Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA MWAKA MPYA KATIKA KANISA KUU LA KATOLIKI JIMBO LA BUKOBA MKOANI KAGERA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma mara baada ya kuwasili katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibusu mkono wa Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini mara baada ya kuwasili katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya Ibada.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea katika katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera mara baada ya kuwasili na kupokewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma (katikati) pamoja na Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini wa kwanza (kulia).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ibada ya mwaka mpya katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma mara baada ya Ibada.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera mara baada ya Ibada.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kaburi la Marehemu Kadinali Rugambwa mara baada ya Ibada kanisani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma mara baada ya kushiriki Misa ya Mwaka mpya kanisani hapo. Katikati ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Wageni Kanisani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma kushoto pamoja na Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na masista kanisani hapo mara baada ya Ibada. PICHA NA IKULU.

Rais Magufuli Akataa Kupanda Kwa Bei ya Umeme

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Atumbuliwa

$
0
0

Rais John Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Felschemi Mramba kuanzia leo, Januari 1, 2017.
Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli amemteua Dkt. Tito Esau Mwinuka kuwa kaimu mkurugenzi wa shirika hilo. Kabla ya uteuzi huo,  Mwinuka alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mahakama yaiamuru Serikali kurekebisha kifungu Sheria ya Mtandao

$
0
0

Haras El Hodood ya Misri imetupia mtandaoni na kueleza kuwa mshambuliaji Ibrahim Ajibu ni mchezaji wao mpya.

Ajibu anaonekana akiwa kwenye picha na wachezaji wengine wa Haras El Hodood ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Misri.

Hata hivyo, Msemaji wa Simba, Haji Manara amelifafanua jambo hilo kwa kusema Ajibu bado ni mali ya Simba.

“Nimeliona hilo suala, naulizwa sana. Lakini ukweli Ajibu bado ni mali ya Simba, bado hatujakaa mezani na hao ndugu zetu kuhusiana naye,” alifafanua.

Simba ilitoa ruhusa ya Ajibu kwenda kufanya majaribio hadi Desemba 31, 2016 na baada ya hapo kama amefuzu, pande hizo mbili zingekaa mezani.


Lakini tayar Haras El Hodood ilitangaza kwamba Ajibu alifuzu vipimo vya afya. Hivyo lilibaki suala la benchi la ufundi kuamua.

Rais Magufuli azuia chakula cha msaada Misenyi.....Awataka Wananchi Wachape Kazi

$
0
0
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amezuia serikali kupeleka chakula cha msaada wilayani Misenyi mkoani Kagera kwa madai kuwa wilaya hiyo haina sababu ya kukumbwa na tatizo la njaa.

Rais Magufuli amekataa serikali kupeleka chakula cha msaada katika wilaya hiyo na kusema haikubaliki kwa eneo hilo lenye mvua za kutosha na hali nzuri ya kilimo na kwamba haiwezekani kulia njaa wakati kuna uwezekano wa kuzalisha kwa ajili ya chakula.

Amesema hayo wakati akiweka jiwe la msingi katika kituo cha afya cha kata ya Ishozi Wilayani Misenyi Mkoani Kagera ambapo yupo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo kukagua maendeleo mbalimbali.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli, amesema kuwa serikali haitaweza kujenga makazi ya kila mwathirika wa tetemeko mkoani Kagera kwa kuwa ina jukumu la kujenga miundombinu itakayokuwa na manufaa kwa jamii nzima kama Zahanati, Shule na barabara.

Amesema kuwa kuna baadhi ya watu ambao nyumba zao hazikuharibika kiasi kikubwa lakini wakadanganywa na baadhi ya watu kuwa watajengewa hivyo wakazibomoa kwa kutaka kujengewa nyumba mpya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.

LWANDAMINA APANGA FULLU MZIKI YANGA IKIIVAA JAMHURI MAPINDUZI CUP LEO

$
0
0


KIKOSI CHA YANGA SC DHIDI YA JAMHURI LEO (Mechi inatarajia kuanza Saa 2:30 usiku kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.)

KIKOSI
1. Deogratius Munishi
2 Juma Abdul
3. Mwinyi Haji
4. Kelvin Yondani
5. Vicent Andrew 
6. Justin Zulu
7. Saimoni Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Amissi Tambwe
10. Haruna Niyonzima 
11. Emanuel Martin

Akiba
- Ali Mustafa 
- Hassan Hamisi
- Nadir Haroub
- Juma Mahadhi
- Deusi Kaseke

- Obrey Chirwa

Magazeti ya Leo Tanzania Jumanne ya January 3, 2016

Feza Kessy awalilia Chidi Benz na Nando baada ya kudhoofu kwa Madawa ya Kulevya

$
0
0
Feza Kessy ana mdogo wake ambaye naye ni muathirika wa madawa ya kulevya hivyo anaelewa kinagaubaga changamoto ya kuwa na mtu wa karibu anayepambana na janga hilo.

Na sasa amewaomba Watanzania kuwaombea wote walioingia kwenye tatizo hilo wakiwemo Chidi Benz na Nando ambao hali zao za hivi karibuni zinasikitisha.

Ameandika kwenye Instagram:
"Let’s pray for our brothers and sisters who are caught up in drug addiction. Chidi ni rafiki yangu for many years Na Nando mdogo wangu, I will Not Post how they look like Now cos kwangu haijakaa sawa. #MadawaYaKulevya sio mchezo it’s time tuache kunong’ona Na tuwe wazi! Hashtags Na Repost won’t help jamaniiiii A plan is needed as a society to fight this devil. Kwa wale ambao wanasema “wakafie mbali” mara “wameyataka wenyewe” let me tell you something;

"Kuna watu wamezaliwa Na addictive personality, wanajaribu Mara moja na ndo mwanzo wa kujiuwa, wengine wanajaribu na wanaacha tu so muache kuhukumu watu kama vile nyie ni Mungu. There is nothing fair about addiction wao wenyewe wanakata tamaa. We need to stop this drug business “Sisi” kama society, we need to teach about it and make our kids fear these drugs, and we also need to love the ones affected, pray for them because huijui Kesho it might come to your house. Ni hayo tu for now."

Let's pray for our brothers and sisters who are caught up in drug addiction. Chidi ni rafiki yangu for many years Na Nando mdogo wangu, I will Not Post how they look like Now cos kwangu haijakaa sawa. #MadawaYaKulevya sio mchezo it's time tuache kunong'ona Na tuwe wazi! Hashtags Na Repost won't help jamaniiiii A plan is needed as a society to fight this devil. Kwa wale ambao wanasema "wakafie mbali" mara "wameyataka wenyewe" let me tell you something; Kuna watu wamezaliwa Na addictive personality, wanajaribu Mara moja na ndo mwanzo wa kujiuwa, wengine wanajaribu na wanaacha tu so muache kuhukumu watu kama vile nyie ni Mungu. There is nothing fair about addiction wao wenyewe wanakata tamaa. We need to stop this drug business "Sisi" kama society, we need to teach about it and make our kids fear these drugs, and we also need to love the ones affected, pray for them because huijui Kesho it might come to your house. Ni hayo tu for now.

A photo posted by Feza (@fezakessy) on


Madawa ya kulevya yamwathiri aliyekuwa mshiriki wa Big Brother - Nando

$
0
0

Ni kijana aliyeshiriki big brother mwaka 2013, kama mwakilishi wa Tanzania, kutokana na hali ngumu ya maisha kijana huyu alijidumbukiza kwenye janga kubwa la matumizi ya madawa ya kulevya

Kwa sasa hali ya Afya ya Nando si nzuri imezorota kutoakana na matumizi ya madawa ya kulevya yaliyo kithiri,

Hii iwe kama kengele kwa vijana wa kisasa kuwa dawa za kulevya sio “ujanja” ni majanga. Unaweza kuanza na kuvuta kisirisiri, lakini majibu ya madhara yake yakawa hadharani na unapotoka hadharani basi muda unakuwa umekwisha kwenda.

Majambazi yapora mamilioni mbele ya askari polisi Dar

$
0
0
Watu  wanaodaiwa majambazi wamepora kiasi cha fedha kinachokadiriwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 25 katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere, eneo la Tazara, Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea  jana saa 4 asubuhi wakati gari hilo likiwa kwenye foleni ya magari eneo hilo la taa za Tazara.

Watu hao wameporwa katika eneo ambalo huwa askari doria wametanda, lakini wakikamata pikipiki zinazotokea eneo la Buguruni.

Aidha taa za Tazara yaliko makutano ya barabara kutokea Buguruni, Temeke, Kariakoo/Posta na Gongo la Mboto ndilo eneo lenye askari wengi wakiwemo wa usalama barabarani.

Wakati tukio likifanyika kulikuwepo askari wenye magwanda maalumu ya askari doria zaidi ya watano wakivurumushana na waendesha pikipiki upande wa Barabara ya Mandela kutokesa Buguruni. Hata hivyo imeelezwa kuwa watu hao waliokuwa wakipeleka benki hawakuwa na ulinzi kama inavyoshauriwa na Jeshi la Polisi.

Majambazi hao waliokuwa watatu, walipora fedha hizo katika gari ndogo aina ya Toyota Rav4 yenye namba za usajili T 455 DFN mali ya kampuni ya kutengeneza mabati ya Sun Share iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyejitambulisha kwa jina la Richard Charles.

Kwenye gari pia alikuwepo mfanyakazi mwingine wa kampuni hiyo, mwenye asili ya China, aliyetambulika kwa jina la Cheng Deng.

Kwa mujibu wa dereva wa gari hiyo, Charles, walikuwa wakizipeleka fedha hizo benki eneo la Quality Centre na ndipo walipovamiwa na watu hao wakiwa na pikipiki aina ya boxer wakati magari yakiwa kwenye foleni wakisubiri taa ziwaruhusu kupita kutoka barabara ya Mandela.

Charles alisema majambazi hao walimwamrisha kufungua mlango na kuwapatia begi la fedha lililokuwa limewekwa katika kiti cha nyuma huku wakimtishia kwa bastola kabla ya kuvunja kioo cha nyuma cha gari hilo na kubeba fedha hizo na kutokomea nazo.

“Kwa kweli hata sielewi mpaka sasa hivi kilichotokea. Walikuja watu wawili mmoja upande wangu mwingine wa bosi wangu wakinitishia kwa bastola nifungue mlango niwape begi la fedha. Ghafla mtu mwingine akavunja kioo cha nyuma kwa kutumia kitako cha bastola na kubeba begi la fedha na kutokomea” alisema Richard.

Askari wenye silaha walifika katika eneo la tukio dakika 20 baada ya tukio hilo wakaishia kuhoji. Hata hivyo askari mmoja ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake alilaumu tabia ya baadhi ya watu kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha pasipo kuomba ulinzi wa polisi jambo linalohatarisha usalama wao na mali zao.

“Kama walijua wanasafirisha kiasi kikubwa hicho cha fedha kwa nini wasingeomba hata ‘escort’ (kusindikizwa kwa ulinzi) ya polisi? Hili ni tatizo, hasa katika kipindi hiki kigumu cha upatikanaji wa fedha, watu wanatakiwa kuchukua tahadhari mapema.” alisema askari huyo.

Credit: Habari Leo

Moto Wateketeza Maduka 14 Arusha

$
0
0

Maduka 14 katika eneo la Mianzini jijini Arusha yameteketea kwa moto jana asubuhi na kusababisha hasara mbalimbali huku jeshi la polisi likiimarisha ulinzi na kusimamia shughuli za uokoaji wa mali zilizosalimika. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye baadhi ya majokofu yaliyokuwa katika baadhi ya maduka hayo. 
Kamanda Mkumbo alisema mara baada ya hitilafu hiyo, moto huo ulishika mitungi ya gesi iliyolipuka na kuanza kusambaa kwa kasi na kuunguza maduka hayo. 
Alisema wamefanikiwa kuokoa baadhi ya mali katika maduka tisa kati ya 14 kwa msaada wa wananchi na wasamaria wema waliokuwa katika eneo la tukio lakini ukubwa wa hasara bado haujajulikana.
 Mmiliki wa moja ya maduka yaliyoteketea, Zena Athuman alisema kabla ya kufungua biashara yake, alifika katika eneo la tukio na kukuta moto huo umeshaanza na hakufanikiwa kuokoa mali yoyote kwa kuwa moto huo ulikuwa ukisambaa kwa kasi ya ajabu. 
Shuhuda wa tukio hilo, Julius Sangeti alisema alifika katika eneo hilo saa 11:30 asubuhi na kushuhudia moto ukiwaka katika duka kubwa la Mianzini na kadri muda ulivyokuwa ukisonga, ndivyo ulivyokuwa ukihamia kwenye maduka mengine na kuteketeza mali.

MASHABIKI WAMLILIA YOUNG DEE BAADA YA MENEJA KUDAI AMERUDIA TENA UNGA

$
0
0

Kwamujibu wa meneja wa Young Dee, Maximillian Rioba, rapper huyo amerejea tena kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

Taarifa hiyo imekuja katika wakati ambao mashabiki wengi wa muziki waliamini kuwa rapper huyo ameachana na matumizi ya unga

Max anadai amejaribu kila awezalo, lakini sasa ameamua kunawa mikono. Amezitoa taarifa hizo Instagram alipokuwa akichat na msichana aitwaye Wendy Eliah.


Kwenye post yake ya Instagram, Max aliandika ujumbe toka kwenye biblia: Walipompinga na kuanza kumtukana, aliyakung`uta mavazi yake mbele yao akisema, “Mkipotea ni shauri lenu wenyewe; mimi sina lawama yoyote juu ya jambo hilo. Na tangu sasa nitawaendea watu na mataifa mengine.” Matendo Ya Mitume 18:6 NENO LA BWANA LIMENENA. KILA MWENYE SIKIO NA ASIKIE….



Baada ya kuenea kwa taarifa hizo, mashabiki wameenda kwenye ukurasa wa Instagram wa rapper huyo kumpa ushauri.

Crown_princess_shorla

Munaoleta hiki kiama kwa wapendwa wetu na kutusonononesha kiasi hiki, roho wa Mungu yu mbele yenu, kiama kitawaangamiza soon, kumbukeni mnaowaumiza walizaliwa, wanawazazi wana mama ambao waliteseka miezi Tisa tumboni na mwisho kuingia labour kwa uchungu wa kufa kupona kuwazaa hao watoto, nawaapia chozi la mama hawa Mungu hatolipa mgongo atawaadhibu, kazaneni kuwauwa watoto wa wenzenu kwa kutaka utajiri wa haraka, moto na hasira ya Mungu I juu yenu, @youngdaresalama my brother don’t do that to your poor daughter and her mother, they really need you more than anyone in this world, plz stop this stupid act, grow up brother we don’t wanna loose you, it’s not too late to change my dear! @maximilianrioba don’t give up on him brother at least pray more for him najua lililo gumu kwa mwanadamu Mungu anajua utatizi wake, even if hatokuelewa na nguvu za Mungu atasimama kutete naye. Tuwaombee zaidi kuliko kuwakatia tamaa, najua inavunja moyo but tutambue hata Mungu hajawahi kutukatia tamaa wanadamu na maudhi yetu yote, let us pray for them! For really inaumiza Sana but they our people, our brothers and our family too.


spycedollydoll

Please don’t go back in Da hell that brought you so much regreats u a good man please do the best and prove wrong people who thought you can’t take care of ur baby princess

ireneemoshi

We mtoto wewe, kwann mnapenda kuwapa.shida wazaz.wenu unafkir mama aliye kubeba miez TSA tumbon anajickiaje ukiharbika wewe, yan kma umerudia matapishi acha aisee unapotea kabsaaa umepata mtoto hem mleee huyo, ukiwa kichaa nan atamuhudumiaa, mbona ujana unakupeleka pabaya namna hyo unapte ujue ur still young, kwan shida n nn mpaka uanze kula vtu vya ajabu watu tunaumia kuona vjana mnaharbikiwa bado wadogo jenga maisha yako acha makundi yasiyo na msng hao wanakupotoshaa tuu hem kuwa kioo cha jamii, au una umekumbwa na pepo, hem mkatae shetan cmama mtoto wa kiumee jenga familia wewe ushakuwa baba, kama ni kweli unaapiga hzo mambo kisr achaaaa, wapote dogoo hem angalia picha za jinsi ulivokuw mwanzo na sasa, je unataka kurud ulpotokaaa.

ms._wise_always

@youngdaresalama Acha ujinga dogo , ww ni baba now … ww sio mtu wakutoa watu machozi tena? wewe hujui unathamani gani? au ni makusudi unataka kijana wa watu ajute?@maximilianrioba Kweli unamtia kwenye majonzi namna hii acha upuuzi ww ni mtu mzima now , You shud standup and be ambassdor of others like Nando and Chidy and also stand for your Tamar also
but WHY?

syper_jr

I cant judge you niggha mwenye haki ya kuongelea your lyf n watu ka kna max wanaokufaham vzuri ila yo still a great rapper af una Tamar baharia langu sooo watever u du all remember is yu have a life n a beautiful babydaughter…..nakumbuka max once cried kweny interview clouds sooo no body can make him change his mind kukusupport mpaka ue back again in line siamin if max iz that dumb mpk kupost hii issue yenu insta a only hope he meant by postin uku atha ppo gotta try tu b on yo side bruh..all the best mwanangu D don give up on your kid

wavy_lord_

@youngdaresalama nigga you started cool unataka utuangushe get the fuck out that shit brother Again get the fuck out nigga that shit aint cool i feel like crying right now @maximilianrioba this shit is fVCkn sad

Jitihada za kumtafuta Young Dee ili aelezee kinachozungumzwa zinaendelea.

MUZAMIRU ATUPIA TENA SIMBA IKIISHINDA KVZ BAO 1-0, WASHAMBULIAJI WAENDELEA KUPOTEZA NAFASI KIBAO

$
0
0


Simba imeshinda mechi yake ya pili katika Kombe la Mapinduzi baada ya kuitwanga KVZ kwa bao 1-0.
Shujaa wa Simba ni Muzamiru Yassin aliyefunga bao katika dakika ya 43 baada ya kuutegua mtego wa kuotea wa mabeki wa KVZ.

Hata hivyo, KVZ ilionyesha soka safi na la kuvutia na kuwapa Simba wakati mgumu.

Washambuliaji wa Simba, Juma Luizio na Pastory Athanas walipata nafasi nyingi za kufunga lakini wakashindwa kuzitumia.

Shiza Kichuya naye alipata nafasi mbili nzuri za kufunga katika dakika za mwisho kipindi cha pili, lakini hakutumia nafasi hizo.

Samba walicheza kwa kushambulia kwa kushitukiza lakini suala la umaliziaji liliendelea kuonekana halina uhakika.

Mechi ya kwanza, Simba iliishinda Taifa Jang’ombe kwa mabao 2-1.


Ushindi huo kwenye Uwanja wa Amaan, bado ilionekana mashabiki wa Simba kutokuwa na furaha sana ikionekana wazi walitaka kuona timu yao ikishinda kwa mabao mengi zaidi, jambo ambalo halikutokea.

Mwishoni zikiwa zimebaki dakika mbili, beki wa KVZ alilambwa kadi nyekundu kwa kumvuta jezi Pastory akienda kufunga. Lakini bado Simba hawakuweza kuitumia vizuri nafasi hiyo.

Magazeti Ya Tanzania Leo Jumatano Ya January 4, 2016

Serikali kuajiri walimu 4000 wa masomo ya Sayansi na Hisabati, Wale wa Maomo Mengine Watulie Maana Hakuna Uhaba Kwa Sasa

$
0
0
Serikali imesema ipo kwenye mchakato wa kuajiri walimu 4000 wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwa katika ziara yake ya kutembela wilaya mpya za jiji hilo, akianzia na Kigamboni siku ya leo.

Majaliwa amesema mchakato wa ajira hizo unaendelea chini ya Ofisi ya Rais Utumishi, na muda wowote kutoka sasa mchakato huo utakapokamilika, majina yatatolewa na walimu hao kuajiriwa.

Kuhusu walimu wa masomo mengine, Waziri Mkuu amesema walimu wa masomo mengine hususani ya sanaa wapo wa kutosha na kwamba wanapaswa kusubiri kwakuwa wao wako wengi zaidi na hakuna uhaba na uhitaji wa walimu hao wa masomo ya sanaa.

Hivi karibuni, Wizara ya Elimu iliwataka wahitimu wa ualimu katika masomo ya sayansi na hisabati kutuma taarifa (CV) zao ili izihakiki kabla ya ajira, mchakato ambao tayari umekamilika na majina yalitumwa katika wizara ya utumishi.

Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella Manyanya wiki mbili zilizopita wakati akiongea na kituo cha EATV alisema kuwa kazi ya wizara yake ilikuwa ni kuhakiki taarifa za wahitimu hao, na si kuajiri, huku akibainisha kuwa zoezi hilo limekamilika na majina yako utumishi ambao ndiyo watahusika na kuajiri.

Pia alisisitiza kuwa kama wizara ya elimu waliomba kupewa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati haraka kwa kuwa uhitaji wao ni mkubwa zaidi na kuwataka wahitimu wote waliotuma taarifa zao, wasubiri watapata majibu muda si mrefu.

Serikali Yafuta Posho Za Vitafunwa, Mazingira Magumu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya posho mbalimbali zisizokuwa za kisheria zinaelekezwa katika miradi ya maendeleo.

Ametia agizo hilo leo (Jumanne, Januari 3, 20017) wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kigamboni akiwa katika ziara yake ya kikazi.

“Kuanzia sasa marufuku Wakurugenzi kutoa posho zisizotambulika kisheria zikiwemo za mazingira magumu, kujenga uwezo na vitafunwa katika halmashauri zenu na badala yake fedha hizo zitumike kwenye miradi ya maendeleo,” amesema.
Agizo hilo litawezesha Jiji la Dar es Salaam kuokoa sh bilioni 130 zilizokuwa zitumike na Halmashauri na Manispaa za jiji hilo, ambazo kwa sasa zitaingizwa kwenye miradi na shughuli za maendeleo.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma nchini kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kuacha kutumia fedha kinyume cha utaratibu na watakaobainika Serikali haitosita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

“Katika halmashauri zetu kila mtumishi anashiriki katika ukusanyaji wa mapato hadi walinzi, lakini mwisho wa siku vitafunwa huliwa na wachache wanaojiita wakubwa huku wengine wakisikilizia kwa nje. Jambo hili haliwezekani,” amesisitiza.
Waziri Mkuu amesisitiza kwamba Mkurugenzi yeyote atakayebainika kulipa posho hizo baada ya siku ya leo atakuwa amejifukuzisha kazi.

Aidha, ameagiza fedha zilizokuwa zikitolewa kwa madiwani kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo zisitolewe moja kwa moja kwa madiwani na badala yake zipelekwe kwenye kata husika na zifuatiliwe matumizi yake.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amezionya halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa kila fedha zinayopelekwa kwenye halmashauri hizo inatumika kama ilivyokusudiwa na atakayebainika kutumia kinyume hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Pia amewataka watumishi wote wa umma nchini kuwajibika ipasavyo na kuhakikisha wanawatumikia vyema mwananchi ikiwa ni pamoja na kuepuka vishawishi na kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa na ufisadi.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametoa siku tatu kwa watumishi 10 wa halmashauri hiyo ambao wamehamishiwa kutoka wilaya ya Temeke wawe wameripoti katika Manispaa hiyo, vinginevyo watakuwa wamejifukuzisha kazi.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa wakati akiwasilisha taarifa ya wilaya hiyo kwa Waziri Mkuu, alisema hadi sasa asilimia 98 ya watumishi waliotakiwa kuhamia kwenye halmashauri hiyo wameripoti isipokuwa 10 na hakuna taarifa zozote juu yao.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

TCRA Yatishia Kuzifutia Leseni Kampuni za Simu

$
0
0
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imetishia kusitisha kwa muda au kufuta kabisa leseni ya biashara kwa kampuni zote za mawasiliano nchini, zitakazoshindwa kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE)

Hatua hiyo ni kulingana na sheria mpya ya fedha ambayo imetoa ukomo wa hadi Desemba 31 mwaka jana kampuni hizo ziwe zimejisajili katika soko hilo.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam hii leo; Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba amesema kwa sasa wanasubiri maelezo kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana  (CMSA) kuhusu idadi ya kampuni za mawasiliano zilizokidhi sifa za kusajiliwa katika soko la hisa kwa ajili ya kuchukua hatua kwa zile zilizokaidi kutekeleza agizo hilo la kisheria.

Mhandisi Kilaba amesema TCRA imeikabidhi CMSA orodha ya kampuni zaidi ya 80 za mawasiliano, orodha ambayo CMSA itaipitia kwa lengo la kuchuja na kupata kampuni ambazo zinastahili kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Kauli ya Mhandisi Kilaba imekuja huku taarifa kutoka soko la Hisa la Dar es Salaam zikionesha kuwa ni kampuni tatu pekee ndizo zimejisajili katika soko hilo, licha ya muda wa kufanya hivyo kufikia ukomo wake Jumamosi ya Desemba 31 mwaka jana.

Polisi kufukua kaburi la binti aliyezikwa kwa siri Arusha

$
0
0
Familia moja  jijini Arusha inadaiwa kumzika kwa siri mtoto wao mdogo wa kike wa miaka mitatu katika kaburi lililofichwa, huku majirani wakidanganywa kuwa binti huyo yupo hai.

Taarifa za kisa hicho cha kusikitisha zimevifikia vyombo vya usalama. Kwa sasa kuna mipango ya kuhakikisha kuwa mwili wa binti huyo, Nuru Losipha aliyezikwa kwa siri na familia yake, unafukuliwa kwa uchunguzi zaidi.

Inadaiwa kuwa Losipha alipoteza maisha wakati akifanyiwa tohara au ukeketaji na ngariba, ambaye jina lake halikufahamika mara moja, huku familia yake ikishuhudia.

Kitendo hicho kilifanyika katika kijiji cha Engutoto Kata ya Mwandeti wilayani Arumeru Desemba 28, mwaka jana, zikiwa zimebaki takriban siku tatu tu, kabla ya mtoto huyo aliyekuwa na umri wa miaka mitatu tu, hajaingia mwaka mpya wa 2017.

Mtendaji wa Kata ya Mwandeti, Njivaini Kivuyo awali alikuwa amepitwa na taarifa hizo hadi vyombo vya habari vilipotinga kijijini hapo kwa uchunguzi na ndipo alipolazimika kwenda kuripoti tukio hilo kwenye kituo cha Polisi cha Ngaramtoni.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo aliapa kuwa liwalo na liwe na kwamba ikiwezekana kaburi litafukuliwa ili mwili wa malaika huyo asiye na hatia, uchunguzwe upya.

“Ndio kwanza nazipata hizi taarifa, na kama polisi tutaomba kibali cha mahakama ili twende kulifukua kaburi husika tujiridhishe kama kweli mtoto huyo amezikwa humo na iwapo tutaukuta huo mwili, basi tutaanza uchunguzi juu ya kifo chake,” alisema Kamanda arles Mkumbo.

Baba wa marehemu, Losipha Kaiser anadai kuwa mtoto wake alifariki kutokana na ugonjwa wa baridi yabisi na kwamba aliugua kwa kipindi kirefu kabla ya kupoteza maisha Desemba 28, mwaka jana. Lakini madai yake hayo yanapingana na ripoti ya muuguzi katika duka la dawa lililopo kijiji cha jirani cha Kidali, anayeitwa Jane Andrew.

“Walimleta mtoto hapa walitaka nimsaidie tiba, lakini tayari huyo binti alikuwa amezimia na kutokwa na damu nyingi,” alidai.

Muuguzi huyo aliwahimiza wamkimbize mtoto hospitali, na hakufahamu nini kiliendelea hadi ripoti za kifo zilipomfikia.

Huku serikali ikipiga marufuku vitendo vya ukeketaji kwa wasichana, bado kuna familia nyingi kwenye mikoa ya Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa, zinaendeleza mila hiyo kwa siri.

Kwa sasa familia hizo zimegundua mbinu mpya ya kuwatahiri watoto wa kike wakiwa wadogo sana, kuepuka kukamatwa.

Ngariba wanaotumika kukeketa watoto, mara nyingi ni akina mama vikongwe wasiokuwa na ujuzi, taaluma za afya na hutumia vifaa butu, ambazo husababisha uvujaji mwingi wa damu na kuwa chanzo cha maambukizi ya magonjwa mengine.

Bill na Hillary Clinton kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Trump

$
0
0
 Bill Clinton na mke wake Hillary wamepanga kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Donald Trump, kwa mujibu wa ripoti.
Familia hiyo itahudhuria sherehe hizo jijini Washington, D.C. January 20 kumwangalia Trump akiapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani.
Pia Rais wa zamani wa nchi hiyo, George W. Bush ametangaza kuwa atahudhuria sherehe hizo pamoja na mke wake, Laura. Hata hivyo taarifa ya Bush imedai kuwa baba yake, George H.W., hatohudhuria kutokana na umri wake kuwa umeenda sana.

Serikali kuja na pedi za kike ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja

$
0
0


Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla amesema serikali inafanya tafiti mbalimbali ili kubaini na kuona kama kunauwezekano wa kupata taulo za hedhi (pedi) ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja.

Alisema hayo jana katika mahojianio na EATV kuhusu jitihada za serikali za kuhakikisha afya ya watoto wa kike inalindwa na kuepusha utoro mashuleni kutokana na tatizo la hedhi isiyo salama hasa maeneo ya vijijini na wale wasio na uwezo wa kuzipata taulo hizo.

“Sasa hivi tupo kwenye mchakato wa kuangalia zile pedi ambazo vijana wanaweza kutumia mwenzi mmoja, miwili hata mwaka mzima, hata kwa miaka miwili,” alisema Kigwangalla. “Kuna nchi mbalimbali wameingiza kwenye soko bidhaa na namna hiyo kwa hiyo na sisi tunaendelea kuangalia tafiti mbalimbali kuhusu usalama wa hizi pedi ambazo unaweza kuzitumia kwa muda mrefu,”

Aliongeza, “Kwa hiyo tunaangalia kama na sisi tunaweza kuziruhusu kuingia nchini na sisi tuziingize sokoni. Lengo letu ni kuangalia usalama kwanza kabla hatujaziruhusu kutumika,”

Amesema serikali inahimiza wazazi na walezi wa watoto wa kike wanapoona mabadiliko yametokea kwa mabinti zao wawafundishe namna ya kujitunza kwa kutumia vifaa ambavyo vipo na vinapatikana kwa urahisi sambamba na kuwapa elimu zaidi ili wawe wasafi na kujiepusha na magonjwa yakuambukizwa.

Kwa upande wake mbunifu wa taulo za kike ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja Bi.Jennifer Shigoli amesema katika maeneo mbalimbali waliopitia kwa ajili ya kubaini changamoto zinazowakuta watoto wa kike katika kipindi cha hedhi wamebaini ukosefu wa elimu ambayo baadhi ya watu wamepata magonjwa yatokanayo na hedhi isiyo salama hivyo ameiomba serikali kutoa ushirikiano katika kumaliza tatizo hilo nchini.
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>