Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

PROFESA MAZRUI AFARIKI DUNIA

$
0
0

Profesa Ali Mazrui enzi za uhai wake.
MSOMI mashuhuri wa masuala ya kisiasa, utamaduni wa Kiafrika na dini ya kiisilamu wa nchini Kenya, Profesa Ali Mazrui ameaga dunia leo akiwa Marekani.


Mazrui alyekuwa anaishi nchini Marekani, amefariki akiwa na umri wa miaka 81baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Taarifa zinadai kuwa Profesa Mazrui atazikwa mjini Mombasa, Pwani ya Kenya alikozaliwa.
Enzi za uhai wake, marehemu alitoa ombi la kutaka kuzikwa Mombasa akisema angependa kuzikwa katika jumba la kihistoria la Fort Jesus.
Kabla ya kifo chake, Marehemu Mazrui alikuwa anafundisha katika Chuo Kikuu cha Binghamton mjini New York, Marekani.

BABA KIUMBE WA AJABU - 01

$
0
0

MTUNZI: ALLY MBETU
##Soma sehemu ya BABA KIUMBE WA AJABU - 02
hapa: ==>www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
Katika dunia ya Mungu kuna mambo mengi ambayo ukihadithiwa unaweza kudhani ni simulizi za kutunga na za kusisimua. Lakini siku zote kila aisifiaye mvua basi ujue imemnyea. Dunia imezungukwa na siri nzito ndani ya majumba ya watu, kuna mambo mazito ambayo ni chukizo kwa Muumba.
Si kila mwenye maisha mazuri au tajiri mali alizonazo kazipata kihalali. Wengi utajiri wao unatokana na nguvu za giza, utajiri anaoambatana na kutoa kafara ya kitu. Wapo wanaotoa kafara watoto, wake au waume zao, pia wapo wanaowageuza watoto, wake au waume zao kuwa mandondocha kama ‘chuma ulete’ wa kuwaongezea kipato.
Nyumba nyingi huwa na vyumba vya siri ambavyo huwa havifunguliwi kutokana na masharti ya mganga na kufanya watu wabaki na maswali. Pia nyumba nyingine unakuta kuna mtoto ambaye akili zake si nzuri, akikaa yupoyupo tu, mate yanamtoka ovyo kumbe ni dawa ya utajiri. Ajabu huyo ndiye anakuwa kipenzi cha baba ambaye anajua siri yake.
Wapo ambao huambiwa kama mtoto huyo atakufa basi na utajiri nao utayeyuka, ni mambo mengi yaliyoizunguka jamii na uchafu wa tamaa za watu kutaka utajiri kwa njia ya mkato na kujikuta wakifanya uchafu au ukatili mkubwa bila kuwa na huruma ilimradi wapate utajiri.
Nayasema haya nikiwa na uchungu mkubwa baada ya baba yangu kutugeuza chuma ulete sisi wanaye kwa ajili ya kumuingizia pesa bila kujua. Nayasema haya baada ya kuteseka zaidi ya miaka saba bila kujua kumbe mateso yangu ndiyo yalikuwa chachu ya utajiri wa familia yangu.
Tangu nilipoanza kupata matatizo yaliyosababisha mateso kila kukicha, hata siku moja sikuruhusiwa kwenda hospitali zaidi ya kutumia dawa za kienyeji zilizokuwa zinapunguza maumivu na si kuniponesha.
Miaka saba nyuma, tatizo kama langu alikuwa nalo dada yangu ambaye nilimfuata mara ya nne ambaye sasa hivi ni marehemu. Mwanzo nilipomuona dada nilijua ni kidonda cha kawaida japo kilinishangaza kuchukua muda mrefu tangu nikiwa na miaka sita mpaka nilipokuwa na utambuzi kujua kuwa dada yangu anateseka na kidonda kile ambacho kilikuwa hakiponi.
Miaka mitatu baadaye nilisikia ugomvi mkubwa kati ya baba na dada, nilijificha na kumsikia dada akisema:
“Nimechoka! Siwezi kuteseka wakati wenzangu wanafaidi kwa mateso yangu, siolewi sina maisha mazuri kama wenzangu niponipo tu. Haya maisha mpaka lini? Nasema sasa hivi naondoka na hili sasa mtafutie mwingine, nakwenda kuishi maisha yangu, kama pesa nimekuingizia sana naomba niondoke.”
“Monika mwanangu, kuondoka kwako kutaharibu kila kitu.”
“Baba acha viharibike, nimechoka.”
“Mwanangu unajua kabisa dawa hii haitaki uchafu, ukikutana na mwanaume tu umeharibu kila kitu.”
“Ndiyo maana nimekwambia tafuta wengine, baba wewe ni kiumbe gani usiye na huruma. Miaka yote nateseka peke yangu wakati wengine wanafaidi, watu wana majumba wana magari ya kifahari lakini mimi bado naishi maisha duni, kuna faida gani kuendelea kuteseka.”
“Basi nipe muda nivifanyie kazi.”
”Sina muda huo nimechoka.”
Kwa kweli kutokana na uchanga wangu wa akili, sikujua baba na dada walikuwa wanabishana nini, pia nilijiuliza dada ana mateso gani ambayo anamlalamikia baba. Lakini baada na mimi kunikuta nilielewa dada alikuwa akimaanisha nini. Maisha tuliyokuwa tukiishi yalikuwa ya ajabu sana, kwa sisi tuliokuwa tukiishi nyumbani tuliishi maisha ya dhiki sana tofauti na utajiri mkubwa tuliokuwa nao.
Tulikuwa na majumba kila kona ya Jiji la Mwanza, pia tulikuwa na mashine za kusaga na kukoboa ambazo ziliingiza pesa nyingi sana. Kaka zangu na dada zangu wote kila mmoja alikuwa na duka kubwa, gari na majumba makubwa. Lakini sisi tuliobakia maisha yetu hayakulingana na utajiri wa baba yetu.
Kitu kingine wakati ule kilichonishangaza ni hali ya mama, pamoja na kuwa na utajiri mkubwa kama ule, kila siku mama alikuwa akiamka asubuhi na kwenda shamba ambako alilima mpaka jioni na kurudi nyumbani. Kila mama aliporudi nyumbani alikuwa akirudi na kuni ambazo alipikia katika jiko la mafiga.
Kwa vile mwanzo zilikuwa akili za kitoto sikuelewa nini kinaendelea wala wakati huo sikujua faida ya utajiri tuliokuwa nao. Kitu kingine ambacho sikukielewa muda ule kilikuwa ni nyumba tuliyokuwa tukiishi. Ilikuwa ni ya zamani ambayo baba aliinunua wakati anaanza maisha.
Lakini haikuwa na mabadiliko yoyote pamoja na mabadiliko ya kimaisha kwa baba kuwa na pesa kama mchanga. Dada baada ya kubishana na baba alikaa kwa wiki mbili.
Siku moja niliporudi sikumkuta, alikuwa ameamua kuondoka, sikujua amehamia wapi. Lakini baada ya siku tatu nilipata taarifa kuwa dada amehamia Mkuyuni ambako alikuwa amepanga na kufungua duka lake. Kuondoka kwa dada kulifanya nyumba igeuke kama pametokea msiba, kitu ambacho kilinishangaza sana.
Kuondoka kwa dada hakukuwa kitu cha ajabu kwa vile dada na kaka zangu wote walipotaka kuanza maisha yao waliondoka lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote. Baba alionekana kukosa raha, mama naye muda mwingi mkono ulikuwa shavuni. Kitu kile kwa kweli kilinishangaza sana.
****
Nakumbuka siku moja ndugu wote walikutana nyumbani kasoro dada Monika na kuwa na kikao kizito, cha ajabu mimi nilitolewa nje hivyo kilichoendelea sikujua kwa vile nilibaguliwa kutokana na kuonekana mdogo nisiye na mchango wowote.
Baada ya kikao kilichochukua zaidi ya saa nne, ndugu zangu waliondoka.
Kuondoka kwao kidogo kulifanya baba achangamke bila kujua walikuwa wamezungumza nini na nini chanzo cha wazazi wangu kuwa katika hali ya majonzi.
Nilijiuliza ilikuwa ni dada kuondoka au kulikuwa na jambo kubwa zaidi, katika akili yangu nilifikiria kuna umuhimu wa kumtafuta dada Monika ili nijue kwa nini ameondoka nyumbani na vilevile ni mateso gani aliyoyapata. Kuna kitu kimoja ambacho kilikuwa kikinishangaza tangu nilipopata akili. Kilikuwa ni donda la mguu la dada ambalo lilikuwepo kila siku na wala halikupata dawa ya kuliponesha.
Nilijikuta nikipata hamu ya kutaka kujua kwa nini dada aliyasema yale maneno ambayo yalionesha machungu kwa kuonekana akizuiwa nyumbani asiondoke lakini wengine wote waliruhusiwa. Kingine kilichoacha maswali kichwani mwangu ambacho kilikuwa hakijakomaa akilini ni hali ya dada kuonekana kama hajaliwi na baba tofauti na ndugu zangu tokea kwenye elimu mpaka maisha ya kawaida.
Wote walikuwa na maisha mazuri kasoro yeye, lakini sikutaka kujua zaidi kwa vile nilikuwa mtoto mdogo nisiye na uwezo wa kuhoji jambo. Nilipeleleza anapokaa dada, mama alinieleza anakaa pembeni ya Soko la Mkuyuni, duka lake linatazamana na soko. Siku moja baada ya kutoka shule nilipitia moja kwa moja hadi kwa dada.
Kufika kwake sikupotea, nilifika bila tatizo kutokana na duka lake kuonekana, pia ndilo lililokuwa kubwa. Nilipofika dukani, dada aliponiona alifurahi sana.
“Karibu mdogo wangu.”
“Asante.”
“Umekuja na nani?”
“Peke yangu.”
“Umepajuaje hapa?” Dada alinishangaa.
“Amenielekeza mama, sehemu yenyewe si ya kupotea.”
“Ni sehemu nyeupe, karibu mdogo wangu.”
“Asante”
“Nyumbani hawajambo?”
“Hawajambo, mama anakusalimia.”
“Baba anajua umekuja huku?”
“Walaaa”
“Karibu soda upoze koo,” alisema dada huku akinifungulia soda.
Nilipokea soda na kuanza kunywa, wakati huo dada alikuwa akihudumia wateja waliokuwa wakinunua bidhaa dukani kwake, baada ya kumaliza kuwauzia alinigeukia.
“Mmh! Habari za shule?”
“Nzuri tu dada.”
“Umetumwa au?”
“Dada siji kwako mpaka nitumwe?”
“Siwajahi kukuona ndiyo maana nashangaa, ni muda gani toka niondoke nyumbani. Najua wote mlinichukia kwa kujua nataka kuwanyang’anya utajiri wenu.”
“Dada mimi sijui chochote zaidi ya baba kukukatalia na kuondoka kwa nguvu, zaidi ya hapo sijui lolote. Na mimi nikukasirikie kwa sababu gani wakati kuondoka kwako kumekuwa mateso na simanzi kwangu kama kuna uwezekano nije nikae kwako.”
“Najua mdogo wangu unanipenda, lakini baba yako hatakubali, ataona nataka kuuhamisha ukoo mzima.”
“Kwani dada kuna nini, mbona mazungumzo yako yamejaa uchungu?”
“Si wenzako wamekuja hapa bila aibu wala huruma na kuzungumza maneno ya kipuuzi,” dada alisema kwa sauti yenye kuonesha huzuni kidogo.
“Tena kweli dada kuna siku kulikuwa na kikao wote walikuwepo kasoro wewe, kwa nini hukuja?”
“Kikao hicho kilikuwa cha kunijadili mimi.”
“Wewe! Umefanya nini?”
“Unajua mdogo wangu wewe bado unakua, lakini kuna mambo ambayo sitaki yakutokee kama yaliyonitokea mimi.”
“Mambo gani?”
“Sasa hivi Masalu unazidi kukua na kupata ufahamu, kidato cha tatu ni upevuko wa akili.”
“Ni kweli dada.”
“Unajua kwa nini nimehama nyumbani?”
“Mmh, sijui.”
“Masalu sasa hivi una akili unajua zuri na baya.”
“Ni kweli dada.”
“Hivi maisha yangu ni sawa na ndugu wengine?”
“Kivipi?”
“Nina nyumba?”
“Hapana”
“Nina gari?”
“Hapana”
“Nina mtoto?”
“Unajua ni kwa nini?”
“Sijui.”
“Hivi maisha tunayoishi ni sawasawa na utajiri wetu?”
“Hapana.”

SIMULIZI HII SIOYAKUKOSA
ITAAENDELEA KESHOOOOOO
##Soma sehemu ya BABA KIUMBE WA AJABU - 02
hapa: ==>www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

BABA KIUMBE WA AJABU - 02

$
0
0
“Ni kweli dada.”
“Unajua kwa nini nimehama nyumbani?”
“Mmh, sijui.”
“Masalu sasa hivi una akili unajua zuri na baya.”
“Ni kweli dada.”
“Hivi maisha yangu ni sawa na ndugu wengine?”
“Kivipi?”
“Nina nyumba?”
“Hapana”
“Nina gari?”
“Hapana”
“Nina mtoto?”
“Unajua ni kwa nini?”
“Sijui.”
 “Hivi maisha tunayoishi ni sawasawa na utajiri wetu?”
“Hapana.”
2
“Hujiulizi kwa nini wengine wanafurahia maisha, wanakula chakula kizuri wanalala pazuri wanatembelea magari ya kifahari wewe na mimi tunateseka wakati baba na mama yetu ni mmoja.”
”Huwa najiuliza, nikienda kwa kina kaka au dada nakula chakula kizuri hata kulala sehemu nzuri tofauti na kwetu.”
“Hivi uwezo wa baba bado mama anaweza kulima tena kwa mkono na kuokota kuni kuja kupikia?”
“Dada hata mimi nachanganyikiwa.”
“Na wewe bila mimi kukuongeza pesa ungenunua hata chungwa ukienda shule?”
“Yaani dada toka uondoke napewa nauli ya daladala tu, tena pesa ya mwanafunzi shilingi mia.”
“Unaona sasa, hebu subiri,” dada alisema huku akimsogelea mteja kumuuzia kitu.
“Na donda lililokuwa mguuni kwangu uliliona kwa muda gani?”
“Mmh, muda mrefu sana.”
“Unaliona tena?” Dada alinionesha sehemu iliyokuwa na donda ambayo ilikuwa imepona na kuweka alama nyeusi.
“Ha! Dada umepona?”
“Nimepona mdogo wangu, lakini utajiri umeingia ufa”
“Ufa! Una maana gani?”
“Donda langu ndilo chanzo cha utajiri.”
“Unasema!” Kauli ya dada ilinishtua.
“Masalu utajiri wetu una siri nzito.”
“Siri! Siri gani hiyo?”
“Masalu utajiri wetu una siri nzito ambayo mimi ndiye niliyeibeba na sasa hivi nimeitua.”
“Una maana gani kusema hivyo?”
“Masalu kuna mambo huwezi kuyajua kutokana na umri wako, lakini kutokana na ukaribu na kuelewana kwetu sina budi kukufunulia yaliyojificha ili ujue nini kimetuzunguka. Mwanzo nisingeweza kukuambia kwa vile nimeelezwa kuwa maisha yangu hayatakuwa marefu hivyo leo nimefurahi sana kuja hapa. Haya nitakayokueleza leo si ya kutunga na kila ulilokuwa na swali nalo leo nitakupa jibu lake.
“Masalu mdogo wangu maisha yetu kabla hujazaliwa yalikuwa ya kawaida tu, baada ya baba kustaafu kazi pesa alizolipwa alinunua nyumba mnayoishi sasa hivi na pick up moja ambayo alifanyia kazi zake za kutuingizia kipato na kufungua duka ambalo lilikuwepo muda mrefu toka nikiwa darasa la nne.
“Maisha yaliendelea kama kawaida huku tukionekana familia yenye uwezo kwa sisi wote kusoma elimu nzuri. Walionitangulia wote walisoma elimu ya sekondari, lakini mimi nilipomaliza darasa la saba sikuweza kuchaguliwa kuendelea na kidato cha kwanza.
“Lakini niliamini ningeendelea kusoma shule ya kulipia kama ndugu zangu walionitangulia. Wakati tukifanya taratibu za kunichukulia fomu ya kuanza kidato cha kwanza, siku moja nikiwa natoka chooni usiku kuna kitu kilinigonga mguuni. Nilipiga kelele kuomba msaada.
“Baba na mama walitoka na kuja nilipokuwa nimeshika mguu huku nikirukaruka, lakini ajabu hakukuonekana kitu chochote cha kuwashtua kutokana na nilivyokuwa. Nikiwa na wasiwasi labda nimegongwa na nyoka baba alinipa dawa ya maumivu na kunieleza patapoa tu.
“Usiku nililala vizuri, lakini asubuhi nilipoamka nilikuta mguu umevimba hata kutembea sikuweza. Sehemu ya juu kidogo ya mguu wa kulia kwa ndani kuliweka alama nyeusi, sikupelekwa hospitali zaidi ya kukandwa na dawa ya majani. Basi mdogo wangu mguu huo umenisumbua kwa muda mrefu bila kupelekwa hospitali.
“Hata muda wa kwenda shule ulipofika sikuweza kupelekwa shule kutokana na hali ya mguu wangu. Mpaka kipindi cha uandikishaji wanafunzi kinakwisha bado hali yangu ilikuwa tete hivyo sikuweza kujiunga na sekondari. Roho iliniuma rafiki zangu wengi walianza kidato cha kwanza. Nikawa mimi na ndani ndani na mimi, sehemu iliyokuwa na weusi ilikuwa ikiwasha na mwisho iliweka kidonda.
“Ajabu baada ya kutoka kidonda, mguu ulirudi katika hali yake ya kawaida, hata mti niliokuwa natembelea niliutupa. Niliona kama muujiza mguu wangu kurudi katika hali yake, niliamini mguu wangu ulikuwa wa kukatwa tu baada ya wazazi wangu kutoonesha juhudi zozote za kunipeleka hospitali.
“Hata nilipoweza kutembea sikuruhusiwa kutoka nje kama wenzangu, maisha yangu yalikuwa ya uani, kidonda changu kila siku kilikuwa kikivuja maji. Mdogo wangu wakati huo sikujua kama kidonda kile kilikuwa na sababu yake. Hali ya  maisha nayo ilibadilika, kulitokea mabadiliko makubwa sana.
“Kwa muda mfupi tulinunua magari, kuongeza majumba kila kona ya Jiji la Mwanza na miradi mingi, ndugu zangu walifunguliwa maduka makubwa Mwanza mjini na mimi kukabidhiwa duka la pale nyumbani ambalo liliongezwa vitu vingi. Naimani mpaka unapata ufahamu ulinikuta dada yako nina kidonda mguuni.
“Siku zote nilihoji kwa nini wazazi wangu hawataki kunipeleka hospitali au kuniwekea dawa. Baba alinieleza kuwa kama wataniwekea dawa ya aina yoyote kidonda mguu utaoza, akaniambia kitapona chenyewe, nami nilikubali mwanzo bila kujua mwisho wake utakuwa nini.
“Pia nilipewa masharti ya kutotembea na mwanaume, nikaambiwa nikifanya hivyo nitakufa. Kwa vile umri wangu ulikuwa mdogo usiotakiwa kujiingiza katika mapenzi halikunisumbua sana. Siku zilizidi kukatika huku maisha yakibadilika kila siku, nami nilivunja ungo wa kuwa na hamu ya wanaume.
“Katika wateja wangu kuna kijana mmoja ambaye kwa kweli tulipendana naye sana na kunitamkia kuwa anataka kunioa si kunichezea baada ya kumueleza simjui mwanaume. Nilimueleza mama ambaye alinikemea sana kuwa nisirudie tena kusema kitu kama kile nitaweza kukorofishana na baba.
“Kutokana na kumuogopa baba niliamua kukaa kimya, siku zilikatika huku utajiri wa baba ukizidi kuwa wa kutisha na ndugu zangu wote wakinunua magari ya kifahari na kujenga maghorofa. Kila nilipotaka na mimi kuhama nyumbani na kuanzisha duka langu, kununua gari zuri na nyumba ya kifahari kama wenzangu nilizuiwa.
“Ajabu nilikaripiwa sana tena eti nisirudie tena kusema hivyo, majibu ya mama yalinishtua sana na kujiuliza iweje wote wawe na maisha mazuri kasoro mimi? Nilijiuliza labda mimi si mtoto wa mzee Makumiyane, lakini mama alinihakikishia ni mtoto halali wa mzee Makumiyane.
“Na hilo niliamua kuliacha kutokana na kumuogopa sana baba, muda ulivyokuwa ukienda ndugu zetu wote waliondoka na kuanzisha maisha yao na kubakia sisi wawili na wazazi wetu. Roho iliniuma sana siku ndugu zangu walipokuja kututembelea, kila mmoja alikuja na gari la kifahari. Hiyo ilikuwa tisa, kumi ilikuwa harusi za ndugu zangu ambazo ziliniumiza roho na baada ya muda walipata watoto.
“Nilijikuta nikijitoa mhanga na kumfuata baba kumuomba haki yangu kama wenzangu, baba alinigombeza kama ilivyokuwa kawaida yake. Lakini nilimueleza kuwa kama hataki basi kuna siku nitatoroka na kwenda kuanzisha maisha yangu kutokana na yeye kutoonesha kunijali au kunipa haki sawa na wenzangu.
“Alinitisha kama nitajaribu kutoka nyumbani nitamtambua, vitisho vyake havikunibabaisha baada ya kuona sina faida ya kuwepo pale eti kisingizio nina duka. Siku iliyofuata nilibeba kila kilicho changu na kuondoka, mama alinibembeleza nisiondoke lakini sikubadili uamuzi wangu. Ilibidi akimbiliwe baba alipokuja alishangaa uamuzi wangu.
 “Nilimueleza nipo tayari kwa lolote atakalotaka kunifanyia, msimamo wangu ulimtisha sana baba na kuamua kuniweka chini na kunieleza siri iliyoniacha mdomo wazi.
“Nikabakia mimi siolewi, sina maisha mazuri, sina mtoto. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuvumilia. Nakumbuka siku moja kijana ambaye alitaka kunioa alikuja na kuniulizia ombi lake, siku ile baba na mama walikuwa wamekwenda kwenye sherehe ya mtoto wa dada aliyekuwa akipata ubatizo.
“Siku ile mdogo wangu lazima niseme ukweli kwa vile sina jinsi, nilitoka na kwenda kwa yule kijana na nilifanya naye mapenzi. Kwa kweli penzi nililopata lilinichanganya nikawa sisikii wala sioni. Ilifikia wakati wa kutoroka usiku kwa kuruka ukuta na kwenda kwa yule bwana.
“Mchezo ulinichanganya sana hata kutamani kuhama nyumbani.
“Kumbe kufanya kwangu mapenzi kulikuwa kunasababisha matatizo katika familia, kwa wiki moja kulitokea mambo ya kutisha. Moja nyumba ya Malimi iliungua moto na hakuna kilichosalimika, kabla hatujatulia gari la kaka lilipata ajali mbaya iliyosababisha lisirudi tena barabarani.
“Baba naye alivamiwa na majambazi akipeleka pesa benki za mauzo ya mwezi mzima. Hali ile ilimchanganya baba na kwenda kwa mganga wake kuulizia sababu ya majanga yale. Jibu aliambiwa mali imeingia uchafu kwa mimi kufanya mapenzi.
“Baba alikuja juu na kunitishia, nami sikumuogopa nilimueleza ukweli kama mimi ndiye chanzo cha utajiri kwa nini niwe na maisha duni wakati watu wasiojua adha niipatayo kutokana na mali wanazochezea kuishi maisha mazuri. Nilimueleza baba kuwa kama hatanipa mali tena iwe zaidi ya ndugu zangu wote lazima nitaondoka na kwenda kuishi maisha yangu.
“Baba alinitisha kwa kusema kama nitaondoka sitakaa muda mrefu lazima nitakufa, vitisho vile sikuviogopa na kumhakikishia kuwa nitaendelea na msimamo wangu na nipo tayari kufa lakini si kuwa kitega uchumi cha watu. Mama naye aliingia kwenye kazi ya kunibembeleza ili nibadili tabia zangu zilizoonekana chafu.
“Nilikubali kubaki nyumbani kwa masharti na mimi natakiwa niwe na gari na duka kubwa ambalo nitalimiliki mwenyewe. Tulikubaliana na mimi kufuta wazo la kuondoka nyumbani. Nilisubiri kutekelezewa niliyoyataka kwa hamu kubwa, nami nilikuwa na hamu ya kuendesha gari, nilikuwa na hamu ya kumiliki mali yangu mwenyewe.
“Siku zilikatika bila kuona dalili zozote za kununuliwa gari wala nyumba, wakati huo nilikuwa nimesimamisha mapenzi na shemeji yako. Mambo yalizidi kunyooka kwa  Malimi aliyeunguliwa nyumba yake kujenga ghorofa analoishi sasa.
“Lakini mwenyewe sikuona kitu chochote, kila nilipouliza niliambiwa nisubiri mambo hayajakaa vizuri. Mambo hayajakaa vizuri wakati ndugu zangu kila kukicha  walibadilika kimaisha? Niliona kama wananichezea, nikaanza kuweka pesa zangu taratibu bila kumshirikisha mtu.
“Shemeji yako nilimtuma anitafutie sehemu ya kufungulia duka akapata huku, nilimpa pesa za kulipia mwaka mzima na kumuagiza anunue vitu vyote muhimu kwa ajili ya duka naye alifanya kama nilivyomuagiza. Unajua Masalu katika maisha yangu huwezi kuamini toka nipatwe na tatizo la mguu lililozaa kidonda sikuruhusiwa kwenda kanisani.
“Ndugu zangu wote ndiyo waliokuwa wakienda kanisani, lakini mimi nilizuiwa kwa kuambiwa kama nitakwenda kanisani nitasababisha maafa makubwa kuliko yale ya kutembea na mwanaume. Nilijiuliza mimi ndiye sitakiwi kwenda kanisani lakini wadogo na dada zangu wote mlikuwa mnakwenda, kwa nini?
“Nilikatazwa hata kusoma Biblia, baba alisema mizimu haitaki kuchanganya mambo ya Mungu na mizimu. Basi nilibakia simjui Mungu wala kanisa. Baada ya kukamilisha vitu vyote muhimu vya dukani, shemeji yako alilisifia duka alivyolijaza. Nilijipanga kwa siri na siku moja nilitoroka usiku na nguo zangu bila wao kujua. Masalu siku mlipoamka na kunikosa ilikuwaje nyumbani?” Dada Monika aliniuliza huku akiwa ametuliza macho usoni kwangu.
“Mmh, kwa kweli walichanganyikiwa sana, walihaha kila kona, familia yote iliitwa asubuhi ile na kukutana. Hata mimi nilizuiwa kwenda shule, kilikuwa kikao kizito kilichokujadili. Niliwasikia wakisema bila kukuona kila kitu kitaharibika, siku ile hakuna kazi iliyofanyika, maduka yote yalifungwa na kuanza kukutafuta.”
“Basi mdogo wangu nilikuja huku kuanza maisha yangu ili kupata uhuru wa maisha wa kupanga mambo yangu bila kuingiliwa na mtu. Pesa niliyokusanya niliamini mpaka iishe nitakuwa nimepiga hatua kubwa katika biashara kwa vile nilikuwa naijua vizuri.
“Walianza upelelezi wa chinichini na kumjua mpenzi wangu ambaye walimbana kwa kumpeleka polisi ili awajulishe nilipo. Mwanzo aligoma kutokana na masharti niliyompa kama wazazi wangu watamuona asikubali. Mpango wetu ulikuwa kuishi pamoja nami nilitaka yeye asirudi tena kule.
“Lakini kwa vile familia yake ipo kule walifanikiwa kumpata na baada ya kumbana sana aliwaleta hapa. Kama utakumbuka siku waliyokusanyana kuja kwangu ilikuwa baada ya kumtuma mtu kwa siri bila kujua ninapofanyia kazi zangu na kuamua kukusanyana kuja hapa ili nikubali kurudi nyumbani.
“Basi walipofika kila mmoja ooh, Monika umefanya vibaya kuondoka nyumbani wakati unafahamu kila kitu. Niliwaeleza siwezi kuumia mimi wakati wenyewe wanakula maisha, kama hivyo basi kidonda changu achukue mtu mwingine. Hakuna aliyekuwa tayari kuchukua ugonjwa wangu.
“Nilijua mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu, mwisho wa yote walikubali niendelee na kazi zangu kwa makubaliano nisitembee na mwanaume au kukitibu kidonda. Niliwakubalia ili kuwaridhisha kuwa nitafanya kama wanavyotaka. Lakini sikuwa tayari kukubaliana na ujinga wao tena.
“Nami nilikuwa na hamu ya kuwa na mwanaume ambaye muda ule alikuwa akija mara moja na wakati huo ndiyo alikubali kuhamia kwangu kabisa.
“Baada ya kuondoka niliendelea na mpenzi wangu ambaye muda huo nilikuwa nakaa naye nyumba moja, kupika na kupakua, sasa hivi yupo kwenye mihangaiko yake muda wake wa kurudi ni saa moja usiku. Ila jumapili huwa haendi popote.
“Tangu nihamie huku siku hizi nakwenda kanisani kama kawaida, ajabu ya Mungu kidonda kilianza kupona chenyewe bila kukiwekea dawa. Kumbe kidonda changu kilivyokuwa kikipona na mambo yalibadilika katika utajiri wa familia yetu. Matatizo yalitawala kwa maduka kuibiwa vitu vyote bila kujua tatizo ni nini.
“Kama kawaida walirudi kwa mganga na kuelezwa kuwa nimeishapona pia ninaendeleza kufanya uchafu katika mali ya familia yangu. Walijikusanya kama ilivyo kawaida na kuja kuniomba niokoe mali ya familia, niliwaeleza katu sitakubali kufanya tena ujinga ule.
“Baada ya juhudi zote kushindikana baba aliniapia mwaka huu siumalizi lazima nitakufa. Nilimhakikishia yeye si Mungu, kama kufa nitakufa kwa amri ya Mungu. Wote waliondoka vichwa chini wakiamini wanarudi katika maisha ya kawaida, tokea siku hiyo sijawaona tena na maisha yangu yanaendelea kama kawaida na muda si mrefu nawe utapata mjomba.”
“Dada una mimba?”
“Ndiyo mdogo wangu.”
“Mmh, Mungu mkubwa.”
“Basi mdogo wangu siri uliyokuwa huijui ndiyo hiyo, nasikia sasa havi mambo yote hayaendi vizuri kabisa na wamechanganyikiwa.”
“Ni kweli dada sasa hivi kila siku baba analalamika na kusema angekuwa na uwezo angekuulia mbali.”
“Sasa aniue kwa sababu gani? Kwa watoto wa mzee Makumiyane ni mimi peke yangu? Niliwaeleza mmoja ajitoe akichukue kidonda change lakini kila mmoja alikaa nyuma kukikimbia kidonda. Basi mdogo wangu nikifa leo ujue nimekufa kwa kukikataa kidonda.

INAENDELEA HAPA

BABA KIUMBE WA AJABU - 03

$
0
0

MTUNZI: ALLY MBETU
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

“Dada una mimba?”
“Ndiyo mdogo wangu.”
“Mmh, Mungu mkubwa.”
“Basi mdogo wangu siri uliyokuwa huijui ndiyo hiyo, nasikia sasa havi mambo yote hayaendi vizuri kabisa na wamechanganyikiwa.”
“Ni kweli dada sasa hivi kila siku baba analalamika na kusema angekuwa na uwezo angekuulia mbali.”
“Sasa aniue kwa sababu gani? Kwa watoto wa mzee Makumiyane ni mimi peke yangu? Niliwaeleza mmoja ajitoe akichukue kidonda change lakini kila mmoja alikaa nyuma kukikimbia kidonda. Basi mdogo wangu nikifa leo ujue nimekufa kwa kukikataa kidonda.
3
“Siogopi kufa hata siku moja, kila kiumbe kitakufa! Kama nitakufa kwa kukataa kidonda nipo tayari, ila namuomba Mungu aniue baada ya kumzaa mwanangu ili niache jina langu,” dada alisema huku machozi yakimtoka,  moyo wangu uliingia baridi ya woga wa ajabu kwa yote niliyoelezwa na dada juu ya siri nzito ya utajiri wetu iliyokuwa ikibebwa na kidonda cha dada.
Kingine kilichonitisha kilikuwa kusikia kuwa dada eti atakufa baada ya kukikataa kidonda. Machozi ya dada yaliniumiza sana moyo wangu na kumuonea huruma.
“Dada kwa nini usikubali kuliko kukubali kufa?”
“Masalu wewe hujui lolote katika maisha, lakini unakumbuka haya niyasemayo  hata kama nikifa leo utayakumbuka maneno yangu. Kwa vile wote wameshazaa na kufanya mapenzi hawawezi kupatwa na kidonda. Wasiwasi wangu kikitoka kwangu kinaweza kurudi kwako.”
“Ha! Dada mbona unanitisha.”
“Kutokana na siri ya kidonda niliyoelezewa na baba, nakumbuka nilimuuliza kwa mfano nikifa itakuwaje? Alinieleza itabidi atafutwe aliye safi ndani ya familia. Nilimuuliza tena ni kwa mwanamke tu? Alinijibu ni kwa mtu yoyote mwanamke au mwanaume aliye msafi, unafikiri nani atakayekichukua kidonda changu kama si wewe?”
“Mimi sikubali.”
“Masalu huna jeuri ya kumbishia baba.”
“Nitahamia kwako.”
“Uhamie wapi nami umesikia lazima nitakufa?”
“Huwezi kufa dada, ni vitisho.”
“Hata nisipokufa siwezi kukukubali tena hicho kidonda kisicho na faida zaidi ya mateso.”
                                                                     ****
Kwa kweli sikuweza kumshawishi dada kutokana na msimamo wake mkali, jioni ilipofika niliagana na dada kwa kupanda daladala mpaka nyumbani. Nilipofika nyumbani nilikuwa na mawazo mengi juu ya maneno ya dada ambayo sikuamini kama yana ukweli wowote, nilipinga kuwa utajiri wetu si kupitia kidonda chake. Nilipoangalia hali ya maisha yetu ilikuwa ya kawaida tofauti na kauli ya dada ya kusema sasa hivi maisha ni magumu upande wa familia.
Chakula tulikula kama kawaida ambacho kwa kweli hakikuwa na hadhi ya utajiri uliotuzunguka. Lakini kwa muda ule sikushtuka kutokana maisha yale ndiyo yaliyokuwa ya kawaida ya siku zote. Japo kwa mbali nilijawa na maswali iweje nyumbani maisha yetu ya kawaida.
Kingine ambacho alikisema dada kiliniingia akilini kilikuwa kwa mama kuamka kila siku asubuhi na kwenda kulima wakati baba alikuwa na pesa nyingi. Kingine nilichokubaliana na dada ni mama kuokota kuni na kuja kupikia wakati dada zetu wanatumia majiko ya umeme na gesi.
Lakini kitu ambacho sikukubaliana naye ni imani za kishirikina kwanza maisha yetu yanategemea ushirikina wa kidonda chake. Katika akili yangu niliamini kidonda cha dada hakikuwa kimepata tiba sahihi. Lakini baada ya kupata tiba sahihi kilipona.  Niliamini dada alitaka kunijengea uadui na wazazi ili niwaone ni watu wabaya wasiofaa.
Sikutaka kumuamini dada zaidi ya kuona anataka kunipotosha, lakini siri ile nilibaki nayo moyoni sikutaka kumwambia mtu. Siku zilizidi kukatika nami niliendelea na masomo kama kawaida. Pamoja na kuyapuuza ya dada na kuyaona kama ya uchonganishi lakini kuna vitu vilikuwa vikitia wasiwasi. Kuna siku nilimsikia baba akimwambia mama kwa sauti iliyoonesha hawakuniona kutokana na kiza kilichokuwepo.
“Mama Monika nimempa mpa muda mwanao wa kutosha, litakalotokea tusilaumiane.”
“Sasa mimi nitafanyaje kama mwenyewe hajihurumii.”
“Hali ni mbaya tukiendeleza huruma tutaadhirika.”
“Baba Monika mimi mwenyewe nilikwenda kwa Monika, lakini kiburi kimemjaa tena amekosa hata heshima kujua anazungumza na mama yake.”
“Mganga amenipa mwezi huu mwisho la sivyo kihame kwa mwingine.”
“Unafikiri kitaenda kwa nani?”
“Hilo suala tutalizungumza baada ya kushindikana kabisa.”
“Yaani Monika kanichanganya sana.”
“Basi uamuzi ni huo sina mwingine.”
“Utakavyokuwa mimi tena simo kayataka mwenyewe.”
Mazungumzo ya baba na mama kumhusu dada Monika yalinishtua sana na kujiuliza baba alikuwa anataka kufanya nini? Nilijiuliza au ndiyo niliyoelezwa na dada Monika juu ya kumlazimisha aendelee kuwa na kidonda na kama kikihama kitaenda kwa nani?”
Pia nilijiuliza mama alikuwa na maana gani kusema yakimkuta dada Monika hayumo ni mambo gani hayo. Nilijikuta nikiingiwa na wasiwasi wa maneno ya dada Monika kuwa baba alimtishia maisha kuwa kama akikataa kuendelea kuwa na kidonda hatadumu lazima atakufa.
Nilijikuta nikikosa raha na kutamani kwenda kumuomba dada akubali kuliko kutokewa na balaa lile. Kwa mbali nilijikuta njia panda kuamini kuwa kidonda cha dada ndicho kilikuwa kikifanya tuwe matajiri. Nilitamani nizungumze na mama kuhusu kujua baba alikusudia kufanya nini kwa dada.
Japo niliogopa kuulizwa nimejuaje, lakini nilipanga siku ya pili sitakwenda shule na kumfuata mama shambani kumuuliza kuna kitu gani dada Monika anataka kufanyiwa baada ya kukataa kuwa na kidonda kile. Usiku kwangu ulikuwa mzito sana niliota mambo mazito ambayo yalinitisha na kunifanya niamke saa nane za usiku na kukesha bila kulala.
Niliota familia yetu ikifanya sherehe kubwa huku dada Monika akiwa amekufa na mwili wake haukuwa na mguu mmoja uliokuwa ukivuja damu, ule mguu uliokuwa na kidonda. Damu ya dada Monika ndugu zetu walikuwa wakinywa kwa furaha. Niliamka na kukaa kitandani nikitweta. Nilijiuliza ndoto ile ina maana gani.
Baada ya muda usingizi ulinipitia, muda haukupita niliota ndoto nyingine mbaya, niliota nimeoza mguu sehemu ya ndani na kuanza kutoka funza, ajabu ndugu zangu walifurahia kama ndoto ya mwanzo ya kufurahia kifo cha dada Monika kwa kumla na kunywa damu yake.
                                                            *****
Nilishituka usingizini na kuogopa kulala tena mpaka asubuhi, asubuhi nilisingizia naumwa. Sikwenda shule, nilitoka ndani na kwenda kulala sebuleni ili kuogopa kuota ndoto za kutisha. Sebuleni nilipolala sikuota ndoto mpaka nilipoamka kujiandaa kwenda kwa mama shamba baada ya kufungua kinywa.
Nilioga na kufungua kinywa kisha nilielekea shambani kwa mama ili nikamuulize kuna kitu gani dada Monika anataka kufanyiwa na baba, kama kumuua ningepinga kwa nguvu zangu zote.
Nilikwenda hadi shambani na kumkuta mama akiwa katikati ya kilimo, sikumsemesha kitu, nilijiuliza iweje tuwe na pesa majumba na magari mama ateseke kiasi kile. Nilizidi kuingiwa na wasiwasi juu la mambo yaliyokuwa yakifanyika.
Baada ya muda nilimwita mama, aliponiona alishtuka na kuniuliza.
“Masalu kuna usalama?”
“Upo mama.”
“Si unaumwa, umekuja huku kufanya nini?”
”Kuna kitu nataka kuuliza mama.”
“Kitu gani?”
Mama alisema huku akiweka pembeni jembe na kunifuata nilipokuwa nimesimama.
“Masalu una nini mwanangu?”
“Mama jana nimeota ndoto mbaya sana.”
“Ndoto gani mwanangu?”
“Kuhusu dada Monika.”
“Monika! Ndoto inahusu nini?”
Nilimhadithia ndoto niliyoota, mama alishtuka na kutulia kwa muda kisha alisema kwa sauti ya chini.
“Sasa wewe wasiwasi wako nini?”
“Mama kuna maneno nilizungumza siku moja na dada Monika kuhusu baba kumtishia kifo na kunieleza kama akifa nijue baba ndiye aliyehusika.”
“Masalu!” Mama alishtuka.
“Naam mama.”
“Mlifikia wapi mpaka mkazungumza hayo?”
“Kuna siku nilikwenda kwa dada Monika na kumuuliza sababu ya yeye kuhama nyumbani. Mama dada alinieleza mambo mengi ya kutisha sana lakini sikuyaamini.”
“Masalu alikueleza mambo gani Monika?”
Nilimuhadithia baadhi ya mambo kisha nilimueleza ya yeye kulima wakati tuna pesa.
“Eti mama hata kulima kwako amesema ni imani za kishirikina iweje tuwe na pesa wewe ulime wakati ungewalipa watu wakatulimia?”
“Mmh, mbona makubwa!” Mama alizidi kushangaa.
Mama alisema huku akitoka shambani na kunisogeza chini ya mwembe.
“Masalu wewe hayo unayaamini?”
“Siwezi kuyaamini japo kuna mengine yana ukweli.”
“Nakuomba asikubaliane na maneno ya Monika ni ya uongo.”
“Mama mbona baba alisema jana litakalomtokea asilaumiwe, nini kitamtokea dada Monika?”
“Wee Masalu!” Mama alizidi kushtuka kuona ninajua vitu vingi.
Ilionesha mama aliamini siyajui mengi kuhusiana na mambo yaliyokuwa yakitendeka nyumbani. Nilimuona akifuta jasho kwenye paji la uso kisha alinipandisha na kunishusha na kusema.
“Masalu wewe ni mtoto, hujui kitu hata nikikueleza hutanielewa, nakuomba uachane na hayo, swali hili ungemuuliza baba yako mngekosana.”
“Mama hujanijibu, jibu si kukosana bali kupata ukweli nilioelezwa na dada Monika juu ya kukataa kwake kidonda na baba kumtishia kuyakatisha maisha yake.”
“Hilo si kweli, ni ujinga wa dada yako kama kufa atakufa na yake.”
“Mama, baba aliposema kuwa asilaumiwe na wewe kusema shauri yake alikuwa na maana gani?”
“Masalu naomba usiniulize swali kama hilo tena,” mama alikuwa mkali.
Niliona nibadili mada kwa kumuuliza swali lingine.
“Halafu mama kwa nini tusitafute mtu atulimie na wewe kupumzika, tuna faida gani kuwa na pesa na wewe mama unaendelea kuteseka?”
“Masalu nakuomba uondoke, nakuona umekosa maneno ya kuzungumza,” mama alikuwa mkali.
Kila neno nililolisema kwa mama lilimuudhi, sikutaka kuendelea kulumbana naye, niliamua kurudi zangu nyumbani nikiwa bado nipo njia panda. Wazo la haraka lilikuwa kwenda kwa dada Monika kumueleza akubaliane na matakwa ya wazazi ili asije kujutia maisha yake. Nilipofika nyumbani nilijawa na mawazo mengi sana kuhusiana na majibu ya mama.
                                                            *****                                                      
Nilipanga siku ya pili nitaaga na kwenda shule lakini kituo changu cha kwanza kingekuwa kwa dada Monika kumueleza hali halisi kutokana maneno ya baba. Siku ile sikushinda na furaha kila nilipokumbuka ndoto nilizoota usiku na majibu ya mama.
Japo niliamini mama hawezi kumueleza baba niliyomuuliza, bado nilikuwa na wasiwasi kama atamueleza basi lazima baba angenishikisha adabu kufuatilia mambo yasiyonihusu. Lakini siku ilikatika bila kuulizwa swali lolote na baba zaidi ya mama kuniita na kunionya nisirudie tena kuuliza mambo yale wala kumueleza mtu yoyote.
Nilimuahidi mama sitarudia kumueleza mtu maneno yale, kwa furaha ya mama alinipa pesa za kula shule kitu ambacho hakuwahi kukifanya zaidi ya kila siku kunipa nauli tu. Niliamini ile itanisaidia kuongeza nauli ya kwenda kwa dada. Usiku nilipolala ndoto ya jana yake ilijirudia.
Nilijikuta nikikesha kwa mara nyingine mpaka asubuhi kwa kuogopa kila nilipofumba macho njozi mbaya zilinifuata. Chumba nilikiogopa na kujiuliza njozi zile mbaya za dada Monika kuliwa nyama huku familia yote ikifurahia zilikuwa na maana gani? Kingine kilichonitisha mguu wangu kuoza na kutoa wadudu.
Nilijikuta nikiogopa kufumba macho na kubaki macho mpaka kunakucha, alfajiri nilisikia habari zilizonishtua sana. Nilimsikia baba akimwambia mama:
“Aliyoyataka mwanao yametimia.”
“Unataka kuniambia Monika ame...”
“Ishia hapohapo na sitaki utoe chozi unajua nini tuliambiwa.”
Nilishtuka na kutoka nje na kuwakuta baba na mama sebuleni, mama aliponiona alishtuka tofauti na baba.
“Mama dada Monika kafanya nini?”
“Kwani umesikia nini?” Baba aliniuliza.
“Sijui...ame..”
“Amefanya nini?”
“A..me..mee,” nilijikuta nikipata kigugumizi.
“Hebu ondoka hapa asubuhi yote nini kimekuamsha,” baba alinifokea.
Nilirudi chumbani kwangu nikiwa bado sielewi dada Monika kafanya nini japo bado wasiwasi wangu ulikuwa labda amefariki kutokana na maelezo ya dada Monika na kauli ya baba juu ya dada Monika. Kwa kauli ya baba ambayo aliifunga, niliamini kabisa dada Monika huenda kweli amefariki. Kwa vile muda wa kujiandaa kwenda shule ulikuwa umekaribia nilikwenda kuoga ili nijiandae na shule.
Baada ya kuoga nilirudi chumbani kwangu kujiandaa kwenda shule, nikiwa bado nipo katika maandalizi nilishtuka kusikia sauti za ndugu zangu, ujio wao wa asubuhi ile ulinishtua sana.Niijiuliza kuna kitu gani kimetokea au ndiyo niliyokuwa nayafikiria ya kifo cha dada Monika? Sikutaka kutoka haraka, nilimalizia kuvaa nguo za shule, baada ya kuvaa nilitoka ili nijiandae.                                                              
Nilishtuka kuwaona dada na kaka zangu wamekaa sebuleni, waliponiona walishtuka na kuniuliza:
“Masalu unakwenda wapi?”
”Shule.”
“Unakwenda shule hujui hapa nyumbani kumetokea nini?”
”Sijui.”
“Mmh, makubwa, Monika amefariki.”
“Eti?
“Monika amefariki.”
“Dada Monika?” Bado sikuamini.
“Eeeh, huyo huyo.”
“Siamini …siamini.”
Bila kujielewa nilijizoa mzimamzima na kujipiga chini na kupoteza fahamu, baada ya huduma ya kwanza nilipata fahamu na kuangua kilio tofauti na wenzangu ambao hakuna hata mtu mmoja aliyemwaga chozi. Juhudi za kunibembeleza zilishindikana. Bila kujielewa nilijikuta nikisema kwa sauti ya juu:
“Yote uliyonieleza dada yangu nilifikiri utani kumbe kweli wamekuua.”
“Alikueleza nini?”
”Baba kwa nini umemuua dada Monika?”
“Wee Msalu maneno gani hayo?”
“Maskini dada yangu kumbe ulikuwa na siri nzito moyoni mwako ambayo imenifumbua leo, ungekufa dada yangu bila kujua lakini Mungu mkubwa.”
“Masalu hebu ondoa uchuro hapa.”
“Siwezi… siwezi, kwa nini lakini umemuua dada Monika?” Niliendelea kulia kwa uchungu huku nikijipigiza chini.
“Nani kamuua Monika?”
“Nyinyi wote kwa tamaa za mali.”
“Masalu unatukosea adabu.”
“Siwakosei adabu bali ukweli ni huo.”
Kaka mkubwa alinichukua na kutoka na mimi uani huku nikiendelea kulia, roho iliniuma kumpoteza kipenzi dada yangu Monika mtu aliyenipenda kuliko yeyote. Kutokuonesha ndugu zangu kuguswa na kifo cha Monika niliamini ndoto niliyoota ilikuwa na maana kubwa. Kama dada Monika wamemla nyama nini maana ya kidonda mguuni kwangu chenye kutoa wadudu?
                                                        ****
Tulipofika nje kaka alinibembeleza na kunieleza maneno ya busara kuhusiana na kifo cha Monika kuwa kilitokana na uzazi wala hakihusiani na masuala ya ushirikina. Na kutokuonesha kuguswa kila mmoja alikuwa akililia moyoni kwa vile hakuna aliyetegemea. 
Kwa vile nilikuwa namheshimu nilimkubalia ili kumridhisha lakini siri ilibakia moyoni mwangu. Wengi walishtuka maneno yangu na kunionya nisiyasikilize ya Monika kwa vile alikuwa ni muongo na mgombanishi, nao nilikubaliana nao ili yaishe.
Ajabu ya mwaka ambayo baada ya akili ya ufahamu kukomaa niligundua kuna kitu kilitendeka mpaka leo hii sijui. Baada ya taarifa za msiba wa dada Monika ambao  hakuna aliyefunua mdomo wake kulia zaidi  yangu mwenyewe.
Taarifa za msiba ule hata majirani hawakujua nyumbani kulitokea msiba. Mwili wa dada ulifuatwa na kurudishwa nyumbani. Gari lililouleta mwili wa dada ilipita mpaka uani. Waliuteremsha na kuuingiza chumbani kisha ndugu wote walitawanyika kwenda kuendelea na kazi zao kama kawaida. Kitu kile kilinishtua iweje kuwepo na msiba hakuna mtu aliyeguswa wala taarifa kuwafikia majirani.
Usiku nilipelekwa kwa kaka ambako nililala siku mbili na kurudishwa nyumbani, niliporudi hali ilikuwa ileile na kunifanya niwe na mawazo ni kweli dada alikufa au taarifa zile zilikuwa mgonjwa mahututi? Kwa hiyo yupo hospitali, sikutaka kuhoji haraka baada ya wiki sikuona mabadiliko wala taarifa zozote za dada Monika.
Hata majirani waliotuzunguka hawakujua kitu zaidi ya ndugu wa mpenzi wa dada Monika kuulizia dada alizikwa wapi. Maswali yale kwa kweli yalinichanganya sana. Kila nilivyojitahidi kuchunguza sikupata taarifa zozote zaidi ya watu kufurahia maisha.
Mwezi ulikatika nikiwa bado njia panda kuhusu maswali dada Monika wakiulizia mazishi yake yalifanyika lini na kwa nini baba hakuwataarifu kama kuna msiba, kama majirani wajumuike pamoja katika msiba ule. Siku moja nilikwenda hadi Mkuyuni kwenye nyumba aliyokuwa akikaa dada Monika.
Nilikuta mlango umefungwa, kuuliza nilishindwa kutokana na kuogopa maswali huenda amekufa na kunifahamu mimi ni nani. Niliamua kurudi bila kupata jibu kuhusiana na kupotea kwa dada Monika kwamba amekufa kweli au hali yake ni mbaya. Lakini nilikumbuka kaka mkubwa aliniambia kuwa Monika alikufa kutokana na uzazi.
Nilijiuliza kama alikufa alizikwa wapi na kwa nini majirani hawajui lolote, na kama kweli alikuwa amekufa mazishi yake yalifanyika wapi. Kutokana na kuja mjini muda mrefu mazishi yote tuliyafanyia mjini. Ingekuwa kama wengine mazishi huyafanyia vijiji walikozaliwa lakini dhana ile baba aliikataa.
Bado sikutaka kukubali, nilizunguka kwenye makaburi labda nitaliona kaburi jipya la dada Monika, lakini sikuona kitu chochote zaidi ya makaburi mapya yenye majina tofauti na la dada Monika.  Nilibakia njia panda siku zote kujiuliza ni kweli dada Monika alikufa au yupo kwa mganga.
Siku moja nilikutana na shemeji aliyekuwa akikaa na dada Monika, nilimuulizia kitu ambacho kilionekana kituko mbele yake.
“Shemu za siku?”
“Nzuri sijui zako?”
“Eti shemu dada Monika yupo wapi?”
“Masalu swali gani hilo? Ina maana mtu akifa huwa anakwenda wapi?”
“Una maana ni kweli dada Monika amekufa?”
“Masalu kioja gani unataka kunionesha, ina maana wakati Monika anakufa wewe ulikuwa wapi?”
“Sasa kama amekufa maiti yake imezikwa wapi?”
“Mimi nitajua wapi, wakati nilifukuzwa?”
“Kama kazikwa mbona hakuna kaburi lake?”
“Masalu upo sawa?”
“Kwani wewe unanionaje?”
“Nakuona haupo sawa.”
“Nipo sawa na akili timamu.”
“Kama kweli una akili timamu usingeniuliza suala la kifo cha Monika.”
“Shemu kama dada alikufa mbona wewe mumewe haukuwepo msibani?”
“Masalu, nilifukuzwa kama mbwa na kutishiwa maisha, kwanza nikionekana nimesimama na wewe nitajitafutia balaa.”
“Shemu una uhakika Monika amekufa?”
“Ndiyo.”
“Ulimshuhudia kabisa amekufa?”
“Monika amefia mikononi mwangu na kuna mengi alinieleza ya kukueleza lakini sikupata muda wa kuonana na wewe. Kama ni kweli aliyosema Monika basi familia yetu itakuwa ina hatari kubwa.”
“Kuhusu utajiri?” Nijikuta naropoka.
“Nalo hilo alilizungumzia, ila wamemtesa sana mke wangu mpaka kifo chake. Kibaya wamemuua hata mtoto wangu aliyekuwa tumboni bila kosa, yaani siamini familia yako kuna na roho mbaya kiasi hicho. Kama mtu kawapatia utajiri akisema amechoka na yeye anataka maisha yake kuna ubaya gani?” Maskini shemeji yangu alizungumza huku akitokwa na machozi, nilijikuta nikitokwa na mimi machozi bila kupenda.
“Masalu familia yenu haifai, unafikiri maisha ya kuongozwa na nguvu za kishirikina mwisho wake nini? Haya sasa wamemuua Monika nani atafuata na kwa taarifa kidonda alichokikataa dada yako kitahamia kwako. Kabla ya kufa kaitaja familia yenu wote kuwa wanagombania roho yake kasoro wewe pake yako na kuonesha jinsi gani huhusiki na mateso ya mke wangu.”
“Mungu wangu!”
“Huo ndio ukweli wenyewe, hujiulizi kwa nini mama yako bado analima kama sio ushirikina, hivi baba yako hana pesa ya kuwapa watu walime na mama yako na utu uzima wake apumzike?”
“Anaweza.”
“Kama anaongeza majumba na magari kwa nini mama yako usipumzike, hebu angalia ndugu zako wakubwa. Nao wana roho ya tamaa ya mali kushindwa kumuonea huruma mama yenu. Nasikia ndani mwenu kuna chumba kisichofunguliwa, unajua kuna nini?”
“Hata sijui!”
“Kwa taarifa yako kuna maiti ya mtoto mchanga ambayo kila baada ya siku tatu hupakwa mafuta ili isiharibike.”
“Shemuuuu! Umejuaje?” Nilishtuka kusikia habari zile, chumba alichokisema kweli kilikuwepo ambacho sikuwahi kukiona kikifunguliwa.
“Dada yako Monika alikuwa na siri nzito moyoni mwake, nyingine alisema hawezi kuniambia labda ungekuwepo kabla ya kufa kwake.”
“Sasa yeye alijuaje kama kuna maiti ya mtoto?”
“Mara nyingi kazi ile aliifanya yeye, baba na mama yenu. Hakuna mtu mwingine aliyeruhusiwa kuifanya.”
“Mmh! Maiti ya mtoto wa nani?”
“Kama una kumbukumbu, nasikia mtoto wa kwanza wa dada yako ambaye ndiye aliye na pesa kuliko wote alimtoa mtoto wake kafara ili kuongeza utajiri.”
                                                                    *****
Kauli ile ilinirudisha nyuma na kukumbuka miaka sita iliyopita dada mkubwa alifiwa na mwanaye lakini mazishi yake sikuyaelewa japo msiba ulikuwa nyumbani. Kingine kilichonifungua macho hakikuwa na tofauti na msiba wa Monika kilikuwa cha kifamilia tena ya ndani hata wanandugu hawakujulishwa. Taratibu nilianza kufunguka akili na kuamini kila lililosemwa na Monika lilikuwa na ukweli mkubwa.
“Asante shemu kwa kunifumbua macho,” nilimshukuru ili tuagane, nilipotaka kuondoka aliniuliza kitu.
“Masalu unataka kuniambia hukuwa na habari Monika amekufa au ulitaka kunitega akili?”
“Shemu, huwezi kuamini kila dakika nimekuwa nikichanganyikiwa juu ya taarifa za msiba wa dada Monika. Kweli niliuona mwili ukiteremshwa kwenye gari. Lakini tokea hapo sikuweza kujua nini kilichoendelea mpaka leo hii.”
“Ulipouliza walikujibu nini?”
“Sijauliza bali nilifanya upelelezi wangu, kila kona nilifika lakini sikupata kuona chochote.”
“Ulichunguza nini?”
“Sehemu za makaburi au kupata taarifa kama hajafa yupo wapi?”
“Una uhakika Monika hakuzikwa?”
“Nina uhakika.”
ITAENDELEASIKU YA KESHOOOOOOOOOOOO

BAADA YA MIEZI 9, THEO WALCOTT FITI, AREJEA MAZOEZINI FULL MZIKI

$
0
0


MSHAMBULIAJI NYOTA WA ARSENAL, THEO WALCOTT AMBAYE ALIKAA NJE KWA MIEZI 9 AKIWA MAJERUHI. AMEANZA MAZOEZI KAMILI AKIWA NA KIKOSI HICHO CHINI YA ARSENAL WENGER.







UTEKAJI WA WATOTO DAR, HALI SASA NI TETE!

$
0
0

Stori: Makongoro Oging’LICHA ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kupitia kwa kamanda wake, Camillius Wambura kutumia nguvu kubwa kukanusha kwamba, hakuna matukio ya utekaji wa watoto wadogo, hasa wanafunzi, lakini matukio hayo YAPO!!
 
Mama aliyempoteza mwanaye akilia kwa uchungu.
UWAZI LINA CHA KUSHIKA
Ili kuliwekea ushahidi suala hilo, Uwazi lina cha kushika mkononi kufuatia wiki iliyopita, wanafunzi wawili wa shule za  msingi wilayani Kinondoni ambako Kamanda Wambura anasimamia jeshi lake walipotea na baadaye kuokotwa wakiwa wameuawa.
MATUKIO YENYEWE
Wanafunzi hao ambao miili yao iliokotwa, mmoja akiwa amenyofolewa sehemu za siri ni Glory William (7), mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Msingwa na Joshua Nicolas (12) wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Temboni, zote ni wilayani Kinondoni kwa Kamanda Wambura.
 
Mama mwingine aliyefiwa akilia kwa uchungu.
MAMA WA GLORY ASIMULIA KWA MACHOZI
Akizungumza na mwandishi wa habari hii siku ya tukio, mama mzazi wa Glory, Faminian Gabriel alisema:
“Jamani wanaposema hakuna utekaji wa watoto huku sisi wazazi tunalia, si sawa! Nakumbuka siku ya jana (Ijumaa) saa kumi jioni mwanangu Glory alirudi toka shule, nilimkumbatia kwa upendo kisha nikamuacha nyumba ya jirani na mfanyakazi wa ndani.
“Mimi niliondoka kwenda kwenye kazi fulani. Niliporudi sikumkuta Glory nyumbani, nilipoulizia nikaambiwa alikuwa na kijana mmoja,” alisema mama huyo.
 
Waombolezaji wakiubeba mwili wa mmmoja wa watoto waliuwawa.
AFIKA KWA MJUMBE
Haikuwa kawaida ya Glory kuwa mbali na nyumbani jambo ambalo lilinitia hofu. Ilibidi nikatoe taarifa kwa mjumbe ambaye tulisaidiana naye kumtafuta lakini bila mafanikio.”
SERIKALI ZA MTAA WAAMBIWA, WASHANGAA
Baadaye pia nilikwenda kutoa taarifa kwenye ofisi za serikali za mtaa lakini mtoto hakuonekana na wao wakashangaa mazingira ya upoteaji wake.
 
Baadhi ya waombolezaji wakiendelea na mazishi.
GIZA HADI KUNAKUCHA MTOTO HAJARUDI
Mama Glory aliendelea kusema kuwa alikaa macho hadi asubuhi bila kumuona binti yake. Wakati anajiandaa kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi sasa, akapata taarifa kwamba kuna mwili wa mtoto umeokotwa mahali.
“Baada ya kupewa taarifa hizo, majirani walifuatana na mimi na ndugu zangu hadi eneo la tukio na walipoukagua mwili ukabainika ni mwanangu,” alisema mama huyo huku akilia.
MWILI ULIVYOKUTWA, INAUMA!
Inaelezwa kwamba, baadhi ya wananchi walipoukagua vizuri mwili huo walitokwa machozi kufuatia kubaini kuwa, hakuwa na sehemu za siri, pia kichwa chake kilionekana kupondwa na tofali, pengine ndilo lililosababisha kifo chake.
 
Baadhi wanafunzi wakiweka shada la mauwa kwenye kaburi la mtoto aliyeuawa.
KUANDAMANA HADI IKULU YA JK
Baadhi ya wazazi waliozungumza na Uwazi kwenye msiba wa mtoto Glory walisikika wakisema wanajipanga kufanya maandamano ya amani hadi Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete kumlalamikia kuhusu kukithiri kwa matukio ya utekaji watoto huku jeshi la polisi likisema hakuna kitu kama hicho.

ALIVYOSEMA MJUMBE
Akithibitisha habari hiyo, Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Saranga kulikotokea tukio, Samora Costino alisema mauaji ya mtoto huyo yana ushirikina ndani  yake na kwamba huyo ni mtoto wa pili kutekwa na kuuawa kikatili.
TANGU MACHI TATIZO LIPO
Mjumbe huyo alisema mtoto Joshua yeye alitekwa Machi 18, mwaka huu akiwa anatoka shule, akauawa na maiti yake ikatupwa mtoni.
 
Hili ni kaburi la mmoja wa watoto waliouawa
BABA MZAZI WA JOSHUA AKUMBUKA MACHUNGU
Uwazi lilifanikiwa kuzungumza na baba mzazi wa Joshua, mzee Nicolas ambaye alikiri mwanaye huyo kutekwa akitoka shule na kuuawa. Alisema:
“Siku hiyo ya tukio mwanangu hakurudi nyumbani kutoka shuleni. Tulimtafuta bila mafanikio hadi kesho yake alipookotwa kwenye mto huko Tabata Mawenzi akiwa ana alama shingoni kuonesha kwamba alipigwa na kunyongwa.
“Hata hivyo, muuaji alijulikana lakini cha kushangaza hajakamatwa hadi leo. Pia nawashangaa polisi kwani hata taarifa ya uchunguzi wa kifo sijapewa jambo lililonifanya niamue kwenda Ofisi ya IGP (Ernest Mangu) ambapo kwa sasa mambo yanaendelea vizuri,” alisema mzee huyo.
 
Marehemu Glory William (7)(kulia)  akiwa na wenzake enzi za uhai wake.
KUMBUKUMBU
Siku za hivi karibuni jijini Dar es Salaam, watoto, hususan wa shule za msingi wamekuwa wakidaiwa kutekwa na watu wanaosemekana hutumia magari aina ya Toyota Noah rangi nyeusi hali inayowafanya wazazi kuwa na hofu.
Baadhi ya shule tayari zimeweka sheria kwamba, wazazi wasiwaache watoto wao kwenda shuleni wenyewe au kupelekwa na watu wasiowaamini.Katika gazeti hili toleo la wiki iliyopita, ukurasa wake wa mbele kulikuwa na habari kubwa yenye kichwa; UTEKAJI WATOTO WATIKISA DAR!
 
Marehemu Joshua Nicolaus Rubanzibwa enzi za uhai wake.
Katika habari hiyo, tukio moja la ajabu lilitokea Vingunguti, Ilala ambapo gari aina ya Noah lilivamia shuleni na kumteka mwanafunzi mmoja na kutaka kuondoka naye.Hata hivyo, mzazi mmoja alishuhudia kitendo hicho na kupiga kelele hadi watu hao wakamwachia mtoto huyo.
Kesho yake, Noah lingine jeusi lilifika kwenye shule ya jirani na ya mtoto wa jana yake kwa lengo la kuzungumza na walimu kuhusu mikopo.Ikadaiwa kuwa, wazazi walipoliona Noah hilo jeusi walilipopoa mawe wakiamini ni lile la jana yake lilirudi tena. Ilibidi Polisi wa Kituo cha Buguruni waitwe kurejesha hali ya amani shuleni hapo.
(CREDIT: GPL)

DENTI AJICHOMA KISU KWA MADAI YA USALITI WA MAPENZI

$
0
0

 Moza Kasim Mohemed akiwa hoi baada ya kujichoma kisu cha tumbo.

Stori: Musa MatejaLOO! Mwanafunzi wa Chuo cha T.I.A tawi la mkoani Singida, Moza Kasim Mohemed (20) ambaye ni mkazi wa jijini Dar es Salaam, amejichoma kisu tumboni kwa madai ya kuchoshwa na usaliti wa mpenzi wake aitwaye Joel ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo hicho.

Tukio hilo la kushangaza lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 10, mwaka huu maeneo ya Jovena katika Hosteli za Miami ambapo Moza alikuwa akiishi na mpenzi wake huyo.
Chanzo chetu kilidai kuwa, siku hiyo muda mfupi kabla ya tukio hilo kulitokea kutoelewana kwa wawili hao ambapo majirani walimsikia Joel akimtuhumu Moza kwamba amekuwa msaliti na anahisi ana simu nyingine ya ziada ambayo anaitumia yeye akiwa hayupo.
 
Muonekano wa kisu hicho baada ya kujichoma.
Timbwili lilisikika kwa muda mrefu kiasi kwamba ilibidi majirani waanze kuchungulia dirishani na wakamsikia Moza akimwambia Joel kwamba, kwa vile hamwamini hadi anafikia kumpiga bora ajichome kisu afie mbali.Kwa mujibu wa chanzo chetu, Joel naye alisikika akimjibu Moza kwa kumwambia kama dhamira yake ni hiyo, basi ajichome tu. 
Akiwa hospitalini baada ya kutolewa kisu tumboni.
Malumbano hayo yaliendelea kuchukua ukurasa mpya ambapo Joel aliendelea kumpa kibano na baadaye alimuacha na kutoka nje, baada ya dakika chache zikasikika kelele za ajabu kutoka kwa Moza ambapo majirani ambao ni baadhi ya wanafunzi wenzake wakatoka na kuingia chumbani na kumkuta akigalagala na damu zikimvuja huku kisu kikiwa tumboni.
“Hawa watu walikuwa na tabia ya kukwaruzana mara kwa mara na Joel alikuwa akimpiga yanaisha ila siku hiyo ilikuwa ni mzozo wa hatari, baada ya tukio watu walijaa lakini kila mtu akawa anaogopa kumgusa Moza, Joel alipata ujasiri yeye na rafiki yake wakambeba na kumkimbiza Hospitali ya Mkoa wa Singida,” kilisema chanzo.
 
Hostel aliyokuwa anaishiiMoza Kasim Mohemed .
Kikaendelea: “Jana (juzi Jumapili) tulikwenda hospitali kumsalimia, tulikuta ameshatolewa kisu na ameshashonwa, hali yake inaendelea vizuri, ila habari ya mjini Singida kwa sasa ni juu ya tukio hilo, hata tulipofika hospitali tulikuta wanafunzi wengi.”

USAHILI WA SERENGETI SUPER NYOTA DIVA WAFANA NDANI YA SUNCIRRO CLUB

$
0
0
 
MCHUJO wa kumpata mshindi wa Serengeti Fiesta Super Nyota Diva kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, umefanyika leo mchana ndani ya Ukumbi wa Suncirro Shekilango, ambapo tayari vijana mbalimbali wamejitokeza kuchuana na hatua ya kwanza tayari imemalizika kwa kupata washindi 5, ambao watachuana ili kuhakikisha anapatikana mshindi mmoja atakayeingia kwenye fainali za shindano hilo ambalo linatarajiwa kufanyika Ijumaa hii ndani ya Ukumbi wa Suncirro kwa kushirikisha wasanii wote waliopatikana kwenye jumla ya mikoa 14, ambayo imepitiwa na Tamasha la Serengeti Fiesta 2014.
 
Mmoja wa washiriki wa Serengeti Super Nyota Diva, akiwania nafasi ya kuwa Diva wa Jiji la Dar mapema leo ndani ya Ukumbi wa Suncirro.
 
Jaji wa mashindano hayo, Elias Barnabas akitafakari jambo wakati mchujo huo ukiendelea.
 
Mmoja wa washiriki akionyesha uwezo wake katika kuimba.
 
Majaji wa shindano hilo kutoka kulia ni mtayarishaji wa nyimbo, Tudi Thomas, DJ Fetty na Elias Barnabas wakiwajibika kuhakikisha wanampata mshindi bora wa shindano hilo.
 
Baadhi ya washiriki wakimshangilia mwenzao wakati akitafuta nafasi ya ushindi jukwaani hapo.
 
Mmoja wa washiriki hao akikamua kuwania nafasi hiyo.
 
Washiriki walioingia kwenye tano bora ya Shindano la Serengeti Super Nyota Diva 2014 jijini Dar es Salaam, wakiwa jukwaani.
 
Mshiriki akiwania nafasi ya kuwa Super Nyota Diva wa mkoa wa Dar es Salaam.
 
Majaji wa mchujo huo, Barnaba na DJ Fetty wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kutaja washiriki walioingia kwenye tano bora.
 
Mrembo akiwajibika jukwaani kuwania nafasi ya kuwa Diva wa Dar.
 
Baadhi ya washiriki wakifuatilia shindano hilo.
 
Mshiriki akiwa stejini mbele huku baadhi ya washiriki wenzake wakimshuhudia wakati akiimba.
HABARI/PICHA: MUSA MATEJA/GPL.

KIINGILIO MECHI YA YANGA, SIMBA 7,000/- , VIP 20,000 - 30,000

$
0
0
 
Geilson Santana ‘Jaja’ akishangilia goli na wachezaji wenzake.
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 7,000.


Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika uwanja huo wenye viti 57,558. Viingilio vingine ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.
Tiketi zitakazotumika kwenye mechi hiyo ni za elektroniki, na zimeanza kuuzwa jana (Oktoba 13 mwaka huu). Tiketi zinapatikana kwa mtandao wa M-PESA, CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo zaidi ya mia moja sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

AUNT: NILIONANA NA NYALANDU UKUMBINI

$
0
0

STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel, amesema hakuna ukweli wowote wa yeye kutanua na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu nchini Marekani, kwani alikutana naye ukumbini, akiwa amealikwa na blog iitwayo Vijimambo ambayo hutangaza utalii wa Tanzania nchini humo kila mwaka.

Alisema wakati wa safari yake hakuelewa lolote kuhusu Waziri Nyalandu na anashangazwa na yanayozungumzwa hivi sasa kwani baada ya kumsalimia walipokutana, hawakuwahi kuonana tena hadi aliporejea, kwani yeye alikuwa amepangiwa kwenye hoteli ambayo pia ndiyo ukumbi wa shughuli hiyo ulipokuwa.
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza jambo.
“Watu wanataka kunijengea uadui na mke wake Faraja Kota ambaye tunaheshimiana sana, mimi nilialikwa kule nikiwa na wasanii wengine, wanamuziki Kassim Mganga na IT na hata malipo ya kazi yangu nililipwa na wao, wanaosema nilitumia hela za wizara sijui wanataka nini, kama wizara iliwapa fedha hao waliotualika mimi sijui,” alisema muigizaji huyo.

USHINDI MTOTO WA MBUNGE, MISS TANZANIA YATIKISIKA

$
0
0

Stori:  Erick Evarist na Musa MatejaOHOOOOH! Siku chache baada ya mtoto wa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, Sitti kujinyakulia U-Miss Tanzania 2014, tayari joto la ushindi huo limetikisa taji hilo na kuibua maswali ‘chungu mbovu’ kuhoji uhalali wa ushindi huo, Risasi Mchanganyiko linashuka na mchongo kamili.
 
Miss Tanzania Sitti Mtemvuakiwa mwenye nyuso ya furaha baada ya kushinda taji hilo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, vuguvugu za uhalali wa ushindi ziliibuka muda mchache kabla ya shindano hilo kuchukua nafasi katika Ukumbi wa Mlimani City, Ijumaa iliyopita ambapo wadau mbalimbali walianza kuhoji kulikoni wafuasi wa mrembo huyo waingie na vipeperushi vingi vyenye picha ya mshindi (Sitti).
“Tatizo lilianzia kwa watu wengi kuingia na vibendera vyenye picha ya Sitti vikionyesha dhahiri kwamba walijua kabla kwamba ni mshindi hivyo kuja wakiwa wamejipanga kabisa,” kilisema chanzo.
Chanzo hicho kilienda mbali zaidi kwa kusema hata katika suala zima la mshindi kuandaliwa gari maalum la Hammer ambalo baadaye lilimchukua na kumrudisha kivyake tofauti na washiriki wengine ambao waliondoka ukumbini hapo na basi waliloandaliwa.
 
Miss Tanzania aliyemaliza muda wake,Happiness Watimanywa akimvika Crown na TajiMiss Tanzania Sitti Mtemvu.
“Waandaaji wanapaswa kutueleza vizuri, haiwezekani watu waandae Hammer waje nalo ukumbini pasipo kuwa na uhakika wa ushindi, ule ni utani,” kilinyetisha chanzo hicho.
Aidha, vuguvugu hilo lilijiongeza zaidi baada ya watu kudai huenda ushindi huo ulitokana na mgongo wa baba yake (mbunge wa Temeke) madai ambayo kwa pamoja yalikanushwa na muandaji wa mashindano hayo, Hashimu Lundenga.
“Hakuna kitu kama hicho, malalamiko kila siku hayakosekani, vipeperushi havikatazwi, majaji sita kati ya tisa waliwekwa na wadhamini (TBL kupitia kinywaji chao cha Red’s), haiwezekani akawahonga majaji wote hao.
 
“Kuhusu gari, hakuondoka ukumbini na Hammer, aliondoka na basi kama washiriki wengine, sijui hayo maneno yanatoka wapi,” alisema Lundenga.
Kwenye shindano hilo, Sitti aliwagaragaza washiriki wenzake 29 na kuondoka na kitita cha shilingi milioni 18. Mrembo huyo ndiye atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia (Miss World) hapo baadaye.

HOTUBA YA JAKAYA KIKWETE KWENYE SHEREHE YA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA NA WIKI YA VIJANA KITAIFA, TAREHE 14/10/2014 – MKOANI TABORA

$
0
0
Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (MB), Waziri wa Habari,
       Vijana, Michezo, Utamaduni na Michezo;
Mheshimiwa Zainabu Omar Mohamedi, Waziri wa Uwezeshaji,
      Ustawi wa Jamii, Vijana Wanawake na Watoto – Zanzibar;
Mheshimiwa Fatuma A. Mwasa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora;
Mheshimiwa Samwel Sitta, Waziri wa Afrika Mashariki, Spika Mstaafu na Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba;
Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri;
Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wa
         Baraza la Wawakilishi;
Ndugu  Mwenyekiti  wa CCM Mkoa wa Tabora;
Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa kutoka Tanzania
        Bara na Zanzibar;
Makatibu Wakuu kutoka Wizara Mbalimbli Tanzania
      Bara na Zanzibar;
Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa;
Waheshimiwa viongozi wa vyama mbalimbali vya Siasa;
Viongozi wetu wa Kiroho kutoka katika Madhebu mbalimbali;
Vijana Wetu;
Ndugu Wananchi;
Mabibi na Mabwana;
Nawashukuru Mawaziri wetu Mheshimiwa Fenella Mukangara wa Serikali ya Muungano na Mheshimiwa Zainabu Omari Mohamed wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kunialika kuja kushiriki katika sherehe za mwaka huu za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.  Napenda pia kutumia nafasi hii kumpongeza na kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tabora na viongozi wenzake na wananchi wote wa Tabora kwa kukubali kuwa mwenyeji wa sherehe hizi na kwa maandalizi mazuri.  Hakika sherehe zimefana sana.  Tunawashukuru kwa mapokezi mazuri na kwa ukarimu wenu.
Pongezi kwa Wizara na Wananchi
Aidha, nawapongeza Makatibu Wakuu, viongozi waandamizi na maafisa wa ngazi mbalimbali wa Wizara zetu mbili husika kwa kazi kubwa na nzuri ya kuandaa na kusimamia utekelezaji wa programu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2014.  Matunda yake mema sote tunayashuhudia na kujivunia.  Pamoja na hao napenda kuwatambua, kuwashukuru na kuwapongeza Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Watendaji wa Halmashauri na viongozi wa Shehiya, Majimbo, Kata, Vijiji na Mitaa kote nchini kwa kuziwezesha Mbio za Mwenge mwaka huu kupita kwa usalama katika maeneo yao.
Mwisho, lakini siyo mwisho kwa umuhimu, nawapongeza na kuwashukuru wananchi wote kwa jinsi walivyoupokea na kuukimbiza Mwenge katika maeneo yao.  Kama tulivyosikia Mwenge umekagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwa miradi 1,451 yenye thamani ya shilingi bilioni 361.3.  Hii ni miradi mingi yenye manufaa makubwa na kufanya mbio hizi kuwa chachu kubwa ya maendeleo hapa nchini.  Hongereni sana.
Pongezi kwa Wakimbiza Mwenge
Nawapongeza sana vijana wetu waliokimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa chini ya uongozi wa Ndugu Rachel Kasanda kwa kazi kubwa na nzuri ya kukimbiza Mwenge kwa siku 165kupitia Mikoa yote, Wilaya zote, vijiji vingi na mitaa mingi kote nchini.  Poleni kwa yote yaliyowakuta lakini uvumilivu wenu na moyo wenu wa upendo na uzalendo kwa nchi yenu ndivyo vilivyotuwezesha kufikia kuiona siku ya leo.  Mwenge mmeufikisha salama Tabora ukiwa unang’ara kama ilivyo kawaida yake.  Nawashukuru kwa Risala yenu na kwa kunikabidhi Kitabu kikubwa chenye Risala za Utii za wananchi wa Tanzania.  Kama ilivyo ada tutazisoma zote na mambo yanayostahili kufanyiwa kazi tutachukua hatua stahiki. 
Ndugu Wananchi;
 Kama mjuavyo, katika sherehe hizi pia tunakumbuka tarehe na siku kama ya leo mwaka 1999 ambapo mpendwa wetu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitutoka hapa duniani.  Ilikuwa siku ya majonzi na simanzi kubwa.  Leo, hata hivyo, siyo siku ya kuomboleza, bali ni siku ya kusherehekea maisha ya kiongozi wetu mpendwa asiyekuwa na mfano wake na muasisi wa taifa letu lililo huru la Tanganyika, Desemba, 1961 na wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 26, 1964 kwa kushirikiana na Mzee Abeid Amani Karume. 
Katika kipindi cha uongozi wake na uhai wake Mwalimu aliifanyia nchi yetu mema mengi ambayo daima hayatasahaulika.  Hivyo basi, siku kama ya leo ni ya kukumbuka kazi zake nzuri pamoja na mambo mengi mazuri aliyotuachia kama urithi.  Ni siku ya kutafakari na kuona namna gani tutayadumisha  na kuyaendeleza.
Sherehe za mwaka huu ni spesheli kweli kweli, kwani zinafanyika siku chache tu baada ya Bunge Maalum la Katiba kukamilisha kazi yake na kukabidhi Katiba Inayopendekezwa.  Katiba hiyo ambayo imepatikana chini ya uongozi wa mwana Tabora, mashuhuri, Mheshimiwa Samwel Sitta imesisitiza ubora na kuendelea kwa Muungano wa Serikali Mbili alizoasisi Mwalimu Julius Nyerere akiwa na Mzee Abeid Amani Karume.  Bila ya shaka mtakumbuka jinsi Mwalimu alivyoupigania muundo huo kwa nguvu zake zote wakati wa uhai wake.  Hatuna budi kulipongeza Bunge Maalum la Katiba kwa uamuzi wake wa busara ambao unamuenzi kwa dhati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kudumisha urithi wake mkuu kwetu ambayo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Sijui tungesema nini katika Sherehe za mwaka huu kama ndiyo tungekuwa na Katiba Inayopendekezwa yenye muundo wa Serikali Tatu?
Mwenge na Taifa Letu
Ndugu Wananchi;
          Mwenge wa Uhuru ni moja ya alama muhimu ya umoja wa nchi yetu na utaifa wetu.  Mwenge umebeba falsafa kubwa ndani yake kuhusu nchi yetu na uhusiano wake na watu wengine duniani hasa wanyonge wenye dhiki wasiokuwa na amani.  Wakati wa harakati za kudai Uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Wakoloni wa Kiingereza Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema “Sisi tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima  Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na heshima palipojaa dharau”.  Dhamira hii ilitimizwa tarehe 9 Desemba, 1961 siku Tanganyika ilipopata Uhuru.  Pamoja na kupandisha  bendera ya taifa huru la Tanganyika kwenye Kilele cha Mlima Kilimanjaro na Mwenge wa Uhuru uliwashwa.
          Miaka michache baadaye utaratibu wa kukimbiza Mwenge ulianza na kuendelea mpaka sasa.   Mwenge wa Uhuru umeendelea kumulika nchi nzima ukipita katika mitaa, vijiji, shehia na majimbo, wilaya na mikoa ukieneza ujumbe wa udugu, umoja, upendo, amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania.  Aidha, Mwenge umeendelea kuwakumbusha Watanzania wajibu wa kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kujiletea maendeleo yao na ya nchi yetu.  Pia wapige vita maovu nchini. 
Kwa kuzingatia dhima nyingine ya Mwenge wa Uhuru, nchi yetu na sisi Watanzania tumejitolea kwa hali na mali kusaidia ndugu zetu Barani Afrika waliokuwa wanatawaliwa kujikomboa kutoka kwenye makucha ya wakoloni na wabaguzi wa rangi.  Ni fahari kwetu kwamba wananchi wa Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia na Afrika Kusini wamepata ukombozi na uhuru wao na sisi tumetoa mchango muhimu.  Ni jambo la faraja kubwa kwamba nchi yetu imeweza kuwapatia hifadhi ndugu zetu wa nchi jirani na hata mbali wakati maisha yao yalipokuwa hatarini kwa sababu ya kukosekana kwa amani au kwa kukimbia mateso ya uongozi wa kikatili na kidikteta.  Ndugu zetu wa Kongo, Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Comoro wanajua ukweli huo.  Na, kwa Uganda tuliwasaidia kuling’oa dikteta Idd Amin na Comoro tumewasaidia kuunganisha tena nchi yao.  Hivi karibuni ndugu zetu wa Sudani Kusini waliniomba tuwasaidie kupatanisha makundi makuu yanayohasimiana katika Chama chao kikuu cha SPLM.  Nimekubali, hivyo tutaanzisha mchakato huo tuone tutafika nao wapi.
Ujumbe wa Mbio za Mwenge
Ndugu Wananchi;
Nimefurahishwa sana na kuafiki ujumbe wa mwaka huu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru unaosomeka “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi:  Jitokeze kupiga kura ya Maoni Tupate katiba Mpya”.  Ujumbe huu ni mwafaka kabisa kwa kipindi hiki cha mchakato wa kupata Katiba Mpya nchini. Pamoja na ujumbe huu mahususi wa kila mwaka, Mwenge wa Uhuru umeendelea kuelimisha jamii na kutoa msukumo kuhusu vita dhidi ya UKIMWI, malaria, dawa za kulevya na rushwa.  Nawapongeza sana Wakimbiza Mwenge kitaifa kwa kuwasilisha ujumbe wa mambo yote manne vizuri. 
Ndugu Wananchi:
Kama mnavyofahamu nchi yetu iko katika mchakato wa kuandaa Katiba Mpya. Mchakato huu sasa umeingia hatua ya juu kabisa baada ya kumalizika kwa Bunge Maalum la Katiba kwa kutunga Katiba Inayopendekezwa.  Baada ya Katiba Inayopendekezwa kukabidhiwa kwangu na kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba tarehe 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma, kazi inayofuata ni Kura ya Maoni ya wananchi kuamua ili nchi yetu ipate Katiba Mpya.  Hatua husika kuhusu matayarisho ya kutekeleza masharti ya Kura ya Maoni zimeshaanza kuchukuliwa.  Nawaomba Watanzania wenzangu muwe na subira.  Mtaelezwa na kuelekezwa ipasavyo. 
Ndugu Wananchi;
Nimebahatika kuisoma Katiba Inayopendekezwa na naendelea kuisoma.  Kwa kweli ni Katiba bora, kuliko hii tuliyonayo sasa yaani Katiba ya mwaka 1977.  Ni Katiba inayotambua na kuimarisha tunu za taifa letu na mambo mazuri ya huko tulikotoka na hapa tulipo.  Ni Katiba inayorekebisha upungufu uliopo sasa na kuweka mifumo mizuri inayoendana na wakati tulionao sasa na huko mbele tuendako.  Kwa lugha nyepesi ni Katiba inayotoa majawabu sahihi kwa changamoto zetu za leo na kesho.
Katiba Inayopendekezwa inatokana na ushirikishwaji mpana wa wananchi wa Tanzania walioko ndani na hata wale walio nje ya nchi.  Ndiyo maana haki na maslahi ya makundi yote zimetambuliwa na kupewa nafasi yake stahiki.  Kama mjuavyo, leo pia ni kilele cha Wiki ya Vijana.  Napenda mjue kuwa Katiba Inayopendekezwa imetambua haki za vijana na kuelekeza kuundwa kwa Baraza la Vijana la Taifa.  Kuundwa kwa Baraza hilo kutawaongezea vijana sauti katika kushiriki kwenye utungaji wa sera na uamuzi unaohusu maendeleo ya vijana na nchi yenu (ambayo ndiyo yetu sote).  Kitakuwa chombo huru cha kuunganisha vijana wote nchini bila kubagua kwa jinsia, rangi, kabila, dini, ufuasi wa vyama vya siasa na maeneo watokako katika kutafuta majawabu ya changamoto zinazowakabili ikiwemo tatizo kubwa la ajira.
 Hii ni fursa ambayo vijana wamekuwa wakiililia tangu kutungwa kwa Sera ya Vijana ya mwaka 1996.   Hatimaye kilio hiki kimepatiwa kitambaa cha kufutia machozi na Katiba Inayopendekezwa.  Shime vijana mjitokeze kwa wingi wakati utakapofika, mpige kura ya kuunga mkono Katiba Inayopendekezwa ili mjitengenezee hatma njema ninyi na vizazi vyenu. Mnayo nafasi sasa ya kihistoria ya kushika hatamu ya maendeleo yenu.  Katiba Inayopendekezwa ni fursa hiyo, hakikisheni haiwaponyoki.
Ndugu Watanzania Wenzangu;
Naomba muisome kwa makini Katiba Inayopendekezwa ili  muielewe na kuona jinsi masuala muhimu kuhusu vijana na wananchi wengine yalivyozingatiwa.  Epukeni kuondolewa kwenye mambo yenye maslahi ya moja kwa moja na ustawi wenu na kubeba agenda hasi za watu wengine.  Kamwe msikubali kutumika na kutumiwa na wanasiasa au wanaharakati kwa mambo ambayo hayana tija kwenu na nchi yetu.  Nawaomba vijana mtambue kuwa kwa sababu ya umri wenu, ninyi ndiyo mtakaoishi na kufaidi matunda ya Katiba Inayopendekezwa kwa miaka mingi ijayo.  Kwa sababu hiyo, itumieni fursa hii vizuri, kutengeneza mustakabali mwema kwenu na kwa vizazi vyenu.  Hatima ya nchi yetu iko mikononi mwenu.   
Ndugu Wananchi;
Bila ya shaka mnajua kuwa mwezi Desemba, 2014 kwa upande wa Tanzania Bara kutafanyika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.  Napenda kutumia fursa hii kuwashauri vijana na wananchi wote wenye sifa stahiki na kujitokeza kugombea uongozi.  Pia nawaomba mjitokeze kwa wingi na kushiriki kwa ukamilifu katika kupiga Kura siku ya uchaguzi.  Kufanya hivyo ndiko kutakakotupatia viongozi wazuri wanaoweza kutuvusha na kutupeleka huko mbele kuzuri tunakokutaka.  Tushirikiane ili tupate viongozi wanaoendana na mahitaji ya sasa na ya miaka ijayo mbele.  Ngazi za kitongoji, mitaa na kijiji ndizo ngazi za msingi za kuanzia za kuleta maendeleo na mabadiliko katika nchi yetu.
 Shughuli za maendeleo na utoaji wa huduma za jamii hasa zinafanyika katika vijiji, vitongoji na mitaa tunayoishi.  Hivyo, mabadiliko mnayoyataka hamna budi yaanzie katika mitaa au kitongoji unachoishi. Hii ndiyo ngazi inayotugusa moja kwa moja kila mmoja wetu katika maisha yetu ya kila siku. Hivyo basi, vijana mjitokeze kugombea uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.  Vile vile, mwakani kwenye Udiwani, Ubunge na Uwakilishi, msibaki nyuma.  Ni haki yenu na ni wakati wenu.  Gombeeni hata kwa nafasi ya Urais, na iwapo kuna mtu anayefanana na ujana na atakuwa ametimiza masharti ya Katiba, asiogope, ajitokeze.  Watu wataamua.  Shime jitokezeni mkawe chachu ya mabadiliko katika maeneo mnayoishi na nchi nzima. 
Wiki ya Vijana
Ndugu Wananchi;
          Kama sehemu ya sherehe hizi, jana nilitembelea Kijiji cha Mfano cha Vijana katika wilaya ya Sikonge.  Nimefurahishwa sana na juhudi zifanywazo na vijana za kujiletea maendeleo.  Nimevutiwa na miradi mbalimbali wanayoitekeleza pale ikiwemo ya kufuga nyuki na kuvuna mazao yatokanayo na nyuki, ufugaji wa kuku na ng’ombe wa maziwa, ushonaji nguo na viatu.  Halikadhalika, shughuli za kilimo na ujenzi wa nyumba bora.  Nimewashauri viongozi wa Wilaya, Mkoa na Wizara waangalie uwezekano wa kuwafanya vijana hao kuwa wakaazi na wamiliki wa eneo hilo la miradi ili kiwe kweli kijiji cha mfano badala ya kuwa mahali pa kupita mithili ya chuo cha mafunzo ya amali.
Baadae nitapata nafasi ya kutembelea mabanda ya maonesho ya kazi wafanyazo vijana na wadau wengine hapa uwanjani.  Maonyesho haya yanathibitisha kwa uwazi fursa zilizopo za kuwaendeleza vijana.  Lililo muhimu kufanya, ni kwa vijana kuwa na upeo mzuri wa ufahamu wa mambo, ubunifu, moyo wa kujituma na kufanya kazi kwa bidii.  Mkifanya hivyo tutaondokana na tatizo la ukosefu wa ajira na umaskini kwa vijana na taifa kwa ujumla.
Ndugu Wananchi;
Kwa kutambua ukweli huu, ndiyo maana Serikali zetu zimeongeza bajeti katika Mifuko ya Maendeleo ya Vijana kupitia Wizara zetu mbili zinazosimamia na kuratibu maendeleo ya vijana.  Shabaha yetu ni kuwawezesha vijana wengi zaidi kupata mikopo na kuwa na mitaji ya kutekeleza miradi yao itakayowawezesha kujiajiri wenyewe na kujipatia kipato. Naikumbusha Wizara inayosimamia na kuratibu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kuhakikisha kwamba fedha za Mfuko huo zinawafikia walengwa na, kwa wakati muafaka.
Kwa upande mwingine nazikumbusha Halmashauri zote za Wilaya na Miji kutekeleza kwa ukamilifu agizo la kutenga asilimia 10 ya mapato yao kwa mwaka kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya Vijana na Wanawake.  Ninazo taarifa kuwa baadhi ya Halmashauri zinalitekeleza vizuri agizo hili lakini zipo nyingine ambazo zinasuasua.  Nataka isiwepo hata Halmashauri moja ya kunyooshewa kidole kwa kutokufanya vizuri kwa jambo lenye manufaa kwa vijana wetu kama hili.  Naomba nitumie nafasi hii leo kuzitaka Halmashauri zote kutoa taarifa za mara kwa mara za utekelezaji wa agizo hili.  Taarifa ya kwanza kwa ajili hiyo itolewe mwisho wa mwezi Desemba, 2014, ifuatayo iwe miezi minne baadae na kila baada ya miezi minne. 
Mapambano Dhidi ya UKIMWI
Ndugu Wananchi;
          Janga la UKIMWI bado ni tatizo kubwa nchini hivyo ni sahihi kabisa kwa Mwenge kuendelea kulisemea.   Inakadiriwa kuwa tunao wagonjwa wa UKIMWI milioni 1.4.   Bahati mbaya waathirika wengi zaidi ni vijana.  Takwimu za maambukizi zinaonyesha pia kuwa wasichana wa umri wa miaka 20 – 24 wako katika hatari ya kuambukizwa karibu mara tatu ikilinganishwa na wavulana wa umri huo huo. 
Ni jambo la kutia moyo kwamba kiwango cha maambukizi kinashuka mwaka hadi mwaka kutokana na shughuli za uhamasishaji ambazo na Mwenge nao una mchango wake.  Kwa mfano, kiwango cha maambukizi kimeshuka kutoka asilimia 5.7 mwaka 2010 hadi asilimia 5.1 mwaka 2012.  Kiwango cha maambukizi ya UKIMWI hapa mkoani Tabora ni wastani wa asilimia 5.1 ambayo ni sawa na kiwango cha kitaifa.  Mwelekeo huu kwa taifa na Tabora ni mzuri lakini tusibweteke bali tuongeze bidii katika mapambano.  Watu watano katika kila 100kuwa wameambukizwa ni wengi mno.  Isitoshe maambukizi mapya 78,843 ni makubwa mno, tunataka maambukizi mapya yawe sifuri.
          Tumeendelea kupata mafanikio ya kutia moyo katika vita dhidi ya UKIMWI.  Idadi ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI wanaopata tiba imeongezeka kutoka 201,181 (2005) hadi 512,555mwaka 2013.   Hali kadhalika tumewezesha huduma za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kutolewa karibu katika Kliniki zote nchini (aslimia 97).  Vilevile, idadi ya waliopima afya zao imeongezeka kutoka watu 365,189mwaka 2005 hadi 20,469,241 mwaka 2013.  Katika mwaka 2013 peke yake, watu 2,793,636 walipima afya zao.  Yote hayo ndiyo yanayochangia kupungua kwa maambukizi. 
Ndugu Wananchi; 
          Ili kushinda vita hii hatuna budi kukumbushana kuachana na tabia na mienendo inayowaweka wanaadamu katika hatari ya maambukizi.  Mimi naamini Watanzania tunaweza kabisa kushinda vita dhidi ya UKIMWI.  Kinachotakiwa ni kuamua kukataa kupata maradhi haya.  Inawezekana, timiza wajibu wako.
Mapambano Dhidi ya Rushwa
Ndugu Wananchi;
          Tumeendelea na mapambano dhidi ya rushwa na mafanikio yanaendelea kupatikana.  Watu wengi zaidi hivi sasa wakiwemo vijana, wamefikiwa na kampeni ya kuwafanya watambue madhila yake, waichukie rushwa na wawe tayari kujitokeza kupambana na uovu huu.    Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeongeza kasi ya kupambana na rushwa.  Katika kipindi cha Julai 2013 hadi Juni, 2014 imefanikiwa kufungua kesi mpya 327, kati ya hizo kesi tatu ni za rushwa kubwa.  Aidha, shilingi bilioni 38.96 zimeokolewa.  TAKUKURU sasa imekwenda mbali zaidi na kuanzisha ofisi za Waratibu wa Kanda (Public Expenditure Tracking System – PETS Coordinators) wenye jukumu la kufuatilia matumizi ya fedha kwenye shughuli za ununuzi hasa kwenye miradi ya maendeleo.
 Tumefanya hivyo kwa kutambua kuwa shughuli za ununuzi kwenye Halmashauri na Serikali Kuu kwa jumla ndiko waliko mchwa wengi, wakubwa na wanene.  Katika kipindi cha 2013/14 pekee, miradi 215 yenye thamani ya shilingi bilioni 20.594 imekaguliwa.  Kati ya miradi hiyo, miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 9.59 ilionekana kuwa na mazingira ya mashaka na uchunguzi wa kina unaendelea hivi sasa.  Itakapothibitika kuwepo kwa dalili za rushwa, hatua zipasazo za kisheria zitachukuliwa bila ya ajizi.
Ndugu Wananchi;
          Tunaweza kupata ushindi mkubwa zaidi katika vita dhidi ya rushwa na mafanikio tunayoendelea kupata ni ushahidi wa ukweli wa kihistoria.  Sisi katika Serikali tutaendelea kutekeleza wajibu wetu kwa kuiwezesha TAKUKURU kwa rasilimali watu, vitendea kazi na majengo.  Mwaka huu pekee tumeiwezesha Taasisi kuajiri Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi 304 ili kuimarisha utendaji katika taasisi yetu hii muhimu.  Tunachohitaji ni ushirikiano wa karibu wa wananchi katika kuwafichua wale wanaojihusisha na vitendo vya rushwa. 
Ukweli ni kwamba watu hao tunaishi nao katika maeneo yetu.  Tuache kuwatukuza na kuwalinda kwani kwa kufanya hivyo tunawaimarisha, na kuwakatisha tamaa watu waadilifu na wale walio mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa.  Tuyachukue mapambano dhidi ya rushwa kuwa ni yetu sote na siyo ya TAKUKURU au viongozi peke yao.  Ushindi dhidi ya rushwa ni ushindi wetu sote. Hali kadhalika, kushindwa vita dhidi ya rushwa ni kushindwa kwetu sote.  Ni hasara kwako na taifa kwa jumla.
Vita Dhidi ya Dawa za Kulevya
Ndugu Wananchi;
          Tunaendelea na mapambano dhidi ya matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya.  Tunaendelea kupata mafanikio pamoja na ugumu uliokuwepo katika mapambano hayo.  Wahalifu wamekuwa wakibadili mbinu na kuongeza nguvu kila kukicha.  Hata hivyo, na sisi tumekuwa na unyumbufu wa kutosha. Ukweli ni kwamba kadri wahalifu hao wanavyoongezeka na ndivyo wanavyoongezeka kukamatwa.  Wakati katika kipindi cha Januari hadi  Septemba mwaka 2013 walikamatwa watuhumiwa 2,000, mwaka huu tangu Januari, hadi kufikia Oktoba, (2014) watuhumiwa 6,875 wameshakamatwa  na kesi zao ziko katika hatua mbalimbali.  Takwimu hizi zinaonyesha namna tulivyoongeza nguvu na tunavyofanikiwa katika juhudi zetu. 
Katika Mkoa wa Tabora peke yake, washitakiwa 177 wamefikishwa Mahakamani.  Kilichonisikitisha zaidi ni taarifa kuwa sasa kilimo cha bangi kinaongezeka kwa kasi mkoani Tabora.  Nawaomba muendelee kuwa wakulima hodari wa tumbaku pekee na siyo kilimo cha bangi.
Ndugu Wananchi;      
Tumeendelea kuchukua hatua nyingi madhubuti kukabiliana na mtandao wa uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya, ndiyo maana taarifa za matukio ya kukamatwa watu katika viwanja vyetu vya ndege zimepungua sana tofauti na mwanzo mwa mwaka huu.  Hii inaashiria kuwa mambo yamekuwa magumu kwenye njia hiyo, lakini tunajua  wanatafuta au watatafuta njia nyingine.  Kwa yote mawili hawatafika mbali, mkono mrefu wa sheria utawafikia. 
Tumeendelea kutoa huduma za kuwasaidia waathirika wa dawa za kulevya kuacha kutumia dawa hizo na kurejea katika maisha ya kawaida.  Vituo vyetu vya majaribio katika hospitali za Muhimbili, Mwananyamala na Temeke sasa vinahudumia waathirika wapatao 1,835 kwa kutumia dawa ya Methadone.  Tanzania ni moja kati ya nchi chache sana Afrika ambazo zimepiga hatua kubwa katika kutibu waathirika wake na wenzetu sasa wanakuja kujifunza kwetu.  Tutafanya zaidi ya tufanyavyo sasa.  Nia yetu ni kueneza huduma hiyo nchi nzima ili kunufaisha vijana wetu wengi.
Ndugu Wananchi;
          Tunayo kila sababu ya kushinda vita hii.  Hatamu ya ushindi wetu iko mikononi mwa wananchi wa Tanzania na vijana ambao ndiyo waathirika na wateja wakubwa wa dawa hizo.  Kataeni kuwa mawakala wa biashara hii haramu na ya maangamizi.  Pia kataeni kuwa watumiaji wa dawa za kulevya.  Biashara hii haiwezi kushamiri iwapo hapatakuwepo na mawakala na wateja wa uhakika.  Sisi Serikalini tunaendelea kuchukua hatua stahiki. Sasa tunapitia upya sheria ili tuweze kuanzisha taasisi mpya yenye mamlaka makubwa ya kupambana na dawa za kulevya kuliko Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya iliyoko sasa.  Maandalizi yamefikia pazuri.  Tutakamilisha jambo hili mapema iwezekanavyo.
Maji na Barabara
Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza naomba niwathibitishie wananchi wa Mkoa wa Tabora kwamba ahadi yangu ya kuleta maji mjini Tabora, Nzega na Igunga kutoka Ziwa Victoria iko palepale.  Tumechelewa kuanza kutokana na kuendelea kutafuta fedha za kutekeleza dhamira yetu hiyo.  Nafurahi kusema kuwa Mungu ni mwema tumefanikiwa.  Serikali ya India imekubali maombi yangu na watatukopesha kiasi cha dola za Marekani milioni 264 kwa ajili ya kutekeleza mradi huu.  Wataalamu wanamalizia michoro ya mradi ili baada ya hapo ujenzi uanze.  Subira yavuta heri, wote tuwe wavumilivu.
Tunaendelea na jitihada za kujenga barabara mbalimbali kwa kiwango cha lami hapa Mkoani Tabora.  Barabara zinazoendelea kujengwa zitakamilishwa na zile zinazoendelea na maandalizi zitaanza pindi tutakapopata fedha.  Lengo letu ni kuunganisha Mkoa huu na Mkoa wa Katavi, Kigoma na Singida kupitia Itigi hadi Manyoni.  Tumezungumza na Kuwait Fund ili watusaidie kujenga barabara ya Nyahua – Chaya wamekubali.  Hali kadhalika, Benki ya Maendeleo ya Afrika wanaelekea kuwa tayari kutupatia mkopo wa ujenzi wa barabara ya Tabora -  Sikonge – Koga - Mpanda.
Hitimisho
Ndugu Wananchi;
Narudia tena kuwashukuru wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine kufanikisha sherehe hizi ambazo zimefana mno.  Baada ya kusema hayo natamka rasmi kwamba shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu zimefikia kilele chake leo.
Nawatakia kila la kheri katika shughuli zenu za kila siku.
Mungu Ibariki Tanzania!
Mungu Ibariki Afrika!

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

ROSE NDAUKA HATAKI TENA MWANAUME

$
0
0
 
Stori:  Gladness Mallya
SIKU chache baada ya uchumba wake kuvunjika, msanii wa filamu Bongo, Rose Ndauka amefunguka na kusema kuwa kwa sasa haitaji tena mwanaume kwani anajikita zaidi katika kufanya kazi.

Akizungumza na gazeti hili juzikati, Rose alisema katika maisha yake ya uchumba alijifunza mambo mengi na anamshukuru Mungu amempa zawadi ya mtoto hivyo anafanya kazi kwa bidii ili aweze kumlea mwanaye vizuri.

Alisema hajutii kwa yaliyomtokea kwa mchumba wake Malik Bandawe, kwani makosa yaliumbwa makusudi ili watu wapate kujifunza, hivyo akili yake kwa sasa anaiwekeza katika kazi zake za sanaa.

DIAMOND AIBU NYINGINE DODOMA!

$
0
0
 
Stori: Richard Bukos, DodomaKWELI ni aibu nyingine! Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Jumamosi iliyopita alikumbwa na aibu nyingine kufuatia onesho lake kufanyika ndivyo sivyo na hivyo kuzua tafrani miongoni mwa mashabiki wake mjini hapa. 
Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akifanya shoo ndani ya Ukumbi wa Matei Lounge mjini Dodoma.
Aibu hiyo ilimkuta staa huyo ndani ya Ukumbi wa Matei Lounge mjini Dodoma ambako sukari huyo wa warembo alikuwa akifanya shoo.
AIBU YENYEWE
Aibu yenyewe iliyompata Diamond ilisababishwa na kuzimika kwa muziki wake mara tatu katika onesho hilo na hivyo kuwafanya mashabiki kupiga kelele huku wengine wakidai pesa zao za viingilio.

...Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiendelea na shoo

MAFUNDI MITAMBO WAHAHA
Hali hiyo iliwafanya mafundi mitambo kurekebisha nyaya kwa zaidi ya dakika 20 kila pale muziki ulipozimika hali iliyosababisha watu kuzidi kupiga mayowe na kumtolea maneno ya shombo Diamond, wengine wakitishia kumpopoa kwa mawe.
Muda mfupi baada ya mitambo hiyo kurekebishwa, mashabiki walianza kuserebuka tena lakini baada ya dakika 45 muziki ulizima tena na kusababisha mayowe mengine ya mashabiki wakiendelea kusema wameliwa pesa zao.
 
Mafundi mitambo wakirekebisha nyaya ili shoo iendelee
WEMA ATAKIWA
Katika zomeazomea ya safari hii,  mashabiki walikwenda mbele zaidi wakimtaka Wema apande jukwaani  kusalimia wakati mitambo ikirekebishwa wakiamini Diamond alikwenda na bebi wake huyo kwenye onesho hilo.
Hata hivyo, mafundi mitambo waliingia tena kibaruani na kurekebisha mambo baada ya dakika 23 muziki ukaendelea.
MAIKI NAZO ZAKOROMA
Diamond alianza kufanya tena makamuzi ndipo maiki nazo zikaanza kukoroma ambapo alianza kuwaomba wasaidizi wake wambabidilishie lakini kila waliyompa ilikuwa ikikoroma na kuwafanya mashabiki wazidi kupandwa na hasira.

Mashabiki wakisubiri shoo ilipobuma
Kitendo hicho kilimfanya Diamond asimamishe onesho na kuanza kumtupia lawama muandaaji (Matei) akidai kuwa ameshindwa kuweka hata betri mpya kwenye maiki alizomuandalia wakati amewatoza mashabiki kiingilio kikubwa cha shilingi 35,000 (kawaida) na 40,000 kwa VIP.
“Haiwezekani bwana, huu ni ubabaishaji wa hali ya juu, mwandaaji gani unaandaa shoo, unawachaji mashabiki kiingilio kikubwa halafu unashindwa hata kuweka betri mpya kwenye maiki? 
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akisubiriri mitambo ikae sawa.
DIAMOND ABANWA NA RISASI JUMATANO
Kufuatia hali hiyo, baada ya shoo, Risasi Jumatano lilimfuata Diamond na kumuuliza kulikoni muziki wake kuwa mwepesi pia kukatikakatika kila mara huku maiki nazo zikikoroma.
“Braza huu muziki siyo kabisa, huu ni muziki wa kupiga kwenye vigodoro lakini siyo wa kufanyia shoo zangu hasa kama hii ambayo watu wameingia kwa bei mbaya, ni kuwaibia watu.
“Mimi ni mtoto wa Kiislam ni lazima niongee ukweli, niliposikia sehemu yenyewe ninayokuja kufanyia shoo inaitwa Matei Lounge nikajua ni sehemu bab’ kubwa lakini kumbe ni ubabaishaji mtupu,” alilalama Diamond. 
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akirejea kuendelea na shoo.
INTAVYUU FUPI
Katika intavyuu fupi, Diamond, alisema anadhani kama anahujumiwa kwani haiwezekani muandaaji ashindwe kuweka vitu muhimu kwenye shoo. alidai wanafanya hivyo wakijua inapotokea tatizo kama hilo anayejulikana ni Diamond.
UJERUMANI, UINGEREZA
Ilianza nchini Ujerumani ambapo staa huyo alinusurika kudundwa kufuatia vurugu zilizoibuka ukumbini alfajiri ya Jumapili ya Agosti 31, mwaka huu baada ya kucheleweshwa kupanda stejini kwenye Ukumbi wa Sindelfingen uliopo Mji wa Stuttgart. 
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akitoa burudani.
Nchini Uingereza nako, Septemba 20, mwaka huu, Diamond alijikuta ndani ya aibu kubwa kwa mashabiki wake kufuatia mwandaaji kuingia mitini katika ukumbi wa LafACE club jijini Londan licha ya mashabiki kujaa.
KASORO YA DAIMOND NI MAMBO YA ‘USWAHILI’
Uchunguzi wa gazeti hili umegundua kuwa, Diamond licha ya kuwa msanii mkubwa kwa sasa lakini bado anaendesha mambo yake ‘kiswahili’ sana. 
Nuhu Mziwanda na bebi wake Shilole wakitoa sapoti katika shoo ya Diamond.
Kwa kawaida, msanii anapokwenda kupiga shoo mahali, kuna utaratibu unaoitwa kwa Kiingereza kama Technical Rider ambapo wasimamizi wake, akiwemo meneja huenda kuukagua ukumbi, usalama, muziki wenye viwango na hata steji shoo ilivyo.
Kama mambo hayo hayatakuwepo, msanii anaweza kugoma kufanya shoo. Lakini mambo yote hayo hutakiwa kuwepo kwenye mkataba wa makubaliano.Meneja wa Diamond, Babu Tale alipopigiwa simu juzi ili kuulizwa kwa nini hakuwepo Dodoma kuhakikisha uwezo wa vyombo vya muziki na maandalizi mengine, hakupatikana hewani!

BABA KIUMBE WA AJABU - 04

$
0
0
  
MTUNZI: ALLY MBETU
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
“Masalu unataka kuniambia hukuwa na habari Monika amekufa au ulitaka kunitega akili?”
“Shemu, huwezi kuamini kila dakika nimekuwa nikichanganyikiwa juu ya taarifa za msiba wa dada Monika. Kweli niliuona mwili ukiteremshwa kwenye gari. Lakini tokea hapo sikuweza kujua nini kilichoendelea mpaka leo hii.”
“Ulipouliza walikujibu nini?”
“Sijauliza bali nilifanya upelelezi wangu, kila kona nilifika lakini sikupata kuona chochote.”
“Ulichunguza nini?”
“Sehemu za makaburi au kupata taarifa kama hajafa yupo wapi?”
“Una uhakika Monika hakuzikwa?”
“Nina uhakika.”
SONGA NAYOOOOO
“Basi kuna sehemu wamemuweka, isiwe naye wamemuweka kwenye hicho chumba  na kumpaka mafuta?”
“Mmh! Sijui.”
“Unaweza kuingia?”
“Mmh! Nitajitahidi kuhakikisha napata ukweli.”
“Basi utakachokipata usikose kunijulisha.”
“Nakuahidi kukuletea kila kitu.”
“Haya shemu kwaheri.”
“Ya kuonana.”
Niliagana na shemu na kurudi zangu nyumbani, nilizidi kuchanganyikiwa na maneno ya pande mbili juu ya ukweli juu ya kifo cha dada Monika. Moyoni niliapa nikipata muda lazima mama ataniambia ukweli.
Siku zilikatika bila kujua taarifa za uhakika kuhusiana na habari tata juu ya kifo cha dada Monika ni kweli amekufa? Kitu ambacho moyo wangu haukukubaliana nacho. Uvumilivu ulinishinda, siku moja nilimfuata mama shambani kutaka kujua ukweli wa dada Monika. Kama kawaida yangu nilidanganya naumwa.                                                         
*****
Baada ya kuondoka na kuniacha nyumbani na mfanyakazi, majira saa nne asubuhi nilikwenda hadi shamba. Nilimkuta mama akipiga jembe kama hana akili nzuri. Moyoni nilimuonea huruma jinsi alivyohenyeka japo tuna pesa, kila dakika niliyakumbuka maneno ya dada Monika kuwa maisha yetu yanaongozwa na ushirikina.
Nilimwita mama ambaye alishtuka kuniona, niliamini kabisa alijiandaa kutokana na kumuuliza maswali mazito siku ya kwanza.
“Wee Masalu mbona huku si unaumwa?”
“Kidogo nimepata nafuu.”
“Haya ulikuwa unasemaje?”
“Kuna kitu mama kinanisumbua kila siku naomba msaada wako kwani naweza kuwa chizi.”
“Wee mwana mbona una mambo kuna nini tena?”
Mama alisema huku akiweka jembe pembeni na kunifuata nilipokuwa nimesimama.
“Masalu  kuna  nini tena?” Mama aliniuliza huku akifuta jasho kwenye paji la uso kwa mkono.
“Mama toka kifo cha dada Monika kuna mambo yamekuwa yakinichanganya na kunifanya kila siku nisijielewe.”
“Masalu mambo gani tena mwanangu kila siku huishi vioja?”
“Kuhusu dada Monika.”
“Monika kafanya nini tena?”
“Mama ni kweli dada Monika amefariki?”
”Masalu wewe si mtoto mdogo sasa, kila mtu anajua Monika amefariki wewe ukiwemo.”
“Mamaa, kama dada Monika amefariki mbona sikuona mazishi wala kaburi lake.”
“Masalu uyaone hayo ili yakusaidie nini?”
“Mama unajua majirani wanatusema vibaya toka taarifa za kifo cha dada Monika.”
“Nani aliwaambia Monika amekufa?”
“Mamaa, kwani kifo cha dada Monika kilikuwa cha siri?”
“Hata kama sio cha siri sio lazima wajue.”
“Hivi mama watu wakiniuliza dada Monika yupo wapi mimi niwajibu nini?”
“Wanyamazie usiwajibu chochote.”
“Lakini mama, kumbe hata yule shemeji aliyekuwa anakaa na dada Monika mlimfukuza asihudhurie mazishi?”
“Ahudhurie ametoa kiasi gani cha pesa kwa dada yako, zaidi ya kutuchanganya kifamilia?”
“Lakini mama tuachane na hayo, kaburi la babu na bibi nalifahamu, kaburi la kaka mkubwa nalifahamu. Makaburi yote yanayotuhusu nayafahamu na kila mwisho wa mwaka huenda kuyazuru familia yote na pia huenda kila mwezi kusafisha na kuyaweka katika hali ya usafi. Lakini kaburi la dada Monika lipo wapi, japo sikuhudhuria mazishi yake?”
“Masalu, wee mtoto mdogo hujui lolote, elewa kuwa dada yako Monika amefariki.”
“Mama, bado hayajaniingia akilini.”
“Masalu hebu niondokee, nilifikiri jambo la maana kumbe ni upumbavu,” mama alisema huku akijiandaa kurudi shambani.
“Mama unaniona mtoto lakini mambo yetu yote yapo hadharani.”
“Mambo gani?” Mama alishtuka na kunigeukia ili kutaka kujua.
“Dada Monika alinieleza mengi kuhusiana kifo chake alichotishiwa na baba kwa ajili ya kukikataa kidonda na kunitisha kidonda kile kitahamia kwangu.”
“Masalu nikueleze mara ngapi kuwa dada yako Monika alikuwa muongo aliyetaka aonekane alichokifanya ni sahihi cha ukosefu wa adabu?”
“Lakini mama mbona mengi aliyonieleza yanatokea? Uongo wake ni nini?”
“Kama nini?”
“Kuhusu wewe kuteseka na kilimo wakati familia ina uwezo mkubwa?”
”Kulima si kujitesa bali kujipa mazoezi.
“Mama, juzi uligombana na baba akikulazimisha uje shamba wakati ulikuwa hujisikii vizuri hata juzi uliniambia hukulala kutokana na maumivu ya mgongo. Mama naona umejisahau pale uliponiambia kuwa baba atakuua kwa vitu vya kulazimishana, bado tu unasema mazoezi. Mama unaweza kuona mnafanya siri lakini kila kitu kipo wazi.
“Unaweza kuona watu wapo kimya, lakini kuna maneno mengi sana juu ya kifo cha dada Monika, hakina tofauti na kifo cha mtoto wa dada Mihayo.”
“Masalu! Hakina tofauti ya nini?”
“Wanasema hata mtoto wa dada Mihayo alipokufa hakuzikwa.”
“Hakuzikwa alifanywa nini?” Maskini mama aliniuliza huku macho yakimtoka pima na kijasho chembamba kilimvuja.
“Eti wanasema kile chumba ambacho hakifunguliwi ndani kuna maiti ya mtoto ambayo huwa mnaipaka mafuta kila siku ndicho chanzo cha dada Mihayo kuwa na utajiri mkubwa kuliko wenzake.”
“Wee mtoto, haya yote umeyasikia wapi?” Mama alishtuka.
“Shemeji aliniambia kuwa kabla dada hajakata roho alimueleza mambo mengi juu ya ushirikina wa familia yetu kutumia kidonda chake kujipatia utajiri na hata alipotoka nyumbani kukataa kuendelea na kidonda ilisababisha kifo chake.”
“Masalu! Alimueleza kuwa kwenye chumba hicho kuna maiti ya mtoto?”
“Ndiyo, tena alimueleza kuwa watu waliokuwa wakiipaka maiti ile mafuta ni wewe baba na yeye dada Monika.”
“Mungu wangu, kayasema hayo Monika?”
“Na wasiwasi mwingine wanasema maiti ya dada Monika huenda nayo haikuzikwa imefichwa kwenye chumba kile cha siri.”
“Ooh... Mungu wangu ...Ooh moyo wangu,” mama alisema huku akishikilia kifua na kuanguka chini. Nilipojaribu kumuamsha hakuamka, nilipiga kelele kwa majirani wa shamba la pili. Sauti yangu iliwakusanya watu ambao walifika na kumpa huduma ya kwanza mama aliyekuwa amepoteza fahamu.
Alipopata fahamu aliwaomba wampe msaada wa kumrudisha nyumbani, jirani yetu mama Kusekwa alimsindikiza mama hadi nyumbani. Tulipofika alituacha na yeye kurudi shambani. Nilijawa na wasiwasi huku nikijilaumu kwa kumueleza mama mambo ambayo niliyaona mazito.
Nikiwa pembeni ya mama aliyekuwa bado amejilaza kwenye zulia huku akipuliziwa na upepo wa feni aliniita:
“Masalu.”
“Naam mama.”
“Kuna mtu aliuliza sababu ya kuanguka kwangu?”
“Ndiyo mama.”
“Uliwajibu nini?”
“Niliwaeleza kuwa ulianguka ghafla.”
“Hawakukuhoji zaidi?”
“Hawakunihoji zaidi ya kukupa huduma ya haraka.”
“Ooh, afadhali.”
“Unajisikiaje kwa sasa?” Nilimuuliza mama kwa huruma.
“Mmh, sijambo kidogo ila nakuomba tuliyozungumza yote usimwambie mtu.”
“Sawa mama.”
Nilimkubalia ili tu kuiacha siku ile ipite pia kutokana na hali yake, lakini bado sikupata jibu la dada Monika amekufa kweli, japo shemeji alinihakikishia amekufa. Na kama amekufa amezikwa wapi au ndiyo yaleyale niliyoelezwa kuwa mwili wake umefichwa ndani.
Moyoni nilibakia njia panda kutaka kujua ukweli kuhusu dada Monika, nilipanga kama mama atashindwa kunieleza basi nitamvaa baba na ukali wake ili nijue amekufa au mzima na kama amekufa amezikwa wapi.
Sikutaka kuliulizia jambo lile haraka kutokana na hali ya mama, niliamua kukaa kimya, lakini moyoni sikuwa na raha kutaka kujua ukweli wa kifo cha dada Monika. Siku moja asubuhi kabla ya kwenda shule mama alinifuata chumbani kwangu na kunieleza nisiende shule kuna sehemu anataka kunituma.
Nilibadilisha nguo zangu za shule na kuvaa za nyumbani, wakati huo alikuwa akijiandaa kwenda shambani. Lakini siku ile hakuwahi kama ilivyo kawaida yake. Tuliondoka nyumbani pamoja kuelekea shambani, baada ya muda wa chai, kutoka  nyumbani mpaka shambani ni mwendo wa dakika 45. Tulikwenda huku tukizungumza, mama aliniulizia habari za shule, nilimuelezea maendeleo yangu japo hakuwahi hata siku moja kushika madaftari yangu kuyaangalia.
Katika kumbukumbu zangu nilielezwa kuwa mama aliishia darasa la sita baada ya kupewa ujauzito na baba kisha kumtorosha. Taarifa hizo alinipa marehemu ambaye sina uhakika kama kweli amekufa au maiti yake imefungiwa katika chumba kisichofunguliwa.
Dada Monika alinieleza kuwa mama yetu alitengwa na familia yake baada ya kubebeshwa ujauzito na baba na kutoroshwa. Kitendo kile ndicho kilichofanya mama aishi maisha ya peke yake bila ndugu, ndugu yake mkubwa alikuwa baba kitu kilichofanya amnyanyase kwa kujua hana pa kwenda.
Sababu ile ndiyo iliyomfanya mama aishi kama mtumwa kwa vile kila alipofanya kosa baba alimtishia kumfukuza. Kwa kweli kitendo cha baba nilikiona cha kikatili sana, kila dakika nilijikuta nikimchukia baba kwa roho mbaya ya kuitesa familia yake kwa ajili ya mali.
Niliamini  mateso ya muda mrefu na shuluba zote, baada ya kupata utajiri wa kushirikina, basi alitakiwa mama atulie na kufaidi matunda ya uchawi wao. Lakini imekuwa tofauti mama kila kukicha amekuwa mtu wa kusurubika. Kilichonishangaza ni ndugu zangu kushindwa kumsimamia mama na kumpunguzia mateso ya kulima na kupasua kuni. Kila nilipomtazama mama yangu roho iliniuma na kujiapiza kama Mungu atanisaidia kupata kazi na kuwa na maisha mazuri basi nitamuondoa kwa baba.
Moyoni nilijiapiza kutokubali kuishi maisha machafu ya ndugu zangu ya kutoa familia zao kwa ajili ya kafara ya hatari na kujiona kama wataishi milele. Nilijiuliza dada Mihayo atamwambia nini mwanaye mbele ya Mungu, aliyemtoa kafara kwa ajili ya utajiri na baadaye kuendelea kumtesa kwa kumlaza kwenye chumba?
                                                             ****
Kuna kitu alinieleza dada Monika juu ya mama na kuniomba nimchunguze, nakumbuka siku hiyo alinieleza:
“Masalu, mama yetu anaishi maisha ya mateso makubwa sana, baba ni shetani asiyefaa mbele ya jamii. Nataka nikueleze kitu kimoja ambacho mimi wananikataza. Kwa taarifa yako nilikatazwa kulala na mwanaume lakini baba ana mwanamke kamjengea nyumba ya gharofa moja.”
Dada Monika aliendelea kunieleza jinsi watu wanavyotumia pesa huku mama akiteseka, alinieleza:
“Mdogo wangu familia yetu yote tutateketea kwa moto wa kiama, hebu ona maisha ya mama yanalingana na utajiri tulionao? Hata kama kuyumba hatuwezi kuishiwa kiasi cha kutisha, sawa na tembo kuugua maralia hawezi kukonda kama mbwa.
“Masalu, sema tu mama mbishi, nilimueleza mapema tuondoke pamoja ili aepukane na maisha ya mateso, lakini mama kama amerogwa na baba haelewi hasikii. Hivi kweli mama yetu ni wakuvaa kandambili za kufunga na kamba?” Nakumbuka siku hiyo dada Monika alizungumza huku akibubujikwa machozi.
Mama anateseka dada Mihayo anamhonga bwana wa pembeni gari, Masalu inauma lakini sina uwezo. Kama kidonda hiki angekuwa nacho mtu mwingine na mimi kuwa na uwezo wa dada Mihayo hata kwa kutoa kafara ya mtoto mama yangu angeishi kama malaika.
Lakini sina uwezo, hata hiki kidogo ninachokipata nikimpelekea mama hatakitumia zaidi ya kugeuzwa ndondocha na baba.”                                                  
ITAENDELEA SIKU YA KESHOOOOOOOOOOOO

DAVIDO KUINGIA KESHO DAR KWAAJILI YA FIESTA, WAJE, VICTORIA KIMANI LEO

$
0
0

Davido ambaye alishirikishwa na Diamond kwenye remix ya ‘Number One’ iliyofanya vizuri barani Afrika, ataingia usiku wa October 16 huku wakali wengine kama Waje, Victoria Kimani pamoja na meneja wa T.I na watu wake wanaingia Jumatano usiku.
 
Akizungumza mmoja ya wana kamati wa tamasha la Serengeti Fiesta, Fauzia, amedai kuwa licha ya wasanii hao aliowataja, huenda list ya wasanii wa Afrika ikaongezeka.
 

“Leo saa 12 na dakika 20 jioni anaingia Victoria Kimani, halafu leo leo saa sita usiku T.I meneja wake. lakini akina T.I. hawaingii leo, lakini meneja wake anaingia na watu wake. Halafu usiku wa saa 7 anaingia Waje. Kesho saa 6 usiku anaingia Davido na crew yake, kesho tena saa 7 usiku anaingia Patoraking, halafu Ijumaa saa 3 na dakika 20 usiku anaingia T.I. Pia Yemi Alade huenda na yeye akawepo kwasababu tupo kwenye mazungumzo naye, alisema Fauzia.

MCHUNGAJI ATOROSHA MKE WA MTU!

$
0
0

MCHUNGAJI anayejiita nabii na mtume, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) aliyetajwa kwa jina moja la Emmanuel amejikuta ndani ya majanga kufuatia madai mazito kwamba amemtorosha mke wa mtu ambaye ni mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema.
 
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema anayedaiwa kutoroshwa na mchungaji huyo.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mchungaji huyo alifika nyumbani kwa Jonas Mrema, mume wa Janet, maeneo ya Tegeta-Nyaishozi jijini Dar na kuishi kama mtumishi wa Mungu lakini polepole alianza mazoea tata na Janet.
“Mume alianza kuhisi mabadiliko ya mkewe kwa mtumishi huyo, lakini nadhani aliona ni mawazo yake tu. Ndipo siku ya siku akashangaa mkewe na mchungaji huyo wameondoka nyumbani hapo.
“Kwa sasa tangu tukio hilo litokee ni miezi kama mitatu. Mume alihangaika sana kumtafuta mkewe hadi jana (Jumatatu iliyopita) ndipo akampata wakiwa na mchungaji huyo kwenye nyumba moja ambako walikuwa wakiishi pamoja,” kilisema chanzo chetu.
 
Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania, Stela Joel akilizungumzia sakata hilo.
Iliidaiwa kwamba, mchungaji huyo alipopekuliwa alikutwa na paspoti ya nchini Burundi wakati yeye ni Mkongo wa Uvira na alionekana kuishi nchini kinyume na sheria hivyo alifunguliwa jalada la kesi kwenye Kituo cha Polisi cha Wazo Hili, Tegeta lenye Kumbukumbu Na. WH/RB/7040/2014- KUISHI NCHINI BILA KIBALI.
Juzi, Amani liliwasiliana na Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania, Stela Joel ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema tayari chama hicho kimemsimamisha uanachana Janet kwa kitendo chake hicho cha kumtoroka mumewe wa ndoa.
“Ni kweli na Chama cha Waimba Injili Tanzania kimemsimamisha uanachama Janet. Hatuna mzaha katika maadili,” alisema Stela.Amani lilimpigia simu mume wa Janet, Jonas Mrema ambapo katika mazungumzo baada ya salamu alipewa pole kwa matatizo ya mkewe, alisema asante kisha alipoulizwa kuhusu hali ilivyo aliomba apige simu yeye baadaye kwa vile alikuwa kikaoni.
Hata hivyo, baada ya saa mbili kupita bila kupiga, Amani lilimpigia tena simu ambapo iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.
CHANZO:GPL

BABA KIUMBE WA AJABU - 05

$
0
0

MTUNZI: ALLY MBETU
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

Mama anateseka dada Mihayo anamhonga bwana wa pembeni gari, Masalu inauma lakini sina uwezo. Kama kidonda hiki angekuwa nacho mtu mwingine na mimi kuwa na uwezo wa dada Mihayo hata kwa kutoa kafara ya mtoto mama yangu angeishi kama malaika.
Lakini sina uwezo, hata hiki kidogo ninachokipata nikimpelekea mama hatakitumia zaidi ya kugeuzwa ndondocha na baba.”                                                             
Kila nilipoyakumbuka maneno ya dada nilijikuta nikitokwa na machozi. Nilikumbuka neno moja ambalo dada Monika alinieleza nilifanyie kazi, aliniambia:
“Masalu, mchunguze mama muda mwingi akiwa peke yake mkono huwa shavuni, na kama utamfuatilia kwa muda baada ya kutoa mkono shavuni hutikisa kichwa na kufuta machozi. Katika maisha yetu toka tupate utajiri wa kishirikina furaha ya mama imetoweka, kutabasamu kumekuwa kama ajali lakini kulia kumekuwa kitu cha kawaida.
Mara nyingi mama amekuwa kila akiwa peke yake kanga huwa mkononi ili kufuta machozi. Vitu vile nilivifanyia kazi na kumueleza dada Monika yote aliyonieleza ni kweli. Aliniuliza swali lingine:
“Masalu umeshawahi kumuona mama akivaa nguo mpya?”
“Hapana,” nilimjibu.
“Hebu jifikirie mama yetu ni wa kuvaa nguo zilizoachwa na wanaye?”
“Nilikuwa sijui.”
“Kama hujui, hata macho yako hayaoni? Masalu sasa hivi wewe si mtoto unaona vitu ambavyo baadaye vinataka majibu kwa kile ulichokiona.”
“Huwezi kuamini dada nilikuwa kama nimefungwa akili, unachonieleza sasa hivi ndiyo kama kwangu kunapambazuka baada ya kukaa gizani kwa muda mrefu. Kama usingenieleza haya ningekufa kibudu.”
Niliamini kabisa kama dada Monika kweli amekufa, basi alikuwa amekufa na mengi moyoni sawa na samaki mwenye mengi ya kuzungumza lakini kila alipofumbua mdomo maji yalimjaa mdomoni. Kama alivyonieleza shemeji kabla ya kufa kutokana na maelezo yake mengi angenieleza mengi mazito.
                                                        ****
Tulipofika shambani mama hakuonesha kama anataka kulima, aliniweka chini ya mti huku akionekana mwingi wa mawazo. Baada ya ukimya mfupi mama aliniita jina langu.
“Masalu.”
“Naam mama.”
“Najua umesikia mengi juu ya maisha yetu, lakini hakuna ukweli kwa yote uliyosikia nakuomba uwapuuze, sawa baba.”
“Lakini mama mbona yote niliyoelezwa yana ukweli.”
“Ukweli upi?
”Mama kwanza naanza na wewe, toka nipate akili sijawahi kukuona ukifurahi, kila siku mtu wa masikitiko na kutokwa na machozi.”
“Ha! Masalu umejuaje?”
“Mama dada Monika kanieleza mambo mengi sana ambayo niliyafanyia kazi na kuupata ukweli juu yako.”
“Ukweli gani?”
“Kuhusu muda mwingi kuweka mkono shavuni na kutokwa na machozi, nilikufuatilia bila wewe kujijua na kuupata ukweli, pia uvaaji wako wa nguo mama toka nipate akili sijakuona ukivaa nguo mpya au nzuri, pia mama hebu angalia ndala zako. Kwa maisha tunayoishi wewe si wa kuvaa ndala za kufunga na waya.”
Niliposema vile mama alijiangalia kama hakujua alichokivaa wakati wa kutoka nyumbani.
“Mama najua yote haya yanatokea kwa ajili ya nini.”
“Kwa ajili gani?”
“Haya ni mateso anayokupa baba, baada ya kutengwa na ndugu zako, na chanzo cha yote ni yeye. Kutokuwa na ukaribu na familia yako, katumia ni fimbo ya kukuadhibia. Hivi mama hata wanao wengine wanajijali wao na kukusahau , bila wewe wangeijuaje dunia?
“Mama maisha haya unayoishi siyo mazuri, nilisikia eti baba alikutishia maisha kama utataka mambo makubwa. Haya ndiyo aliyoyakataa dada Monika kidonda akitunze yeye wengine wale maisha mazuri. Matokeo yake mnaamua kumuua na kuificha maiti yake.”
“Masalu nani kaificha maiti ya Monika?”
“Ipo wapi?”
“Masalu swali gani hilo, kila anayekufa si huzikwa?”
“Mbona mtoto wa dada Mihayo hakuzikwa?”
“Masalu una uhakika gani?”
“Dada Monika hakunificha yote nisemayo ni yeye aliyeniambia ni mengi sana nayajua kuliko mtu mwingine.”
“Masalu yote usemayo ni kweli, nakuomba usimwambie mtu yoyote habari hizi.”
“Kama ni kweli naomba kuanzia leo kazi ya kulima aachiwe mtu mwingine, uvae nguo nzuri ili ulingane na utajiri wa familia yetu.”
“Masalu hilo haliwezekani.”
“Kwa nini?”
“Baba  yako ataniua, naomba mwanangu yote unayoyaona yaache kama yalivyo, na ukizidi kumchokonoa anaweza kukuua.”
“Kama alivyomuua dada Monika?”
“Usiseme hivyo Masalu.”
“Mama tunafichana nini? Hivi utajiri ndiyo unaotufanya tukose huruma kwa wenzetu?”
“Masalu nakuomba usichimbe sana.”
“Hapana mama, huwezi kujua sasa hivi tunaonekana vipi mbele ya macho ya watu, kwa taarifa yako inasemekana Monika hajazikwa amewekwa ndani kwa imani za kishirikina.”
“Nani kasema?”
“Aliyekuwa akikaa na dada Monika ndiye anayeeneza habari hizi.”
“Yeye kajuaje?”
“Mama ina maana ninapozungumza na wewe unakuwa wapi? Nilikueleza kuwa kabla ya kufa dada Monika alimpa siri kubwa ya maisha yetu na sababu ya kifo chake. Pia alimueleza kuwa alikuwa na siri nzito ambayo asingemwambia mtu zaidi yangu mimi.”
 “Mmh, sasa huyo kijana kinamhusu nini kututangaza vibaya?”
“Kinachomuuma ni kumuulia mtoto wake asiye na hatia.”
“Hivi baba yako akijua kuwa ndiye anayetutangaza vibaya kwa watu kutakuwa na usalama kweli?”
“Atamfanya nini?”
“Masalu wee acha baba yako hana dogo, anaweza hata kumkata kichwa.”
“Akimuua atapata faida gani? Si ndiyo atakuwa anaongeza chuki kwa watu?”
“Masalu mwanangu, kwa umri wako hata nikueleza kitu hutanielewa, nakuomba kila ulilosikia liache lilivyo, wewe bado mtoto mdogo litakuchanganya.”
“Sawa nimekuelewa, ila naomba ukweli wa jambo moja.”
“Jambo gani?”
”Kuhusu ukweli wa dada Monika.”
“Ukweli upi?”
”Ni kweli amekufa?”
“Ndiyo.”
“Amezikwa wapi?”
“Mmh! Si makaburini.”
“Makaburini gani?”
“Kwa kweli siwezi kujua makaburi gani sikwenda kuzika.”
“Mama kuna makaburi tofauti na tuliyoyazoea?”
“Hakuna.”
“Na misiba yote huanzia kanisani kisha kupelekwa kuzikwa?”
“Ndiyo.”
“Sasa msiba wa dada Monika mliupeleka kanisa gani?”
“Masalu hata ukijua itakusaidia nini?  Aliyekufa amekufa huwezi kumfufua.”
“Hata kama siwezi kumfufua, dada Monika ndiye kipenzi changu, kaburi lake kwangu ni kielelezo cha kumuona kipenzi changu.”
“Masalu nakuomba suala hilo uachane nalo.”
“Yote nitaachana nayo si la dada Monika.”
“Masalu ukitaka kujua mengi utakosana na baba yako.”
“Kwa hiyo ukweli dada Monika maiti yake haikuzikwa?”
“Masalu nakuomba mwanangu chondechonde achana na hayo ili maisha yako yawe salama.”
“Kwa hiyo nikitaka kujua baba ataniua?”
“Hawezi kukuua ila utakuwa matatizoni.”
“Mmh! Sawa mama,” nilikubali kwa shingo upande kutokana na kuonekana kumuweka mama katika wakati mgumu.
Sikutaka kumsumbua sana mama yangu kutokana na maelezo ya dada Monika, kila nilipomtazama nilimuonea huruma. Nilimuahidi mama toka moyoni mwangu sitaulizia lolote kuhusiana na dada Monika wala kitu chochote kuhusiana na familia yetu.
Kauli yangu ilimfurahisha mama na kuonekana hawezi kuamini nilichokisema.
“Kweli Masalu.”
“Kweli mama, nakupenda sana mama yangu.”
“Asante Masalu, nakuomba kila unachokijua huenda hata mimi mama yako sivijui kwa vile baba yako alimpenda sana Monika hata siri zingine sizijui ambazo alikueleza wewe na pengine kabla ya kufa angekueleza,” maskini mama yangu alisema huku akitokwa na machozi, kitu kilichozidi kuniumiza nami machozi yalianza kunitoka kwa mbali.
“Nimekuelewa mama yangu, nimekuelewa sina budi kukusikiliza.”
“Asante Masalu, siku zote niliamini wewe na Monika ndiyo watoto wangu wanaonijali, endelea kunijali mwanangu wewe ndiye tegemeo langu, soma unikomboe.”
“Nitafanya hivyo mama yangu, nakuahidi kuwa kimbilio lako.”
“Asante mwanangu.”
Baada ya mazungumzo marefu tulirudi nyumbani, lakini  bado aliniacha na maswali lukuki moyoni mwangu, nilijikuta nakubaliana na shemeji, bwana wa Monika kuwa mwili wa dada umefichwa ndani pamoja na mtoto wa dada Mihayo.
                                                SIKU TATU BAADAYE
Siku tatu baadaye nilipata taarifa za kusikitisha za kifo cha utata cha shemeji aliyekuwa bwana wa Monika. Taarifa zilizonitisha na kuamini mazungumzo yangu na mama juu ya taarifa zinazosambazwa na shemeji zilimfikia baba na kuamua kufanya umaruhuni wake.
Ndugu walisema aliporudi nyumbani alianza kusema anasumbuliwa na kichwa huku akisema kama akifa atakuwa ni baba. Na usiku alipiga kelele akilitaja jina la baba, kitu kilichozidi kuaminisha kwamba anahusika moja kwa moja ili kumkomoa baada ya kusikia akitutangazia sifa mbaya familia yetu.
Kifo kile kiliongeza sifa mbaya kufikia hatua familia ya aliyekuwa mpenzi wa marehemu dada Monika kuja kutushambulia kwa maneno ya kutuita wachawi. Siku hiyo nilikuwepo, mama wa marehemu alikuja nyumbani na kuanza kutoa shutuma nzito kwa sauti ya juu huku watu wakisikiliza.”
“Mmeniulia mwanangu kwa imani zenu za kichawi ili muwe matajiri, kumuua mtoto wa Mihayo hamkuridhika mmemuua Monika na kumficha ndani bado tu mmeona haitoshi mmemuua mwanangu. Nawaambia damu ya mwanangu haiendi bure.”
Taarifa zile zilipelekwa kwa baba ambaye aliita polisi na kumchukua yule mama na kumpeleka kituoni. Kwa kweli kilichoendelea sikujua zaidi ya kumsikia baba akitamba atamuonesha. Pamoja na yule mama kupelekwa polisi familia yetu ilitawaliwa na sifa mbaya ambazo wengi walizisikia na kuzisambaza kwa watu kuwa maisha yetu yametawaliwa na utajiri wa kishirikina ambao ulikuwa ukipitia kwenye kidonda cha marehemu dada.
Nilijikuta nikiishi maisha ya kukosa amani, hata tembea yangu ilikuwa ya mashaka kwa kuhofia maneno ya watu. Siku zilikatika walisema mchana, usiku wakalala. Walizungumza sana mwisho wakanyamaza na kusahaulika na maisha yakaendelea.
Katika maisha yetu hakuna kilichobadilika, nilimaliza kidato cha nne kwa kupata matokeo mabaya. Niliamini kufanya vibaya kulitokana na migongano ya mawazo iliyotokana na kuchanganywa na mambo yote yaliyotokea yakihusu familia yetu, na taarifa nilizopewa na dada Monika juu ya kifo chake na matukio mengi ya kishirikina yaliyoilenga familia yetu.
Wazo la kurudia mtihani wa kidato cha nne, lilipingwa na baba na kusema atanipatia shughuli nyingine. Roho iliniuma kwani ndoto zangu zilikuwa kusoma kwa bidii ili siku moja nimkomboe mama kwenye mateso ya kuwekwa kifungoni na baba.
Miezi sita baada ya matokeo mabaya ya kidato cha nne, baba alionesha mapenzi makubwa kwangu tofauti na zamani. Alifikia hatua ya kuzunguka nami kila kona kwenye shughuli zake. Siku nyingine alinipa pesa za matumizi ambazo alinieleza ninunue kitu chochote nikitakacho.
Kwa akili za kitoto nilianza kubadilika na kuyaona yote niliyoelezwa juu ya ukatili wa baba ni uongo. Baba alikuwa mtu mzuri kwa kuninunulia nguo za thamani, nilionekana kweli mtoto wa mtu mwenye pesa tofauti na mwanzo nilivyokuwa nasoma shule.
Baba siku zote alinisifia kuwa mimi ndiye mtoto anipendaye kuliko wote, kauli zile za baba zilinifanya nisahau hata wazo la kumuuliza juu ya dada Monika. Siku moja tulikuwa tumekaa kwenye moja ya hoteli ya baba huku akiniruhusu kula nikitakacho, baada ya chakula baba alinichukua na kuingia naye kwenye ofisi yake iliyokuwa ndani ya hoteli ile ambayo sikuwahi kuingia siku za nyuma.
Baada ya kuingia ofisini baba aliendelea kunimwagia sifa.
“Masalu unajua nakupenda sana kuliko watoto wangu wote.”
“Najua baba.”
“Hebu niambie unataka nini nikufanyie ili ujue napenda sana.”
“Cha kwanza kunipa nafasi ya kurudia masomo niliyoanguka katika mtihani wangu ili nifanye vizuri, bado nina hamu ya kuendelea kusoma.”
“Tofauti na hilo?”
“Siwezi kusema kwa sasa mpaka nitakapofanya mtihani wangu wa marudio.”
“Masalu, kusoma si muhimu sana kwako, kama pesa zipo nitakufungulia mradi wako ili uendeleze maisha yako.”
“Lakini...”
ITAENDELEA SIKU YAKESHOOOOOO

LULU ATOA JIBU KWA MKONGO ANAYETAKA KIMAPENZI

$
0
0

SiKU chache baada pedeshee Mkongo, Mwami Rajabu kutangaza kuwa anamtaka staa wa sinema Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa gharama yoyote, mwigizaji huyo ametoa jibu linaloonesha dhahiri kwamba alikuwa radhi kumkubalia.
 
Staa wa sinema Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’
Akizungumza na waandishi wetu mara baada ya habari ya Mkongo huyo kuandikwa gazetini hivi karibuni, Lulu alisema kilichomshangaza kutoka kwa mwanaume huyo ni kwamba hakutakiwa kuanika hisia zake katika vyombo vya habari kama kweli ana nia ya dhati, angemtafuta mwenyewe au kwenda kujitambulisha nyumbani kwao.
“Namshangaa sana huyo Mkongo kwa kweli  kama angekuwa na mapenzi ya kweli asingeyaeleza kwenye magazeti, angenitafuta au angekuja nyumbani kwetu hapo ningemuona kweli ananipenda,” alisema Lulu.
 
Pedeshee Mkongo, Mwami Rajabu.
Staa huyo aliendea kumwaga chache kuwa, kama mwanamke, anahitaji kupewa heshima yake na kudai kuwa wanaume wengi wa sasa wamejisahau kupindisha mila za Kiafrika kufuata taratibu na badala yake wanatanguliza fedha mbele.
“Nadhani watu wamesahau mila za Kiafrika kabisa, huwezi kuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanamke halafu utumie rafiki au vyombo vya habari umpate, hiyo inakuwa siyo heshima kabisa,” alisema Lulu.
CREDIT: GPL

ROSE MUHANDO ADAIWA KUTAPELI TENA!

$
0
0

MWANAMUZIKI mkali wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amedaiwa tena kuhusika katika utapeli wa shilingi milioni mbili.

Muandaaji wa shoo hiyo, Ibrahim alidai kuwa Rose alitumiwa kiasi hicho cha pesa kama sehemu ya malipo ya kazi hiyo iliyokuwa ifanyike Jumapili iliyopita katika Ukumbi wa Hoteli ya Landmark uliopo Ubungo, jijini Dar lakini hakutokea.
“Huu ni utapeli wa hali ya juu, maana alipewa pesa yote ya shoo, cha kushangaza hakutoa taarifa yoyote ya dharura, simu akipigiwa hapokei na wala meseji hajibu,” alisema Ibrahim.
Rose alipopigiwa simu ili kujua madai hayo kama yana ukweli, simu yake iliita bila ya kupokelewa hivyo akatumiwa meseji ambayo nayo ilionesha kumfikia lakini hakujibu chochote.
 
Mwimbaji wa nyimbo za Injili, John Lisu.
Hivi karibuni, Rose alidaiwa kuingia mitini na shilingi milioni moja aliyopewa kama malipo ya kutumbuiza katika uzinduzi wa albamu ya mwimbaji wa nyimbo za Injili, John Lisu.
(CREDIT: GPL)

Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>