Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

TAIFA STARS, YAPEWA BENIN IPASHE MISULI MOTO DAR OKTOBA 12

$
0
0

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inashuka uwanjani Oktoba 12 mwaka huu kuikabili Benin katika mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Programu ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa ajili ya mechi hiyo itatangazwa baadaye na Kocha Mkuu Mart Nooij.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaendelea na taratibu nyingine kwa ajili ya mechi hiyo ikiwemo usafiri wa Benin kuja nchini, ambapo timu hiyo inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Oktoba 10 mwaka huu ikiwa na msafara wa watu 28.
Pambano la Stars na Benin litatanguliwa na mechi ya kudumisha upendo kati ya viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu.
Wakati huo huo, kutokana na mechi hiyo ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inafanyiwa marekebisho madogo, na marekebisho hayo yatatangazwa kesho (Septemba 26 mwaka huu).

ZIARA YA WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA VITUO VYA UMEME VYA MBAGALA,G/MBOTO NA KINYEREZI

$
0
0

 Waandishi wakiwasili kituo cha kupoza umeme Mbagala wakipokewa na Meneja Miradi Mhandisi Emmanuel Marirabona,(wa tatu kushoto) wakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba,(kushoto) na Meneja Miradi-Ufuaji Umeme, Mhandisi Simon Jilima,(wa pili kushoto). 
 Transfoma ya kuchuja nguvu za umeme iliyopo Mbagala.
 Wafanyakazi wakiendelea na kazi katika kituo cha Mbagala.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco,Felchesmi Mramba,(kulia) na Meneja Miradi Emmanuel Marirabona.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Assah Mwambene (kulia) akizungumza na waandishi zamira ya kutembelea vituo vya kuzalisha Umeme Jijini Dar es Salaam akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco,felchesmi Mramba.
 Waandishi wakiwa katika kituo cha Umeme Gongolamboto.
 Transfoma ya inayowekwa Gongolamboto.
 Mashine ikisafisha mafuta ya transfoma yaliyopo katika mapipa.
 Mafuta ya transfoma
 Waandishi wakiwa kituo cha Kinyerezi.
 Maofisa habari wa Tanesco.Neema Mbuja (wa pili kushoto) na Khadija Ahamed (kulia).
 Waandishi wakioneshwa eneo la Kinyerezi.
 Jengo la Utawala likiendelea kujengwa kituo cha Kinyerezi.
 Waandishi wakipewa maelezo na Meneja Miradi -ufuaji umeme,mhandisi Simon Jilima (katikati)
 tenki litakalowekwa maji ya kuzimia moto endapo utaleta taabu Kinyerezi.
Transfoma kubwa iliyopo kituo cha Kinyerezi.

KWIZERA, KIONGERA WAPATIWA VIBALI VYA KUPIGA KAZI SIMBA SC, CHA OKWI CHADUNDA…SABABU HAIJULIKANI

$
0
0
  Pierre Kwizera atapiga kazi kama kawaida Simba SC baada ya kupatiwa kibali.
 
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAMIDARA ya Uhamiaji Tanzania imetoa vibali vya kufanyia kazi kwa wachezaji wawili wa Simba SC, Mrundi Pierre Kwizera na Mkenya Paul Kiongera pamoja na kocha wao, Patrick Phiri, lakini haijatoa kibali cha mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba wamefanikiwa kupata vibali vya wachezaji hao na kocha Phiri, lakini pamoja na kupeleka pia maombi kwa ajili ya kibali cha Okwi, hakijatoka. 
“Bado hatujajua sababu za kutotoka kwa kibali cha Okwi, lakini tunaendelea kufuatilia ili tujue, kwa sababu huyu ni mchezaji wetu halali, ambaye tulikamilisha taratibu za kumsajili baada ya mkataba wake na klabu yake ya awali, Yanga SC kuvunjika,”amesema Poppe.
Mapema jana, Idara ya Uhamiaji iliwazuia wanne hao kufanya kazi Simba SC hadi hapo watakapopatiwa vibali- lakini sasa wanaweza kuendelea na kazi, kasoro Okwi ambaye kibali chake kimekwama. 
Simba SC inashuka dimbani Jumamosi hii kumenyana na Polisi Morogoro katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na maana yake iko hatarini kumkosa Okwi. 
Okwi anaweza kukosekana katika wakati ambao Simba SC inamkosa mshambuliaji mwingine, Kiongera ambaye ni majeruhi anayetakiwa kuwa nje kwa wiki sita. 
Simba SC pia itawakosa kipa Ivo Mapunda, beki Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ na winga Haroun Chanongo ambao wote ni majeruhi, lakini habari njema tu ni kwamba kiungo ‘mchapakazi’ Jonas Mkude yuko tayari kuanza kazi Jumamosi. 
Mapunda ni majeruhi wa muda mrefu kama Kiongera, ambaye anatakiwa kuwa nje kwa wiki nane, wakati Issa na Chanongo wiki ijayo wanaweza kurudi kazini.Haijulikani ‘zengwe’ la Okwi litachukua muda gani kumalizika kabla ya mchezaji huyo kurejea uwanjani. 
Simba SC ilianza Ligi Kuu kwa sare ya 2-2 na Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Taifa, Jumapili iliyopita licha ya kuongoza kwa 2-0 hadi mapumziko- maana yake itahitaji ushindi Jumamosi ili kujiweka mguu sawa katika mbio za kuwania ubingwa.

MSIBA WAZIMA MBWEMBWE ZA AUNT MAREKANI

$
0
0

Staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amelazimika kusitisha bata alizokuwa akila nchini Marekani baada ya kupata msiba wa mdogo wake aliyefariki dunia juzikati.
Staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel akiwa mamtoni.
Chanzo chetu makini kilieleza kuwa, Aunt alipata taarifa za mdogo wake huyo (si wa damu) aliyekuwa akiishi naye aitwaye Ziada kufariki dunia akiwa mamtoni hivyo ikamlazimu kurudi Bongo ili kushiriki kwenye mazishi.

Ijumaa lilipata bahati ya kuwasiliana na Aunt ambaye alisema ameshitushwa na taarifa hizo na alikuwa njiani kurejea Dar.“Nimeumia sana, Ziada alikuwa ni mdogo wangu tuliyependana sana lakini Mungu kamuita, hakuna jinsi,” alisema Aunt kwa masikitiko.
CREDIT: IJUMAA

MADEE ALIVYOSOTESHWA POLISI

$
0
0
 
Na Waandishi Wetu
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva a.k.a Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ hivi karibuni alilala katika Kituo cha Polisi cha Kigamboni, Dar  akihusishwa na utekaji wa dereva wa bodaboda, Suedi Waziri (pichani) kisha kumpa kipigo ambapo inadaiwa alisoteshwa kinomanoma.
 
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva a.k.a Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ akiwa mikononi mwa Polisi
Baada ya tukio hilo lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, Ijumaa lilinasa picha zinazomuonyesha msanii huyo akihenyeshwa kituoni hapo huku mmoja wa watu wanaoishi karibu na eneo hilo akinyetisha kuwa, licha ya ustaa wake Madee alikiona cha mtemakuni.
 
Dereva wa bodaboda, Suedi Waziri aliyetekwa na kushambuliwa na Madee.
“Mimi nilikuwepo pale kituoni, nilimshuhudia akiwa amepigwa pingu huku polisi kama sita hivi, mmoja akiwa na silaha wakiwa wamemuweka chini ya ulinzi wakimpeleka mahakamani.“Alionekana aliyechoka sana huku akiwa na hofu ila inavyodaiwa baadhi ya watu wake wa karibu walikuwa wakihaha kumnusuru baada ya kulala selo,”  kilidai chanzo hicho.
 
Majeraha ya mguuni aliyopata Suedi Waziri baada ya kushambuliwa na Madee.
Kufuatia msala huo, msanii huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kigamboni na baadaye kuwekewa dhamana na baba yake ambapo kesi yake itatajwa tena Oktoba 6, mwaka huu.
Madee anadaiwa kumteka Suedi na kwenda kumsulubu nyumbani kwake Manzese baada ya kijana aliyekuwa amepakia kwenye bodaboda yake kukwapua simu ya msanii huyo na kukimbia.
Katika kushinikiza simu yake irudishwe ndipo Madee alipomtaiti Suedi na mwisho wa siku akaishia mikononi mwa polisi kwa kufunguliwa kesi iliyosomeka: VJB/RB/625/2014 KUTEKWA KWA BINADAMUImeandikwa na Mayasa Mariwata, Shani Ramadhani na Rhoda Josiah.
CREDIT: GLOBAL PUBLISHERS

WAMBURA AWATAJA WALIOSABABISHA MECHI YA YANGA, SIMBA KUSOGEZWA

$
0
0

Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura amewataka wapenda soka kuvuta subira hadi kesho ili kujua mechi ya watani iliyoondolewa Oktoba 12 itachezwa lini.

Lakini akasema hakuna chochote kilichosababisha zaidi ya uamuzi wa Benin kutaka kucheza Oktoba 12.
 
"Tulikuwa tunapambana kupata mechi, Benin waliona siku hiyo ndiyo wana nafasi.
"Ukizingatia imo ndani ya kalenda ya Fifa, sasa nafikiri hakuna kosa lolote," alisema Wambura.
 
"Watu wavute subira, tutawatangazia Leo lini mechi hiyo itachezwa. Usiku wa kuamkia leo walikutana na bodi ya ligi kulijadili suala hilo."
 
Mashabiki wamekuwa wakilalamika kwamba kusogezwa kwa mechi hiyo kunaashiria kubebwa kwa Simba iliyokuwa ina wachezaji wengi majeruhi.

MBINU 10 ZA KUFUFUA PENZI LILILOKUFA -2

$
0
0

Namshukuru Mungu kwa kuniweka hai mpaka leo tunapokutana tena katika busati letu la mahaba, kuendelea kujadiliana kuhusu mada tuliyoianza wiki iliyopita ya mbinu za kufufua penzi lililokufa. 
Kabla hatujaendelea, tujikumbushe kwa kifupi tulichojadiliana wiki iliyopita. Nilikufafanulia tafsiri ya penzi lililokufa ni ile hali ya kuishi na mpenzi wako ambaye mlipendana sana mwanzoni lakini sasa kila kitu kimebadilika.

Hampendani tena, ukuta mrefu wa chuki umejengeka kati yenu kiasi kwamba hamfurahii tena kuwa pamoja, kila mmoja anatamani uhusiano ufike mwisho aendelee na maisha yake.

Tulizichambua mbinu kadhaa zinazoweza kurudisha uhai kwenye penzi lililokufa zikiwemo kujiwekea nadhiri kutoka ndani ya moyo wako kwamba upo tayari kulifufua penzi lako lililokufa, kutafakari chanzo cha matatizo yenu na kukubali kuwajibika.

Pia tulijadili mbinu nyingine kuwa ni kumsamehe bure kabla hata hajakuomba msamaha, na kumsaidia kazi ndogondogo za nyumbani na tukamalizia kidogo kwa kuangalia mbinu ya sita ambayo ni kurejesha mawasiliano. Leo tunaendelea na mbinu nyingine zilizosalia zinazoweza kukusaidia kurejesha uhai kwenye penzi lako.

7. Rejesha mapenzi kwake
Yawezekana ikawa vigumu kwako kuanza kumpenda tena baada ya kuishi kwenye migogoro kwa kipindi kirefu lakini kama kweli unataka kufufua penzi, anza kumuonesha kwamba unampenda.


Kama unapata wakati mgumu kurudisha mapenzi, jaribu kujenga taswira kichwani mwako kwamba umekutana na mpenzi mpya na ndiyo mnaanzisha uhusiano wa mapenzi.

Kuna usemi wa Kizungu usemao: Love conquers all (Mapenzi yanashinda nguvu vitu vyote). Ukimuonesha mapenzi, migogoro, chuki na uhasama vitayeyuka vyenyewe taratibu kwa sababu penzi la kweli lina nguvu sana.

8. Uaminifu asilimia 100
Kama awali ulikuwa na tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani bila sababu za msingi, badilisha ratiba zako. Kama ulikuwa unaweka password kwenye simu yako, itoe na mruhusu kushika simu yako kwa uhuru. Usiende kupokelea simu nje au pembeni, kuwa muwazi kwake kadiri uwezavyo.


Kama ulikuwa na ‘michepuko’, achana nayo kabisa na elekeza nguvu zote kwa mpenzi wako. Taratibu utaona anaanza kukuamini tena na endeleza uaminifu kadiri uwezavyo. Utaugusa moyo wake na penzi lake kwako litaanza kuchanua upya.

9. Mkumbushe maisha yenu wakati wa furaha.
Mnaweza kutazama picha zenu za harusi mkiwa pamoja au mlizopiga kipindi cha mwanzo cha uhusiano wenu. Utazirudisha kumbukumbu zake nyuma na atakumbuka matukio ya furaha zaidi kuliko maudhi.

Unaweza pia kumfanyia mambo mliyokuwa mkiyafanya pamoja kipindi mlipokuwa na furaha kama kutazama sinema nzuri pamoja, kusikiliza muziki anaoupenda au kumtoa ‘out’ kwenye mazingira mliyokuwa mkienda kipindi mapenzi yenu yalipokuwa motomoto.10. Mfanyie mambo mazuri
Jitahidi kadiri ya uwezo wako kufanya mambo yatakayokuwa yanamfurahisha. Mnunulie zawadi, hata kama ni ndogo zitaufurahisha moyo wake. Mwambie maneno mazuri ambayo pengine ulishaacha kumwambia kwa kipindi kirefu.


Msifie kama yeye ni mrembo au hendisamu, mueleze kuwa hujawahi kupenda kama unavyompenda yeye na mchombeze kwa maneno mazuri kila mara unapokuwa karibu naye. Rudisha upendo kwa ndugu zake, marafiki zake na watu wake wa karibu.

Jitahidi kutafuta muda wa kutosha wa kukaa naye kila siku, hata kama ubize wa kazi unakuelemea, tenga muda kwa ajili ya kuwa naye, kula naye chakula cha jioni, kutoka ‘out’ pamoja na kwenda kwenye matembezi mkiwa pamoja huku muda mwingi ukijitahidi kuwa na tabasamu usoni mwako.

Uzuri wa mbinu hizi, ukizifanyia kazi kwa ukamilifu, matokeo yake yanaonekana haraka kuliko unavyotegemea. Kama huamini, anza leo na zingatia mbinu zote kisha utaona matokeo mwenyewe. Utakuwa umefanikiwa kurejesha furaha kwenye penzi lenu na atakupenda zaidi kuliko hata ilivyokuwa mwanzo. Cha msingi ni kujizuia kurudia maudhi mara kwa mara.

BILIONEA AMPANGISHIA LULU JUMBA LA KIFAHARI

$
0
0
 
Stori: Hamida Hassan, Gladness Mallya na Musa Mateja.
Madai mazito ya kushtua mtaani yanasema kwamba staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, mambo yake kwa sasa yapo juu ya mstari baada ya bilionea kutoka jijini Arusha (jina tunalihifadhi kwa sasa) kudaiwa kujitosa kumlea akianza kwa kumpangishia jumba kubwa la kifahari.
 
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, akiwa na begi la fedha.
TWENDENI USHUANI
Habari hizo za mitaani zilidai kwamba bilionea huyo amempangishia Lulu mjengo huo wa maana uliopo ushuani maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Kimuonekano, nyumba hiyo iliyoshuhudiwa na wanahabari wetu mwanzoni mwa wiki hii haina tofauti na ile mijengo iliyozoeleka ya mastaa wakubwa wa Marekani kwa maana ya kujitosheleza kwa kila kitu ndani yake.
Kwanza ni nyumba yenye fensi kubwa na kuingia getini lazima ujieleze ‘vizuri’ na ukiingia huufikii mlango wa nyumba kwani kuna ‘kamwendo’.
Nje ya nyumba hiyo kuna ‘parking’ ya magari madogo zaidi ya kumi huku chini kukiwa na tarazo na pembeni kuna bustani nzuri iliyopandwa maua ya kuvutia.“Amehamia hivi karibuni, anaonekana muda wa kutoka na kuingia tu.
Nyumba anayoishi staa huyo.
“Lulu ni binti mrembo mwenye mvuto wake, ukizingatia ana nyota pia ya kupendwa, kwa hiyo siyo mtu wa kukaa uswazi,” alidai mtoa habari wetu na kuongeza:
“Bidada kaula maana nasikia jamaa ameahidi kumpa matunzo ya nguvu.
“Alianza kwa kumnunulia lile gari la kifahari la Toyota Rav4 New Model analotembelea Lulu, sasa naona kamuweka pazuri na kweli nyumba inaendana na hadhi yake.
ADAIWA KUMPA JEURI YA KUWAFUNIKA KAJALA, WEMA
“Nasikia jamaa amempa jeuri ya kuwafunika kabisa Kajala (Masanja) na Wema (Sepetu) ambao inasemekana wana mkwanja wa kumwagamwaga ovyo.”
LULU LAIVU!
Kupitia Kipindi cha Nirvana kinachorushwa na EATV, Lulu alionekana ndani ya mjengo huo uliojaa mazagazaga ya thamani.Mjengo huo una makabati makubwa ya nguo na viatu kiasi kwamba mtu unaweza ukahisi umeingia kwenye duka la nguo (boutique) na viatu kibao.
Akizungumza kwa kujiamini Lulu alisema kuwa anapenda vitu vizuri hasa linapokuja suala la kupiga pamba ndiyo maana amejaza pamba kali kwenye makabati.“Kimsingi sipendi shida, napenda kuvaa vizuri, kula vizuri, kulala pazuri na mambo yote mazurimazuri,” alisema Lulu.
Elizabeth Michael ‘Lulu’,akiwa kwenye pozi.
BILIONEA GANI?
Ili kupata undani wa mwanaume huyo, gazeti hili lilichimba ambapo kwa mujibu watu wa karibu na Lulu, jamaa huyo ni mfanyabishara mkubwa wa madini jijini Arusha.
“Kama mtakumbuka, huyo jamaa aliwahi kuwagombanisha Lulu na Husna (Maulid) kwani mwanzoni alikuwa mwanaume wa Husna.“Hivi unajua kabla ya ishu hiyo, Lulu na Husna walikuwa mashosti lakini baadaye wakawa kama paka na panya kisa tu ni huyo bilionea,” kilidai chanzo hicho.
LULU ASAKWA
Baada ya kunyetishiwa habari hiyo ya mtaani, gazeti hili lilimsaka Lulu hadi nyumbani kwake na lilipomkosa lilimtafuta kwa njia ya simu na alipopatikana alifunguka:
“Kiukweli kabisa nyumba ninayoishi sasa mimi na familia yangu siyo kwamba nimepangishiwa wala kununuliwa na sijui bilionea au kigogo yeyote, hayo ni maneno ya watu tu. Unajua watu wanaongea sana, wanadhani mimi siwezi kujimudu,” alisema Lulu kwa kujiamini.
 Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS


AMANDA AZUA BALAA MTAANI

$
0
0

Msanii wa filamu, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni alizua balaa la aina yake baada ya kukatiza mtaani akiwa amevaa kigauni kilichokaribia kuacha wazi makalio yake.
 
Msanii wa filamu, Tamrina Posh ‘Amanda’ akiwacharukia wanaume waliokuwa wanampigia miluzi huku wakimzodoa.
Tukio hilo lililowashangaza wengi lilijiri eneo la Mwenge Bamaga jijini Dar wakati msanii huyo alipokuwa akitembea kuelekea kwenye mgahawa uliopo eneo hilo.
Huku akitembea kwa staili ya ‘hamsini…mia…hamsini…mia…’, Amanda alionekana kufanya makusudi kwani kadiri wanaume walivyokuwa wakijikusanya kumshangaa, ndivyo alivyoongeza mikogo na kuwaacha miudenda ikiwatoka.
 
‘Amanda’ akiingia kwenye gari kuondoka 
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wanaume ambao wengi wao ni madereva wa Bajaj na mafundi gereji walionekana kumzodoa huku wakieleza kuwa, ni msanii asiyejiheshimu.
“Yule kutuvalia sisi vile ndiyo nini? Mavazi yale yanavaliwa klabu usiku tena wanaovaa vile ni wale wasioithamini miili yao, tukisema anatutangazia biashara tutakuwa tunakosea?” alihoji fundi mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma.
 
Tamrina Posh ‘Amanda’ akipozi.
Katika kujua sababu ya kuvaa kigauni hicho, mwandishi wetu alimfuata Amanda lakini kabla ya kuulizwa chochote aliingia kwenye gari na kuondoka zake baada ya kuwachimba mkwara waliokuwa wakimpigia miluzi. Baadaye alipopigiwa, simu iliita bila kupokelewa.

PICHA ZA BOB JONIOR AKIWA GLOBAL TV ONLINE JIONI

$
0
0


 Msanii wa muziki na producer, Bob Junior akifanya mahojiano na Global TV Online jioni hii.
 Msanii wa muziki na producer, Bob Junior akifanya mahojiano na Global TV Online jioni hii.

 Bob Junior akiwa katika pozi 'bab kubwa'.
 Mtangazaji wa Global TV Online na msanii wa Bongo Fleva, Pamela Daffa (kushoto) akiwa Bob Junior.
 
Bob Junior akifafanua yake.
Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist (kushoto) wakipozi na Bob Junior

 Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul (kushoto), wakipozi na Bob Junior.

(PICHA NA JONATHAN KITUNDU/GLOBAL TV ONLINE)

UNANG’ANG’ANIA KUPENDA USIPOPENDEKA ILI IWEJE?

$
0
0
Bila shaka wasomaji wa safu hii mko vizuri na mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Kwa upande wangu mimi ni mzima wa afya.Ni siku nyingine Mungu ametujalia uzima tunakutana kupeana mawili matatu yahusuyo maisha ya uhusiano.
Mapenzi yana nafasi kubwa katika maisha ya wanadamu, mapenzi ni hisia kali zilizoko ndani ya miili yetu ndiyo maana inatokea mtu anampenda mtu kiasi cha kutaka hata dunia nzima ijue kama amependa.
Uzuri wa mapenzi ni kupendana, kila mmoja ampende mwenzake. Ikitokea mmoja amempenda mwenzake halafu huyo anayependwa haoneshi ushirikiano hapo ndipo kunapokuwa na tatizo.
Anayependa anafanya jitihada za nguvu kuhakikisha somo lake linaeleweka lakini wapi, jibu linakuwa ni ‘no’. Jibu linakuwa hilo kwa sababu unayempenda yeye hakupendi.
Nimekuwa nikipata maswali mengi katika safu ya ushauri, wengi wanang’ang’ania kupenda mahali ambapo kimsingi hapapendeki. Yule anayependwa, moyo wake unakuwa hautaki tu kuridhia. Upendo haupo kwake, kuna aina ya mtu ambaye yeye anampenda na si wewe.
Kwa kuwa mapenzi ni hisia, mtu anakuwa mgumu kukubaliana na matokeo. Anang’ang’aniza penzi kwa nguvu zote. Anakuwa tayari kuligharamia penzi hilo kwa namna yoyote. Akili inamtuma kwamba ipo siku atamuelewa na moyo wake upate pumziko.
Akili yake hapo haiwazi kabisa kwamba kuna mtu unaweza ukampenda na yeye asikupende. Anasahau kabisa ule msemo wa ndege mzuri  hutua katika mti aupendao. Hawazi kwamba sifa alizoziona kwa huyo anayempenda naye ana sifa zake kwa mtu anayempenda.
Kabla hatujaendelea, ngoja nikupe mfano hai. Kuna mtu tumpe jina la A (jina lake halisi lipo). A yeye ameteseka kwa muda mrefu kumpenda mtu ambaye hampendi, amefanya jitihada nyingi kuhakikisha anampata binti mmoja lakini wapi. Majibu anayopewa ni zaidi ya kuudhi lakini eti akawa hakati tamaa.

Anasema amemweleza binti huyo kwamba anampenda, amewatuma marafiki zake, ametuma zawadi mbalimbali kama maua, vocha na nyinginezo lakini vyote hivyo vilikuwa ni kazi bure.
Mtoto wa kike haoni wala hasikii, hataki tu! Alionyesha msimamo wa hali ya juu. Hakutaka kugeuka nyuma. Sasa je, kupitia mfano huo tunajifunza nini?
Binti alifanya vile kwa sababu moyo wake haupo pale. Kama ingekuwa ni tamaa basi pengine angekubali mapema kutokana na mbinu mbalimbali ambazo A alizitumia. Ndugu zangu, penzi halilazimishwi maana ukilazimisha athari zake ni kubwa huko mbele ya safari.
Mbaya zaidi, uking’ang’ania sana, anaweza kukubalia leo kwa kuwa umemwonyesha fedha au zawadi mbalimbali, kesho zinaweza kuwa hazipo, hawezi kuona umuhimu wako tena. Wapo watu wa aina hiyo, wanaweza kukuvumilia kwa muda mrefu wakachoka na kwa kuona unazo, wanaamua kukubali ili wakutumie.
Watu wa namna hiyo ndiyo wale wanaosema: “acha nimlie maana kila unavyomueleza hakuelewi. Mwanaume king’ang’anizi huyu.” Atakula, atatumia fedha zako lakini akili na mawazo yake yanakuwa kwa mtu mwingine tofauti ampendaye.
Atakuficha juu ya mpenzi wake, atakuongopea na kukurubuni kwa maneno ya wizi ili aweze kukuibia vizuri kumbe akili yake haipo kwako. Utamsindikiza katika safari yake ya kuelekea kwenye ndoa huku wewe ukiamini ndiyo mume wako, kisha anakuacha solemba.
Watu wa namna hiyo ni hatari. Wanakuua huku unajiona. Tena wengine wanakuchekea kabisa machoni kumbe akili zao hazipo kabisa. Hatoangalia ameishi na wewe muda gani zaidi ya kuufuata moyo wake unapopenda. Utajuta!
Wakati anataka kuchukua maamuzi magumu, hatoangalia umedumu naye miaka kumi au kumi na tano. Siku moja tu anaamka na kukwambia hakutaki, hakutaki kwa sababu hakupendi.
Itaendelea wiki ijayo.
 Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

BABY MADAHA ATAMANI PENZI LA WEMA, DIAMOND

$
0
0

MWANAMUZIKI mwenye vituko kila kukicha Bongo,  Baby Joseph Madaha, ametoa dukuduku lake la moyoni na kusema kuwa kila kukicha anayatamani mapenzi ya Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ kama angekuwa yeye.

Mwanamuziki mwenye vituko kila kukicha Bongo,  Baby Joseph Madaha akipozi.
Akizungumza na paparazi wetu, Baby alisema kuwa kila akiwaona Wema na Diamond anatamani sana na yeye awe kwenye uhusiano wenye kupendwa na kuhamasisha kama ulivyokuwa wa mastaa hao kiasi ambacho amefikia hatua ya kuwaonea wivu.

“Kiukweli nikiwaona hawa watu nasikia mpaka wivu na kuna wakati natamani niwe mimi jamani maana sifikiri kama kuna ‘kapo’ kali hapa Bongo kama hii jamani, naitamani hadi basi,” alisema Baby.
 Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

MAMA KANUMBA AFICHUA MAZITO YA RAY, MWANAYE

$
0
0
Stori: Mwandishi WetuBAADA ya hivi karibuni siri kufichuka kwamba Kundi la Bongo Movie linateswa na laana ya marehemu Steven Kanumba, mama yake Flora Mtegoa ameibuka na kueleza mazito yakiwemo ya aliyekuwa rafiki wa mwanaye, Vincent Kigos ‘Ray’, Risasi Jumamosi linakupa mchapo.
 
Mama yake marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
Akizungumza kwa hisia kali Mama Kanumba alisema anaungana na katibu msaidizi wa klabu hiyo, Devotha Mbaga kwamba kundi hilo lina laana ya Kanumba kwani naye kama mzazi ni shahidi kutokana na mwanaye kila wakati alikuwa akimfuata nyumbani akilia na kusema kwamba hawatakaa waelewane milele.
“Kanumba alikufa akiwa ameshajitoa Bongo Movie kutokana na majungu waliyokuwa wakimwandama kila kukicha na maneno yake ya siku chache kabla hajaaga dunia alikuwa akisema kwamba kundi hilo halitakaa lielewane milele kwa kuwa walikuwa wakimchukia na kumsemea majungu bila sababu hali iliyokuwa ikimsababisha kulia na kulalama kila wakati.

Aliyekuwa rafiki wa Kanumba, Vincent Kigos ‘Ray’.
“Alisema ukweli ni kwamba kundi hilo linakosa kuwa na maendeleo kwa sababu wanaendekeza majungu hivyo akaniambia mama nimejitoa huko japokuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi yaani sitaki tena,” alisema Mama Kanumba.
Mama Kanumba alidai sababu ya ugomvi wa Ray na Kanumba ulitokana na kugombanishwa na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ingawa siku chache kabla ya kifo cha Kanumba, familia zote mbili zilikaa na kusuluhisha ikawa imebaki kupeana mikono lakini Mungu hakupenda iwe hivyo, akamchukua Kanumba.
“Siwezi kusahau aliyewagombanisha Kanumba na rafiki yake wa damu Ray ni Steve Nyerere lakini tulikaa kama familia na Sikukuu ya Pasaka ndiyo Ray na Kanumba walikuwa wapeane mikono na kumaliza tofauti zao lakini Mungu akamchukua kabla ya siku hiyo kufika,” alisema Mama Kanumba.
 
Marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake.
Alipotafutwa Steve Nyerere kuhusiana kuhusishwa katika ugomvi wa Ray na Kanumba, alifunguka:
“Mama anatapatapa, Ray mtu mzima mimi nitamgombanisha na Kanumba kwa lipi? Siyo kweli. Mbona mimi sikuwa na tatizo lolote kati yao, Kanumba hadi anafariki tulikuwa vizuri, kabla  hajafa alinipigia simu twende Mashujaa (bendi). Ningekuwa mimi ni tatizo tungeelewana? Halafu kwanza kwa nini hayo maneno yaibuke sasa? Nashindwa kumuelewa huyo mama.” 
CHANZO: GPL

KIVAZI CHA JOKATE MH! JIONEE NA WEWE

$
0
0

 Mwanamitindo na mtangazaji mahiri Bongo, Jokate Mwegelo.
MWANAMITINDO na mtangazaji mahiri Bongo, Jokate Mwegelo amezua utata baada ya kupiga picha akiwa ametinga suruali iliyochanika.

Akizungumzia picha hiyo ambayo imevuja katika baadhi ya mitandao, Jokate alisema alivalia mavazi hayo hivi karibuni Afrika Kusini alipokuwa amekwenda kurekodi wimbo wake mpya (hakuutaja jina) na alivaa makusudi ili kuonesha utofauti.
 
Jokate Mwegelo akipozi na mzungu.
“Nimeamua tu kuwa tofauti maana hata watu wengi walikuwa wakijiuliza kulikoni mimi kuvaa hivyo  lakini mimi nafikiri lazima kuna wakati tunatakiwa kuonekana tofauti na siyo mapambo muda wote ukibadilika hata unachofanya unakuwa tofauti,” alisema Jokate.

AUNTY LULU NIMETENDWA VYA KUTOSHA

$
0
0



MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amefunguka kuwa ametendwa vya kutosha na marafiki hivyo kwa sasa hahitaji tena kuwa na rafiki.
 
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’
Akipiga stori na mwandishi wetu, Aunty Lulu alisema kwa nyakati tofauti marafiki wamemponza akaachika kwenye uhusiano wa wapenzi wake, kumgombanisha na watu anaofanya nao kazi na mambo mengi yanayofanana na hayo hivyo kwa sasa hahitaji marafiki.
 
‘Aunty Lulu’ akipozi.
“Nimetendwa sana na marafiki, bora niachane nao niishi kivyanguvyangu, nijitafutie maisha yangu mwenyewe. Sihitaji kabisa marafiki kwa sasa,” alisema Aunty Lulu.

MCHUNGAJI ASHTUA KUMUOA DOGODOGO!

$
0
0

Stori: Haruni SanchawaMCHUNGAJI Peter Rashid Abubakari wa Kanisa la RGC lililoko Mbezi ya Shamba jijini Dar, amedaiwa kuoa mke wa pili aitwaye Pamela Didas Asenga akiwa na umri wa miaka 20 tu ‘dogodogo’, Risasi Jumamosi limetonywa.
 
Mchungaji Peter Rashid Abubakari wa Kanisa la RGC akimuoa 'dogodogo', Pamela Didas.
Kwa mujibu wa chanzo, ndoa hiyo ilifungishwa na Askofu Innocent Lugagi wa Kanisa la White House la Durban, Afrika Kusini, Agosti 29, mwaka huu.
Mke mwingine wa mtumishi huyo wa Mungu anaitwa Zuwena (Catherine) aliyemuoa mwaka 1985. Lakini kuna madai kwamba, mke huyo amemwacha.
 
Mchungaji Peter Rashid Abubakari akipiga picha na mke mpya wakati wa harusi.
Chanzo chetu ndani ya kanisa hilo kilidai kwamba, mchungaji huyo aliwaambia waumini wake aliamua kumuoa Pamela kwa vile ndoa yake ya mwanzo aliifunga akiwa  Muislam na alifungishwa na shehe (hakumtaja jina).
“Alituambia Mungu amemfunulia na amempa mke mwingine mwema ambaye ni binti mbichi, watu wewee,” kilisema chanzo.
 
Mchungaji Peter Rashid Abubakari akiwa mke mpya.
Habari zaidi zinasema kuwa, mchungaji huyo baada ya kutua nchini, Jumapili moja akiwa kanisani kwake aliwatangazia waumini wake, hasa wanaume kwamba kama wana wake ambao walichukuana wakati wa ‘ujinga’ na wamekaa nao kwa miaka mitatu au zaidi na hawana tabia ya Kimungu, mkorofi na mchokozi na hawajafunga nao ndoa, wawaache ili Mungu awape wake wema.
Sasa baada ya picha za mtumishi huyo kusambaa hadi kwenye mitandao, Risasi Jumamosi, juzi lilifika kanisani kwake Mbezi ili kuzungumza naye lakini hakuwepo.
 
Mchungaji Peter Rashid Abubakari akiongoza maombi kanisani.
Baadhi ya waumini walioweza kuzungumza na Risasi Jumamosi walionesha kushtushwa na kitendo cha mchungaji wao kumuoa Pamela lakini hawakuwa tayari kusema neno!
Baadaye mwandishi wetu alimtafuta mchungaji huyo kwa njia ya simu ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Nipo Kiluvya kikazi lakini hilo lipo ila ni jambo langu binafsi siyo la kulitangaza.”
Baadaye alimtumia ujumbe  mwandishi akiwa ameuandika hivi:
“Sanchawa mimi ni Nabii wa Mungu Yehova, uliponipigia tu kila kitu Mungu akaniambia nia yako na kusudi lako.” 
 
Mchungaji Peter Rashid Abubakari.
Pia Risasi Jumamosi lilizungumza na baadhi ya wachungaji wa makanisa ya kiroho Tanzania ili kuwasikia wanasemaje kuhusu kitendo cha mtumishi huyo kufunga ndoa nyingine.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao magazetini, baadhi ya wachungaji hao walimpongeza Mchungaji Peter kwamba, aliona alikokuwa na anakokwenda ndiyo maana aliamua kuchukua uamuzi huo.
 Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS

TENGENEZA WEBSITE, BLOG YENYE MUONEKANO WA KUVUTIA

EVELYN BAASA NDIYE REDD’S MISS TANZANIA PHOTOGENIC 2014

$
0
0

Miss Tanzania Photogenic 2014, Evelyn Baasa.
 
Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora yaRedd’s Miss Tanzania Photogenic 2014, wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi   wa taji hilo, Evelyn Baasa (katiakti) jana. Wengine kutoka kushoto ni Nicole  Sarakikya, Lilian Kamazima, Lilian Timothy na Dorice Mollel.
 
Warembo wakilisakata rumba kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo.
 
Baadhi ya warembo wakipiga picha ya pamoja na mshindi huyo wa Taji la Miss Tanzania Photogenic 2014
MlimbwendeEvelyn Baasa (19) jana aliibuka kidedea kati ya walimbwende wenzake 30 na  kutwaa taji la Redds Miss Photogenic 2014.
Kwa kushinda taji hilo Baasa ambaye alinzania mbio za taji la Miss Tanzania katika Kitongoji cha Karatu naabadae kuingia Miss Arusha na Kanda ya Kaskazini amekuwa   mrembo wa kwanza kuingia Nusu Fainali ya mashindano Miss Tanzania 2014.
Shindano hilo ni moja kati ya mataji matano ambayo yanashindaniwa na warembo hao ambapo  washindi wake wanapata tiketi ya kuingia Nusu Fainali ya shindano hilo litakalo  fanyika mapema mwezi ujao. 
Miongoni mwa mataji hayo ni Miss Tanzania Photogenic, Miss Tanzania Top Model, Miss   Tanzania Personality, Miss Tanzania Sports Lady na Miss Tanzania Talent.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa Shindano la Miss   Tanzania, Hashim Lundenga ‘Uncle’ amesema jopo la majaji watatu ambao ni wapiga  picha na wadau wa masuala ya urembo  wa masuala ya urembo Tanzania walikaa na kumchagua mshindi huyo kupitia picha mbalimbali za warembo hao.
Majaji  waliowezesha kupatikana kwa mshindi huyo ni Mpigapicha mkongwe wa masuala ya urembo nchini Mroki Mroki ambaye anafanyakazi na Magazeti ya Serikali ya Daily News na Habarileo, Mtayarishaji wa vipindi Elliud Pemba wa True Vision na Afisa Itifaki Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Mukhsin Kassim.
Taji la Redd’s Miss Tanzania Photogenic lilikuwa linashikiliwa na Redd’s Miss Tanzania  2013 Happyness Watimanywa.Warembo wengine waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Miss Photogenic ni Dorice Mollel, Nicole Sarakikya, Lilian Timothy na Lilian Kamazima.
Kesho warembo hao watachuana tena kuwania taji la Miss Top Model katika shindano litakalofanyika Triple A jijini Arusha.

MAYWEATHER AONYESHA JEURI YA FEDHA, AJAZA MANOTI KITANDANI

$
0
0

Kweli jamaa ana fedha ya hatari, bondia ambaye hajawahi kupigwa hata pambano moja, Floyd Mayweather ametupia mtandaoni picha akiwa na mamilioni ya fedha.

Mayweather amefanya hivyo akiwa na noti lundo za dola ya Marekani, halafu yeye akionekana hana habari.
Picha hiyo iko kwenye akaunti yake ya Instagram ambako SALEHJEMBE imeinasa.
Mwenyewe ameonekana akiendelea na mambo yake, kama hakuna lolote.
Mayweather ,37, alichoka mkwanja wa dola milioni 32 baada ya pambano lake la pili dhidi ya Marcos Maidana.

WIMBO MPYA: TANZANITE - WIMBO WA LULU

Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>