Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

Aina 10 za Wanawake Zitakazofanya Maisha yako Kuwa Magumu

$
0
0
Katika kuangalia tabia za wanawake, nakuja na orodha ya wanawake ambao kama mwanamume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.

1. Mtumiaji
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.

2. Mwanamke asieomba msamaha
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Owk kwanza ni kuwa aina hii ya mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.

3. Mlalamishi
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.

4. Asiyejielewa
Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la. Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.

5. Anayetawala na kutotosheka
Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile ambavyo anavyotaka yeye. Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii ya mwanamke watakufanya bwegu muda unaposongea, yaani watakukalia kichwani na wao kujifanya mabosi.

6. Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote
Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani, bila hata kufikiria wenzao.

7. Nusa Nusa
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza mindoko yako. Unaweza kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu nk. Owk aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Kila anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana nayeye mara moja.

8. Asie na maono
Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke aina hii hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimmuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope
sana.

9. Mcheza ndondi
Hii ni aina ya mwanamke amabye anakasirika kwa haraka na akichukizwa na chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake ni vita. Aina hii ya mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.

10. Mtoto wa mama
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza wazazi wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu mwanamke aina hii hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake ndani yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kudhamini maoni yako kabla kuwauliza wazazi wake.

Diamond Kufulia, Tutasubiri Sana!

$
0
0
EDSON Arantes do Nescemento maarufu kama Pele ndiye mwanasoka anayetajwa kuwa na kipaji halisi cha kucheza kandanda kuliko wengine wote, ingawa Diego Amando Maradona amekuwa akiipinga dhana hiyo, akitaka dunia imtambue yeye kuwa ndiyo mwanasoka mwenye sifa hiyo.

Hata hivyo, soka ni mchezo wa kudumu na wachezaji ni watu wa kupita. Baada ya Pele kuitawala dunia enzi zake, alifuata Maradona, akaja Ronaldinho na Zinadine Zidane na sasa ni wakati wa Lionel Messi.
Hawa ni miongoni mwa binadamu wachache waliowahi kuamua waufanye nini mpira na kwa wakati gani. Ungeweza kuwa shabiki wa timu pinzani, lakini ukajikuta unainuka kushangilia wakati Ronaldinho Gaucho anapoamua kubadili uelekeo wa mpira katika namna isiyoelezeka.
Pamoja na upinzani unaotajwa kuwepo hivi sasa baina ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, lakini katika ukweli halisi, raia huyo wa Argentina anakosa mpinzani wanapozungumza kuhusu mtu mwenye mamlaka ya kuuamrisha mpira uwe vile anavyotaka mbele ya wapinzani wake.

diamondUtangulizi huu unamhusu Diamond Platnumz, kama tutaamua kuzungumzia Bongo Fleva. Kuna watu waliutawala kabla yake. Sugu pengine ndiye wa kwanza kuitawala Bongo Fleva kama solo artist, akaja Juma Nature, Afande Sele (kumbuka aliibuka kinara wa mkali wa Rhymes Bongo), Mr Nice na Ali Kiba.
Si kwamba hakukuwa na wasanii wengine waliosumbua kipindi chao, lakini wao ndiyo walikuwa alama ya Bongo Fleva. Na bahati mbaya, wengi wao hawakuweza kukitumia vizuri kipindi chao. Walitumia umaarufu wao kupata pesa nyingi kupitia shoo za majukwaani.
Wapo walioishia hapo, lakini kuna watu walitumia nyakati zao kutengeneza ‘connection’ zilizowawezesha kurekebisha maisha yao kiasi kwamba hata kama hawafanyi tena muziki wa kutegemea shoo, lakini maisha yao yapo ‘under control’.
Wakati Afande Sele akitwaa Taji la Mfalme wa Rhymes 2004, alikuwa hot cake, kila mtu alitaka afanye naye kazi na shoo zake zote zilijaza mashabiki kupita maelezo. Hakuna maneno yanayofaa kumzungumzia Mr Nice juu ya namna gani alikuwa ameiteka Bongo Fleva.
Ninapomtazama Diamond kama msanii, ninamuona ni mtu ambaye ametumia vyema wakati wake akiitawala Bongo Fleva kwa kujitengenezea msingi ambao utamfanya aingize mamilioni ya fedha, hata akiacha kukamata mic. Kwanza alijitahidi kulifanya jina lake liwe brand barani Afrika, kitu ambacho amekimudu kwa ufanisi mkubwa.
Leo hii, siyo rahisi kuifikia Afrika ya burudani ambayo haimjui Diamond. Baadhi ya wasanii wetu wanafahamika huko nje kwa sababu sasa muziki wetu unafuatiliwa kwa sababu yake.
Amesajili lebo ambayo hivi sasa ndiyo kubwa hapa nchini, WCB. Kuna lebo nyingi, lakini bila shaka, licha ya uchanga wake, hii iko ‘active’ na ndiyo maarufu zaidi. Ina wasanii wanne, Rich Mavoko, Harmonize, Raymond na Queen Darleen.
Ametumia mamilioni ya shilingi kununua vifaa vya muziki vya kisasa kabisa. Hivi sasa ana bendi yake ambayo akipanda nayo jukwaani, nyimbo zake zinapigwa katika ubora uleule ambao unakuwepo kama ataweka CD.
Amewatengeneza wasanii wake. Ukimuacha Mavoko, ambaye ni msanii mkubwa hata kabla hayupo WCB, wengine wote wamekuzwa na Diamond na leo hii, wanaweza kufanya shoo ya peke yao na kujiingizia mamilioni.
Haufanyi muziki kama kitu cha kumpatia sifa ili awapate wasichana kirahisi, bali anaufanya kama kazi nyingine zilivyo. Ndiyo maana anakesha studio, akijaribu kufanya kila aina ya muziki na kote amefaulu.
Zipo tetesi kuwa Vodacom wameingia mkataba na Diamond ili kufanya Wasafi Tour katika mikoa 10. Endapo itafanikiwa, yeye ataingiza fedha mara mbili, kwanza kama msanii lakini pia kama bosi wa kampuni yake.

Kama hili litakuwa ni tetesi sawa, lakini namuona Diamond akiingia mkataba na kampuni moja kubwa kwa ajili ya kitu kama hiki miezi si mingi ijayo. Ikifanyika hivi, maana yake ni kuwa atakuwa amebuni kitu cha kudumu, ambacho kinaweza kufanyika kila mwaka.
Katika dunia inayobadilika kuhusu haki za wasanii, kama kasi yake itaendelea kama dalili zinavyojionyesha, uhai wa Diamond kimapato ni wa milele.


Badala ya mashabiki pinzani kumuombea mabaya, wakimtolea mfano wa waliowahi kuwika na kupotea, Diamond awe mfano wa jinsi wasanii wa Tanzania wanavyoweza kufanikiwa na kuzalisha ajira kwa ustawi wa taifa letu. Kupitia muziki, kijana huyu ameajiri vijana watanzania 42, wakiwemo wa kudumu na part time, vipi tukiwa na wasanii kumi kama yeye?


Makala: Risasi Vibes; Risasi Mchanganyiko, Jan 4-6, 2017, Toleo 1388

Wanaume Tata Wamtisha Gigy Money

$
0
0

WANAUME wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, maarufu kama wanaume tata, wamemtisha Video Queen wa Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kiasi cha kusababisha kuwatangazia hatari endapo wataendelea kummendea mpenzi wake.


Akipiga stori na Risasi Vibes, Gigy Mwoney alisema wanaume hao tata wamekuwa wakimtumia mtu wake huyo aitwaye Moj, meseji za kumtaka kimapenzi hali ambayo inamchefua na kuamua kuwatangazia kwenye mitandao ya kijamii kuacha mara moja.
“Nawatangazia tena wanaume tata wanaomtaka mpenzi wangu kimapenzi, waache mara moja maana nilishawapa tahadhari na wengine wameacha vinginevyo nitawataja hadharani maana ninawajua na wamekuwa wakimtumia sana meseji,” alisema Gigy Money.

Ningekuwa Diamond nisingejiita simba – Darassa

$
0
0
Hit maker wa wimbo ‘Muziki’ Darassa ameweka wazi maana ya ule mstari wake wa “sio simba, sio chui, sio mamba” kwa kusema Diamond hakupaswa kujiita simba kwani simba ni mnyama ambaye anaweza kuuliwa anapozidiwa nguvu.

Darasa amedai Diamond ni msanii ambaye amehangaika sana kutoka kimuziki hivyo mafanikio yake na uwezo wake wa muziki alitakiwa ajiite jina lingine kwa kuwa Daimondi ni zaidi ya Simba kwa sasa kwani ni zaidi ya mnyama Simba.

“Ningekuwa Diamond nisingejiita simba,” Darassa alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Ninavyomuona Diamond ni zaidi ya Simba, kuna watu wanaua simba, simba, kajichanganya, kaingia kijijini kapotea, Diamond kwa kitu anachofanya ni zaidi ya simba, angeweza kujiita jina lingine lolote kubwa, kafanya vitu vingi sana,”

Pia rapper huyo alidai wanyama wote ambao amewataja katika wimbo wake hawaogopi kwa kuwa ana kitu kikubwa ndani yake na yeye ni mwanaume na anajiamini kwa muziki wake anaofanya.

“Kwa upande wangu nimesema siyo simba, siyo chui siyo mamba, mamba ni mnyama anayetisha sana kwenye maji, simba anatisha sana porini, chui ni hunter mzuri, so katika vitu vyote ambavyo viko humo, mimi humo kote simo, ninacho kitu ambacho kinaweza kunifanya nikwambie aaaaah”. Amemalizia Darassa

Godbless Lema Arudishwa Tena Gerezani, Ni Baada ya Serikali Kuwasilisha Notisi Ya Kupinga Dhamana yake Mahakama ya Rufaa

$
0
0
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, leo imeshindwa kusikiliza rufani ya Jamhuri dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupinga dhamana yake, baada ya mawakili wa Serikali kuwasilisha notisi ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa wakipinga kusikilizwa kwa rufani hiyo .

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Salma Maghimbi   alitarajiwa kutoa uamuzi juu ya rufaa ya Jamhuri iliyopinga  Lema kupatiwa dhamana Novemba 11 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Desderi Kamugisha katika kesi namba 440 na 441/2016 ya kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli, ambapo siku hiyo Jamhuri iliwasilisha notisi ya mdomo.

Baada ya Lema kufikishwa mahakamani saa 3.25 asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali, huku pia polisi wakiwa wametanda viwanja vya Mahakama Kuu ndani na nje sanjari na gari moja la maji ya kuwasha, baada ya  mawakili wa pande zote kujitambulisha Jaji Maghimbi alisoma notisi ya Jamhuri kupeleka shauri hilo Mahakama ya Rufaa na kueleza kufungwa kisheria kutoa uamuzi wa rufani hiyo.

Magaeti Ya Tanzania Leo Alhamisi ya January 5, 2016

ALL GOALS: Zimamoto vs Yanga January 4 2017, Full Time 0-2

$
0
0


January 4 2017 Dar es Salaam Young Africans ilicheza mchezo wake wa pili wa Mapinduzi Cup 2017 dhidi ya Zimamoto katika uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar, Yanga katika mchezo huo walifanikiwa kuifunga Zimamoto goli 2-0, magoli yakifungwa na Simon Msuva dakika ya 11 na 21.

Jike Shupa Awaanika Mastaa Anaowauza Kwa Vigogo, Yumo Wolper, Masogange

$
0
0

DAR ES SALAAM: Imefichuka! Wakati mastaa mbalimbali wakijinasibu mara kwa mara kupitia vyombo vya habari kuwa hawafanyi biashara ya kuuza miili yao kama inavyodaiwa na baadhi ya watu, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ amekiri kuwauza wenzake kibao kwa vigogo, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza kukujulisha.

Jike Shupa ambaye ni ‘video queen’ kwenye nyimbo mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva, bila kujijua, amejikuta akiingia kwenye mtego wa kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers na kutaja idadi ya mastaa huku akieleza kila msanii ana dau lake tofauti, hakuna bei maalum.

ILIKUWA HIVI

Baada ya OFM kupata habari kutoka kwa vyanzo vyake mbalimbali kwamba mwanamama huyo anawauza wenzake, wakiwemo mastaa na kudaiwa kuwa ni kinara mkubwa wa biashara hiyo, OFM iliingia mzigoni na kupata majibu chanya.



AANZA KUINGIZWA KINGI

Makachero wa OFM waliwasiliana na Jike Shupa na mmoja wao akamuomba waonane ili aweze kupata huduma ya kuunganishwa na msanii atakayepatiana kwa bei ya wastani.

Jike Shupa baada ya kuelezwa hivyo alimuomba kachero huyo aliyejitambulisha kwake kama mfanyabiashara kuwa wakutane maeneo ya Kinondoni kwenye mgahawa mmoja maarufu majira ya saa moja usiku ili waweze kuzungumza vizuri kuhusu dili hilo.

OFM YAWAHI KUFIKA MGAHAWANI

Saa moja usiku kachero wa OFM alikuwa katika eneo la tukio, alipofika kwenye mgahawa huo alikaa na kumsubiri Jike Shupa ambaye aliingia na vijana wawili aliowatambulisha kuwa ni wadogo zake, ikiwa ni dakika 15 zaidi ya muda wa makubaliano.

OFM: Karibu sana Jike Shupa.

Jike Shupa: Asante, umenisubiri sana eeeh?

OFM: Yeah, lakini siyo tatizo.

Jike Shupa: Pole sana.


Baada ya Jike Shupa kukaa na mhudumu kumsikiliza anachohitaji (OFM ililipia bili yote), mazungumzo kati yake na OFM yalipamba moto na baada ya muda, alielezwa moja kwa moja kuwa dili alilotaka kumpa lilikuwa ni kumpata Amber Lulu ili awe naye kimapenzi, jambo ambalo lilionekana kuwa jepesi mno kwa Jike Shupa.

ATANGAZA DAU

Jike Shupa alimhoji OFM kama alikuwa na fedha za kutosha maana kazi yake yeye ‘anadili’ na watu wenye fedha tu na kwa kumuuza Amber Lulu, alisema atachukua shilingi milioni moja na nusu ikiwa ni nje ya fedha ambazo Amber Lulu atataka kulipwa.

‘MFANYABIASHARA’ FEDHA SI TATIZO

Kuonesha kwamba fedha si chochote, kachero wa OFM hakubisha juu ya hilo, alichofanya ni kumwambia kuwa nusu ya fedha alizokuwa anahitaji  angemlipa muda mchache wakati wakiendelea na mazungumzo, lakini akataka kujua kutoka kwa mwanamke huyo kama amewahi kuwauza mastaa wengine kama anavyofanya kwa Amber Lulu?


Jike Shupa: Wako wengi tu, ambao huwa ‘ninawa-connect’ (kuwaunganisha) na mabwana, mfano, (akataja jina la msanii mkubwa ambaye tunahifadhi jina lake kwa sababu hatukumpata), Tunda, Masogange, Wolper na wengine wengi.

ETI HAKUNA ANAYEMCHOMOLEA

“Hakuna staa wa kike ambaye simfikii, ni wewe tu kusema unamtaka yupi, unatoa pesa halafu mimi namaliza mchezo wote.

“Unawaona hata hao vijana niliokuja nao (anawanyooshea kidole walipokuwa wamekaa)? Hao ni mashoga, huwa nawaunganishia watu (wanaume) wanaowataka kufanya nao mapenzi.”


OFM YAMMWAGA KIAINA

Baada ya OFM kukamilisha upelelezi wake na kujiridhisha kuwa kweli Jike Shupa ni kuwadi na anawauza wasanii wenzake wa kike pamoja na mashoga kwa mapedeshee, ilimtoka ‘kisanii’ mwanadada huyo huku ikiwa na ushahidi wa kutosha.

WATUHUMIWA WAFUNGUKA

Alipotafutwa Masogange na kusomewa mashitaka yake, awali alianza kwa kusema hana urafiki kivile na Jike Shupa na kwamba waliwahi kukutana naye mara moja tu.


“Sina urafiki kivile, nachukia sana mtu kuzungumza kitu ambacho sijafanya, kwanza huyo Jike Shupa mwenyewe hana mtu wa kuniunganisha naye. Hebu ngoja nimpigie sasa hivi nimpe vidonge vyake, sipendagi ujinga mimi,” alisema Masogange na baada ya kumpigia na kumkosa, alimuandikia meseji ndefu Jike Shupa ya kumsuta ambayo aliikopi na kuipiga picha kisha kumtumia mwandishi wetu.

Jike Shupa hakujibu ujumbe huo wa kichambo ambao ulionesha umefika kwenye simu yake.

AMBER LULU NAYE ANENA

Kwa upande wake Amber alikanusha vilivyo madai hayo ya kuuzwa na kama haitoshi, alisema hana hata urafiki naye.

“Huyo labda anatafuta kiki, sina hata urafiki naye ataniuza kivipi? Sinaga hizo habari,” alisema Amber.


WOLPER NAYE AMKANA

Alipotafutwa Wolper na kuelezwa kama amewahi kupigwa bei na Jike Shupa, alimkana kuwa hamtambui na kusema anaomba atumiwe picha ili japo amuone anafananaje, kwani watu wa aina hiyo anashindwa kuwaelewa awaweke kwenye kundi gani.

“Unajua kama ana akili timamu si mwezi mchanga, inabidi nidili naye na ikiwezekana nimshtaki maana atakuwa amenizushia jambo ambalo sijawahi kulifanya lakini kama ni mwezi mchanga (hajakamilika kiakili), naweza nikamsamehe,” alisema Wolper.

MASTAA ZAIDI WAFUNGUKA

Mastaa wa kike mbalimbali walipotafutwa na kuelezwa habari hizo kila mmoja alionesha kukasirika na kuzungumza lake.


BABY MADAHA

“Huyo Jike Shupa hawezi kuniuza mimi labda hao anaoonana nao na suala la kuuzwa ni la mtu binafsi huwezi kuuzwa kama ng’ombe.

“Huyo msanii ana uwezo wa kuwauza wale anaowamudu kwangu atagonga mwamba kwani hatuongei lugha moja, yaani viwanja ninavyoenda ni tofauti na vyake, wanaume anaokutana nao ni tofauti na wale nitakaokutana nao mimi, kwanza Kinondoni na Mbezi ni wapi na wapi?”

SHAMSA FORD

“Mimi nimeolewa hilo haliwezi kunitokea kabisa waulizeni hao ambao hawaeleweki nina mume ndani tayari.”

ISABELA MPANDA

“Huyo Jike Shupa hawezi kuniuza kwa sababu ninajitambua labda hao wengine na sina shida na siwezi kuuzwa kama karanga, huwa naenda kwa mwanaume ninayemtaka.”

ROSE NDAUKA

“Jamani hivyo ni vitu vya kipumbavu siwezi kuvizungumzia wala kumzungumzia mtu kama huyo.”

NENO LA MHARIRI

Kwa kuwa OFM imemnasa Jike Shupa ‘live’ akithibitisha madai ya kuwa anawauza wenzake, anapaswa kuachana na vitendo hivyo mara moja kwani vinakwenda kinyume na mila na desturi za Kitanzania.

Ni tabia ambazo zinakwenda kinyume na mafundisho ya imani za dini zote, ni wakati wa Jike Shupa na mastaa wenzake wote wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kikahaba kuachana navyo na kutafuta mkate wa kila siku kwa njia halali.

Stori: waandishi Wetu, Risasi Mchanganyiko, Jan 4-6, 2017, Toleo 1388

Jeshi la Polisi Laua Majambazi Watatu Dar es Salaam

$
0
0
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameuawa katika tukio la kurushiana risasi na polisi katika eneo la Mikocheni, karibu na Shule ya Sekondari Feza jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro watuhumiwa hao waliuawa jana asubuhi na majina yao bado hayajafahamika.

Alisema marehemu hao ni waliohusika katika tukio la kupora zaidi ya Sh milioni 26 katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere, eneo la Tazara, Dar es Salaam.

Hata hivyo, alipoulizwa ufafanuzi zaidi wa tukio hilo na je watuhumiwa hao walikuwa na usafiri gani, Sirro alisema kuwa hizo ni taarifa za awali na taarifa rasmi atazitoa leo.

Alisema kwamba miili ya marehemu, imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 
Taarifa zaidi zinadai kwamba watuhumiwa hao akiwemo mwanamke aliyejisalimisha, ambaye ndiye alikuwa dereva wao, walikuwa na mpango wa kufanya uvamizi katika maeneo hayo, ambapo pia baadhi yao walifanikiwa kukimbia.

Lakini, Polisi haijathibitisha taarifa hizo na imeeleza kuwa itatoa taarifa  zaidi leo. 

Wolper atumia Instagram kumpiga chini Harmonize

$
0
0

Kwenye post hiyo iliyokuwa na picha ya Harmonize pamoja na emoji za alama ya kopa iliyopasuka, Wolper ameandika: Nina akili timamu me syo mtoto mdogo, endelea na maisha yako it over waambie rasmi usifiche @harmonize_tz i hate love.”

Looks like Harmonize kauvunja moyo wa Wolper kiasi cha kuamua kuyachukia mapenzi kiasi hicho! 

Ujauzito Feki wa Nisha Wamsababishia Haya

$
0
0

Mcheza filamu maarufu katika soko la filamu Bongo Movie, Salma Jabu, maarufu kama Nisha Bebee amejipotezea uaminifu mtaani anapoishi na jamii nzima inayomzunguka kwa kitendo cha kuudanganya umma mwishoni mwa mwaka 2016.

nishaaaajNisha aliibuka na kudai kuwa ni mjamzito na ujauzito huo aliupata kutoka kwa mmoja wa wasanii wa Bongo Fleva kwa kubakwa. Habari ya ujauzito wa Nisha ilipata mashiko kwa jamii kwani ilithibitishwa na Nisha mwenyewe katika mahojiano katika kipindi cha XXL cha Clouds FM mwisho mwa mwaka jana.nishaWakazi jijini Dar es Salaam wamedai ya kwamba kitendo alichofanya Nisha si sahihi kwani huwezi kuudanganya umma kwa jambo kubwa kama hilo la ujauzito. Wakati Nisha anakanusha kuwa hakuwa mjamzito ingetokea taarifa za kutupwa mtoto sehemu basi jamii ingejua wazi Nisha ndiye aliyetupa mtoto. nishaa

nishabebeeHivyo kwa jambo hilo si busara na pia ni hatari sana kutafuta umaarufu kwa njia za udanganyifu. Kwa sasa Nisha anaonekana kama muigizaji tu hata katika maisha halisi. Mfano akifika msibani anaonekana kama amefika kuigiza tu wala si hashiriki shughuli za kijamii.

WANAOWAMALIZA CHID BENZ, NANDO NI HAWA

$
0
0




WIMBI la vijana kuzidi kutopea kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya ‘unga’ linazidi kuwa kubwa na safari hii, upepo mbaya umewakumba mastaa wa tasnia mbalimbali Bongo ambapo hali za kiafya za wasanii kama Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ na mwakilishi wa Tanzania kwenye Shindano la Big Brother, Ammy Nando zinasikitisha, chanzo kikiwa ni unga huo.
Picha zinazosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, zinawaonesha Chid Benz na Nando wakiwa taabani kiafya kiasi kwamba kama ulikuwa unawajua enzi za ‘uzima’ wao, leo unaweza kuwapita barabarani bila kuwatambua! Wamechoka, wanatia huruma.

MAGUFULI AOMBWA KUINGILIA KATI
Ni kutokana na hali za wakali hao ambao walikuwa wakifanya vyema hapo awali kabla ya kutumbukia kwenye safari ya mauti ya matumizi ya madawa ya kulevya, wadau mbalimbali waliozungumza na gazeti hili, wamepaza sauti kwa Prezidaa Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’  wakiuliza kwa nini yupo kimya wakati nguvukazi inateketea?
“Kwa kasi ya utendaji kazi wake, naamini Rais Magufuli hashindwi kufanya jambo kumaliza kabisa hili tatizo linalomaliza nguvu kazi ya taifa kila kukicha,” alisema msomaji mmoja wa Amani aliyejitambulisha kwa jina la Hamis Nandozi, mkazi wa Kimara Suka.

WANAOWAMALIZA CHID BENZ, NANDO NI HAWA
Nandozi alisema kuwa, mbaya zaidi wanaomuuzia unga Chid Benz wanafahamika, waliomharibu  Nando wanafahamika na wanaowamaliza vijana mitaani pia wanafahamika. Why (kwa nini?) hawachukuliwi hatua? Tunamuomba Rais Magufuli aingilie kati sakata hili, anaweza kwa kuwa ndiyo mambo anayoyapatia sana ya kutatua kero za watu. Hii nayo ni kero.”
MAJINA YA WAUZA IKULU
Nandozi akaendelea: “Mimi nakumbuka niliwahi kumsikia rais aliyetangulia, Dk. Jakaya Kikwete ‘JK’ akisema kwamba wauza unga wote anawafahamu na tayari orodha ya majina yao ipo mikononi mwake. Mimi namuomba Rais Magufuli aipitie ile orodha kwa kuwa naamini JK hakuondoka nayo, awashughulikie wauza unga wote, wanaotuharibia vijana wetu.”

POLISI WABEBESHWA LAWAMA
Msomaji mwingine mkazi wa Shinyanga, Mathayo Kapalatu alisema kuwa, anawatupia lawama polisi kwa vile wao wana uwezo wa kuwasaka wauza unga na kuwatokomeza kwa kuwa mtandao wanaujua.
Alisema: “Polisi wanajua mpaka gari likiibwa, nani kaiba kwani wanajua wezi wa magari ya kifahari wako wapi, wezi wa magari makubwa wako wapi! Polisi wanajua wapi kunauzwa gongo, wapi kunauzwa unga, wapi kunauzwa bangi. Polisi wanajua hata kibaka akikata wavu wa dirisha, ule ukataji tu wanajua ni nani, sasa wanashindwaje jamani kuumaliza mtandao wa wauza unga?” 

CHID BENZ
Ni mkali wa ngoma ya Dar es Salaam Stand Up, inadaiwa kwamba alianza kutumia madawa ya kulevya karibu miaka minne iliyopita lakini haikuwa rahisi kwa watu wa nje kumgundua, kwa sababu bado alikuwa anajimudu.
Hata hivyo, mambo yalianza kubumburuka Oktoba 24, 2014 alipokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa safarini kuelekea Mbeya ambapo alikutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin yenye thamani ya shilingi 38,638 na bangi ya shilingi 1,720.
Aliburuzwa Mahakama ya Kisutu, Dar na kupigwa faini ya shilingi 900,000 na kuachiwa huru. Kuanzia hapo akawa hawezi kujificha tena, aliendelea kutumia unga ambao ulimfanya ‘akongoroke’ mwili, ule ubabe wake na mwili mkubwa aliokuwa nao, vyote vikayeyuka kama theluji iyeyukavyo juani.
Hali yake kwa sasa inasikitisha, anashinda mitaa ya Kinondoni, akiwa amepoteza kabisa unadhifu wake, kama unatembea na taswira ya yule Chid Benz wa kipindi kile, aliyekuwa anajiita King Kong, sasa amebadilika kabisa na kuwa mtu mwingine tofauti.
Juhudi zilizofanywa na Babu Tale na Kalapina na wengine, za kumpeleka sober house (nyumba ya kuwasaidia waathirika wa unga) zimegonga mwamba, ‘gari’ limewaka na hakuna wa kulizima mpaka Mheshimiwa Rais Magufuli atakapoamua kuingilia kati suala hilo.
Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba alimtembelea mama yake Chiz Benz nyumbani kwake, Chanika wilayani Ilala, Dar kujaribu kuangalia namna ya kumsaidia kijana wake, lakini mpaka gazeti hili linaingia mitamboni, bado Chid Benz yupo mitaani akiendelea kujimaliza kwa kula ngada!

AMMY NANDO
Nando ni mwakilishi wa Tanzania kwenye Shindano ya Big Brother Africa 2013, ambaye alitolewa mjengoni baada ya kuhusika kwenye ugomvi mpaka kufikia hatua ya kumtishia mwenzake kisu, hali yake ni taabani kwa sasa! Huwezi kuamini kwamba ndiye yule ‘handsome boy’, aliyekuwa akipapatikiwa na wanawake.
Nimewahi kufanya kazi kwa karibu na Nando, kipindi alichokuwa akifanya kazi ya uandishi wa habari mtandaoni. Nikiri kwamba ni miongoni mwa vijana wenye uelewa mkubwa mno! Anajua vitu vingi kuhusu teknolojia, historia, sanaa na mambo mbalimbali yanayoendelea duniani kote.
Makala zake alizokuwa akiandika ni ushahidi tosha wa  karama kubwa aliyojaliwa na Mungu. Hata hivyo, tangu awali alionesha kutokuwa sawa kwenye suala zima la matumizi ya vilevi. Alianza kama masihara, muda mwingi akipenda ‘kubugia’ pombe kali na kuvuta sigara, wakati mwingine hata wakati wa kazi.
Lakini kumbe ndiyo safari ilikuwa imeanza. Hakuishia hapo, akajiingiza kwenye mdomo wa mamba na kuanza ‘kula mambo’! Picha yake inayosambaa mtandaoni, imewashtua wengi, nikiwemo mimi. Ni vigumu kuamini kwamba ndiye yule Nando ninayemjua! Unga umemsambaratisha kabisa na kuua kipawa chake. Naamini Magufuli hawezi kukubali vijana ambao ni ‘taifa la leo’, wakiangamia hivi. Lazima atafanya kitu.
Hata hivyo, naamini Nando hajafikia hatua ya kuwa ‘chronic’ kihivyo, anaweza kusaidiwa na akarudi kwenye hali yake ya kawaida kwani hata watu wake wa karibu wanaeleza kwamba, akiwa hajapata mambo, anajitambua!
“Lakini kumsaidia yeye pekee haitoshi kwa sababu wapo vijana wengi nyuma yake, wanaopitia mapito kama yake! Dawa pekee ni kuwadhibiti wauza unga wanaowaharibu vijana hawa! Magufuli, where are you?” alisema msomaji mwingine, Salehe Njuguna, mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam.

RAY C
Jitihada za rais wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete za kumsaidia Ray C ziligonga mwamba! Mwanadada huyu ambaye enzi zake alikuwa akisifika kwa jina la Kiuno Bila Mfupa kutokana na wimbo alioutunga kutamba enzi hizo, anaangamia. Licha ya mara kadhaa kujitokeza hadharani na kukiri kuacha kutumia madawa, kuna wakati aliendelea mpaka hivi karibuni ilipodaiwa ameacha na anajipanga kurudi kwenye gemu.

USHAURI KWA SERIKALI
“Mimi ushauri wangu, hawa wauzaji waundiwe sheria kali kama ilivyo nchi nyingine. Unajua China ukikamatwa na madawa ya kulevya, hakuna kumung’unya maneno ni kitanzi tu. Natamani hiyo sheria ije Bongo, vijana wetu wanaangamia wakati wauzaji wanabadilisha tu magari ya kifahari kila siku, leo Benz, kesho Vogue, keshokutwa BMW, lakini akina Chid wao tunawahesabia siku za kuishi, hapana! Inatosha sasa, Magufuli aingilie kati,” alisema mzee Juma Msongo, wa Temeke jijini hapa.
Akaendelea: “Hivi inashindikana nini polisi kuingia mtaani na kuwakamata akina Chid ili waende wakaonesha wanaponunulia madawa ambao nao wataonesha kwa mawakala wao wakubwa mpaka wa kwanza kabisa? Mbona rahisi tu.”
 

Na Waandishi Wetu, Gazeti la Amani, Januari 5-11 | 2016 Toleo Na 946

VIDEO: MWIGULU NCHEMBA AONYA WAKULIMA NA WAFUGAJI, KUMWAGA DAMU NI KUITAFUTA LAANA

Gigy Money: Kama Ukimwi, basi Kiba Lazima... Soma hapa ujionee kafunguka

$
0
0


Video queen matata ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha redio moja jijini hapa, Gift Stanford ‘Gigy Money’, ametema cheche akisema kuwa, watu wote wanaomsema kwamba kutokana na kuvaa nusu utupu na kujiachia na midume mbalimbali huenda ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi, waache kwani kama ni kweli basi wengi wangekufa kwa sababu ameshatembea na mastaa kibao Bongo.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Gigy alisema kwamba amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa mbalimbali wakubwa Bongo akiwemo Mbongo Fleva, Ali Kiba na kudai kuwa, kama kuambukizwa virusi angeanza yeye na wengine wangefuata.

“Unajua watu wanashangaza sana. Kama mtu ana virusi vya Ukimwi hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu anayempenda, ningependa watu waache unyanyapaa. Ninachojua mimi sina Ukimwi kwa kuwa nilipima kwa shinikizo la mpenzi wangu wa sasa (Moulad Alpha ‘Moj’) na watu niliotembea nao wanaendelea vizuri tu, wengine wachumba zao wananyonyesha,” alisema Gigy.

Video queen huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, kuvaa nusu utupu ni kitu anachopenda kufanya toka ndani ya moyo wake hivyo hakuna mtu wa kumwambia kitu au kumkataza hata siku moja na wala siyo mgonjwa wa akili bali anafanya kitu kujifurahisha nafsi yake si ya mtu mwingine.


“Mimi nasikilizaga moyo wangu unasema nini, si mtu anasema nini juu yangu hivyo kama kuvaa nusu uchi wana hofu na mimi waondoe hilo kwa maana kama ni Ukimwi wengi wangeondoka siku nyingi kwenye ramani ya dunia hii maana hakuna niliyemuacha kwa mastaa unaowajua,” alisema Gigy kwa kujiamini.
Gigy ameshatoka kwenye magazeti mbalimbali akidaiwa kutembea na mastaa kama Hemed Suleiman ‘PHD’, Richard Martin Lusinde ‘Rich Mavoko’, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Seif Shaban ‘Matonya’ na Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.


Mwingine aliyewahi kutajwa ni Mtangazaji Gardner G. Habash ‘Captain’ na Mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan.

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humprey Polepole atangaza neema kwa Wanafunzi waliokosa mikopo

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humprey Polepole amewatangazia neema wanafunzi wa elimu ya juu waliokosa mikopo, akiwataka wamtafute ili awaoneshe cha kufanya

Polepole ambaye alikuwa kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV  aliuzwa na baadhi ya watu kuhusu tatizo lililopo la mikopo ya elimu ya juu, ambapo aliwajibu kuwa serikali imekwishatoa maelekezo kwamba haiwezi kumkopesha kila mtu na kwamba inatoa mikopo kwa vigezo vilivyowekwa.

Kuhusu watu wasioweza kujigharamia elimu hiyo na wamekosa mikopo, amewashauri kuahirisha masomo yao, ili wafanye kazi ambazo zitawasaidia kupata pesa na ndani ya mwaka mmoja ana uhakika watakuwa wamepata pesa zinazohitajika na kuendelea na masomo yao.

Polepole alitaja baadhi ya shughuli ambazo angewashauri wazifanye kuwa ni pamoja na kilimo huku akitolea mfano baadhi ya watu aliowashauri wajiingize kwenye kilimo cha matikiti na wakaufanyia kazi ushauri huo, ambapo baada ya muda wameona matunda yake.

"Waliokosa mikopo vyuo vikuu wanitafute, nitawaonesha cha kufanya, na wawe tayari kuahirisha masomo mwaka mmoja"

Akizungumzia uamuzi wa serikali kusimamisha ajira, Polepole amesema serikali haiwezi kuendelea kuajiri wakati inafanya kazi ya kuondoa wafanyakazi hewa ambao wanalitia hasara taifa na kuwataka watanzania waendelee kuwa watulivu na kumuunga mkono Rais Magufuli, ili amalize mchwa wote serikali na kisha ajira zitatoka.

"Nawaambia vijana wakati unasubiri ajira usibweteke kwani mtu anayebweteka akipata kazi ataharibu kazi yetu"

Kuhusu serikali kuajiri walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati pekee, Polepole amesema uamuzi huo ni sahihi kwa kuwa taifa lina uhaba mkubwa wa walimu wa Sayansi na Hisabati kuliko walimu wa masomo ya sanaa.

"Tunao utimilifu wa walimu wa sanaa, tunao upungufu wa walimu wa Sayansi"

Waziri Mkuu Aagiza Akiba Ya Mahindi Iliyopo Iendelee Kutunzwa

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua maghala ya nafaka yanayomilikiwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea na kuagiza akiba ya mahindi iliyopo iendelee kutunzwa hadi msimu ujao wa mavuno.

Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Januari 4, 2017) wakati akizungumza na baadhi ya watumishi wa NFRA Kanda ya Songea pamoja na viongozi na watendaji wa mkoa wa Ruvuma mara baada ya kukagua akiba ya nafaka iliyomo kwenye maghala ya kituo hicho.

Waziri Mkuu alisema mabadiliko ya tabia nchi yamefanya mvua zichelewe kunyesha katika mikoa mingi nchini ukiwemo mkoa wa Ruvuma ambao kwa kawaida mwezi Januari mvua ya kutosha inakuwa imeshanyesha na huwa kuna baridi nyingi.

“Angalieni ninyi wenyewe hali ya joto iliyopo hivi sasa, kwa kawaida mvua ingeshaanza kunyesha mwezi huu na mahindi yangekuwa yameanza kurefuka. Lakini hadi leo (jana) naambiwa mvua imenyesha mara mbili tu na mahindi yaliyopandwa yameanza kunyauka.”

“Kama mvua haijanyesha hadi leo, ni lazima tuchukue tahadhari, na hata mvua ikija hatujui itaendelea kunyesha hadi lini na kwa kiasi gani. RC, Ma-DC na ma-DED toeni elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa akiba ya chakula. Waambieni waachane na ngoma za unyago na sherehe za kipaimara ambazo hutumia kiasi kikubwa cha chakula,” alisisitiza.

“Msiruhusu kutoa mahindi yaliyopo na kuyauza. Hizo tani 10,500 zilizopo ziendelee kuhifadhiwa hadi tutakapoamua vinginevyo,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa NFRA Kanda ya Songea, Bw. Majuto Chabruma alimweleza Waziri Mkuu kwamba msimu huu walipanga kununua tani 22,000 za mahindi kutoka kwa wakulima lakini hadi kufikia Desemba 31, 2016, wamefanikiwa kununua tani 10,335.3 zenye thamani ya sh. bilioni 5.28.

Alisema kanda ya Songea ni miongoni mwa kanda saba zilizo chini ya NFRA ambayo inahudumia mkoa wa Ruvuma. Alizitaja kanda nyingine zinazohudumia mikoa yote nchini kuwa ni Arusha, Kipawa, Dodoma, Shinyanga, Makambako na Sumbawanga.

“Kanda ya Songea inayo maghala sita yenye uwezo wa kuhifadhi ytani 29,000 za nafaka. Lakini hivi sasa kanda hii imeingizwa kwenye Mpango wa Kuongeza Uwezo wa Hifadhi (NFRA Storage Expansion Project) na lengo la Wakala ni kufikia uwezo wa kuhifadhi tani 700,000 ifikapo mwaka 2020,” alisema.

“Kanda ya Songea tumenunua viwanja viwili vyenye ukubwa wa mita za mraba 16,986 ambapo zitajengewa silos 12 zenye uwezo wa kuhifadhi tani 46,000 na maghala mawili yenye uwezo wa kuhifadhi tani 5,000 kila moja na hivyo kuwa na ongezeko la tani 56,000 mradi huu utakapokamilika.”

Alisema kukamilika kwa mradi huo, kutaiwezesha kanda ya Songea kuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 85,000 ndani ya maghala na vihenge kutoka tani 29,000 za sasa.

Alipolizwa ni kwa nini hawajaweza kutimiza tani zote walizojipangia kununua, Bw. Chabruma alisema kuimarika kwa barabara za mkoa huo kumetoa changamoto kwa wakala kwani wananchi walianza kuuza mahindi kabla ya msimu wa ununuzi haujaanza (kawaida ni Julai mosi kila mwaka).

“Kuimarika kwa barabara za mkoa kumesaidia kufungua biashara na mikoa ya jirani na hivyo kuwawezesha wakulima wa Ruvuma kupata soko nje ya mkoa kabla NFRA haijaingia sokoni na kuanza kununua nafaka kwa wakulima vijijini,” alifafanua.

Alisema changamoto nyingine inayowakabili ni ubora hafifu wa nafaka kutoka kwa wakulima ambao alisema ni tatizo tangu hatua za awali za uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara. 
“Ubora hafifu wa zao la mahindi ulionekana zaidi kwenye nafaka zilizooza, punje zilizovunjika, wadudu hai, rangi mchanganyiko na takataka,” alisema.

Waziri Mkuu leo anatembelea wilaya ya Songea na kukagua kituo cha kupoozea umeme katika kijiji cha Mtepa, atakagua kituo cha afya cha Madaba ambako pia atazungumza na watumishi wa ummakatia sekondari ya Madaba kabla kuhutubia mkutano wa hadhara. Pia atakagua shamba la miti la TFS katika kijiji cha Wino.

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU

Kafulila kupokea kadi ya Chadema jimboni Kwake Mwezi Huu

$
0
0
Aliyekuwa  Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, amesema atapokelea kadi ya Chadema jimboni mwake baadaye mwezi huu.

Kafulila alitangaza kuhama NCCR-Mageuzi na kurudi Chadema kwa alichoeleza kuwa ndicho chama kilichojipambanua kuelekea safari ya mabadiliko ifikapo mwaka 2020.

Kada huyo tayari amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe kumjulisha kuwa anajivua uanachama na  anarudi Chadema.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Kafulila alisema ameamua kuwa atapokelea kadi hiyo jimboni kutokana na mapenzi aliyonayo kwa wananchi wake.

"Nimepanga kuchukua kadi mwezi huu jimboni, kwa kuwa ilikuwa nichukue kadi mwanzoni lakini ilishindikana kutokana na siku kuu, hivyo siku yoyote kuanzia sasa nitachukua,"alisema.

Wakati anajiuzulu NCCR-Mageuzi na kurudi Chadema, alisema hakufanya uamuzi kwa kukurupuka bali alitafakari na kushauriwa na wananchi wa jimbo lake, na kuridhika kurudi huko.

"Nilitafakari na kushauriwa sana jimboni na kuridhika kwamba Chadema ndiko sehemu inayojipambanua kwa mikakati ya kuleta mabadiliko yanayotarajiwa na Watanzania na ni vema kukusanya nguvu ya kila mwenye kiu ya mabadiliko ndani ya chama kimoja, ili kufupisha safari ya mabadiliko," alisema.

Alipoulizwa kwa nini amerudi Chadema wakati aliyekuwa Katibu  Mkuu wa Chama hicho, Dk Wilbrod Slaa alipata kumwita sisimizi kwa  alichoeleza kuwa hakuwa na imani naye, alijibu kuwa siasa ni malengo si uhusiano binafsi.

Kafulila aliongeza kuwa wanasiasa wanaunganishwa na malengo zaidi ya urafiki na kwamba malengo yake sasa ni kuendelea kupigania mabadiliko ya kimfumo yanayoenea zaidi kwenye chama hicho (Chadema) kuliko kingine.

Novemba 10, 2009 Kafulila alijivua uanachama wa Chadema na kuhamia NCCR-Mageuzi kutokana na kuondolewa kwenye nafasi ya uofisa habari wa chama hicho.

Pia akiwa NCCR-Mageuzi, alitimuliwa uanachama kwa kudaiwa kukiuka taratibu za chama hicho na tuhuma za kutaka 'kumpindua' Mwenyekiti, James Mbatia.

Hata hivyo, suala hilo lilipata suluhu baada ya Mbatia kuteuliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kuwa Mbunge. Wakiwa bungeni, Mbatia na Kafulila walikutana, kuzungumza na hatimaye kumaliza mzozo wao.

Kigogo Afanya Tukio La Kutisha Dar! Adaiwa Kumfungia Mke Wake Ndani Kwa Miaka 5

$
0
0


DAR ES SALAAM: Mwalimu mstaafu wa chuo kikuu kimoja, Gideon  Mwakabuta (60), amebeba shutuma nzito kufuatia madai kwamba, kwa muda wa miaka mitano amemfungia ndani mkewe wa ndoa, Grace Mwakabuta ambaye pia ni karani wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jijini hapa.
Mzee Mwakabuta na mkewe huyo ni wakazi wa Wazo Hill jijini hapa.
Kisa cha kumfungia kinatajwa ni afya ya karani huyo kuwa mbaya akikabiliwa na ugonjwa wa ajabu ambao ulimsababishia kupooza mikono na mwili kutokuwa na nguvu hivyo kushindwa kutembea, kuongea na kushiriki shughuli zozote za ujenzi wa taifa achilia mbali za kifamilia kama mke.

 
MAJIRANI
WAMFUNGIA KAZI
Tukio hilo la kushangaza lilibumburuka hivi karibuni baada ya baadhi ya majirani kumfungia kazi mstaafu huyo kwa nia ya kufichua uovu huo ambao kibinadamu hawakuuona kama ni sawasawa.
Jirani mmoja (jina linahifadhiwa) ana mkasa mzima wa jinsi mwanamke huyo alivyoanza kuumwa na mumewe kudaiwa kumfungia ndani:
“Unajua ni muda mrefu takriban miaka kumi huyu mama alianza kuumwa ambapo ndugu mbalimbali walifika nyumbani kwake na kumuomba mumewe wampeleke hospitali baada ya kuona anaumwa na kulala ndani tu pasipo kupelekwa hospitali.
“Haikujulikana alikuwa akiumwa nini lakini Mwakabuta pia haikujulikana alikuwa akiwajibu nini hao ndugu maana sisi tukawa tunaendelea kumwona mkewe akiwa ndani tu.”

MADAI YA MUME
KWA MAJIRANI
Aidha, jirani huyo alisema kuwa, mwanaume huyo alidai kwamba, anamtibia mwenyewe mke wake lakini ndugu walifika tena kwa ajili ya kumpelekea dawa za kienyeji wakiamini huenda zingemsaidia lakini hazikupokelewa kwa madai kwamba, yeye ndiye anampatia dawa.
“Kwa kweli sisi kama majirani tumekuwa tukiumia sana kwa hii hali ya mwanamke wa jirani. Ilifika mahali tukasema huenda siku moja mumewe ataamua kumpeleka hospitali, lakini tukaona siku zinapita,” aliongeza jirani huyo.

MKE AANZA KULIA,
KUPIGA KELELE
Habari zaidi zenye kuibua majonzi zinasema kuwa, baada ya Grace kuendelea kuteseka kwa ugonjwa huo ambao ulikuwa haujulikani ni upi, alianza kupiga kelele akilia kwa uchungu wa maumivu.
“Mbaya zaidi ni kwamba, ugonjwa wake anakakamaa misuli na hawezi kufanya lolote zaidi ya kulala tu, amekuwa kama mtu asiye na wasaidizi. Ukimwona huwezi kuamini kwamba ni mgonjwa anayepata msaada wa kitabibu au wa kibinadamu.
“Grace alianza kuumwa tangu wazazi wake wakiwa hai, nao  walijaribu kumpigania afya yake lakini ikashindikana mpaka wote sasa wamefariki dunia, Grace bado anaumwa tu,” alisema jirani mwingine.

WAANDIKA BARUA
USTAWI WA JAMII
Majirani hao waliendelea kusema kuwa, baada ya kuona hali ya Grace inazidi kuwa mbaya kila kukicha kwani walikuwa wanapata nafasi ya kumjulia hali, waliamua kuandika barua ya siri na kuipeleka Idara ya Ustawi wa Jamii ambako wanashughulika na matatizo ya kifamilia.
“Ustawi wa Jamii na wao waliamua kuandaa mpango wa kuvamia nyumbani kwa Mwakabuta na kumchukua mkewe kwa nguvu kumpeleka hospitali kupata matibabu,” alisema jirani huyo.

SIKU YA TUKIO
Siku ya tukio la Ustawi wa Jamii kuvamia nyumbani kwa Mwakabuta ilikuwa Jumamosi iliyopita ambapo walimkuta mzee mwenyewe akiwa amejifunga kanga, baada ya utambulisho na kumuuliza alikiri mkewe yupo ndani anaumwa lakini akasema amekuwa akimpeleka hospitali na kwenye tiba nyingine bila mafanikio.
“Ilikuwa kazi ngumu kumchukua mkewe kumpeleka kwenye gari maana Mwakabuta alikuwa hataki. Na hata wakati wa kumtoa mkewe chumbani ili aandaliwe, alikataa kusaidiwa akisema kazi hiyo ataifanya mwenyewe kwa sababu ni mkewe mpendwa anayempenda sana.
Hata hivyo, kazi ikafanyika, mke akaingia kwenye gari na mumewe akiwemo na kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala.
“Mimi nahisi pana tatizo kwani si rahisi kwa mke unayempenda ukamwacha aumwe vile ndani siku zote. Na hata madai yake Mwakabuta kwamba amekuwa akimtibia mkewe yanatia shaka kwani hali ya mkewe si ya mtu anayefanyiwa uangalizi kwa ugonjwa,” aliongeza jirani huyo.

MUME MIKONONI
MWA POLISI
Habari zaidi ni kwamba, baada ya kuvamia nyumbani kwa mzee huyo na mkewe kuchukuliwa akiwa hoi, mbele ya safari, Mwakabuta aliishia mikononi mwa Polisi wa Kituo cha Kawe ambako alikuwa anashikiliwa hadi wakati gazeti hili linakwenda mitamboni.

MKE ANAENDELEA
NA MATIBABU
Juzi, Amani lilifika Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kumjulia hali mwanamke huyo na ikibidi kupata picha akiwa amelazwa hapo, lakini halikuweza kumwona na kuambiwa anaendelea vizuri na matibabu na hatakiwi kusumbuliwa.

NENO LA MHARIRI
Ushauri ni kwamba pamoja na mume kukamatwa lakini bado na yeye anahitajika kuchunguzwa huenda hata yeye hayuko sawa kutoka na mawazo au jambo lingine lolote ambalo hajawahi kulisema kwa jamii.
Tukio hili ni la kushangaza sana na la kufungulia mwaka lililowaacha watu na maswali mengi. Je, Grace hakuwa na watoto? Je, ni kwa sababu gani  mumewe alimfungia? Ili kupata majibu ya maswali hayo, endelea kufuatilia magazeti ya Global.
Ili kupata tamko la serikali, jana Amani lilimpigia simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Suzan Kaganda ili kumsikia anasemaje kuhusu madai hayo ambapo alithibitisha kushikiliwa kwa Mwakabuta kwenye Kituo cha Polisi cha Kawe.
“Ni kweli, tukio hilo la Mwakabuta kukamatwa lipo kwetu, tunamshikilia. Alikamatwa Jumamosi. Lakini mkewe alipelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.
“Sisi bado tunamshikilia Mwakabuta kwani upelelezi unaendelea ili kubaini usahihi wa madai dhidi yake. Kwa mujibu wa ndugu na baadhi ya majirani, Grace aliumwa, akawa anatibiwa lakini baadaye mumewe akaacha kumtibia na kumfungia ndani tu. Hayo ndiyo madai yaliyopo.
“Upelelezi ukikamilika ikaonekana ni kweli alifanya tendo lile, hatua itakayofuata ni kumpeleka mahakamani,” alisema Kamanda Kaganda.
Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa maelezo ya kituoni, Mwakabuta anafanya shughuli zake binafsi na mkewe Grace alikuwa mwajiriwa mpaka anakumbwa na ugonjwa.
“Kwa maelezo ya kituoni, Mwakabuta kwa sasa anafanya shughuli zake. Sasa kama ni mstaafu mimi sijajua. Mkewe alikuwa mwajiriwa lakini kutokana na matatizo ya maradhi nadhani isingewezekana kuendelea kufanya kazi. Sasa sijajua kama ajira ilikoma au vipi,” alimaliza kamanda huyo.

MKE ANAENDELEA
NA MATIBABU
Aidha, jana Amani lilifika tena hospitalini hapo na kuzungumza na ndugu mmoja ambaye alifika kumwona Grace, alisema anaendelea na matibabu ambapo madaktari wanachofanya kwa sasa ni kuchukua vipimo mbalimbali ili kubaini hasa tatizo lake.


“Mimi mwenyewe nimekuja kumwangalia Grace, lakini nimetoka kwa kuwa madaktari wameingia, wanasema wanaendelea kumfanyia vipimo mbalimbali ili kubaini tatizo lake la msingi ni nini,” alisema ndugu huyo bila kuwa tayari kutaja jina lake.
Akielezea maisha enzi za afya yake, ndugu huyo alisema kuwa, Grace alikuwa na afya njema tu na alikuwa mwanamke mwenye kujali wengine na kushirikiana na watu kama kawaida.
“Sijajua hasa nini kilimpata. Lakini alikuwa kawaida sana. Kuhusu umri, sina kumbukumbu sawasawa ila nadhani anaweza kuwa kwenye miaka 45 mpaka 50. Lakini sina uhakika sana,” alisema ndugu huyo.
Kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa watoto, ndugu huyo alisema hawezi kulisemea zaidi ya mzee Mwakabuta mwenyewe.

Imeandikwa;
 Hamida Hassan na          Imelda Mtema.





TAARIFA YA UZUSHI KUHUSU MANJI KUSITISHA KUKODI TIMU YA YANGA YASAMBAZWA MITANDAONI, CHAMPIONI YAFAFANUA

$
0
0


KUNA BARUA INAYOSAMBAZWA MITANDAONI, KWAMBA GAZETI LA CHAMPIONI LIMEFANYA MAHOJIANO NA MWENYEKITI WA YANGA, YUSUF MANJI KUWA AMESITISHA UKODISHWAJI WA TIMU NA NEMBO YA YANGA. HUO NI UZUSHI MTUPU NA GAZETI LA CHAMPIONI HALIJAFANYA MAHOJIANO NA MANJI.

PIA TUNATOA ONYO UPUUZI KAMA HUO WA KUSAMBAZA VITU VYA UZUSHI KWA KULITUMIA GAZETI HILI. IWAPO TUTAMBAINI MTU, TUTAMCHUKULIA HATUA ZA KISHERIA.

MHARIRI

HABARI HIYO YA UZUSHI
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, amesitisha kuendelea na zoezi la kuikodisha timu na nembo ya klabu hiyo na kuwaambia wasaidizi wake, wasitishe mipango yote ya maendeleo waliyokuwa wameanza kuifanya.

Manji amewaambia wasaidizi wake kusitisha maandalizi ya Ligi ya Vijana ya Matawi ya Yanga, lakini amewaambia waandae siku rasmi ambayo atazungumza na vyombo vya habari na kuwaomba radhi Wanayanga ambao wamemuunga mkono muda wote.

Habari za uhakika ambazo Championi Jumatano limezipata, zinasema Manji alizungumza na wasaidizi wake jana mchana ikiwa ni dakika chache baada ya TFF kufanya mkutano na waandishi wa habari na kusema hawatambui suala la Yanga kuikodisha timu na nembo kwa Kampuni ya Yanga Yetu Ltd, kwa miaka 10.
“Leo alionekana ni kama mtu aliyekata tamaa au asiyefurahishwa na jambo. Amewaita wasaidizi wake na wamefanya kikao, hakikuwa kirefu sana.

“Amewaambia ameamua kuachana na masuala ya kuikodisha Yanga, pia amesema ameona ni vizuri kuachana na masuala ya mpira.
“Kilichomuudhi ni wale wasiotaka mchakato wa mabadiliko Yanga, lakini hawatoi hoja za msingi,” kilieleza chanzo.
“Wasaidizi wake walikuwa wameanza mchakato wa kutengeneza mfumo wa Ligi ya Vijana ya Matawi ambao ungeigharimu Yanga yetu takribani Sh milioni 280 kwa ajili ya vifaa, uendeshaji na kadhalika.

yangaaa-5
“Lakini kuna suala amelizungumzia la uchaguzi, hilo sijaelezwa vizuri. Huenda Yanga wakaitisha uchaguzi tena ili kuchagua viongozi yeye atakapotangaza kujiuzulu rasmi.

“Anaweza kufanya hivyo, yaani kutangaza kujiuzulu na kutangaza uchaguzi, pia kuwaomba radhi wanachama na mashabiki waliomuunga mkono muda wote.”

Juhudi za kumpata Manji zilianza jana saa 7 mchana baada ya kupata taarifa hizi; lakini ilishindikana.
Mmoja wa wasaidizi wake alipopigiwa, alituma ujumbe mfupi: “Nipo kwenye kikao, nitafute baadaye.”
Alipopigiwa Manji saa 9 alasiri, akapokea, ilikuwa hivi:

Championi: Hallow
Manji: Nani mwenzangu?

Championi: Tunafuatilia kuhusiana na uamuzi wako wa kujiuzulu Yanga, tunataka kujua ni kwenye klabu au zoezi la kukodisha pekee.
Manji: Tafadhali niacheni, kuweni kama binadamu. Nimechoka jamani, kuweni waungwana na mimi ni binadamu. Mniache nipumzike (simu ikakatwa).

Yanga
Baadaye mmoja wa wasaidizi wake alipiga simu akitaka kujua alikuwa anatafutiwa kipi. Alipoulizwa suala la kujiuzulu kwa Manji, akasema:
“Sasa ndugu yangu unataka kuniingiza matatizoni, nafikiri tuache atangaze mwenyewe, naomba nipokee simu nyingine.” Kisha akakata simu.

Manji ambaye aliiongoza Yanga kwa misimu minne, mitatu ikifanikiwa kuwa bingwa Tanzania Bara, Kombe la FA na kucheza robo fainali ya Kombe la Shirikisho, ndiye kiongozi kipenzi cha Yanga wengi hasa wanaovutiwa na mafanikio ya timu yao.

Juhudi za kuendelea kumpata ili kuzungumza naye na kupata kila kitu kuhusiana na hili, zinaendelea.

Suala la kutaka kuikodisha timu ndiyo limezua zogo, huku wachache wanaopinga wakishindwa kuanika sababu hasa za msingi zinazowafanya wapinge.

HII HAPA BARUA YA JERRY MURO KUOMBA MSAMAHA TFF YAVUJA....

$
0
0



Barua ikimuonyesha Mkurugenzi wa Habari wa Yanga, Jerry Muro akiomba kupunguziwa adhabu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imevuja mtandaoni.

Barua hiyo inaonyesha Muro aliandika Julai 7, mwaka jana akiomba kupunguziw aadhabu ya mwaka mmoja baada ya kuutumikia kwa miezi sita.

Muro alifungiwa na TFF kwa mwaka mmoja kwa madai ya utovu wa nidhamu.
Hivi karibuni, Mkurugenzi wa kitengo cha habari cha klabu ya Simba, Haji Manara alimuombea msamaha Muro na kuishauri TFF kumuondolea adhabu hiyo.
SALEHJEMBE, inamuunga mkono Muro kuomba radhi kwa kuwa ni sehemu ya uungwana wa mwanadamu kufanya jambo hilo.

SALEHJEMBE inaiasa TFF, kuliangalia ombi la Muro na ikiwezekana kulifanyia kazi kwa kumsamehe.



Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>