Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

SI KITU BILA PENZI LAKO-20

$
0
0
 
NYEMO CHILONGANI
Ilikuwa ni siri kubwa sana ambayo ilikuwa ikiendelea katika maisha ya Bruno Deutcsher. Mara kwa mara alikuwa akielekea katika kisiwa Rogen kwa ajili ya kuwawinda wanyama wadogo wadogo ambao alikuwa akiwatumia kutengenezea gundi iliyokuwa ikitumiwa sana nchini Ujerumani.
Biashara hiyo ikaonekana kumuingizia fedha nyingi kiasi ambacho alinunua nyumba kubwa za kifahari pamoja na magari kadhalika. Ingawa jina lake halikuwa kubwa kama majina ya wafanyabiashara wengine lakini Bruno alikuwa akiheshimika sana.
Mara kwa mara alikuwa akielekea katika kisiwa cha Rogen ambako huko alikuwa akiendelea kuwauwa wanyama mbalimbali na kisha ngozi zao kutengenezea gundi. Miaka yote hiyo ndio ilikuwa kazi yake kubwa, kuwauawa wanyama na kisha kutengeneza gundi.
Kitu kilichomfanya kufanya kila kitu kisiri ilitokana na serikali ya Ujerumani kuweka ulinzi mkubwa sana katika kisiwa cha Rogen. Hakutakiwa mtu yeyote kuingia katika kisiwa hicho kwani kilikuwa kisiwa chenye wanyama wakali ambao hata wengine hawakupatikana katika sehemu yoyote ya Ulaya.
Bruno hakuonekana kuogopa, bado alikuwa akielekea katika kisiwa kile huku mikononi mwake akiwa na bunduki pamoja na mikuki iliyokuwa na sumu kali. Kila mnayama ambaye alikuwa akimuona mbele yake, alikuwa halali yake.
Sauti za watu zilikuwa zikisikika kutoka katika sehemu ambayo wala haikuwa na miti mingi. Bruno akaonekana kushtuka kupita kawaida. Hakuamini kama katika kisiwa kile kungekuwa na watu wengine ambao walikuwa wakija porini pale. Maswali kibao yalikuwa yakimiminika kichwani mwake juu ya watu wae ambao walikuwa wamefika katika kisiwa kile.
Hofu ya kudhani kuwa watu wale walikuwa walinzi ikaanza kumuingia, alitamani kukimbia ili kuepuka kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Kila alipotaka kukimbia, akajikuta akisimama na kusonga mbele kuangalia ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea.
Wanaume wawili walikuwa wakionekana vizuri machoni mwake huku kijana mmoja akiwa chini akilia. Mara mlio wa bunduki ukasikika, Patrick akushika mguu wake na kuanza kulia. Risasi ilikuwa imezama mguuni mwake na kuutoboa mfupa wa ugoko wake.
Kilio kikubwa kilikuwa kikisikika kutoka kwa Patrick, kilio kile kilimfanya Bruno kushikwa na huruma kupita kawaida. Vijana wale walikuwa wakiendelea kufurahia, kilio ambacho alikuwa akilia Patrick kilionekana kuwapa furaha kupita kawaida.
“Tutaendelea kupanda juu” Sauti ya kijana mmoja ilisikika.
Akaikoki tena bunduki yake na kisha kujiandaa kumpiga tena na risasi. Mara akashtukia mkuki ukiwa umezama shingoni mwake. Kijana mwingine, hata kabla hajapata wazo la nini alitakiwa kufanya, nae akashtukia mkuki mwingine ukizama shingoni mwake.
Kutokana na sumu kali iliyokuwa imepakwa katiika mikuki ile, wakajiukuta wakianguka chini. Bruno akaanza kupiga hatua za haraka haraka kumfuata Patrick mahali pale alipokuwa. Bado Patrick alikuwa akilia kwa maumivu makali huku akiwa ameushika mguu wake, mfupa wake wa mguu wake ulikuwa umevunjika.
Kitu alichokifanya Bruno ni kuzichukua nguzo za Patrick na kuzipaka damu ambazo zilikuwa zikiendelea kuwatoka vijana wale ambao alikuwa amewapiga mikuki ya shingoni. Alipomaliza kuwapaka, akaibeba miili ile na kwenda kuificha porini zaidi.
Alipomaliza akarudi pale alipokuwa Patrick na kisha kuanza kumbeba huku akiwa mtupu. Bruno alifanya vile makusudi huku akiwa na lengo la kutaka kuwapiga changa la macho watu ambao wangefika mahali pale kwa kutaka kujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kimeendelea kwa kuamini kwamba watu wale walikuwa wamekuja na wenzao ambao waliwaacha katika boti yao.
Patrick alikuwa katika hali mbaya sana, mguu wake ulikuwa umejeruhiwa vibaya na risasi ile ambayo ilimuingia. Akapakiwa botini na safari ya kuelekea mjini kuanza.
Bruno alikuwa akiendesha boti kwa kasi, alitaka kufika ufukweni haraka ambako hapo angechukua gari lake na kisha kuelekea nyumbani kwake. Ndani ya dakika kumi, akawa amekwishafika ufukweni. Ukimya ulikuwa umetawala mahali hapo kutokana na njia ile ambayo mara kwa mara alikuwa akiitumia kuwa njia ya panya.
Akambeba Patrick mgongoni na kisha kumuingiza garini na safari ya kuelekea nyumbani kwake kuanza. Maswali kibao yalikuwa yakimiminika kichwani mwake, alitamani sana kumfahamu mtu ambaye alikuwa amembeba lakini kutokana na giza kuwa kubwa, wala hakuweza kumfahamu japokuwa alijua kwamba mtu yule alikuwa mweusi.
Mara baada ya geti la nyumba yake kufunguliwa, moja kwa moja akaliingiza gari lake na kisha kumshusha Patrick garini na kuanza kuelekea nae ndani ya nyumba yake huku aiwa amembeba begani mwake. Alipomfikisha katika chumba kimoja ambacho kilionekana kuwa kama zahanati ndogo, akamlaza katika kitanda.
Akachukua simu yake na kumpigia daktari wake ambaye alimtaka afike mahali hapo haraka iwezekanavyo. Ni ndani ya dakika kumi, daktari akawa amefika mahali hapo ambapo akaanza kukiosha kidonda cha Patrick na kisha kuanza kuitoa risasi ambayo ilikuwa ndani ya mfupa wake ugokoni.
“Kweli mguu utarudi katika hali ya kawaida kweli?” Bruno alimuuliza Dokta Paul.
“Utarudi, ila atachukua muda mrefu kidogo kitandani. Baada ya hapo tutampa kibaiskeli cha kutembelea huku mguu wake ukiwa kwenye P.O.P” Dokta Paul alisema.
Maisha ya Patrick yalikuwa juu ya kitanda ndani ya nyumba hiyo, hakutakiwa kutoka kwenda sehemu yoyote ile. Kila siku dokta Paul alikuwa akifika nyumbani hapo kwa ajili ya kuhakikisha matibabu kwa Patrick. Wote walikwishajua kwamba mtu ambaye walikuwa wakimtibia alikuwa yule Patrick ambaye alikuwa amechaguliwa kuwa mchoraji bora na ndiye ambaye alikuwa ametangazwa kuuawa porini kwa kuliwa na wanyama wakali.
Waliendelea kukaa na Patrick kwa muda mrefu mpaka pale alipopata nguvu ya kukaa juu ya kibaskeli na kukifanya kuwa miguu yake. Kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea ndani ya nyumba ile kilioekana kuwa siri kubwa kwani waliamini kama siri ingetoka basi mtu ambaye aliwatuma vijana wale kumuua Patrick wangefika mahali pale na kumuua.
Miezi mitatu ikakatika na Patrick kuanza kujisikia nafu, kutokana na dawa kali ambazo alikuwa amepewa, akaanza kutembea kwa kuchechemea mpaka pale ambapo akaanza kutembea kamakawaida.
Kitu ambacho alikuwa akikitaka kukifanya mahali hapo ni kumpigia simu mchungaji Smith pamoja na familia yake na kuwaambia kuwa yeye ni mzima na alitarajiwa kurudi nchini Marekani siku yoyote ile.
“Unajisikia vizuri kabisa?” Bruno alimuuliza.
“Ndio. Ninajisikia vizuri” Patrick alijibu.
“Ila kuna kitu ningependa usikiseme kwa mtu yeyote yule” Bruno alimwambia Patrick.
“Kitu gani?”
“Jinsi nilivyokuokoa kisiwani. Unajua kama utasema kila kitu, utaniweka katika wakati mgumu sana kwani serikali itanikamata kwa kuingia ndani ya kisiwa kile” Bruno alimwambia Patrick.
“Usijali Bruno. Kwa kuwa umeniokoa katika mdomo wa kifo, amini kuwa sitoongea kitu chochote kile” Patrick alimwambia Bruno na kisha kuchukua simu kumpigia mchungaji Smith pamoja na Vanessa kuwataharifu juu ya uwepo wake.
*****
Furaha haikupatikana kwa Vanessa, kila siku alikuwa mtu wa majonzi. Moyo wake ulikuwa umeumia kupita kiasi. Maisha kwake pasipo Patrick yalionekana kuwa ya kinyonge kupita kiasi. Vanessa alikuwa katika wakati mgumu kupita kawaida, machozi ndio ilikuwa sehemu ya maisha yake.
Furaha yote ambayo alikuwa nayo katika kipindi alichokuwa na Patrick ikaonekana kupotea. Afya yake ikaanza kuonekana kudhoofika kutokana na mawazo aliyokuwa nayo juu ya Patrick ambaye hadi katika kipindi hicho, kila mtu alikuwa akijua kwamba alikufa kisiwani.
Siku nyingine Vanessa hakuwa akielekea shuleni, kila alipokuwa akiziangalia sehemu ambazo mara kwa mara alikuwa akipenda kukaa pamoja na Patrick, alionekana kuumia kupita kawaida. Maisha yake yakaonekana kubadilika, Vanessa yule ambaye alikuwa katika kipindi kile cha nyuma pamoja na Patrick alionekana kuwa tofauti na Vanessa huyu ambaye alikuwa katika kipindi hiki.
Kila wakati Vanessa alikuwa akiangalia simu yake, jina la Patrick lilikuwa likionekana vizuri simuni mwake. Bado maumivu makali yalikuwa yakiendelea kuwepo moyoni mwake.
Miezi miwili ilikuwa imepita tangu wamazike Patrick katika makaburi ya Louis ambayo palikuwa pakizikwa watu waliokuwa maarufu. Vanessa aliyatamani maisha yake ya zamani ambayo yalikuwa na furaha lakini kila kitu kikaonekana kubadilika.
Vanessa akashtuka kutoka katika lindi la mawazo mara baada ya kuisikia simu yake ikianza kuita. Simu iliendelea kuita, Vanessa akaichukua na kuanza kuiangalia. Namba ikaonekana kuwa ngeni machoni machoni mwake, alichokifanya ni kuikata ili kumuondolea usumbufu.
Akasimama katika kiti ambacho alikuwa amekalia na moja kwa moja kuelekea katika kiti kingine darasani pale alipokuwa. Simu ile ikaanza kuita tena, wanafunzi wote wakaanza kumuangalia. Vanessa akaichukua simu ile na kuangalia tena kioo, namba ile ngeni ndio ambayo ilikuwa ikipiga tena, alichokifanya ni kuikata tena.
Vanessa alionekana kuchanganyikiwa na hali ambayo alikuwa amekutana nayo katika kipindi hicho. Hakuonekana kuhitaji usumbufu wowote ule. Alionekana kuhitaji muda mwingi wa kupumzika kuliko kuongea ovyo na watu. Kuna kipindi alikuwa akiichukia sana simu yake kwani muda mwingi ilimfanya kutokutulia kutokana na watu wengi kumpigia simu na kumpa pole kwa kile kilichotokea.
Simu ile ikaanza kuita kwa mara ya tatu, Vanessa akaiangalia simu ile na kuikuta namba ile ile ambayo ilikuwa ngeni simuni mwake. Kama kawaida yake, akaikata na kuizima kabisa simu yake. Vanessa akailalia meza yake ya kusomea na kutulia.
Mara mwalimu Kerri akaingia darasani hapo na macho yake kuanza kuangalia huku na kule hali iliyoonyesha kwamba alikuwa akimtafuta mtu fulani. Alipomuona Vanessa, akaanza kupiga hatua kumfuata huku wanafunzi wengine wakimwangalia.
Alipomfikia, akamuinua na kisha kumwambia kwamba amfuate ofisini. Vanessa akainuka na moja kwa moja kuanza kumfuata mwalimu Kerri. Vanessa hakuonekana kuelewa sababu ambayo ilimfanya mwalimu Kerri kuja kumuita na kwenda nae ofisini pasipo kuongea kitu chochote kile.
Macho yake yakatua kwa mchungaji Smith pamoja na mkewe, Rachel ambao macho yao yalikuwa yamejawa na tabasamu pana. Vanessa akaonekana kushtuka, akaanza kujiuliza maswali kibao kuhusiana na tabasamu yale lakini hakupata jibu.
“Kuna nini?” Vanessa aliuliza huku akionekana kushangaa.
“Habari njema” Mchungaji Smith alijibu.
Vanessa akaonekana kushtuka, hakujua habari njema hizo zilizozungumziwa na mchungaji Smith zilimaanisha nini kwake. Akajiona kuwa na hamu ya kutaka kuzisikia habari hizo njema ambazo mchungaji Smith pamoja na mkewe, Rachel walikuwa wamekuja nazo mahali hapo.
“Habari njema kuhusu nini” Vanessa aliuliza.
“Patrick....” Mchungaji alijibu.
Vanessa akanyong’onyea, akamuona mchungaji kumtonesha kidonda ambacho kilikuwa kimeanza kupona. Akaanza kumkumbuka zaidi Patrick ambaye walikuwa wamemzika miezi miwili iliyopita. Akayapeleka macho yake kwa walimu wengine ambao walikuwa ndani ya ofisi ile, walimu wote walikuwa wakionyesha nyuso zilizojaa tabasamu.
“Patrick anakuja. Patrick hakufa kama ilivyotangazwa. Nimeongea nae simu na amesema kwamba anakuja. Ninafikiri kwa sasa atakuwa ndani ya ndege” Mchungaji alimwambia Vanessa.
Vanessa akaonekana kushtuka, hakuamini kama kweli kitu alichokuwa akikisikia masikioni mwake kilikuwa kweli au si kweli. Alijiona kuwa ndotoni ambako baada ya muda angeamka kutoka katika usingizi mzito. Akajaribu kuyafikicha macho yake kuona kwamba alikuwa ndotoni au katika uhalisia.
“Unasemaje?” Vanessa aliuliza huku akionekana kutokuamini.
“Patrick anakuja. Kwani hakukupigia simu nusu saa iliyopita?” Mchungaji alimuuliza Vanessa.
Mawazo ya Vanessa yakarudi katika simu ambayo alikuwa amepigiwa katika kipindi kichache kilichopita. Akaanza kujuta kwa kitendo chake cha kutokuipokea simu ile ambayo ilikuwa ikiingia katika simu yake. Vanessa akaonekana kuumia kupita kawaida.
Akaichukua simu yake kutoka mfukoni, akaiwasha na kuanza kuitafuta namba ile ambayo ilikuwa imeingia katika kipindi kichache kilichopita. Alipoipata, akaanza kuipiga. Simu ile ikaanza kuita, iliendelea kuita zaidi na zaidi, ikapokelewa na sauti nzito kusikika.
“Patrick......” Vanessa aliita.
“Wewe ni nani?” Sauti ya Bruno ilisikika.
“Rafiki yake, Vanessa. Alinipigia simu muda mchache uliopita. Naomba kuongea nae” Vanessa alimwambia Bruno.
“Hayupo. Amepanda ndege kuja huko Marekani. Nafikiri kesho asubuhi ataingia” Bruno alimwambia Vanessa ambaye akakata simu.
Vanessa akashindwa kujizuia, machozi ya furaha yakaanza kumtoka. Hakuamini kama kweli Patrick yule ambaye alikuwa ameambiwa taarifa zake ndiye alikuwa Patrick yule ambaye alikuwa akija na ndege kutoka nchini Ujerumani.
Mwalimu mkuu akaanza kuelekea katika ofisi yake ambako akakichukua kipaza sauti kidogo na kuanza kuongea. Kutokana na vispika vidogo vilivyokuwa viemchomekwa katika kila pembe shuleni hapo, sauti yake ilikuwa ikisikika vizuri.
Taarifa juu ya Patrick ikatolewa, hakukuwa na mtu ambaye alionekana kuamini. Wanafunzi wa shule ya Vinguard waliona tukio hilo kuwa kama muujiza mkubwa ambao wala haukutarajiwa kutokea katika maisha yao. Kila mmoja akawa na kiu ya kutaka kumpokea Patrick ambaye alitarajiwa kuongia asubuhi ya siku inayofuatia.
Ni ndani ya dakika sabini tu, waandishi wa habari wakaanza kufika shuleni pale na kutaa kupata ukweli wa mambo. Kile ambacho walikuwa wamekisikia ndicho ambacho waliambiwa shuleni hapo. Taarifa ikatangazwa katika vyombo vyote vya habari nchini Marekani.
Kila mtu ambaye alizisikia habari zile alionekana kutokuamini kabisa. Watu wakajiandaa vilivyo kumpokea Patrick, watoto ambao kazi yao ilikuwa ni kubeba maua wakatafutwa. Serikali ya Marekani ikamuzandaa Waziri wa Mambo ya Ndani Bwana Thomson kwa ajili ya kusimamia mapokezi uwanjani hapo.

Je, nini kitaendelea?

SERENGETI WAKO SAWA, WAANZA KWA SARE DHIDI YA MALI, MABINGWA WA AFCON

$
0
0


Timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti imeanza vizuri michuano ya Kombe la Mataifa Afrika baada ya sare ya bila kufungana dhidi ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Mali.

Boys walionyesha kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu huku wakijilinda katika kila idara katika mechi hiyo ya Afcon, michuano inayofanyika nchini Gabon.

Mashambulizi ya Boys yalikuwa ni yale ya kushitukiza lakini wakatumia muda mwingi kujilinda kwa mipango dhidi ya Mali ambao wachezaji wake walikuwa na maumbo makubwa zaidi.


Sare hiyo, inaifanya Serengeti kuanza vizuri michuano hiyo ikiwa imekujikusanyia pointi ya kwanza.

SI KITU BILA PENZI LAKO-22

$
0
0
 
NYEMO CHILONGANI
Kila siku Victoria alikuwa mtu wa kwenda kazini, kutokwenda kazini lilionekana kuwa suala gumu katika maisha yake. Kila siku alikuwa akipata usumbufu kutoka kwa wafanyakazi mpaka kwa bosi wake ambaye bado alikuwa akimlaghai kwa fedha alizokuwa nazo.
Victoria alionekana kuwa tofauti na wasichana wengine, ingawa katika kipindi hicho alikuwa na uhitaji mkubwa wa fedha lakini hakutaka kujirahisisha kwa ajili ya fedha. Bado alikuwa na msimamo mkali katika maisha yake, msimamo wa kutomkumkubalia mwanaume yeyote zaidi ya Patrick.
Patrick bado alikuwa kichwani mwake, siku zote alikuwa akimkumbuka kupita kawaida, majonzi ya kutokumuona Patrick ndio yalikuwa sehemu ya maisha yake. Hakujua ni kitu gani ambacho kiliendelea katika maisha ya Patrick mara baada ya kuondoka pale porini na kuelekea asipopafahamu.
Victoria alkuwa ametoka kazini huku akionekana kuchoka kupita kawaida, kazi ambazo alikuwa amezifanya kwa siku hiyo zilionekana kumchosha. Alionekana mpweke huku akitembea kwa mwendo wa taratibu kuelekea nyumbani alipokuwa akiishi na nesi Getrude.
Watu zaidi ya mia moja walikuwa wamesimama nje ya nyumba yao kwa mtindo wa duara. Victoria akaonekana kushtuka kupita kawaida, akaanza kupiga hatua kuelekea kule ambako umati wa watu ulipokuwa umesimama. Kitu cha kwanza mara baada ya kuufikia umati ule, akaanza kupenya penya mpaka mbele kabisa.
Macho yake yakatua kwa nesi Getrude ambaye alikuwa amelala chini huku mapovu yakimtoka mdomoni. Victoria akaonekana kushtuka kupita kiasi, akapiga magoti chini na kumshika Getrude. Tayari macho yake ambayo yalikuwa makavu yakaanza kutoa machozi.
Victoria hakuelewa ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea mahali hapo. Wasiwasi ukaanza kumshika, akayapaleka macho yake kwa watu ambao walikuwa wamesimama kuwazunguka, macho yake tu yalionyesha kwamba alikuwa akitaka kufahamu ni kitu gani ambacho kilitokea mahali hapo.
“Alianguka ghafla, nafikiri kama ana kifafa” Mwanaume mmoja alimwambia Victoria.
Victoria akapigwa na mshtuko, hakuwa na taarifa yoyote kama Getrude alikuwa na kifafa cha aina yoyote ile. Hakutaka kuyapuuzia maneno yale, akasaidiana na watu waliokuwa mahali pale na moja kwa moja kuanza kumpeleka hospitalini.
“Haitowezekana kumtibia mahali hapa. Alipoanguka, aliangukia uti wa mgongo, kwa vyovyote vile ni lazima asafirishwe na kupelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam” Dokta alimwambia.
Victoria akaonekana kuishiwa nguvu, maneno aliyoambiwa na dokta yalionekana kumsikitisha. Hakuwa na fedha za kutosha na hata nauli tu ya kumsafirisha Getrude kwenda Dar es Salaam pamoja nae hkuwa nayo kabisa. Akajiona kuwa na uhitaji wa kupata fedha.
“Sisi kama wafanyakazi wenzie hospitalini hapa, tutamsaidia fedha za matibabu. Cha msingi wewe tafuta fedha za nauli tu” Dokta alimwambia Victoria.
Victoria akajiona kushushiwa mzigo mkubwa, ingawa hakuwa na fedha za kutosha za kukata tiketi ya treni lakini akaona ahueni. Kitu alichokifanya ni kuondoka hospitalini hapo na moja kwa moja kuelekea kazini kwake. Lengo lake kubwa lilikuwa ni kuonana na bosi wake, Bwana Mayayu ambaye kila siku alikuwa akimtaka Victoria.
“Nitakusaidia Victoria...” Bwana Mayayu alimwambia Victoria huku akimwangalia kwa macho yaliyojaa mahaba.
Bosi Mayayu akasimama kutoka katika kiti chake na kisha kuanza kupiga hatua za taratibu zilizojaa mapozi kumfuata Victoria, kabla hajaongea kitu chochote kile, akaupeleka mkono wake begani kwa Victoria na kuanza kumpapasa papasa Victoria.
Victoria akaonekana kukasirika, akasimama na kumwangalia bosi Mayayu kwa macho yaliyojaa hasira. Mayayu akaachia tabasamu pana ambalo aliamini lingemlegeza kabisa Victoria. Victoria akageuka kwa lengo la kutoka ofisini mule, Bwana Mayuya akamshika mkono.
Victoria alipogeuka, akageuka na kofi zito ambalo lilimuingia hasa Bwana Mayuya ambaye akayumba. Victoria akaufungua mlango na kutoka nje ya ofisi ile. Bwana Mayuya akaonekana kukasirika kupita kiasi, kitendo cha kupigwa kofi na mtu kama Victoria ambaye alikuwa mfanyakazi wake aliyeishi kwa kutumia fedha zake kilionekan kuwa dharau katika maisha yake.
Akaanza kupiga hatua kumfuata secretari wake ambaye alikuwa amebaki na mshangao baada ya kumuona Victoria akiwa ametoka ofisini kwa bosi wao huku akioekana kuwa na hasira.
“Huyu mbuzi sitaki kumuona tena akija mahali hapa.....umesikia?” Bwana Mayuya alimwambia sekretari wake.
“Ndio bosi. Tatizo nini?”
“Nimekwambia asije...ebo...haunielewi?”
“Nimekuelewa” Secretari aliitikia.
Njia nzima Victoria alikuwa akilia, hakuamini kama kule ambako alitakiwa kupata msaada ilishindikana. Alipofika nyumbani, akaanza kuelekea katika nyumba za majirani zake na kisha kuanza kuwaomba msaada wa fedha za nauli.
Kutokana na kila mtu kujua kila kilichotokea, wakaamua kumsaidia kwa moyo mmoja. Victoria akapata kiasi cha shilingi elfu thelathini na tano ambacho alikiona kumfaa kwa kusafiri kutoa Tabora mpaka Dar es Salaam. Victoria hakutaka kuchelewa, siku iliyofuata akaanza safari kutoka Tabora kwenda Dar es Salaam.
******
Mawasiliano kati ya hospitali ya Nzega na Muhimbili yakafanyika kiasi ambacho wala haikuwa shida kwa Victoria. Alipofika katika stesheni ya Railways iliyokuwa jijini Dar es Salaam, gari la wagonjwa lilikuwa mahali pale likiwasubiri.
Victoria hakuonekana kuwa na fahamu, muda wote alikuwa kimya. Victoria hakuonekana kuwa na furaha kabisa, alijiona kupitia katika kipindi kigumu sana maishani mwake. Kila wakati aipokuwa akimwangalia Getrude, sala ya kimoyo moyo ilikuwa ikiendelea moyoni mwake.
Gari ile la wagonjwa lilifika katika hospitali ya Muhimbili baada ya dakika nne kutoka Railways. Moja kwa moja akateremshwa na kuwekwa juu ya machela ambayo ikaanza kusukumwa kuelekea katika jengo la hospitali ile.
Huduma ya kumuhudumia Getrude ikaanza mara moja. Kila kitu kilikuwa kimefika katika ofisi ya dokta mkuu juu ya hali ambayo alikuwa nayo Victoria. Akaruhusiwa kulala hospitalini hapo mpaka katika kipindi ambacho Getrude atapata nafuu na kuruhusiwa.
Siku ya kwanza ikapita, siku ya pili, ya tatu mpaka wiki, bado Getrude hakuwa amefumbua macho yake, alikuwa amelala katika usingizi wa kifo. Victoria bado alikuwa akiendelea kulala hospitalini pale huku dokta mkuu akitumia kiasi cha fedha katika kumnunulia chakula cha kila siku.
“Kuna nini? Mbona mnaonekana tofauti sana leo?” Victoria aliwauliza manesi ambao walionekana kuwa haraka haraka.
“Mmarekani amekuja. Yule Mtanzania aliyeshinda shindano la uchoraji” Nesi mmoja, Fatuma ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Victoria toka afike hapo, alimwambia.
“Mbona mimi simfahamu” Victoria alimwambia
“Utamuona tu”
“Sasa nyie mnaelekea wapi?”
“Nje. Tunakwenda kumpokea, si kila siku kumuona kwenye televisheni” Nesi Fatuma alisema na kuondoka.
Victoria alijikuta akibaki peke yake mahali pale alipokuwa amekaa benchini. Ukimya ndani ya hospitai ile ulikuwa mkubwa huku kwa mbali kelele za watu zikiwa zinasikika kwa nje. Victoria hakutaka kutoka nje kumuona mtu huyo ambaye hadi kufikia hatua hiyo, aliona mtu huyo kuwa maarufu ambaye kila mtu alitamani kumuona na hata kumgusa.
Victoria alibaki benchini huku akiangalia chini. Mawazo yake yalikuwa juu ya Getrude ambaye bado hakuwa na fahamu kabisa. Mara kelele zile zilizokuwa zikisikika nje zikaanza kuhamia ndani. Mtu huyo ambaye alikuwa amepokelewa na manesi pamoja na madaktari alikuwa ameingia ndani ya jengo lile. Kwa haraka haraka daktari mmoja akaanza kupiga hatua kumfuata Victoria pale alipokuwa amekaa benchini.
“Binti. Ungekwenda kidogo hapo nje...kuna kazi inaanyika mara moja” Dokta yule alimwambia Victoria ambaye akasimama na kuanza kuondoka kuelekea kule ambako watu wale walikuwa wamepitia.
Uso wake ulikuwa ukiangalia chini huku kwa mbali machozi yakianza kumlenga. Hakutarajiwa kama angeweza kutolewa mahali pale kwa ajili ya kumpisha mtu ambaye alikuwa ametoka nchini Marekani. Victoria akapishana na watu wale ambao walikuwa zaidi ya ishirini pamoja na waandishi wa habari.
Victoria alikuwa akipiga hatua za haraka haraka kuelekea nje huku uso wake ukiangalia chini, hakutaka kumwangalia mtu yeyote usoni kwa wakati huo kutokana na kuonekana kwamba alikuwa akilia. Aliendelea zaidi na zaidi kupiga hatua kuelekea nje, mara akashtuka baada ya kusikia akiitwa kwa nyuma.
“Victoria.....Victoria....Victoria...” Alisikia vilivyo akiitwa.
Mara ya kwanza Victoria alipuuza, aliendelea kupiga hatua kuelekea nje. Bado sauti ile ilikuwa ikiendela kumuita. Victoria akapigwa na mshangao, hakujua kama kulikuwa na mtu yeyote Dar es Salaam ambaye alikuwa akimfahamu zaidi ya baadhi ya madaktari waliokuwepo hospitalini pale.
Aliisikiliza vizuri sauti ile ambayo ilikuwa ikimuita, haikufanana na sauti ya daktari yeyote yule hospitalini pale lakini sauti ile wala haikuwa ngeni masikioni mwake, akajaribu kukumbuka mahali ambapo alikwishawahi kuisikia sauti ile. Victoria akashtuka kupita kawaida mara baada ya kuikumbuka sauti ile, mwili wake ukapigwa ganzi, kijasho chembamba kikaanza kumtoka.
Akasimama huku kwa mbali akionekana kutetemeka kupita kawaida. Akauinua uso wake. Kila alipotaka kugeuka nyuma kumuangalia muitaji, alisita kufanya hivyo japokuwa sauti ile alionekana kuikumbuka vlivyo ingawa miaka miwili ilikuwa imepita tangu aisikia.
“Ni mimi, Victoria. Naomba ugeuke nyuma mpenzi” Sauti ile ilisikika.
“Patrick........” Victoria alijisemea moyoni hata kabla hajageuka na kumuangalia muitaji.
******
Maisha ya Patrick yalikuwa hatarini, hakuonekana kumuaini mtu yeyote katika kipindi hicho. Kila wakati alikuwa akiishi kwa wasiwasi. Alimfahamu vilivyo muuaji yule ambaye alikuwa amefanya mauaji mengi kwa watu weusi. Alikuwa akimuogopa sana mtu huyo kuliko kitu chochote.
Aliamini kwamba huo haukuwa mwisho wake wa kumtafuta, alijua fika kwamba ni lazima agemtafuta tena. Maisha yake yalikuwa yakfanya kila kitu mara moja moja tu mpaka pale ambapo angerudi nchini Marekani na kuwaeleza Polisi juu ya mtu ambaye alikuwa amemteka nchini Ujerumani.
Baadhi ya vitu ambavyo alikuwa akivifanya hakuwa akififanya mara mbili mbili. Njia ambayo alikuwa akipita wakati anaondoka basi wakati wa kurudi alikuwa akipita njia nyingine. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake siku zote, hakutaka kuyabadilisha staili ya maisha yake mpaka pale ambapo mtu yule angetiwa nguvuni.
Gari ambalo alikuwa akilitumia katika kipindi ambacho alikuwa akiingia katika katika sehemu fulani, basi alikuwa akiondoka na gari jingine. Hayo ndio yalikuwa maisha yake kila siku, hakutaka kuyakatisha maisha yake hasa katika nchi ya kigeni.
“Siwezi kuingia katika gari lile” Patrick alimwambia Vanessa.
“Kwa nini?” Vanessa aliuliza.
“Haya ndio maisha yanguniliojiwekea katika maisha yangu ya sasa. Haukumbuki nilivyokuwa nikifanya nchini Marekani Vanessa?” Patrick alimuuliza Vanessa.
“Nakumbuka”
“Safi sana. Hayo ndio maisha yangu. Nitaingia ndani ya gari lenu” Patrick alimwambia Vanessa.
Kila mmoja alionekana kushangaa utaratibu ambao Patrick alikuwa amejiwekea juu ya maisha yake. Patrick pamoja na Vanessa wakaanza kupiga hatua kulifuata gari ambao alikuwa amepakizwa Vanessa katika kipindi ambacho walikuwa wameingia katika hospitali ile.
Mara mlio wa bomu ukasikika, gari lile ambalo alitakiwa kuingia Patrick lilikuwa limelipuka. Watu wakaanza kutawanyika huku wengine wakiita jina la Patrick kwa kudhani kwamba Patrick alikuwa amelipuliwa katika lile gari.
“Mungu wangu! Patrick! Umejuaje?”
“Kila siku Mungu yupo pamoja nami” Patrick alimwambia Vanessa.
Safari ya kuelekea Ikulu ikaanza mara moja ambako huko wakakaribishwa chakula cha usiku. Ilikuwa ni furaha kubwa kwa rais wa Misri Bwana Mahomoud kula chakula pamoja na Patrick ambaye alikuwa mtu maarufu sana duniani.
Siku iliyofuata, safari ya kuelekea nchini Tanzania ikaanza. Safari ya kuelekea nchini Tanzania haikuwa katika ratiba ila iliingia ghafla baada ya Patrick kutaka iwe hivyo. Tayari akaonekana kuwa na wasiwasi mkubwa. Alitamani kwanza afike nchini Tanzania hata kabla ya kuelekea katika nchi mbili zilizobakia.
Safari kutoka nchini Misri iliwachukua masaa manne, wakaanza kuingia katika nchi ya Tanzania. Watu wengi walikuwa wamesimama uwanja wa ndege. Ingawa taarifa zilikuwa zimefika kwa kuchelewa sana kuingia kwa Patrick nchini Tanzania lakini watu wakajitoa vilivyo, masaa sita ambayo walipewa kwa kujiandaa yalikuwa yametosha kabisa kwa wao kufika uwanja wa ndege kwa ajili ya kumpokea mtu wao, ndugu yao na mtoto wao, Patrick.
Patrick akayapeleka macho yake chini, fuaha kubwa ikamtawala, machozi yakaanza kumtoka, hakuamini kama kweli kwa wakati huo alikuwa akitarajiwa kutua katika ardhi ya nchi ya Tanzania, nchi ambayo alikuwa amezaliwa na kukulia.
Ndege ikatua na kuanza kutembea kwa mwendo fulani na kisha kusimama. Mlango ukafunguliwa. Patrick hakutaka kuwa wa mwisho kama ambavyo alifanya katika sehemu nyingine, alikuwa wa kwanza kufika mlangoni. Kelele za shangwe zikaanza kusikika mahali hapo, Patrick akaanza kupiga hatua kushuka ngazi huku akijifuta machozi ambayo yalikuwa yakimtoka.
Vanessa, Matilda na Simpson ndio ambao walikuwa wamefuatia kwa nyuma. Patrick akajiona akishuka ngazi taratibu, alichokifanya ni kuanza kupiga hatua za haraka haraka mpaka alipofika chini ambako akapiga magoti chini.
Tayari shati lake ambalo alikuwa amelivaa lilikuwa limeloanishwa na machozi ambayo yalikuwa yakimtoka. Waandishi wa habari wakaanza kumpiga picha Patrick ambaye bado alikuwa akiendelea kulia mahali pale. Baada ya muda, akasimama na kuanza kumpa mkono Mheshimiwa Peter Charles, ambaye alikuwa Waziri wa Mkuu.
Watoto waliokuwa na maua wakafika mahali hapo na kumgawia Patrick maua ambayo walikuwa nayo mikononi. Muda wote Patrick alikuwa akionekana kuwa na furaha kupita kawaida..
Patrick pamoja na wakina Vanessa wakaingia ndani ya gari ambalo likaanza safari ya kuelekea katika jengo la uwanja wa Taifa ambako Watanzania zaidi ya elfu themanini walikuwa wamekusanyika wakimsubiri yeye. Patrick alikuwa akipunga mikono kwa Watanzania ambao walikuwa wamekusanyika barabarani.
Muda wote Patrick alikuwa akilia, kila alipokuwa akiliangalia jiji la Dar es Salaam alikuwa akizikumbuka siku zile ambazo alikuwa akiishi kwa Gibson.
Safari ile ikaishia katika eneo la uwanja wa ndege. Ulinzi ulikuwa mkubwa kwa kila mtu ambaye alitaka kumgusa patrick. Patrick na wenzake wakaanza kupiga hatua kuelekea ndani ya uwanja ule. Mara baada ya kuonekana tu, uwanja mzima ukaanza kupiga kelele za shangwe.
Patrick hakutakiwa kukaa zaidi ya dakika thelathini uwanjani hapo kitu ambacho kilimfanya kupelekwa mpaka katika jukwaa mbele kabisa na kuanza kuongea. Kitu cha kwanza ambacho alikuwa amekiongea mahali hapo ni kuhusu maisha yake.
Alieleza kila kitu ambacho kilitokea katika maisha yake. Kila mtu mahali pale alionekana kusikitika. Historia ya Patrick ilionekana kumgusa kila aliyekuwa akiisikiliza mahali pale.
“Wazazi wangu waliuawa kwa kuteketezwa na moto. Jambo hilo liliniuma na kila siku litaendelea kuniuma” Patrick alisema huku umati wote ukiwa umegubikwa na huzuni.
Je, nini kitaendelea?
Tukutane Jumatano mahali hapa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Mei 16, 2017

$
0
0

 Hapa tumekuanikia kurasa za mbele na za nyuma za magazeti yote ya Tanzania leo, Mei 16, 2017. Ni yale ya Hardnews, Udaku na Michezo.

Waziri wa Elimu awasimamisha kazi vigogo wa Taasisi ya Elimu ya Tanzania

$
0
0

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako leo Jumatatu jioni amewasimamisha kazi Kaimu Kamishna wa Elimu, Nicholas Bureta na Kaimu  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Tanzania (TIE), Dr. Elia Kidga kufuatia sakata la kasoro zilizopo katika vitabu vya kujifunzia wanafunzi.

Waziri Ndalichako ametangaza hatua hiyo kufuatia kuibuka kwa mjadala bungeni leo jioni kuhusu kasoro kwenye vitabu hivyo ambavyo vimechapishwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kufundishia. Miongoni mwa makosa yaliyobainika kwenye vitabu hivyo, ni kurasa ulioandikwa kuwa Dodoma ndio mji mkubwa Tanzania.

Waziri Ndalichako amewasimamisha viongozi hao na ameliambia bunge kuwa uchunguzi wa kina unafanyika na baada ya kukamilika hatua za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika.

Wabunge walitishia kuzuia kupitisha bajeti ya Wizara ya Elimu hadi hapo wizara itakapotoa uamuzi wenye mantiki katika kutatua tatizo hilo lililozua mvutano mkubwa.

“Kwa mamlaka niliyonayo, namuagiza Kaimu Kamishna wa Elimu na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), kuondoka ofisini mara moja ili kupisha uchunguzi,” alisema Ndalichako

Baada ya waziri kutoa agizo hilo, wabunge waliridhia kupitisha bajeti ya wizara hiyo.

Rais Magufuli aivunja Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA)

$
0
0
Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 15 Mei, 2017 ameivunja rasmi Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) na ameagiza mali na shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na CDA zihamishiwe Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.

Mhe. Rais Magufuli ameivunja CDA kwa kutia saini hati ya Amri ya Rais ya kuivunja Mamlaka hiyo Ikulu Jijini Dar es Salaam, tukio ambalo limeshuhudiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi, Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. Jordan Rugimbana na viongozi mbalimbali wa wizara.

Mhe. Rais Magufuli amesema ameamua kuivunja CDA na kuhamishia majukumu yake katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ili kuondoa mkanganyiko wa utoaji wa huduma kwa wananchi uliokuwa ukisababishwa na mgongano kati ya vyombo hivyo viwili na pia kuendana na mahitaji ya sasa ambayo yamedhihirisha kuwa hakuna haja ya kuwepo kwa CDA.

Kufuatia uamuzi wa kuivunja CDA, Mhe. Dkt. Magufuli pia ameivunja Bodi ya CDA, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa CDA Mhandisi Paskasi Muragili atapangiwa kazi nyingine na ameagiza wafanyakazi wote wa Mamlaka hiyo wahamishiwe Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma na ofisi nyingine za Serikali kadiri inavyofaa.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameagiza hati zote za kumiliki ardhi zilizokuwa zikitolewa na CDA kwa ukomo wa umiliki wa miaka 33 zibadilishwe na kufikia ukomo wa umiliki wa miaka 99 kama ilivyo katika maeneo mengine nchini ili kuwavutia wawekezaji hasa wa viwanda.

“Wananchi wa Dodoma wamelalamikia tatizo hili kwa muda mrefu sana, hata nilipokuwa kwenye kampeni zangu za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 walilalamika sana, sasa nimetekeleza niliyowaahidi, naamini kwa uamuzi huu malalamiko ya wananchi yatapata utatuzi na pia tutakuwa tumeondoa kikwazo cha umiliki wa muda mfupi wa ardhi uliosababisha wawekezaji kushindwa kujenga viwanda Dodoma.

“Sasa majukumu yote yanahamishiwa Manispaa ya Dodoma, sitaki kuendelea kusikia visingizio, mkajipange mambo yaende vizuri” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa uamuzi huo na wameahidi kusimamia kwa ukaribu mchakato wa kuhamisha majukumu ya CDA kwenda Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.

Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ilianzishwa kwa Amri ya Rais ya tarehe 01 Aprili, 1973 na kutangazwa kupitia tangazo la Serikali namba 230 na imevunjwa rasmi leo tarehe 15 Mei, 2017 kwa Amri ya Rais na kuchapishwa katika gazeti la Serikali.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
15 Mei, 2017

BAADA YA HANS POPPE, UONGOZI WA SIMBA KUKUTANA NA MO DEWJI

$
0
0
 
 
Uongozi wa Simba umepanga kukutana na Mohamed Dewji na kumaliza tofauti zao.

Dewji maarufu kama Mo, aliamua kujitoa katika suala la mchakato wa mabadiliko baada ya klabu ya Simba kuingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya ubashiri ya SportPesa.

Mo alionyesha kukasirishwa baada ya uongozi kutomshirikisha yeye pamoja na wajumbe wengine wa kamati ya utendaji, jambo aliloliita kutoaminiana miongoni mwao.

“Uongozi utakutana na Mo, itakuwa leo au kesho ili kulimaliza suala hilo. Kinacholengwa ni kuonyesha busara baada ya matatizo yaliyotokea.

“Kama ambavyo umeona, uongozi umefika kwa Hans Poppe, umekaa na kuzungumza naye na suala limefikiwa kwa kupatikana muafaka.


“Sasa ni lazima kukutana na Mo, Simba hatutaki mifarakano,” kilieleza chanzo.

ZLATAN AAMUA KUJIPUMZISHA ZAKE MAREKANI, BAADA YA UPASUAJI

$
0
0


Baada ya upasuaji wake wa goti kwenda vizuri, Zlatan Ibrahimovic ameamua kubaki nchini Marekani na kujipumzisha.

Zlatan ataukosa msimu wote wa Ligi Kuu England ikiwemo mechi ya fainali ya Europa League dhidi ya Ajax ya Uholanzi.
Hali hiyo inatokana na kuumia goti na kufanyiwa upasuaji nchini Marekani na sasa ameamua kujipumzisha mjini Miami, Florida.






Meck Sadick, majaji wa mahakama kuu waandika barua kuacha kazi

$
0
0


KUJIUZULU: Rais Magufuli ameridhia kujiuzulu kwa viongozi wafuatao; RC Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, majaji wa Mahakama Kuu, Aloysius Mujulizi na Upendo Msuya.

Godbless Lema awashangaa wanaomdhihaki baada ya kumpongeza Nyalandu kufuatia kuwasaidia majeruhi wa ajali ya basi la Lucky Vicent

$
0
0

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amewashangaa wanaomdhihaki na kumshambulia kwa maneno makali mara baada ya kumpongeza mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu kufuatia kuwasaidia majeruhi wa ajali ya basi la Lucky Vicent.

Amesema kuwa kwa hapa nchini kuwa mpinzani wa siasa za bongo ni kazi ngumu sana, hivyo inahitaji kuwa na ujasiri wa kuweza kupambana ili uweze kushindana na kila anayekushambulia hata kwa lile jema unalolifanya.

Baada ya Mbunge Godbless Lema (Chadema) kumshukuru Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) Lazaro Nyalandu kuna kundi la watu liliibuka na kuanza kutoa maneno ya dhihaka kwa Lema huku wengine wakipongeza na kusema ni jambo la kheri kwa mbunge huyo kutambua kazi iliyofanywa na Nyalandu, lakini baada ya mijadala hiyo kuzidi kuwa mikuba Lema aliibuka na kutoa kauli hii kuwajibu waliokuwa wakimdhihaki.

“Kuwa mpinzani wa siasa Tanzania ni kazi ngumu sana, ila hatukati tamaa kwa sababu upendo wetu ni mkuu kuliko dhihaka. Mungu awabariki” aliandika Godbless Lema

Wazee Wa Kimila Waanika Maajabu ya Mti Uliotoa Uhai Watu 5, Arusha

$
0
0






ARUSHA: Ilikuwa lazima wafe! Hivyo ndivyo walivyokuwa wakisema baadhi ya watu walioshuhudia tukio la kutisha la mti mkubwa aina ya Mkuyu kuangukia nyumba ya Jonathan Kalamboya (55) Mei 9, mwaka huu na kuua watu watano wa familia yake katika Kijiji cha Ngeresi, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha.

Mti huo uling’oka saa saba usiku kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mfululizo mkoani Arusha hivyo kusababisha maafa hayo ya vifo vya watu watano wa familia ya mzee Kalamboya ambao ni Jonathan Jonathan (16) Gloria Jonathan (11) Giliad Jonathan (31), Lazaro Lomnyaki (26) na Best Jonathan (20).

UWAZI KIJIJINI NGERESI

Baada ya tukio hilo, kama kawaida yake ya kuchimba na kuchimbua, gazeti hili lilifika eneo la tukio na kufanikiwa kupata undani wa vifo hivyo kwa kuzungumza na mzee Kalamboya aliyekuwa na haya ya kusema:

“Mimi wakati janga hili linatokea nilikuwa kazini zamu ya usiku mjini Arusha katika Hospitali ya Dk. Mohammed. Mke wangu alikwenda kumsaidia mkwe wetu aliyekuwa amejifungua.

“Wakati narudi nyumbani asubuhi, nilikutana na mama mmoja akaniambia juu ya tukio hili kwani aliniambia watoto wangu wamefukiwa na mti, nilipigwa na butwaa, nikajikuta nachanganyikiwa.

“Baadaye kuna mtu tena alinipigia simu akaniambia nisubiri watakuja kunichukua na gari lakini mimi nikapanda basi, sikufika nyumbani nikakutana na ndugu na jamaa wakanipeleka kwa mjomba wangu.

“Walinipeleka kwa mjomba kwa sababu waliniambia nyumbani kwangu hakuna makazi tena na watoto wamefariki dunia, nimebaki na wawili tu. Niliumia sana, sikuweza kuamini mara moja taarifa hizo.”

MAITI ZAFUKULIWA BAADA YA SAA SITA

Mzee huyo aliongeza kuwa, alipofika nyumbani ndipo alipothibitisha kuwa, alikuwa amebaki na watoto wawili tu kufuatia wengine kufariki dunia.

Alisema maiti za watoto wake zilikaa zikiwa zimekandamizwa na mti huo kwa saa sita kwani tangu saa nane usiku hadi saa moja asubuhi ndipo walipofanikiwa kuzitoa.

POLISI NAO WALICHELEWA KUFIKA

“Polisi walifika wakiwa wamechelewa kutokana na ubovu wa barabara. Hata hivyo, waliwasifu vijana kwa ushirikiano mkubwa wa uokoaji walioufanya,” alisema.

WATOTO WALIONUSURIKA KIFO

Kwa kudra za Mwenyezi Mungu, watoto wawili wa mzee huyo walinusurika kifo baada ya mmoja anayesoma kidato cha pili, Zakayo Jonathan kuchomoka ndani na mdogo wake wakati mti ukibingirika zaidi ya mita 150 kuelekea kwenye nyumba yao.

Akilisimulia Uwazi jinsi walinyonusurika kimaajabu, mtoto huyo alisema: “Nilianza kusikia mawe yakigonga nyumba nikadhani ni tetemeko la ardhi. Harakaharaka nilimchukua mdogo wangu na kutoka ndani kupitia dirishani, baada ya sekunde chache mti mkubwa uliokuwa

 ukitoka juu ya mlima ukagonga na ukasambaratisha nyumba yetu.

“Nilianza kulia na kupiga yowe na mdogo wangu kuita majirani ambao walifika na kukuta mti umefunika nyumba yetu.

“Kilichoniliza zaidi ni kwamba nilijua mti huo umewafunika kaka zangu, hivyo kwa vyovyote nilijua wameshafariki dunia,” alisema Zakayo huku akitokwa na machozi.

WAZEE WA KIMILA NAO WANENA

Wazee wa kijiji hicho wakiwemo wa kimila waliozungumza na Uwazi kuhusu vifo hivyo walisema, mti huo kwa jinsi wanavyoufahamu, kwa kuanguka kwake ilikuwa lazima uue lakini ni tukio ambalo limewashitua sana.

Wazee hao ambao wamekula chumvi nyingi walisema kuwa, mti huo ambao unakadiriwa kuishi zaidi ya miaka 200, ulikuwa ukitumika kwa mambo ya matambiko ya kimila kwa muda mrefu kiasi kwamba wapo ambao walikuwa wakihofia kuukaribia.

“Mti huu ulikuwa ukitumika kwa mambo ya kimila, mambo ya matambiko tangu enzi za mababu, kwa hiyo unaweza kuona siri iliyopo ya vifo vya ndugu zetu hao,” alisema mzee mmoja ambaye hata hivyo hakutaka jina lake liandikwe gazetini bila kufafanua zaidi.

Alisema licha ya imani hasi waliyonayo baadhi ya watu, mambo mengi ya heri pia yalikuwa yakiombwa na wazee wa enzi hizo chini ya mti huo lakini wameshangaa ulivyokuja kupoteza maisha ya watu tena katika mazingira ya kimaajabu.

“Ajabu moja kubwa ni kwamba mti huu baada ya kung’oka ulipasuka vipande viwili, kimoja kikakwepa nyumba na kingine kikaenda kufunika nyumba.

“Umeona wale nyuki, walikuwepo kwenye mti ule kwa miaka mingi na wala hawadhuru watu, wengine huamini pia kwamba wapo kwa ajili ya matambiko,” alisema bila kufafanua.

Mwandishi wetu alipoambiwa juu ya nyuki hao aliingiwa na woga, akataka kuondoka eneo hilo lakini alihakikishiwa na wazee hao kwamba hawezi kung’atwa, hivyo hakuwa na haja ya kukimbia.

MSIKIE HUYU!

Naye kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la John, mkazi wa kijiji hicho aliliambia Uwazi kuwa, mti huo licha ya kwamba ulikuwa ukitumika kwa matambiko lakini wengi walikuwa wakiamini unafuga majini.

“Unajua hii miti yenye umri mrefu kama huu inakuwa na mambo mazito, ndiyo maana wengi wanasema ilikuwa lazima uue, ndugu zetu wamekufa vifo vibaya sana, Mungu awapumzishe mahali pema peponi,” alisema kijana huyo.

Miili ya vijana hao wa mzee Kalamboya ilizikwa Juni 13, mwaka huu huku watoto watatu wakizikwa katika kaburi moja na hakuna aliyeweza kueleza sababu ya kufanya hivyo.

MKUU WA MKOA AGUSWA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliyehudhuria mazishi hayo aliwapa pole wafiwa kwa niaba ya serikali ambayo iligharamia mazishi.

Ofisi ya mkuu huyo wa mkoa iliahidi kutoa mabati 50 na mifuko ya saruji 50, pia ilitoa shilingi milioni 3.5 ili mzee huyo aweze kukarabati nyumba yake iliyosambaratishwa na mti huo.

Yeyote aliyeguswa na habari hii anaweza kumsaidia mzee huyu kwa chochote kwa kutumia namba yake, 0766 818906 kwani sasa yeye na familia yake iliyobaki wanaishi kwa mjomba wake- Mhariri.

Mtoto Majeruhi wa Lucky Vincent Afanyiwa Upasuaji Marekani

$
0
0


Taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu imeeleza kuwa
“Madaktari wamesema wamemfanyia upasuaji wa bega ‘shoulder’, mtoto Doreen ambaye ni mmoja wa watoto watatu waliojeruhiwa kwenye ajali ya basi la Lucky Vincent Nursery and Primary School.
“Mtoto huyo amefanyiwa pia upasuaji wa nyonga ‘hip’ ambapo baadae leo mtoto huyo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa taya ‘jaw’.
“Pia mtoto huyo atafanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo‘spine’ kesho.
“Tuendelee kumweka yeye na wenzake katika maombi na sala zetu!”











Watoto Wilson na Sadia walipowasili uwanja wa Sioux City usiku wa kuamkia leo. Walipelekwa Moja kwa Moja Mercy hospitali.

Muonekano Mubashara wa Wema Sepetu

$
0
0










Supastaa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu, ametupia picha mpya kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram, zikimuonesha akiwa na mwonekano mpya ambapo muda mfupi baadaye, mashabiki zake walianza kutoa maoni yao, wengi wakionesha kufurahishwa na mwonekano wao mpya.
Mashabiki hao wamembatiza Wema kwa jina jipya, wakimuita Malkia wa Instagram Tanzania. Picha hizo zimepigwa na Bernard Atilio.

'LIVE' YANGA 0-0 TOTO AFRICANS, KIPINDI CHA KWANZA, UWANJA WA TAIFA

$
0
0


MAPUMZIKO
Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza, timu zote zinaenda kupumzika vyumbani.
Dakika ya 48: Yanga wanafanya shambulizi, kipa wa Toto anafanya makosa lakini mpira unatoka inakuwa kona, inapigwa mabeki wanaokoa.
Dakika ya 47: Washambuliaji wa Yanga, Chirwa na Tambwe wanakosa maelewano mazuri baada ya kusogea na mpira hadi karibu na lango la Toto.
Dakika ya 45: Mwamuzi wa akipa anaonyesha dakika 3 za nyongeza.
Dakika ya 43: Yanga wanaendelea kucheza soka la kuelewana, wnaapiga pasi nyingi.
Dakika ya 40: Yanga wanapata kona kutokana na Chirwa kutumia nguvu kubwa wakati akishambulia.
Dakika ya 40: Kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko, anapiga shutikali, kipa anapangua inakuwa kona.
Dakika ya 37: Timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Dakika ya 32: Yanga nao wanajibu mapigo wanatengeneza mashambulizi, Tambwe anaonekana kuana kupambana, Yanga wanamiliki mpira hasa sehemu ya katikati.
Dakika ya 30: Toto wanaonekana kuanza kuelewana na kujipanga kufanya mashambulizi kwa Yanga, wanapata kona.
Dakika ya 26: Toto wanapata kona, wanapiga mpira lakini kipa wa Yanga, Beno anaudaka mpira na kumrushia Chirwa ambaye anaingia nao kwa kasi lakini walinzi wa Toto wanamuwahi.
Dakika ya 25: Lusajo Lerient anapata nafasi nzuri ya kufunga lakini anashindwa kuitumia.
Dakika ya 22: Juma Abdul anafanya kazi nzuri anapanda kushambulia lakini mpira unawahiwa na mabeki wa Toto wanautoa.
Dakika ya 20: Yanga wanamfanya kipa wa Toto, David Kissu kuwa bize kutokana na kufika langoni kwake mara kwa mara.
Dakika ya 15: Yanga wanapata kona, inapigwa lakini kipa wa Toto anafanya kazi nzuri, anapiga mpira mrefu kuelekea kwa mchezaji wake Wazir Jr.
Dakika ya 10: Chirwa anachezewa faulo.

Dakika ya 5: Toto wanarudi nyuma wachezaji wao kuanza kuzuia.

Dakika ya 2: Yanga wanaendeleza kasi kama kawaida, inavyoonekana wanatafuta bao la mapema.
Dakika ya 1: Yanga waanza kwa kasi
Mwamuzi anaanzisha mchezo
Kabla ya mchezo kuanza, mwamuzi alipuliza filimbi na upande wa timu zote, wakasimama kutoa heshima.
Kikosi cha Yanga ambacho kitashuka uwanjani leo kukipiga dhidi ya Toto Africans kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika Ligi Kuu ya Vodacom tayari kimeshatoka, wachezaji 11 watakaoanza hawa hapa:
1. Beno Kakolanya
2. Juma Abdul,
3. Haji Mwinyi
4. Kelvin Yondani
5. Vincent Bossou
6. Thaban Kamusoko
7. Juma Mahadhi.
8. Haruna Niyonzima
9. Amisi Tambwe
10. Obrey Chirwa
11. Geofrey Mwashuiya
Akiba
Deogratius Munishi, Hassan Kessy Nadir Haroub, Matheo Antony, Deusi Kaseke , Emmanuel Martin na Justine Zulu.

Yanga, SportPesa Kusaini Mkataba Mnono Kesho Jumatano

$
0
0


Baada ya kusaini mkataba na Simba, sasa Kampuni ya SportPesa inatarajiwa kusaini mkataba na Klabu ya Yanga, kesho Jumatano.
Awali kulikuwa na taarifa kuwa mkataba huo ambao ulikuwa usainiwe tangu wiki iliyopita, ilipangwa usainiwe leo Jumanne wakati Yanga ikicheza dhidi ya Toto Africans katika Ligi Kuu ya Vodacom lakini kutokana na mambo kadhaa kutokuwa sawa ikabidi ipangwe kesho Jumatano.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa kila kitu kimekamilisha na mkataba huo wa Yanga na kampuni hiyo ya Sportpesa sasa utasainiwa kiroho safi baada ya pande zote kukubaliana.

Pamoja na hivyo habari kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa dili lao lina thamani kubwa kiasi kuliko lile la Simba ambalo lina thamani ya shilingi bilioni 4.9.

Katika mkataba huo wa Simba, klabu hiyo itapokea shilingi milioni 888 katika mwaka wa kwanza huku kukiwa na ongezeko la asilimia tano kwa kila mwaka katika miaka mitano ya mkataba huo.

Kama hivyo haitoshi, Simba imepewa motisha iwapo watachukua ubingwa wa ligi kuu watapewa shilingi milioni 100 Huku Sportpesa wakitenga shilingi milioni 250 iwapo Simba wakibeba Kombe la Kagame au michuano iliyo chini ya Caf.

Hivyo Wanayanga wanasubiri kwa hamu juu ya mkababa huo ambao ulisababisha kuibuka kwa mgogoro mzito wa kiuongozi. Ikumbukwe kuwa katika miezi ya hivi karibuni Yanga imekuwa ikipitia kipindi kigumu kutokana na mwenyekiti wake Yusuf Manji kuwa na matatizo binafsi na hivyo kutokuwa karibu na klabu ambapo yeye ndiye amekuwa akitoa msaada mkubwa wa fedha.

Rais Magufuli Atembelea Shirika La Utangazaji La Taifa - TBC

$
0
0





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya ziara ya kushtukiza katika makao makuu ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) yaliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa ambaye hakutaka jina lake kutajwa alieleza kuwa, Rais Magufuli aliwasili kituoni hapo majira ya saa 5 asubuhi, na miongoni mwa mambo aliyoyafanya ni kusikiliza changamoto zinazowakumba wafanyakazi wa shirika hilo.

“Rais alitembelea hapa majira ya asubuhi na alizungumza na wafanyakazi wa TBC. Ujio wake ulikuwa ni kwa lengo la kujua hasa changamoto tunazokabiliana nazo katika eneo letu la kazi,” kilisema chanzo hicho.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Mei 17, 2017

$
0
0


 Hapa tumekuanikia kurasa za mbele na za nyuma za magazeti yote ya Tanzania leo, Mei 17, 2017. Ni yale ya Hardnews, Udaku na Michezo.

WAMEBANA WAMEACHIA YANGA BINGWA, HAWA NDIYO YANGA IMESHINDA MECHI NYINGI VPL

$
0
0
 

HEBU piga picha, pale unapofikiri umening’inia kwenye mti na kuepuka shimo halafu ghafla mti unakatika na unatumbukia shimoni! Hivyo ndivyo alivyofanya straika Mrundi, Amissi Tambwe mbele ya mamia ya mashabiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana. Ilikuwa ni wakati Toto Africans wakiamini wamepata pointi moja muhimu mbele ya Yanga
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kubana weeee, lakini ghafla dakika za mwisho Tambwe akawararua na kupoteza matumaini yao ya kusalia kwenye Ligi Kuu Bara msimu ujao baada ya kichapo hicho cha bao 1-0.


Bao hilo la Tambwe lililiza watu wenye rangi mbili. Kwanza, ni wale wenye rangi nyekundu na pili, ni wale wenye rangi za njano za Kimwanzamwanza, kwani matokeo hayo yanamaanisha kuwa ubingwa kwa Simba sasa ni ‘byebye’. Hakuna tena nafasi kwa Simba kutwaa ubingwa msimu huu. Yanga wamefikisha pointi 68, wakiwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa huku kila timu ikiwa imebakiza mechi moja ligi iishe. Simba wana pointi 65 na sasa watalazimika kushinda zaidi ya mabao  12-0 katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mwadui, ikimaanisha kwamba hakuna tena ubingwa msimu huu walioukosa tangu mwaka 2012. 


Bingwa ni Yanga. Matumaini pekee ya Simba ni pointi tatu za mezani watakazozifuatilia Fifa lakini kama Yanga asiposhinda mechi ya mwisho dhidi ya Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Kama Yanga akishinda, pointi hizo zinakuwa hazina maana tena. Kwa upande wa Toto, ili kusalia ligi kuu, watalazimika kushinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Mtibwa kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro huku wakiombea wapinzani wao wote katika vita ya kuporomoka daraja, wasipate matokeo mazuri, vinginevyo ni kilio kwa Wanamwanza. Timu hiyo inabaki katika nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi 30. Bao la Tambwe alilifunga dakika ya 79 akiunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa na Juma Abdul. 

Bao hilo lilipatikana baada ya Yanga kulisakama lango la Toto kwa muda mrefu bila mafanikio. Tambwe sasa anafikisha mabao 11 kwenye chati ya wafungaji na amebakiza mabao manne amfikie Yanga mwenzake, Simon Msuva ambaye hakucheza jana kutokana na majeraha na kuna hatihati ya kucheza tena msimu huu. Baada ya mchezo huo, wachezaji wa Yanga walizunguka uwanja mzima wakishangilia ubingwa ambao dhahiri kabisa sasa ni wao

MADEGA ASIMULIA MWANAYE ALIVYOGONGA WATU NA BAADAYE KUWAWA AKIKIMBILIA DAR

$
0
0



Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Imani Madega amesimuliwa namna alivyopata msiba mkubwa wa kufiwa na mwanaye.

Mwanaye huyo anaitwa Omary Madega na amefariki baada ya kupata ajali akiwa anaendesha gari la Madega akijaribu kuwakimbia madereva bodaboda.
Omary anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 32, aliuawa wakati akiwakimbia bodaboda katika eneo la Chalinze mkoani Pwani akiwa anatumia gari la baba yake mdogo, Madega ambaye kitaalamu ni mwanasheria.
Akizungumza na Championi Jumatano, Madega aliyeonyesha masikitiko makubwa alisema gari lililosababisha ajali ni Mitsubushi Pajero, mali yake.
“Nina msiba mkubwa sana ndugu yangu. Nilisafiri kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze ambako nilipitiliza kwenye project yangu. Nikiwa huko gari lilisumbua.
“Nikamuita Omary ambaye ni mtoto wa kaka yangu aje alishughulikie. Alipofika pale alikuwa na fundi, akamchukua na mtu ambaye amekuwa akisimamia nyumba yangu ninapokuwa Dar es Salaam pamoja na Shamba Boy wangu.
“Wote wanne waliondoka kwenda kuifuata gari nilipoiacha. Walipofika haikuwa na tatizo kubwa, kawaida ikishapoa huwa inawaka, basi wakaichukua. Sasa si unajua vijana, wakaona waingie mtaani kidogo.
“Kama dakika 10 tokea waondoke, nikapigiwa simu kwamba Omary kagonga watu watatu pale sheli na inasemekama mmoja amepoteza maisha na alikuwa anabishana na madereva bodaboda. Mwisho aliondoa gari kasi kama akiendelea Dar es Salaam.

“Dakika 5 baadaye sijajua hata cha kufanya, nikapigiwa simu ile gari imepata ajali na Omary amefariki dunia pamoja na yule mtunza nyumba,” alisema Madega.


Kwa Mujibu Madega Omary amezikwa Jumapili, mtunza nyumba wake kazikwa juzi na mchungaji wake bado ana hali mbaya katika hospitali ya Tumbi kwa kuwa mguu wake umevunjika vibaya na unahitaji upasuaji.

Simba: Mpeni Msuva Tuzo Yake Ya Ufungaji Bora Bara

$
0
0

KOCHA Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja raia wa Uganda, amesema katika mbio za kuwania Tuzo ya Mfungaji Bora Bara msimu huu, anaona kiungo wa Yanga, Simon Msuva ndiye mwenye nafasi kubwa ya kuitwaa.

Mayanja amemtaja Msuva huku kiungo huyo akiwa ndiye kinara baada ya kufunga mabao 14 akifuatiwa na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting mwenye mabao 13, huku Mbaraka Yusuph wa Kagera Sugar na Obrey Chirwa kutoka Yanga wote wakiwa nayo 12. Takwimu hizo ni kabla ya mechi ya jana kati ya Yanga na Toto Africans. Akizungumza na Championi Jumatano, Mayanja alisema Msuva ana nafasi kubwa ya kuchukua tuzo hiyo kutokana na kujituma kwake uwanjani huku pia akiwa na uwezo wa kufunga mabao kwa njia yoyote ile.
 
“Ushindani mkubwa uliokuwepo msimu huu umesababisha washambuliaji wengi kufunga mabao machache kuliko msimu uliopita ambapo kinara alimaliza ligi akiwa na mabao 21, ukiangalia kwa sasa hali jinsi ilivyo, hakuna atakayeweza kufikia mabao hayo.

“Lakini ushindani wa kuwania tuzo ya ufungaji bora unaonekana kuwa ni mkali kwani ukiangalia orodha yao utagundua kuna wachezaji kama wanne wanaoshindania tuzo hiyo, lakini kwa upande wangu naona Msuva ana nafasi kubwa ya kuwa mfungaji bora msimu huu.

“Nasema hivyo kwa sababu ana uwezo wa kufunga kwa kichwa pamoja na kutumia miguu yote, lakini hata yule straika wa Ruvu Shooting (Abdulrahman Mussa), naye anakuja vizuri, hivyo Msuva nampa nafasi ya kwanza akifuatiwa na huyo wa Ruvu Shooting, nafikiri mwisho atapewa tu tuzo yake,” alisema Mayanja. Ikumbukwe kuwa, msimu uliopita, Amissi Tambwe wa Yanga ndiye aliyeibuka kinara wa ufungaji akifunga mabao 21, akifuatiwa na Hamis Kiiza aliyekuwa akiichezea Simba na kufunga mabao 19.
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>