Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya May 19, 2016


Zitto Kabwe, Halima Mdee na John Heche Wawekwa Kitimoto.....Wahojiwa Kwa Dadkia 90 Kwa Kufanya Fujo Bungeni

$
0
0
MBUNGE wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT-Wazalendo) na wenzake wawili, jana wamehojiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika kwa kufanya fujo bungeni kuhusu suala la Bunge kutorushwa ‘live’.

Mbali na Zitto, wengine waliohojiwa ni pamoja na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema). Wabunge hao walihojiwa kwa tuhuma za kufanya fujo bungeni wakati ilipotolewa hoja ya Bunge kutorushwa moja kwa moja ‘live’, akiwa pamoja na wabunge wawili; Mdee na Heche.

Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya kamati hiyo, kimesema Zitto alihojiwa na kamati hiyo kwa muda wa zaidi ya saa moja kwa makosa mbalimbali, ikiwamo kufanya fujo bungeni Januari 27, mwaka huu.

Taarifa hizo zilieleza kuwa Zitto alifanya fujo hizo baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, kuahirisha kujadili hoja ya serikali iliyowasilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, kuhusu Bunge kutorushwa ‘live’.

Hatua hiyo inatokana na hoja iliyowasilishwa na Zitto aliyetaka kuahirishwa kujadili hotuba ya Rais kutokana na kauli ya Waziri Nape ya kutorushwa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.

Zitto, alihojiwa na kamati hiyo ya Mkuchika kwa kilichoelezwa alisimama na kuomba mwongozo kuhusu jambo ambalo limekwishatolewa uamuzi kinyume na Kanuni ya 72 (1) na 68 (10 ya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari 2016.

Mbali na hilo pia anadaiwa kusimama na kuzungumza bila utaratibu kinyume na Kanuni ya 60 (2) na 12 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, jambo ambalo lilileta fujo na kuvunja shughuli za Bunge.

Katika barua za mwito zilizosainiwa na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah, Mei 12, mwaka huu, inaelezwa kwamba pamoja na mambo mengine na Mwenyekiti wa Bunge kumsihi mbunge huyo bado aliendelea kuzungumza na kusimama ikiwa ni kuonesha dharau kwa mamlaka ya Spika na shughuli za Bunge kinyume na kifungu namba 24 (d) na (e) cha Sheria ya Kinga na Haki za Bunge.

Barua hiyo ilieleza kuwa kutokana na vitendo hivyo vinavyokiuka Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, Sura namba 296 na Kanuni za Bunge, wabunge hao walionywa kuwa endapo wasingefika mbele ya kamati hiyo jana hatua za kisheria zingechukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa kifungu cha 15 na 31 (1)(a) na sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Yapandisha Mshahara Kima cha chini Hadi 300,000/ Kutoka 150,000 Ya Hapo Awali

$
0
0

Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetangaza bajeti ya Serikali hiyo ya Sh bilioni 841.5 kwa mwaka wa fedha 2016/2017; na kupandisha mshahara kwa kima cha chini kutoka Sh 150,000 hadi Sh 300,000.

Hatua hiyo imelenga kuongeza ufanisi na kupambana na ugumu wa maisha kwa wafanyakazi wake, kubana matumizi ya ndani na kuifanya nchi kuwa ya viwanda. 
Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk Khalid Salum Mohamed ndiye aliwasilisha bajeti hiyo katika Baraza la Wawakilishi mjini Zanzibar.

Alisema vipaumbele katika bajeti hiyo ni katika kuimarisha sekta ya elimu, afya na miundombinu ya bandari na uwanja wa ndege. 
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakadiria kutumia Sh bilioni 841.5 kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Kati ya fedha hizo, Sh bilioni 445.6 kwa kazi za kawaida na Sh bilioni 395.9 kwa kazi za maendeleo.

Alisema katika mwaka wa fedha 2016-2017 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ipo katika mchakato wa kukamilisha na kuanza kwa miradi miwili mikubwa ya miundombinu, ambayo ni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume katika jengo la abiria.

Aidha alisema ujenzi wa bandari ya kisasa ya Mpigaduri, utasaidia kuongeza mapato na ajira kwa wananchi wa Zanzibar mara utakapomalizika. 
Dk Salum alisema bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 inakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwamo kupungua kwa fedha kutoka kwa washiriki wa maendeleo; na ndiyo maana bajeti hiyo itajikita zaidi katika kuweka kipaumbele cha makusanyo ya kodi ya ndani.

“Tumeweka kipaumbele zaidi katika makusanyo ya kodi kupitia vyanzo vyake, ambapo taasisi za ukusanyaji kodi Mamlaka ya Mapato (TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) tumezipa majukumu makubwa zaidi katika makusanyo ya kodi,” alisema Dk Salum.

Alifahamisha kwamba TRA inatarajiwa kukusanya Sh bilioni 188.8, wakati ZRB itakusanya Sh bilioni 237.4. Waziri huyo alisema muelekeo wa uchumi wa Zanzibar ni kufikia uchumi wa kati na usipungue asilimia nane kwa mwaka na kuifanya nchi kuwa ya viwanda.

Alisema SMZ imelenga Zanzibar kuwa nchi ya viwanda katika sekta ya kilimo na uvuvi na kuimarisha sekta ya utalii.
 Aidha, alisema serikali imesikia kilio cha kupungiza kodi ya mishahara ya wafanyakazi zaidi kipato cha chini, ambapo sasa kitapunguzwa kutoka asilimia 13 hadi 9. 
Salum alitangaza kwamba katika bajeti ya fedha kwa mwaka 2016-2017, hakutakuwa na ongezeko la kodi kwa lengo la kupunguza mzigo kwa wananchi.

Edward Lowassa na Fredrick Sumaye Watajwa Katika Sakata la Uuzwaji wa Nyumba za Serikali.......Mbowe Atoa Ufafanuzi

$
0
0
Uuzwaji wa nyumba za serikali umegeuka mwiba huku wabunge wakiendelea kuhoji hatua zilizochukuliwa kutokana na kadhia hiyo

Hatua hiyo iliyotekelezwa mwaka 2002  hadi 2004 ilizusha malalamiko mengi tangu wakati huo na sasa imeibuka tena bungeni

Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano jana, mbunge wa Nachingwea, Hassani Masala (CCM) alihoji mfumo uliotumika kuuza nyumba za serikali

Alisema haungi mkono kwa vile umesababisha viongozi wapya wa serikali wanaoteuliwa kujikuta wakiishi katika nyumba za wageni.

Mjadala huo uliibuliwa juzi na msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni kupitia kwa waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema kabla ya Mwenyekiti wa Bunge Mussa Azzan Zungu kumtaka kuondoa baadhi ya maneno katika hotuba yake likiweo suala la uuzwaji wa nyumba za serikali.
 Ritha Kabati Amvaa Lowassa
Akichangia mjadala huo jana, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ritha Kabati alimtaja aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa kuwa alinunua nyumba ya serikali iliyouzwa mwaka 2002 yenye jengo namba 68.

Alisema hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilisema nyumba za serikali 7,921 ziliuzwa tangu mwaka 2002 hadi 2004 na kutaka serikali ya awamu ya tano kurejesha nyumba hizo kutokana na walionunua kukiuka mikataba na malengo ya mauzo.

“Naomba niwaambie usiangalie boriti lililo katika jicho la mwenzako wakati kwako lipo, kwani hata mgombea wao wa urais Edward Lowassa alihusika kwa kununua nyumba ya plot namba 68 na Fredrick Sumaye alikuwa Waziri Mkuu na kuhusika kuuza nyumba hizo,” alisema Kabati.

Baada ya kueleza hayo, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema) aliomba kumpa taarifa mbunge huyo kuwa taarifa hiyo ni kwa maslahi ya taifa, hata kama mhusika atakuwa katokea kambi ya upinzani sheria itachukua hatua.
"Kambi ya upinzani tunapoibua jambo huwa linakuwa kwa maslahi ya Taifa, hivyo ni vyema wabunge wote mtambue kuwa kosa likifanywa na kiongozi  ni lazima hatua zichukuliwe bila kujali ni wa Chadema, CUF au CCM.
"Tunapokuwa tunatoa uamuzi kama kambi ina maana sheria ifuate mkondo wake." Alisema Mbowe huku akishangiliwa na wabunge wa UKAWA

Awali katika michango mbalimbali ya wabunge wa upinzani wamekuwa wakilalamikia kuuzwa nyumba hizo za serikali na kudai kuwa watumishi wapya wengi walioajiriwa, wamekuwa wakikosa maeneo ya kuishi.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) akichangia mjadala huo alilalamikia kuuzwa kwa nyumba hizo pamoja na nyingine za Tazara zipatazo 500 na kuamua kumpatia Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ripoti aliyodai inaonesha nyumba hizo zilivyouzwa.

SEVILLA NDIYO WENYE EUROPA CUP, WAITWANGA LIVERPOOL ILIYOTANGULIA 3-1 NA KULIBEBA KWA MARA YA TATU MFULULIZO

$
0
0

LIVERPOOL: Mignolet, Clyne, Lovren, Toure, Moreno, Milner, Can, Lallana, Firmino, Coutinho, Sturridge. 
Subs: Ward, Benteke, Henderson, Lucas, Allen, Origi, Skrtel.
Booked: Skrtel, Origi 
Scorer: Sturridge 35'

SEVILLA : Soria, Mariano, Rami, Carrico, Escudero, Krychowiak, Nzonzi, Coke, Banega, Vitolo, Gameiro. 
Subs: Sergio Rico, Kolodzieczak, Iborra, Cristoforo, Pareja, Konoplyanka, Llorente.
Booked: Vitolo, Banega
Scorer: Gameiro 47', Coke 64', 70'
Referee: Jonas Eriksson






Sakata la Escrow na IPTL Laibuka Upya Bungeni

$
0
0
Kambi ya upinzani imeliibua upya  bungeni sakata la Escrow, Richmond na umiliki wa kampuni ya IPTL, huku ikihoji sababu za Rais John Magufuli kutoheshimu maazimio ya Bunge ya kumwajibisha Sospeter Muhongo, badala yake kumteua tena kuwa Waziri wa Nishati na Madini.
Hoja hizo ziliibuliwa na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika wakati akiwasilisha maoni ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2015/16 na makadirio ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2016/17.

Muhongo alikuwa akiiongoza wizara hiyo wakati kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kuhifadhi fedha za malipo umeme kusubiri kumalizika kwa mzozo wa kimkataba baina ya kampuni ya IPTL, inayozalisha umeme  na Shirika la Umeme (Tanesco).

Bunge lilimuona Profesa Muhongo kuwa alishindwa kuwajibika na kusababisha Serikali kupoteza mapato.
Profesa Muhongo alilazimika kujiuzulu wadhifa huo saa chache kabla ya Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kutangaza baraza jipya.

Hata hivyo, Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma lilimsafisha na kashfa hiyo iliyohusisha malipo yaliyofanywa kwa mawaziri, majaji, wabunge na watumishi waandamizi wa umma.

Jana, Mnyika, ambaye ni mbunge wa Kibamba (Chadema), alirejea maazimio ya Bunge la Kumi akisema lilishafanya maamuzi kuhusiana na mikataba ambayo Serikali inaingia na kampuni mbalimbali, hasa kwenye sekta ya nishati na madini.

“Katika maazimio ya Bunge kuhusiana na fedha, ufisadi uliofanyika katika akaunti ya Tegeta Escrow na umiliki wa IPTL yanayohusu sekta ya nishati na madini, bado hayajatekelezwa kwa ukamilifu wake,” alisema Mnyika.
 Akinukuu Azimio Namba 2, Mnyika alisema liliagiza kwamba Serikali iangalie uwezekano wa kununua mitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwa Tanesco kwa lengo la kuokoa fedha inazolipa kwa kampuni hiyo binafsi.

Alisema kambi hiyo inasikitika kuona kwamba mbali ya Serikali kushindwa kununua, bado inaendelea kulipia gharama za uwekezaji na hivyo kuendelea kukiukwa kwa azimio hilo.

Akizungumzia azimio la saba linalohusu kuwajibishwa kwa mawaziri na watendaji wakuu wa wizara na bodi ya Tanesco, Mnyika alisema Profesa Muhongo naye aliwajibishwa kwa uteuzi wake kutenguliwa, lakini Rais Magufuli amemteua tena kuongoza wizara hiyo.

“Rais bila ya kujali nini Bunge lilishaazimia katika kikao ambacho na yeye alikuwa sehemu ya azimio hilo, akamteua Muhongo kuendelea kuiongoza wizara hii. Kambi ya upinzani inaliona jambo hili kama ni dharau sana kwa Bunge na ni fedheha binafsi kwake,” alisema.

Alisema kambi ya upinzani imelazimika kunukuu maazimio hayo kutokana na ukweli kwamba Serikali imeshindwa kabisa kutekeleza maazimio ya Bunge na badala yake mikataba hiyo inaendelea kutekelezwa kama ilivyoingiwa.

“Mfano mzuri ni Tanesco kuendelea kuilipa IPTL fedha za capacity charge mpaka sasa. Jambo hili linazidi kuliondolea shirika hilo la umeme uwezo wa kuwahudumia wateja wake kwa kuwa haliwezi kuwekeza zaidi katika miundombinu ya kusambaza umeme kutokana na kutokuwa na fedha za kutosha,” alisema.

Gardner Amjibu Lady Jay Dee, Agoma kuomba Radhi

$
0
0

Hatimaye mtangazaji wa Clouds Fm, Gardner G. Habash amemjibu aliyekuwa mkewe, Lady Jay Dee, aliyemtaka aombe radhi ndani ya siku saba kwa kauli aliyoitoa iliyodaiwa kuwa imelenga kumdhalilisha. Katika majibu yake amekana madai hayo.

Siku chache zilizopita, Gardner alionekana katika kipande cha Video akisherehesha tukio la kumsaka mrimbwende wa chuo cha Tanzania Institute of Accountancy (TIA) jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa “yule binti sina tatizo naye, nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi…”, kisha wimbo wa ‘Ndindindi’ wa Jay Dee ukachezwa na DJ.

Kama ilivyokuwa kwa Lady Jay Dee aliyetoa siku saba za kuombwa radhi kupitia kwa mwanasheria wake Amani Tenga, Gardner amejibu kupitia mwanasheria wake Stephen Axwesso.

Katika barua yake kwa mwanasheria wa Lady Jay Dee, mwanasheria huyo wa Gardner amekiri kuwa ni kweli mteja wake alizungumza maneno hayo alipokuwa katika shughuli iliyotajwa, lakini alidai kuwa hakuna sehemu aliyomtaja mkewe huyo wa zamani.

Alisema kuwa madai ya upande wa Lady Jay Dee hayana mashiko na alimshauri mwanasheria huyo kupitia upya sheria inayozungumzia wanandoa waliotalakiana ili aweze kumshauri vizuri mteja wake kuhusu suala hilo.

Nakala ya barua hiyo pia imetumwa Clouds Media Group na kwa Rais wa Wanafunzi wa Chuo cha TIA.

Magazeti Ya Leo Ijumaa ya May 20, 2016


Wizara ya Nishati Yatengewa Tril.1.22/- Katika Bajeti ya Mwaka wa fedha 2016/17

$
0
0
WIZARA ya Nishati na Madini imetengewa Sh trilioni 1.22 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17 huku fedha za miradi ya maendeleo zikiwa ni asilimia 94 ya fedha hizo.

Pia katika kuongeza kiwango kikubwa cha uzalishaji wa nishati, kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa, asilimia 98 ya Bajeti ya Maendeleo imetengwa kwa ajili ya sekta ya nishati.

Aidha, serikali imeongeza bajeti ya maendeleo ya fedha za ndani kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kufikia Sh bilioni 534.4, huku wateja wa umeme wa REA na Tanesco wakifikia 220,128. Mbali na hayo, kiwango cha upatikanaji wa huduma ya umeme kimeongezeka kufikia asilimia 40.

Hayo yalisemwa bungeni jana mjini Dodoma na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2016/17.

Profesa Muhongo alisema bajeti ya wizara kwa mwaka 2016/17 ni Sh trilioni 1,22,583,517,000, na kati ya fedha hizo, Sh 1,056,354,669,000 ni fedha za miradi ya maendeleo sawa na asilimia 94.

“Kwa kuzingatia Ibara ya 43(a) ya Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 inayoelekeza serikali kuongeza kiwango kikubwa cha uzalishaji wa nishati ili kuongeza mchango wake kwenye Pato la Taifa, asilimia 98 ya Bajeti ya Maendeleo imetengwa kwa ajili ya sekta ya nishati,” alisema Profesa Muhongo.

Alisema katika mwaka wa fedha 2015/16, waliidhinishiwa na Bunge Sh bilioni 642.12, na kati ya fedha hizo, Sh bilioni 502.30 sawa na asilimia 78 ya bajeti yote zilikuwa ni bajeti ya maendeleo.

“Hata hivyo, Bajeti hiyo iliongezeka kutoka shilingi bilioni 642.12 hadi shilingi bilioni 762.12. lengo la ongezeko ni kutekeleza miradi mikubwa ya kufua umeme ukiwemo Mradi wa Kinyerezi II – MW 240 ili kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini,” alisema Profesa Muhongo.

Megawati zaongezeka
Akizungumzia sekta ndogo ya umeme, alisema uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme nchini umeongezeka kutoka megawati 1,226.24 Aprili, 2015 hadi kufikia megawati 1,461.69 Aprili, 2016 sawa na ongezeko la asilimia 19.

“Ongezeko hilo limechangiwa na mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia baada ya kukamilika kwa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara na Lindi hadi Dar es Salaam,”alisema.

Aidha, alisema mahitaji ya juu ya umeme yameongezeka kutoka megawati 988.27 Desemba, 2015 hadi kufikia megawati 1,026.02 Machi, 2016 sawa na ongezeko la asilimia nne. 
Kuhusu upatikanaji wa umeme nchini, alisema kiwango cha huduma ya upatikanaji wa umeme kimekuwa kikiongezeka mwaka hadi mwaka.

“Watanzania waliofikiwa na huduma hiyo wameongezeka kutoka asilimia 36 mwezi Machi, 2015 hadi kufikia takribani asilimia 40 mwezi Aprili, 2016. 
“Ongezeko hilo limetokana na juhudi za serikali za kusambaza umeme nchini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),” alisema Profesa Muhongo.

Alisema kuanzia Julai, 2015 hadi Aprili, 2016 idadi ya wateja waliounganishwa na umeme wa REA pamoja na Tanesco ni 220,128 sawa na asilimia 88 ya lengo la kuunganisha wateja 250,000 ifikapo Juni mwaka huu. 
Umeme bila MCC 
“Katika kuongeza wigo wa upatikanaji wa umeme vijijini, serikali imeongeza Bajeti ya Maendeleo ya fedha za ndani kwa REA kutoka shilingi bilioni 357.12 kwa mwaka 2015/16 hadi shilingi bilioni 534.4 kwa mwaka 2016/17. Tumeongeza asilimia 50 na hakuna fedha za MCC (Shirika la Changamoto za Milenia) hapa,” alisema Muhongo.

"Ongezeko hilo ni kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2015 – 2020. Aidha, fedha za nje zilizotengwa kwa ajili ya mradi huo ni shilingi bilioni 53.21 sawa na asilimia tisa na hivyo kufanya jumla ya bajeti yote ya REA kwa mwaka 2016/17 kuwa shilingi bilioni 537.61.”

Mitambo kuongezwa 
Akizungumzia miradi ya kuzalisha na kusafirisha umeme, alisema serikali itatekeleza miradi mingi ambayo baadhi itakamilika katika mwaka wa fedha 2019/2020.

Alisema katika juhudi za kuongeza uzalishaji umeme, serikali imepanga kuongeza mitambo mingine ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi – I Extension wa megawati 185.

Alitaja mingine ni Kinyerezi II megawati 240, huku akitaja miradi iliyo katika hatua za mwisho za maandalizi ya miradi ambayo ni Kinyerezi III (megawati –MW 300), Rusumo Falls MW 80), Malagarasi MW 45 na Kanoko MW 87.

Kuhusu miradi ya usafirishaji umeme, alisema ujenzi wa mradi wa Iringa hadi Shinyanga wa kilovolti 400 umefikia wastani wa asilimia 89, ambao gharama zake ni Sh bilioni 387.5 na utakamilika Septemba mwaka huu.

Alisema serikali inaendelea kutekeleza miradi ya ujenzi wa njia za kusafirisha umeme zenye uwezo mkubwa hususan kilovolti 400. 
Miradi ambayo utekelezaji wake unatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2019/20 aliitaja kuwa ni Singida – Arusha – Namanga kv 400, Bulyahulu – Geita kv 220, Geita – Nyakanazi kv 220, North East Grid kv 400 na Somanga – Kinyerezi kv 400.

Aidha, alisema mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 400 kutoka Somanga Fungu hadi Kinyerezi, Tanesco imeshakamilisha ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaopisha mradi huu. 
“Hadi kufikia mwezi Aprili, 2016 shilingi bilioni 26.06 tayari zimelipwa na Tanesco kwa watu 947 katika wilaya za Ilala na Temeke,” alieleza.

Katika kuboresha miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini, mwaka 2014 Tanesco ilianzisha Kampuni Tanzu ya Tanzania Concrete Poles Manufacturing Company Limited (TCPCO), kwa ajili ya kujenga viwanda vya kutengeneza nguzo za zege nchini.

“Baada ya kukamilisha maandalizi ya ujenzi wa viwanda hivyo, TCPCO inatarajia kuanza uzalishaji wa nguzo za zege mwaka 2016/17,” alisema.

Kuhusu punguzo la viwango vya bei za umeme, Profesa Muhongo aliliarifu Bunge kuhusu punguzo hilo lililoanza Aprili mosi, mwaka huu.

Alisema serikali imepunguza bei ya umeme kwa kati ya asilimia 1.5 na 2.4, na pia imeondoa tozo ya kuwasilisha maombi ya kuunganishiwa umeme ya Sh 5,000 na tozo ya huduma ya mwezi ya Sh 5,520 kwa wateja wa umeme wa Daraja la TI na DI, ambao wengi wao ni wa majumbani.

“Hatua hii itawasaidia watumiaji wadogo wa umeme mijini na vijijini kumudu gharama hizo, hivyo kuboresha shughuli za kijamii na kiuchumi,” alisema Profesa Muhongo aliyerejea katika wizara hiyo baada ya kuwahi kuiongoza katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Kuhusu gesi asilia, alisema kukamilika kwa ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Mtwara kupitia Lindi hadi Dar es Salaam kumeongeza mchango wa uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia kufikia asilimia 49.

Aidha, alisema uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia umewezesha gharama za uzalishaji umeme nchini kupungua kutoka wastani wa Sh 262 hadi 229 kwa uniti moja ya umeme.

Profesa Muhongo alisema bomba hilo lenye urefu wa kilometa 542 ni pamoja na mitambo ya kusafisha gesi asilia katika maeneo ya Madimba (Mtwara) na Songo Songo (Lindi). Mradi huo ulizinduliwa rasmi Oktoba, 2015 na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete.

Akizungumzia shughuli za utafutaji gesi asilia, alisema Kampuni ya Dodsal imekamilisha tathmini ya kiasi cha gesi asilia kilichogunduliwa katika kisima cha Mambakofi – I kwenye Kitalu cha Ruvu Mkoa wa Pwani. Alisema tathmini hiyo inaonesha uwepo wa gesi asilia kiasi cha futi za ujazo trilioni (TFC) 2.17.

“Hivyo kufanya gesi asilia iliyogunduliwa nchini hadi Mei, 2016 kufikia TCF 57.25 ikilinganishwa na TCF 55.08 zilizokuwepo mwezi Aprili, 2015. Kati ya kiasi hicho, TCF 47.13 zipo kwenye kina kirefu baharini na TCF 10.12 zipo nchi kavu,” alisema.

Akizungumzia usambazaji wa gesi asilia jijini Dar es Salaam, alisema lengo la mradi huo ni kujenga mtandao wa kusambaza gesi asilia kwa njia ya mabomba na iliyoshindiliwa (CNG).

Kigogo wa CCM Ataka Maalim Seif Sharif Hamad Akamatwe

$
0
0

Kigogo wa CCM aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Sukwa Said Sukwa amevishauri vyombo vya dola visiwani Zanzibar kumchukuliwa hatua haraka Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kwa kauli yake aliyoihusisha na kosa la uhaini.

Sukwa aliitaja kauli ya Maalim Seif aliyoitoa alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara kisiwani Pemba kuwa Dk. Ali Mohamed Shein hatamaliza kipindi chake cha urais mwaka 2020 na kwamba ni dikteta.

Sukwa amesema kuwa kauli hiyo ya Maalim Seif haipaswi kupuuzwa hata kidogo kwakuwa kauli kama hizo ni zaidi ya sumu.

“Sivilazimishi vyombo vya dola kufanya ninavyotaka, lakini tunashauri tu visipuuze ushauri wetu kwa sababu ulimi wa mtu unaweza kuwa sumu hatari kuliko matendo yake,” Sukwa aliliambia gazeti la Raia Tanzania.

Maalim Seif amekuwa akifanya mikutano kuwataka wananchi kumuunga mkono kuikataa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Shein, akieleza kuwa uchaguzi wa marudio haukuwa wa haki.

Diamond Atajwa Kuwania Tuzo za BET 2016

$
0
0
Diamond Platinumz anaendelea kupaa katika ulimwengu wa muziki kimataifa ambapo mwaka huu pia nyota yake imeng’aa kwenye tuzo kubwa za Black Entertainment Television (BET 2016).
 
Mwimbaji huyo ametajwa kuwania kipengele cha Best International Act: Africa akichuana na wasanii wengine nguli Afrika ambao ni pamoja na AKA kutoka Afrika Kusini, Cassper Nyovest wa Afrika Kusini Black Cofee wa Afrika Kusini, Yemi Alade wa Nigeria, Wizkid wa Nigeria, Mzvee wa Ghana na Serge Beynaud wa Ivory Coast.

Tuzo hizo zitafanyika Juni mwaka huu nchini Marekani ambapo Diamond pia ametajwa kati ya watakaotumbuiza.

CUF Yataka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Aombe Radhi

$
0
0

Chama cha Wananchi(CUF) kimemtaka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awaombe radhi watanzania kwa kuwadhalilisha kuwa hawapendi kufanya kazi, badala yake  wanashinda kuangalia Bunge, hali ambayo imeisababisha lisirushwe moja kwa moja.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF Taifa, Twaha Taslima amesema Waziri Mkuu alitoa tuhuma hizo kwa wananchi akiwa nchini Marekani hivi karibuni,wakati  siyo kweli kwamba watanzania wanakesha kuangalia bunge tangu  linapoanza hadi linakwisha bila kufanya kazi.

Hivi karibuni Waziri Majaliwa akizungumza na watanzania waishio Uingereza alisema sababu ya bunge kutorushwa moja kwa moja ni kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’

“Kama ni hivyo basi maisha ya watanzania wengine yangekwama hivyo Serikali ya awamu ya tano kazi yake kubwa sasa ni kutaka kuwarudisha watanzania kwenye woga wa kutoiwajibisha Serikali kwa kisingizio cha hapa kazi tu slogani hii ni ya kuua demokrasia,” amesema Taslima.

Taslima ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu hali ya demokrasia nchini na mwelekeo wa CUF baada ya Uchaguzi.

Amesema kuna madhara mengi katika kukandamiza demokrasia, ikiwamo wananchi kujenga chuki na Serikali, hivyo kushindwa kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za maendeleo.

Taslima ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi waliowezesha chama hicho kuongeza idadi ya wabunge kutoka 34 mwaka 2010 hadi 42 katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba mwaka jana.

Amesema CUF baada ya kumaliza shughuli za uchaguzi inajipanga kufanya ziara nchi nzima, lakini pia inajiandaa na uchaguzi wa kuziba mapengo ya uongozi ngazi mbalimbali kuanzia kwenye matawi hadi taifa.

“ Kwa sababu tofauti baadhi ya nafasi za uongozi badi zipo wazi  hivyo  ndani ya kuipindi cha miezi miwili ijayo tunatarajia kujaza nafasi hizo, wakati ile ya Mwenyekiti wa taifa ambaye alijiuzulu itajazwa Agosti chama kitakapoitisha mkutano mkuu wa taifa,” amesema.

Akizungumzia kuhusu ushirikiano ulivyo baina ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Taslima alisema umoja huo ulishinikizwa na wananchi walioichoka CCM, hivyo walihitaji vyama hivyo viunganishe nguvu ili kushika dola.

“Lakini ni wazi kwamba sheria hairuhusu kuungana hivyo UKAWA tupo nje ya sheria lakini hatujavunja sheria, sasa tunafikiria kuanza kufanya mchakato wa kujijenga ndani ya misingi ya sheria kwa chaguzi zijazo,” amesema Taslima.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF, Sheweji Mketo amesema ushindi wa majimbo 10 walioupata unatokana na tathimini ambayo waliifanya mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.

“Baada ya uchaguzi ule kupita tulifanya CUF tulifanya tathimini ambapo tulibaini kwamba kuna majimbo 54 ambayo CCM licha ya wananchi kuichoka, lakini ilishinda kwa sababu kulikuwa na wagombea wengi wa vyama vya upinzani hali iliyosababisha kushindwa suluhisho lilikuwa ni kuungana,” amesema .

Ne-Yo Ametua Bongo Tayari Kwa Kutoa Burudani Tamasha La Jembeka

$
0
0
jembeka

Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Marekani, Shaffer Chimere Smith maarufu kwa jina la NE-YO amewasili jana usiku katika uwanja wa ndege wa kimtaifa wa Julius Nyerere (JNIA) tayari kwa kutoa burudani ya aina yake katika tamasha kubwa la “Jembeka Festival” litakalofanyika kesho tarehe 21 May jijini Mwanza. Mara baada ya kuwasili msanii huyo alisema alipelekwa katika hotel ya Hyatt Regency ambako yeye na timu yake nzima wamefikia na baadaye alijumuika na waalikwa wachache katika “Meet & Greet Party”

Akizungumza mara baada ya NE-YO kuwasili hotelini hapo Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema “tumefurahi sana kuwa na NE-YO hapa Tanzania na tunataka kuhakikisha kwamba tunawapatia wateja wetu burudani ya Tamasha la Jembeka Festival 2016 limeandaliwa na kampuni ya Jembe chini ya udhamini mkuu wa kampuni ya mawasiliano nchini Vodacom Tanzania litafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba. Vodacom Tanzania imedhamini ujio wa mwanamuziki huyu ili kuwapatia burudani ya kimataifa wateja wake na watanzania wote kwa ujumla. NE-YO ambaye ataimba steji moja na wanamuziki wa Tanzania wakiwemo Fid Q, Juma Nature, Mr Blue na wengine wengi, sambamba nao pia atakuwepo mwanamuziki nyota wa Afrika Mashariki, Diamond Platnumz. Kumbuka wawili hawa wako katika matayarisho ya ngoma yao ambapo Diamond amemshirikisha NE-YO na kwa mujibu wa Diamond Platnumz watatambulisha wimbo huo hapo kesho katika tamasha la “Jembeka Festival”


Mkurugenzi wa Vodacom pia aliwahimiza wapenda burudani wote kununua tiketi zao mapema kujiandaa na tamasha kubwa la aina yake hapo kesho. Wateja wa Vodacom wanaweza kununua tiketi kuhudhuria tamasha hili kubwa kupitia M-Pesa kwa kufuata hatua zifuatazo.

1. Piga *150*00# chagua 4 LIPA KWA M-PESA

2. Chagua 3 CHAGUA KWENYE ORODHA

3. Chagua 2 MANUNUZI

4. Chagua 3 JEMBEKA FESTIVAL

5. Weka namba ya kumbukumbu – 200200

6. Weka kiasi

7. Weka PIN yako ya M-PESA

8. Bonyesha 1 kuthibitisha.

Tukutane Jembeka Festival


Unaweza kufahamu zaidi kuhusu mtandao wa 4G na maeneo unapopatikana kwa kubofya HAPA 

Lady Jaydee Kumuanika Mpenzi wake Ambae ni Mrithi wa Gardner Leo!

$
0
0
Exclusive! Lejendari wa Bongo Fleva kwa zaidi ya miaka kumi na tano, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee au Jide’, anatarajia kumuanika mrithi wa aliyekuwa mumewe, Mtangazaji wa Kituo cha Radio CloudsFM, Gardner G. Habash ndani ya saa 24, Ijumaa lina data kamili.

HABARI ZA KUAMINIKA
Kwa mujibu wa habari za kuaminika zilizothibitishwa na uongozi wa staa huyo, Jide atamtambulisha mchumba wake huyo kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa Mlimani City leo, Dar ambapo pia atafanya shoo ya saa tatu mfululizo, inayokwenda kwa jina la Naamka Tena.
“Itakuwa ‘sapraizi’ kwa mashabiki wote wa Jide ambapo sapraizi hii itaendana na shoo ya kihistoria ya Naamka Tena atakayoipiga kwa saa tatu akiwa na bendi yake (Lady Jaydee and The Band),” alisema mmoja wa viongozi wanaomsimamia ambaye hakutaka kutajwa gazetini.


JIDE ALIPOTOKEA
Jide alifunga ndoa na Gardner Mei 14, 2005 ambapo waliishi na kufanikiwa kuwa na mali mbalimbali ikiwemo ujenzi wa nyumba, Ukumbi wa Nyumbani Lounge na Bendi ya Machozi

FIGISUGISU NA GARDNER
Mvutano wa wawili hao ulidaiwa kuanzia kwa Jide aliyeamua kuomba talaka kwa kile kilichosemekana kuwa Gardner alipata kazi ya kutangaza redio moja nchini Kenya hivyo kama angeenda huko wakati ni meneja wake, angeshindwa kuwa naye huku pia figisufigisu nyingine nyingi zikijitokeza kama kubadilisha jina la Ukumbi wa Nyumbani Lounge na kuwa M.O.G na mambo mengine ikiwepo kusalitiana na kupigana.

WAFIKISHANA MAHAKAMANI
Baada ya mvutano wa muda mrefu, wawili hao walifikia hatua ya kufikishana katika Mahakama ya Mwanzo ya Manzese jijini Dar, miezi michache iliyopita na mahakama kuamua kuvunja rasmi ndoa yao ya Kikristo na kila mmoja kupewa hati yake ya talaka.

Chanzo: Global Publishers

Breaking News: Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Waziri Wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga Baada Ya Kuingia Bungeni Akiwa Amelewa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016.

Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kufuatia kitendo cha Mheshimiwa Charles Kitwanga kuingia bungeni na kujibu swali linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

20 Mei, 2016

Waziri Mkuu Afafanua Kuhusu Kutenguliwa Kwa Uteuzi Wa Waziri Kitwanga

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa akiwa kazini.

“Zipo sheria za utumishi ambazo mtumishi hatakiwi kunywa pombe na wala hapaswi kulewa akiwa kazini… mtumishi anapaswa kuwa na akili timamu inayokuwezesha kufanya kazi za Serikali,” alisema.

Ametoa ufafanuzi leo usiku (Ijumaa, Mei 20, 2016) wakati akijibu swali la mwandishi wa TBC1 aliyetaka kujua kama taarifa zilizoenea kuhusu kutenguliwa kwa Waziri huyo ni za kweli.

“Ni kweli Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016 baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi. Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake leo asubuhi,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amesema kuna swali aliloulizwa ambalo hakulijibu vizuri na kwamba swali hilo litapaswa kurudiwa kuulizwa baada ya wabunge kuomba muongozo wa swali hilo.

IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU,
S L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, MEI 20, 2016

Picha: A-Z Shoo ya Lady Jay Dee Mlimani City usiku wa kuamkia leo

$
0
0


JAY DEE NAAMKA TENA M CITY (2)JAY DEE NAAMKA TENA M CITY (3)JAY DEE NAAMKA TENA M CITY (4)JAY DEE NAAMKA TENA M CITY (5)JAY DEE NAAMKA TENA M CITY (6)JAY DEE NAAMKA TENA M CITY (7)JAY DEE NAAMKA TENA M CITY (8)JAY DEE NAAMKA TENA M CITY (9)JAY DEE NAAMKA TENA M CITY (10)JAY DEE NAAMKA TENA M CITY (11)JAY DEE NAAMKA TENA M CITY (12)JAY DEE NAAMKA TENA M CITY (13)
JAY DEE NAAMKA TENA M CITY (1)
Malkia wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee usiku huu amefunika vilivyo katika shoo yake ya Nasimama Tena iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City.
Staa huyo akiwa na vijana wake wamepiga shoo kali ya Live iliyochukua saa tatu na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki walioshindwa kujizuia kukaa kwenye viti vyao na kunyanyuka mara kwa mara kwenda stejini kucheza nyimbo mbalimbali za malkia huyo.
Shoo hiyo imehudhuriwa na mastaa kibao wa Bongo Fleva na Bongo Movies wakiwemo Alikiba, Idrisa Sultan, Wema Sepetu, Elizabeth Michael na wengineo kibao.
Usikose kuangalia Global TV Online kuona video za matukio yote yaliyojiri.
Picha: Clarence Mulisa, Gabriel Ng’osha na Rishard Bukos / GPL

Magazeti Ya Leo Jumamosi ya May 21, 2016

Maoni ya Zitto Kabwe baada ya Rais Magufuli Kumfuta kazi Waziri Charles Kitwanga

$
0
0
Habari kubwa iliyoteka vyombo mbalimbali vya habari jana usiku ni habari ya Rais Magufuli Kumfuta kazi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga
Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ametumia ukurasa wake wa facebook kuandika mtazamo wake baada ya Rais Magufuli kufanya maamuzi hayo .

“Uamuzi wa Rais kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani unatuma ujumbe mmoja – hataki mchezo. Rais amethibitisha kuwa anao uwezo wa kutumbua hata aliowateua. Ni maamuzi muhimu sana kwa Kiongozi wa aina yake. Wale vijana waliokuwa wanatumwa kumtetea wasimame kumtetea. Rais kaonyesha Uongozi ‘ no nonsense “

Video ya dakika 7 ikimuonyesha Waziri Kitwanga akijibu swali huku amelewa Bungeni

$
0
0
Rais  wa Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania Dr. John P. Magufuli jana  alitengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Charles Kitwanga  kufuatia kitendo cha waziri huyo kuingia bungeni na kujibu swali linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.

==>Hapa chini kuna Video ya dakika 7 ikimuonyesha Waziri huyo  akijibu swali huku amelewa
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>