amehukumiwa kwenda jela miezi miwili kutokana na kukutwa na kosa la kumfanyia fujo askari polisi nchini Ufarasa. Beki huyo mwenye umri wa miaka 23 alifanya kosa hilo jijini Paris, Mei 30, mwaka huu ambapo inaelezwa alimshambulia na kumtolea maneno makali. Mbali na adhabu hiyo pia amepigwa faini ya euro 600 na mahakama na zinaweza kuongezeka euro 1,500. 


Mwanasheria wa mchezaji huyo amesema atakata rufaa kupinga adhabu hiyo, lakini bado kanuni zinamruhusu kuibadili na kuifanya kuwa adhabu ya kuitumikia jamii badala ya kwenda jela. Pia mchezaji huyo anatarajiwa kuwemo katika kikosi cha PSG kitakachocheza keshokutwa Jumatano katika Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Ludogorets.

 Mpaka sasa ameshaichezea PSG mechi 5 msimu huu na kutoa asisti kwa Edinson Cavani katika mechi dhidi ya Arsenal, wiki mbili zilizopita.

RAIS DK.SHEIN ATEMBELEA MRADI UJENZI WA NYUMBA ZA KISASA FUMBA

$
0
0
 Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group,(kulia ) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu Nd,Ayoub Mohamed Mahmoud.
 Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akifuatana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa (kushoto) pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group,(wa tatu kushoto) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) Salum Nassor Khamis,akifuatiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohamed.
 Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipanda ngazi ya moja ya nyumba zinazojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya  Azam Groupakifuatana na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo   Bw.Said Salim Bakhresa  wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo.
 Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa mashine za kutengenezea lami katika Kampuni ya Ujenzi ya  Azam Group N.P.Singh (wa pili kulia) wakati  alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum,(katikati) Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa na (kushoto)Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) Salum Nassor Khamis.
 Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa(kulia) wakati alipotembelea Mtambo wa  kutengenezea lami katika Kampuni ya Ujenzi ya  Azam Group leo wakati  alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi (wa pili kulia) Mtaam wa Mtambo N.P.Singh.
[Picha na Ikulu.]26/09/2016.

SPIKA NDUGAI ATEMBELEA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiwasili Mjini  Zanzibar kwa kutumia Boti wakati alipofanya ziara ya kutembelea Baraza la Wawakilishi mapema leo Septemba 2016.
 Spika wa Bunge  Mhe Job Ndugai akisalimiana  na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (katikati)  alipowasili katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kushoto ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma.
 Spika wa Bunge  Mhe Job Ndugai (kulia) akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (katikati) na Naibu Spika wa Baraza hilo  Mhe Mgeni Hassan Juma wakati alipowatembelea.
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa tatu toka kulia) akifuatilia kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati alipowatembelea. Wapili kulia ni Spika wa Baraza hilo Mhe Zuberi Ali Maulid na wa kwanza kulia ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai kiwasalimia Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar alipotambulishwa wakati wa kikao cha Baraza hilo.
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (kulia) na Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma (kushoto).
Spika wa Baraza la Wawakilishi  Mhe Zuberi Ali Maulid akimuelezea jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai wakati wa ziara hiyo.

Aunty Ezekiel Akerwa na Wanaosema ni Snitch na Anajipendekeza Kwa Zari

$
0
0
Anti Ezekiel Awashuki wanaosema anajipendekeza kwa Zari ・・・

 #Regrann from #auntyezekiel - Naitwa Aunty Ezekiel Grayson jujuman Ukipenda ...Mama Cookie Mnyakyusa hasilia ...Sasa bac Nataka niwaambie kitu kimoja mana kujibu mmoja mmoja Muda huo sina ni hv Nafanya ntakalo sifanyi Mtakayo mana nina uhakika nyie mnaokaa kubishana na mm vibanda vya mbavu za zaMmbwa zinawashinda so muda mnaokaa mkafatilia yangu mngeenda tafuta lakufanya ....Oooh njaa Yes I say tena Yes mana mnataka nibadili Red kuwa Yellow kwani yule c ni boss wa mkata viuno wang au!!!Sasa kama ni boss ulitaka nibishe niseme mm ndio Boss bac nifungue band yetu acheze!!!Mnawazimu nn na Namuheshimu kama Mshkaji rafiki boss wa bwanaangu na siwezi acha kushirikiana na Familia yake eti kisa Ushuzi mtasema nn...Sitaki kutaja majina ya watu ila kilichopo ndio ukweli asilia Mama Tee ndio mwanamke na Mama watoto wa Nasibu no way hata tulambe rami kubadili ni ngumu Ila mwenyewe akibadili bac na Sisi tutabadili ila kwa sasa ni Mama tee Shukrani gud Day #msaliti kulingana na wakati eti umemuacha mumeo jela mlitaka nikagongane nae jela Au nikae miaka 20 akitoka nina miaka 50 nazaa lini nalea lini nakufa lini Wapuuzi nn msinichefue mie msitake niongee yasiyowahusu...Mnanitoa Povu kama mmenilaza kwenye sabuni ya Unga

AliKiba ‘alinimind’ sana baada ya kuzagaa taarifa kwamba nipo tayari kwenda WCB – Abdul Kiba

$
0
0


Miezi michache iliyopita Abdul Kiba ambaye ni mdogo wake na AliKiba alinukuliwa vibaya na vyombo vya habari kwamba yupo tayari kujiunga na label ya ‘WCB’ ya Diamond kauli ambayo ilileta shida kwa mashabiki wa AliKiba pamoja na team yake.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video yake ya wimbo ‘Bayoyo’ ameiambia Bongo5 kuwa kauli hiyo ilimfanya aonekane msaliti.
“AliKiba alijisikia vibaya kwa sababu alijua kama ndo vile tena ndugu yake nimekuwa msaliti kumbe ni watu walipata definition nyingine na ni kitu ambacho hakiwezekani ila niliweza kufanya interviews nikaweka mambo sawa,” alisema Abdul Kiba.
Akifafanua kauli yake aliyozungumza na kutafsiriwa vibaya Abdul Kiba alisema “Siku ambayo nilifanya interview walinielewa vibaya maongezi yangu, unajua unaposikia kwamba kuna kazi hakuna kazi ya bure, kazi yoyote lazima iwe na malipo, nilikubali kwamba kama WCB watanihitaji kwa kolabo au show naweza nikajoin nao kufanya kazi ila sikutoa kauli kwamba naweza kwenda label yao kwa sababu hata mimi na label yangu,”
Pia muimbaji huyo amewashukuru mashabiki wa team Kiba kwa kuendelea kuwasapoti wasanii wake pamoja na kazi zao.

VANESSA ATOKWA POVU KUAMBIWA ANAJICHUBUA

$
0
0



Ubuyu unaotrendi Bongo unamgusa staa wa Bongo Fleva anayekamata anga za kimataifa, Vanessa Mdee ‘V-Money’ ambaye wikiendi iliyopita alitawala mitandao ya kijamii kwa picha yake iliyomuonesha akiwa amevaa kibukta na kuachia maungo yake wazi kisha mashabiki wakahoji kuwa rangi ya maungo haifanani na rangi ya uso wake ‘eti baadhi ya sehemu amekunywa maji mengi’. 
 
Mwana-ubuyu wetu alipoona picha hiyo imefunika mitandaoni, aliamua kuangaza kwenye kila akaunti ambapo alikutana na komenti nyingi zilizoonesha madai kuwa mwanadada huyo, kuna wakati huwa anaediti sura yake na kuonekana mweupe na kuna wakati anakuwa na ngozi ya maji ya kunde. Hata hivyo, wapo waliomvaa jumlajumla wakidai amekuwa akitumia mkorogo na kusahau baadhi ya maungo lakini pia wapo waliodai kuwa ni picha za Instagram ambazo mtu ana uwezo wa kuzifanya zikang’aa na akaonekana apendavyo.

 “Picha za mtandaoni ni noma! Unaweza ukadhani kitu kimetoka Ulaya leoleo lakini ukikutana nacho laivu, utajiuliza mara mbilimbili. Hicho ndicho kinachotokea kwa akina dada walio wengi wanaopenda kuuza sura,” alisema Antonio, mmoja wa wachangiaji mtandaoni. Baada ya Wikienda kuona ishu ya Vanessa imekuwa gumzo kutokana na komenti hizo ndipo likajiongeza na kuufanyia kazi ubuyu huo kwa kutafuta ukweli kwani mbali na rangi ya ngozi, pia wapo waliomdisi kimavazi lakini pia wapo waliompongeza kwa kwenda na wakati wakidai kuwa anavaa kimataifa zaidi. Wikienda kama kawaida yake lilimsaka Vanessa ili kumfikishia tuhuma zake za kujiediti na kutumia mkorogo. 
 
VANESSA ATOKWA POVU 
Katika kumtafuta Vanessa ili kuzungumzia kile kilichotrendi mtandaoni, Wikienda lilimwendea hewani kupitia simu yake ya mkononi kwani hakuwepo Dar badala yake ilielezwa kwamba yupo nchini Kenya akirekodi na mwanamuziki mkubwa wa Marekani, Trey Songz. Intavyu ya Vanessa na Wikienda ilikuwa hivi; Wikienda: Vanessa mambo vipi? Kuna maswali kadhaa nataka kukuuliza, uko free tuchati? Vanessa: Oke. 

Wikienda: Kuna picha zipo mtandaoni umebebwa stejini, mashabiki wako wanasema make-up zinakusaidia na wengine wanadai unajichubua usoni tu, mwilini umeusahau! Je, wewe unaliongeleaje hilo? Vanessa: Unadhani swali lako linanijenga nini mimi? Nakuomba uchunguze maswali yako kabla ya kuniuliza. 

Wikienda: Swali lina maana kubwa, wewe ni kioo cha jamii, kwa kuwekwa mtandaoni na kujadiliwa kuwa unajichubua, huoni kama unachafuliwa? Kwangu mimi nimeona nikupe nafasi ya kufunguka huenda kuna watu wanataka kukuharibia. 
 

Vannesa: Kwa sasa niko Kenya, nafanya kazi na msanii mkubwa wa Kimarekani, Trey Songz hujaandika lakini unataka kuniuliza maswali ya ajabu tu, kweli hayo ni maendeleo? Wikienda: Kazi yangu ni kuuliza kila kitu kama nakiona hakiendi sawa hasa kwa mastaa kutokana na gazeti ninaloliandikia, wewe jibu tu kwani nimekupa nafasi. Vannesa: Umenikwaza, naomba tuachane kwa sasa! Baada ya kuachana na Vanessa, kumbe alimpatia meneja wake namba ya mwandishi wetu ambaye alimtafuta Mwana-ubuyu kwa ajili ya kuweka mambo sawa ambapo naye alifunguka kama hivi.

 Meneja: Naitwa Tommy kwa jina. Ni meneja wa Vanessa, naomba tuwasiliane tafadhali. Wikienda: Poa una jipya lipi? Naona mmepaniki mpaka wewe umenipigia. Meneja: Yaah! Nimeona maswali unayomuuliza Vannesa, naona kama unauliza kabla ya kuchunguza nadhani kazi yako inakutaka kuwa makini kwanza. Wikienda: Mimi niko makini sana ila ninyi mmepaniki, staa hatakiwi kupaniki, anatakiwa kujibu kile anachoulizwa tu. 

Meneja: Oke! Mimi ndiye msemaji wa mwisho wa Vanessa, niulize nitakujibu. Wikienda: Kuna madai kuwa msanii wako anajichubua kwa sababu kuna picha imetrendi akiwa stejini na mwanaume, maungo yake yanaonekana kuwa meusi wakati usoni ni mweupe, je, unaweza kulijibu hilo? 

Meneja: Kwanza nikurekebishe, yule mwanaume ni Jux, lakini Vanessa hajichubui, anaipenda ngozi yake na nikwambie tu kwenye ulimwengu wa kisasa, Smat Phones zinatofautiana na inawezekana picha zinakuwa na ubora tofauti kutokana na kamera za simu kwani utakuta huyu anatumia Tecno, mwingine anatumia Iphone, lazima ubora wake utakuwa tofauti. “Tunaona kila kitu kinachoandikwa mtandaoni na siyo kila action inatakiwa kuwa na reaction. 

Sometimes ukikaa kimya pia nalo nijibu. Wewe unajua tupo kwenye karne gani. Smart phones ni nyingi na kila simu ina uwezo wa kamera yake. “Huwezi kumzuia shabiki, hata akiwa na aina yoyote ya simu, akitaka kupiga picha na Vanessa, nitaruhusu tu. “Kwa hiyo, quality ya picha iliopigwa na kamera ya shabiki wa Vanessa haikuwa sawa na wala siyo kwamba anajichubua,” alifunguka meneja huyo.
Alimalizia: “Vanessa anapenda ngozi yake na hana sababu ya kujichubua. She is comfortable in her skin aliyozaliwa nayo.”

 NENO LA MHARIRI 
Ubuyu unampongeza Vanessa kwa kuwa mvumilivu kwani maneno yaliyowekwa mtandaoni yanataka moyo, lakini ili uwe staa unatakiwa kukubaliana na kila linalotokea kwani kuna watakaokukubali na watakaokukataa. Lengo la kuandika Ubuyu huu ni kumpa nafasi ya kufungukia suala la mkorogo kwani si zuri na kumkubusha kama anatumia, basi aache kwa ajili ya afya yake. Ikumbukwe tu kuwa ubuyu hauna lengo la kumkandamiza staa yeyote bali ni kumrekebisha pale anapokosea na anapotofautiana na shabiki wake kuwekwa sawa kwani ndiyo kazi ya kolamu hii.

BIGO LA KWANZA KWA MANCHESTER CITY, KEVIN DE BRUYNE NJE MWEZI MZIMA

$
0
0
Baada ya kuwa na mwanzo mzuri wa msimu wa 2016/17, Manchester City imepata pigo la kwanza baada ya kiungo wake, Kevin de Bruyne ambaye amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu kutarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nne.


Kocha wa Man City, Pep Guardiola alisisitiza kuwa wanaweza kuendelea kufanya vizuri bila ya mchezaji wao huyo ambaye anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja. 







De Bruyne ambaye ni kiungo mshambuliaji aliumia katika mechi ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Swansea City, katika Premier League na kutolewa katika dakika ya 81 kwenye Uwanja wa Liberty, nafasi yake ikachukuliwa na Jesus Navas.



Tayari Guardiola alithibitisha kuwa watamkosa mchezaji huyo kuanzia mechi ya keshokutwa Jumatano dhidi ya Celtic katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI ATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi  Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wafanyakazi waliokuwa wakimshangilia wakati akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa  Meneja wa Kitengo cha Kontena wa  Kampuni ya Ushushaji Shehena ya makasha  Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)  Bw. Donald Talawa  alipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa  Meneja wa Kitengo cha Kontena wa  Kampuni ya Ushushaji Shehena ya makasha  Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)  Bw. Donald Talawa  alipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa mapendekezo  kwa  Kampuni ya Ushushaji Shehena ya makasha  Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa  Meneja wa Kitengo cha Kontena wa  Kampuni ya Ushushaji Shehena ya makasha  Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)  Bw. Donald Talawa  alipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mary Mhayaya kuhusu  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu zoezi la  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu zoezi la  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya kupimia kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya kupimia kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo  kuangalia sehemu ya kupimia kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongozwa na Mhandisi Mary Mhayaya kuhusu akikagua mtambo wa  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mary Mhayaya kuhusu  chumba cha mitambo ya  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo ya chumba cha ukaguzi wa mizigo (scanner) inayoingia nchini  katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo ya chumba cha ukaguzi wa mizigo (scanner) inayoingia nchini  katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 
 Wafanyakazi wa bandari ya Dar es salaam wakimlaki kwa furaha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipofika kuongea nao baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 

 Mwenyekiti wa Wafanyakazi wa Bandarini Bw.  Mashaka Karume akieleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 
 Wafanyakazi wa bandari ya Dar es salaam wakimsikiliza   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipofika kuongea nao baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga  wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia mkono kuwaaga  na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016

Magazeti ya Tanzania Leo Jumanne ya Septemba 27, 2016

'Panya Road' Waibuka Upya Na Kutesa Wananchi Moshi Baa Jijini Dar Es Salaam

$
0
0

Na Dotto Mwaibale

KUNDI la uhalifu la watoto wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 25 maarufu kama panya road linatishia usalama wa wananchi na mali zao maeneo ya Moshi Baa na vitongoji vingine katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Kufuatia kukithiri kwa vitendo hivyo katika kipindi kisichopungua wiki mbili tayari watoto watatu walikuwa wakidaiwa kuhusika na kundi hilo wameuawa na wananchi wenye hasira kali.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Dar es Salaa jana   mkazi wa eneo la Moshi Baa Relini aliyejitambulisha kwa jina la Mwarami Abubakar alisema hali sio shwari katika eneo kufuatia matukio ya kila siku ya kuvamiwa wananchi kujeruhiwa na kuporwa mali zao na kundi hilo.

"Tayari vijana wawili wiki iliyopita wamechomwa moto na wananchi wenye hasira huku mwingine akipigwa juzi hadi kutolewa utumbo na kufariki papo hapo," alisema Abubakar.

Mkazi mwingine wa eneo la Kwa Mkolemba Khamisi Fadhil alisema kundi hilo limekuwa likifanya vitendo hivyo mchana kweupe na wanatembea kuanzia vijana nane hadi 10 wakiwa na silaha za jadi kama nondo, visu na mapanga na mtu yeyote wanayekutana naye ni lazima wampige na kumpora.

Wenye maduka wanalazimika kufunga kuanzia saa moja jioni kuhofia kundi hilo ambalo huvunja milango ya nyumba na kufanya uporaji" alisema Fadhil.

Fadhil alisema maeneo ambayo vijana hao wameshamiri ni Moshi Baa Relini, Kwa Mkolemba, Diwani na Bomba mbili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Kamishna Msaidizi (ACP), Salum Hamdan alisema polisi imejipanga vilivyokukabiliana na vitendo hivyo katika mkoa wake.

"Kwanza napenda kukuambia kwamba hakuna kundi linalojiita panya road wote tunawahesabu ni wahalifu kama walivyo wahalifu wengine na hivi ninavyongea na wewe tupo katika siku ya sita ya operesheni ya kukakamta watu wanaojihusisha na uhalifu wa ujambazi wakiwemo wanaouza pombe haramu ya gongo," alisema Kamanda Hamdan.

Aliongeza kuwa katika mkoa wake hivi karibuni utakuwa shwari baada ya askari wake kusambaratisha watu hao wanaofanya vitendo hivyo.

Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062

Waziri Mkuu Majaliwa atoa wiki moja kwa Afisa Elimu kutafuta walimu wa kidato cha tano na sita

$
0
0
WAZIRI MKUUkuu  Mhe. Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Yussuph Kipengele kupeleka walimu wa kufundisha masomo ya kidato cha tano na sita katika shule za sekondari za Mkongo na Utete wilayani Rufiji. 
 
Ametoa agizo hilo  Jumatatu, Septemba 26, 2016  wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jumba la Maendeleo wilayani Rufiji.  baada ya Mbunge wa Rufiji, Muhammed Mchengelwa kumwambia kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu wa kidato cha tano na sita licha ya kuwa na shule. 
 
"Hatuwezi kuwa na shule ambazo hazina walimu, nasikia hapa anayefundisha ni Mkuu wa shule na mwalimu mmoja tu, wakati kule Kibaha kuna walimu walmerundikana ,sasa fanya realocation tarehe 4,Oktoba uniletee taarifa walimu wamefika Rufiji.",alisema Waziri Mkuu. 
 
Akizungumzia suala la upungufu wa watumishi wa umma kwenye sekta mbalimbali, Waziri Mkuu alisema baada ya kazi ya uhakiki watumishi hewa itakapokamilika, serikali itaangalia kwenye maeneo yenye upungufu na hivyo kutangaza ajira. 
 
 "Hivi sasa serikali inakamilisha masuala ya uhakiki wa watumishi, tukimakamilisha na kujua idadi ya watumishi na maeneo yenye upungufu tutaanza tena kuajiri, tulisitisha kupisha kwanza kazi hii,alisema Waziri Majaliwa. 
 
Kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji Waziri, Mkuu alisema watendaji wa halmashauri na vijiji wanapaswa kutenga maeneo ya wafugaji na wakulima na kutaka mifugo isiongezwe kwenye maeneo ambayo hayajaruhusiwa. 
 
 Alisema wenyeviti wa vijiji wanapaswa kusimamia utekelezaji wake katika mpango wa matumizi bora ya ardhi na kwamba atakayeruhusu idadi kubwa ya mifugo kuingia kijijini zaidi ya ile iliyokubalika atawajibishwa ikiwemo kufukuzwa kazi na hatua nyingine za kisheria. 
 
 "Hatuwezi kuendelea kuwa na watumishi wasio na nidhamu, wale wote watakaoingia mifugo zaidi ya uwezo wa kijiji wafukuzwe kazi na kuchukuliwa hatua, lakini pia wafugaji ni marufuko kuingiza mifugo kwenye mazao ya wakulima"alisema Waziri Mkuu. 
 
 Kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kwenda makao makuu ya wilaya ya Rufiji, Utete, Waziri Mkuu aliahidi kuchukua ombi hilo na kusema bajeti ijayo litatengewa fedha kuwa ajili ya kufanya maandalizi ya upembuzi kuona gharama yake kabla ya kutangaza zabuni ya ujenzi. 
 
 Kuhusu utengenezaji wa madawati, Waziri Mkuu alisema ifikapo Oktoba 30, mwaka huu kila wilaya nchini inapaswa iwe imekamilisha utengenezaji wa madawati hayo kwenye shule nchini. 
 
 Aidha, alisema ipo miradi mingi inayoendeshwa kwa maslahi binafsi ukiwemo mradi wa Bonde la Rufiji(RUBADA), ambao wamebaini kuna ubabaishaji mkubwa, hivyo wamepeleka timu ya wataalamu kuhakiki ili wale wabadhirifu wachukuliwe hatua. 
IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMATATU, SEPTEMBA 26, 2016

SITALIA TENA- 01

$
0
0

MTUNZI: NYEMO CHILONGANI
Where do you live?” (unaishi wapi?)“Tanzania! You?” (Tanzania! Wewe?)
“Oman.”“This is my first time to chart with an African girl, you look stunning...” (hii ni mara yangu ya kwanza kuwasiliana na mwanamke wa Kiafrika, umependeza)“Thank you Kaseem.” (Nashukuru Kaseem)
Msichana Saida alikuwa kwenye kompyuta yake ya mapajani akiwasiliana na mwanaume aliyekutana naye katika Mtandao wa Kijamii wa Facebook, Mwarabu aliyekuwa akiishi nchini Oman.
Muda wote uso wa Saida ulikuwa kwenye tabasamu pana. Kitendo cha kuwasiliana na mwanaume huyo kilimfanya kujawa na furaha tele huku muda wote uso wake ulitawaliwa na tabasamu pana.
Kijana aliyekuwa akiwasiliana naye kipindi hicho aliitwa kwa jina la Kassem Abdulaziz. Alikuwa mwanaume wa Kiarabu aliyekuwa akiishi nchini Oman. Mara ya kwanza walikutana ndani ya Mtandao wa Facebook, japokuwa Saida alikuwa msichana mrembo aliyewaletea mapozi wanaume wengi katika mtandao huo lakini kwa Kaseem akashindwa kukataa, alipotumiwa meseji ya kwanza tu, akamjibu na kujikuta wakiwasiliana kila siku.
Moyo wake ukatokea kuvutiwa na mwanaume huyo wa Kiarabu. Alikuwa na sura nzuri, ndevu alizozinyoa kwa staili ya O huku nywele zake akiwa amezipendezesha kwa dawa za nywele zilizomfanya kuvutia na kupendeza machoni mwa msichana yeyote yule.
Saida hakutaka kuishia kuangalia picha moja tu, alichokifanya ni kufungua katika sehemu ya picha za mwanaume huyo na kuanza kuangalia picha nyingine. Akatokea kumpenda lakini hakutaka kuweka wazi, waliendelea kuchati siku hadi siku, wiki hadi wiki pasipo kuonana.
Saida hakutaka kuficha, alichokifanya ni kuwaambia marafiki zake kuhusu Kaseem. Kila mmoja alimshangaa. Hawakumshangaa kwamba kwa nini alikuwa na mwanaume huyo, walichoshangaa ni kwa nini alimwamini mwanaume wa mtandaoni.
Marafiki zake wakamwambia kwamba lingekuwa jambo jema kama angeachana naye lakini Saida hakutaka kusikia kwani moyo wake ulitekwa, hakuona kama angeweza kuachana na mwanaume huyo ambaye kwake, tayari alimuona kuwa mwanaume wake wa ndoto.
Alichokifanya ni kuwaonyeshea picha za Kaseem, marafiki zake hawakuamini kama kweli duniani kulikuwa na mwanaume aliyekuwa na sura nzuri kama alivyokuwa Kaseem. Nao wakajikuta wakianza kumtamani.
“Ni mwanaume mzuri sana, mpaka nakuonea wivu,” alisema rafiki yake aliyeitwa Grace. Aliishikilia simu ya Saida na kuanza kuangalia picha za mwanaume huyo.
“Ninampenda sana...” alisema Saida.
“Umemwambia?”
“Anajua hilo nadhani, ila sijamtamkia kwa maneno, naogopa,” alisema Saida na kisha kutoa kicheko kidogo.
Mawasiliano yakapamba zaidi. Kila siku ilikuwa ni lazima kuwasiliana na mwanaume huyo. Mawasiliano hayakuishia kwenye Facebook tu, wakahamia kwenye WhatsApp na kuanza kuwasiliana huko.
Wakawa huru, wakatumiana sana picha mbalimbali. Kwa jinsi alivyoonekana, Kaseem hakuwa mwanaume masikini. Alikuwa akipiga picha kwenye magari mazuri, ya gharama ambayo yalimtoa udenda Saida.
Alitamani kumuuliza kuhusu familia yao lakini akaamua kunyamaza, hakutaka kuonekana kama alizipenda fedha zake, alichotaka kumuonyeshea ni mapenzi mazito, hata kama mwanaume huyo angekuwa masikini, basi angempenda hivyohivyo.
“Wewe unaishi Tanzania sehemu gani?” aliuliza Kassem.
“Dar es Salaam.”
“Ooh! Ningependa siku nije huko nikuone. Nitaruhusiwa?” aliuliza Kaseem.
“Hakuna tatizo. Karibu!”
Baada ya kuwasiliana kwa miezi mitatu ndipo Kaseem alipoamua kutupa karata yake, akaamua kumwambia Saida kile kilichoendelea ndani ya moyo wake, jinsi alivyokuwa akimpenda na kuhisi mapenzi mazito ndani ya moyo wake.
Kwa Saida, hakutaka kuwa na pingamizi, alimpenda mwanaume huyo na hatimaye wakajikuta wakiingia katika dimbwi la mahaba mazito. Wakapendana sana, kwa Saida, hakutaka kuwa na mwanaume yeyote yule zaidi ya mwanaume huyo ambaye hakuwahi kuonana naye katika maisha yake zaidi ya kuona picha zake tu na video walizokuwa wakitumiana katika Mtandao wa WhatsApp.
“Naomba nikwambie kitu,” alisema mwanaume huyo.
“Niambie!”
“Lakini naomba iwe siri! Usimwambie mtu, hasa ndugu na marafiki zako!” alisema Kaseem, kidogo Saida akashtuka.
“Hakuna tatizo!”
“Umekwishawahi kumsikia mtu anayeitwa Fabrouz Abdulaziz?”
“Hapana! Ndiye nani?”
“Mtafute Google.”
“Sawa.”
Alichokifanya Saida ni kumtafuta mwanaume huyo aliyeambiwa. Kutokana na jina la mwanaume huyo kuwa kubwa, wala Saida hakupata wakati mgumu, akamuona mtu huyo na kuanza kumwangalia.
Akashtuka. Mwanaume huyo alikuwa mmoja wa mabilionea wakubwa katika nchi za Uarabuni. Alikuwa akimiliki kiasi kikubwa cha fedha, visima vya mafuta, migodi na hoteli kubwa nchini Oman.
Saida hakuishia hapo, alichokifanya ni kuangalia familia ya mzee huyo. Hakuamini baada ya kuona kuwa mzee huyo bilionea alikuwa na watoto wawili tu, msichana aliyeitwa Faudhia na mwanaume aliyeitwa Kaseem, na alipofungua picha kumuona huyo Kaseem, macho yake yakatua kwa mwanaume huyohuyo aliyekuwa akiwasiliana naye.
“Kaseem...is it true?” (Kaseem...ni kweli?)
“About what?” (kuhusu nini?)
“What I’ve seen,” (kile nilichokiona)
“Please...don’t tell anyone!” (naomba usimwambie yeyote...tafadhali)
Saida akatulia, hakuamini kama kweli alikuwa mpenzi wa mtoto wa bilionea kutoka nchini Oman. Akashusha pumzi ndefu kisha kuanza kuziangalia tena picha za Kaseem, akaangalia magari aliyokuwa akipiga picha Kaseem na nyumba aliyokuwa amesimama mbele yake, akajikuta akichanganyikiwa akili yake.
“I want you to marry me,” (nataka nikuoe) alisema Kaseem.
“Kaseem...”
“Please...be my wife..” (naomba uwe mke wangu, tafadhali) alisema Kaseem kupitia video fupi katika WhatsApp.
Alitoka katika familia ya kawaida, haikuwa kwenye utajiri wa umasikini. Kipindi hicho ndiyo kwanza alikuwa ameanza chuo, kitendo cha kuambiwa na Kaseem kwamba alitamani sana awe mke wake kikamchanganya.
Saida hakutaka kujibu harakaharaka, akatulia na kumwambia Kaseem kwamba alihitaji muda na angemjibu kuhusu hilo alilomwambia. Hakutaka kuwashirikisha marafiki zake, alichokifanya ni kutumia muda wake na kuanza kujiuliza kama alikuwa sahihi kumkubalia Kaseem au la.
Wakati mwingine akawa anajiuliza kama kweli Kaseem yule mtoto wa bilionea Abdulaziz alikuwa huyo aliyekuwa akiwasiliana naye au mwingine. Baada ya kujifikiria sana kuhusu hilo, baadaye akajipa jibu kwamba huyo alikuwa ndiye yeye kwani hata alipomwangalia kwenye Wikipedia, alikuwa yeye.
“Nimkubalie au? Mungu wangu! Naomba jibu lako,” alisema Saida. Ilikuwa rahisi sana kwa msichana kukubali kuwa na mtu kama Kaseem, ila kwake, kidogo moyo wake ulikuwa na hofu kubwa.
Je, nini kitaendelea?
Tukutane Siku ya kesho
Kutokana na maombi ya watu hadithi ziwe mbili. Nimeamua kuianza na
Itakuwa inaendelea hapa na katika website hii bonyeza link http://www.2jiachie.com/search/label/Simulizi

Penzi la Wakongo Lamaliza Mastaa Bongo!

$
0
0


Imefichuka kuwa, baadhi ya wanaume kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) waliopiga makazi yao Bongo, wamewamaliza mastaa nchini kutokana na penzi la pesa wanalolimwaga kwao, Uwazi limechimba. 


Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na mastaa waliokwishagawa penzi kwa Wakongo hao, kinachoonekana sasa ni mashindano ya mastaa wa Bongo kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anafaidi pesa za mapedeshee hao licha ya kwamba, mapenzi yao hayadumu. “Jamani nyie watu wa Global, sidhani kama mmewahi kufanya uchunguzi wa kina na kubaini kuhusu hawa wanaume wa kutoka Kongo. Baadhi yao wamekuwa wakigawa pesa ili kuwapata mastaa wa Bongo.
 

“Ndiyo maama ukifuatilia utagundua kuwa, kila kukicha, Mkongo f’lani kamchukua staa f’lani. Mbaya zaidi, mastaa wanazungukana wenyewe kwa wenyewe. Leo utasikia Mkongo yupo na huyu, kesho yupo na yule na wenyewe mastaa wanajua, lakini hawakatai maana wao wanataka pesa tu,” alisema mtoa habari huyo ambaye naye ni staa lakini asiyetaka ‘kujinajisi’ na jasho la Wakongo hao. Mnyetishaji huyo aliendelea kuweka wazi kwamba, maisha ya Wakongo hao hapa Bongo ni ya taiming:
 
 “Kuna wakati wanachacha sana. Lakini wakipata ndiyo kufuru yao inakuwa kwa wenzangu na mimi. Mimi aka! N’takula pesa za mwanaume mwenye mapenzi na mimi lakini siyo wanaofuata majina makubwa kama fasheni. Nyie fuatilieni mtagundua mastaa walionasa kwa Wakongo wote wana majina makubwa, sasa hapo amebaki nani?

 “Halafu hawa jamaa, pesa nyingi wanazipata kutoka kwenye nchi za Ufaransa, Ubelgiji na Dubai. Sijui kule wanafanya dili gani? Ila akitokea amekwenda kule akiwa mchovu, akirudi hatulali mjini. Kwa kweli pesa ni za kumwaga kwani katika hali halisi, wanaume hao wanawazidi wa Kitanzania kwa kuhonga. “Wapo mastaa wanahongwa shilingi milioni ishirini mpaka hamsini. Ndiyo maana unawaona mastaa wenzangu wengine hawachezi filamu muda mrefu, lakini wanaishi sawa, wanakula, wanavaa, wanakwenda saluni, wana magari, wanaweka mafuta na wanafanya bethidei tena za kufuru.”
 

KUMBUKUMBU YA UWAZI 
Kumbukumbu ya gazeti hili, mpaka sasa, mastaa wa Bongo ambao wameshaandikwa kwenye magazeti pendwa kuwa wanatoka au wamewahi kutoka na wanaume Wakongo ni kama ifuatavyo: Wema Sepetu na Husna Idi, wao wameshaandikwa kutoka na Mkongo aitwaye Mwami Rajab ambapo siku za karibuni, mkewe wa Mwami, Nora Chilu alijitokeza na kuwapiga mkwara mastaa hao kuachana na mumewe.

 Jacqueline Wolper, yeye amewahi kuandikwa kutoka na Mwami, lakini baadaye wakamwagana na kunasa kwa Mkongo mwingine, Putin ila kwa sasa wememwagana. Hivi karibuni, mwigizaji mwingine Bongo, Shamsa Ford  ambaye kwa sasa ni mke wa mtu, aliandikwa akidai kuwa, Mkongo wa Wolper na Wema (hakumtaja jina) amemtongoza
lakini akamchomolea mbali. 

 
Pia, mwanamitindo mwenye mvuto Bongo, Hamisa Mobeto amewahi kuandikwa kunasa mtungo wa Mkongo, Mwami. Mobeto alibainika baada ya meseji zake za simu kunaswa akiomba pesa za kulipia mapazia. Staa mwingine aliyewahi kuandikwa kutoka na Mkongo huyo ni Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’. Pia, aliyewahi kushiriki Bongo Star Search, Baby Joseph Madaha, hivi karibuni aliandikwa kumzoa bwana wa Wema ambaye ni Mkongo aliyejulikana kwa jina la John na walilala wote hotelini nchi jirani. 

Kuhusu msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ yeye aliwahi kuandikwa na Mkongo, Mwami. Mkongo huyo alisema anamtaka msanii huyo kwa gharama yoyote ile. Lakini siku chache, Lulu alijibu kuwa, kama Mkongo huyo angekuwa na mapenzi ya kweli asingeyaeleza kwenye magazeti.

Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>