Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

Zari ampeleka Tiffah kufanyiwa tambiko

$
0
0
Zarinah Hassan ‘Zari’ akichochea kuni.
Stori:Musa Mateja, 
DAR ES SALAAM: Utamaduni! Mzazi mwenzake staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’, anadaiwa kumpeleka mwanaye Latiffah Nasibu ‘Tiffah’ (miezi 5) kijijini kwao Uganda ambako amefanyiwa tambiko la kimila huku Diamond akiichomolea mbali safari hiyo, Ijumaa Wikienda lina kitu cha kushika mkononi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo linalofanywa na makabila mengi ya Afrika, lilijiri Ijumaa iliyopita mjini Jinja, nchini humo na kuhudhuriwa na wana ukoo wa Zari, wakiwemo pia wajomba huku bibi Zari akiwa ndiye mwenye shughuli hiyo kwa kusaidiwa na mwanaye, bibi Tiffah ambaye pia ni mama mzazi wa Zari, Halima Hassan.
ZARI ALITOKEA BONGO
Chanzo chetu kimesema kuwa, Zari aliondoka jijini Dar es Salaam siku moja baada ya kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya ambapo alifunga mizigo yake kuelekea nyumbani kwake Afrika Kusini kuwachukua wanaye wengine, Pinto, Didy na Quincy Ivan Ssemwanga na kuambatana nao hadi Jinja kwa bibi yake.

TWENDE NA CHANZO
“Ebwana ngoja nikupe habari ya kushangaza juu ya huyu mzazi mwenzake na Diamond, Zari. Sikuwahi kutegemea kama mwanamke huyu ninavyomuona na mambo yake ya Kizungu-zungu lakini kafunga safari hadi kwa bibi yake, Uganda kwa ajili ya kufanya mambo ya kimila kwa mtoto wake, Tiffah. Safi sana. Nasikia hata wale wengine walifanyiwa walipokuwa watoto kama Tiffah.

1
Mama Zari akiwa na mjukuu wake.
“Juzikati tu, baada ya kula Mwaka Mpya alimuomba Diamond waende wote Uganda kwa ajili ya kumfanyia tambiko Tiffah, lakini Diamond alichomoa safari hiyo, hakwenda.
“Nilizungumza na Diamond juu ya suala hilo akasema kuwa, yeye ameshindwa kwenda kutokana na kutoamini sana mambo hayo ya mila na desturi ambazo si za kabila lake,” kilisema chanzo hicho.

MBUZI ACHINJWA
Chanzo kiliendelea kuweka wazi kwamba, miongoni mwa mambo yaliyofanyika kwenye shughuli hiyo ni kuchinjwa kwa mbuzi aliyekomaa ambapo nyama yake ilipikwa mpaka kuiva bila kuungwa na vikorombwezo vyovyote kisha watu wakala.

ZARI APIKISHWA KIENYEJI
Katika hali ambayo mashabiki wake hawakuizoea, Zari katika mwendelezo wa mila hiyo, alielekezwa kupika nyama ya mbuzi huyo kwenye sufuria kubwa lililofunikwa juu kwa majani ya migomba ya ndizi badala ya mfuniko. Pia, Zari alitumia jiko la kuni lenye mafiga matatu kupika huku likitoa moshi.

zarinaaaa 
‘Zari’ akiwa na Tiffah.
KWENYE MSOSI
Baada ya msosi huo kukamilika, Zari, watoto wake, wajomba zake, mama yake na ndugu wengine walikaa kwenye mkeka nje na kula kwa pamoja. Inadaiwa baada ya mlo ndipo wazee wenye kuaminiwa katika jamii walisema maneno yenye heri kwa ajili ya makuzi ya Tiffah.

DIAMOND ILIKUWA ATAMBULISHWE RASMI
Habari zaidi zinasema kuwa, licha ya Tiffah kufanyiwa ‘madongoloji’, kama Diamond angekubali kwenda ilikuwa akatambulishwe rasmi ukweni kwake ambapo ndugu wa Zari wangeonana naye ‘laivu’ na kumkaribisha kama mchumba wa Zari.

DIAMOND ATOA NENO KWA WIKIENDA
Baada ya kupewa mchongo huo, Wikienda lilimtafuta Diamond ana kwa ana kwa nia ya kutaka kujua kwa nini aligoma kuambatana na Zari nchini Uganda ili kufanikisha tambiko la mwanaye ambapo alisema hajagoma kwenda bali majukumu yaliyo mbele yake yalimzuia.

11850013_466174470220105_1281926624_n“Mimi sijagoma kwenda Uganda na Zari kama wengi wanavyoweza kusema, ila ukweli ni kwamba nashughulikia studio na ofisi yangu mpya. Si unajua tumehama pale tulipokuwa (Sinza-Mapambano) na sasa tupo hapa (Sinza-Mori).
“Nisipokuwepo kwenye ufungaji huu wa vyombo na samani hizi hakuna anayeweza kujua mimi nataka ofisi hii iweje na studio ifungweje. Kama ningekwenda basi yote yangefanyika,’ alisema Diamond.

CHANZO: GPL

Mazito yaibuka ndoa mpya ya Wastara

$
0
0
HAYA ni mazito! Nyuma ya shughuli ya kuolewa kwa staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma na Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Juma iliyofungwa Alhamisi iliyopita, kuna matukio ya kustaajabisha ambayo Ijumaa Wikienda limeyabaini.
Ndoa hiyo iliyofungwa kimyakimya, ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa mwigizaji huyo, Tabata-Barakuda, jijini Dar ambapo ilihudhuriwa na watu wachache tofauti na ilivyotarajiwa kutokana na umaarufu wa wanandoa hao.

NDOA ILIFUNGWA KWA SIMU
Imebainika kuwa, awali ndoa hiyo ilikuwa ifungwe saa kumi jioni na baadaye kuelezwa ilisogezwa mbele hadi saa 12 jioni, hata hivyo haikufungwa muda huo baada ya bibi harusi kuchelewa kufika akitokea saluni alikoenda kupambwa na kulazimika shehe afungishe ndoa hiyo kwenye simu wakati Wastara akiwa kwenye foleni barabarani.

BWANA HARUSI AGOMA KUPIGWA PICHA
Imeelezwa kuwa, baada ya bwana harusi kutinga na wapambe wake alitoa onyo kali huku likisisitizwa na wapambe wake kuwa hairuhusiwi kupiga picha na kutuma kwenye mtandao wowote wa kijamii kwa vile ndoa hiyo ilikuwa ya siri.

…AGOMA KUMFUNUA BIBI HARUSI
Katika hali ya kushangaza, baada ya bibi harusi kuwasili aliingizwa katika chumba maalum kwa ajili ya kumsubiri mumewe na hata alipoingia ndani, shehe alimuomba amfunue mkewe ili kumhakikisha kama ndiye yeye kitu ambacho alikipinga na kudai hakuwa na shaka naye na kuomba waendelee na kitu kingine.

SAMSUNG CAMERA PICTURESWASTARA ASHINDWA KUPATA MSOSI
Jambo lingine ambalo lilizua minong’ono ni Wastara kushindwa kupata muda wa kula chakula ambacho kiliandaliwa kwa sababu baada ya kumaliza kupiga picha za familia na kushikana mkono na mumewe, mumewe alimtaka waondoke huku akimwambia dereva wao awashe gari.

WADOGO WA SAJUKI WALIA
Katika hali ambayo haikuweza kufahamika mara moja, wadogo wa aliyekuwa mumewe wa pili wa Wastara, merehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Mohamed Kilowoko na Njegere Kilowoko waliangulia kilio kwa kile walichodai walikuwa na huzuni na furaha.

Pam D azindua Video yake ya Popo Lipopo Maisha Basement...Picha zaidi ya 20 zipo hapa

$
0
0





























 Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Pamela Daffa akizindua wimbo video yake mpya ya Popo Lipopo ndani ya Maisha Basement usiku wa kuamkia leo kwa kuimba na mashabiki wake.













Red Carpet ya Uzinduzi wa Video ya Popo Lipopo Maisha Basement, Dar

$
0
0

 Watu mbalimbali wakiwa wamejiachia katika Red Carpet ya uzinduzi wa Video Mpya ya  Pam D Popo Lipopo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo Maisha Basement jijini Dar.



















CUF Haiko Tayari Kurudia Uchaguzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad Aongea Na Waandishi wa Habari

$
0
0


Hatimaye, Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ametoa msimamo wake na chama chake kufuatia mazungumzo ya siri ya kutafuta suluhu ya mkwamo wa kisiasa unaotokana na tangazo la kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.

Akizungumza leo na waandishi wa habari katika hotel ya kitalii ya Serena jijini Dar es Salaam, Maalim Seif amesisitiza kuwa hoja ya kurudia uchaguzi wa Zanzibar kama inavyoelezwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), haina msingi, haikubaliki na sio halali kikatiba.

“Hoja ya kurudia uchaguzi haina msingi, haina uhalali, ni hoja ambayo inaweza kuzaa fujo na vurugu na inaweza kuleta mzozo mkubwa wa kikatiba wa kisheria. Sidhani kama tunataka kuwapeleka huko watanzania,” alisema Maalim Seif.

Makamu huyo wa kwanza wa rais wa Zanzibar ameeleza kuwa tayari wameshafanya vikao nane vilivyowashirikisha wagombea urais pamoja na marais wastaafu wa Zanzibar lakini hawakukubaliana kurudia  uchaguzi kama baadhi ya viongozi wa CCM walivyoeleza.

Aidha, Maalim Seif amekanusha kilichoelezwa na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd baada ya kukutana na Rais John Magufuli, kuwa rais alisema warudie Zanzibar kujiandaa na marudio ya uchaguzi kwani rais hakusema hivyo alipokutana naye.

Maalim Seif amesema kuwa ana imani kubwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli katika kuleta maridhiano na ufumbuzi wa mgogoro wa Zanzibar kutokana na mazungumzo aliyofanya naye hivi karibuni katika Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa endapo uchaguzi mkuu utatakiwa kurudiwa, zipo changamoto nyingi za kikatiba ambazo zitakwamisha zoezi hilo hivyo uchaguzi huo hautawezekana.

Ametaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kupitishwa kwa fedha za kugharamia uchaguzi na baraza la wawakilishi ambalo hivi sasa halipo kwa kuwa limefikia ukomo wake.

Mbali na hilo, Maalim Seif alieleza kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salum Jecha anapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu kwa kutoa tamko lisilo halali la kufuta uchaguzi huo huku akifahamu dhahiri kuwa hana nguvu hiyo kikatiba.

Ameitaka ZEC iongozwe na makamu mwenyekiti wake kwa mujibu wa katiba pamoja na wajumbe wengine kukamilisha utaratibu wa kuhakiki matokeo ya uchaguzi na kumtangaza mshindi.

Maalim Seif ameeleza kuwa anafahamu dhahiri kuwa kuna mpango wa kutangaza kwa nguvu marudio ya uchaguzi Februari 28 mwaka huu, lakini yeye pamoja na chama chake hawatakubali.

Rais Magufuli Amjulia Hali Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye Aliyelazwa Hospitali Ya Taifa Ya Muhimbili leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 11 Januari, 2016 amemtembelea na kumpa pole Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Frederick Sumaye ambaye amelazwa katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Frederick Sumaye alilazwa katika Taasisi hiyo siku nne zilizopita kwa matibabu ya moyo na madaktari wanaomtibu wamemhakikishia Rais Magufuli kuwa anaendelea vizuri ikilinganishwa na wakati alipofikishwa katika Taasisi hiyo.

Pamoja na kumpa pole, Rais Magufuli pia amemuombea apone haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake ya kila siku.

Akizungumza mara baada ya kuonana na Rais, Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye amemshukuru Rais Magufuli kwa kwenda kumuona na kueleza kuwa kitendo hicho kimeonesha jinsi alivyo na upendo wa dhati na anavyowajali watu wake.

Kuhusu hali yake, Mheshimiwa Sumaye amesema anaendelea vizuri, anapata matibabu mazuri na kwamba kwa kuwa hali yake ni nzuri anatarajia kuruhusiwa kuondoka hospitali hapo baada ya muda mfupi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
11 Januari, 2016
 
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam Januari 11, 2016 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye na Mama Esther Sumaye alipokwenda kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu huyo Mhe Freredick Sumaye katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam Januari 11, 2016

Rais Magufuli Amtembelea Na Kumfariji Mama Maria Nyerere Kufuatia Kufiwa na Mkwewe Bi Leticia Nyerere

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 11 Januari, 2016 amemtembelea na kumpa pole mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere kufuatia kifo cha Mkwewe Leticia Nyerere kilichotokea jana huko Maryland Marekani alikopelekwa kwa ajili ya kupata matibabu mapema mwezi huu.


Pamoja na kutoa mkono wa pole kwa Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani Jijini      Dar es Salaam, Rais Magufuli pia amewapa pole wanafamilia wote na amewaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na ndugu yao.

Msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere Bwana Joseph Butiku amemueleza Rais Magufuli kuwa familia inaendelea na taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Marekani na itatoa taarifa baadaye.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
11 Januari, 2016

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mama Maria Nyerere kufatia kufiwa na Mkwe wake Bi Leticia Nyerere aliyefariki huko nchini Marekani. Rais alikwenda nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani Dar es salaam kumpa pole Mama nyerere Januari 11,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapa pole wanafamilia alipofika nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani Dar es salaam kumpa pole Mama nyerere Januari 11,2016
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo juu ya uataratibu wa msiba kutoka kwa mwanafamilia Joseph Butiku
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na wanafamilia
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na wanafamilia alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha Mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani.

Seif: Mimi si makamu tena wa rais

$
0
0

 Katibu Mkuu wa CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hatma ya mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad ametangaza rasmi kuwa yeye si makamu tena kwa sababu muda wa serikali iliyoongozwa na Dk. Ali Mohamed Shein kikatiba ulikwisha tangu tarehe 2 Novemba, 2015. Anaandika Jabir Idrissa… (endelea).
Amesema kwa mujibu wa Ibara ya 28(2), muda halali wa rais utakuwa umefikia kikomo itakapotimu miaka mitano tangu siku ambayo kiongozi huyo alikula kiapo cha utii cha kushika wadhifa huo.
Wakati huohuo, amesema Rais John Magufuli anapaswa kuchukua uongozi wa juhudi za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar, baada ya kuonekana kuwa wenzake hawana nia njema.
Maalim Seif amewaambia wahariri na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam leo kwamba Dk. Shein na mawaziri wake wamekuwa wakibakia madarakani kwa ubabe tu kwa kuwa kikatiba muda wa serikali yake ulishakwisha.
“Mimi si Makamu wa Kwanza tena. Kama kubakia basi nimebaki kwa sababu ya kuweka kinga tu ya wafuasi wetu kwa kuwa hata mwenzangu Dk. Shein ambaye pamoja na mimi ndio hatutegemei kuwepo kwa Baraza la Wawakilishi, yupo lakini si rais halali kwa sababu hiyo hiyo ya kumaliza muda wake,” amesema.
Hilo la kama yeye bado ni Makamu wa Kwanza wa Rais au laa, ni moja ya maswali aliyoulizwa katika mkutano huo aliouitisha kwa lengo la kuzungumzia mazungumzo yanayofanyika ya kutafuta utatuzi wa mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar.
“Ukweli uongozi wa Dk. Shein upo kibabebabe tu lakini ulishamaliza muda wake rasmi Novemba 2, 2015. Ndio maana tunasema kwamba kitendo cha Jecha Salim Jecha kuufuta uchaguzi pasina kuwa na mamlaka kumeifanya Zanzibar kutokuwa na serikali wala Baraza la Wawakilishi,” amesema.
Amesema yeye yupo kwa sababu na hao wenzake wanaendelea kushikilia nafasi zao, lakini kwake kuwepo ni muhimu kwa kuwa bila ya hivyo wafuasi wake watapata madhara makubwa.
Maalim Seif ametoa msimamo huo huku akiwa ameshasoma taarifa ndefu ya maandishi iliyojaa ufafanuzi wa vifungu mbalimbali vya sharia kuelezea msimamo wake na Chama cha Wananchi (CUF) kuwa Dk. Shein si rais halali na wala mawaziri si halali.
CUF ilishatangaza kuwa mawaziri wake saba katika Baraza la Mawaziri la Dk. Shein hawapo kazini tangu Novemba 12 siku ambayo kimahesabu ilitarajiwa kuwa ya mwisho kwa mamlaka ya Rais kuweza kuitisha Baraza la Wawakilishi iwapo kungetokea dharura kabla ya kuapishwa kwa baraza jipya baada ya uchaguzi.
Maalim Seif ambaye aliambatana mkutanoni hapo na wasaidizi wake katika chama, wakiwemo wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa (BKUT), amesema mazungumzo yake na Dk. Shein pamoja na marais wastaafu wa Zanzibar, yamefikia hatua ngumu kukamilika.
Amesema kwamba baada ya kuwa hawajaafikiana kutoka na kila upande kubaki na msimamo wake – yeye akishikilia kuwa uchaguzi haukufutwa kihalali kwa mujibu wa sharia, na wenzake CCM Dk. Shein na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi kushikilia lazima uchaguzi urudiwe – ilitakiwa Dk. Shein aitishe kikao cha mwisho cha kusomwa taarifa ya yale waliyojadiliana.
“Dk. Shein amekuwa akikwepa kuitisha kikao hicho kwa wiki mbili ameshinda kukiitisha licha ya mimi kumuandikia barua na kumkumbusha… amekuwa akisema kwamba bado wanahitaji muda zaidi kujadiliana na wenzake,” amesema na kuamini kuwa tayari mwenendo huo ni uthibitisho kuwa tangu awali Dk. Shein hakuwa na nia njema katika kuitisha mazungumzo hayo.
Maalim Seif amesema baada ya vikao vinane kufanyika huku wananchi wakiwa wamekaa kimya wakisubiri, anadhani ni muhimu wananchi wajulishwe kinachoendelea hasa kwa kuwa haoni kama viongozi wenzake hao wa CCM wana dhamira njema ya kuondoa mgogoro.
Katika taarifa aliyoisoma huku matangazo ya mkutano huo yakirushwa moja kwa moja hewani na vituo vitatu vya televisheni – Azam, ITV na Star TV – Maalim Seif amesema badala ya Dk. Shein kuitisha kikao cha kuwezesha taarifa iliyoandaliwa na sekretarieti kusomwa, zipo taarifa za uhakika kuwa CCM imeagiza Tume ya Uchaguzi ikutane Januari 14, ili kutangaza tarehe ya uchaguzi wa marudio.
Amesema hoja ya uchaguzi wa marudio ilishindwa mapema, kwa sababu haina msingi wowote wa kisheria hasa kwa vile Tume yenyewe iliridhika kuwa uchaguzi ulikwenda vizuri mpaka hatua ya utangazaji wa matokeo.
“Hata ukisoma tovuti ya Tume ya Uchaguzi utakuta taarifa ya mwisho iliyomo ni inayosema uchaguzi katika hatua zake zote mpaka kufikia kutangaza matokeo ya kura ulikwenda vizuri… ukizingatia na taarifa za waangalizi wa uchaguzi wa ndani na wa kimataifa, hakuna hoja ya kurudiwa uchaguzi.
“Hawa CCM kila wanakokwenda na hata katika mazungumzo wanapotakiwa wawasilishe mezani ushahidi wa uchaguzi kuvurugika wanashindwa kutoa vielelezo vyovyote. Sasa uchaguzi urudiwe kwa hoja ipi kama hakuna ushahidi kuwa uliharibika,” amesema.
Maalim Seif amesema wakati Jecha anatoa tangazo la kufuta uchaguzi, Oktoba 28, mwenyekiti huyo mwenyewe alikuwa ameshatangaza matokeo ya majimbo 33 na majimbo yaliyobaki kura zilishajumuishwa.
Amesema Oktoba 28 ilikuwa siku ya mwisho kisheria kwa Tume kukamilisha kazi ya kutangaza matokeo ya urais na kwa hivyo “ilitakiwa Jecha aongoze kikao cha kukamilisha kazi hiyo lakini hakuonekana kazini, na makamu mwenyekiti akalazimika kuendesha kikao lakini ghafla Jecha akasikika anatoa tangazo la kufuta uchaguzi, hatua ambayo hana mamlaka nayo kisheria.”
Maalim Seif amesita kueleza CUF itakachokifanya iwapo Tume itaridhia shinikizo za uongozi wa juu wa CCM Zanzibar, kutangaza tarehe ya uchaguzi wa marudio.
Hata hivyo amesema hali hiyo itakapotokea itakuwa ni juu ya kikao cha juu cha chama – Baraza Kuu la Uongozi – kutoa uamuzi baada ya kupata maelezo ya matokeo ya mazungumzo.
Amesema ni wakati sasa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kutumia mamlaka yake kuongoza juhudi za utatuzi wa mgogoro huo kwa kuwa bado anaamini kuwa ana dhamira ya kutimiza ahadi yake ya kusisitiza haja ya mgogoro huo kutatuliwa kwa amani na maridhiano.



Leo Ndiyo Leo, Nani Kuwa Mwanasoka Bora wa Dunia wa Mwaka 2015?

$
0
0
Nyota mmoja wa soka kati ya watatu wanaosakata kabumbu katika vilabu viwili vya Hispania Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Neymar leo anatarajia kutajwa kuwa mwanasoka bora wa dunia kwa mwaka 2015.

Nyota huyo atatangazwa majira ya saa 4 na nusu usiku wa leo na kukabidhiwa tuzo ya FIFA ya Ballon d’Or Jijini Zurich Uswisi.

Lionel Messi mwenye tuzo nne za Ballon D’Or hadi sasa, anajivunia rekodi kadhaa alizoweka mwaka 2015 ikiwemo ya kuisaidia klabu yake ya barcelona kutwaa kombe ya Ulaya huku akifunga mabao 10 na kusaidia 6, rekodi ya ufungaji bora wa klabu yake katika mashindano yote ambapo alimaliza msimu akiwa na mabao 43 na kuiwezesha Barcelona kutwaa taji la ligi nchini Hispania pamoja na kombe la Mfalme.

Mbali na kuisaidia Barcelona, pia aliisaidia timu yake ya taifa Argentina kufika fainali ya Copa Amerika.

Cristiano Ronaldo ambaye amekwisha chukua tuzo hiyo mara tatu, baada ya tuzo mwaka jana aliendelea kufanya vizuri hususani katika ufungaji ambapo alimaliza msimu akiwa na mabao 48 huku akilingana na Messi kwa ufungaji katika UEFA Champions League kwa kupachika mabao 10.

Mbali na hilo, katika mwaka huo, Ronaldo alifanikiwa kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid na kuwapiku Alfredo Di Stefano na Raul.

Mwingine anayewania tuzo hiyo ni Neymar ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya Barcelona akisaidiana na Messi pamoja na Suarez na kuiwezesha klabu hiyo kutwaa makombe matatu katika msimu mmoja, pamoja na mengine mawili ambayo ni Kombe la dunia kwa vilabu pamoja na UEFA Super Cup yanayoifanya Barcelona kuweka kabatini vikombe vitano ndani ya mwaka mmoja wa kalenda.

Mshindi anapatikana kwa kupigiwa kura na makocha pamoja na manahodha wa timu za taifa huku baadhi ya wadau wa vyombo vya habari pia wakijumuishwa.

TASWIRA YA SAMATTA ALIVYOMUONYESHA KIKWETE TUZO YAKE, NAYE AKAMKABIDHI JEZI YA TP MAZEMBE

$
0
0
Mshambuliaji nyota wa TP Mazembe na Taifa Stars, Mbwana Samatta leo amemkabidhi jezi yake Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.

Samatta alikwenda kumtembelea Kikwete katika makao makuu ya CCM ambayo yeye ni mwenyekiti wake na kumshukuru kutokana na mchango wake wakati akiwa Rais wa Tanzania.


Baada ya kumuonyesha tuzo yake ya Mwanasoka Bora Afrika ndani ya Afrika, Samatta alimkabidhi Kikwete jezi namba 9 anayoivaa Mazembe. Alifanya hivyo mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

FIFA YAIPA ETOILE SIKU 60 KULIPA DENI LA OKWI SIMBA, YATISHIA KUISHUSHA DARAJA

$
0
0
KATIKA MKUU WA FIFA ALIYESIMAMISHWA, JEROME VALCKE

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) iliyokutana Disemba 15 mwaka jana, imeiagiza klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kuilipa Simba SC ya Tanzania fedha  za uhamisho wa mchezaji Emmanuel Okwi ndani ya siku sitini (60) kuanzia Januari 7, 2016.

Katika taarifa hiyo ya Fifa na nakala yake kutumwa kwa TFF, Etoile du Sahel na Simba SC, Kamati ya Nidhamu imefikia uamuzi huo baada ya klabu ya Etoile du Sahel kupuuza kuilipa klabu ya Simba SC kiasi cha dola za kimarekani 300,000 za uhamisho wa mchezaji wa Emmanuel Okwi uliofayika Januari 2014.

Katika barua hiyo ya maamuzi ya kikao hicho, Kamati ya Nidhamu imesema baada ya siku sitini (60) zilizotolewa kwa klabu ya Etoile kuwa imeilipa Simba SC kumalizika bila malipo hayo kuwa yamaefanyika, wataagiza Etoile du Sahel kukatwa pointi sita katika michezo yake ya Ligi Kuu ya Tunisia.

Na kama klabu ya Etoile itashindwa kulipa deni hilo hata baada ya kukatwa pointi sita, Kamati ya Nidhamu ya Fifa itaamua kuishusha daraja klabu hiyo kutoka Ligi Kuu mpaka ligi daraja la kwanza.

Chama cha Soka nchini Tunisia (FTF) kimekumbushwa kutekeleza maelekezo hayo ya Kamati ya Nidhamu ya Fifa ya kuipokonya pointi sita Etoile du Sahel, na endapo FTF itashindwa kufanya hivyo basi itafungiwa kujishugulisha na shughuli zote za mpira zinazosimamiwa na Fifa.

Aidha Kamati ya Nidhamu ya Fifapia imeigiza klabu ya Etoile du Sahel kulipa faini ya dola za kimarekani 20,000 ndani ya siku sitini (60) baada ya kupokea uamuzi huo wa kamati.

TFF imepewa jukumu la kuhakikisha Simba inalipwa deni hilo ndani ya muda uliopangwa wa siku sitini (60) na endapo klabu ya Etoile du Sahel itashindawa kufanya hivyo basi TFF iitarifu kamati ya nidhamu ya Fifa juu ya suala hilo.


Kikao hicho cha Kamati ya Nidhamu kiliiongozwa na Mwenyekiti Claudio Sulser (Uswisi), Makamu Mwenyekiti Kia Tong Lim (Singapore), na mjumbe Fiti Sunia (Visiwa vya Samoa)

Mwenza wako kutoshinda nyumbani ni tatizo

$
0
0


Ni Jumatatu nyingine tunakutana wanajamvi wa XXLove katika kujifunza namna ya kukabiliana, kuzielewa na kuziishi changamoto mbalimbali tunazokutana nazo kwenye uhusiano, lengo likiwa ni kuboresha uhusiano huo na kuufanya uwe bora na wa kuigwa kwa mwaka huu wa 2016 na miaka mingine mingi tutakayojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Wanawake wengi wamekuwa wakiwalalamikia wapenzi wao kutokushinda nyumbani hasa siku za mapumziko, binafsi ninaamini kutokushinda huko kwa wanaume majumbani mwao kunachangiwa na vitu vingi sana ambavyo vinaweza kuwa ni vidogovidogo ila vyenye kukwaza.
Hakuna kitu kidogo, ila kizuri kinachopendwa na wapenzi wengi, hasa wa kike kama mpenzi, mchumba au mume wake kushinda nyumbani siku za mapumziko, wanawake wanapenda sana ‘kupetiwapetiwa,‘ wanapenda kupita mbele ya wenza wao wakijitingisha walivyojaliwa ili wenza wao waone. Wanapenda kupata muda wa kuzungumza na wenza wao kuhusu maendeleo ya familia yao japo kwa wiki mara moja na kuendelea.
Tatizo linaloonekana ni kwamba wanaume wengi huwa hawako tayari kubaki nyumbani kwa muda mrefu, siku ya/za mapumziko kwa kuhofia malumbano ya hapa na pale.
engine ni kwa sababu ya tabia za mwenza wake (wewe mwanamke), anaamini kwa jinsi ulivyo akisema ashinde tu ndani basi siku haiwezi kuisha bila kushikana shati au kutukanana, hivyo anaona bora kwenda zake kwa washkaji au baa kula masanga ili akirudi nyumbani muda wa migongoro na malumbano uwe angalau umepungua kidogo.
Ushauri wangu, angalia na rekebisha mapito yako, jiulize ni nini? Tabia ipi? kero au karaha zipi kwa mwenza wako zinazomfanya asishinde nyumbani au pengine ni tabia yako ya kidomodomo, gubu au kisirani?
image_1440378020_39411389Ukiweza kujua vyanzo vinavyomfanya mwenza wako asishinde nyumbani, itakuwa ni vizuri sana na kama utavifanyia kazi basi naamini mapenzi yako kwa mwaka 2016 yatakuwa matamu mno na yenye furaha.
Ingawa siyo wote wanakimbia kero za wenza wao, wanaume wengine ndiyo wanapopatia sababu ya kufanya mambo yao kama kula masanga, kukutana na marafiki, kufanya dili zao za nje ya ofisi na hata kuchepuka kwa wenye tabia hiyo.
Hebu fanya mwaka 2016 kuwa wa neema kwako, kama ni mwanamke jirekebishe, nawe mwanaume badilisha baadhi ya tabia zako, pengine ndizo chanzo kikubwa cha malumbano yenu yanayosababisha ninyi kukwidana, kutengana nakadhalika.
Kwa kuzingatia na kuufanyia kazi upungufu wenu ni hakika mtakuwa kama mnalipevusha upya penzi lenu, mwanamke badilisha vijitabia vyako vya ajabu, mwanaume pia fanya utaratibu wa kupumzika nyumbani siku ya mapumziko, watoto, mwenza wako wanakuhitaji, hata mifugo yako kama ng’ombe na mbwa nayo inakuhitaji ndiyo maana siku ukitaka kuipa chakula huwa inafurahi sana kwa sababu inahitaji uwepo wako.
Mpenzi msomaji kama umewahi kukumbana na tatizo nililolieleza hapo juu, tafadhali tuma maoni yako na yatatoka wiki ijayo kwenye kona hii. Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook, Instagram na kundi la WhatsApp kujua mengi kuhusu mapenzi.

Umeshajua unapendwa, unatikisa kiberiti ili iweje?

$
0
0


Mada ya leo, kuna kawaida ambayo si rasmi imejijenga kwa mtu akishagundua anapendwa. Anajaribu kumtikisa mwenzake ili kupima tu ule upendo kutoka kwa mwenzake. Anajaribu kufanya jambo ambalo anajua kabisa hata haliwezekani katika hali ya kawaida, yeye atafanya tu ili aone utasemaje.
Tabia hii ipo kwa wanawake na wanaume lakini zaidi hufanya na wanawake. Mwanamke anakuwa anajua anapendwa, anatambua mpenzi au mume wake anampenda lakini anajaribu kumchokonoa ili kuona kama anapendwa kweli. Hiyo ndiyo furaha yake.
Mfano, anaweza kumuambi; ‘mbona kuna mtu kaniambia amekuona baa ukiwa na mwanamke.’ Anauliza swali hilo akiwa anajua kabisa si kweli. Anajua shughuli za mpenzi wake za kila siku namna ambavyo zinambana.
Hajakaa sawa, anajua mpenzi wake amechoka lakini badala ya kumpa pole ya kazi na kumfariji kwa namna inayofaa, anamuambia; ‘naomba ukanichotee maji bombani.’
Huo ni mfano tu. Mwanamke huyo anakuwa haumwi, mzima wa afya. Anatambua fika mpenzi wake amechoka kwa wakati huo lakini anamjaribu hivyo ili asikie atajibu nini.
Anaweza kujua kwamba mpenzi wake hapendi kitu fulani, kwa makusudi anakifanya hicho kitu ili kuona mpenzi wake atachukua hatua gani.
Hao ndiyo wanawake. Kwa upande wa wanaume pia wapo wa aina hiyo.
Akishagundua anapendwa, anaanza kutikisa kiberiti kwa kumjibu vibaya mpenzi wake. Anafanya vile akiamini kwamba kwa vile mpenzi wake anampenda sana, hawezi kufanya lolote. Analeta pozi tu makusudi moyoni akitoa kauli za ‘hapindui huyu…ameshakolea kwangu.’
Marafiki zangu, hapa lazima tujifunze kitu! Ukiona unapendwa sana na mwenzako, unapaswa kurejesha upendo kama au zaidi ya huo unaooneshwa na mwenzako. Unapaswa kuthamini penzi la mwenzako kwa hali na mali. Huna sababu ya kutikisa kiberiti, unaweza kufanya hivyo halafu ikawa ugomvi mkubwa utakaosababisha akuchukie kabisa.
Kumtikisa mwenzako siyo sifa. Umeshajua mwenzako anakupa upendo wa dhati, kwa nini na wewe usimuoneshe kama unampenda? Mapenzi ni hiari, kama mlikubaliana, mkapeana mikakati yenu, kwa nini msumbuane kwa vitu vya kipuuzi? Faida ya kuishi kwa amani na furaha katika uhusiano si ya mtu mmoja bali ni yenu wote.
Kama mmepanga safari ya kuelekea kwenye ndoa, hakuna haja ya kupimanapimana. Msichezeane hisia. Wewe mwenzako anakuwa ameshawekeza nguvu, akili na upendo wake, usimtafutie ‘visababu’ vya ajabu vitakavyosababisha ugomvi kila wakati.
Kwa leo ni hayo, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri ya kusisimua!

Lionel Messi atwaa tuzo ya Ballon d'Or

$
0
0


 Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona, na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, ametwaa tuzo ya mchezo bora wa dunia.
Messi mwenye miaka 28 alishinda kwa 41.33% kwa kura zote zilizopigwa, huku Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya pili kwa 27.76% na Neymer akipata 7.86%.
Hii ni mara yake ya tano kutwaa tuzo hiyo.
Kwa upande wa wanawake nyota wa Marekani Carli Lloyd, ameibuka kuwa mchezaji bora kwa upande wa wanawake.
Goli bora la mwaka likifahamika kama Puskas limwendea Wendell Lira anayekipiga katika Atletico Goianiense ya Brazil.
Kocha wa Barcelona Muhispania Luis Enrique amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa kuiongoza barca kufanya vizuri barani Ulaya kwa kutwa mataji matano msimu uliopita.
Jill Ellis kocha wa kikosi cha taifa cha Marekani amekuwa kocha bora wa wanawake baada ya kuongoza timu ya taifa ya Marekani kufanya vyema katika michuano ya kombe la dunia.

KWA PICHA ZAIDI
BONYEZA HAPA ===> bit.ly/1IZM1UE

Gari la mchungaji Msigwa lazua balaa

$
0
0

DAR ES SALAAM: Gari la kifahari linalodaiwa kuwa ni la Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa limezua balaa kufuatia mwandishi wetu kumpigia simu ya kutaka kumuuliza swali ambalo lilitoka kwa wapigakura wake kufuatia madai kwamba amelinunua gari hilo kwa shilingi milioni mia mbili.
Jumapili iliyopita, mwandishi wetu alimwendea hewani mbunge huyo na kuanza kwa kumpa hongera kwa kununua gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser V8.
Mchungaji: Nenda kwenye pointi.
2016-Toyota-Land-Cruiser-facelift-front-three-quarter-unofficial-render (1)Mwandishi: Kuna habari kwamba umenunua gari la kifahari wakati uliwahi ‘kumchana’ aliyekuwa mbunge wa jimbo lako…
Mchungaji: (anafoka) Mbona nyinyi waandishi mnafuatafuata habari za watu? Hamjui kuwa mimi nina vitu vya thamani vingi kuliko hili gari!
Mwandishi: Hapana, hayo ni malalamiko ya wapiga kura wako, wanasema kwamba wewe uliwahi kumsema aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Iringa, Monica Mbega kwamba …
Mchungaji: (anafoka tena) Mnataka kuni-intimidate (kunitisha)? Mimi kuwa na gari hata kama lingekuwa la thamani ya shilingi milioni 500 kuna ajabu gani? Au mnataka kusema nimehongwa na… (anamtaja waziri mmoja wa zamani.)
Mwandishi: Mchungaji unakwenda mbali, haya ni malalamiko ya wapiga kura wako. Ungesikiliza kwanza…
Mchungaji: (anafoka zaidi) Hakuna! Ndiyo maana nyie waandishi wa habari mnakufa masikini. Kazi yenu kufuatafuata maisha ya watu.
Simu inakatika, mchungaji akapiga yeye, mwandishi akampa mhariri wake azungumze…
Mhariri: Mchungaji mbona unazungumza maneno mazito sana?
Mchungaji: (akiwa hajui kwamba sasa anaongea na mhariri wa gazeti) Hakuna, nyinyi hamjui kuwa mke wangu ni mtu mkubwa sana benki ya… (anaitaja jina). Ana uwezo, tena ana mshahara mkubwa kuliko wa wabunge. Nina mashamba makubwa mbona hujanipa hongera? Una uhakika gani kuwa hili ni gari langu?
Mhariri: Ndiyo maana tukakuuliza. Basi kama nimekosea, nisamehe mimi saba mara sabini mchungaji.
Mchungaji: Tena hizo habari mziandike hivyohivyo, wekeni ukurasa wa kwanza kabisa (akakata simu).

CHANZO: GPL

CCM wajibu mapigo Z’bar, uchaguzi upo pale pale

$
0
0

 Makamu wa pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi

SAA chache baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza kasoro na athari za kurudia Uchaguzi uliofutwa kinyume cha sheria na Jecha Salim Jecha, viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wametangaza kuwa uchaguzi utarudiwa.Anaandika Josephat Isango … (endelea).
Wakizungumza na vijana wa chama hicho katika viwanja vya Maisara viongozi wa juu wa chama hicho wamesisitiza kuwa uchaguzi wa Zanzibar upo pale pale na utarudiwa kadiri tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) itakavyotangaza.
Wa kwanza kutoa msimamo huo alikuwa ni Makamu wa pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, aliyesema kuwa uchaguzi huo utarudiwa hata ikiwezekana vyama vyote vikijitoa CCM kitashiriki peke yake
“Uchaguzi wa marudio upo pale pale, tunajua uchaguzi ulifutwa kihalali, mjitayarishe kwa uchaguzi wa marudio. CUF wamesema watatumia nguvu ya umma, tunawakaribisha na wataona matokeo yake” alisema Balozi Iddi.
Katika mkutano huo uliokuwa unarushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha ZBC, Dk  Alli Mohamed Shein alipongeza msimamo wa Balozi Iddi, na kusema atabaki kuwa rais hadi uchaguzi utakaporudiwa.
Dk Shein alisema yupo madarakani kwa kushauriwa na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kwamba hajavunja katiba na kama itatokea mahakama ikatoa ufafanuzi kuwa anakosea kuwepo hapo kikatiba basi ataondoka madarakani
“Mahakama ikisema nakosea nitaondoka, Rais yupo Baraza la Mapinduzi lipo na Mawaziri wapo, nitaita waandishi wa habari Ikulu na mimi nimjibu Maalim Seif kwani kuna mengi amenisingizia” alisema.

Muna love amshinda LULU kwa kupiga pamba za ukweli picha 10 zipo hapa

Mtanzania Muna Love aonyesha urembo wake kwa picha hizi

$
0
0

Mrembo MUNA ALPHONCE 'MUNAMAPENZ' ameonyesha urembo wake kweli kwa picha hizi katika pozi mbalimbali.
KUONA PICHA ZAKE ZAIDI YA 20 
BONYEZA HAPA ==>bit.ly/1ZhsQb0
KUONA PICHA ZAKE ZAIDI YA 20 
BONYEZA HAPA ==>bit.ly/1ZhsQb0

Taarifa ya Uteuzi wa Wabunge Kwenye Kamati za Kudumu Za Bunge

$
0
0

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA WABUNGE KWENYE KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE.

Katibu wa Bunge anatoa taarifa kwa umma kwamba:

(a) Kwa mujibu wa Kanuni ya 116 (3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano amepewa mamlaka ya kuteua Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa namna ambayo itawezesha kila Mbunge kuwekwa kwenye Kamati mojawapo. Katika kufanya uteuzi huo, Spika huzingatia vigezo mbalimbali vilivyoainishwa katika Kanuni ya 116 (5);

(b) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mhe. Job Yustino Ndugai (MB), ametekeleza mamlaka yake ya uteuzi kwa mujibu wa Kanuni tajwa hapo juu, kwa kuwateua kwanza Wabunge Kumi na Tano (15) kuwa Wajumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge.

 Kamati hiyo imeundwa na kutangazwa kabla ya Kamati zingine ili ifanye marekebisho ya Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge kuhusu majukumu ya Kamati zingine za Bunge kwa kuyashabihisha na majukumu ya Serikali kwa kuzingatia Muundo wa Baraza la Mawaziri lililopo sasa.

 Lengo kuu ni kuleta urahisi, ufanisi na tija kwa Bunge katika kuisimamia na kuishauri Serikali;

(c) Kwa msingi huo, Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge, ambayo Spika ndiye Mwenyekiti wake na Naibu Spika ni Makamu Mwenyekiti, Kiongozi wa Upinzani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao ni Wajumbe kwa nyadhifa zao itakutana katika Ofisi ya Bunge, Dar es Salaam siku ya Ijumaa tarehe 15 Januari, 2016 saa tano kamili asubuhi katika Ukumbi wa Spika. Wajumbe wengine ni: -
 
(i) Mhe. Makame Kassim Makame, MB. - Jimbo la Mwera;

(ii) Mhe. Tundu Antipas Mughwai Lissu, MB. - Jimbo la Singida Mashariki;

(iii) Mhe. Jasson Samson Rweikiza, MB. - Jimbo la Bukoba Vijijini;

(iv) Mhe. Ally Saleh Ally, MB. - Jimbo la Malindi;

(v) Mhe. Magdalena Hamis Sakaya, MB. - Jimbo la Kaliua;

(vi) Mhe. Salome Wycliff Makamba, MB. - Viti Maalum;

(vii) Mhe. Dkt. Jasmine Tiisekwa Bunga, MB. - Viti Maalum;

(viii) Mhe. Zainab Athman Katimba, MB. - Viti Maalum;

(ix) Mhe. Balozi Adadi Mohamed Rajab, MB. - Jimbo la Muheza;

(x)Mhe. Dkt. Charles John Tizeba, MB. - Jimbo la Buchosa; na

(xi) Mhe. Kangi Alphaxard Lugola, MB. - Jimbo la Mwibara.

(d) Spika atakamilisha uteuzi wa Wajumbe katika Kamati zingine za Bunge kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Pili wa Bunge tarehe 26 Januari, 2016, Mjini Dodoma ili kutoa fursa kwa Kamati zote kuchagua Viongozi wake na kuandaa Mpango Kazi kwa mwaka 2016/17; na

(e) Wabunge wote wanatangaziwa kuwa wawe wamefika Dodoma tarehe 20 Januari, 2016 tayari kwa kuanza kwa Kamati za Bunge na Mkutano wa Bunge, isipokuwa Kamati ya Wabunge (Caucus) wote wa Chama cha Mapinduzi wanatakiwa kuwa Mjini Dodoma tarehe 17 Januari, 2016 kwa Mkutano wao.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
Ofisi ya Bunge,
S. L. P. 9133,
DAR ES SALAAM.
11 Januari, 2016.

Magazeti ya Tanzania Leo Jumanne ya January 12, 2016

Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>