Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

Pluijm awapa mtihani wa kwanza Yanga

$
0
0
KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, raia wa Uholanzi, ameupa mtihani wa kwanza uongozi wa klabu hiyo baada ya kusema anahitaji benchi lake la ufundi liboreshwe.
Hans ameanza kukinoa kikosi cha Yanga hivi karibuni baada ya kukifuata kikosi hicho nchini Uturuki akibeba mikoba ya Mholanzi mwenzake Ernie Brandts aliyetupiwa virago. Hans amesaini mkataba wa miezi sita.
Akizungumza  Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abadallah Bin Kleb, alisema kocha amefurahishwa na kikosi alichokiona lakini amehitaji marekebisho kadhaa katika benchi lake hilo la ufundi.
“Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata kutoka Uturuki, hali ya kikosi inaendelea vizuri na kocha amefurahia viwango vya wachezaji tofauti na alivyofikiria ambapo amefanya tathmini ya mchezaji mmojammoja.
“Ila amehitaji kuongezewa nguvu katika benchi la ufundi, vitu vingine anavyohitaji viboreshwe ni vidogovidogo ili kukiimarisha zaidi kikosi.
“Timu inatarajia kurudi nchini tarehe 23 (Alhamisi ijayo) mara baada ya kumaliza kambi yao nchini humo tayari kwa kuanza mzunguko wa pili wa ligi,” alisema Bin Kleb.
Yanga itafungua pazia lake la mzunguko wa pili Januari 25, kwa kuvaana na Ashanti United kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

DIVA, B 12, MCHOMVU WARUDISHWA KAZINI CLOUDS

$
0
0
Loveness Malinzi ‘Diva’.
WATANGAZAJI maarufu Bongo wa Redio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Hamis Mandi ‘B 12’, Adam Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva’, wamerudishwa kazini baada ya kuomba msamaha.
Hamis Mandi ‘B 12’.
Watangazaji hao walisimamishwa na uongozi wa Clouds baada ya kuchoshwa na tabia yao ya utovu wa nidhamu hivi karibuni.
Adam Mchomvu.

NDINGA MPYA YA LADY JAYDEE

PSPF KWA KUSHIRIKIANA NA FLAVIANA MATATA FOUNDATION WAKABIDHI VIFAA VYA SHULE KISARAWE

$
0
0

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chanzige iliyopo Wilaya ya Kisarawe Mkoa
wa Pwani wakifurahia zawadi za madaftari pamoja na mabegi vilivyotolewa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa kushirikiana taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa ajili ya kuwasadia watoto wanaoishi katika mazingira magumu mkoni humo. Katikati ni mwanzilishi wa taasisi hiyo, Flaviana Matata. Hafla hiyo ilifanyika wilayani Kisarawe, mwishoni mwa wiki. 
Mwalimu wa Shule ya Msingi Kimanzichana iliyopo Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani, Kulwa Kijangwa  akipokea msaada wa vifaa vya shule kutoka kwa Ofisa Mahusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Hawa Kikeke uliotolewa kwa kushirikiana na taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa ajili ya kuwasadia watoto wanaoishi katika mazingira magumu humo. Katikati ni mwanzilishi wa taasisi hiyo, Flaviana Matata. Hafla hiyo ilifanyika wilayani Kisarawe, mwishoni mwa wiki. 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chanzige iliyopo Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani wakicheza ngojela mbele ya wageni wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya shuleni hapo.
Wapigapicha wakiwa kazini.
Mwanamitindo Flaviana Matata akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaosoma katika Shule ya Msingi Chanzige ambao  wanaoishi katika mazingira magumu wilayani Kisarawe. Taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa kushirikiana na PSPF walikabidhi vifaa mbalimbali vya shule kwa ajili ya watoto hao.(Picha na Francis Dande) 

MZEE ARNOLD WIFRED NKHOMA APUMZISHWA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR

$
0
0
DSC_0001
Baadhi ya waombolezaji waliofika kwenye msiba wa Mzee Arnold Nkhoma wakisaini kitabu cha maombelezo nyumbani kwa mmoja wa mabinti wa marehemu Prof. Alice Wamunza Nkhoma.
DSC_0007
Baadhi ya waombolezaji wakimfariji mmoja watoto wa marehemu Bi. Agnes Nkhoma Darch (katikati).
DSC_0074
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa mtoto wa marehemu Prof. Alice Wamunza Nkhoma, Changanyikeni - Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
DSC_0096
Roy Ledama (kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya waombolezaji.
DSC_0109
Familia ya Marehemu Mzee Arnold Nkhoma pamoja na waombolezaji wakipata chakula cha mchana kabla ya kutoa heshima za mwisho.
DSC_0114
DSC_0148
DSC_0167
DSC_0198
Gari lilibeba mwili wa Marehemu Mzee Arnold Wifred Nkhoma likiwasili nyumbani kwa binti yake Changanyikeni, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
DSC_0201DSC_0231
Wajukuu wa marehemu wakiwa wamebeba Jeneza la Babu yao kuliingiza ndani tayari kwa heshima za mwisho kabla ya kuelekea Kanisani kwa Ibada.
DSC_0238DSC_0264
Mwili wa Mzee Arnold Wifred Nkhoma tayari kwa kutoa heshima za mwisho.
DSC_0330
Familia ya karibu ya marehemu.
DSC_0290
Kushoto ni mabinti wawili wa Marehemu wakiwa na ndugu zao wakaribu kwenye majonzi mazito.
DSC_0275
Vitukuu wa marehemu mzee Arnold Nkhoma.
DSC_0285DSC_0295
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho.
DSC_0345DSC_0360
Mtoto wa Marehemu Prof. Alice Wamunza Nkhoma akitoa heshima za mwisho kwa baba yake mpendwa Mzee Arnold Nkhoma.
DSC_0363
Mtoto wa marehemu Bi. Agnes Nkhoma Darch akitoa heshima kwa baba yake.
DSC_0366DSC_0368
Mjukuu mkubwa wa marehemu Bi. Usia Nkhoma Ledama akitoa heshima za mwisho kwa babu yake.
DSC_0372
Vilio na simanzi vilitawala.
DSC_0374
Ndugu wa karibu wa marehemu wakiendelea kutoa heshima za mwisho.
DSC_0379
Mama Usia na mjukuu wake Vanessa Roy Ledama wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu.
DSC_0381
Mjukuu wa marehemu Bi. Sawiche Wamunza Nkhoma akitoa heshima za mwisho kwa babu yake.
DSC_0383 

Dear Gambe - Young Killer ft Belle 9 New music 2013

Kikwete aisaliti CCM

$
0
0
MABADILIKO ya Baraza la Mawaziri aliyoyafanya Rais Jakaya Kikwete, yamewasha moto ndani ya Chama chake Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai kuwa amekisaliti chama hicho tawala, Tanzania Daima limedokezwa.

Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM taifa, anadaiwa kukisaliti chama chake kwa kuwarejesha mawaziri mizigo ambao hivi karibuni walipendekezwa na Kamati Kuu (CC) ya CCM kwamba wang’olewe kwa utendaji wao mbovu.

Ikumbukwe kwamba chimbuko la mawaziri mizigo lilitokana na ziara ya Katibu Mkuu, Abdulhaman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi taifa, Nape Nnauye, katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ambapo waliwataja baadhi ya mawaziri kuwa ni mizigo.
Katika mikutano tofauti ya hadhara, viongozi hao wa juu wa CCM walimtaka Rais Kikwete awatimue mawaziri mizigo kwa madai kuwa walishindwa kuendana na kasi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Wakiwa bado ziarani katika mikoa hiyo, Kinana alisema mawaziri mizigo watahojiwa na Kamati Kuu ya CCM na hata baada ya kuwahoji, CC iliyoketi mbele ya Rais Kikwete mjini Dodoma ilipendekeza watimuliwe.

Mawaziri waliotajwa kuwa mizigo ambao jana waliapishwa na kurejea kwenye nafasi zile zile ni pamoja na Waziri wa Kilimo na Chakula, Christopher Chiza, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe.

Lakini baada ya kuwaacha mawaziri mizigo, Rais Kikwete aliwatupa nje mawaziri watano, akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa na nafasi yake kuchukuliwa na Dk. Binilith Satano Mahenge na Naibu wake anakuwa Ummy Ali Mwalimu.

Katika mabadiliko hayo, pia Rais Kikwete aliwatupia virago manaibu waziri wanne, ambao ni Gregory Teu, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Philip Mulugo, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Goodluck ole Medeye, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Benedict ole Nangoro.

Baadhi ya makada maarufu wa chama hicho ambao waliomba majina yao yahifadhiwe, waliliambia gazeti hili kuwa kitendo cha Rais Kikwete kutomtimua hata waziri mmoja kati ya wale waliopendekezwa na chama chake baada ya kujiridhisha kwamba hawana uwezo kiutendaji, ni usaliti wa hali ya juu na unakiweka chama hicho katika mazingira mabaya.
“Si tu kwamba amekiweka chama mahali pabaya, bali pia amewashushia hadhi mzee Kinana na Nape ambao wamerejesha imani ya wananchi kwa chama kwa kiwango kikubwa,” alisema kada huyo ambaye pia ni mmoja wa wenyeviti wa CCM wa moja ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu (CC) ya CCM, alisema hata baada ya Kinana na Nape kutaja majina ya mawaziri mizigo na kutaka waitwe kuhojiwa na Kamati Kuu, Rais Kikwete aliwataka viongozi hao wa chama kuongeza majina mengine ya mawaziri mizigo ili wahojiwe na kuchukuliwa hatua.

“Katika orodha ya Kinana na Nape, Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya,  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia, hawakuwemo. Hawa waliongezwa baadaye kwa agizo la Rais. Na  bado kulikuwa na pendekezo hata la kutaka kumwita na kumhoji Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kwamba amezembea kupata fedha za msaada kutoka nje kwa ajili ya kuboresha reli na bandari.

“Rais kama mwenyekiti ameshiriki kikao cha kuwahoji na amepokea mapendekezo, leo amepuuzia mapendekezo ya chama. Wana CCM watawaangaliaje kina Kinana na Nape? Watawezaje kwenda tena kwenye ziara na kuikosoa serikali yao?” alihoji kada huyo.
Kiongozi mwingine wa CCM jijini Dar es Salaam, alisema kwa kawaida chama kinachoongoza serikali ndicho chenye nguvu na kinapotoa maoni dhidi ya serikali kiliyoiunda lakini yatekelezwe.

Kada huyo alikwenda mbali zaidi kwa kumlaumu Rais Kikwete kuwa hata kwenye mchakato wa Katiba kuna uwezekano mkubwa mazungumzo yake na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kuhusu serikali tatu ni tofauti na msimamo anaouzungumza kwenye chama.

“Warioba na tume yake wamekuja na mapendekezo ya serikali tatu, wanapokutana na rais kujadili maoni hayo, bila shaka wanaimba lugha moja, anapokuja kwenye chama kinachoamini kwenye serikali mbili, anaimba wimbo huo huo. Mwisho wa siku msimamo wake uko wapi? Sitashangaa kuona chama kitaachwa kwenye mataa kama kilivyoachwa kwenye hili la wabunge mizigo,” alisema.

Alipofuatwa ofisini kwake kutaka atoe maoni kuhusu mabadiliko hayo na mapendekezo ya CCM kutaka mawaziri mizigo wang’oke, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye,  kwanza hakupatikana kwa maelezo kwamba alikuwa na kikao na Katibu Mkuu, Kinana,
Alipopigiwa simu yake ya mkononi, alisema hana cha kusema na badala yake alimtaka mwandishi wetu kuwasiliana na msaidizi wake, Daniel Chongolo.

Hata hivyo Chongolo alijibu kwa kifupi kuwa:  “Tuache Rais Kikwete awaapishe mawaziri wafanye kazi, kuhusu kauli ya mawaziri ambao walihojiwa na Kamati Kuu ya CCM litazungumzwa siku yoyote.”

Hata hivyo wakati Nape akishikwa kigugumizi kutoa kauli, Ikulu jana ilitetea kurejea kwa mawaziri mizigo

Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema ili waziri awe mzigo kuna mambo mengi ya kuangalia.

“Siamini kama kuna waziri mzigo. Unaweza kusema waziri huyo ni mzigo, lakini lazima ujiulize kwanini? Kama hana fedha za kutosha kuendeshea wizara, utasemaje kuwa ni mzigo? Kama hana watendaji wazuri, utasemaje kama waziri huyo ni mzigo?  Kwa hiyo kuna  mambo mengi ya kuangalia,” alisema.

Katika mabadiliko ya mawaziri waliotangazwa juzi, Rais Kikwete aliwatimua mawaziri wengine watano na kuingiza sura mpya kumi, huku mawaziri wanne wakipandishwa hadhi.
Sura mpya katika baraza hilo ni Mwigulu Nchemba (Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Uchumi), Asha-Rose Migiro (Waziri wa Katiba na Sheria), Jenista Muhagama (Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Yumo Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (Naibu Waziri Wizara ya (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo), Godfrey Zambi, Mbunge wa Mbozi Mashariki, (Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika), Titus Kamani (Waziri mpya wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) na Naibu wake atakuwa Kaika Saning’o Telele.

Pindi Chana (Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto), Dk. Kebwe S. Kebwe (Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii) na Mahamod Mgimwa (Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii).

CHANZO NI TANZANIA DAIMA
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb) Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ikulu jijini Dar es salaam siku ya jana. Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
 Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani akila kiapo.
 Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb) Waziri wa Maliasili na Utalii akila kiapo.
 Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii akila kiapo.
Rais Kikwete akimuapisha  Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb) Waziri wa Fedha.
Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb) Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi akila kiapo.
Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb) Naibu Waziri wa Fedha akila kiapo.
Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb) Naibu Waziri (Nishati) akila kiapo
 Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb) Naibu Waziri wa Maji.
Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb) Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.
 Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb) Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akila kiapo.
Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akila kiapo.
Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb) Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika akiapishwa.
 Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)  Naibu Waziri wa Fedha akila kiapo.              
 Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb) Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii akila kiapo.
Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb) Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

HISIA NA MSISIMKO UNAVYO-POTEA KATIKA MAPENZI!

$
0
0
WAKATI fulani unatakiwa kujihakikishia kuwa, mke au mume uliyenaye anakuwa wako wa maisha yako yote. Kuapa tu mbele ya viongozi wa dini, kuwa atakuwa wako, haitoshi! Kuna mengi zaidi ya kufanya.
Kazi ya viongozi wa dini, mila au serikali ni kuwaunganisha tu. Kazi yao humalizikia hapo, sasa suala la furaha ya ndoa ni kazi yenu wenyewe kama wanandoa mkiwa ndani.
Ndugu zangu, hivi umeshawahi kujiuliza; kwa nini mwanandoa anatoka nje? Anafuata nini? Unajua unaweza kushangaa, ukiambiwa fulani anatoka na mwanamke mwingine nje, wakati mke wake ni mzuri wa umbo, sura na tabia.
 Watu wakimwangalia wanamsumbua kila kukicha, wanaota ni lini watampata japo kwa muda mfupi tu! Lazima ujiulize swali hili. Lakini hata wewe ambaye labda umeshatoka nje au upo katika fikra hizo, lazima ujiulize, unatafuta nini nje?

Mume/mkeo ana kasoro gani? Nini tatizo? Nawe ambaye mwenzi wako ametoka nje na una hakika na jambo hilo, inakupasa pia ujiulize na upate majibu ya swali hilo. Kwa nini ametoka nje? Kuna nini huko nje ambacho wewe humpi?

Rafiki zangu, asikudanganye mtu, tatizo kubwa kabisa huanzia katika kupoteza hisia. Ukiwa na mwenzi wako, yakafanyika makosa na likatokea tatizo la kupotea kwa hisia za mapenzi, ndiyo chanzo cha yote hayo.
Hakuna kanuni za moja kwa moja za mapenzi ndugu zangu lakini yapo mambo ambayo kiukweli kama yakizingatiwa vizuri, msisimko wa mapenzi huongezeka na kujikuta ukizidi kumuona mwenzi wako mpya kila siku.

TATIZO HUANZIA HAPA
Wengi huwa hawapati muda wa kufikiri na kutafakari juu ya jambo hili, lakini furaha ya mtoto wa kwanza, wakati mwingine hugeuka kero na msumari katika ndoa.
Wote hufurahia mtoto wao mpya lakini mama asipokuwa makini ndiyo kipindi ambacho anaweza kujikuta akipoteza msisimko wa tendo kwa mumewe. Kwa kawaida, mwanamke akishajifungua na muda wa kukutana na mumewe ukifika, mshawasha wake huwa wa juu zaidi.
Ni kipindi ambacho mwanamke humhitaji mumewe kwa muda mrefu zaidi. Atapenda awahi kurudi nyumbani, wale pamoja na kulala mapema ili aweze kufurahi naye.
Tatizo linakuja katika utaratibu mpya wa maisha baada ya kujifungua. Baadhi ya wanawake hujisahau na kuanza kufanya mambo yanayopunguza msisimko bila kujua.
Bahati nzuri ni kwamba, wakielezwa huelewa haraka sana. Hebu twende tukaone zaidi...

MAPENZI KUHAMIA KWA MTOTO
Kwanza kabisa mwanamke akipata mtoto hujikuta  akimpenda zaidi mwanaye kuliko mumewe. Si kwamba hampendi mume wake tena lakini mapenzi kwa asilimia kubwa kipindi hiki huhamia kwa mwanaye.

Mwanamke anaweza kukesha usiku mzima, mwanaye akiwa pembeni yake na kumwacha mumewe peke yake. Hili ni tatizo na husababisha kupunguza msisimko wa mapenzi. Ni jambo hatari ambalo linaweza kusababisha mume kufikiria kuwa na mwanamke mwingine wa nje.

Si ajabu kichwani anaamini hafanyi makosa bali anakuwa na mwanamke wa muda kwa ajili ya kumpisha mkewe amlee kwanza mtoto wao. Acha kujidanganya rafiki, hilo ni kosa kubwa sana. Kwenye ndoa, usaliti ni sumu!
Wiki tutamalizia mada yetu.

MASOGANGE ANAONGOZA KUTUPIA PICHA MTANDAONI

$
0
0
Video Queen , Agness Gerard ' Masogange' anayeongoza kutupia picha nyingi kwa siku katika Mtandao wa ISTAGRAM.

BARUA KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, JAKAYA MRISHO KIKWETE

$
0
0


 Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
KWA: MHE. RAIS WA JAMHURI YA  MUUNGANO WA TANZANIA, JAKAYA MRISHO KIKWETE
Ndugu,
YAH: UNYANYASAJI ULIOPITILIZA WA BODI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WASOMAO CHINA

Tafadhali rejea mada iliyotajwa hapo juu.
Mheshimiwa Rais, awali ya yote, tunapenda kuchukua fursa hii kukupa pole na majukumu yako ya kila siku na kukutakia heri ya Mwaka Mpya.

Mheshimiwa, tunaandika  barua hii ya  wazi kwako tukiomba  kutatuliwa  matatizo  yetu  makuu   mawili. Tumefikia hatua hii  baada  ya  kushindwa  kupata  suluhisho la  matatizo  haya kwa  watendaji  walio  chini  yako  ambao ni Bodi ya  Mikopo (HESLB)  na Ubalozi wa Tanzania  nchini China (kupitia mwambata  wa  wanafunzi).

1.    Ucheleweshwaji  uliopitiliza  wa pesa  za  kujikimu.
2.    Kiwango  kidogo cha  pesa ya  kusafirishia na kutolea  mizigo.

UCHELEWESHWAJI ULIOPITILIZA WA PESA ZA KUJIKIMU:
 Kwa  masikitiko  makubwa tunapenda kuwasilisha tatizo   la ucheleweshwaji uliopitiliza wa  pesa  za  kujikimu kwa  wanafunzi  tunaoendelea na masomo yetu nchini China. Kwa mujibu  wa  utaratibu  wa Bodi  ya Mikopo ni kwamba pesa  hii ya  kujikimu  inayozungumziwa ilipaswa iwe  imemfikia  kila mwanafunzi  kwa  mwaka  wa  masomo  kila  uanzapo  mwezi wa  tisa (Septemba).  Lakini katika   hali ya kusikitisha,  pesa  hii  bado haijatufikia   hadi  sasa  mwezi Januari.

Tumejaribu  kuchukua  hatua  nyingi  za  awali ikiwemo  kuwasiliana  na  ubalozi wtu  kwa kupitia  mwambata  wa  wanafunzi  wasomao  China (ushahidi    upo ) pia tumefanya  mawasiliano  na Bodi  ya  Mikopo moja  kwa  moja  bila  mafanikio yoyote (ushahidi  upo ushahidi ) zaidi ya  kuambulia  majibu yasiyo  na  kichwa  wala  miguu (ushahidi upo ).

Licha ya sisi kuwa wavumilivu kwa miezi zaidi ya mitano sasa, bado tunaendelea kupewa majibu mepesi ya kwamba tuendelee kuwa na amani na wavumilivu kwamba pesa zitakuja tu lakini haijulikani ni lini, mwezi gani na nini hasa chanzo cha kucheleweshwa mikopo hiyo?
Ikizingatiwa   kuwa  kuna baadhi  ya  wanafunzi  wanatarajia  kuhitimu mwezi  wa  saba (Julai) licha  ya  kwamba  wanahitaji  pesa  ya kujikimu  ila  pia  watahitaji pesa  kwa ajili  ya  kusafirishia  mizigo yao pindi watakapomaliza  muda  wao wa masomo  nchini China.  

KIWANGO KIDOGO CHA PESA YA KUSAFIRISHA MIZIGO:
Moja ya  changamoto  kubwa  ambayo imekuwa ikitukabili  wanafunzi  tusomao  China na  hasa  wakati  wa  kuhitimu  masomo  yetu ni  usafirishaji  wa  mizigo (vitu  mbalimbali  vikiwemo  vifaa  vya  utafiti, vitabu  na  vitu  binafsi).

Kwa wanafunzi waliohitimu  kabla ya mwaka 2013  walikuwa wanapewa pesa  ya kusafirishia mizigo kuanzia Dola za Kimarekani 3,000  hadi  3,500  lakini baadaye Bodi ya Mikopo iliamua kupunguza pesa hiyo  kufikia Dola za Kimarekani 1,200. 
Ukweli ni kwamba gharama  za usafirishaji wa mizigo kutoka China kwenda Tanzania zimeongezeka kwa kasi sana na  pesa hii  kwa  uhalisia  haitoshi hata  kidogo.

Kwa mshangao mkubwa na bila kushirikishwa  kwa wanafunzi  tusomao  China ambao  ndiyo  wanufaikaji, Bodi ya Mikopo iliamua kupunguza pesa hiyo kwa zaidi ya asilimia 100 hadi kufikia Dola za Kimarekani 1,200, pamoja na kwamba kiasi kilichoombwa baada  ya  utafiti  wa  kina  juu  ya gharama za  usafirishaji  na  utoaji  mizigo viliambatanishwa.
Kiasi hicho kusema ukweli hakikidhi gharama za usafirishaji wa mizigo ya wahitimu kutoka sehemu mbalimbali za China kwenda nyumbani Tanzania.

Mfano mwaka jana wanafunzi walishindwa kusafirisha baadhi ya vitu vyao kutokana na gharama kuwa kubwa sana na ambao waliweza kuongeza pesa kutoka mfukoni mwao na kusafirisha walishindwa kuvitoa pale bandarini Dar es Salaam.

HITIMISHO:
Kutokana na matatizo haya na mengine mengi ambayo tunashindwa kuyaeleza hapa, suala hili limesababisha usumbufu mkubwa kwa wanafunzi katika shughuli zao za kimasomo.  Hii  ni  pamoja  na  baadhi  ya  tafiti zao kushindwa  kufanyika ipasavyo.

Ombi letu kwa Mh.  Rais ni kwamba tunaomba tupatiwe ufumbuzi wa matatizo   yetu haraka kwa sababu tumeshavumilia  vya  kutosha.  Tunaomba pesa ya kujikimu  iwe inatumwa  kwa wakati na pia  pesa ya kusafirishia mizigo ipatiwe ufumbuzi.
 
Aidha irejeshwe kama ilivyokuwa awali au ikiwezekana iongezwe ili kukidhi  gharama za usafirishaji na utoaji  mizigo  Tanzania.  

Mheshimiwa Rais, ni wazi kuwa tumehuzunishwa na kusikitishwa sana na udhalilishaji, uonevu na unyanyaswaji tunaofanyiwa kutokana na kutowajibika kwa baadhi ya watendaji wa Bodi ya Mikopo na ubalozi  wetu ama kwa kutambua au kutotambua wajibu wao.
Tunaamini suala letu utalipa uzito unaostahili.
 
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati na pia tunakutakia mafanikio mema katika shughuli zako za ujenzi wa taifa.
Wako wanafunzi  wa Tanzania walio China.

MBUNGE WA CHALINZE, SAID BWANAMDOGO (CCM) AFARIKI DUNIA

$
0
0

Mbunge wa Chalinze, Said Ramadhani Bwanamdogo enzi za uhai wake.
HABARI zilizotufikia hivi punde ni kwamba Mbunge wa Chalinze, Said Ramadhani Bwanamdogo (CCM), aliyekuwa amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI)  amefariki dunia!

MMILIKI WA YANGA AIBUKA, ATAKA KWENDA KWA KIKWETE

$
0
0

Juma Mwambelo.
Na John Joseph wa Championi.
ALIYEJITANGAZA kuwa mmiliki wa klabu ya Yanga, Juma Mwambelo, amesema yu tayari kukabidhi nyaraka zinazotafutwa na uongozi wa klabu hiyo kwa Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, alitangaza kwenye mkutano wa Yanga kwamba Mwambelo anashikilia hati za umiliki wa klabu ya Yanga kimakosa na anatakiwa kuzikabidhisha haraka iwezekanavyo kabla ya kuchukuliwa hatua.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwombelo alisema yupo tayari kumpa Rais Kikwete naye aukabidhi uongozi wa Yanga chini ya Yusuf Manji.
“Kweli hati hizo ninazo kwa kuwa mimi ni mmiliki wa Klabu ya Yanga, ila Rais Kikwete pekee ndiye naweza kumkabidhi, hata mwanaye Ridhwani nimewahi kumueleza kuhusiana na hili,” alisema.

“Mimi ndiye mmiliki wa Klabu ya Yanga, nina hati miliki halali ya klabu, hii hapa (anaonyesha), nina hati miliki ya jengo la Jangwani, pia ninayo ya jengo la Mafia, lakini hiyo waliiba na tayari nilisharipoti polisi.
“Kuhusu hati ya jengo la Jangwani ipo benki na yenyewe sijailipia kwa kuwa kuna deni, deni hilo ni zile fedha ziliyotumika kujenga Uwanja wa Kaunda. Hivyo,
deni likilipwa benki itakubali kutoa hati kisha kuirudisha wizarani na kutolewa rasmi.

“Nashangaa Yanga wanapodai wanatumia katiba mpya, hii siyo halali, katiba halali ya Yanga ni ile ya mwaka 1967 ambayo nakala yake hii hapa (anaonyesha),” alisema.

Alipoulizwa juu ya uhalali wa wanachama wa sasa wa klabu hiyo, alisema: “Wanachama wengine wote ni feki, mpaka unatokea mgawanyiko mwaka 1975, wanachama halali wa Yanga walikuwa 400, kuanzia hapo hakuna wanachama halali tena, hata akaunti zinazotumika siyo za klabu.

“Hapa nilipo nimekuja polisi (Magomeni) ili kutoa taarifa ya kujihami, nahofia kupigwa kutokana na walichokisema kwenye mkutano,” alisema.
Katika mkutano mkuu wa Jumapili, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Karume, PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam, uongozi wa Yanga ulimtaja mzee Juma kuwa ndiye aliyeiiba hati ya jengo la klabu hiyo tangu Juni 24, 2009.

“Mimi nilipigwa na watu mwaka 1987 nikapoteza fahamu kwa siku tano, tangu pale sijawahi kwenda klabuni wala uwanjani kuitazama Yanga, hata huyo Mrisho Ngassa simjui, namuona tu kwenye magazeti, kikubwa ninachotaka ni utaratibu ufuatwe ndani ya Klabu ya Yanga,” alisisitiza huku akitabasamu.

SNURA TUHUMA NZITO

$
0
0
Snura Mushi.
STAA wa wimbo wa Majanga, Snura Mushi ameingia kwenye majanga baada ya kudaiwa kukacha na deni la prodyuza Mohammed Kandoro wa Studio za Fire Music ambaye alimrekodia nyimbo kadhaa wakati akisaka kutoka.

Habari kutoka kwa chanzo cha kuaminika zinasema kuwa Snura ameingia mitini na kiasi cha Tsh. 400,000 za prodyuza huyo na kwamba sasa amehamia studio nyingine.

Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Kandoro na kumwuliza kuhusu ukweli wa minong’ono hiyo, ambapo alikiri na kusema: “Ni kweli namdai laki nne. Nimefanya naye kazi kwa muda mrefu lakini sasa naona ameamua kuondoka na deni langu.”

Snura alipopigiwa simu na kuelezwa kuhusu madai hayo, alifunguka: “Kama kuna deni basi meneja wangu HK (Hyper Man) ndiye anayehusika, maana kila kitu nilimkabidhi yeye na naamini alilipa, sasa kama hakulipa hayo ni mambo yanayomhusu yeye, si mimi tena.”

Katika kutafuta mzani wa habari, gazeti hili liliwasiliana na meneja wa Snura, HK ambaye alisema hana deni lolote analodaiwa na Kandoro, ingawa alikiri kumhamisha Snura studio.

“Kilichopo ni kwamba tumehama kwenye hiyo studio, sina ugomvi nao wala Snura hajawahi kutofautiana naye. Tumefanya hivi kwa lengo la kutafuta ladha tofauti... hayo mambo ya madeni, si kweli.

Hivi kama leo hii tunaweza kulipa zaidi ya shilingi milioni moja na laki nne (1,400,000) tunashindwaje kulipa laki nne tu? Hayo ni maajabu,” alisema HK.

Logarusic: Rage alitakiwa kuniuliza mimi

$
0
0
KOCHA Mkuu wa Simba, Mcroatia, Zdravko Logarusic, amesema hatafanya kazi na kocha   Mganda, Amatre Richard, kwa kuwa hajahusishwa kwenye uteuzi wake.
Tayari imebainika kuwa Mganda huyo ameshatua nchini, akidaiwa kuletwa na mwenyekiti wa timu hiyo, Ismail Aden Rage, ambaye alionyesha hofu ya kuteuliwa kwa Selemani Matola huku akitaka arejeshwe kikosi cha vijana.

Akizungumza na Logarusic ‘Loga’, alisema katika uteuzi wa kocha msaidizi, lazima kocha mkuu ahusike kwani yeye ndiye mwenye uwezo wa kujua mtu atakayemfaa kwenye benchi la ufundi.

Aliongeza kuwa, kabla ya kutua Simba, aliomba mapema kufahamishwa sifa za msaidizi wake na kuridhika na utendaji wa Matola, hivyo hayupo tayari kufanya kazi na kocha mwingine zaidi ya Matola.
“Kwangu mpaka sasa sijui chohote, lakini kama ni hivyo walitakiwa kuniambia mimi, kiheshima mwenyekiti alitakiwa kunifuata na kunieleza.

“Niseme ukweli kama kweli ndiyo hivyo mimi sipo tayari kufanya kazi na kocha huyo, ninachotaka mimi ni kuendelea kufanya kazi na Matola kwa kuwa tunaelewana na sifa zake nilizikubali tangu awali,” alisema Loga.

Amatre yupo hapa nchini na inaelezwa kuwa ameletwa na Rage kwa kuwa awali kocha huyo alikuwa kwenye benchi la ufundi la Simba lakini hakumaliziwa fedha zake za mshahara, hivyo anatakiwa kufanya kazi ili amalizie mkataba wake.

YANGA YAENDELEA KUJIFUA, KUONDOKA KESHO UTURUKI

$
0
0
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans leo imeendelea na mazoezi ya asubuhi katika viwanja vya hoteli ya Sueno  katika kuendelea kujiweka sawa kabla ya kuanza safari kesho mchana ya kurejea nchini Tanzania tayari kwa mikikimikiki ya mzunguko wa pili wa VPL 2013/2014.
Kocha mkuu Hans Van Der Plyum ameendelea kuwaandaa wachezaji wake na kuyafanyia marekebisho kadhaa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita dhidi ya Simurq PIK kabla ya kesho kuanza safai ya kurejea nyumbani tayari kwa kufungua dimba siku ya jumamosi dhidi ya Ashanti United.
Katika mazoezi ya leo asubuhi kocha Hans amesema kikosi chake kinaendelea vizuri mpaka sasa, hakuna majeruhi na wachezaji wanajituma na kuwajibika kwa kujua wajibu wao ni nini hivyo inakua rahisi pia kushika maelekezo yake.

Mara baada ya mazoezi ya asubuhi kocha Hans amesema timu itaendelea tena na mazoezi ya jiioni kuanzia majira ya 9:30 kwa saa za huku sawa na 10:30 kwa saa za Afrika Mashariki ambapo hayo ndo yatakua mazoezi ya mwisho kabla ya kesho kuanza kwa safari ya kurejea Tanzania.

"Nina uzoefu na soka la Afrika takribani kwa miaka 15, wachezaji niliowakuta hapa Young Africans wana uwezo mzuri wote, wanajituma, wana nidhamu na upendo wa hali ya juu kitu ambacho kwa mwalimu yoyote lazima atafurahia mazingira hayo kwani hata ufanyaji wake kazi unakua mzuri "alisema Hans."

Aidha Hans ameongeza kwa siku tisa alizokaa na wachezaji wake Sueno Hotel Beach Side Antalya katika mazoezi na mafunzo aliyokuwa anawapatia anaamini sasa timu yake ipo tayari kutetea Ubingwa wa Ligi pamoja na kufanya vizuri kwenye na mashindano ya kimataifa .

Kambi ya siku 14 katika hoteli ya Sueno Beach Side  Manavgat jijini Antalya imekua nzuri sana kwani wachezaji na benchi la ufundi kwa ujumla wameweza kutimiza wajibu wao ambapo dhumuni kubwa ilikua ni kufanya mazoezi, kupata michezo ya kirafiki kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili VPL na mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika.

Young Africans ambayo imeweka kambi nchini Uturuki kwa takribani siku 14 mpaka sasa, iliweza kucheza michezo minne ya kirafiki dhidi ya timu za Ankara Sekerspor na Altay SK za Ligi Daraja la pili nchini Uturuki kabla ya kuivaa timu ya KS Flumartari ya Albania kisha kumaliza na timu ya Simurq PIK ya Azerbajain.

Matokeo ya mechi hizo ni:

11.01.2014

Young Africans 3 - 0 Ankara Sekerspor

(Didier 10, Okwi 46,  Kiiza 61)

15.01.2014

Young Africans 2- 0 Altay SK

(Didier 46, Okwi 57)

18.01.2014

Young Africans 0 - 0 KS Flumartari

20.01.2014

Young Africans 2 - 2 Simurq PIK

(Didier 13, Ngasa 30)  -  (Anderson 45, Sattarli 56)

MUONEKANO WA SASA WA WEMA SEPETU

MCHUMBA WA LULU SI SIRI TENA!

$
0
0

HAYAWIHAYAWI hatimaye yamekua! Siku chache baada ya sexy lady wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ kutangaza sifa za mwanaume atakayemchumbia, amejitokeza mtu anayetaka kuchukua jumla na si siri tena.
Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
SIFA ZAKE
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa familia ya staa huyo anayekimbiza sokoni na filamu yake ya Foolish Age, mchumba huyo anaitwa Johnson lakini ni maarufu kwa jina la JR na pia ni Mkristo kama ilivyo kwa Lulu.
JR ni mfanyabiashara kigogo wa jijini Dar mwenye ‘mahela’ ya kufa mtu.
Pia mchumba huyo ni bosi wa kampuni kubwa ya uandaaji, usambazaji wa kazi za sanaa Bongo.

ALISHAKWENDA KWA AKINA LULU
“Kwa taarifa yenu, tayari JR anafahamika vizuri kwa akina Lulu kwani alishakwenda kujitambulisha na kuna maneno kwamba ndiye aliyempangia nyumba kubwa, Tegeta jijini Dar.
“Unajua yule jamaa aliona fursa akaitumia. Baada ya Lulu kutoka mahabusu kwa matatizo ya kifo cha mwandani wake, Steven Kanumba ndipo JR akafanya juu chini kumnasa hadi akafanikiwa,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Muda siyo mrefu zitasikika cherekochereko za Lulu kuolewa.
“Ukweli ni kwamba hata mama Lulu (Lucresia Karugila) amemkubali yule mchumba kwani ndiye anayemfanya Lulu aonekane kama alivyo kwa sasa.
“Sasa hivi Lulu anaishi kwenye bonge la nyumba kule Tegeta (Dar) na suala la usafiri si ishu. Anabadili tu magari. Kusema kweli kwa sasa bidada mambo yamemwendea vizuri.
“Anachoogopa tu yasitokee kama yale ya Clement wa Wema Sepetu.”
AMANI LASAKA WAHUSIKA
Baada ya kumwagiwa upupu huo, gazeti hili liliwasaka wahusika mmoja baada ya mwingine ili kupata mbivu na mbichi za ishu hiyo.
Mama Lulu, Lucresia Karugila.
MAMA LULU
Kwa kuwa ni jambo la kifamilia, gazeti hili lilipozungumza na mama Lulu, Lucresia Karugila alisema si jambo baya kwa mwanaye kuwa na mchumba hivyo anamkubali (huyo mchumba) huku akiweka wazi kuwa hana kipingamizi chochote.
Alipoulizwa jina la mwanaume huyo na kwamba ni kigogo mwenye fedha nyingi, mzazi huyo alitoa ruksa aulizwe Lulu mwenyewe.
“Mimi sina sababu ya kumkataa mwanaume ambaye wamekubaliana na mwanangu, kikubwa ni makubaliano, namkubali,” alisema mama Lulu.
HUYU HAPA LULU
Kwa upande wake Lulu mambo yalikuwa hivi;
Amani: Mambo vipi Lulu?
Lulu: Poa, naongea na nani?
Amani: (akatajiwa jina la mwandishi) kwanza hongera kwa kupata mchumba.
Lulu: Nani kawaambia?
Amani: Kwa kazi yetu hii hatushindwi kujua. Je, ni kweli umepata mchumba?
Lulu: Ndiyo lakini nisingependa sana kulizungumzia hilo.
Amani: Anaitwa nani?
Lulu: Siwezi kumtaja leo (Jumanne iliyopita). Nitawatajia tu ninyi subirini. Itakuwa surprise (mshangao), siku si nyingi nitamuanika.
Amani: Je, ni kweli ni maarufu kwa jina la JR? Au wewe tutajie hata jina la mwanzo tu.
Lulu: Nimeshasema jamani nitawatajia kwani ninyi mna haraka gani?
Amani: Je, ni kweli ni mmiliki wa kampuni ya burudani? (anatajiwa kampuni).
Lulu: Hayo yote yatafahamika kwenye utambulisho. Naomba niishie hapo ‘coz’ sina cha zaidi kuhusu ishu hiyo jamani subirini siku si nyingi.
 
MAMA KANUMBA
Baada ya kujiridhisha kuwa sasa Lulu ana mchumba rasmi, ‘kijumbe’ wetu alimfikishia taarifa aliyekuwa mama mkwe wa staa huyo wakati akiwa na Kanumba, mama Kanumba, Flora Mtegoa ili naye atie neno.
Mama Kanumba hakuwa na kipingamizi juu ya suala hilo zaidi ya kuchekelea huku akiweka wazi kuwa Lulu kwa sasa anaweza kuolewa.
“Mimi sina tatizo kabisa, namjua. Lulu anaweza kuolewa na nimempa baraka zote,” alisema mama Kanumba ambaye kwa sasa ni shosti mkubwa wa mama Lulu.
JR SASA
Hata hivyo, gazeti hili halikuishia hapo kwani lilisaka namba ya simu ya kiganjani ya mwanaume huyo ambapo ilipopatikana, alipigiwa, mambo yakawa hivi:
Amani: Habari yako mkuu JR?
JR: Safi, nikusaidie nini?
Amani: Mimi…(akatajiwa jina la mwandishi na kampuni) wewe ndiye JR mmiliki wa kampuni ya…(anatajiwa jina la kampuni).
JR: Kwanza mimi siyo JR ni GR. Huyo JR ni mdogo wangu.
Amani: Mbona sisi tumetajiwa JR ambaye anamiliki kampuni ya...(anatajiwa tena jina la kampuni).
JR: Oke, ndiyo mimi nikusaidie nini?
Amani: Taarifa tulizonazo ni kwamba una uhusiano na Lulu? Yaani wewe ndiye mchumba wake?
JR: Ndiyo, sitaki maswali (tusi na kukata simu).
Tangu kitokee kifo cha Kanumba ambaye alikuwa na uhusiano wa siri na Lulu, bidada huyo hajawahi kuwa na mwanaume hadi huyo mchumba aliyejitokeza.

CHANZO NI GAZETI LA AMANI/GPL

MAJANGA MAN UTD: MANCHESTER UNITED YAONDOLEWA CAPITAL ONE CUP KWA MATUTA

$
0
0
 
 Shangwe: Wachezaji wa Sunderland wakishangilia kutinga fainali baada ya kuwaondoa Man Utd.
Majonzi: Wachezaji wa Manchester United wakiwa na nyuso za huzuni.
Kifo cha nyani: Rafael wa Man Utd akikosa penalti iliyowapa ushindi Sunderland.
Tukutane Machi 2 Wembley: Sunderland wakiwashukuru mashabiki wao 9,000 waliofika uwanjani kuwashangilia na kuwaomba wakutane Wembley katika fainali na Manchester City.

TIMU ya Manchester United imeendelea kusuasua katika michuano mbalimbali baada ya kuondolewa na Sunderland katika nusu fainali za michuano ya Kombe la Ligi maarufu kama Capital One Cup iliyopigwa Old Trafford.

Manchester imetupwa nje ya mashindano hayo kwa mikwaju ya penalti baada ya matokeo ya awali kuwa sare ya 3-3 na Sunderland kushinda kwa penalti 2-1.

Baada ya matokeo hayo, Sunderland inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi 18 juu ya Cardiff City katika Ligi Kuu ya England, itakutana na Manchester City Machi 2 mwaka huu katika fainali itakayopigwa uwanja wa Wembley.

KWA NINI UKUBALI MPENZI AKUDHALILISHE KISA PESA ZAKE?

$
0
0
NI wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana tena kupitia ukurasa huu namba moja kwa kuandika makala kali zinazogusa maisha yetu ya kimapenzi. Ni matumaini yangu umzima bukheri wa afya na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama kawaida.
Mpenzi msomaji wangu, kama ulikuwa hujui ni kwamba mapenzi ya sasa yameingiliwa! Kama ni muziki basi waswahili wanasema disko limeingiliwa na Mmasai. Nasema hivyo kutokana na yale ninayoyaona kwenye uwanja wa mapenzi.

Yaani sasa hivi ni kweli hapendwi mtu bali pochi lake lililonona. Kuna walioingia kwenye uhusiano na watu ambao kiukweli hawana mapenzi nao ila pesa imewasukuma.
Wapo waliokubali kuingia kwenye ndoa na watu ambao katika mazingira ya kawaida wasingekubali lakini kwa sababu ya mali na pesa wameshawishika.

Hata hivyo, si wote walioingia kwenye penzi kwa kufuata pesa wana furaha maishani mwao. Wengi wao sasa wanajuta, wanahisi wamefanya makosa makubwa kuyaacha maisha yao ya kimapenzi yashikiliwe na pesa.

Ukweli ni kwamba, pesa na mapenzi ni vitu viwili tofauti ambavyo hata kama vina uhusiano wa karibu lakini mapenzi yanaweza kuwepo hata kama pesa haipo.

Wanaofuatilia historia wanajua kuwa, enzi hizo mababu na mabibi zetu hawakuwa wakijua pesa lakini mapenzi waliyokuwa wakioneshana yalikuwa ya aina yake. Walipendana kwa maana halisi ya kupendana kutoka kwenye mioyo yao.

Sasa hivi mambo yamegeuka, pesa imekuwa ikitangulizwa mbele kwenye suala la uhusiano na matokeo yake sasa mapenzi yanakuwa ya kimaigizo. Mtu hakupendi lakini anaonesha kukuzimikia ile mbaya kwa sababu tu ameona pochi limetuna, likisinyaa na yeye anaingia mitini.
 
Mbaya zaidi sasa hivi wapo ambao wamekubali wadhalilishwe na wafanyiwe kila aina ya unyanyasaji eti tu kwa kuwa wamedondokea kwa mtu mwenye nazo. Hiki ndicho nilichopanga kukizungumzia leo.
Hivi karibuni niliongea na dada mmoja ambaye alinisimulia kisa cha kushangaza sana kuhusu mpenzi wake. Kwa maelezo yake ni kwamba, mpenzi wake ana pesa nyingi lakini cha ajabu amekuwa akimdhalilisha katika maeneo mbalimbali, hebu msikie;

“Familia yetu ni maskini na baada ya kumpata yule kaka, alikuwa akiihudumia familia yangu kwa ujumla. Nilikuwa nikimpenda na hata alipoonesha ubinadamu wake wa kuijali familia yangu nikaongeza mapenzi.
  “Kinachoniumiza mimi ni kwamba, kila ninapokutana naye ananilazimisha nimpe mapenzi kinyume na maumbile. Ninapomkatalia, ananikasirikia na inaweza kupita hata wiki bila kuwasiliana.
“Mbaya zaidi huwaambia ndugu zangu kuwa namkorofisha na wao hunijia juu. Kusema ukweli huyu kaka
ananidhalilisha na ukimuangalia huwezi kuamini kama anaweza kuniomba kitu kama hicho.”
Maelezo ya huyu dada yalinipa simanzi, nikagundua kwamba kwa hali ngumu ya maisha iliyopo wapo ambao wanakubali kudhalilishwa na wapenzi wao kwa sababu ya pesa.

Huko mtaani wapo wanaokubali kufanya mapenzi kinyume na maumbile eti ili wasije wakaachwa, huu ni ulimbukeni!
Hata kama ana pesa zake lakini asizitumie kukufanya wewe chochote anachokitaka.

Kwa kifupi kulazimisha mapenzi kinyume na maumbile ni kujidhalilisha sasa kama unaye mpenzi ambaye anakulazimisha kufanya mchezo huo na kwa kuwa na wewe una shida zako unakubali, unakosea sana.
Jitathmini na usijirahisi kwa sababu ya pesa.

Wanawake wasiwape wanaume nafasi ya kuwadhalilisha kwa sababu ya pesa zao. Wanaume nao wawe na utu, watambue kufanya mapenzi kinyume na maumbile kuna madhara makubwa kwao na kwa wanawake pia.
Ni hayo tu kwa leo.

Mapanga yaanza uchaguzi mdogo Arusha

$
0
0
UCHAGUZI mdogo wa udiwani Kata ya Sombetini umeanza kwa vurugu baada ya wanachama watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kujeruhiwa na kundi la vijana walinzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Green Guard.

Aidha, mgombea wa CCM kwenye kata hiyo, David Lesikari, akiwa na watu wengine  anadaiwa kuwashambulia na kitu chenye ncha kali wanachama wawili wa CHADEMA na kumjeruhi mwingine kichwani na mgongoni.

Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani Arusha, Ephata Nanyaro, aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa vurugu hizo zilitokea Januari 20 mwaka huu na kwamba licha ya wanachama wao kuumizwa, Jeshi la Polisi liliwakamata na kuwageuzia kesi kuwa wao ndio waliofanya vurugu.

Alisema siku hiyo saa nane mchana mwanachama wao, Vitalis Bernad, alipigwa shoka la kichwa na kijana aliyedai kuwa kiongozi wa CCM wakati akipita kwenye kona ya Mbauda akiwa kwenye pikipiki yenye bendera ya CHADEMA wakielekea kwenye mkutano wa mgombea wa chama chao, Ally Bananga.

“Kwa bahati Bernard alikuwa amevaa kofia ngumu za waendesha pikipiki hivyo hakuumia sana lakini watu waliokuwa pale walijaribu kumkimbiza mhusika lakini hawakufanikiwa, kwani alikimbilia kwenye ofisi ya CCM ambapo walitokea kundi la watu wenye mapanga kutoka ndani ya ofisi hizo jambo lililowafanya wananchi kutawanyika kwa hofu,” alisema Nanyaro.

Alisema Bernard akiwa na viongozi wa CHADEMA walienda polisi kufungua taarifa namba Ar/RB/982/2014 kwenye kituo kidogo cha Mbauda karibu na ofisi hizo za CCM ambapo waliwaeleza polisi kuwa mtuhumiwa yuko ndani ya ofisi hizo lakini hawakutaka kwenda kumkamata.

Mwenyekiti huyo wa wilaya alisema siku hiyo hiyo saa 12 jioni Wanachadema wawili, Loserian Laisi na Mozec Joseph wakitokea kwenye mkutano wa kampeni wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki walivamiwa na kundi la watu wakiongozwa na mgombea wa CCM ambapo waliwashambulia kwa mapanga na silaha za jadi.

Nanyaro alisema katika tukio hilo Loserian alikatwa kichwani na kiunoni kwa kitu chenye ncha kisha kutelekezwa migombani kabla ya kusaidiwa na wasamaria wema waliompeleka Kituo cha Polisi cha Sombetini kupata fomu ya matibabu (PF3) na kwenda hospitali.

“Polisi bila weledi walichukua maelezo kwa saa mbili huku Loserian akiwa kwenye maumivu na damu zikimtoka hata hivyo alipatiwa matibabu katika hospitali ya Kaloleni, akiwa anaendelea na matibabu polisi walifika hospitalini na kumchukua hadi Kituo Kikuu cha Polisi na kumweka rumande,” alilalamika Mwenyekiti huyo wa CHADEMA.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alikiri ofisi yake kupokea taarifa za vurugu za jioni huku akibainisha kwamba taarifa za tukio la mchana hakuzipata.

Akizungumza na, Kamanda Sabas alisema kwenye tukio hilo la jioni vijana wa CHADEMA wakiwa kwenye pikipiki mmoja alishuka na kumpiga vibao mgombea wa CCM, Lesikari, ambapo wananchi walioona walipandwa na hasira hivyo kuwashambulia na kukiri kwamba vijana wa CHADEMA kuhojiwa na polisi kuhusu tukio hilo.

“Unaweza kupigwa karibu ya kituo cha polisi haimaanishi waliokupiga ni polisi, hivyo huyo inawezekana kabisa alipigwa hapo kona ya Mbauda karibu na ofisi za CCM lakini wahusika si Wana CCM, kwenye kesi kinachotafutwa ni ushahidi si hisia,” alisema kamanda huyo.
CHANZO NI TANZANIA DAIMA
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>