Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

SIRI NZITO ZAFICHUKA TRAFIKI WA MHABA

$
0
0
 
Na Ojuku Abraham
BAADA ya kuvuja kwa picha katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita, iliyowaonesha askari wawili wa usalama barabarani wakiwa ‘kimahaba niue’ ndani ya sare za kazi na kusababisha kupoteza ajira zao kutokana na kukiuka maadili, siri zaidi nzito zimezidi kuvuja kuhusiana na ishu hiyo na Amani limemuibua afande wa kike baada ya kumsaka sana.
 
Askari aliyefukuzwa kazi kutokana na kosa la ukiukaji wa maadili, Veronica Mdeme.
Kwa mujibu wa vyanzo makini kutoka wilayani Misenyi mkoani Kagera, askari wa kike aliyeonekana kwenye picha hiyo chafu, WP. 8898 Veronica Mdeme, inadaiwa kuwa alipata uhamisho kutoka polisi mkoani humo na kupelekwa katika wilaya mpya ya Misenyi mwaka 2011 ambako mwaka mmoja baadaye, ndipo akapigwa picha hiyo iliyoleta gumzo kubwa ndani na nje ya Bongo.
Ilidaiwa kwamba, picha hiyo ilipigwa katika barabara ya lami iendayo Mutukura, umbali wa Kilomita 50 kutoka Misenyi na kwamba askari hao walikuwa katika Kituo cha Polisi cha Kyaka.
Nguzo ya umeme inayoonekana nyuma yao, ni zile zinazopeleka umeme nchini Uganda kutoka Bwawa la Umeme la Mtera, Tanzania.
ILIKUWA PICHA YA KISHKAJI TU LAKINI…
Habari zilidai kuwa, askari hao Veronica, F.7788 Mpaji Mwasumbi na PC Fadhil Linga, walikuwa zamu moja na kwamba picha hiyo ilipigwa katika mazingira ya kishkaji tu lakini baadaye ikaja kuzua balaa kubwa.
Ilisemekana kwamba, Linga ndiye aliyewapiga picha wenzake ambao habari zisizothibitishwa zilisema kuwa walikuwa na uhusiano wa kijamii.
Madai yalizidi kutiririshwa kwamba baada ya kupigwa kwa picha hiyo, Linga alibaki na nakala katika kamera yake kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya kugundua kuwa kumbe ilikuwa ni dili.
AWAGEUZIA KIBAO
Ilidaiwa kwamba, katika hali isiyotarajiwa, Mpaji na Veronica hawakuamini masikio yao baada ya Linga kuwaambia kwamba alihitaji kupata ‘kitu kidogo’ kutoka kwao ili aweze kuendelea kuhifadhi siri ya picha hizo.
Ilisemekana kuwa afande huyo aliwaambia wawili hao kama ataivujisha picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii, watapoteza kazi.
“Baada ya kuambiwa hivyo, jamaa walilegea kabisa. Mwanzoni walitia ngumu lakini walipoona jamaa amekomaa, hawakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana naye, hivyo akawa anapata kitu kidogo kila alipojisikia  na kuwa nipe nikupe na hakuna uhakika kama dada Vero alisalimika kwenye mambo mengine kwani naye alikuwa akitumia nguvu kubwa kuhakikisha mumewe hajui,” kilidai chanzo hicho.
 
Veronica Mdeme akiwa kwenye pozi.
WAAMUA KUJILIPUA, WAMSHTAKI
Ilielezwa kwamba, baada ya ‘kutolewa upepo’ kwa muda mrefu na kuonekana kama wangekuwa ATM ya kudumu ya Linga, Mpaji na Veronica waliamua kujilipua na kwenda kumshtaki kwa kigogo wa juu wa jeshi la polisi mkoani humo ambaye anatajwa kuujua mchezo mzima ulivyokuwa.
Ilisemekana kwamba, kiongozi huyo alilichukulia jambo hilo kwa uzito wake na kuwakalisha wote watatu ili kuzungumza nao.Iliendelea kudaiwa kuwa katika kikao kati ya askari hao na bosi wao, wawili hao walikiri kupigwa picha hiyo na kuomba msamaha, lakini wakamlalamikia mwenzao ambaye naye alikiri kufanya kitendo hicho, kwa kuwageuza kuwa ATM.
Ilidaiwa kuwa mkubwa huyo alimuamuru Linga kuzifuta picha hizo na kuwataka kusameheana, kwani kitendo walichokifanya ni kibaya na kinachoweza kuhatarisha ajira zao. Linga alikubali ‘kuzi-diliti’ picha hizo!
WAGAWANYWA, LINGA ARUDIA
Ikazidi kudaiwa kuwa ili kuwafanya waishi kwa amani, waligawanywa katika vituo tofauti vya kazi mkoani humo huku mmoja wao, Mpaji akipelekwa Dar ambako alikwenda kusoma Chuo cha Polisi Kurasini.
“Wakiwa katika vituo hivyo tofauti, Linga alitulia kwa muda mchache tu kabla ya kuanza tena usumbufu wake, hasa kwa Veronica ambaye anadaiwa kuwa mke wa mtu. Ni katika usumbufu huo wa mara ya pili, akina Mpaji wakaamua kumjibu jeuri jamaa, hawakuwa na uoga tena kwa vile suala lao lilishafahamika kwa wakubwa,” kilisema chanzo chetu.
Inaelezwa kwamba majibu ya jeuri kutoka kwa Vero na Mpaji yalimuudhi Linga ambaye kwa lengo la kuwakomoa, aliamua kuzitupa picha hizo katika mitandao mbalimbali ya kijamii ambako nako zilizagaa kwa kasi ya moto wa kifuu na kuwafikia watu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari vilivyoamua kuripoti.
 
Veronica Mdeme alipokuwa akidendeka na askari mwenzie.
“Picha hiyo ilipoonekana mtandaoni, moja kwa moja polisi walijua imewekwa na Linga kwa sababu hakukuwa na mtu mwingine aliyefahamu kuhusu picha hiyo. Ndiyo maana wote watatu walifukuzwa kazi siku moja, hawakuwa na sababu ya kuhangaika kujua nani kaweka,” kilisema chanzo hicho.
PICHA YA MREMBO YAWA GUMZO
Baada ya kufukuzwa kazi kwa wahusika hao watatu, kumekuwa na picha za mrembo mkali ambaye amekuwa akifananishwa na Veronica huku kukiwa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kama kweli ni yeye (angalia picha ukurasa wa mbele).
Kwa mujibu wa maoni lukuki katika mitandaoni, kama kweli mrembo huyo ndiye huyo askari wa kike, basi jamaa aliyekuwa naye kimahaba, alistahili adhabu yoyote kuliko kukosa mahaba hayo.
“Ni kama walivyoimba wale watoto wa Yamoto Band, yaani nzi kufia kwenye kidonda siyo ufala bali kupenda. Huyu mtoto mashalaah,” ilisomeka sehemu ya maoni ya stori hiyo ambayo ndiyo habari ya mjini kwa sasa.
Juzi, Amani lilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe ili kumsikia nini kinaendelea baada ya askari hao kufukuzwa kazi lakini hakuwa hewani.
Naye msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Advera Senzo alipopigiwa simu na kuulizwa alisema walishafukuzwa kazi hakuna kingine lakini akaelekeza apigiwe simu Mwaibambe.

MAMA AMNG’ATA ULIMI ‘SERENGETI BOY’KISA MAPENZI

$
0
0

 Kijana Paulo Simon aliyekatwa ulimi na mwanamke mmoja anayefahamika kama Mama Abuu.

Na Joseph Ngilisho, ArushaHATARI! Katika hali isiyotarajiwa, mwanamke mmoja aliyefahamika kama Mama Abuu amefanya tukio la ajabu baada ya kumng’ata na kumkata ulimi kijana Paulo Simon mwenye umri wa miaka 18, kufuatia ‘Serengeti Boy’ huyo kukataa kufanya naye mapenzi katika eneo la Tindigani, Kimandolu mjini Arusha hivi karibuni.

Akisimulia kwa kuandika kwenye karatasi, Simon ambaye sasa amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru jijini hapa, alisema alikuwa akiuza baa katika eneo hilo wakati mwanamke huyo alipotokea na kukaa kaunta na kuanza kunywa pombe kama wateja wengine.
Alisema ilipofika saa 6:30 usiku wateja wengine wote waliondoka na kubakia mama huyo pekee, kitu kilichomfanya naye afunge baa. Lakini alipomaliza kufanya hivyo mama huyo alimfuata na kumweleza kuwa alihitaji kufanya naye mapenzi.
 
Kijana Paulo Simon(majeruhi) akiandika maelezo kwa Polisi kwa njia ya maandishi.
“Sikuwa na mazoea naye, nilipokataa kufanya naye mapenzi, alinisogelea na kunishika sehemu zangu za siri na kuanza kuzivuta, nilipopiga kelele akanishika kichwa na kunilazimisha ‘kunidendesha’, akafanikiwa kuingiza mdomo wake kwangu na kunikata ulimi wangu, akaondoka nao na kwenda kuutema karibu na mlango wa bar,” alisema Simon ambaye wahudumu wa hospitali hiyo wamelazimika kumwekea ndoo ili awe anatemea damu kutokana na kujaa mdomoni.
Alisema baada ya kukatwa ulimi ambao sasa unamletea maumivu makali, alifanikiwa kufika nyumbani kwake kabla ya tajiri yake kumchukua na kumpeleka hospitalini ambako amelazwa.
Jeshi la Polisi mkoani hapa limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa ameshatiwa mbaroni huku uchunguzi ukiwa unaendelea. Hali ya majeruhi inaendelea vizuri.
CREDIT:GPL

NINI CHA KUFANYA MUMEO ANAPOZAA NJE YA NDOA?

$
0
0

Nianze kwa kumshukuru Mungu ambaye ameniweka hai mpaka siku hii ya leo, tunapokutana tena kwenye uwanja wetu huu kujuzana, kujadiliana, kuelimishana na kuzungumzia ishu mbalimbali zinazohusu uhusiano wa kimapenzi.

Leo nataka kuzungumza na wewe mama, dada, shangazi au mwanamke ambaye upo kwenye uhusiano wa kudumu, nikimaanisha umeolewa. Je, umewahi kugundua, kuhisi au kuambiwa kwamba mumeo mliyeishi pamoja kwa kipindi kirefu, amezaa mtoto na mwanamke wa nje?
Bila shaka kila mmoja atakuwa na majibu yake lakini katika mada hii nataka kuzungumza zaidi na wahusika, wanawake ambao wamewahi kutokewa na tatizo hili. Ni ukweli usiofichika kwamba wanaume wengi siku hizi wamekuwa na mchezo wa kuzaa nje ya ndoa.
Yaani amekuoa na mnaishi pamoja kama mume na mke, mmejaliwa kupata mtoto au watoto lakini kumbe nyuma ya pazia, yupo mwanamke mwenzako ambaye naye amezalishwa na mumeo. Je, unapaswa kufanya nini katika mazingira kama haya?
Mada ni nzito na ndiyo maana napenda zaidi kusikia kutoka kwa waliotokewa na tatizo hili kwani naamini kupitia wao, wengine watajifunza na hata watakapokuja kutokewa na hali kama hii, watajua namna ya kupambana nalo.
Je, ukigundua mumeo ana mtoto nje ya ndoa, utadai talaka, utamtafuta mwizi wako mpaka umpate na kumshikisha adabu, utamsaka mtoto ili umdhuru au utafanya nini? Hebu sikiliza ushuhuda wa mwanamke huyu ambaye nimewahi kukutana naye, akanisimulia mkasa wake ambao leo ndiyo ulionisukuma kuja na mada hii.
“Mimi ni mwanamke ambaye nimeolewa miaka minne iliyopita na kufanikiwa kupata watoto wawili. Wa kwanza ana miaka mitatu na huyu mwingine bado hajafikisha hata mwaka mmoja. Mume wangu ni mfanyakazi wa kampuni moja kubwa jijini Dar es Salaam.
Kwa kipindi chote tangu tuoane, tumekuwa tukiishi kwa amani na upendo wa hali ya juu mpaka miezi michache iliyopita ambapo nimegundua jambo baya mno katika ndoa yangu.“Nimegundua kwamba mume wangu ana mtoto mwingine ambaye ana umri wa miaka miwili.

Huyo mwanamke aliyezaa naye, mwanzo walikuwa wakifanya kazi pamoja ingawa sasa nasikia hayupo tena kazini kwa mume wangu ila nimesikia tetesi kwamba mume wangu ndiye aliyempangia chumba na anamhudumia kila kitu na siku nyingine huwa anaenda nyumbani kwake.
Nipo njia pandaa najihisi nakaribia kupatwa na ugonjwa wa moyo, ndoa yangu naiona chungu, namchukia sana mume wangu japokuwa ameniomba msamaha, sidhani kama nitamsamehe, naomba ushauri, nifanyeje?”
Hayo ndiyo maelezo aliyonipa mwanamke huyo ambaye kiumri bado ni mbichi na ndoa yake ndiyo hiyo ina miaka minne. Mpendwa msomaji wangu, bila shaka umeyaelewa vizuri maelezo ya dada huyu na tayari unayo majibu ya kumpa. Je, utamshauri nini?
KOSA LA MSINGI
Kosa la msingi ambalo mume wa dada huyu alilifanya ni usaliti. Yaani licha ya mwenzake kumpenda kwa moyo wote, aliamua kuchepuka na kwenda kwa mwanamke mwingine na kumpa ujauzito, kosa juu ya kosa.
Kosa la usaliti pekee ni baya na kama tulivyowahi kuzungumza kipindi cha nyuma, humchukua muda mrefu sana mtendewa wa usaliti kurudi kwenye hali yake ya kawaida na kurejesha mapenzi kwa aliyemtenda. Wengine hujikuta wakishindwa kabisa kusamehe na kusahau yaliyotokea.
Inapotokea usaliti umesababisha mtoto wa nje, uzito wa kosa huwa mkubwa zaidi na hata namna ya kulishughulikia, ni lazima wanandoa wote wawe makini sana kwani vinginevyo, huo unaweza kuwa mwisho wa ndoa au mapenzi kati ya wawili hao.

Tukutane wiki ijayo kwa mwendelezo wa mada hii ambayo naiweka mezani ili sote tuweze kuijadili. Kwa maoni, ushauri nicheki kupitia namba zilizopo hapo juu.
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

BABA KIUMBE WA AJABU - 06

$
0
0

MTUNZI: ALLY MBETU
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

“Masalu unajua nakupenda sana kuliko watoto wangu wote.”
“Najua baba.”
“Hebu niambie unataka nini nikufanyie ili ujue napenda sana.”
“Cha kwanza kunipa nafasi ya kurudia masomo niliyoanguka katika mtihani wangu ili nifanye vizuri, bado nina hamu ya kuendelea kusoma.”
“Tofauti na hilo?”
“Siwezi kusema kwa sasa mpaka nitakapofanya mtihani wangu wa marudio.”
“Masalu, kusoma si muhimu sana kwako, kama pesa zipo nitakufungulia mradi wako ili uendeleze maisha yako.”
“Lakini...”
“Masalu hakuna haja ya kubishana, naomba ujiandae kuna duka moja nimelifungua na kuanza kazi wewe ndiye msimamizi mkubwa.“
Nilijikuta nakosa cha kuzungumza na kukubaliana na baba japo nafsi yangu ilitaka kusoma ili nimkomboe mama yangu. Nilijua kukubali mradi ule japo utakuwa chini yangu bado utakuwa wa nguvu za kishirikina kwa kuhofia huenda siku za mbele baada ya kuoa na kupata mtoto akatolewa kafara.
Baba alinitolea hati za kumiliki duka lile lenye jina langu na kunionesha sehemu ya kusaini. Nilisaini na kuniahidi kunifanyia mambo makubwa kuliko ndugu zangu wote. Baada ya kutoka pale aliniingiza kwenye gari lake na kunipeleka mjini Barabara ya Pamba kwenye duka langu.
Nililikuta duka lipo wazi na watu wakiendelea na mauzo ya vitu, lilikuwa duka kubwa la kuuza vitu vya jumla na rejareja. Tulipofika dada mmoja ambaye alikuwa akinifahamu aliniuliza:
“Leo Masalu ndiyo umeamua kuja?”
“Alikuwa anamalizia masomo,” baba alijibu.
“Karibu bosi.”
“Asante.”
Nilijibu huku nikiingia dukani na kwenda kukaa kwenye kiti changu kilichoandaliwa kwa ajili ya kukalia niwapo kazini. Baada ya kukagua duka lililokuwa likilingana na maduka ya  ndugu zangu, baba aliondoka na kuniacha nisimamie duka langu.
Alinipitia jioni na kunirudisha nyumbani, nilipofika nyumbani nilimueleza mama kuwa nimepewa duka na baba. Ajabu mama badala ya kufurahi alitokwa na machozi, kwa vile tulikuwa peke yetu nilimuuliza:
“Mama unalilia nini?”
“Mmh, najua hukufurahi na unaweza usifurahi.”
“Kwa nini mama?”
“Ni vigumu kunielewa kwa sasa lakini tumuombe Mungu aepushe mbali.”
“Mama mbona sikuelewi?”
“Suala la shule limeishia wapi?”
“Baba amekataa na kusema tayari ameishanifungulia duka, na leo ndiyo nimekabidhiwa rasmi.”
“Mmh! Haya”
“Kwani  kuna nini?”
“Hakuna ubaya.”
“Mama kuna kitu hutaki kuniambia.”
“Hakuna kitu kikubwa zaidi ya kukatika kwa ndoto yako ya kusoma.”
“Mama nitasoma tu.”
“Kwa duka lako, si unawaona ndugu zako walivyo bize na maduka yao hata muda wa kunikumbuka hawana.”
“Mama nitajipanga, siku hizi kuna masomo ya jioni.”
Siku zilikatika, biashara nayo ilizidi kushika kasi, hata mwili wangu ulibadilika na kuonekana mtu mzima kutokana na kunenepa, hata sauti yangu ilibadilika. Lakini ilikuwa tofauti na wenzangu, mimi nilibakia nyumbani na mama pamoja na mfanyakazi mmoja, niliamua kumpumzisha mama kazi za shamba, lakini mama aling’ang’ania kwa kusema kama akiacha kwenda shamba atafukuzwa na baba.
Nilipomuuliza baba naye alinijia juu na kunionya nisiingilie mambo yake, sikuwa na jinsi, nilimuacha mama aendelee kulima huku nikitumia vijana kumsaidia mama, ambaye alifanya kazi ndogondogo. Kingine ambacho sikukubaliana na baba ni kuhusu mavazi ya mama yaliyokuwa yamechoka.
Hapo sikukubali hata kidogo na nilikuwa tayari kwa lolote.
“Masalu unataka tubishane?” baba alinikaripia.
“Kwa hili baba sikubaliani nawe hata kidogo.”
“Umeanza kuvimba kichwa kwa vipesa unavyopata?”
“Si kuvimba kichwa, nipo sahihi, kama mali zako chukua lakini nimechoka kuiona hali hii mpaka lini?”
Sikuogopa chochote cha baba mpaka tulipokubaliana kumnunulia mama nguo mpya, pamoja na mzozano huo bado baba hakuonekana kukasirika sana. Mama alibadilika  na  kuanza kuvaa vitenge vya gharama, hata kandambili alivaa mpya.
Ndugu zangu walipokuja nyumbani hawakuamini kumkuta mama yetu kapendeza. Walipomuuliza aliwaeleza ni kwa ajili yangu, walinifuata kutaka kujua nimewezaje kumbadili baba kukubali mama kuvaa nguo mpya. Niliwaeleza ni msimamo hakuna kitu kingine, maisha yaliendelea.
Katika vitu ambavyo baba alinionya ni kutembea na wanawake, nilikumbuka kauli za dada Monika kuwa alianza kuelezwa asijihusishe na wanaume na mwisho alipata kidonda cha kichawi.
Nilimkubalia kumridhisha tu, lakini niliendelea kuwa na uhusiano na binti mmoja ambaye ndiye tuliyepanga kuoana siku za mbeleni. Siku zote mambo yangu nilikuwa nayafanya kwa siri kubwa bila baba kujua kwa kuamini sina uhusiano wa kimapenzi na mwanamke.                                                       
                                                                           ****
Siku moja nikiwa nimelala niliota kitu kama nyoka, lakini sikukielewa vizuri kikiniuma kwenye mguu wa kulia kwa ndani. Nilishtuka lakini hakukuwa na kitu chochote, niliendelea kulala. Kesho yake nilikwenda dukani kama kawaida na kuendelea na shughuli zangu.
Wiki moja baadaye nilianza kusikia muwasho sehemu niliyoota nimeumwa na kitu kama nyoka. Nilimueleza mama asubuhi baada ya kujikuna mpaka kukaleta weusi sehemu iliyokuwa ikiniwasha. Mama alishtuka, jambo lililonitisha.
”Mama mbona umeshtuka?”
“Baba yako alikueleza nini?”
“Kuhusu nini?”
“Huo muwasho wako?”
“Hata, sijazungumza lolote.”
“ Mmh!” Mama aliguna.
“Unaguna nini?” nilimuuliza.
“Hapana.”
“Mbona kama unanitisha, unakuwa hauna tofauti na wa dada Monika?”
“Ni kweli.”
“Unataka kuniambia ndiyo huu?”
“Ndiyo.”
“Mungu wangu nimekwisha.”
“Wala hujaisha, ukifuata masharti yake hauna tatizo.”
“Kwa hiyo na mimi nitakuwa na kidonda kama dada Monika?”
“Ndiyo lakini hakiumi.”
“Na nikikosea nitakufa kama dada Monika?”
“Monika kafa na yake.”
“Mamaa, juzi tulizungumza nini, leo unanibadilikia?” Nilimuona mama akitaka kuficha mambo.
“Masalu nakuomba suala hili muulize baba yako na usimueleze kuwa tumezungumza.”
“Sawa mama.”
Niliachana na mama huku mwili wote ukininyong’ea kwa kujua niliyoelezwa na dada Monika yametimia.
Siku ile hata hamu ya kwenda kwenye duka langu sikuwa nayo, kwa kuamini nilikuwa nimeishaharibika. Nilishinda ndani huku nikilia lakini mama alitumia muda wake kunibembeleza kuwa sijaharibika kama ninavyo fikiria.
“Masalu usilie mwanangu.”
“Mama kwa nini mnanitendea unyama kama huu kosa langu nini?”
“Huna kosa mwanangu, kidonda hiki humfuata yule aliyeteuliwa na mizimu.”
“Wataniteua vipi wakati mimi sitaki?”
“Huwezi kukataa.”
“Mama nina malengo yangu wewe unajua.”
“Ni kweli, lakini hakuna wa kumzuia baba yako uamuzi wake.”
“Mama na mimi nitakufa kama dada Monika?”
“Kwa nini?”
”Siwezi kufuata masharti ni magumu.”
“Si magumu ukizingatia.”
“Siwezi mama siwezi...,” nilikatwa kauli na sauti ya baba aliyekuwa akimwita mama. Nilimuona mama akishtuka na kuanza kutetemeka na kijasho chembamba kilimvuja.
“Mama vipi?”
“Naomba usimwambie baba yako niliyokueleza, ataniua.”
“Siwezi kumwambia.”
“Ng’wana Manoni.”
“Lama,” mama aliitikia huku akitoka chumbani kwangu.
“Vipi mbona unatoka chumbani kwa mtoto?”
“Hajisikii vizuri.”
“Na shamba hujaenda?”
“Baba Mihayo nimwache Masalu anaumwa niende shamba?”
“Kwani anaumwa sana?”
“Toka asubuhi analia tu.”
“Kafanya nini?”
“Mmh, nenda ndani ukamuone.”
“Masalu,” baba aliniita.
“Naam baba.”
“Eti kuna nini?”
“Kuna vitu ambavyo sielewi.”
“Vitu gani?” Baba alisema huku akiingia ndani.
Alipoingia ndani alinikuta nimeshikilia mguu.
“Kuna nini?”
“Baba sehemu hii inaniwasha sana kufikia hatua ya kunikosesha raha.”
“Hebu nione,” nilimuonesha baba, baada ya kuona alisema:
“Kumbe hiki?”
“Ndiyo baba.”
“Sasa tatizo nini?”
“Kinaniwasha.”
“Usikikune kitapoa chenyewe.”
“Hapana baba bora niende hospitali.”
“Masalu usiende hospitali, ugonjwa juu si wa kawaida.”
“Wa nini?”
“Utajua tu baadaye, lakini chonde usiende hospitali.”
“Au ndiyo kama wa dada Monika?”
“Eti?” Kauli yangu ilimshtua baba na kunitazama mara mbili kama ndiyo siku yangu ya kwanza kuniona.
“Eti umesemaje?”
“Baba mbona umeshtuka hivyo?”
“Sijakuelewa, hebu rudia swali lako.”
“Nauliza, kisiwe kidonda kama cha dada Monika.”
“Mama yako ndiyo kwakwambia? Leo atanitambua,” baba alikuja juu.
“Baba badala ya kunijibu swali langu unakimbilia kutaka kumpiga mama au ndiyo umemuona gunia lako la mazoezi,” nilizidi kumchanganya baba na maneno yangu ambayo hakufikiria hata siku moja nitayatamka.
“Masalu mbona unanikosea heshima?”
“Sijakukosea heshima ila nataka kujua ukweli wa muwasho huu kwa vile nilibashiliwa kipindi kirefu.”
“Na nani?”
“Na dada Monika”
“Alikubashiria nini?”
“Alinieleza kuwa kifo chake kimetokana na kukikataa kidonda hiki, na ulichomuahidi ndicho kilichotokea.”
“Muongo, unamsingizia Monika wakati uongo wote kakupa mama yako.”
“Baba utamuonea mama bure, mama hajanieleza chochote zaidi ya kunifanya mtoto mdogo mambo ninayoyajua.”
“Mambo gani?”
“Kuhusu chanzo cha utajiri kidonda cha dada Monika mpaka kifo chake kilisababishwa nini na utabiri wake kidonda kikitoka kwake kinakuja kwangu.”
“Mmh,” baba aliguna, kisha alinitazama kwa muda na kuangalia juu kabla ya kushusha tena pumzi.
“Masalu.”
“Naam.”
“Niambie ukweli mama yako kakuambia nini juu ya huu muwasho?”
“Kaniambia ni muwasho wa kawaida, utapoa wenyewe.”
“Hakukuambia kitu kingine?”
“Hajaniambia, ndiyo maana nilijua ananidanganya, dada Monika alinipa siri nyingi, zingine hata mama hajui na bahati mbaya wakati anakufa nilikuwa mbali lakini kuna mengi mazito alitaka kunipa juu ya familia yetu.”
“Monika alikuambia nini?”
“Alinieleza jinsi kidonda chake kilivyoanza kama muwasho na mwisho kilikuwa kidonda kisichouma zaidi ya kutoka maji na kukatazwa asiyafute.”
“Mmh, pamoja na uongo wake nakuomba usimuamini ni mfitini yule.”
“Baba unataka kunihakikishia kidonda hiki sio kama cha dada Monika?”
“Nimekueleza usimfuate Monika ni muongo.”
“Kama muongo naomba na mimi uniondolee masharti ya kuwa na mke.”
“Masalu, umri wako bado.”
“Baba mimi si mdogo, ukweli ni kwamba huu muwasho mwisho wake ni kidonda ambacho kitaingiza pesa kwa njia ya kumwagika maji. Baada ya dada Monika kuyashindwa masharti yako uliamua kumuua na mimi nahofia utaniua.”
“Narudia tena kukueleza Monika ni muongo.”
“Baba nasema kama ndicho kidonda hiki basi nami nitakufa kama dada Monika.”
“Masalu kuna sababu ya kuzungumza kwa kituo.”
“Sawa baba lakini kaa ukijua kama muwasho huu mwisho wake ni kidonda cha utajiri sikitaki nakuomba unirudishe shuleni.”
“Nikurudishe shuleni fedha za shule utazipata wapi?”
“Kwani lazima nipate kidonda ili nisome?”
“Utasoma, lakini kumbuka fedha zinatafutwa na njia zake pesa zipo nyingi.”
“Moja wapo ni kidonda changu?”
“Masalu tutazungumza, hebu vaa kuna mali mpya nimeituma dukani mwako twende ukaiangalie.”
ITAENDELEASIKU YAKESHOOOOOOOOOOO

LULU: BONGO MOVIES ISHABUMA

$
0
0

STAA wa filamu mwenye makeke mengi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kwa mtazamo wake anaona Bongo Movies imebuma hivyo ameamua kukomaa na shule ili awe na kitu kingine tofauti na sanaa.
 Staa wa filamu mwenye makeke mengi, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Lulu alisema kuwa kwa sasa yuko Chuo cha Uhazili Magogoni, Posta jijini Dar akichukua ‘course’ ya Utawala wa Umma (Public Administration) kwa ajili ya kupata ujuzi mwingine kichwani.
“Mwe-nzangu naona Bongo Movies kunaelekea kubaya, bora hata nikomae na shule angalau hata niwe na kitu kingine kichwani nipate mbadala wa sanaa,” alisema Lulu.

MSHANGAO MISS TANZANIA 2014

$
0
0

Mshtuko! Siku chache baada ya kutwaa Taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu ameibua mshangao wa aina yake kutokana na utata wa umri wake, Ijumaa limesheheni data.
 
Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akionesha cheti mara baada ya kuhitimu masomo.
Utata huo uliibuka saa chache mara baada ya shindano hilo kufanyika Oktoba 10, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo wadau mbalimbali walianza kuhoji.
UTATA WENYEWE HUU HAPA
Mara baada ya mrembo kutangazwa mshindi, habari za chini kwa chini zilidai kwamba Sitti alijinasibu kuwa ana umri wa miaka 18 na elimu ya (digrii mbili) (masters), mambo ambayo yaliwashtua wengi na kuanza kuhoji uhalali wa umri huo ukilinganisha na kiwango chake cha elimu.
“Mh! Haiwezekani, kama ana miaka kumi na nane atakuwa alianza darasa la kwanza akiwa na miaka miwili?” Alihoji mdau mmoja ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini.
 
Mrembo, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akipozi.
ELIMU YA BONGO IKOJE?
Kwa mfumo wa elimu nchini ulivyo, mtoto huanza darasa la kwanza akiwa na kati ya miaka mitano hadi saba, jambo ambalo haliingii akilini kwa Sitti kwani hesabu zinakataa hata kwa mtu asiyesomea mahesabu.
Ukiachilia mbali shule ya awali (nursery) ambayo huchukua kati ya miaka miwili hadi mitatu, ukihesabu miaka saba ya elimu ya msingi (primary), miaka minne ya sekondari (ordinary level), miaka miwili ya kidato cha tano na sita (advanced level) na miaka mitatu ya shahada kwanza (bachelor degree), jumla ni miaka 16.
 
Mlimbwende, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu.
Pia kuna madai kwamba ametumia mwaka mmoja kusomea shahada ya pili (masters) huku kukiwa na muda ambao kwa kawaida huwa unapotea baada ya kumaliza kidato cha nne kwenda cha tano na baada ya kumaliza kidato cha sita kwenda chuo kikuu.
INA MAANA ALIANZA DARASA LA KWANZA AKIWA NA MIAKA MIWILI?
Kwa mantiki hiyo, kama kweli Sitti ana umri wa miaka 18, basi atakuwa alianza darasa la kwanza akiwa na miaka miwili, jambo ambalo ni msamiati mpya kwa jamii ya Kibongo.
 
Mrembo, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akifurahia jambo na marafiki zake wa mamtoni.
BABA MZAZI ANASEMAJE?
Ili kuondoa utata na tafrani inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii hadi kufikia hatua ya watu kutukanana, gazeti hili lilimtafuta baba mzazi wa Sitti ambaye ni Mbunge wa Temeke, Dar kwa leseni ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Abbas Zuberi Mtemvu alipopatikana alifunguka:
“Umri wake ni kama alivyosema mwenyewe siku ile (miaka 18), kama mnataka kujiridhisha nendeni hata huko Miss Tanzania mtaoneshwa passport (hati ya kusafiria) yake…,” alisema mzazi huyo huku akiomba aachwe kwanza ashughulikie wananchi wa jimboni kwake.
 
Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akiwa na baba yake, Mhe. Abbas Zuberi Mtemvu.
TUMUAMINI MZAZI?
Hata kama tukiamini maelezo ya mzazi, maana yake ni kwamba mrembo huyo alianza darasa la kwanza akiwa na miaka miwili, jambo ambalo linazidi kuongeza utata katika sakata hilo.
AKATAA KUHITIMU MASTERS
Alipobanwa zaidi kuhusu taarifa zinazosema kuwa mwanaye amehitimu masters, mzazi huyo alikanusha na kudai kwamba mwanaye amehitimu bachelor degree (shahada).
“Kuhusu masters mnakosea, mwanangu hana masters, ana bachelor, nilimshauri achukue masters lakini akaomba nimuache ashiriki kwanza mashindano ya u-miss ndiyo aje aendelee baadaye,” alisema mheshimiwa huyo.
 
Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu wakati wa kutwaa taji
NI AIBU NYINGINE KWA LUNDENGA?
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, suala la warembo kudanganya umri limekuwa ni sugu hivyo kuleta tafsiri ya aibu kwa muandaaji wa mshindano hayo, Hashim Lundenga akidaiwa kupigwa changa la macho pindi anapowapokea katika mchakato wa awali.
 
Pasipoti ya kusafiria ya Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu.
“Hii ni aibu nyingine kwa Lundenga kwani haiwezekani mtu akaingia akasema ana miaka kumi na nane halafu awe na elimu kama hiyo, anashindwaje kulibaini hilo mapema?” Alihoji mdau mkubwa wa urembo nchini akikumbushia kisa cha Wema Isaac Sepetu, Miss Tanzania 2006/07 ambaye naye alidanganya umri akasema ana miaka 18 wakati alikuwa na kumi na saba.
 
Leseni ya udereva ya Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu.
MSIKIE LUNDENGA SASA
Alipotafutwa Lundenga ili kuzungumzia suala hilo, alijibu kwa kifupi na kukata simu:
“I can’t answer that question (Siwezi kujibu swali hilo)…siwezi.”
SITTI ANASTAHILI KUWA NA UMRI GANI?
Ukiachilia mbali muonekano, baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa ukifuata utaratibu wa mfumo wa elimu Bongo, Sitti alipaswa angalau awe na umri wa miaka 23, hata kama madai ya kurushwa madarasa ni sahihi.
 
Muandaaji wa mshindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga akifafanua jambo
Yaani angeanza darasa la kwanza akiwa na miaka saba, angesoma shule ya msingi kwa miaka saba, sekondari miaka minne, kidato cha tano na sita miaka miwili na chuo miaka mitatu, jumla angekuwa na umri wa miaka 23 kwa sasa ambayo ni pungufu ya miaka 25 iliyotajwa kwenye wasifu wake mtandaoni huko nchini Marekani. 
SITTI AMEFIKAJE HAPA?
Data zinaonesha kwamba, baada ya kumaliza kidato cha sita, Sitti alihamia jijini Dalas kwenye Jimbo la Texas, Marekani ambapo mbali na kusomea elimu ya chuo kikuu nchini humo, amewahi kuigiza filamu inayojulikana kwa jina la Lost In Abroad.
CREDIT:GPL

RAYUU: ‘WOLPER APIME UKIMWI’

$
0
0

 Msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’.
MSANII wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amemtaka msanii mwenzake, Jacqueline Wolper apime Ukimwi kama alivyofanya yeye.

Akipiga stori na paparazi wetu, Rayuu alisema anamheshimu Wolper na kamwe hawezi kumsema vibaya lakini alishangaa kuambiwa na mashosti wake kwamba anamsema yeye ana Ukimwi.
“Nilishangaa sana kwa kweli hilo jambo liliniumiza roho na linaniuma mpaka kesho, eti anawaambia watu mimi ni muathirika, lini alinipima au ana uthibitisho gani na hilo,” alisema Rayuu na kuongeza:
“Kutokana na kunikosesha raha kwa kiasi kikubwa kwa jambo hilo, niliangua kilio nikaamua kwenda kupima na kuyaanika majibu yangu kwenye Istagram ili aumbuke kwa kuwa nipo safi, kama na yeye anaweza, akapime tuone majibu yake.”
 
Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper.
Kutokana na mtafaruku huo, mapaparazi wetu walifanya juhudi za kumsaka Wolper pasipo kuzaa matunda, ambapo simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na hata pale alipotumiwa ujumbe mfupi wenye mlolongo mzima wa ishu hiyo, hakujibu.

LADY JAYDEE AVUNJA MKATABA NA GARDNER

$
0
0

HABARI mpya kutoka kwa mastaa wanaodaiwa kuvunjika kwa ndoa yao, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ na Gardner G. Habash ‘Kaptaini’, inasemekana wamevunja mkataba wa kuendesha Mgahawa wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar.
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, wawili hao walidaiwa kufikia uamuzi wa kuvunja mkataba baada ya kuona ndoa yao inasuasua kutokana na migogoro.“Lady Jaydee au Jide alipoona mambo yanakwenda ndivyosivyo alimshauri Gardner wavunje mkataba wa Nyumbani Lounge ili kila mmoja awe na businesses (biashara) zake.
“Walimfuata mmiliki wa jengo, wakamwambia kwamba wanavunja, akawakubalia,” kilinyetisha chanzo makini.  Chanzo hicho kilizidi kwenda mbali zaidi na kudai kuwa mgahawa huo kwa sasa unamilikiwa na mzungu.
 
‘Lady Jaydee’ na Gardner G. Habash ‘Kaptaini’ wakati wakiwa pamoja.
“Mgahawa kwa sasa unamilikiwa na Mzungu mmoja ambaye amenunua baadhi ya vitendea kazi walivyokuwa wakivitumia na Jaydee amekuwa akimsaidia mzungu huyo baadhi ya mambo kwa kuwa ni mgeni Bongo ila sasa Nyumbani Lounge itafunguliwa kwa jina jipya la M.O.G na Jaydee atafanya shoo ya ufunguzi kama msanii tu,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kushibishwa maelezo hayo, mwanahabari wetu alimtafuta Jide bila mafanikio lakini Gardner alipopatikana, alijibu kwa kifupi.
“Siwezi kuzungumza chochote katika suala hilo.”
Jide na Gardner wanadaiwa kutengana na kila mmoja akiishi kivyake lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha.

MENEJA AIYEYUSHA MIMBA YA SNURA

$
0
0

 Meneja wa Snura, Mohamed Kavu ‘HK’ akiwa naye.
BAADA ya ukimya wa muda mrefu huku ikidaiwa kuwa staa wa Mduara Bongo, Snura Mushi amepachikwa ujauzito, meneja wa msanii huyo, Mohamed Kavu ‘HK’ amezidi kuyeyusha ukweli na kudai msanii wake hana mimba.]

Akizungumza na paparazi wetu mara baada ya uchunguzi makini kufanyika na kubaini staa huyo amehamia kwa mpenzi wake mkoani Mbeya, meneja huyo alikataa katakata kuwepo kwa suala la ujauzito.
“Hana mimba. Yupo Afrika Kusini, anashuti video yake lakini tunatarajia baada ya wiki mbili atakuwa amerudi.”
 
Staa wa Mduara Bongo, Snura Mushi.
Badala ya wiki mbili, paparazi wetu alimpa meneja huyo mwezi mzima lakini hakutokea, alipoulizwa kwa mara nyingine, alisema Snura alitarajiwa kuingia Bongo juzi, Oktoba 16. Tunaendelea kufuatilia.
Kwa muda mrefu Snura amekuwa kimya pasipo kuposti kitu kwenye mitandao ya kijamii wala kufanya shoo ya aina yoyote.

KINACHOWAPONZA WEMA, KAJALA HIKI HAPA!

$
0
0

KAMA walivyo Wema Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel kwa sasa ndivyo walivyokuwa Wema na Kajala Masanja miezi kadhaa iliyopita.Wema na Kajala walikuwa mashosti wa kufa mtu, walishibana na kupeana siri zao zote hususan zile za ndani kabisa.
 
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ .
Kudhihirisha kwamba wameshibana, kuna wakati Wema aliamua kujitolea Sh. Mil 13 kulipa faini ambayo ilimnusuru Kajala kuswekwa gerezani.Baadaye walikuja kutofautiana, kila mtu akaishi kivyake. Yakazungumzwa mengi kuhusu chanzo cha ugomvi wao lakini pointi ya msingi ni kupishana kauli kibinadamu kama watu wengine wanavyoweza kutofautiana na kupatana.
Kwa upande wao suala la kupatana limekuwa zito, ugomvi wao haufiki tamati huku kila kukicha ni malumbano ambayo yanawagawa mashabiki.
 
Mastaa wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel wakipozi.
Tatizo kubwa linalochagiza ugomvi wao ni mitandao ya kijamii, kumezuka makundi ambayo yamekuwa yakitumia utabiri wao wanaoufahamu wenyewe kuzidi kuchochea ugomvi uliokuwepo kati ya mastaa hawa wawili na wengine wakitumia matusi mpaka ya nguoni kutukana wa upande wa Wema na Kajala.
Makundi hayo ndiyo yamekuwa chachu kubwa ya bifu lao na kuzidisha mapambano kati ya mastaa hawa ambao naamini wanapendana sana, sitaki kuamini kabisa kama Wema hampendi Kajala, na sitaamini kama Kajala hampendi Wema.
 
Staa wa filamu Bongo,Kajala Masanja.
Ndiyo maana siku ambayo walipatana na kuzungumza kwa muda nyumbani kwa msanii Aunt Ezekiel, mastaa hao walipata fursa ya kukaa pamoja na kuzungumza  baada ya ugomvi wao kila mmoja alitoa chozi kuonyesha jinsi gani kila mmoja anaumia anapokuwa mbali na mwenzake.
“Mimi nilikuwa napenda sana kukuangalia wewe na siyo timu zinazotuzunguka zinazidi kututia chumvi tugombane, nakupenda na ninajua ni rafiki mwema kwangu lakini unasikiliza sana maneno ya watu,” ni maneno ya Kajala niliyosikia akimwambia Wema.
“Najua hivyo na wewe unafahamu nakupenda sana na ni rafiki ninayefurahi tukiwa pamoja nikiwa nawe siku zote,” alijibu Wema.
 
Mastaa wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’, Aunt Ezekiel na Kajala Masanja katika picha ya pamoja
Maneno hayo waliyoambizana huku kila mmoja akitoa machozi, yalisahaulika kwa siku tatu tu kwani viliibuka vitu ambavyo havikujulikana vilipotokea na kuanzisha ugomvi mwingine mpya na kuwafanya wawili hawa kuvurugana tena kwa kasi mpya na nguvu mpya.
Nathubutu kusema kwamba ugomvi wa mastaa hawa mara nyingi unachagizwa na mitandao ya kijamii. Hizi zinazojiita Team Wema na Team Kajala ndiyo tatizo kubwa.Nasema ni tatizo kwa sababu hata ukiangalia kwa makini, kipindi cha nyuma mastaa hawa walipokuwa wanaanzisha urafiki wao, timu hizo hazikuwepo ndiyo maana waliweza kudumu.
Kwa nini wanakubali kutawaliwa na hizi Team? Kwa nini waruhusu maisha yao ya kila siku yaingiliwe uhuru wao wa kufanya mambo yao? Si sawa!
Mimi naamini kabisa kama mastaa hawa wangekuwa na ugomvi wao bila hizi Team kuingilia kati wangeweza kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao mapema sana lakini tatizo kuna watu wa pembeni wenye kuzoa maneno huku na kupeleka kule.
Kwa jinsi ninavyoona mimi, hizi Team zikiendelea hivi na kwa mastaa wengine, ipo siku watasababisha hata mauaji kwa jambo ambalo halina kichwa wala miguu. Niwasihi Kajala na Wema wasijisahau kuwa wao ni biashara, mashabiki wengi wanapenda kuona kazi zao, wangeweka tofauti zao pembeni wafanye kazi na washirikiane hata kutengeneza filamu ya pamoja.
Naamini wakiweka pembeni hizi Team, wakaacha kusikiliza maneno ya kinafiki yanayoundwa na baadhi ya wasanii wasiopenda urafiki wao, basi wataishi vizuri na watafanya kazi zao pamoja!

SERENGETI FIESTA 2014 YAFUNIKA DAR

$
0
0
Rapa kutoka nchini Marekani, Clifford Harris,'T.I' akitoa burudani kwenye tamasha la Fiesta Leaders Club jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
Nyomi baada ya kukongwa nyoyo na T.I usiku wa kuamkia leo Ledears Club.
Clifford Harris,'T.I' staili yake kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2014 Dar.
Msanii kutoka Nigeria, David Adedeji Adeleke 'Davido' akitoa burudani kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 ndani ya Ledears Club.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma 'Diamond' (kushoto) na Davido wakiimba Remix ya My Number 1 katika serengeti fiesta 2014.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma 'Diamond' akikamua jukwaani.
Msanii wa Bongo Fleva, Linah Sanga akilishambulia jukwaa.
Linah Sanga na wacheza shoo wake wakiendelea kutoa burudani.
Msanii wa Bongo Flava, Shaa akifanya yake.
Shaa akiwapagawisha mashabiki (hawapo pichani).
Waje kutoka NIgeria akifanya yake.
 
Victoria Kimani akiwajibika.
Recho akitumbuiza katika Tamasha la Fiesta.
 Rachel na wakikata mauno na wacheza shoo wake.
Msanii mahiri wa Bongo Flava, Ali Kiba akiwapagawisha wapenzi wa burudani.
Ali Kiba (kulia) akiwa na mdogo wake Ally Kiba pamoja na Abdul Kiba (kushoto).
Staa wa Bongo Fleva, Emanuel Elibariki 'Nay wa Mitego'akitumbuiza katika Tamasha la Fiesta.
Wasanii wa kundi la Weusi Nikki 2 (kulia), Joh Makini (katikati) na G-Nako (kushoto) wakifanya yao.
Msanii wa Bongo Fleva, Mwana FA akifanya yake.
Nyomi baada ya kukongwa nyoyo na burudani za Serengeti Fiesta Leaders Club.
Msanii wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee akifana yake na Ommy Dimpoz.
Madansa wa Vanessa Mdee wakifanya yao.
(PICHA NA MUSA MATEJA, RICHARD BUKOS/GPL)

Akon Alivyofanya Show Congo Ndani Ya Puto Kuhofia Ebola.

$
0
0
Ilikuepuka maambukizi ya ugonjwa wa Ebola akiwa kwenye tamasha kubwa la amani Congo, msanoo Akon kutoka Marekani amefanya show ndani ya Puto gumu la plastic huko Goma.

Kauli mbio ya show hio ilikuwa Umoja ila alichofanya Akon kilikowa tofauti kwani alionekana kujihadhari sana na kuguswa na mtu yeyote kutoka nchi hio akiamini kuna ugonjwa wa Ebola kila kona ya Africa.

 
 
 
 

KUNA MADHARA YA KUISHI PAMOJA KABLA YA KUOANA?-2

$
0
0

Ni wiki nyingine tunapokutana tena katika ukurasa wetu huu mzuri, kubadilishana mawazo kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo uhusiano wa kimapenzi. Mada tuliyokuwa tumeianza wiki iliyopita ilikuwa ikihoji kwamba je, kuna madhara ya kuishi pamoja kabla ya kuoana?
Maoni yamekuwa mengi, kila mmoja anasema lake. Wapo ambao wamekubaliana na mimi kwamba si vizuri kuishi pamoja kabla hamjaoana ingawa wapo wengine ambao wamesema ni sawa kuishi pamoja kabla ya kuoana kwa sababu wao wanaishi hivyo kwa kipindi kirefu.
Mimi si mjuaji wa kila kitu ndiyo maana nikataka tubadilishane mawazo, kila mtu aseme vile anavyojua na mwisho, tuhitimishe kwa pamoja. Nilianza kukueleza kwamba sababu ya kwanza inayofanya kitendo cha kuishi pamoja kabla ya kuoana kisiwe sawa, ni vigumu zaidi kwa watu wanaoishi pamoja kuoana ingawa wapo ambao waliishi pamoja namwisho wakaoana.
Sababu ya pili nilikueleza kwamba kama wewe ni mwanamke, mwanaume wako hataiona thamani yako kwa kuwa umekubali kuishi naye kienyeji bila kufuata utaratibu na sababu ya tatu tuliyoijadili, ni kwamba mume wa kweli hapendi mteremko.
Wanaume wengi ambao wanatafuta wake wa kuishi nao, hawapendi wanawake ambao wanajirahisi au ambao wanawapata bila jasho. Sasa ikiwa wewe mwanamke kabla hata mpenzi wako hajakuchumbia tayari umeshahamishia nguo zako kwake, atajisifia nini mbele za wenzake?
Ataamini wewe ni mwanamke mwepesi ambaye mwanaume yeyote anaweza kukupata kwa urahisi. Muache mumeo mtarajiwa ahangaike kukupata ikiwa ni pamoja na kuja kwa wazazi wako au ndugu zako. 
4. ATAKUOA KWA SABABU YA SHINIKIZO
Ni ukweli usiofichika kwamba watu wanaoishi pamoja, shinikizo kutoka kwa watu wanaowazunguka kuhusu kuoana huwa kubwa sana. Kila siku ndiyo utakuwa wimbo, ‘utanioa lini?’, mwisho ili kukwepa usumbufu, mwanaume huamua kuoa ili tu kumridhisha mwanamke na siyo kwa sababu anampenda. Matokeo yake ni kuingia katika ndoa ambayo haikuwa na ridhaa kutoka pande zote mbili.
5. NI RAHISI KUPEANA TALAKA
Mkianza kuishi kabla ya kuoana, maana yake ni kwamba mtazoeana sana mapema, kila mmoja atayajua mapungufu ya mwenzake na ni hapo ndiyo kukoseana adabu kutakapoanza na mwisho mtaishia kupeana talaka.
NINI CHA KUFANYA?
Ukiwauliza watu wengi wanaoishi pamoja bila ndoa, majibu yao watakwambia bado wanajipanga kwa maana ya kutafuta mahari, kujenga nyumba au kutafuta fedha za harusi. Hata hivyo, kikwazo kikubwa kwa wengi kimeonekana ni suala la mahari na gharama za ndoa.
Kama wewe na mwenzi wako mnapendana kwa dhati, mambo haya hayatakiwi kuwazuia kuoana. Mnaweza kuamua kupanga kufunga ndoa yenye sherehe ndogo ambayo haitawagharimu fedha nyingi. Hata suala la mahari, mnaweza pia kuzungumza na wazazi wa pande zote mbili ikawa inalipwa kwa awamu.
Hakuna suala linaloleta heshima kwenye jamii kama kufunga ndoa halali. Si hivyo tu, hata mbele za Mungu, watu wanaosihi bila ndoa maana yake wanazini na kuvunja amri ambazo zimewekwa na Mungu. Kwa nini uishi kwenye dhambi? Chukua hatua sasa, andaeni mipango mfunge ndoa.

DK. CHENI: RUSHWA YA NGONO WANAITAKA WENYEWE!

$
0
0
KASHFA! Staa wa filamu za Kibongo, Muhsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ amekanusha tabia ya wasanii wakubwa kuwaomba rushwa ya ngono wasanii chipukizi na kudai wanaziendekeza wao wenyewe.

Staa wa filamu za Kibongo, Muhsein Awadhi ‘Dk. Cheni’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Dk. Cheni alisema yeye hajawahi kumuomba msanii rushwa ya ngono, isipokuwa anaamini walio wengi huanzisha mahusiano yaliyo rasmi kwa makubaliano yao kutokana na hisia zinavyowasukuma.

“Sizani kama ni rushwa ya ngono, naamini wengi wanakubaliana, sehemu ya watu wengi mnapokutana inatokea watu kupendana na kuwa wapenzi hilo nakubali sababu ni jambo la kawaida hata wasanii kwa wasanii kupendana, sidhani kama mtu anaweza kulazimishwa kufanya mapenzi ili acheze filamu, mpaka watu kufanya tendo hilo wameshakubaliana,” alisema Dk. Cheni.

AUNTY LULU AMPA SOMO JOHARI LA MAPENZI

$
0
0

 Staa wa Bongo Movies, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.
SOMO! Staa wa Bongo Movies, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ ameibuka na kumtaka msanii mwenzake, Blandina Chagula ‘Johari’ kukubaliana na matokeo ya aliyekuwa mpenzi wake Vincent Kigos ‘Ray’ kwamba kwa sasa ana uhusiano na mtu mwingine.

Akistorisha na paparazi wetu, Aunty Lulu alimtaka Johari kukubaliana na matokeo na aige mfano wake kwani aliachana na Bond Bin Sinan ambaye kwa sasa ana mpenzi mwingine hivyo asimchukie Chuchu Hans anayetoka na Ray kwa sasa kwani kuachana ni jambo la kawaida katika mapenzi hivyo hatakiwi kuwa na kinyongo.
 
Msanii Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’.
“Mimi nimepitia kwenye maisha hayo ndiyo maana namshauri Johari akubaliane na matokeo kwamba Ray kwa sasa yupo na Chuchu Hans na asiwe na kinyongo naye ampende na aongee naye vizuri tu kwani ndiyo maisha,” alisema Aunty Lulu.

FLORA, H-BABA WAMFUNIKA WEMA KWA MJENGO

$
0
0

HESHIMA! Wanandoa, muigizaji Flora Mvungi ‘H.Mama’ na mwanamuziki Hamis Ramadhan ‘H.Baba’ wamemfunika mwigizaji Wema Sepetu kwa kupanga ghorofa.
 
Mjengo wa wanandoa, muigizaji Flora Mvungi ‘H.Mama’ na mwanamuziki Hamis Ramadhan ‘H.Baba’
Akizungumzia mjengo huo walioupanga maeneo ya Mbezi-Jogoo, jijini Dar, H. Mama alisema yeye na mume wake wameamua kupanga nyumba hiyo si kwa sababu ya kumfunika mtu bali wanapenda kuwa huru na kuishi vizuri.
 
Flora Mvungi ‘H.Mama’ akiwa ndani ya mjengo hup na familia yake.
“Hatushindani na mtu katika maisha yetu bali cha msingi tunaangalia nafsi zetu zinataka nini, kuhusu gharama yake, niache kidogo,” alisema Flora.Wema amepanga nyumba ya kawaida maeneo ya Kijitonyama jijini Dar.

LINAH, MCHUMBA’KE WATIBUANA!

$
0
0

MCHELE ulionyooka! Staa wa Bongo Fleva, mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Estelina Sanga ‘Linah’ na mchumba’ke, Nangari Kombo wanadaiwa kutibuana, kisa kikidaiwa ni maneno ya wanafiki yasiyokuwa na ukweli.
 
Staa wa Bongo Fleva, mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Estelina Sanga ‘Linah’
Habari za chini ya kapeti zilinyetisha kwamba mtiti kati ya wawili hao ulijiri juzikati baada ya Kombo kudaiwa kuanza kumtuhumu Linah kuwa anapokuwa kwenye ziara za matamasha kama Fiesta huwa anamsaliti na wanaume wengine.
 
Lina akiwa na mpenzi wake, Nangari Kombo.
Chanzo hicho kilidai kwamba, kufuatia madai hayo Kombo alimuanzishia Linah bonge la tafrani na kujikuta kila mmoja anachukua hamsini zake.
Linah alipoulizwa kuhusu ishu hiyo alisema: “Ni kweli kulitokea kutoelewana but (lakini) tumeyamaliza, tupo vizuri sana.”

FIESTA 2014: KAMA NOMA NA IWE NOMA!, CLOUDS WAMPANDISHA DAVIDO

$
0
0

Stori:  Waandishi Wetu
Kama noma na iwe noma! Tamasha la Serengeti Fiesta 2014, wikiendi iliyopita lilifunga mitaa ya Jiji la Dar na viunga vyake ambapo burudani ya kufa mtu ilidondoshwa kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar na kugubikwa na matukio kibao nyuma ya pazia, likiwemo la msanii kutoka Nigeria, Davido ‘kupafomu’ pamoja na serikali kumkataza, Ijumaa Wikienda lina ripoti kamili.

Nyomi ya watu ikiwa imefurika Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar kumshuhudia T.I katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014
SHUGHULI YAANZA
Shughuli ilianza kwa madansa ‘kusheki’ ambapo Kundi la Makomando ndilo lililoanzisha makamuzi na kupokea shangwe kubwa.
Baada ya Makomando, Wanaume TMK wakiongozwa na Chegge na Temba ndiyo waliofuatia, wakapiga shoo hevi na kupokea shangwe kubwa.
 
Madee na Dogo Janja walipafomu pamoja baada ya kitambo kirefu tangu walipogombana,
Vanessa Mdee akafuatia na kunogesha na madansa wake kwa zogoazogoa, akaja Ommy Dimpoz ambaye naye alikamua kisawasawa bonge la shoo.
Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akitumbuiza kwa staili yake kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2014 Dar Leaders.
SAPRAIZI YA DIMPOZ
Kwa mara ya kwanza, Ommy Dimpoz alitambulisha remix ya wimbo wake wa Tupogo kwa mahadhi ya mnanda au mchiriku ambapo yeye na madansa wake waliserebuka kinoma wakishirikiana na Msaga Sumu.
YOUNG KILLER, BANANA ZORRO NAO JUKWAANI
Baada ya hapo, mtu mzima Banana Zorro alivamia jukwaa akiwa na Young Killer na Umebadilika ambapo nao walipokelewa vizuri na nyomi iliyokuwa imefunga uwanjani kabla ya Young Killer kubaki mwenyewe na kukisanua ileile.
Msanii Wajekutoka Nigeria akitoa shoo.
MSANII KUTOKA DUBAI MH!
Msanii wa kwanza mgeni kupanda stejini alikuwa Ash Hamman kutoka Dubai ambaye ngoma zake hazikuwa zikijulikana kiivyo.
ZAMU YA WAJE KUTOKA NIGERIA
Msanii wa pili mgeni alikuwa ni Waje kutoka Nigeria ambaye alianza kwa kufundishwa kutamka maneno ya Kiswahili yakiwemo ‘nipeleke nyumbani’ ambaye kimavazi aliacha maswali kwa kuvaa kisweta cha aina.
Msanii huyo alimpagawisha Madam Rita na kujikuta akishindwa kujizuia, akaserebuka na kinywaji chake mkononi.
Msanii kutoka, Kenya Victoria Kimani akipagawisha mashabiki jukwaani.
VICTORIA KIMANI
Msanii wa tatu kutoka nje alikuwa ni Victoria Kimani wa Kenya ambaye aligonga ngoma zake mbili lakini kilichoonekana ni kwamba zilikuwa hazijulikani na wengi pamoja na kwamba alipata shangwe kimtindo.
Mwingine wa kimataifa alikuwa ni Bob Man wa Nigeria ambaye alipagawisha kwa reggae baada ya kupiga akapela ya Wimbo wa One Love wa Bob Marley huku akichombeza na maneno ya Kiswahili kama ‘mambo vipi’ na ‘nakupenda’. Alipojaribu kuwasifia warembo wa Kibongo, masela wakamaindi kidizaini fulani.
Bob Man aliendelea kufanya yake akisaidiwa na Victoria Kimani, wakakamua Prokoto ambapo Dimpoz aliungana nao, shangwe zikazidi kupamba moto.
Burudani ilizidi kukolea, akapanda mtangazaji na msanii wa Bongo Fleva, Adam Mchomvu ambaye alikamua kwa sana.
Msanii zao la THT, Rachel akikamua stejini na mashabiki zake
RACHEL, WACHEZA SHOO WAKE WAVAMIA JUKWAA
Msanii zao la THT, Rachel naye alipanda jukwaani na mashabiki wake sita waliokuwa wamevalia nguo zinazofanana, wakakamua ngoma yake ya Nashukuru Umerudi, na nyingine kibao lakini mashabiki walipooza kimtindo kwani nyimbo zake zilikuwa na mzuka wa chini, ikafuatia ngoma nyingine ya Umependeza, mashabiki kwa mbali wakaanza kuamka.
BARNABA NA SHAA NAO WAPANDA JUKWAANI
Msanii mwingine, Barnaba Elias ‘Barnaba Boy’ naye alifuatia na ngoma yake mpya ya Wahalade, nyomi ikaamka na shangwe zikaanza kuonekana kutoka kila upande, akafuatia Shaa ambaye alitoa kali baada ya kutaka aitwe Mrs MJ (Master Jay).
Msanii Shaa akiendelea na makamuzi ndani ya Viwanja vya Leaders Kinondoni.
Ikafuatia burudani ya nguvu kutoka kwake ambapo alikamua Wimbo wa Lover Lover, ukaamsha popo, ukafuatia Promise, mashabiki wakazidi kuchangamka huku wacheza shoo wa msanii huyo nao wakizikonga nyoyo za mashabiki.Akaendeleza makamuzi, akafanya Remix ya Hoi iliyowakumbusha watu mbali, akamalizia na Sugua Gaga iliyobamba vibaya.
NYANDU TOZ, BLU NOMA SANA
Msanii Nyandu Toz naye alifuatia jukwaani akipigwa tafu na Blu na memba wengine wa Micharazo, wakapata shangwe ya kufa mtu. Blu akabaki peke yake jukwaani, akakamua kinoma. Baada yake, walipanda jukwaani Yamoto Band, watu wakachangamkia makamuzi yao ile mbaya.
Msanii wa kitambo Mwana FA akikamua ngoma zake kali stejini.
MWANA FA ADHIHIRISHA UKONGWE WAKE
Mwana FA naye alipanda kwa staili ya kipekee, ngoma zake mpya na za kitambo zikawabamba mashabiki ile mbaya.
Mtangazaji Godwin Gondwe aliushtua umati uliokuwepo uwanjani hapo ambapo alisikika akitangaza taarifa ya habari ya dharura (breaking news), watu wakakaa mkao wa kusikia kilichojiri, kumbe anampandisha Stamina, akakamua kinoma na kupishana na Nay.
DIAMOND, ALI KIBA KAMA SIMBA NA YANGA
Muda uliwadia ambapo watangazaji mayanki wa Clouds FM, Hamis Mandi ‘B12’ na Dj Fetty walipanda jukwaani na kuanza kuwauliza mashabiki nani mkali kati ya Diamond na Ali Kiba, watu wote wakajibu: Kibaa! Kibaa!
Mkali wa ngoma ya Mwana, Ali Kiba na Mdogo wake Abdu Kiba wakikonga nyoyo za mashabiki stejini.
Wakauliza tena nani mkali kati ya Simba na Yanga, kila mmoja akatoa jibu lake.
ALI KIBA KWA STEJI
Mkali wa ngoma ya Mwana, Ali Kiba alipanda jukwaani, akapokelewa na shangwe la kufa mtu ambapo kwa upande wa mastaa, Rose Ndauka, Dida, Jack Pentzel na mumewe walimshangilia Ali Kiba kinoma, Halima Kimwana na Aunt Ezekiel wao walikuwa tofauti kabisa na Ali Kiba, walikuwa wakimsubiri Diamond.
Ali Kiba alifanya makubwa jukwaani, katikati kiliingia kibwagizo ambapo kiti cha kifalme kilifutwa vumbi, Ali Kiba akakikalia na kuvalishwa taji la ufalme, maneno ya The Return of The King yakakisindikiza kibwagizo hicho, ikafuatia ngoma ya Mwana iliyomaliza ubishi, mpaka anashuka jukwaani, bado mashabiki walionekana kuwa na kiu kubwa.
Kundi la weusi likiwakilisha.
LINAH, WEUSI NI SHEEDAH!
Baada ya hapo, msanii zao la nyumba ya vipaji Tanzania, Esterlina Sanga ‘Linah’ aliyekuwa ametinga kivazi ‘chenye hoja’ alipanda jukwaani, akafunika mbaya na ngoma zake kali ikiwemo Ole Themba, wacheza shoo wake kibao wakakamua ile mbaya kitamaduni na kuchangamsha shoo nzima. Walifuatia Weusi waliopanda na sapraizi ya kupanda jukwaani kwa msanii Lord Eyez, makamuzi ya kigumu yakaendelea ambapo wakali kibao wakiongozwa na Joh Makini walifanya yao, uwanja wote ukalipuka kwa shangwe ya nguvu kwa muda mrefu.
Diamond Platinumz na Davido wakionyesha umahiri jukwaani.
DIAMOND AAAH WAPI!
Ilifuatia zamu ya mkali wa ngoma ya Mdogomdogo, Diamond Platinumz ambapo mashabiki wake walitangulia, akafuatia Diamond ambapo aliimba Remix ya Uswazi Take Away na Chegge, kombati zikazagaa jukwaani hata alipopanda Nay wa Mitego kumsindikiza kwenye ngoma ya Muziki Gani. Hata hivyo, shangwe hazikuwa kiivyo kama kwa Ali Kiba, akaendelea kukamua ngoma kibao lakini cha ajabu wakati akiendelea na shoo, zilianza kusikika kelele za kumtaja Ali Kiba, mpaka mchizi anamaliza, zomeazomea zilikuwa zikisikika chini kwa chini.
DAVIDO KAMA NONA NA IWE NOMA!
Licha ya mahakama kumzuia Davido kufanya shoo kutokana na matatizo ya kimkataba, waandaaji wa shoo hiyo, Clouds Media Group walimpandisha kuashiria kama noma na iwe noma na kuifanya serikali iduwae, harufu ya vita kati ya waandaaji na serikali ikaanza kunukia. Jina la Davido lilipotangazwa, tofauti na wasanii wengine, ilimchukua zaidi ya dakika nne kupanda jukwaani, akaibuka na kuanza makamuzi.
Hata hivyo, bado hakupata shangwe za nguvu kama ilivyotegemewa, akaimba nyimbo ambazo hazijulikani na wengi.
Mkali T.I, rapa kutoka nchini Marekani akifunga Shoo kwa makamuzi makali hadi naiti kali.
'Hata alipopanda Diamond kukamua naye Number One Remix, mambo yalikuwa ni yaleyale, hakukuwa na shangwe kama ilivyotegemewa. Kwa mbali watu walionekana kuamka alipokamua Skelewu na kumalizia na Aye.
T.I JUKWAANI
Mkali T.I, rapa kutoka nchini Marekani aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu, alidondoka jukwaani na kukamua ngoma zake kibao pamoja na zile alizoshirikishwa, amshaamsha zikatawala mwanzo mwisho na kuhitimisha msimu wa burudani wa Serengeti Fiesta 2014. Ilikuwa ni sheeeda!
Imeandaliwa na Erick Evarist, Andrew Carlos, Musa Mateja, Richard Bukos, Nicolaus Trac na Chande Abdallah.

KADINDA AMFUATA JACK PATRICK GEREZANI

$
0
0

 Martin Kadinda wakati  akiwa na Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’.
Imekaa poa sana! Ubuyu kutoka Hong Kong, China unadai kwamba mbunifu wa mavazi Bongo, Martin Kadinda hivi karibuni alimfuata Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ gerezani aliyefungwa nchini humo kwa msala wa kukamatwa na madawa ya kulevya.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Kadinda ambaye ni meneja wa Wema Isaac Sepetu zilidai kwamba katika safari yake nchini humo, alifuatana na Wema na Petit Man.
Mbunifu wa mavazi Bongo, Martin Kadinda akipozi.
“Kadinda amepongezwa sana kwa hatua yake hiyo, kuhusu kama alionana naye au alichoongea naye, tusubiri arudi maana bado yupo China,” alisema rafiki wa mmiliki huyo wa lebo za mavazi za Single Button na Kwachukwachu.

ALICHOKIFANYA MBOWE! HAA! ..JIONEE MENYEWE

$
0
0
Stori: Mwandishi Wetu
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani (Bungeni), Freeman Mbowe, wiki iliyopita alipamba vilivyo mitandao ya kijamii, haikuwa kwa sababu ya tishio la maandamano kuhusu Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wala Katiba Mpya, ‘topiki’ ilikaa kimapenzi zaidi. 
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani (Bungeni), Freeman Mbowe akimkumbatia mkewe, Dk. Lillian Mbowe.
Watu aah! Mheshimiwa Mbowe, ooh hivi, mara vile! Tathmini ya gazeti hili inaonesha kuwa asilimia kubwa wanampongeza mbunge huyo wa Hai (Chadema), kwamba ni mume mzuri na baba bora wa familia yake.
Hujanyaka topiki? Wiki iliyopita katika mitandao zilienea picha za Mbowe akiwa kwenye sherehe ya kifamilia, iliyofanyika Oktoba 12, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Kivukoni, Serena Hotel, Dar es Salaam,  huku zikimuonesha anambusu mkewe, Dk. Lillian Mbowe kwa hisia kali za malovee.
KWA NINI PONGEZI?
Uchunguzi wa gazeti hili katika mitandao ya kijamii kupitia ‘komenti’ mbalimbali pamoja na maoni ya watu kadhaa waliohojiwa mitaani na mwandishi wetu, picha hizo zinampambanua Mbowe kama kiongozi wa kisasa ambaye anajua jinsi ya kuwajibika kifamilia.
Watoa maoni wengi, wamemfananisha Mbowe na Rais wa Marekani, Barack Obama kwamba ni mfano wa kuigwa katika viongozi wanaojali familia.“Obama kwa mkewe Michelle na wanaye Sasha na Malia, ni wazi yeye ni baba bora wa familia. Kamanda Mbowe amedhihirisha kuwa siasa hazimuweki mbali mpaka akasahau familia, nimependa sana picha hizi za Mbowe na familia yake,” alisema Julie Macklin wa Sinza, Dar es Salaam. 
Mh. Freeman Mbowe akishoo love kwa mkewe.
Pingu Mabula katika ukurasa wake wa Facebook, aliandika: “Nimefurahishwa sana na hii picha (inayomuonesha akimkisi mkewe, huku watoto wao watatu wakiwa wanawatazama kwa tabasamu), natamani viongozi wote wawe na mahaba ya kuridhisha kwa familia zao kama hivi.”
Mwanahawa Red-guard, aliweka picha kama ambayo Pingu aliitundika Facebook kisha akasindikiza kwa maneno: “Njia ya muongo ni fupi sana, kuna waliokuwa wanadai kamanda Mbowe na mkewe hawaelewani, mara picha haziendi, hii ni kuonesha jinsi ambavyo mtu mzima alivyotulia na mkewe.
“Unakuwa na mkeo lakini hutaki kumuonesha upendo, watoto hawaoni upendo wa wazazi wao mpaka nao wanaathirika kisaikolojia, lakini picha hii ni wazi Mbowe anajenga kitu upendo ndani ya familia, wazazi wanapendana, watoto pia watapendana tu, vilevile wakiwa na familia zao watazijenga kwa upendo pia.”
PICHA PENDWA
Pamoja na ukweli kwamba picha za Mbowe akimbusu mkewe ni nyingi lakini moja iliyovutia wengi ni ile ambayo mwenyekiti huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anambusu mkewe, huku watoto wao ‘firstborn’ Dudley, Nicole na Denis wakiwatazama kwa tabasamu.

Mh. Freeman Mbowe akimbusu mkewe huku watoto wakitabasamu
Uchunguzi umeonesha kuwa picha hiyo ndiyo iliyoongoza kwa ‘kupostiwa’ katika Mitandao ya  Kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram na mingine, huku blogu kadhaa zikiifanya habari, vilevile ikitumwa sana katika makundi ya WhatsApp.
MCHUNGAJI HARRIS KAPIGA APONGEZA
Mchungaji wa Kanisa la Nchi ya Ahadi ambaye pia ni mhamasishaji wa masuala ya kiuchumi na familia, Harris Kapiga, aliipongeza picha hiyo na akasema hashangai kwa nini inapendwa sana na watu kutokana na ujumbe inaofikisha.
Kapiga alisema: “Ni picha bora sana kwa familia. Ipo hivi, wewe baba ukitaka uwape zawadi bora kabisa watoto wako basi mpende mama yao. Ndiyo maana katika picha hiyo watoto wanatabasamu, ni zawadi kubwa sana ambayo Mbowe amewapa kwa kuonesha jinsi anavyompenda mama yao.
“Kingine ni kwamba mwanaume amepewa mamlaka, inapotokea mume anambusu mkewe hadharani kama Mbowe alivyofanya, inaonesha jinsi ambavyo upendo wake kwa mkewe hauna shaka. Ni upendo wa dhati kabisa.
“Tafiti zinaonesha pia kuwa familia nyingi za wanasiasa huchukia siasa kwa sababu ya kukosa uwepo wa baba kwa muda mwingi. Vivyo hivyo kwa madaktari, wachungaji na kadhalika, huchukia huduma za baba zao lakini Mbowe ameonesha kuwa kiongozi mkubwa wa kisiasa hakuzuii kuwajibika ipasavyo ndani ya familia.”
 
Baba na Mh. Freeman Mbowe akiwa na familia yake.
MWANASAIKOLOJIA CHRIS MAUKI ANENA
Mtaalamu wa Saikolojia na Uhusiano ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Chris Mauki, alisema kuwa picha za Mbowe akimbusu mkewe hadharani zimemuongezea thamani kijamii kwa sababu watu wanawapenda wanaume wanaobeba majukumu ya kifamilia.
“Unadhani kwa nini Obama ni kiongozi mashuhuri sana duniani na anapendwa sana na watu, ni kwa sababu ya ile tabia yake ya kuwa karibu na familia yake. Kuna watu wanampenda Obama si kwa sababu ya nguvu kubwa aliyonayo kisiasa, ni kwa sababu anajipambanua kuwa baba bora wa familia.
“Jamii kubwa sasa inakosa upendo wa wazi kutoka kwa akina baba. Akina baba wengi wanaona kumbusu mkewe hadharani na kuwa karibu na familia siyo suala lenye maana kubwa, kwa hiyo wale ambao wanayafanya hayo waziwazi huonekana mashujaa.
“Mbowe anapongezwa kwa sababu ni shujaa kwenye jamii kwa sababu alichokifanya wengi hawakifanyi. Familia nyingi zinakosa upendo na kufanya mpaka watoto kuathirika kisaokolojia, watoto wanaharibika,” alisema Dk. Mauki na kuendelea:
“Viongozi wa kisiasa wanapokuwa wanajali familia zao, inatia hamasa kubwa. Hata kama nyumbani hawajibiki vizuri kifamilia lakini kwenye jamii anapokuwa muwajibikaji na watu wanamuona, huvutia wengi na kupendwa sana.”
KAMANDA MBOWE AFAFANUA
Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema kuwa picha hizo zilipigwa siku ambayo kwa hakika alikuwa mwenye furaha sana kutokana na mambo mawili yaliyogusa familia yake.
“Kwanza mke wangu alikuwa anatimiza umri wa miaka 50 ya kuzaliwa, vilevile firstborn wetu Dudley alikuwa amemaliza shahada yake ya kwanza Chuo Kikuu cha Sussex, Uingereza, kwa mambo hayo mawili, tuliona ipo haja ya kufanya sherehe, ukizingatia watoto wetu wengine wawili Nicole na Denis walikuwa wamerejea nchini kwa sababu nao wanasoma nje ya nchi.
“Siku hiyo ya tukio ilikuwa Jumapili, tulianza kwa kwenda kanisani Azania Front tukatoa sadaka, baada ya hapo tulikwenda Serena Hotel kwenye Ukumbi wa Kivukoni ambako chakula cha mchana kilikuwa kimeandaliwa, tukajumuika na ndugu wengine pamoja na marafiki.
“Haikuwa sherehe tu kusema labda nilikurupuka kumbusu mke wangu, ilikuwa sherehe ya kifamilia, kumpongeza mke wangu na mtoto wetu,” alisema Mbowe.
CHANZO NI GAZETI LA UWAZI LA LEO
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>