Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

BEAUTIFUL ONYINYE- WEMA SEPETU KATIKA POZI TOFAUTI


TIMU TAJIRI DUNIANI ZIPO HAPA

$
0
0

1. Real Madrid - £444.7m
2. Barcelona -£413.6m
3. Bayern Munich-£369.6m
4. Manchester Utd-£363.2m
5. Paris Saint-Germain-£341.8m
6. Manchester City-£271m
7. Chelsea-£260m
8. Arsenal-£243.6m
9. Juventus-£233.5m
10. AC Milan -£225.8m   

CHELSEA YAMPATA MRITHI WA MATA MAPEMAA

$
0
0
KLABU ya Chelsea imeipiga bao Liverpool katika kuwania saini ya mshambuliaji wa FC Basle, Mohamed Salah baada ya kumnasa kwa dau la Pauni Milioni 11.
 Dili imetiki: Chelsea imemsaini nyota wa Basle, Mohamed Salah, ambaye aliwafunga mabao marmbili msimu huu

Wekundu wa Anfield walikuwa mbioni kumsajili mshambuliaji huyo wa Misri na mazungumzo yalikuwa katika hatua nzuri hadil Chelsea ilipopiga gia kubwa na kumpokonya tonge mdomoni Brendan Rodgers Jumatano.

Huku Juan Mata akiwa njiani kuhamia Manchester United, The Blues inataka kuziba pengo la Mspanyola huyo kupitia Salah, ambaye aliwavutia katika Lifgi ya Mabingwa msimu huu kwa kuwafunga katika mechi zote za makundi likiwemo la ushindi nchini Uswisi.

VUMBI LIGI KUU KUTIMKA WIKIENDI

$
0
0
Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza kesho (Januari 25 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazochezwa katika miji ya Bukoba, Dar es Salaam na Tanga.
Mabingwa watetezi Yanga watakuwa wageni wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati kwenye jiji hilo hilo Uwanja wa Azam Complex kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Azam FC na Mtibwa Sugar kutoka Morogoro.

Coastal Union na Oljoro JKT zitaumana kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Kagera Sugar ikiikaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Raundi ya 14 ya ligi hiyo itaendelea Jumapili (Januari 26 mwaka huu) kwa mechi mbili. Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa shuhuda wa mechi kati ya Simba na Rhino Rangers kutoka Tabora wakati maafande wa JKT Ruvu na Mgambo Shooting watapambana Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Viingilio kwenye mechi ya Ashanti United na Yanga vitakuwa sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Viingilio mechi ya Mkwakwani vitakuwa sh. 10,000 kwa sh. 3,000, Uwanja wa Azam Complex sh. 10,000 kwa sh. 3,000, Uwanja wa Kaitaba ni sh. 5,000 kwa sh. 3,000.

MWANADADA JACQUELINE DUSTAN ANG’ANG’ANIA KUZAA NA MZUNGU

$
0
0
Mwanadada Jacqueline Dustan ambaye ni msanii wa filamu aliyeibukia kwenye Shindano la Maisha Plus season II, ameonekana kung’ang’ania kuzaa na Mzungu kufuatia maelezo yake kwamba harudi Bongo mpaka atundikwe mimba na mtasha.
Jacqueline Dustan.
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa nchini Thailand, Jack alisema uwepo wake nchini humo kwa muda mrefu anajilengesha kwa mwanaume wa Kizungu ambaye atampenda na ikiwezekana amzalie mtoto.
“Kwa kweli nitarudi Bongo endapo tu nitapata mtoto mmoja wa kitasha, sasa niko bize kutafuta mchumba ambaye ni salama kwangu ili niweze kupata naye mtoto mmoja tu,” alisema Jack.

Ni takriban mwezi wa sita sasa msanii huyo yuko nchini humo huku anachokifanya kikiwa hakijulikani licha ya kuwepo kwa madai kuwa, wasanii wengi wanaokwenda huko wanajiuza.

TAMKO LA YANGA KUHUSU SUALA LA OKWI

$
0
0
Hati ya Usajili wa Emmanuel Okwi kama inavyoeneka kwneye system ya CAF.
Uongozi wa klabu ya Young Africans umeamua kuweka hadharani ukweli kuhusiana na usajili wa mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi ambaye kamati ya maadili na hadhi za wachezaji imemzuia kuichezea Young Africana mpaka watakapopata uthibitisho kutoka FIFA.

Young Africans ilikamlisha usajili wa mshambuliaji huyo tangu Disemba 15 mwaka 2013, na kupata hati ya uhamisho wake wa kimataifa (ITC) ambayo iliwasilishwa TFF pamoja na fomu mama za usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Baada ya kukamilisha zoezi hilo TFF ilipitisha jina lake kwa kutupatia leseni no: 921225001 ambayo inamruhusu mchezaji kuichezea Young Africans na kisha kulituma CAF Disemba 31, 2013 kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika  ambapo CAF nao walimuidhinisha kuwa mchezaji halali wa Young Africans kwa mashindano hayo.

Cha kustaajabisha siku mbili kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Kamati ya Maadili na hadhi za wachezaji wakamzuia mchezaji huyo kuichezea Young Africans ilihali akiwa ameshaidhinishwa na TFF na CAF kuwa mchezaji halali wa Young Africans.

Swali?? walikuwa wapi Kamati ya Maadili na Hadhi za Wachezaji kujiridhisha juu ya usajili ambao ulishakamilika tangu Disemba 15 2013?

Wanakuja kutoa maamuzi hayo mwezi mmoja na nusu baada ya dirisha la usajili kufungwa, ikiwa ni siku mbili kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom??

SAKATA LA MHESHIMIWA CATHY MAGIGE NA ZITTO KABWE...SOMA HAPA

$
0
0


 Cathy Magige.
Mheshimiwa Cathy Magige, amewataka wale wote wanamuhusisha kuwa na video yake akiwa Zitto Dubai kuitoa kwa public au popote inapoweza kuonekana na Wananchi ili ukweli uonekane wazi kuliko wanachokifanya sasa hivi yaani kumchafulia jina bila sababu. Mheshimiwa Cathy, Mbunge wa Viti Maalum Vijana CCM aliyasema hayo leo kwa simu akiongea na Blogu hii kwamba amesshitushwa sana na ujumbe wa simu ambao umekuwa ukisambazwa kila kona ya Tanzania na hata kumfikia Dada yake aliyeko Ohio, ambaye alimtumia mara moja baada ya kupokea tu ujumbe huo. Pamoja na maelezo mengi sana yakumtukana Zitto ujumbe huo unasomeka hivi:-

"Hii email itapokewa na zaidi ya watu 50. Nimeifanya makusudi, na kama unabisha haukwenda Dubai na Catherine Magige, niko tayari kuweka scanned copies ticket zenu na video zenu za siri mkiwa huko"

Mheshimiwa Magige, anawaomba wale wanaohusika na kusambaza ujumbe huu mitandaoni na kwenye simu za watu wajitokeze na kutoa ushahidi huo wa Video na copy za Ticket walizosafiria kama ni kweli wanazo ama sivyo waache uzushi huo ambao anasema hauna maana na wala hauna ukweli wowote. Mheshimiwa anasisistiza kwamba tatizo lao ni Zitto sasa haelewi ni kwa nini wanajaribu kuchafua na wengine wasio na makosa kama yeye, anarudia tena kwa wale wote wanaodai kuwa na huo ushahidi wa yeye kuwa na Zitto, popote pale watoe ushahidi huo ili ukweli uonekane wazi na wananchi wote badala ya uzushi usio na maana wenye nia ya kumchafulia jina.   
Chanzo ni  http://williammalecela.blogspot.com

NAFASI ZA KAZI KADA YA AFYA


MOURINHO: CHELSEA HAIKUWA NA UWEZO WA KUMZUIA MATA KUHAMIA MAN UNITED

$
0
0
KOCHA Jose Mourinho amesema Chelsea haikuwa na nguvu kumzuia Juan Mata kujiunga Manchester United.
Mspanyola huyo amekwenda kufanyiwa vipimo Old Trafford ili rasmi awe mchezaji wa United atakapozufu. 
Dau la Pauni Milioni 37 tayari limesainiwa na klabu zote na vipengele binafsi vya Mkataba vimefikiwa na mchezaji huyo.
Mata atakuwa tayari kuanza kuitumikia timu ya David Moyes katika mechi na Cardiff City Jumanne.  

Ameondoka: Kiungo Juan Mata anaelekea kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 37 kutua Manchester UnitedBlessing: Jose Mourinho said the club had to be 'respectful' of Mata as his move to United draws near
Baraka zote: Jose Mourinho amesema hakuwa na uwezo wa kumzuia Mata kuhamia United

Dk Kigwangalla hatarini CCM

$
0
0
Dar es Salaam.
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangalla yuko hatarini kuvuliwa uanachama wa chama hicho, hatua ambayo endapo itachukuliwa itasababisha apoteze nafasi yake ya ubunge.
 Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangalla akichangia jambo bungeni siku za hivi karibuni mjini Dodoma. Picha na Maktaba 

Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Nzega mkoani Tabora tayari umemjadili Dk Kigwangalla katika vikao vyake vya Kamati za Usalama na Maadili na Kamati ya Siasa, kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu wa mbunge huyo.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana jioni zinasema baada ya vikao hivyo vilivyofanyika Januari 11 mwaka huu, imeazimiwa kuwa suala la Dk Kigwangalla pamoja na madiwani watano wilayani humo lipelekwe katika ngazi ya CCM mkoa na baadaye taifa.

Dk Kigwangalla jana alipotafutwa kuzungumzia suala hilo alisema: “Hata mimi nimesikia taarifa hizo, isipokuwa sijapewa taarifa rasmi. Ila nafahamu kwamba vikao vya chama vilikuwepo na mimi niliitwa ila kama ambavyo nimeshasema siwezi kuhudhuria”.

Gazeti hili lilimtafuta Mbunge huyo machachari kutokana na taarifa yake aliyoitoa kwenye mitandao ya Facebook na Tweeter akieleza kuhusu taarifa za kuwapo mpango wa kumfukuza uanachama.
Kupitia mitandao hiyo Dk Kigangwalla aliandika: “Nimepokea taarifa kuwa madiwani walioungana na wananchi wa Nzega pamoja na mimi kupinga uamuzi wa Baraza la Madiwani kuzigawa pesa kwenye Kata wameadhibiwa na Kamati ya Siasa ya Chama Wilaya ya Nzega, bila kusikilizwa na ilhali miongoni mwa ‘mahakimu’ hawa ni watu waliokuwa wakilalamikiwa na madiwani na wananchi. “

Mbunge huyo aliongeza: “Nimepewa taarifa kuwa mapendekezo ya adhabu dhidi yangu kutoka wilayani kwenda vikao vya juu, ...tena bila kusikilizwa maana nilitoa udhuru, ni kuwa ninyang’anywe kadi ya uanachama wa CCM. Nimeshangazwa sana na kusikitishwa na jinsi chama kinavyoendeshwa Nzega.”

Mbunge huyo alisema anaamini viongozi wakuu wa CCM wanafuatilia kwa karibu suala hilo na watachukua hatua stahiki, huku akisema hatahudhuria tena kikao chochote cha CCM wilayani humo.
“Kama chama hiki kimefika huku, kwamba kuna watu wana nguvu kuliko chama, kwamba wachache wanaweza kuwaonea wengine kwa kuwa wana vyeo na mamlaka ya kufanya hivyo na hakuna wa kuingilia kati na kusema ‘no’, basi sina haja ya kuendelea kupambana,” aliongeza.

Aliendelea: “Nimechoka, sintokata rufaa wala sintolalamika tena. Watekeleze hukumu hiyo. Sintojitetea na sintohudhuria kikao chochote kile kuanzia sasa, nimechoka kupambana na watu wenye nguvu, nimechoka. Ni bora kuwa mnyonge, lakini ukabaki na uhai, uzima, heshima na furaha yako”.

Kauli ya CCM Nzega
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nzega, Amos Kanuda alikiri Dk Kigwangwalla kujadiliwa katika vikao vya chama vya wilaya, ikiwamo Kamati ya Siasa.
Alisema makosa ya Mbunge huyo ambayo yalijadiliwa katika kikao hicho ni kufanya mkutano wa hadhara na kuwaporomoshea matusi madiwani wenzake ambao hawakuwa upande wake wakati wakijadili mgawo wa fedha.

Mwenyekiti huyo alisema CCM baada ya kuona mgogoro huo wa madiwani wake unakua, kiliamua kuwajadili watuhumiwa na kwamba uamuzi wa kikao hicho ni siri.
Alisema CCM bado inaendelea kumjadili mbunge huyo na kwamba kikao kingine kitafanyika Februari mosi mwaka huu.

Alisema uamuzi wa kikao hicho utapelekwa CCM Mkoa wa Tabora na wao watalijadili na kupeleka mapendekezo yao chama taifa.

Chimbuko la mgogoro
Mgogoro uliokigawa CCM katika Wilaya ya Nzega, unatokana na tofauti za kimtazamo kuhusu jinsi ya kutumia fedha Sh2.3 bilioni zilizotolewa na Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Resolute kama kodi ya huduma kwa halmashauri ya wilaya hiyo.

Dk Kigwangalla pamoja na madiwani kadhaa wanapinga kupindishwa kwa azimio la Baraza la Madiwani ambalo lilielekeza fedha hizo zitumike kuanzisha Benki ya Jamii ya Nzega (Nzega Community Bank Ltd - NCB) na Kampuni ya Ujenzi ya Jamii ya Nzega (Nzega Community Construction Corporation Ltd - NCCCL).
Lengo la Kampuni ya NCCCL lilikuwa ni kujenga uwezo kwa kuwa na vifaa vya ujenzi wa barabara za halmashauri na mashine ya uchimbaji wa visima kwa ajili ya huduma za maji.

Hata hivyo, wakati utekelezaji wa azimio hilo ukiwa umeanza, Januari 4 mwaka huu kiliitishwa kikao cha dharura kwa lengo la kubadili maazimio ya awali.
Zamu hii madiwani wakiungwa mkono na uongozi wa CCM wa wilaya walikuja na mpango kwamba fedha hizo zigawanywe kwenye kata, azimio ambalo linapingwa vikali na baadhi ya madiwani wakiongozwa na mbunge huyo.

Baada ya azimio jipya kupitishwa, Dk Kigwangalla aliitisha mkutano wa hadhara na kuwahutumia wananchi na mwishoni mwa mkutano huo wananchi waliazimia kufungua kesi mahakamani kuzuia kutumika kwa fedha hizo.
CHANZO NI MWANANCHI

Ferguson aitabiria makubwa Man Utd

$
0
0
London, England.
Sir Alex Ferguson anaamini bado Manchester United ina nafasi ya kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu.
Klabu hiyo ya Old Trafford ipo nafasi ya saba kwa sasa wakiwa nyuma kwa pointi 14 kwa vinara wa ligi Arsenal ukiwa imebakia michezo 16.

Lakini Ferguson, ambaye amestaafu kuifundisha United Mei mwaka jana, amesisitiza kuwa mabingwa hao bado wanaweza kutetea taji hilo.

“Sijaifuta timu yoyote katika mbio hizi,” alisema kocha huyo mwenye miaka 72 na kuongeza kuwa United ya sasa inayofundishwa na David Moyes, itakuwa bora zaidi katika kipindi hiki kilichobakia cha msimu.

Ferguson alizipongeza timu sita za juu yaani Arsenal, Manchester City, Chelsea, Spurs, Everton na Liverpool, lakini alisema United bado “ipo nyuma yao katika mbio hizo”.
Vigogo hao wa Old Trafford wakiwa na mwenendo wa kusuasua tangu Moyes alipochukua jukumu la kuifundisha timu hiyo wakiondolewa katika Kombe la FA na Kombe la Ligi, japokuwa wamefuzu kirahisi kwa 16 bora ya Ligi ya Mabingwa.

United pia imefungwa mara tatu mfululuzo kwa mara ya kwanza tangu 2001 wakati waliponyukwa katika siku saba za kwanza za Januari, wakilala mbele ya Tottenham, Swansea na Sunderland.
Pia kwa sasa wapo nyuma kwa pointi sita kwa Liverpool inayoshika nafasi ya nne hivyo wapo kwenye uwezekano wa kukosa kucheza Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu 1992.
Ferguson alisema: “Napata wakati mgumu kuingia nne bora.

Napata wakati mgumu zaidi kusema nani atanyakuwa ubingwa wa ligi.”
Moyes amefuzu mara moja kucheza Ligi ya Mabingwa akiwa na Everton pale 2005, lakini alitolewa na Villarreal katika mechi za mtoano.

Moyes mwenye miaka 50, alichukua jukumu la kuifundisha United baada ya kukaa miaka 11 ndani ya Goodison Park kabla ya Ferguson kumteua kama mrithi wake Old Trafford.

Bodi ya Ligi yaionya Yanga

$
0
0
Dar es Salaam. 
Bodi ya Ligi Kuu imewapiga mkwara uongozi na wanachama wa Klabu ya Yanga kutothubutu kufanya hujuma kwenye mitambo ya Kituo cha Televisheni cha Azam.
Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Silas Mwakibinga alisema kuwa atakayehusika kwa namna yoyote kufanya vurugu au hujuma, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Mwakibinga alisema vyombo vya usalama vimejiandaa kutoa ulinzi mkali uwanjani hapo na kwamba wataofanya vurugu watakamatwa na kufikishwa mahakamani.

DIAMOND PLATINUMZ, HAMISA MOBETO WANADAIWA KUWA WAPENZI

$
0
0

Hamisa Hassan Mobeto ambaye ni model na actress anayesusua katika tasnia ya filamu nchini anadaiwa kuwa mapenzini na Diamond Platinumz a.k.a Sukari ya warembo huku uhusiano wao ukidaiwa kuwa wa muda mrefu tu ila wamefanya kuwa siri. 


 Hamisa Hassan Mobeto.


Chanzo kimoja kilichodai kuwa karibu na Hamisa ambaye alishawahi kushiriki Miss Tanzania kiliuambia mtandao huu "Hivi mnajua kuwa Diamond anawachanganya kwa wakati mmoja Wema na Hamisa Mobeto?, Hamisa na Diamond ni wapenzi muda sasa but wanafanya siri, Hamisa anamwangalia tu Wema akiwewesekea penzi la Diamond huku yeye akijilia vyake".

Hamisa alipotafutwa na mtandao huu ili kutolea ufafanuzi madai hayo hakuweza kupatikana.

MTOTO WA ROSE NDAUKA HUYU HAPA

HAPPY BIRTHDAY NICOLAUS TRAC


KIGOGO WA WEMA NOMA SANA!

$
0
0
NOMA sana! Baada ya kupigwa cha mbavu (kuachwa) na Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu huku akimnyang’anya vitu vyote vya ofisini, yule kigogo wa ikulu, Clement a.k.a CK, hivi sasa anadaiwa kutoka na shosti wa staa huyo, Naima Shaa.
Naima Shaa.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti namba moja la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda, Naima anatamba na kuwapiga vijembe wasichana wa mjini kuwa anatoka na CK mwenye mkwanja mrefu (bado fedha hazijaisha).

Nakwambia hatunywi maji, mtoto kadata kabisa hadi ameamua kujichora ‘tatuu’ ya jina la Clement  kwenye bega lake la kulia. Inahusu?” kilihoji chanzo chetu.
Wema Sepetu.
NI MTOTO WA MBUNGE
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa Naima ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shaa (CCM) hivi sasa anaonekana na mdogo wa CK huku wakiitana shemeji wa ukweli.
“Sasa hivi jamaa anajilia vyake mdogomdogo kwa mtoto Naima pale kati, naona ameamua kumalizia machungu ya Wema kwa Naima.
“Unaambiwa nyuma ya pazia stori ni kwamba anataka Wema aumie ndiyo maana ameamua kubanjuka na Naima huku akijua kabisa kuwa ni marafiki.
“Unajua kama mtu akikuumiza kimapenzi, ukitembea na rafiki yake naye anaumia vibaya mno. Kwani hukumbuki ilivyokuwa kwa Penny (Penniel Mungilwa) alipochukuliwa na Diamond (Nasibu Abdul)? Ilikuwa ni ili kumuumiza Wema na kweli walifanikiwa. Ndicho anachokifanya CK,” kilitiririka chanzo hicho.
WATU WAMEDATA
Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa Naima ambaye mara nyingi haoni soni kuonesha tatuu ya jina la Clement, amekuwa akijinadi kuwa yeye ndiye mrithi halali wa Wema na kwa sasa kigogo huyo haoni wala hasikii kwake.
 
Tatoo ya Clement mgongoni mwa Naima.
“Naima naye amedata kabisa na sidhani kama anaogopa Wema kujua kama yeye ndiye hasa anatembea na kigogo huyo kwa kipindi hiki,” kilisema chanzo hicho.
UNATAKA KUMSIKIA NAIMA?
Baada ya kupata taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Naima ili kuthibitisha madai hayo ambapo alikiri kumfahamu CK lakini akadai watu wanamsingizia.
Alipoulizwa kuhusu  tatuu aliyochora yenye jina la Clement, Naima alisema ameandika ‘Element’ na siyo ‘Clement’ (tazama picha, akili ya kuambiwa changanya na yako).
“Yeleuuuwi...jamani watu wananisingizia. Hii tatuu niliyochora nimandika jina Element na siyo Element (angalia maneno yanafafa! Moja alikuwa anamaanisha Clement),” alisema Naima na kukata simu.
WEMA ANAJUA CHOCHOTE?
Baada ya kuwasiliana na Wema kwa njia simu na kumuuliza kuhusiana na madai ya zilipendwa wake kulipiza kisasi kwa rafiki yake, Naima, alisema kuwa habari hizo ameshazisikia lakini anasikitika kwa kuwa kigogo huyo karuka majivu na kwenda kukanyaga moto.
Alisema kuwa ishu hiyo haimuumizi na zaidi sana anawaombea wawili hao maisha mema ya kimapenzi ilimradi moyo wake umeshatua kwa umpendaye.
“Moyo wangu ulishatulia kwa nimpendaye, nawatakia maisha mema,” alisema Wema.
NYUMA YA PAZIA
Uchunguzi wa gazeti ulibaini kuwa nyuma ya pazia la habari hii kuna mambo mengi ya namna CK na Naima walivyokutana.
“Ni Kinondoni pale Mwanamboka. Mke wa CK alikuwa na baa pale ambayo siku hizi imefungwa.
“Naima alikuwa ni mke wa mtoto wa Mwanamboka. Walikuwa wanakutana pale baa. Ndipo mambo yalikoanzia.
“Unajua hata Naima ameingia kwenye gogoro la kindoa na mumewe kwa muda mrefu. Kisa ni huyo CK. Ona sasa wote wamekosa ndoa. Sinema inaendelea,” kilimalizia chanzo chetu.
CHANZO NI GPL

PENNY: DIAMOND KAMA CHIZICHIZI VILE!

$
0
0
Penny alifunguka hayo mbele ya kinasa sauti ambapo mbali na kutamka kauli hiyo, alifunguka mambo mengi yaliyohusu penzi lao ambalo alilitaja kuwa wamelipumzisha kwa kupeana nafasi.
Akizungumzia sifa za staa huyo aliyeogelea naye penzini kwa kipindi cha mwaka mmoja na ushee hivi, Penny alisema watu wote wanamjua Diamond ni kama chizichizi vile kutokana na mapepe anayoyafanya akiwa mzigoni lakini linapokuja suala la uhusiano, anakuwa makini sana.

“Diamond ni kama chizichizi vile lakini kwa ndani ni mtu makini sana. Anajua kulea, anajua umuhimu wa mapenzi na anaelewa anatakiwa kumfanyia nini mpenzi wake anapokuwa nyumbani, anajali,” alisema Penny na kuongeza:
Penny.
“Watu wamuanavyo nje na jinsi alivyo katika maisha ya kawaida ni tofauti kabisa, mapepe anayafanya anapokuwa jukwaani na sehemu nyingine zinazohusu kazi yake na si nyumbani.”
Katika aya nyingine, Penny alitiririka na mistari kuwa, baada ya kuona penzi lao limetawaliwa na misukosuko, walikaa chini kwa pamoja na kuamua kupeana nafasi ya kila mmoja wao kufanya mambo yake, hakuna kati yao aliyemtamkia mwenzake kuwa sikutaki.
Alisema katika maisha huwa hapendi vitu vya kuambiwa, hata aliposikia taarifa za Diamond kurudiana na Wema kwa mara ya kwanza nchini China, hakuamini hadi walipokuja kukaa naye na kuzungumza ndipo walipoamua kupeana nafasi.
Diamond.
Hata hivyo, Penny alisema anaamini kuwa Diamond amerudiana na Wema lakini yeye kwa sasa ‘bado yupoyupo sana’, akakiri kuwa anatongozwa na watu tofauti na endapo ikitokea akaamua kuanzisha uhusiano mpya, hatahitaji mtu maarufu kwani anahitaji maisha yake kuwa ya siri, tofauti na zamani.

MCHUMBA MPYA WA ELIZABETH MICHAEL 'LULU' HUYU HAPA

$
0
0
Huyu ndo mchuma wa Lulu kwa sasa tutawaletea jina lake Siku za kariuni.

MZEE DUDE AFARIKI DUNIA

$
0
0
Mzee Dude enzi za uhai wake.
MSANII wa kundi maarufu la vichekesho na uigizaji la Futuhi, Mzee Dude amefariki dunia akiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando iliyopo jijini Mwanza siku ya jana jioni!
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!

MSIBA: MCD WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA!

$
0
0


Sudi Mohamed, 'MCD' (pichani, juu na chini) ambaye ni mpinga tumba maarufu nchini Tanzania amefariki dunia usiku huu akiwa Moshi ambako alikwenda kwa ajili ya matiabu zaidi yapata miezi mitatu iliyopita. Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa Bendi ya Twanga Pepeta, Meneja Hassani, MCD alipelekewa nauli ya kurudi jijini Dar esalaam leo ili arejee kesho lakini mauti yakamfika usiku mida ya saa tano na nusu. MCD amewahi kupiga katika bendi kadhaa za muziki wa dansi ikiwemo Mashujaa Band na African Stars ambako alirejea tena. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi - ameen!

Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>