Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akutana Na Balozi Wa Tanzania Nchini Uingereza, Dkt. Asha- Rose Migiro

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  na Balozi wa Tanzania  nchini Uingereza, Dkt. Asha – Rose  Migiro kabla ya mazungumzo yao  Ofisini kwake jijini Dar es salaam  Mei 17, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt. Asha – Rose Migiro  ofisini kwake jijini Dar es salaam Mei 17, 2016.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Idris Sultan Amwandikia Wema Sepetu Ujumbe Mzito

$
0
0


Uhusiano wao umepitia misukosuko mingi ikiwemo kuachana mara kadhaa lakini Idris Sultan na Wema Sepetu hawajalikatia tamaa pendo lao.

Ni muda mrefu tangu Idris aandike kitu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu penzi lake na Wema baada ya kudai wameamua kuuweka uhusiano wao private kwa sasa. Lakini sasa mshindi huyo wa Big Brother Africa ameshare ujumbe mahsusi kwa mpenzi wake huyo.

“I am proud to say the mistakes we have made have not only made us stronger but better, faster, wiser, love too strong, stronger than any of us,” Idris ameandika kwenye picha ya Wema aliyoiweka Instagram.

“We ni kasumbufuuu, unasusasusa, wivu ndo usiseme, kugombana hadi kulia but in the end of the day i will open my arms na utajileta mwenyewe utaniangalia usoni and tell me “I hate you” and lay on my chest. I will smile and say “I love you too”. We have gone through heaven and hell and now you’re my bestfriend, family, wifey, lover you’re my cherry . #WolfQueen.”

Hivi karibuni wawili hao waliingia kwenye matatizo makubwa baada ya video inayomuonesha Wema akimbusu mwanaume mwingine kusambaa mtandaoni. Idris alikiri kuumizwa na jambo hilo.

David Kafulila Afunguka Haya Baada ya Kushindwa Kesi yake leo

$
0
0
David (NCCR Mageuzi) Kafulila kayaongea haya Baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kutoa maamuzi ya Kesi ya kupinga Matokeo ya uchaguzi aliyokuwa Ameifunguwa na hivyo kumpa ushindi Hasna Mwilima( CCM).

Wema, Petit ndani ya bifu

$
0
0
Imevuja! Urafi ki wa muda mrefu wa muigizaji nyota, Wema Sepetu na mshika kamera wake, Petit Man umeingia dosari baada ya kudaiwa kuwa wawili hao wako ndani ya bifu, Risasi Mchanganyiko linakujuza.
 
Chanzo makini kilisema kuwa Wema na Petit ambao hapo awali walikuwa wakiambatana kama kumbikumbi, kila kona walipoonekana, hivi sasa ni kama paka na panya kwani hakuna mawasiliano kati yao.

 “Wema na Petit hali ya hewa imechafuka, kwa sasa hawaongei kabisa kwa sababu Muna ambaye ni rafiki yao wote anadaiwa kumwambia maneno yaliyomkasirisha madam kuhusu mpigapicha huyo na kusababisha bifu hilo kali,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kupata ubuyu huo, gazeti hili liliwatafuta wahusika na wa kwanza kupatikana alikuwa Petit Man, aliyekiri kuchafuka kwa hali ya hewa.

“Unajua mimi na Wema nipo naye kwa miaka tisa sasa na ni kama familia moja, hivyo tatizo lililopo kati yetu litaisha tu na kumalizwa kifamilia kwa hiyo watu wasilivalie sana njuga,” alisema. Kwa upande wake Muna ambaye ni rafi ki wa wote wawili, alisema anasikia watu wakizungumza kuhusu kuwagombanisha Petit na Wema, kitu ambacho alidai siyo kweli, kwani hawezi kuwagombanisha watu ambao ni kama ndugu na kwamba yupo tayari kusawazisha matatizo kati yao badala ya kuchochea.


 “Mimi kwa kweli nawashangaa watu wanaosambaza hayo maneno ni kwa vile tu hawajui, mimi siwezi kuwagombanisha wale ni familia moja, waligombana kwa ishu zao wenyewe, sihusiki nazo na mara nyingi ninachofanya kama wana tatizo huwaweka sawa ili waendelee na uhusiano mzuri na si kuwagombanisha,” alisema Muna. Lakini jitihada za gazeti hili kupata kauli ya Wema zilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa hadi linaingia mitamboni.

Kigogo amjengea mjengo Vai wa Ukweli

$
0
0
Licha ya madai kuwa soko la fi lamu Bongo limeshuka na hivyo kutokuwa na faida kwa wasanii, muigizaji Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ anadaiwa kujengewa nyumba na kigogo anayetajwa kuwa ni mfanyabiashara, maeneo ya Mbezi-Msumi, jijini Dar.


 Chanzo cha uhakika kililiambia gazeti hili kwamba Vai wa Ukweli tangu awe na kigogo huyo maisha yake yamebadilika kwani muda mwingi anakuwa bize na kusimamia ujenzi wa nyumba yake hiyo ambayo hivi sasa imefi kia usawa na madirisha.

 “Vai yuko vizuri sana sasa hivi, maana muda mwingi anakuwa kwenye nyumba yake hiyo akiwasimamia mafundi kwa hiyo zile tabia za kupiga misele kwenye viwanja mbalimbali vya starehe siku hizi zimepungua.

 “Kuna habari kwamba anajengewa na kigogo ambaye ni mfanyabiashara mkubwa wa madini hapa mjini maana si unajua fi lamu hazilipi na yeye mwenyewe hana kazi nyingine ya maana anayofanya,?” kilisema chanzo hicho.

 Baada ya kupata habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Vai wa Ukweli na kumuuliza kuhusu ishu hiyo, ambapo alijitetea kama ifuatavyo; “Jamani ni kweli ninajenga lakini sijengewi na mtu yeyote, watu waache umbeya, najenga kwa hela yangu mwenyewe ambayo nimeipata kwenye fi lamu na nyingine kwenye biashara zangu nyingine.”

 Hata hivyo, licha ya gazeti hili kutaka kufahamu kuhusu ‘biashara zake zingine’ ni zipi, muigizaji huyo alipotezea bila kutoa ufafanuzi.

CHANZO: GPL

Jacqueline Wolper: Nampenda sana Hamonize mpaka kufa, A-Z ya mapenzi yao ipo hapa

$
0
0


Ama kweli penzi ni kikohozi, kulificha huwezi. Baada ya usiri mzito kutawala, hatimaye imebainika kuwa The Big Boss wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ndiye ‘aliyeinjinia’ penzi jipya mjini la muigizaji Jacqueline Wolper na kijana anayekuja kwa kasi kwenye Bongo Fleva, Rajabu Abdulhan ‘Harmonize’. 

RISASI LILIANZA KUTONYWA
 Awali, gazeti hili lilitonywa kuhusu penzi hilo jipya na chanzo chake makini na kueleza namna ambavyo Diamond alivyokuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha Hamonize ambaye ni memba wa WCB ‘anamng’oa’ Wolper. “Diamond ndiye aliyesimamia mchakato mzima. Katumia kila mbinu kuhakikisha Wolper anaingia kwenye himaya ya mdogo wake. Nafikiri pia atakuwa ameangalia na suala zima la kibiashara, muziki sasa hivi unataka msanii azungumzwe,” kilisema chanzo hicho.
 


DOGO NDIYE ALIANZA KUSUMBUA 
“Hamonize ndiye aliyeanza kuvutiwa na Wolper. Akamwelezea Diamond hisia zake, kama unavyojua tena Diamond si mtu wa kuremba, fasta tu akaweka mambo sawa. Kila kitu kikaenda kwenye mstari,” kilisema chanzo chetu. 

MKONGO HANA CHAKE 
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kutokana na Diamond kumwaga ‘sumu’ za kutosha na Wolper kuingia penzini ‘mzimamzima’ ndani ya muda mfupi, Mkongo aliyekuwa anammiliki mrembo huyo hana tena chake kwa sasa. “Aaah! Mkongo hana chake tena kwa sasa. Wolper hasikii wala haoni. Amechanganyikiwa na penzi la Hamonize kiasi ambacho hataki kusikia habari ya mwanaume mwingine yeyote,” kilisema chanzo hicho.

 MAMBO HADHARANI MITANDAONI 
Mara baada ya chanzo hicho kumwaga ubuyu huo, wakati Risasi Mchanganyiko likiendelea kufanya uchunguzi wake, ghafla likakumbana na video ya wawili hao kupitia mtandao wa kijamii wa ‘Snap Chat’ ambayo ilimuonesha Wolper akiwa ‘hajiwezi’ kwenye gari akiimbiwa wimbo wa Number One wa Diamond na Hamonize aliyekuwa akiendesha gari hiyo. 

WOLPER AJILIPUA 
Bila kupoteza muda, Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Wolper ambaye bila hiyana alieleza jinsi gani alivyofika ‘Kigoma, mwisho wa reli’ kwa Hamonize ambapo alimmwagia sifa bwa’mdogo huyo kwa kudai hajawahi kupenda kama alivyompenda staa huyo anayetamba na wimbo wa Bado. 

“Tena mimi naona kuwa sio mpenzi nambatiza jina la mume kabisa, maana nampenda mpaka kufa kuna wakati sijielewi ni mapenzi ya aina gani haya jamani na ninajuta kwa nini sikuingia huku mapema mpaka nikaanza kuhangaika kwa matapeli wa mapenzi. 

ACHOMOA KUHUSU DIAMOND KUHUSIKA 
“Hahaha siyo Diamond bwana aliyetuunganisha. Unajua mimi nilikuwa napata ujumbe kutoka kwa
marafiki zangu wa karibu kuwa Harmo ananipenda lakini nikawa bado sijaamua kuingia kwenye mapenzi, na hata tulivyoanza rasmi alikamilisha furaha yake kwani alifanikiwa kufunguka mwenyewe, nikamuelewa,” alisema Wolper. 


AMFUNGUKIA MKONGO 
Alipoulizwa kuhusu mpenzi wake Mkongo aliyekuwa akifahamika na wengi hususan baada ya kuzagaa kwa picha zinazomuonesha akivalishwa naye pete ya uchumba, Wolper alisema huko ameshapita, alidanganywa vya kutosha: “Nilikuwa nadanganywa sana, kumbe nilikuwa na mtu ambaye tayari ana mke wake hivyo sikuwa na budi zaidi ya kulivua pendo kwake. 

AZIDI KUJILIPUA
Kama hiyo haitoshi, Wolper alizidi kufunguka kuwa hatosikia la mtu kuhusu Hamonize, watakuwa pamoja kwa maisha ya tabu na raha kwani ndiye mtu ameweza kumponya vidonda vya Mkongo kwa haraka sana hivyo hatohangaika tena. “Sasa hivi sitojali chochote kwa kweli kwa maana Hamonize ndiyo ameweza kuponya vidonda vyangu kwa haraka sana nitakuwa naye katika hali yoyote shida na raha tutasonga tu,” alisema Wolper. 

HARMONIZE HUYU HAPA 
Risasi lilimvutia waya Hamonize ili kuweza kumsikia naye anazungumza nini kuhusu kukabidhiwa moyo na Wolper, aling’aka na kumuachia swali mwanahabari kisha kukata simu. “Kwani mmeshawasiliana na Wolper?” Alipopigiwa tena, alijibu: “Mbona amesema hajaongea na nyinyi?” 

DIAMOND JE? Jitihada za kumpata Diamond ili aweze kuzungumzia penzi hilo jipya na namna alivyohusika kuunganisha ‘mambo’ hazikuzaa matunda baada ya kupigiwa simu saa 7, 7:45, 8:15, 9 na saa 10 jioni juzi Jumatatu lakini muda wote ilionekana imezimwa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya May 18, 2016

Bavicha Walaani Hotuba ya Godbless Lema Kuzuiwa Bungeni........Wataka Waziri Kitwanga Ajiuzulu na Akigoma Awajibishwe

$
0
0

Wakati uchunguzi wa kampuni ya Lugumi inayodaiwa kushindwa kutekeleza mradi wa utambuzi wa vidole kwenye vituo vya polisi ukiendelea, Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga kujiuzulu wadhifa wake kupisha uchunguzi huo.

Limesema haiwezekani waziri anayetajwa kuhusika katika sakata hilo kuendelea na kazi huku Jeshi la Polisi linalodaiwa kutapeliwa na kampuni hiyo likiwa chini ya wizara yake.

Hata hivyo, waziri huyo amewajibu vijana hao wa upinzani kwa kusema hawezi kubishana na watoto na hayo waliyoyatoa ni mawazo yao binafsi wana haki ya kuyasema.

“Nimeshasema mara nyingi, siwezi kuzungumza tena kuhusu haya mambo. Wao kama wamesema waache waseme,” alisema.

Baraza hilo lililoibuka na hoja tatu jana, limesema kama waziri huyo atagoma kujiuzulu kupisha uchunguzi unaofanywa na kamati ndogo ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Rais John Magufuli anapaswa kumwajibisha ingawa suala hilo ni gumu kutokana na uswahiba uliopo kati ya kiongozi huyo mkuu wa nchi na Kitwanga.

Kampuni ya Lugumi ilibainika kutotimiza matakwa ya mkataba wake baada ya kufunga mashine 14 tu kati ya 108 zilizotakiwa kufungwa, licha ya kulipwa zaidi ya asilimia 90 ya fedha kwa mujibu wa mkataba ambazo ni Sh37 bilioni.

Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2013/14 ndiyo iliyofichua udhaifu huo na baadaye Bunge kuanza uchunguzi baada ya kutoridhishwa na maelezo ya Wizara ya Mambo ya Ndani na polisi kuhusu mkataba huo.

Kitwanga anahusishwa na Lugumi kupitia kampuni ya Infosys anayodaiwa kuwa ni mmoja wa wanahisa. Infosys ambayo imekanusha kuhusika katika sakata hilo, imedaiwa kuwa iliisaidia kampuni ya Lugumi kupata vifaa kutoka kampuni ya Dell ya Marekani ili viweze kufungwa kwenye vituo vya polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita alisema: “Hotuba ya upinzani inaeleza kuwa Lugumi inamilikiwa na Kitwanga na ana ubia hilo siyo siri. Kilichoelezwa kama kingesomwa bungeni kingemfanya apoteze uhalali wa kuwa waziri na tunajua Magufuli hawezi kumfanya chochote maana ni maswahiba.

“Hotuba ile pia ilimtaja Rais ila cha ajabu upinzani wakaambiwa wafute maneno ‘rais’. Rais Magufuli ameshindwa kuitumbua Lugumi na kwa kilichotokea bungeni suala hilo haliguswi.”

Alisema Rais anapaswa kujibu hoja zilizotolewa na wapinzani kuhusu Lugumi na kubainisha kuwa kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza kampuni hiyo haiwezi kutenda haki wakati Kitwanga akiendelea kuwa waziri.

Katibu mwenezi wa baraza hilo, Edward Sembeye alisema: “Katika ripoti ya CAG ameeleza juu ya ununuzi wa ile feri kuwa ni mbovu na haifanyi kazi hivi hili siyo jipu?

Kuhusu suala la Jaji Mkuu, Mwita alisema kitendo cha kuisifia Sheria ya Mtandao alipokuwa London, Uingereza hivi karibuni si kizuri kwa maelezo kuwa kazi ya majaji ni kutafsiri misingi ya kikatiba: “Tunamtaka afute kauli hii na aseme sheria hiyo imetungwa itumike lakini uzuri na ubaya wake hapaswi kuusema maana ni kama anatoa hukumu kabla watuhumiwa hawajafikishwa mahakamani.”

YANGA NA SAGRADA ESPERANCA KIPYENGA KUPULIZWA 'TISA JUU YA ALAMA' LEO

$
0
0


Na Prince Akbar, DUNDO
YANGA SC inajitupa kwenye Uwanja wa Sagrada Esperanca mjini Dundo, Angola jioni ya leo kumenyana wenyeji, Sagrada Esperanca katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza Saa 9:00 Alasiri kwa saa za Angola na Saa 11:00 jioni kwa Saa za Tanzania.

Yanga iliwasili Dundo usiku wa juzi baada ya safari ya kutwa nzima wakipitia Luanda, ambako waliunganisha ndege nyingine kwa saa mbili kuja mjini wa wenyeji wao, Sagrada Esperanca.

Yanga iliyofikia katika hoteli ya bora zaidi mjini humo, Diamante, Yanga itahitaji sare ili kuingia hatua ya makundi, baada ya awali kushinda 2-0, mabao ya Simon Msuva na Matheo Anthony wiki iliyopita Dar es Salaam.
Kocha Mholanzi wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema kwamba ana imani kurejea kwa wachezaji wake wawili Wazimbabwe, kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Donaldo Ngoma kutaiogezea nguvu timu yake. 

Wawili hao waliukosa mchezo wa kwanza kutokana na kuwa wanatumikia adhabu ya kadi za njano walizopewa kwenye mechi mfululizo dhidi ya Al Ahly ya Misri mwezi uliopita Dar es Salaan na Cairo, Yanga ikitolewa kwa jumla ya mabao 3-2, baada ya sare ya 1-1 nyumbani na kufungwa 2-0 ugenini.
Mechi hiyo itachezeshwa na marefa wa Madagascar, Hamada el Moussa Nampiandraza atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Velomanana Ferdinand Jinoro na Jean Thierry Djaonirina.

Yanga imeangukia katika kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Shirikisho, baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2, ikilazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam na kufungwa 2-1 Alexandria.

Yanga ilianza vizuri tu kwa kuzitoa Cercle de Joachim ya Mauritius kwa jumla ya mabao 3-0, ikishinda 1-0 ugenini na 2-0 nyumbani kabla ya kuitoa na APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 2-1 Kigali na kutoa sare ya 1-1 Dar es Salaam.

Kwa upande wao, Sagrada Esperanca katika Raundi ya Awali waliitoa Ajax Cape Town ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya kufungwa 2-1 ugenini na kushinda 2-0 nyumbani. Katika Raundi ya kwanza wakaitoa LD Maputo ya Msumbiji kwa jumla ya mabao 2-1 ikishinda 1-0 nyumbani na kutoa sare ya 1-1 ugenini na kwenda hatua ya 16 Bora, ambako waliitoa V. Club Mokanda ya Kongo kwa jumla ya mabao 4-1 wakishinda 2-1 ugenini na 2-0 nyumbani.
Vikosi vya leo vinatarajiwa kuwa; Yanga; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Deus Kaseke.

Sagrada Esperanca; Yuri Jose Tavazes, Roadro Juan da Semero, Dennis Conha Morais, Asenio Cabungula, Antonio da Silva Oliveira, Ntaku Zabakaka, Manuel Paulo Joao, Alentua Tangala Rolli, Osvaldochitumba Palana, Manuel Sallo Conha na Antonio Kasule. 

Upinzani Wamtega Rais Magufuli....Watumia Njia Mbadala Bungeni Kukumbushia Uuzwaji wa Nyumba za Serikali, Wadai MV Dar es Salaam Ni Jipu Lililoiva

$
0
0
Kambi ya Upinzani imelizidi maarifa  Bunge na kurejesha sakata la kuuzwa nyumba za Serikali ambalo juzi lilisababisha kiti cha Spika kuagiza yaondolewe maneno yanayomtaja Rais katika hotuba ya maoni mbadala.

Juzi, Kamati ya Kanuni za Bunge ilihariri hotuba ya msemaji wa kambi ya upinzani wa Wizara ya Mambo ya Ndani, ikiondoa maneno yanayomtaja Rais John Magufuli na badala yake kuweka neno Serikali kwenye sakata la uuzwaji nyumba za Serikali.

Kamati hiyo pia iliondoa suala la mkataba wa Jeshi la Polisi na kampuni ya Lugumi Enterprises, rushwa, mauaji ya wanasiasa, mwenendo wa Rais na Bunge kulinda wahalifu, jambo lililomfanya msemaji wa kambi hiyo, Godbless Lema kukataa kusoma hotuba yake.

Lakini jana katika hotuba ya kambi ya upinzani kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, mbunge wa Vunjo, James Mbatia alilirejesha sakata hilo akieleza kuwa ni muda sahihi kwa Rais John Magufuli kurekebisha kasoro zilizojitokeza wakati akiwa waziri ili kurejesha imani katika jamii.

Mbali na sakata hilo, pia Mbatia alizungumzia sakata la kivuko cha Mv Dar es Salaam ambacho kinatakiwa kifanye safari kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo, akikielezea kuwa “ni jipu ambalo limeiva kwa viwango vyote na sasa linatakiwa litumbuliwe mara moja”.

Suala la Mv Dar es Salaam liliungwa mkono na Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Zitto alisema kuwa hoja ya kivuko hicho lazima ichukuliwe hatua ili iaminike kuwa kuna nia ya dhati ya kupambana na ufisadi nchini.

“Naona suala hili linakwepwakwepwa, hivyo litolewe maamuzi,” alisema Zitto.

Pia mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini alisema suala la Mv Dar es Salaam kuwa iko chini ya kiwango, liliwahi kusemwa na mbunge wa upinzani lakini Serikali ikakataa.

Hata hivyo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) amesema ukweli katika ripoti yake. “Hili suala inabidi liangaliwe kwa kuwa kuna watu wanahitaji kutumbuliwa hivyo hao watu waangaliwe,” alisema Selasini.

Akisoma hotuba ya maoni mbadala ya kambi ya upinzani, Mbatia alisema wakala wa majengo nchini ndiye muhusika mkuu katika kuhakikisha nyumba za Serikali zinakuwa katika hali nzuri kwa watumishi wa Serikali kuishi.

“Katika muktadha huo, kambi ya upinzania inalikumbusha Bunge kwamba kati ya mwaka 2002 mpaka 2004 Serikali iliuza nyumba 7,921 na mpaka mwaka 2008 ilikuwa imejenga nyumba 650 tu,” alisema Mbatia.

Alisema katika biashara hiyo ya kuuza nyumba zilizokuwa mali ya Tamisemi, Serikali ilipata Sh252 milioni lakini sasa inahitaji kusaka zaidi ya mara mbili ya kiasi hicho kujenga nyumba za fidia.

Mbatia alisema Serikali ingetumia Sh677.6 milioni kujenga nyumba mpya ili zirejeshwe Tamisemi.

“Kwa vile hata wale waliouziwa nyumba hizo, kuna taarifa kati yao wapo walioziuza na kujipatia faida kubwa kinyume na mikataba ya mauzo hayo, kambi ya upinzani inapendekeza wanyang’anywe nyumba hizo kwa kukiuka mikataba na malengo ya mauzo.”

Mbatia alisema kumbukumbu rasmi za Bunge zinaonyesha Serikali ilitoa taarifa kuwa kamati iliundwa kuchunguza mchakato wa mauzo ya nyumba hizo na ilitarajiwa kumaliza kazi Februari 2007, lakini hadi leo hakuna taarifa iliyotolewa na Serikali na kuitaka Serikali ya Awamu ya Tano izirejeshe.

Akinukuu kumbukumbu rasmi za Bunge za Aprili 25, 2008 wakati wa kikao cha 18 cha Mkutano wa 11, Mbatia alisema baada ya mjadala mkubwa wa hoja binafsi iliyowasilishwa na mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro, Bunge kwa kauli moja lilipitisha azimio kuwa nyumba hizo zirejeshwe serikalini.

“Bunge linaazimia kwamba Serikali ifanye yafuatayo: Itekeleze mara moja bila kusita, agizo la Rais kurejesha nyumba zilizouzwa kinyume cha utaratibu na kwa watu ambao hawakuwa watumishi wa Serikali wakati huo na vilevile nyumba ambazo hazikupaswa kuuzwa kama zile zilizopo kwenye maeneo ya utawala wa Serikali,” alisema akinukuu azimio hilo.

Mbatia aliitaka Serikali itafsiri kaulimbiu ya “hapa kazi tu” kwa kuelekeza azimio hilo, akisema Kikwete alikosa uthubutu wa kusimamia msimamo wake.

“Tunajua uuzwaji huo ulisimamiwa na wizara aliyokuwa akiiongoza yeye (Rais Magufuli) na kuna uwezekano mkubwa kwamba alisimamia maamuzi ambayo hakuwa na uwezo wa kuyakiuka,” alisema Mbatia.

“Sasa ni muda sahihi Rais Magufuli kurekebisha kasoro alizozisimamia katika mchakato huo ili kurejesha imani katika jamii.”

Kivuko cha Bagamoyo
Kuhusu kivuko cha Bagamoyo, Mbatia alisema kilinunuliwa na Temesa chini ya uongozi wa Waziri wa Ujenzi wa Serikali ya Awamu ya Nne ambaye ndiye Rais wa sasa.

Mbatia alisema kwa mujibu wa ripoti ya CAG katika hesabu za Serikali Kuu za mwaka ulioishia Juni 30, 2015 iliyotolewa Machi 2016, alibaini ununuzi wa boti ‘feki’ na mbovu uliofanywa na Temesa na kugharimu dola 4,980,000 za Marekani (sawa na Sh7.9 bilioni).

Alisema CAG alibaini masuala makuu mawili ambayo ni kasi ya kivuko hicho ni tofauti na kasi iliyotakiwa kuwapo na pia cheti cha kukikubali kivuko hicho kilikuwa kinyume na Kanuni ya 247 ya Sheria ya Manunuzi ya Umma.

“Tabibu wa kutumbua jipu hili yuko wapi? Au msemo usemao kuwa ‘mganga hajigangi’ unatumika hapa?” alihoji.

Juzi jioni hali kama hiyo ya kuzungumza masuala yaliyozuiwa na Kamati ya Kanuni za Bunge, ilijitokeza wakati wabunge wakijadili Hotuba ya Makadirio na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

Akichangia mjadala huo, Lema alianza tena kuzungumzia suala la Lugumi, akisema kabla ya kuandika hotuba hiyo alikaa pamoja na Waziri Charles Kitwanga wakila ugali nyumbani kwake na kumtaka amwambie ni mambo gani ayajumuishe kwenye hotuba yake ambayo yangeisaidia nchi.

“Haya mambo ambayo mimi nimeyaandika, nimeyajadili nyumbani kwake tukiwa tunakula ugali. Na nakwambia mimi ni mara ya pili kuingia bungeni. Ninazijua siasa za Bunge.

"Ninakuomba mheshimiwa uniambie mimi kama kambi ya upinzani ninaweza kuzungumza mambo gani ambayo Serikali haiwezi kuja nayo direct. Usiponiambia mimi nitakunyookea na nitataka majibu.

“Waheshimiwa wabunge, nimeuliza swali ambalo nimeambiwa na kamati niliondoe, kwamba hivi kamati ya Bunge inapotembelea kote huko kutafuta sakata hili la Lugumi, CAG anashindwa kutwambiwa kama mkataba ule ulikuwa thamani yake ya fedha na vifaa ni OK au ni no, anashindwa kujua?” alihoji Lema huku akishangiliwa.

Hii Ndio Hotuba ya Mbunge Godbless Lema iliyokataliwa Bungeni..Isome Hapa

$
0
0
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KATIKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MHE. GODBLESS JONATHAN LEMA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA HIYO, KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017

Inatolewa chini ya Kanuni ya 99 (9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la Aprili, 2016.

______________________


1.0 UTANGULIZI


Mheshimiwa Spika, Kwa dhati namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema , nawashukuru pia Mke wangu Neema, Watoto wangu Allbless, Brilliant, Terrence na Precious Mawazo, pamoja na Wazazi wangu kwani wamekuwa msaada mkubwa sana kwangu katika shughuli zangu zote kwa maombi na sala . Kwani kufanya kazi ya Siasa za Mabadiliko Tanzania ni kazi ngumu na iliyojaa mateso, vitisho na hata kifo, lakini kwa ajili ya siku zao njema za baadae, ninapaswa kuendelea na kuvumilia katika kazi hii na wajibu huu muhimu ili kutafuta mwanga mpya wa Taifa letu katika siku za usoni.


Mheshimiwa Spika, Namshukuru Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Mhe. Freeman Aikael Mbowe kwa busara, ujasiri na maamuzi yake katika kuamua mambo yenye mwelekeo chanya katika Chama chetu na Nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, Nawapongeza pia wale wote waliojiunga na Chama chetu na Ushirika wetu wa Ukawa katika mwaka ule wa Uchaguzi hasa katika hatua za mwisho, nampongeza Mhe. Edward Ngoyai Lowassa na mke wake Mama Regina Lowassa ambaye ni mfano wa kuigwa, Mhe. Fredrick Tulaway Sumaye ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Kamati kuu wa CHADEMA na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na wengine wengi kwa ujasiri na maamuzi mazito waliyofikia.


Mheshimiwa Spika, nina washukuru wananchi wa jimbo la Arusha Mjini kwa imani yao kubwa kwa Chama chetu na kwangu kwa kuweza kutupa madiwani 24 kati ya 25 na kufanikisha kuongoza Halmashauri ya Jiji la Arusha.


2.0 HALI YA USALAMA NA AMANI YA NCHI YETU


2.1 MAADILI YA FAMILIA


Mheshimiwa Spika, Taifa lolote Duniani msingi wake ni familia , hivyo njia sahihi ya Taifa kuwa na usalama wa kweli katika Jamii ni muhimu Serikali ikajua kuwa Jamii ni Familia, kuongelea hali ya usalama na amani ya Nchi yetu bila kuongelea maadili ya familia zetu ni kupotosha fikra zetu.


Mheshimiwa Spika, ukweli ni kwamba familia yenye maadili, wajibu na inayomcha Mungu ni jamii bora itakayozalisha Raia wema wenye wajibu na tija kwa Taifa, hatuwezi kuwa na Nchi yenye nidhamu na ustawi pasipo kuwa na familia zenye wajibu katika malezi .


Mheshimiwa Spika, Wazazi wengi leo tukiwemo Waheshimiwa Wabunge na Jamii ya kada mbali mbali tunafikiri kuwa tumekosa nafasi ya kukaa na familia zetu, na hivyo tumeamua ku- out source malezi ya Watoto wetu na familia zetu, hivyo watoto wengi wanao kuwa katika karne hii, ni watoto wanaolelewa ama na wasaidizi wa shughuli zetu majumbani, mitandao ya jamii, Shule, na makundi mengine tusiyoyajua, ambayo hayajui mila, utamaduni, desturi na maadili ya Jamii zetu.


Mheshimiwa Spika, hii ni hatari kwa usalama wa Taifa, unapokuwa na Taifa lenye familia ambazo hazina malezi mazuri ni ukweli usiopingika kuwa, ni lazima utegemee kizazi kisichokuwa na mwelekeo wa kimaadili. Hivyo ni muhimu Wazazi na Taifa likajua wajibu wa usalama na amani ya Nchi unaanzia kwenye malezi bora katika ngazi ya familia .


3.0 AMANI NI TUNDA LA HAKI.


Mheshimiwa Spika, hali ya Amani katika Nchi yetu iko katika mashaka makubwa na kwa bahati mbaya Serikali inaufahamu ukweli ila kwa sababu inazozijua yenyewe imeamua kupuuza ukweli huo wa kushindwa kutofautisha kati ya amani na utulivu katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika , Taifa hili lina utulivu unaosabishwa na hofu inayojengwa kwa mabavu na silaha na sio amani, kuna mateso makubwa wanayoyapata wananchi wa Taifa hili kila siku, umasikini, njaa, ukandamizwaji, ubaguzi, uonevu, udhalilishwaji na mateso ya jinsi mbali mbali kutokana na kukosa uongozi unaojali maisha ya Watu.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni baada ya uchambuzi na tathimini ya “Hali ya Usalama na Amani ya Nchi yetu” kabla wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015, tumebaini kuwa nadharia na mwenendo wa demokrasia ya vyama vingi hapa nchini iliwekwa kando, na badala yake sura nzima ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015, uligeuka kuwa “Military Operation” yaani “Operesheni ya Kijeshi” kwa kisingizio cha kulinda amani.


Mheshimiwa Spika, tarehe 25 Oktoba 2015 siku ambayo wananchi walipiga kura, Katika Jengo la Mlimani City, CCM na timu yao ya Kampeni ya Rais John Pombe Magufuli walifanya zoezi la kuhesabu kura za mawakala wao kutoka vituo mbalimbali nchini yaani “Parallel Voter Tabulation” bila kubughudhiwa na Jeshi la Polisi, wakati huo huo UKAWA wakifanya zoezi kama hilo la “Parallel Voter Tabulation” katika vituo vitatu vya ICT ndani ya Jiji la Dar es Salaam, na vituo vyote hivyo kuvamiwa na Jeshi la Polisi ambalo lilizuia zoezi hilo kufanyika, kuvunja na kuharibu baadhi ya vifaa vilivyotumika kama vile laptop, kuwanyang’anya simu na laptops vijana zaidi ya 160 waliokuwa wanajitolea kufanya zoezi hilo, kuwasweka rumande kwa muda wa siku tatu mfululizo bila kuwafungulia mashitaka, kuwatishia kuwa wanatuhumiwa kwa makosa ya kufanya biashara haramu ya kusafirisha binadamu (human trafficking) na kuwafungulia mashitaka ambayo hayana msingi.


Mheshimiwa Spika, mnyonge anayelia moyoni kwa huzuni ya kuonewa ni hatari kwa usalama wa Nchi na Dunia , vikundi vingi vya uhalifu Duniani kwa asilimia kubwa vimesababishwa na utawala wa kibabe, uonevu na ukandamizwaji usiovumilika na huko ndiko tunakoelekea kama Taifa.


Mheshimiwa Spika , matendo mabaya haya yaliofanyika wakati wa uchaguzi mkuu uliopita Zanzibar na Tanzania bara ni ishara ya watawala kuelekeza Nchi yetu katika mapigano ya sisi kwa sisi katika siku za usoni .


Mheshimiwa Spika, unapokuwa na Jamii inayoamini kuwa mfumo wa demokrasia hauwezi kuwapa wananchi viongozi wanaowataka , maana yake ni dhahiri kwamba unaanza kuifundisha jamii hiyo kufikiri njia mbadala ya mabadilko katika Nchi .


Mheshimiwa Spika , kuwa na Tume ya Uchaguzi inayotiliwa mashaka na Jamii ni hatari kwa usalama wa Nchi yetu. Ni muhimu sasa kama Taifa kutafakari uwepo wa katiba ya wananchi na Tume Huru ya Uchaguzi itakayorudisha imani ya Wananchi katika Uchaguzi wa Kidemokrasia.


Mheshimiwa Spika , Mungu adhihakiwi apandacho Mtu ndicho avunacho, utulivu mnaouona Zanzibar na kwingine kokote kule kuliko na ukandamizaji ni nafsi zinazojadili mwelekeo mpya wa maisha yao katika utawala wa Nchi yao.


Mheshimiwa Spika , Zanzibar mmeshinda uchaguzi kwa hila na sio kwa haki, wekeni kumbu kumbu maneno ya Kambi Rasmi ya Upinzani leo kuwa, ipo siku Zanzibar itakuwa ni sehemu ngumu ya kuishi Binadamu kama hamtachukua hatua sasa ya kurekebisha mlichokifanya Zanzibar na Tanzania Bara katika uchaguzi uliopita .


Mheshimiwa Spika , kwani tunajiuliza maswali mengi , je tutarudi tena kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 kwa njia ya demokrasia ? au tutafakari njia nyingine mbadala, kwani demokrasia katika Taifa hili imethibitisha kuwa tunaweza kushinda uchaguzi lakini tukaporwa matokeo na tusitangazwe kuwa washindi.





4.0 MAUAJI YA VIONGOZI WA KISIASA.


Mheshimiwa Spika , Viongozi wa kisiasa hasa wale wa Upinzani wamekuwa wakiishi kwa kubaguliwa na kwa mateso makubwa sana hata wengine kuuwawa kwa sababu ya kazi na wajibu wao katika siasa na jamii.


Mheshimiwa Spika , nikianza kueleza wale wote waliopatwa na madhara ya vipigo , kusingiziwa kesi , na wengine kuuwawa , ninaamini kwamba hotuba hii haitoshi isipokuwa labda tuandike vitabu.


Mheshimiwa Spika ,Rafiki na ndugu yetu mpendwa Alphonce Chemu Mawazo, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita aliuawa kinyama kule Katoro- Busanda - Geita , mchana , hadharani , tena karibu na kituo cha Polisi.


Mheshimiwa Spika, sisi tulilia sana na kuhudhunika sana hata mpaka leo, na tulipohitaji kumzika kwa heshima anayositahili kama rafiki na Kiongozi wetu hatukuruhusiwa na Polisi , tulipigwa sana mabomu na wengine kama Mwenyekiti wetu wa Vijana Taifa Patrobas Katambi walipewa kesi ya kushambulia jambo ambalo ni la kutunga na uzushi.


Mheshimiwa Spika , Mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo ulizuiwa kuagwa kwa ubabe na Jeshi la Polisi bila sababu za msingi mpaka Mahakama ilipotoa haki ya mwili kuagwa kule jijini kwao Busanda Geita.


Mheshimiwa Spika, Marehemu Mawazo ameacha Binti yake mzuri na mwenye akili nyingi Precious akiwa darasa la nne, Baba yake ameuwawa si kwa sababu alikuwa mwizi , bali aliamini katika siasa tofauti na demokrasia kwa maslahi ya Taifa.

Mheshimiwa Spika, wakati mioyo yetu ikilia ndani kwa huzuni, kwa dhuluma, uonevu, ukandamizwaji, vipigo hata vifo vya marafiki zetu na ndugu zetu katika kazi zetu za siasa tunazofanya, nyie mnaona mambo haya ni ya kawaida.

Mheshimiwa Spika, hii ni hatari kwa usalama wa Taifa, kwani subira na uvumilivu vitakapoishiwa nguvu, kuna dalili ya mauaji ya ulipizaji visasi kuanza na itakapofika hapo usalama na amani ya Taifa letu utakuwa mashakani sana.


Mheshimiwa Spika, Kama Rais Magufuli anaweza kuanzisha Mahakama ya Mafisadi ambao wapo hai, Kambi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa majawabu kwa nini mpaka dakika hii bado tume ya kimahakama ya kuchunguza vifo tata (Judicial Commission of Inquiry) haijawahi kuundwa, ili kutoa haki kwa Watanzania. Japo kuwa ilikuwa ni ahadi ya Waziri Mkuu katika katika Serikali ya awamu ya nne.




5.0 MIKATABA TATA YA JESHI LA POLISI.


5.1 Mkataba tata wa Lugumi na Jeshi la Polisi.


Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali , ilihoji utekelezaji wa mkataba wenye utata wa vifaa vya Mfumo wa Alama za Vidole (AFIS) ulioingiwa kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Kampuni ya Lugumi Enterprises.


Mheshimiwa Spika, kumetokea majibishano na malumbano mengi kwenye vyombo vya habari na miongoni mwa wabunge wa Bunge lako tukufu, hasa pale walipoanza kuhoji utekelezaji wa mkataba huo hasa kuhoji juu endapo vifaa hivyo vinafanya kazi.

Mheshimiwa Spika, Kufuatia majibishano na malumbano yaliyojaa utata ambao lazima upatiwe majibu yasiyo na shaka yoyote, hivyo basi, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka Serikali kutoa majibu ya moja kwa moja bila kupepesa macho. Tunataka Maswali yafuatayo yajibiwe hapa bungeni;


Mheshimiwa Spika,

1) Kwa kuwa mikataba ya serikali kwa mujibu wa sheria lazima ufuate sheria za manunuzi na kuthibitishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Je, Utaratibu huu ulifuatwa?

2) Je Mkataba huu wa LUGUMI ENTERPRISES na JESHI LA POLISI umetekelezwa ama haukutelezwa, na kama ulitekelezwa ni kwa kiwango gani, na ikiwa kulikua na tatizo la utekelezaji, Je, Jeshi la Polisi lilichukua hatua zipi?

3) Je, ni kampuni ngapi ambazo zinahusika na hatua za utekelezaji wa Mkataba kati ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi, kwa kuwa kampuni ya INFOSYS ambayo mmoja wa wamiliki wake ni Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga inatajwa kufunga vifaa hivyo (AFIS).

4) Ni kwanini C.A.G katika ukaguzi wake hakuhoji kuhusu uhalali na ulinganishi wa thamani ya pesa ya manunuzi na faida ya vifaa hivyo?

5) Kampuni ya INFOSYS (inayomilikiwa na Mhe. Kitwanga) imedai kulipwa na Jeshi la Polisi, takribani Dolla za Marekani 74,000, Je fedha hizi Kampuni ya Mhe. Kitwanga ililipwa kwa kazi ipi iliyofanya na Jeshi la Polisi?

6) Ni kwanini mpaka sasa , Rais Magufili hajachukua hatua dhidi Said Lugumi, na aliyekuwa IGP Said Mwema / Emmanuel Nchimbi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na kuwasimamisha kazi wale wote ambao bado wako kazini juu ya mkataba tata wa Lugumi ?

7) Tunamtaka Rais , kutengua mara moja uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe na kumrudisha nchini mara moja , kwani alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Ndani na ni imani ya Kambi rasmi kuwa alijua mambo yote yanayoendelea ya mkataba wa Lugumi



Mheshimiwa Spika , Ni imani ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuwa Mhe.Waziri Charles Kitwanga, anazo taarifa za Mkataba huu na utekelezaji wake aidha kutoka kwenye Kampuni yake ambaye yeye ni Share holder ( Mbia ) ambayo ilifunga vifaa hivi au anazo taarifa ya utekelezaji wa Mkataba huu kutoka Jeshi la Polisi ambalo liko chini yake kwa kiwango chote kuhusu mambo yote ya Mkataba huu.


Mheshimiwa Spika, Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) , alinukuliwa na vyombo vya habari pale alipoulizwa kuhusu sakata la Lugumi na Mikataba yake na Jeshi la Polisi kutotekelezwa, alijibu majibu mafupi Katika gazeti la Raia Mwema la tarehe 27/04/2016 namnukuu “siyo kweli, watu wana ugomvi wao kibiashara, lakini nakueleza wazi kwamba, tembelea vituo vyote tulivyokubaliana, utakuta mashine zipo. Inawezekana zingine hazifanyi kazi kwa sababu ya kukosekana kwa internet” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, kulingana na maswali ambayo tumeuliza hapo juu na uchambuzi wetu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inashauri kama ifuatavyo;


Mheshimiwa Spika,

1. Kwa vile Waziri wa Mambo ya Ndani anahusika kwa karibu katika Mkataba huu kupitia Kampuni yake ya INFOSYS na vile vile Jeshi la Polisi liko chini yake , je ? haoni kuwa ni busara kwa yeye kujiuzulu ili kutoa nafasi ya Uchunguzi kuepusha mgongano wa maslahi ndani ya Jeshi la Polisi na kwenye Kampuni ambayo yeye ni mmoja wa wamiliki ?



Mheshimiwa Spika,

2. kwa vile inaonekana kupitia vyombo vya habari na kauli za viongozi mbali mbali kuwa upo uwezekano wa Polisi kuwa wametapeliwa na vifaa hivyo havijafungwa, Kambi ya Upinzani Bungeni inautaka uongozi wote wa juu wa Jeshi la Polisi kujiuzulu mara moja, kwani kama wao wameshindwa kujua ukweli wa vifaa vilivyofungwa kwenye vituo vyao vya Polisi ama vipo au havipo, watawezaje kuchunga na kulinda mali na usalama wa raia wengine?


Mheshimiwa Spika,

3. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inataka majibu yote yanayohusu Mkataba wa Lugumi na Jeshi la Polisi kuhusu utekelezaji wake uwekwe wazi hapa bungeni na wizara husika.


5.2 Sakata la Kuuzwa kwa ardhi ya Polisi Oysterbay


Mheshimiwa Spika, Sakata la Kuuzwa kwa ardhi ya Polisi Oysterbay limeleta mashaka makubwa ndani ya jamii na baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi, pamoja na Rais Magufuli kutilia mashaka jambo hili.


Mheshimiwa Spika, Kwa vile kuna ukakasi na mashaka ya rushwa, tunaliomba bunge liazimie na kuitaka Serikali kuleta mara moja mkataba huu na mingine yote yenye sura kama hii ndani ya Bunge lako tukufu, ili ipitiwe na kufanyiwa tathimini endapo mikataba hiyo ilifuata utaratibu na ina tija kwa Taifa na hii iwe ni kwa mikataba yote iliyofanyika wakati wa Serikali ya awamu ya nne ya Mh Jakaya Kikwete , pamoja na ule wa ununuzi wa boti

( Mv Dar es salaam ) uliofanywa wakati Rais wa sasa Mh Dr Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi.


Mheshimiwa Spika samba samba na hilo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka pia Serikali kuleta mikataba ya uuzwaji wa Nyumba za Serikali kazi ambayo aliisimamia Rais Magufuli mwenyewe wakati huo .


Mheshimiwa Spika , kwa vile Rais wa sasa alihusika kuuza nyumba za Serikali ni imani yetu kuwa Kambi rasmi ya Upinzani itapata ushirikiano wa kutosha juu ya utata wa mikataba hii tete ya uuzaji wa nyumba hizi.


6.0 RUSHWA, SURA YA SERIKALI NA BUNGE TISHIO LA HALI YA USALAMA.


6.1 Rushwa na Bunge kutumika kuwalinda wahalifu nchini


Mheshimiwa Spika , Mh Andrew Chenge (MB)ametuhumiwa na imethibitika hapa Bungeni na katika taasisi za Uchunguzi za Kimataifa (SFO) kuwa alihusika kwa karibu na kwa ufanisi katika sakata la kashfa ya ununuzi wa rada ya Taifa.


Mheshimiwa Spika , Mwandishi Andrew Feinstein , Colonel .U.S. Army (retired) katika Kitabu chake “ THE SHADOW WORLD - Inside the Global Arms Trade, katika ukurasa wa 188-196, amefanya uchambuzi wa kina jinsi Andrew Chenge alivyofanikiwa kukwapua fedha za Wananchi kiasi cha pesa za Kimarekani dolari 1.2 milioni kupitia Kampuni yake ya Franton Investment Ltd Jersey na Kampuni hii ya Andrew Chenge ikampa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dr. Idrissa Rashid pesa za Kimarekani dolari $600,000 kupitia Kampuni ya Gavana huyu inayojulikana kwa jina la Langley Investment Ltd.


Mheshimiwa Spika, Lakini kwenye utawala huu wa utumbuaji majipu, Andrew Chenge ni Mkiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkiti wa Kamati ya sheria ndogo, jambo hili lina sura ya dharau na fedhea kwa Bunge lako tukufu na kwa jamii.


Mheshimiwa Spika, Wako wengi wenye sura hizi za Mh Chenge na wengine ni Mawaziri ambao wamekuwa na kashfa mbali mbali kwenye Serikali iliyopita lakini wameonekana kwenye madaraka tena katika Serikali hii ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais aneyeamini katika utumbuaji majipu , wakati kuna majipu mengine asiyoweza kuyatumbua ndani ya baraza la Mawaziri.


Mheshimiwa Spika , Taifa linapokuwa na huzuni juu ya utawala unaopuuza na kudharau Wananchi , kwa vyovyote vile hali ya amani na usalama inakuwa mashakani na kuwatia moyo watumishi wengine wa Umma katika masuala yanayohusu ufisadi, rushwa na ubadhirifu kwamba sio mambo mabaya. Ndio maana imekuwa ni vigumu kukemea rushwa katika ngazi mbalimbali za utawala wa nchi hii ikiwemo Jeshi la Polisi.


6.2 Kuingiliwa kwa Uhuru wa Bunge na Mhimili wa Dola


Mheshimiwa Spika , tishio lingine la hali ya usalama Nchini ni Serikali kuingilia Uhuru wa Bunge , ni ajabu kubwa kwamba chombo kinachopanga matumizi ya fedha za Serikali ni Bunge , lakini kwa wakati huu tumeona Serikali ikiondoa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge kwa kisingizio cha kubana matumizi , kazi ambayo hata hivyo kama ingekuwa ni hoja basi jambo hilo lingefanywa na Bunge na sio Serikali.


Mheshimiwa Spika, Wananchi kupata habari na kujua wanachojadili wabunge wao ni hitaji la lazima la Kikatiba na sio hisani ya Serikali, malumbano yetu dhidi ya hoja mbali mbali ndani ya Bunge yalikuwa ni muhimu kwa ustawi wa usalama wa Nchi yetu.


Mheshimiwa Spika, Wananchi , walipotuona kupitia vyombo vya habari mbali mbali , tukilumbana juu ya maisha na maendeleo yao , jambo hili lilikuwa linasidia kupunguza tension na uchungu kwa jamii kwani walikuwa wanashuhudia tukipigana na kulumbana juu ya ustawi wa maisha yao , walipata matumaini waliposikia majibu ya Serikali hata kama yalikuwa ni uongo.


Mheshimiwa Spika , Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni inasikitishwa na jinsi Bunge letu linavyoendelea kukosa nguvu na kuingiliwa na mihimili mingine ya dola kwa kuelekezwa ni kipi cha kufanywa na kipi si cha kufanywa. Ni wazi sasa bila chenga kuwa Bunge hili limeingiliwa na dola na sasa ni Bunge kibogoyo jambo linalohatarisha usalama na amani ya nchi, kwa kuwa Dola sasa inaweza kufanya chochote na isionekane kukemewa na Bunge ambalo kazi yake ni kuisimamia Serikali, badala yake sasa hivi Serikali ndio inalisimamia Bunge.


Mheshimiwa Spika , kisingizio cha gharama kubwa za kurusha matangazo ni uongo mkubwa ambao hata shetani anaushangaa, kwani hata vyombo vingine vya habari vilivyokuwa vinarusha matangazo ya “live” kwa gharama zao navyo vimezuiwa sio na Serikali bali na uongozi wa Bunge uliodhibitiwa na Serikali ya Dkt. Magufuli.

6.3 Tabia ya Rais Magufuli na Usalama wa Nchi.


Mheshimiwa Spika, wakati Taifa letu linapita kwenye changamoto nyingi Kama vile ukosefu wa sukari, umeme, umasikini, mizigo kupungua bandarini , madini ya Tanzanite kuanguka bei na ubadhirifu uliokithiri katika mfumo wa utawala. Rais mwenyewe ameonekana kufuatilia na kufanyia kazi habari za kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa tabia hii ya Rais Magufuli, kama Taifa tunahitaji maombi haraka, kwani Rais ataumiza watu wengi sana kwa kufuatilia maneno ya mitaani kwa njia mbali mbali , kwani kwa madaraka aliyonayo Rais bila shaka ataumiza watu wengi. Mfano, Sakata la Mke wa Waziri Mahiga na Trafiki barabarani. Ni jambo dogo sana na la karaha kuona linazingatiwa na Rais .


Mheshimiwa Spika, haikuwa busara Rais kukemea familia ya Waziri wake mbele ya vyombo vya habari na kuagiza askari huyu kupandishwa cheo bila kujua historia ya utumishi wake .


Mheshimiwa Spika , kwa nini mambo haya ni muhimu kuyasema na kwa nini ni hatarishi kwa usalama wa Nchi, tulipoonza vikao vya Kamati za Bunge, vyombo vya habari vilimnukuu Rais akielezea mpango wake wa kuanza kurekodi Mawaziri wake wanaolalamika juu ya staili yake ya uongozi. Kwa hiyo leo ukienda kwenye ofisi za Mawaziri, unaona, hofu, mashaka, kutokujiamini, mambo yatakayo punguza ufanisi, ubunifu na uhuru katika utendaji wao, jambo linalopeleka Taifa kuzorota katika Nyanja zote kwa utumishi wa umma jambo ambalo ni hatari kwa Taifa.


7.0 UGOMVI KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI


Mheshimiwa Spika, Ugomvi kati ya Wakulima na Wafugaji ni tatizo kubwa na ambalo lisipotatuliwa kwa makini na haraka , Nchi yetu itaendelea kushuhudia mauaji kwa raia wake .


Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inashauri Serikali kutenga mara moja na kupima maeneo kwa ajili ya wakulima na wafugaji , tatizo hili haliwezi kutatuliwa kwa bunduki na mabomu ya machozi isipokuwa mipango maalumu ya upimaji ardhi na ushauri wa kitalamu juu ya ufugaji wa kisasa na ukulima wa kisasa unaweza kuwa njia ya kupunguza tatizo na kuliondoa kabisa.


Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya upinzani inaishauri Serikali kuanzisha mfumo wa mauzo ya wanyama kwa kuzingatia vipimo vya uzito na kuuza kwa mizani yaani kilogramu na si kuuza kwa kutazama mifugo kwa macho na kupanga bei. Kwa kufanya hivyo wafugaji watajali zaidi na kuona tija ya kuwa na mifugo michache na kuwanenepesha kuliko kuwa na mifugo mingi isiyo na afya.


8.0 HALI YA UHALIFU NCHINI


Mheshimiwa Spika, Hali ya Uhalifu nchini bado ni mbaya na kasi ya kupunguza uhalifu hairidhishi, taarifa za Takwimu za Hali ya Uhalifu Januari-Juni, 2015 zilizotolewa na ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi zimeonesha kuwa kuna ongezeko la asilimia 9.8 ya makosa ya jinai hapa nchini. Taarifa hiyo imeonesha kuwa matukio madogo ya makosa ya usalama barabarani yakiongezeka kwa asilimia 16.4 kutoka mwezi Januari – Juni, 2014 mpaka kufikia Januari – Juni, 2015.


Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kuwa mara zote ndani ya muda wote wa Bunge la 10, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilikuwa ikiishauri Serikali juu ya hatua mbalimbali za kuchukua dhidi ya matukio ya ajali za barabarani ambazo zinagharimu maisha ya wananchi wa Taifa hili ambao ni nguvu kazi inayopotea, na kuwaacha vijana wengi wakipoteza wazazi wao na kubaki mayatima. Taarifa za Takwimu za Hali ya Uhalifu Januari-Juni, 2015 zimebainisha kuwa “Jumla ya watu 1,849 walifariki kutokana na ajali za barabarani ikilinganishwa na watu 1,777 waliofariki Januari hadi Juni, 2014. Hili ni ongezeko wa watu 72 sawa na asilimia 4.1”.


Mheshimiwa Spika, Ubunifu pekee wa Serikali katika Jeshi la Polisi ilikuwa na kuwapatia mashine za EFD ili wasiendelee kufanya kazi ya kuhakikisha usalama barabarani na badala yake “kudandia” kazi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kukusanya mapato. Ni aibu kubwa sana kwa Jeshi letu la polisi kujisifia kwa ukusanyaji wa mapato kutokana na makosa ya barabarani badala ya kutoa taarifa za namna gani Jeshi hilo limepunguza uhalifu wa makosa ya barabarani. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro alikaririwa na vyombo vya habari akidai kuwa “Kikosi cha usalama barabarani kanda ya Dar es Salaam kimekusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.9 kama faini za makosa ya barabarani kuanzia Februari 1 hadi 22, mwaka huu”


Mheshimiwa Spika, Itoshe tu kusema kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haijaridhishwa na mbinu na weledi hafifu unaotumiwa na Serikali ndani ya Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu hapa nchini. Taarifa ya Hali ya UhalifuJanuari-Decemba, 2014 imeonesha ongezeko kubwa sana, (substantial increase) ya uhalifu nchini kwa asilimia 32.5, kutoka makosa milioni 1.2 mpaka makosa milioni 1.6.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaishauri Serikali kuzingatia ushauri wote uliotolewa na Kambi kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe maelezo ya kina juu ya mpango mkakati wa kupunguza kiwango cha uhalifu hapa nchini na kueleza ni kwa kiwango gani wanafanya kazi ya Usalama wa Raia na Mali zao.




9.0 UKOMESHAJI BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA NCHINI


Mheshimiwa Spika, Ifahamike kuwa kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita Kambi Ramsi ya Upinzani Bungeni, imekuwa ikiishauri Serikali juu ya hatua za kuchukua katika kukomesha matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.


Mheshimiwa Spika , ushauri wetu juu ya jambo hili nikuitaka Serikali ikatafute ushauri wetu wote wa huko nyuma katika hansard na kuuzingatia mara moja , kwa ajili ya kuokoa Taifa letu.





10.0 HALI ZA MAHABUSU NA WAFUNGWA MAGEREZANI

10.1 Kuondoa adhabu ya Kifo iliyo kinyume na Katiba ya Tanzania

Mheshimiwa Spika, Mwaka 2015, inakaridiwa kuwa watu 472 walipatikana na hatia na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa, kati ya hao wanaume ni 452 na wanawake 20, ambapo wafungwa 228 wanasubiria kunyongwa hadi wafe kwa mujibu wa sheria, na wafungwa 244 wanasubiria kusikilizwa kwa rufaa zao, hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya Haki za Binadamu (LHRC, 2015).

Mheshimiwa Spika, adhabu ya kifo inakiuka misingi ya Kikatiba, ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kuwa “Kila mtu anayo Haki ya Kuishi na kupata kutoka katika Jamii hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa katiba hii” Lakini pia hajaanza kutumiza masharti ya katiba yetu kwa kuwa bado hukumu za vifo zinatolewa. Hata hivyo bado Serikali ya Tanzania haijatia saini makubaliano ya sehemu ya pili ya mkataba wa International Convention on Civil and Political Rights wa mwaka 1966, ambapo Second Optional Protocol to the International Convention on Civil and Political Rights, ya mwaka 1989 ambayo inataka nchi wanachama kukomesha adhabu ya kifo.

Mheshimiwa Spika, inaishauri Serikali kusaini na kuridhia mkataba wa Second Optional Protocol of the International Covenant on Civil and Political Rights, ili kuilinda katiba yetu na kutimiza matakwa ya kikatiba ya kulinda uhai wa kila Mtanzania.

10.2 MSONGAMANO WA MAHABUSU NA WAFUNGWA MAGEREZANI.

Mheshimiwa Spika, Kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikiitaka Serikali kuchukua hatua ya kupunguza msongamano wa wafungwa na mahabusu Magerezaji sambamba na kuboresha lishe na huduma za afya kwa Wafungwa na Mahabusu.

Mheshimiwa Spika, Mwaka wa fedha 2015/2016, aliyekuwa Waziri wa mambo ya Ndani wakati huo, Mhe. Mathias Chikawe, alisema kuwa uwezo wa magereza yetu ni kubeba wafungwa 27,653, wakati mpaka kufikia mwaka 2015 mwezi machi magereza ilikuwa na wafungwa 33,027.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haijaridhishwa na hatua ambazo Serikali ilizichukua kwa mwaka wa fedha uliopita katika harakati za kupunguza msongamano wa magereza. Hatua za Parole, Msamaha wa Rais na Kifungo cha nje bado hazitoshi kwa kuwa hatua hizo zinalenga kupunguza msongamano bila kuangalia hali ya mazingira ya mahabusu na wafungwa wanaobakia ndani ya magereza. Tuliendelea kuisisitiza Serikali kuwa huduma za afya, uchakavu wa miundombinu ya vyoo na mabafu, na ufinyu wa vyumba vya kulala, ukosefu wa matandiko na magodoro pamoja na lishe kwa mahabusu na wafungwa zimeendelea kuwa duni.

Mheshimiwa Spika, Mwaka wa fedha 2015/2016, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iliishauri Serikali kuwa ili kupunguza msongamano wa mahabusu magerezani iandae utaratibu kwa Jeshi la Polisi kuwa kabla halijawakamata watu na kuwaweka mahabusu basi uchunguzi wa kina ufanyike, tofauti na sasa ambapo mtu anayehisiwa tu kuwa ni mhalifu anaweza kuwekwa mahabusu na kukaa huko hadi miaka zaidi ya mitano na baadae kuambiwa kuwa hana hatia, huu ni uvunjaji wa haki za Binadamu.

Mheshimiwa Spika , hata hivyo sababu nyingine mojawapo inayofanya mahabusu kujaa katika magereza zetu , zinachangiwa na matumizi mabaya ya Sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai kifungu cha 91 ambacho kinampa mamlaka Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) kuondoa Shauri la jinai Mahakamani lakini kuondolewa kwa shauri hilo hakuzuii mamlaka kumshtaki tena kwa kosa lile lile mtuhumiwa.

Mheshimiwa Spika, Jeshi la Polisi wamekuwa wakitumia vibaya masharti ya kifungu hiki ambapo mara baada ya mtuhumiwa/watuhumiwa kuachiwa wamekuwa wakikamatwa tena na Jeshi la Polisi mara nyingi ikiwa katika maeneo ya Mahakama.

Mheshimiwa Spika, kambi rasmi ya upinzani Bungeni inashauri mbali na uwepo wa parole, na vifungo vya nje ni vema magereza zikaimarisha na kuwa kitengo maalumu cha wafungwa watakao fanya kazi za huduma za jamii na Kitengo cha mazingira na upandaji miti hasa kwa kifungo chini ya mwaka mmoja au na zaidi ili kunusuru uharibifu wa mazingira unaohatarisha Taifa letu kuwa jangwa . Kazi yao kubwa iwe kuhudumia idadi miti kwa kuipanda na kuitunza adhabu zao ziwe na manufaa kwa jamii na sura ya Taifa.

11.0 HATIMA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Mheshimiwa Spika, Katika hotuba yangu ya mwaka wa fedha 2015/16 nikiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, niiliitaka Serikalikutoa ukomo wa muda, ambapo kila raia wa Tanzania atapatiwa Kitambulisho chake cha Taifa na kuainisha gharama zilizotumika katika mchakato mzima wa kutengeneza vitambulisho vya Taifa.

Mheshimiwa Spika, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Bwana Dickson E. MAIMU, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kuanzia, tarehe 25 Januari, 2016 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu tarehe 26 Januari 2016. Katika taarifa ile ilibainika kuwa “Taarifa zilizomfikia Rais zinaonesha kuwa NIDA hadi sasa imetumia Sh.179.6 bilioni.”

Mheshimiwa Spika, Katika taarifa ile, Rais aliagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) wafanye ukaguzi maalum wa manunuzi yote yaliyofanywa na NIDA. Sasa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka Serikali kuliambia bunge hili tukufu kuwa ni lini inatarajia kuileta bungeni ripoti ya Ukaguzi Maalumu ulioagizwa kufanyika na Rais Magufuli, ili bunge sasa liweze kutimiza majukumu yake yaliyoanishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 63 ibara ndogo ya (2)

Mheshimiwa Spika, Ripoti hiyo ya uchunguzi maalumu wa NIDA itakapowasilishwa ndani ya Bunge hili, wabunge kwa niaba ya wananchi tutaweza kufahamu mbivu na mbichi na kujua hatma ya vitambulisho vya Taifa, hatma ambayo mpaka sasa Serikali imekosa majibu yake.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni pamoja na masuala mengine kuhusu ushauri tuliotoa katika vitambulisho vya Taifa, bado tunaona kuwa mfumo mzima wa kuwatambua Watanzania upo “shaghala bagara” kutokana na kuwepo kwa vitambulisho vya aina nyingi kama vile Leseni za Udereva na Kadi ya Mpiga kura, hivyo kulifanya Taifa kuingia hasara kubwa ya kutengeneza vitambulisho kwa watu wale wale. Huku ni kukosa ubunifu.

Mheshimiwa Spika, Gazeti la Mtanzania la tarehe 2 Machi 2016, liliripoti kuwa “mchakato wa utoaji wa vitambulisho vya Taifa unatarajiwa kuanza upya, kutokana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kukiri kuwapo kwa upungufu katika vitambulisho vya sasa.” Huu ni udhaifu mkubwa wa Serikali kukosa ubunifu, kitendo kinachopeleka hasara kwa Taifa bila watu kuwajibishwa.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa maelezo ya kina kuwa ni kwa sababu gani ilifanya uzembe mpaka vitambulisho vya Taifa vikaanza kutolewa huku kukiwa na udhaifu uliobainika baada ya zoezi la kuvigawa kuanza.

Mheshimiwa Spika, Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni tunaishauri Serikali kuunganisha mfumo wa vitambulisho vya Taifa na vitambulisho vya aina nyingine kama vile leseni za udereva, Utambulisho wa Namba ya Mlipa Kodi, Vitambulisho vya Bima za Afya, Hati za Kusafiria na Kadi za Mpiga kura ili kuwa na “National Database” ambayo inajumuisha taarifa zote za Watanzania, jambo ambalo litaepusha upotevu wa kumbukumbu na kurahisisha michakato ya kutoza kodi na kuongeza ufanisi katika ufuatiliaji wa wapi wananchi wapo, wanafanya nini na wanaweza vipi kuisaida Serikali kutimiza majukumu yake kama vile ulipaji kodi kwa wakati na ufuatiliaji wa ulinzi wa Raia wetu wanasafiri nje ya nchi.

11.1 UKIUKWAJI WA TARATIBU ZA KUSITISHA AJIRA ZA WAFANYAKAZI 597 WA NIDA

Mheshimiwa Spika, Tarehe 7 Machi 2016, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa alisitisha ajira za vijana 597 waliokuwa wanafanya kazi kwa mkataba, bila kufuata taratibu za kusitisha ajira. Watumishi hao hawadai kurudishwa kazini, lakini wanachodai ni kulipwa stahiki zao kwa mujibu wa mkataba wao wa ajira.

Mheshimiwa Spika, waliokuwa watumishi wa NIDA waliositishiwa mikataba yao ya ajira wana madai ya zaidi ya bilioni 2.3. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA alitoa tangazo tarehe 11 April 2016, katika gazeti la Mwananchi ukurasa wa 16 kuwa NIDA itaanza kufanya malipo ya madai yao kuanzia Jumatano tarehe 13 April 2016 saa 3.00 asubuhi, lakini Mheshimiwa Spika, Taarifa zilizoifikia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ni kuwa mpaka dakika hii ninavyoongea hakuna fedha zozote zilizolipwa kwa waliokuwa waajiriwa hao 597 wa NIDA waliositishiwa ajira zao.

Mheshimiwa Spika, huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu wa kumfukuza mtumishi kinyume cha sheria kiholela na hatimaye kutomlipa stahiki zake ipasavyo jambo ambalo ni kinyume na misingi ya utawala bora.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina taarifa na imebaini kuwa mamlaka hiyo haikuwahi kupeleka makato ya wafanyakazi katika Mfuko wa Kijamii wa GEPF kuanzia mwezi Julai 2015 mpaka tarehe 7 Machi 2016 ambapo ajira zilisitishwa.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kulieleza bunge hili sababu za Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA kushindwa kulipa madai ya wafanyakazi wapatao 597 walioachishwa kazi tangu mwezi Disemba 2015 ambapo hawakulipwa stahiki zao kwa miezi mitatu mfululizo tangu mpaka ilipofika tarehe 7 Machi 2016 ambapo ajira zao zilisitishwa rasmi.




12.0 UMUHIMU WA JESHI LA POLISI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAO.


Mheshimiwa Spika, Serikali yoyote makini Duniani inaweza kujenga ustawi wa maisha ya raia wake kwa kutambua umuhimu wa Ulinzi na Usalama katika Taifa. Lakini kuhitaji ulinzi kwa walinzi ambao huwapi ulinzi wa maisha yao kama mishahara bora na masilahi mengine ni sawa na kumeza dawa ya tumbo kwa kutumia konyagi.


Mheshimiwa Spika, Watumishi wote wa umma wanahitaji ungalifu bora kutoka Serikalini , lakini watumishi wetu wanaolinda amani na usalama wa raia wanahitaji upendeleo kwa kiwango fulani zaidi , kwani kazi ya ulinzi ni kujitoa maisha kwa ajili ya wengine .


Mheshimiwa Spika, mishahara ya Polisi na posho zao zote bado ni ni ndogo sana , na ndio maana kuondoa rushwa ndani ya jeshi la Polisi kwa kuendesha warsha , semina elekezi , kutoa miongozo , na vipeperushi ni jambo ambalo haliwezi kufanikiwa , katika sala ambayo Bwana Yesu aliwafundisha wanafunzi wake, kuna mahali sala hiyo inasema na nukuu “ USITUTIE MAJARIBUNI BALI UTUOKOE NA YULE MWOVU “


Mheshimiwa Spika , rushwa ndani ya Jeshi la Polisi imejengwa na utawala wa Serikali ambao umeshindwa kujali masilahi bora ya Walinzi wetu hawa ikiwa ni pamoja na Jeshi la Magereza , kwa hiyo Serikali ndiyo inayowatia Askari wetu majaribuni katika suala la kuomba na kupokea rushwa kwa kuwalipa fedha kidogo sana kwa ajili ya maisha yao .


Mheshimiwa Spika, hakuna Polisi wala Askari magereza anayeweza kujenga nyumba kwa mshahara na marupurupu anayopokea , wanaishi maisha magumu na ya taabu sana , ndio maana wakiona kosa wanaona fedha badala ya uwajibikaji na na kutenda haki.


Mheshimiwa Spika, Serikali inapaswa kuwalipa walinzi wetu hawa vizuri ili kufanya kazi ya Jeshi la Polisi au Jeshi la Magereza / Zima moto na Uokoaji iwe ni kazi ya fahari kuanzia kwenye familia kama zilivyo kazi nyingine .


12.1 JESHI LA ZIMA MOTO NA UOKOAJI


Mheshimiwa Spika, Katika hotuba ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wakati wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2011/2012 pamoja na mambo mengine alipendekeza kuwa kutokana na kuongezeka kwa majengo makubwa nchini ambayo ni chanzo cha mapato serikali ianzishe mamlaka ya kuyasimamia (Real Estate Regulatory Authority) kwa ajili ya kuhakikisha kuwa inapata mapato na kusimamia uzingatiaji wa miundo mbinu na kanuni za kiusalama katika ujenzi.

Mheshimiwa Spika, Aidha pamoja na masuala ya mapato tunaitaka serikali katika ihakikishe kuwa inatoa maelekezo kwa taasisi na watu binafsi ambao wanamiliki majengo au wanatarajia kuwa na majengo kuhakikisha kuwa wanajenga na kuweka visima kwa ajili ya maji ambayo yatatumika kama kutakuwa na janga la moto katika majengo yao au maeneo yao Hii itasaidia sana kuondoa tatizo la magari ya zima moto kuishiwa maji kila linapotokea janga la moto na hili ni kwa mujibu wa sheria ni bora sheria hii ikazingatiwa na kufuatiliwa.


Mheshimiwa Spika , Kambi rasmi ya upinzani Bungeni inalitaka na kulishauri Jeshi la Uokoaji na zimamoto kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani kuzipa mamlaka Halmashauri za Miji , Manispaa na Majiji uwezo wa kusimamia kikamilifu maeneo ya makazi na kuhakikisha kuwa kila nyumba inayoishi binadamu au anakofanyia kazi inakuwa na uwezo na miundo mbinu ya kuzima moto na kila nyumba iwe ni lazima kuwa na Mtungi wa kuzimia moto ( Fire extinguisher ) na kazi hizi ziachwe kwa Halmashauri za Miji , Manispaa , Majiji husika kwa kushirikiana na Jeshi la zima moto na uokoaji

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika kipindi chote cha Bunge la 10, tumekuwa tukiishauri Serikali kufanya maboresho makubwa ya Jeshi la Zima Mto na Uokoaji kwa kulipangia bajeti ya kutosha kwa ajili ya miradi ya Maendeleo ili jeshi hilo liendeshwe kisasa zaidi katika kukabiliana na majanga ya ajali za moto na matukio ya uokoaji.

Mheshimiwa Spika, Hata hizo bilioni 53 zilizoombwa na Jeshi la Zima Moto na Uokoaji inaonesha kiasi gani Wizara yenyewe na Jeshi kwa ujumla halijatambua umuhimu wa kitengo hiki. Jeshi la Zima moto linahitaji Helkopta za kisasa zenye uwezo wa kuzima moto. Jeshi hili la zima moto linahitaji kuwa na uwezo wa kuzima moto kwenye misitu mikubwa kunapokuwa na janga la moto, milima inapopata majanga ya moto kama mlima Kilimanjaro, Jeshi hili linapaswa kuwa na uwezo wa kuzima moto, vile vile Jeshi linatakiwa kuwa na uwezo wa kuzima moto katika maeneo ya nchi ambayo magari hayawezi kufika kwa urahisi.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaona umuhimu wa Jeshi hili utathibitika baada ya Chama Cha Mapinduzi kuondoka madarakani, ili uongozi wenye maono mapana uje na kutazama Jeshi hili katika sura na mfano tulioeleza hapo juu. Bilioni 53 walizoomba inapaswa kuwa bajeti ya Jeshi la Zima moto ya kufanya dhifa ya nyama choma yaani (barbecue)


13.0 UHAMIAJI HARAMU NA USALAMA KATIKA MIPAKA YA NCHI


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeendelea kuishauri Serikali kuhusu usalama wa mipaka ya nchi yetu kuwa ipo hatarini dhidi ya matukio ya uhalifu wa kimataifa na matukio ya ugaidi, kutokana na ongezeko la wahamiaji haramu ambao wanaingia nchini kupitia mipaka yetu na wanakamatwa wakiwa ndani ya nchi tayari wakisafirishwa kwenda kwenye mataifa mengine kusini mwa jangwa la Sahara.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni tunaishauri Serikali kutumia mbinu za kisasa ili kuzuia wahamiaji haramu wanaotumia nchi yetu kama “transit gate” ya kuhamia kwenye mataifa mengine hasa kutoka mataifa ya Kaskazini mwa Afrika kwenda kusini mwaka bara la Afrika.


Mheshimiwa Spika , vile vile Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali iangalie namna ya kuanzisha ofisi za uhamiaji kwenye maeneo muhimu yanayotumika kama matobo kwa wahamiaji haramu .


14.0 HITIMISHO


Mheshimiwa Spika, Asilimia zaidi ya 50% ya wabunge waliomo ndani ya Bunge hili wengi ni wapya maana yake ni kwamba, michakato ya kura za maoni katika vyama vya siasa ni sehemu ya kubadilisha mwanasiasa na pia mfumo wa demokrasia unatoa uhuru wa jinsi hiyo katika uchaguzi.


Mheshimiwa Spika, Martin Niemoller alikua mchungaji wakati wa utawala wa Kinazi Ujerumani akiwa mstari wa mbele kupinga utawala wa mabavu , alichukuliwa mateka katika kambi (concentration camp) na alisema maneno yafuatayo;

“First they came for the Socialists, and I did not speak out—
Because I was not a Socialist.

Then they came for the Trade Unionists, and I did not speak out—
Because I was not a Trade Unionist.

Then they came for the Jews, and I did not speak out—
Because I was not a Jew.

Then they came for me—and there was no one left to speak for me.”

Mheshimiwa Spika, ni muhimu wabunge, viongozi wa vyama na serikali na watu wote wajue tunapoishauri Serikali juu ya sheria na sera za nchi ni busara na upendo wa hali ya juu kujua kwamba uamuzi tunaoufanya humu ndani leo ni kwa faida na maslahi ya watoto wetu na watoto wa watoto wetu. Kwa bahati mbaya itikadi za vyama vyetu zimenunua utashi, ukweli na utu wetu.


Mheshimiwa Spika, Rais Magufuli ana jambo muhimu la kufanya ili athibitishe anachokiita huruma yake kwa masikini nalo ni kuwapa masikini katiba yao (Rasimu ya Warioba) iliyobeba maoni waliyoyatoa katika Tume ya Warioba kabla ya kuchakachuliwa na Bunge la Katiba.

Mheshimiwa Spika, ni namma moja tu inaweza kumsaidia Rais kukabiliana na ufisadi , ubadhirifu wa mali za umma na mengineyo yenye sura hizi , na namna hiyo ni kuacha uhuru wa Bunge katika kazi zake za kuisimamia Serikali .


Mheshimiwa Spika, James Freeman Clarke alisema maneno haya “The difference between a politician and a statesman is that a politician thinks about the next election while the Statesman think about the next generation.”Sisi tunafikiria nini?


Mheshimiwa spika, tatizo la wanasiasa wengi wa Taifa hili kila wanapomaliza uchaguzi papo hapo, ndipo wanaanza kufikiria uchaguzi unaofuata. Ndio maana mawazo ya vikao vya vyama vyetu (Party Caucus) yanakuwa muhimu kuliko msingi wa siku za usoni za nchi yetu. Hili nalo ni tishio kubwa la usalama wa Taifa letu. Kwani wanaopaswa kushauri, kuelekeza na kusimamia wameukataa wajibu wao bila aibu.


Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kusema, zawadi pekee mbunge yoyote anayoweza akatoa kwa wazazi wake, watoto wake, familia yake na nchi yake ni yeye kuwa na uwezo wa kusimamia ukweli, demokrasia, utu na haki kwa gharama yoyote ile.
………………………………………..

Godbless Jonathan Lema (Mb)

MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI NA

WAZIRI KIVULI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tarehe 16 Mei, 2016

Vannesa Mdee, Shilole kimenuka kwenye mtandao wa Instagram

$
0
0
Headline zinachukuliwa na Warembo kudoka Kiwanda cha Bongoflevani na hii ni baada ya May 17 2016 Shilole kupost picha kwenye Account yake Instagram ambayo wengi wametafsiri ni dongo kwa msanii mwenzake Vanessa Mdee, May 18 2016 Vanessa Mdee amezichukua headline kwa Kupost picha ya Shilole na kuandika caption inayosomeka hivi.
Nikupe KICKII ujulikane au sio? Kila siku twanyamazaga ndiyo mtugaragaze. Sit the f**k down. Mimi sio uliowazoea. P.s: You ain’t worth this post inashushwa sasa hivi #MessageSent‘>>>Vanessa MdeIMG-20160518-WA0015
Post hiyo ya juu ni baada ya hizi post mbili za Shilole kwenye account yake ya instagram
shishi
IMG-20160518-WA0016

KIKOSI KAMILI CHA YANGA HIKI HAPA TAYARI KUWAVAA WAANGOLA

$
0
0
 
KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA ESPERANCA KATIKA MJI WA DUNDO NCHINI ANGOLA. MECHI ITACHEZWA SAA 9 KWA ANGOLA NA 11, SAA ZA AFRIKA MASHARIKI.


1. Deogratius Munishi 
2. Juma Abdul 
3. Oscar Joshua 
4. Vicente Bossou 
5. Nadir Haroub 
6. Mbuyu Twite 
7. Simon Msuva 
8. Thabani Kamusoko 
9. Amisi Tambwe 
10. Donald Ngoma 
11. Haruna Niyonzima 

BENCHI:
1. Ally Mustafa 
2. Mwinyi Haji 
3. Kelvin Yondani 
4. Deus Kaseke 
5. Geofrey Mwashiuya 
6. Mateo Anthony 

7. Paul Nonga

Bima za Magari, Pikipiki zinapatikana Accept Insurance

$
0
0
ACCEPT INSURANCE BROKERS
Linda maisha ya watu Uwapendao na Accept Insurance,
TUNATOA HUDUMA ZA BIMA ZIFUATAZO:
Bima za Magari / Pikipiki nk
• Bima ndogo (Third Party
• Bima kubwa (Comprehensive
Bima ya Afya (Health Insurance)
Bima ya Moto (Fire Insurance)
Bima ya Migodi (Mining Insurance)
Bima ya Ajali Binafsi (Personal Accident)
Kinga ya Umma (Public Liability)
Majanga Yote (All Risks)
Bima ya Pesa (Money Insurance)
Bima ya Wizi (Theft or Burglary)
Bima ya Makandarasi (Contractors Insurance)
Bima za Wafanyakazi (Workmen’s Compesation)
Bima ya Usafirishaji (Goods in Transit)
Bima ya Safari (Travel Insurance)
Bima ya Usafirishaji wa Majini (Marine Insurance)
Cold Room Insurance - Flower Farm/Irrigation
Bima ya Hatifungani (Bond Insurance)
Kwa kukata bima ya mali zako.
Karibu ofisini kwetu Morocco,Dar es Salaam
Kwa mawasiliano zaidi piga namba 0679 640 648
0687 640 649
Website/Tovuti: www.acceptinsurance.co.tz
Email: info@acceptinsurance.co.tz

WATEJA WA VODACOM WAENDELEA KUBADILISHA KADI ZAO ZA SIMU KUFURAHIA MTANDAO WA 4G

$
0
0



Wateja kampuni ya mawasiliano nchini Vodacom Tanzania wameendelea kubadilisha kadi zao za simu katika maduka ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam ili kufurahia mtandao wenye kasi ya 4G. Vodacom Tanzania ilizindua kampeni hiyo Jumatano ya wiki jana inayokwenda kwa kauli mbiu ya HAPA KASI TU ina lengo la kuwapatia wateja wake huduma ya intaneti yenye kasi zaidi ikijulikana pia kama LTE.


Mbali na kuzindua mtandao wa 4G LTE kampuni hiyo pia imeimarisha mtandao wa 3G ambao unapatikana katika maeneo yote ya miji mikubwa nchini Tanzania. Akizungumza katika uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia alisema “huduma hii ni mpya kabisa yenye kasi ya ukweli na kwa kuanzia itatolewa kwa wateja wote wa Vodacom walio jijini Dar es Salaam na kisha itasambazwa mikoani ili kufikia Watanzania wengi zaidi”


Jinsi ya kubadilisha kadi ya simu kwenda 4G

Mteja wa Vodacom Tanzania atatakiwa kuwa na simu yenye uwezo wa kupata mtandao wa 4G LTE kisha atatembelea duka la Vodacom lililo karibu nae na atapatiwa kadi ya 4G BURE. Mbali na kupata kadi hiyo bila malipo mteja pia atazawadiwa kifurushi cha intaneti chenye 4GB BURE. Baada ya kubadilisha sim card yako, fanya speed tes
kupitia http://speedof.me/ kushuhudia spidi ya hatari na #Vodacom4G #hapakasitu

Unaweza kufahamu zaidi kuhusu mtandao wa 4G na maeneo unapopatikana kwa kubofya HAPA 

Matumizi ya Mitandao ya Kijamii Kama Instagram na Facebook Kupigwa Marufuku Ofisi za Serikali

$
0
0
Serikali imeanza mchakato wa kutekeleza mpango wa kudhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii katika ofisi za umma ili kuongeza ufanisi.

Mpango huo umelenga kuzuia mitandao ya kijamii ikiwamo Facebook, Twitter, Whatsapp na Instagram.

Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala wa Serikali Mtandao (Ega), Suzan Mshakangoto alisema mpango huo umelenga kuwadhibiti watumishi wa umma wanaotumia mitandao hiyo kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 9.30 alasiri.

Alisema sehemu kubwa ya wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wa taasisi za umma wameshapewa mafunzo mbalimbali kufanikisha mpango huo.

Hatua hiyo imekuja baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue kuuagiza wakala huyo miezi mitano iliyopita kutafuta njia madhubuti ya kudhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii ofisini ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Mtumishi akishaingia ofisini hataweza kutumia mitandao ya kijamii na huduma za barua pepe nje ya mfumo wa Serikali kama Yahoo na Gmail. Tunawataka watumie mfumo wa barua pepe za Serikali ili wafanye mawasiliano salama,” alisema Mshakangoto.

Utekelezaji wa mpango huo huenda ukachukua muda kidogo kuanza kwani Mshakangoto alisema taasisi zote za umma zaidi ya 500 zinatakiwa kuunganishwa kwenye Mkongo wa Taifa lakini huenda ukaanza na taasisi 72 zilizounganishwa zikiwamo wizara zote, wakala wa Serikali na idara kama Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Ega ilianzishwa miaka minne iliyopita kwa ajili ya kujenga mfumo wa mtandao wa Serikali, kuimarisha uratibu, usimamizi na uzingatiaji wa viwango vya Serikali Mtandao katika utoaji wa huduma kwa umma. Pia, kuimarisha mifumo shirikishi ya Tehama na kuboresha uwezo wa taasisi za umma katika kutekeleza Serikali mtandao.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ega, Dk Jabiri Bakari alisema sasa wamejikita kuhakikisha mifumo yote ya taasisi za umma inaingiliana kama ilivyobainishwa kwenye miongozo ya Serikali Mtandao ili kurahisisha mawasiliano na kuongeza uwajibikaji.t

YANGA INASONGA HATUA YA MAKUNDI KWA JUMLA YA MABAO 2-1

$
0
0

MPIRA UMEKWISHAAAAAAAADk 90+8 Kipa Dida wa Yanga yuko chini anagaagaa baada ya kupigwa jiwe na shabiki aliye nyuma ya lango
Dk 90+7 Anaingia Mwashiuya kuchukua nafasi Msuva
Mwamuzi bado hajaonyesha kibao cha muda wa nyongeza, mzozo unaendelea hapa uwanjani. Haijulikani hata nini kitafuatia, tutaendelea kuwajuza

Sasa ni Dk ya 90
Dk 89, Anaingia Yondani, anatoka Tambwe
Penalti inapigwa hapa, Dida anaokoaaaaaaaaaa
Wapigapicha kutoka Tanzania wako jukwaani wamefuatwa na kuzuiwa kupiga picha
Fujo zimetawala, vurugu uwanjani hadi polisi wameingia
PENAAAAAAT Dk 87,Wanapata penati baada ya Cannavaro kumwangusha mshambuliaji aliyekuwa anaingia langoni

KADI Dk 86 Cannavaro analambwa kadi nyekundu
Dk 85, Ngoma kaumia, anabebwa na kutolewa nje na machela, lakini wanaonekana kumkimbiza harakaharaka, hali inayosababisha mzozo kidogo
Dk 83, Mechi ni ngumu bado, Yanga wanaonekana kuongeza ulinzi zaidi, kingine wanapaswa kujilinda na fauloSasa bado Dk 10 tu, Yanga wanalazimika kuendelea kuweka ulinzi makini zaidi. Kaseke anaonekana kuwa msaada katika ukabaji

Sasa ni Dk 78, mpira bado unaonekana ni mashambulizi ya zamu. Yanga wawe makini na washambuliaji wa Sagrada, wanaonekana kulazimisha kutaka kuingia kwenye boksi. Wakifanikiwa ni rahisi kwao kufunga au kujiangusha

Dk 75, Ngoma anageuka na kupiga shuti vizuri lakini linapaa juu kidogo
Dk 73, Ngoma anatolewa tena kwenda kutibiwa nje, hii ni mara ya nne.
Dk 71, Sagrada wanashambulia zaidi. Sasa wanabadilisha kutoka mipira ya krosi na kupiga ile ya chini wakitaka kupenyeza katikati ya uwanja

Dk 64 sasa, kidogo Yanga wanaendelea kucheza pasi za haraka, ingawa Sagrada pia wanashambulia mara kwa mara. Dida anaonekana kuwa makini zaidi
SUB: DK 60, Pluijm anamtoa Kamusoko anamuingiza Deus Kaseke. Nafikiri ni kuhofia kupata kadi nyekundu, maana baada ya kupewa kadi ya njano, mwamuzi alishamuonya mara moja. Dalili kwamba angecheza faulo nyingine ingekuwa kadi
Dk 58, Ngoma yuko chini, anaonekana kuwapa wakati mgumu sana. Wachezaji Yanga na wale Esperanca wanazozana sana hapa

Dk 53 sasa, mechi inakwenda kwa kasi sana na Yanga bado wanaonekana kuchangamka
Kipindi cha pili kimeanza, Esperanca wanaonekana kuanza kwa kasi wakipania kupata bao la pili. Lakini Yanga nao wanasukuma mashambulizi

HALF TIME:



Dk 42 hadi 44 Yanga walionekana kuamka na kupiga pasi nyingi. Hata hivyo hawakufanya mashambulizi makali sana. Inaonekana wanakuwa makini sana ili wasifungwe bao tena

Dk 41 sasa, mpira unaonekana kubalansi ingawa Yanga wamekuwa wakishambuliwa zaidi
Dida analambwa kadi ya njano, haikuwa sahihi lakini inaonekana baadaye kuna mchezaji wa Yanga atalambwa kadi nyekundu maana mwamuzi anaitengeneza mapema. Dida aliomba kurudishiwa mpira na waokota mpira waliung'ang'ania, mwamuzi kasema alizozana nao.


KADI: Dk 36 hizi, Cannavaro analambwa kadi ya njano, lakini Love alijilegeza kumtafutia msala. Yanga wanalazimika kuwa makini na kadi hizo za njano. Pluijm pia inabidi awaeleze mapumziko au kuzifanyia kazi
BAO
Dk 25, Esperanca wanapata bao kupiria mshambuliaji wao mkongwe Love Kabungula aliyeunganisha krosi baada ya mabeki Yanga kushindwa kuuwahi mpira

 Dk 24, inaonekana wachezaji wa Esperanca wamepania kuwafanya wa Yanga wapanik
-Kamusoko tayari kalambwa kadi ya njano, Yanga inabidi wawe makini kwa kuwa inaonekana wazi mwamuzi kama anatafuta kadi nyekundu

Dida naye anaanguka hapa baada ya kupangua mpira, inaonekana aligongwa. Kama kuna njama hivi ya kutaka kuwaumiza baadhi ya wachezaji au kuwatafutia kadi

Ngoma anaanguka baada ya kufanyiwa madhambi, lakini inaonekana mwamuzi hajali, mechi inaendelea kwa dakika mbili zaidi.

Mechi imeanza kwa kasi sana, Esperanca wanaonekana wamepania kupata bao la mapema ili kuwachanganya Yanga.


Picha matata za Muna Love usipite zicheki hapa

$
0
0

MUNA ALPHONCE 💏👉👉MUNAMALOVEEE

ADD ME snapchat munamapenz. MANAGER DIRECTOR AT MUNALOVE ENTERTAINMENT.








MECHI YA KOMBE LA CAF LAKINI ASKARI KILA SAA WANAINGIA UWANJANI

$
0
0

HIVI NDIVYO HALI ILIKUWA INAENDELEA UWANJANI, KILA MARA ASKARI WANAINGIA HADI UWANJANI KUZUIA TAFRANI. HII ILITOKANA NA WACHEZAJI WA ESPERANCA KUWA WAKIWAPIGA WACHEZAJI WA YANGA. 

KABLA SIJAFA NAOMBA DUNIA INISAMEHE-8 (MWISHO)

$
0
0

Uingereza
“How was Nigeria?”
“Its was fine but the search for professor Owo became unsuccessful!”(Nigeria ilikuwa nzuri lakini hatukufanikiwa kumpata profesa Owo!)
“Why?”(Kwanini?)
“They said he died in an accident while on journey in Cambodia!”(Walisema alikufa akiwa safarini huko Cambodia)
Wapelelezi wa Scortland Yard waliokuwa wametumwa nchini Nigeria kumsaka profesa Owo walimweleza mkuu wao kila kitu walichokiona nchini humo na sababu iliyowafanya washindwe kumpata profesa Owo.
“Welcome home!”(Karibuni nyumbani)Mkuu wao wa kazi aliwakaribisha nyumbani.
****
Pamoja na umri mkubwa aliokuwa nao mke wa chifu Onuku penzi kati yake na Harrison lilizidi kukomaa na mama alizidi kuchanganyikiwa zaidi kadri siku zilivyozidi kupita na Harrison nae alizidi kumpa mama mapenzi mazito zaidi ili azidi kumchanganya na kupata mzigo zaidi ya gesi bure na kusafirisha Uganda ambako alijipatia pesa nyingi na kuzidi kutajirika pamoja na kuwa afya yake hakuiamini.
Kila chifu Onuku aliposafiri mke wake alihamia nyumbani kwa Harrison ambako walitanua na kufaidi maisha!
Lagos nzima waliuelewa uhusiano uliokuwepo kati ya Harrison na mke wa chifu, ilivyoonekana ni chifu peke yake ndiye hakulielewa jambo hilo na hapakuwa na mtu wa kumpa ukweli kwa sababu watu wote walimwogopa na kumhofia! Ilikuwa si rahisi mtu kumtamkia chifu jambo hilo sababu watu wote walijua ni kiasi gani alimheshimu na kumwamini mke wake!
Ili kuondoa wasiwasi ambao alihisi ilibidi mke wa chifu amtambulishe Harrison kwa mumewe kama mteja wao wa gesi kutoka Uganda! Bila kufahamu kilichokuwa kikiendela kati yao chifu Onuku alifurahi sana kukutana na Harrison.
“Ni mteja wetu mzuri kwani ananunua gesi nyingi sana kila mwezi!”
“Kijana hongera sana ni vijana wachache sana wanaoweza kufanya biashara vizuri, wengi wanaishia kutumbua tu!”
“Ahsante sana mzee nimefurahi sana kukufahamu maana mara nyingi umekuwa safarini, muda wote nimekuwa nikifanya kazi na mama tu!”
“Hamna matatizo mama yako anaiweza kazi vizuri sana sina wasiwasi wowote juu yake, ninafikiri mnafanya kazi vizuri au siyo mama?”Chifu alimgeukia mke wake.
“Vizuri sana huyu ni kijana safi sana hana matatizo na anatulipa vizuri!”
“Kwa hivi sasa anaishi wapi hapa Lagos?”
“Yupo Lagos hoteli!”
“Kijana kwanini unaishi hotelini wakati sisi wazazi wako tuna nyumba nzuri na kubwa kiasi hiki?”
“Napenda kuishi kwa uhuru baba!”
“Lakini pia hapa kwetu unaweza kuishi vizuri kwa uhuru, tuna nyumba nyingine kubwa ipo kulee mwisho mbali kabisa na hii ya kwetu kwani mtategemea kuishi hapa kwa muda gani?”
“Mimi?”
“Ndiyo!”
“Nitakaa hapa kwa muda mrefu sana maana bado biashara yangu inaendelea!”
“Basi tafadhali naomba uhamie hapa nyumbani, mama hebu hakikisha mteja anahamia hapa leo hiihii, unataka aje kukutana na watu wengine wamchukue biashara ni ushindani!” Alisema chifu Onuku huku akitabasamu hakujua kama alilokuwa akilifanya ni kosa kubwa.
Ni siku hiyo hiyo tu mkewe alihakikisha Harrison amehamisha begi lake la nguo kutoka katika nyumba aliyokuwa amempangishia.
“Sasa itakuwaje?”
“Kwa sababu anang’ang’ania wewe hamia tu tena atakuwa ameturahisishia mambo yetu kwani kila atakapokuwa safarini wewe utakuwa mume wangu, shauri yake!”
“Sawa vipi kuhusu vitu tulivyonavyo ndani ya nyumba?”
“Nitaviuza na nyumba nitaipangisha kwa watu wengine wakae sawa darling?”
“Hakuna tatizo!”
Harrison alipoonyeshwa nyumba aliyotaka kuishi alishindwa hata kuamini, ilikuwa nyumba kubwa nzuri na yenye kila kitu cha thamini ndani yake ilijitegemea kwa kila kitu na Harrison alitambulishwa kwa Stella msichana wa kazi aliyetakiwa kumfanyia kila kitu akiwa hapo nyumbani.
Watu wote nchini Nigeria waliamini chifu Onuku alikufa katika ajali ya gari na aliyeijua siri kuwa hakufa alikuwa ni mkewe peke yake na pamoja na kumpenda Harrison hakudiriki kumwambia siri hiyo hata siku moja.
*****
“Mzee yupo kweli?”
“Yupo ila huwezi kumwona huwa haonani na watu kirahisi, akiwa hapa nyumbani hupatikana nyuma ya kompyuta akifanya mahesabu yake! Na huondoka asubuhi sana kwenda kwenye shunguli zake nakurudi usiku ila anasafiri leo hii kwenda Uingereza!”
“Aisee kwa hiyo tutapata nafasi ya kuonana siyo?” Aliuliza Harrison.
“Siyo kuonana tu ila utakuwa unalala chumbani kwangu mpaka atakaporudi!”
“Hapana! Je akinikuta ndani nitafanya nini?”
“Hawezi kukukuta kwa sababu hunipigia simu kabla ya kurudi!”
“Kweli?”
“Ndiyo!”
Jioni ya siku hiyo Harrison na mke wa chifu walimsindikiza chifu Onuku uwanja wa ndege katika safari yake ya wiki tatu nchini Uingereza, kila mtu moyoni mwake siku hiyo alikuwa na furaha kupita kiasi, walifurahia safari ya chifu Onuku ili wapate nafasi ya kutanua na kufanya mambo yao vizuri na kweli siku hiyohiyo usiku Harrison alihamia katika chumba cha chifu Onuku na wakaanza kufaidi maisha pamoja.
Siku moja kabla ya chifu Onuku kurejea kutoka safarini Harrison alirejea tena chumbani kwake, hakuna mtu aliyehisi kitu chochote kati ya Harrison na mama Onuku kwa sababu ya tofauti kubwa ya umri iliyokuwepo katikati yao, kwa mama Onuku Harrison alikuwa ni kama mtoto wake wa kuzaa.
Mpaka miezi sita baadaye Harrison alikuwa bado akiishi katika himaya ya chifu Onuku, afya yake ilizidi kudhoofika siku hadi siku kwa ugonjwa wa kifua! Kwa sababu alishakuwa kama mtoto wa familia ya chifu Onuku na mkewe, walilazimika kumshughulikia kwa matibabu, alikohoa sana usiku na alipopimwa makohozi mara tatu alionekana kuwa na kifua kikuu.
Hapakuwa na suala jingine la kufanya zaidi ya kumrejesha nchini Uganda ambako miezi sita baadaye alifariki dunia kwa ugonjwa wa Ukimwi! Idadi kubwa ya vijana wa rika lake nchini Uganda walikuwa wamekufa kwa ugonjwa huo hatari.
Hivyo hakuna aliyeshangazwa sana na kifo cha Harrison, watu walishalia sana mpaka mioyo yao ikawa sugu sababu katika eneo la Mbalala alikoishi kwa mwezi mmoja walikadiriwa kufa vijana wasiopungua wawili kwa ugonjwa huo
***
Taarifa ziliporudishwa Nigeria kuwa Harrison alikufa kwa Ukimwi watu wengi waliomfahamu walisikitika sana kwani wakati huo ndio ugonjwa huo ulishaanza kuitishia nchi hiyo ingawa kulikuwa hakujawa na wagonjwa wengi sana wa Ukimwi bado.
Mke wa chifu alilia sana kusikia habari hizo na kila siku mume wake aliendelea kumfariji akijua alisikitishwa sana na kifo cha mteja wake, kumbe mama alilia kwa sababu alijua hata yeye Ukimwi alikuwa nao na angekufa muda si mrefu, kilichomuumiza zaidi ni kumwambukiza mumewe ambaye hakushtahili kabisa kushiriki katika kifo hicho.
Kwa wiki nzima mke wa chifu alilia na alikuwa na simanzi baya moyoni mwake, alishindwa kula na hata kusema chochote, ilimlazimu chifu aache kazi zake zote na kuanza kushinda nyumbani.
Siku ya sita chifu alilazimika kuondoka nyumbani kwa muda mfupi kuelekea kwenye visima vyao vya mafuta kaskazini ya Nigeria ili kuangalia shughuli zao ziliendelea vipi? Hakukaa sana lakini aliporudi nyumbani kwake muda wa saa kumi jioni aligutuka alipokuta barua ya ajabu sebuleni kwake!
Mpendwa,
Owo!
Kifo cha Harrison kinamaanisha kifo changu mimi na kifo changu kinaamisha kifo chako!.
Moyo wa chifu Onuku uliruka pigo moja alihisi kuishiwa nguvu miguuni, barua ile ilimtisha sana!
Nitaona aibu sana nitakapokuangalia usoni pindi nitakapoanza kuugua? Nimeamua kufa ili kujiepusha na hasira yako nakiri kwa mdomo wangu kuwa nilikutana kimwili na Harrison na nina imani nimeambukizwa Ukimwi na hiyo inaamaanisha wote ikiwemo wewe pia umeambukizwa na sote tutakufa! Nimeamua kutangulia ili kuuepuka uso wako, Ukimwi unatesa na unaumiza na mimi sitaki kufa kifo cha aina hiyo! Ninajisikia mkosaji sana moyoni mwangu na sasa ninakuomba sana uniruhusu kukutangulia!” Ilimaliza barua hiyo.
Wakati anamaliza kuisoma barua hiyo chifu mwili mzima ulikuwa ukitetemeka na jasho jingi likimtoka, aliingia moja kwa moja hadi chumbani nako pia hakumkuta mkewe, alishindwa kuelewa alikuwa wapi alianza kuita lakini hakuitikiwa.
Ghafla alisikia mkojo umembana na kuingia bafuni kukojoa ni huko bafuni ndiko alikomkuta mkewe akiwa ameanguka chini mkojo ulikatika palepale na kusahau kilichomfanya aingia bafuni!
Alimtingisha mke wake bila kuamka, aligundua mke wake tayari alishakufa, kwa haraka alitoka nje na kusogeza gari hadi mlangoni, akiwa amechanganyikiwa aliubeba mwili wa mke wake na kuuingiza ndani ya gari, wafanyakazi wote wa nyumba yake walishangaa ni nini kilikuwa kimempata mke wa bosi wao, walijaribu kumdadisi chifu lakini hakuwapa jibu badala yake aliomba geti lifunguliwe na kutoa gari nje.
Alipofika hospitali na madaktari walipopima alikuwa tayari ameshaaga dunia! Chifu aliomba mwili wa mke wake ufanyiwe uchunguzi wa kutosha kugundua ni ni hasa kilimuua, majibu yalipotoka ilibainika kuwa alikunywa kiasi kikubwa cha dawa aina ya Diazepam na kufa akiwa usingizini.
Chifu alichanganyikiwa kupita kiasi, aligundua ugonjwa alioutengeneza mwenyewe na kufikiri aliukimbia ulikuwa umeingia ndani ya damu yake, alilia sana lakini ukweli ulibaki palepale kuwa ukimwi ulikuwa umerejea tena kwake, alijilaumu mwenyewe kwa makosa mengi, kwa kuiua jamii ya watu wasiokuwa na hatia.
Hata yeye mwenyewe alishindwa kujipa msamaha! Ukimwi kufika kwake kupitia kwa mke wake aliichukulia kama adhabu kwa kazi yake haramu aliyoifanya, hakuwa na njia ya kujiokoa mwenyewe pamoja na kuwa ni yeye aliyemtengeneza mdudu huyo, aliikubali hali hiyo na kusubiri kifo.
Miaka miwili baadaye:
Hali ya chifu Onuku ilikuwa mbaya alikuwa mgonjwa taaban akiwa amelazwa katika moja ya hospitali zake, iligundulika wazi ulikuwa ni Ukimwi na alikuwa akisubiri siku zake mamia ya watu walifurika kila siku hospitalini kumsalimia chifu Onuku aliyekuwa akiugua Ukimwi.
Wengi wa walioufahamu uhusiano uliowahi kuwepo kati ya mke wa chifu na Harrison walimtupia lawama nyingi sana mkewe huyo kwa kumuua chifu wao aliyewasaidia
Siku chache kabla ya kifo chake chifu Onuku aliita waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya nje na vya ndani ya nchini Nigeria, alikuwa ameamua kuwaeleza ukweli juu ya ugonjwa wake.
“Nimewaita kuwaelezeni ukweli, mimi ninayeongea na nyinyi ndiye chifu Onuku mwenyewe niliyesingizia kupatwa na ajali na kufa, niliibadilisha sura yangu makusudi ili kuepuka watu waliokuwa wakinitafuta, nilisakwa sana na serikali ya Uingereza.
“Ulisakwa kwa nini?”
“Kabla ya kuja hapa Nigeria kutoka Uingereza niliitwa profesa Owo! Mimi pamoja na wenzangu wawili tulitengeneza wadudu ambao wanasababisha ugonjwa huu unaoniua mimi mwenyewe na wadudu hawa walikuwa katika chanjo ya polio na kuletwa huku Afrika nililipwa pesa nyingi sana ambazo nilikuja nazo hapa Nigeria kuanzisha biashara yangu!”
Alielezea kila kitu na mwisho aliomba dunia imsamehe kabla hajafa! Taarifa hizo zilipofika Uingereza waliletwa wapelelezi kumkamata ili akashtakiwe Uingereza lakini alifariki njiani kabla hata ya ndege kutua nchini humo.
Mwisho.
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>