Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

PENNY AKONDA APOTEZA UZITO KILO 18

$
0
0

TANGAZAJI wa Runinga ya DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameamua kujikondesha mwili ambapo amefanikiwa kupoteze uzito usiopungua kilo  18 mwilini.
 
Akizungumza na Weekly Star Exclusive, Penny alifunguka kuwa, kutokana na kuona mwili wake unavimbiana, aliamua kufanya mazoezi maalum ya kupunguza mwili sambamba na kufanya ‘dayati’ ambayo imembadilisha muonekano wake (tazama picha ndogo).
 
“Nimeamua tu kuubadilisha muonekano wangu wa unene kwani nilikuwa ninazidi kuwa bonge, kweli nimefanikiwa maana hata uzito nimepungua kwa sasa.
 
“Kabla sijaanza kufanya mazoezi nilikuwa na kilo 85 lakini sasa nimepungua hadi kufikia kilo 67, ni mafanikio makubwa ambayo nimeyapata katika zoezi langu la kupunguza uzito,” alisema Penny ambaye ni ‘ubavu’ wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
 
Kuhusu msosi, kwa sasa Penny asubuhi anakula ‘ma-apple’ mawili au kipande cha papai, mchana anakunywa juisi na usiku anamalizia na saladi ya samaki au kuku, analala.

KOCHA MPYA AZAM FC ATUA, ATAMBULISHWA RASMI

$
0
0


KOCHA mpya wa Azam FC Joseph Omog hatimaye leo ametua rasmi jijini Dar tayari kwa kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho.

Omog raia wa Cameroon ametua leo saa 3:00 asubuhi na Ndege ya Shirika la Kenya ambapo mara baada ya kuwasili alipelekwa moja kwa moja katika ofisi kuu za timu hiyo zilizopo Mzizima na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Mara baada ya kusaini mkataba huo Omog anayechukua nafasi ya Muingereza Stewart Hall alitambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari na mwenyekiti wa timu hiyo Said Mohamed ambaye alimtaja kocha huyo kuwa ni kati ya makocha bora sita wanaopatikana Bara la Afrika.
Mohamed maarufu kama Mzee Said amesema Azam inafuraha kubwa kumpata Omog ambaye uongozi wa timu hiyo umeona ndiye anayestahili kuchukua nafasi ya Stewart aliyesitisha mkataba mwezi uliopita.

Omog kwa upande wake kocha wa zamani wa kikosi cha A.C Leopards ya Congo Brazaville alionyesha kushangazwa na mapokezi aliyoyapata ambapo amesema mara baad ya kusaini mkataba huo sasa kazi yake kubwa ni kuhakikisha timu hiyo inaoata mafanikio ndani ya uwanja

Kivutio kikubwa katika ujio wa kocha huyo ni kuja na mwanaye Henry Omog ambaye ni beki wa zamani wa  Canon de Yaunde huku akiwa ndiye meneja wa baba yake huyo.

BERKO ATUA SIMBA, AHAHIDI KUPAMBANA NA DHAIRA

$
0
0


ALIYEKUWA kipa wa Yanga Mghana Yaw Berko ametua leo jijini Dar tayari ya kuanza maisha mpya na Simba SC.


 Berko ametua jijini leo asubuhi na ndege ya Shirika la Kenya akitokea kwao Ghana na kulakiwa na kiongozi wa ufundi wa Simba Danny Manembe.

Mara baad ya kutua Berko alipata nafasi ya kuzungumza na Salehjembe akisema anaijua Simba vizuri huku pia akimjua kipa wao namba moja Abel Dhaira ambapo atahakikisha anapambana katika mazoezi ili kujihakikishia nafasi katika timu hiyo.

“Naijua Simba, mimi sio mgeni hapa, namjua pia kipa wao yule wa Uganda lakini namtanguliza Mungu, lakini pia nitajituma mazoezini ili kuweza kujipatia nafasi.

PICHA ZA RED CARPET EBSS 2013

$
0
0


DSC_0003
Hiki ndicho kinachoendelea kwa sasa,upande wa redcarpet hapa Escape 1 Mahali ambako anazaliwa super star wa mwaka 2013 kupitia Epiq Bongo Star Search.
DSC_0002
DSC_0006
DSC_0004
DSC_0006
DSC_0015
DSC_0018

TASWIRA KUTOKA FAINALI ZA EBSS 2013

$
0
0

Mwanamuziki Snura Mushi akiwajibika jukwaani kwa kucheza wimbo wake wa 'Nimevurugwa'.
 
Mwanamuziki Walter Chilambo ambaye ndiye mshindi wa shindano la EBSS 2012 akitumbuiza
 stejini
PICHA ZOTE NA GLOBAL PUBLISHERS.

MSHINDI WA EBBS 2013 NI EMMANUEL MSUYA, AMEONDOKA NA MIL 50

$
0
0
Mshindi wa EBBS 2013 Emmanuel Msuya.

Washiriki walioingia Tatu Bora kutoka kushoto ni Elizabeth Mwakijambile, Emmanuel Msuya na Mellisa John.
Emmanuel Msuya akilia machozi ya furaha baada ya kuingia Tatu Bora.
Washiriki Elizabeth Mwakijambile, Emmanuel Msuya na Mellisa John wamefanikiwa kuingia Tatu Bora katika fainali za EBSS 2013 ndani ya Escape 1, Mikocheni jijini Dar muda huu. Wasanii walioaga mashindano ni Maina Thadei na Amina Chibaba.
PICHA ZOTE NA GPL

ZITTO: URAIS, MABILIONI YA USWISI VINANIMALIZA

$
0
0
Dar es Salaam. 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema tuhuma alizosomewa na uongozi wa Chadema katika kikao cha Kamati Kuu sizo zilizoelezwa na chama hicho mbele ya waandishi wa habari na viongozi wa chama hicho.
Aidha, amesema kuwa vita aliyopo siyo kati ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu wengi, akitaja magenge ya watu wanaotaka urais 2015 na walioficha fedha nje ya nchi walioungana wakiona tatizo lao ni yeye hivyo kutaka kumwondoa bungeni.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili kwa njia ya simu, Zitto alisema kuwa hadi sasa bado hajapokea tuhuma 11 anazokabiliwa nazo, hivyo hajui makosa hayo na bado anasubiri akabidhiwe kwa maandishi.

Ana ugomvi gani na viongozi wenzake?

Alipotakiwa kueleza iwapo ana ugomvi na watu ndani ya Chadema,  Zitto alisema kuwa huenda mambo hayo yanatokea kwa sababu mahasimu wake wa kisiasa wa ndani na nje wameamua kuungana na kupambana naye ili kumdhoofisha kisiasa kwa masilahi yao.

“Matatizo yaliyopo ni mafanikio yangu, …. nadhani hii siyo vita kati ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu wengi, pengine magenge ya watu wanaotaka urais na wale walioficha fedha zao nje wamekaa pamoja wanaona tatizo lao ni Zitto… wanajua siwezi kusemea nje maana sina kinga…, hivyo wanataka kuniondoa bungeni…” alisema.

 Aliongeza kuwa kwenye siasa kinachohitajika ni kusimamia misingi, jambo alilosema binafsi amekuwa akilifanya katika kipindi chake chote cha kisiasa.

Zitto alisema kuwa ni vyema wananchi wakawapima wabunge wao kwa kazi wanazozifanya bungeni akibainisha kuwa kati ya mwaka 2011 hadi 2013, yeye amewasilisha hoja nyingi nzuri zilizo na mashiko ikilinganishwa na wabunge wenzake wanaomtuhumu kutumiwa na CCM.

“Je, mbunge anayetumika na Chama Cha Mapinduzi anaweza kupeleka hoja ya kumng’oa Waziri Mkuu na kumshinikiza Rais mpaka akasimamisha kazi mawaziri wanane? Je, mbunge anayetumika anaweza kushikia bango watu wanaotorosha fedha nje ya nchi?” alihoji Zitto.

Tuhuma za usaliti

“Sizijui hizo tuhuma 11 kwa sababu nilichoelezwa kwenye kikao cha Kamati Kuu sicho kilichoelezwa na chama kwenye mkutano wake na waandishi wa habari… hivyo sijui kabisa hizo tuhuma zangu ni zipi mpaka sasa,” alisema.

Alisema kuwa kwenye Kamati Kuu alilaumiwa kwa masuala matatu. Akizitaja: “Nililaumiwa kuwa sifanyi kazi za chama, la pili kuwa nimemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali akague vyama kutokana na kuwa na nia mbaya na chama hicho. Tuhuma ya tatu ni ile ya kukataa kupokea posho bungeni ambapo nadaiwa kulenga kuwadhalilisha wabunge wenzangu.”
0
inShare

Zitto alisema kuwa baada ya kuzijibu tuhuma hizo mbele ya wajumbe wa kikao cha Kamati Kuu na katika mkutano wake na waandishi wa habari, akashangazwa na tuhuma alizoziita mpya kuwa anatuhumiwa kutokana na waraka ambao yeye hahusiki nao, licha ya kutajwa kuwa mfaidika tu.

“Mimi sihusiki na waraka wowote, huo unaodaiwa kusambazwa kwenye mitandao wala mwingine wowote… ni wajibu wa chama kueleza mimi nahusikaje na waraka ule,” alisema.

Madai ya Mwanasheria wa Chadema kuvunja Katiba

Zitto alisema jambo linalompa shaka kuwa huenda suala lake limelenga kumdhoofisha kisiasa ni kitendo cha mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu kuamua kuvunja katiba ya chama hicho kwa makusudi.

Alifafanua: “Katiba ya chama (Chadema), inasema kwamba kiongozi wa ngazi fulani ataondolewa kwenye uongozi na ngazi iliyomchagua. Mimi nilichaguliwa na Baraza Kuu la Chama, siyo Kamati Kuu… sasa iweje Kamati Kuu iniondoe?”

Alisema kimsingi Kamati Kuu haina mamlaka ya kumvua uongozi bali ina mamlaka ya kuweza kumsimamisha uongozi kusubiri kikao kilichomchagua kufanya uamuzi wa kumwondoa katika uongozi au kumrejesha.

Zitto alidai kuwa Lissu alisema uongo kuwa hata Dk Wallid Kabourou aliondolewa uongozi na Kamati Kuu na kwamba ukweli ni kuwa Dk Kabourou alijiondoa mwenyewe na kuhamia CCM na kwamba hata Chacha Wangwe hakuondolewa na Kamati Kuu isipokuwa alisimamishwa na kusubiri Baraza Kuu ambapo kabla ya Baraza Kuu kuketi alifikwa na mauti.

Kwa nini hapokei posho?

Alipoulizwa ni kwa nini yeye hapokei posho za wabunge alisema suala la posho siyo lake binafsi bali ni suala la imani na msimamo wa chama hicho, ambao waliuweka wakati wa kampeni na ni miongoni mwa mambo waliyowaahidi wapigakura wakati wa kampeni, hivyo yeye anachofanya ni kutimiza tu ahadi.

Aliongeza kuwa wakati wa kampeni za mwaka 2010, walikuwa wakiwaeleza wananchi kuwa wabunge wanapokea fedha nyingi na kuwa wakichaguliwa watapunguza posho hizo na kwamba Chadema ilipofanikiwa kushinda chama kilikubaliana watekeleze ahadi zile.

Alidokeza kwamba walikubaliana kutekeleza kwa kuanza na mambo mawili moja likiwa kukataa kuchukua posho za vikao, maana ni kinyume cha utaratibu na suala la pili ni kuacha kutumia shangingi la Serikali ambalo linatumika na Kiongozi wa Upinzani Bungeni.

Alisema katika kutekeleza uamuzi huo Mbowe alitangaza hatua ya kurudisha shangingi na yeye (Zitto) kama Waziri Kivuli wa Fedha akatangaza kuacha kupokea posho.

“Tulikubaliana wote tutekeleze hayo… lakini wenzangu wakashindwa kuyatekeleza, na mwenzangu akalirudia gari na analitumia mpaka sasa… kwangu mimi mafunzo niliyofundishwa kisiasa ni kwamba unayoyasema, yatekeleze, wenzangu hiyo ‘principal’ ya kutekeleza wanayoyasema hawana,” alisema.

Kuhusu tuhuma kuwa anakataa posho lakini anapokea rushwa kubwa kubwa, Zitto alisema iwapo kuna mtu aliye na ushahidi na hilo aupeleke vyombo vya dola, wamshtaki na achunguzwe kisha achukuliwe hatua.

Alisema mbali na posho, wabunge wanaongoza kwa kupewa misamaha ya kodi mbalimbali ukiwemo msamaha wa kodi ya uingizaji wa magari.

“Hii nayo tulikubaliana kuikataa… na katika kulitekeleza hili, nilipoagiza gari langu nilikataa msamaha nikalipa kodi hadi nilipoitwa na Kamishna wa Kodi na kuulizwa iweje nilipe kodi wakati nina msamaha wa kodi nikamjibu kuwa ni suala la ‘principal’ tu,” alisema.

Ruzuku

Kuhusu suala la ukaguzi wa ruzuku ya chama, Zitto alisema yeye anapokuwa Mwenyekiti wa PAC anasimamia taifa, hasimamii chama, hivyo kwa nafasi yake ya PAC na kamati nzima waliona siyo halali vyama vya siasa kukaa bila kukaguliwa.

Alisema alipigania suala hilo tangu mwaka 2011 alipomwandikia barua Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali kumuuliza kwa nini hakagui hesabu za vyama vya siasa wakati sheria inataka vikaguliwe.

Je, ana shaka kuhusu matumizi ya ruzuku ndani ya Chadema?

“Nitaweza kusema jambo hilo kwa uhakika baada ya ukaguzi kufanyika. Mpaka sasa hakuna chama ambacho kimekaguliwa, hivyo inawezekana matumizi mabaya ya ruzuku yako CCM, CUF, NCCR-Mageuzi, Chadema au yako katika vyama vyote…

“Haiwezekani kila mwaka sisi (wabunge) tunaipigia kelele Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, haiwezekani kila mwaka tunaipigia kelele Bodi ya Korosho, halafu vyama vya siasa ambavyo vinapokea zaidi ya Sh29 bilioni kila mwaka, tukisema, tuonekane wasaliti,” alisema Zitto.

Chadema yajibu

Alipotakiwa kuzungumzia madai hayo ya Zitto, jana Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa alisema kuwa hawezi kulumbana na mtu kwa njia ya magazeti na kwamba kazi yake yeye ni kufafanua Katiba, kanuni na miongozo ya Chadema pindi inapohitajika. Anaripoti Ibrahim Yamola.

Alisema endapo kama kuna vifungu katika Katiba, kanuni au miongozo vilivyokiukwa katika kufanya uamuzi hayo vibainishwe na si kuongea katika magazeti bila kueleza makosa yaliyofanyika.

“Mimi kazi yangu si kulumbana katika magazeti, kama anaona (Zitto), kuna mambo yamekiukwa anatakiwa kuyawasilisha sehemu inayohusika ili hatua zaidi zichukuliwe.

Wewe mwandishi umeoa? (Mwandishi; hapana), ungekuwa umeoa ningekuuliza hivi; unaweza kutoa siri za ndani za mke wako kwa watu wengine?,” aliuliza Dk Slaa.

Akizungumzia kuhusu mikutano inayoendelea mikoani, alisema haina lengo la kuwaeleza wananchi juu ya uamuzi wa Kamati Kuu ya kuwavua madaraka Zitto na wenzake, bali ni utekelezaji wa mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho uliofikiwa Junuari mwaka huu.

“Mikutano hiyo imeanza tangu Aprili mwaka huu, iko katika ngazi za vijiji na vitongoji vikikijenga chama na wala si kwa dhana yoyote zaidi ya hiyo,” alisema Dk Slaa.

CREDIT: MWANANCHI

KAMPUNI 100 BORA ZATAJWA

$
0
0
Dar es Salaam.  
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amesema kuwa, Serikali itaendelea kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara ili wawekezaji wa nje na ndani waweze kutekeleza majukumu yao bila kikwazo.


 Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk Abdallah Kigoda

Dk Kigoda aliyasema hayo juzi usiku alipokuwa kwenye hafla ya kuzitambua Kampuni 100 Bora zinazokua kwa kasi nchini (Top 100 Mid–Sized Companies), ambapo Kampuni ya Kipipa Millers Limited ya jijini Mwanza ilishika nafasi ya kwanza.
Kampuni hizo zilitambuliwa na kupewa tuzo kutokana na shindano linaloendeshwa na 

Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL) na KPMG Tanzania na kudhaminiwa na Benki ya NBC pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Dk Kigoda alisema shindano hilo linaimarika kila mwaka na lina nafasi kubwa ya kuimarisha uchumi kwa Kampuni za Afrika Mashariki.

Alisema ili kampuni hizo ziweze kufikia mafanikio, Serikali itajitahidi kuweka mazingira yatakayoziwezesha kufanya shughuli zake vizuri na kufanya uzalishaji kwa gharama nafuu.
Alizitaka kampuni zilizofanikiwa kuingia kwenye kundi la kampuni 100 bora, kujitambua kuwa sasa wao ni washindi na hivyo wajitahidi kufanya shughuli zao kitaalamu zaidi.
“Kwa kiwango hiki mlichofikia sasa ni washindi, mfanye kazi zenu kitaalamu zaidi,”  alisema Dk Kigoda.

Alisema kwa sasa Tanzania imeshuka kwenye nchi zenye viwango vizuri vya kufanya biashara duniani, hali inayofanya baadhi ya wawekezaji kukimbia.
Alieleza suala hilo linaipa Serikali changamoto ya kutengeneza mazingira bora na rafiki ili kuvutia wawekezaji kufanya shughuli zao kwa faida.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Zuhura Muro alisema kwa kushirikiana na KPMG, wanaendesha shindano hilo kwa sababu wanaelewa kuwa hiyo ni njia muhimu ya kuhamasisha kampuni kufanya vizuri.

Alisema kuwa, kampuni hizo ni muhimu kwa uchumi wa nchi na ustawi wake kwani kodi wanazolipa ndizo zinazotumika kwa maendeleo ya nchi.

“Sasa ni wakati wetu wa kuinuka, lakini hatuwezi kuinuka bila kuwa na watu muhimu kama ninyi (kampuni 100 bora) kwani ndiyo mnaotengeneza ajira, nyie ni watu muhimu sana kwa uchumi wa nchi hii,” alisema Muro.

Huu ni mwaka wa tatu wa shindano hilo, mwaka 2011 Kampuni ya BQ Contractors ya Dar es Salaam ilishika nafasi ya kwanza, huku mwaka 2012 Kampuni ya Helvetic Solar Contractors ya jijini Arusha ikichukua nafasi hiyo.

Mara baada ya kutangaza kuwa mshindi jana,  Mkurugenzi Mkuu wa Kipipa Millers Limited, Oliver Matemu alisema hakutarajia kushika nafasi hiyo.

“Nilipokuwa hapo ndani nilikuwa nasikia tu wakitangaza, walipofika nafasi ya 50 bila kusikia tukiitwa nilijua kuwa sisi tumerukwa,” alisema Matemu.
Matemu alisema kuwa, kampuni yake inajishughulisha na usagaji wa nafaka na kuzisambaza pamoja na kusambaza bidhaa za Kiwanda cha Bia cha Tanzania (TBL).
“Kilichotufanya tukaibuka washindi ni namna ambavyo tunajitahidi kuandaa hesabu zetu,” alisema Matemu.

Alisema kuwa, alianza shughuli hiyo kwa kununua unga kwenye mashine za watu na kuusambaza wakati huo akiwa na mtaji wa kati ya Sh1.5 milioni.
“Kwa sasa kwa mwaka nafanya biashara ya kama Sh5 bilioni,” alisema.
Kampuni nyingine zilizoingia kwenye 10 bora ni Otonde Group of Companies Tanzania Limited, iliyoshika nafasi ya pili, SEEDCO Tanzania Limited ya tatu, Kays Logistics Company Limited ya nne, Sihebs Technologies Company Limited  ya tano na Techno Brain Tanzania Limited ya sita. 
Kampuni nyingine ni Anjari Soda Factory Limited nafasi ya saba, NPK Technologies Limited nane, Palray limited ya tisa na Fomcom International Limited  nafasi ya 10.

SABAU-KIDUCHU - NEW AUDIO SIKILIZA NA KUDOWNLOAD HAPA

MZEE NA ‘JAHAZI LAKE’ WACHENGUA MASHABIKI DAR LIVE

$
0
0
Shabiki aliyevaa kihasara akinengua jukwaani.
Khadija Yusuf akiimba.
Mzee Yusuf akinengua na mpiga gitaa wake.
…Akiwaimbisha mashabiki.
Mashabiki wakiserebuka kivyao.
Shabiki akijimwaya.
Kijana aliyetuhumiwa kukwapua pochi akiwa chini ya ulinzi na pochi alilokwapua.
UKUMBI wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam, jana usiku ulifurika mashabiki katika onyesho la bendi ya taarabu ya Jahazi inayoongozwa na staa Mzee Yusuf.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL)

JALI ILIYOWAUA PAUL WALKER, ROGER RODAS ZATOLEWA

$
0
0
Mabaki ya gari aina ya Porsche baada ya kugonga mti Jumamosi iliyopita na kumwua yeye na Roger Rodas.
 
Paul Walker akipozi mbele ya kamera wakati wa kushuti filamu ya " Fast and Furious 5," huko Rome, Italia, mwaka  2011.
Wazima moto na askari wakilidhibiti eneo la ajali, ikiwa ni pamoja na kuwazuia marafiki na ndugu wasijitose kwenye moto wa mlipuko wa gari husika.
Eneo la ajali linavyoonekana likiwa limejaa moshi.
Wachunguzi wakiwa eneo ambapo gari hilo lilianza kugonga nguzo ya umeme katika Mtaa wa Hercules karibu na eneo la Kelly Johnson Parkway huko Valencia.
VIDEO kuhusu ajali iliyomwua mcheza sinema maarufu Mmarekani Paul Walker  (40) na Roger Rodas (38) wakati gari lao aina ya Porsche Carrera GT lilipoacha njia na kugonga mti kabla ya kuwaka moto, imetolewa na mmoja wa mashuhuda amesema tukio hilo ni ajali na halikuhusiana na kitu chochote kingine.
Ajali hiyo iliyomhusisha staa wa filamu ya Fast and Furious,  ilitokea Jumamosi wiki iliyopita huko California, Marekani.
Ajali hiyo ilirekodiwa na video za usalama zilizokuwa juu ya jengo moja la karibu ambazo zilionyesha moshi mwingi ukipanda juu na baadaye kutokea mlipuko.
Mashuhuda mwingine ambaye ni dereva amesema kwamba Rodas na Walker walilichukua gari lao kwenda kulijaribu kwa vile walihisi lilikuwa na dosari na wala hawakuwa wakiliendesha kwa ajili ya burudani.
CHANZO NI DAILY MAIL

Rais Kikwete amteua Engineer Felchesmi Mramba kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Engineer Felchesmi Mramba kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Desemba 2, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo umeanza leo hii.

Kabla ya uteuzi wake, Eng. Mramba alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo la TANESCO.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

2 Desemba, 2013

KATUNI

RAIS KIKWETE AMTEUA DR. ASHA-ROSE MIGIRO KUWA MBUNGE WA HESHIMA

$
0
0
Dr. Asha-Rose Migiro.TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dr. Asha-Rose Migiro kuwa Mbunge.
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam leo, Jumanne, Desemba 3, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dr. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Desemba 2, 2013.
Dr. Asha-Rose Migiro ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chama cha Mapinduzi.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
3 Desemba, 2013

LEMA ATUNGIWA NYIMBO YA USHUJAA ARUSHA‏ - HIPO HAPA

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

RAY: CHUCHU NDIYE MKE WANGU

$
0
0

SINEMA ya madai mazito dhidi ya mastaa wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’, Ruth Suka ‘Mainda’ na Chuchu Hans ambaye ni mke wa mtangazaji Frank Mtao kuchanganywa kimapenzi na Vincent Kigosi ‘Ray’ sasa inaendelea na mhusika mkuu Ray amefunguka na kueleza yake ya moyoni huku akisisitiza: “Chuchu ndiye mke wangu, tarajieni makubwa soon (hivi karibuni).”
Akizungumza wikiendi iliyopita katika Viwanja vya TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa na mechi kati ya wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Muvi, Ray aliwashangaa waandishi kwa kumshambulia kutoka kimapenzi na Chuchu.
 
Mwandishi alianza kwa kumwuliza: “Ray magazeti yanaandika kuhusu wewe kutoka na Chuchu Hans ambaye ni mke wa mtu. Mainda amezungumza mengi. Kukaa kwako kimya bila kufafanua chochote siyo kitu kizuri. Tafadhali, hebu zungumza japo kidogo kuhusu madai ya Mainda.”
RAY: Sikia nikuambie, huyo Mainda utoto unamsumbua. Haniumizi kichwa kabisa. Kuhusu Chuchu... si mmeshaandika? Endeleeni kuandika lakini soon mtashuhudia kitu kikubwa sana.

RISASI: Ni kitu gani hicho?
RAY: Niacheni na Chuchu wangu.... kifupi ndiye mke wangu na itawashangaza wengi. Halafu mimi nawashangaa sana. Yaani mimi kutoka na Chuchu mnakuzaaaa... mbona alivyokuwa na ma-boyfriend zake wengine hamkuandika? Kwa sababu ni Ray basi mkaona ni habari. Mimi ninavyojua Chuchu siyo mke wa mtu.
Kwanza mimi sijamchukua kutoka mikononi mwa mumewe kama mnavyosema. Chuchu tayari alikuwa na maisha yake mapya. Nilimchukua kutoka kwa Libert (hajafafanua zaidi ni nani). Mbona alivyokuwa na huyo Libert  hamkuandika? Kifupi niacheni na maisha yangu.
RISASI: Vipi kuhusu Johari?
RAY: (Huku akikimbia kuingia uwanjani) Tena huyo mama yako (akimuonesha mwandishi Johari) anakuja.
Mwandishi wetu aliachana na Ray aliyekuwa akiingia uwanjani na kumfuata Johari lakini hakuwa tayari kusema chochote achilia mbali hata kumsikiliza mwandishi wetu!

TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni gazeti hili liliandika habari yenye kichwa MAINDA: NIMETOA MIMBA YA RAY. Ndani yake Mainda alifunguka mengi ikiwemo kuchanganywa kimapenzi na Ray, yeye na wenzake Johari na Chuchu Hans.
CREDIT:GPL

ZIARA YA KATIBU MKUU DK WILLIBROD SLAA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa ataanza ziara ya siku 20 katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida kuanzia Desemba 4-23, mwaka huu.
Lengo la ziara hiyo ambayo imetokana na maombi ya muda mrefu ya viongozi wa chama katika maeneo husika, ni kuimarisha na kukagua uhai wa chama katika ngazi za chini hususan kata na majimbo mikoa hiyo.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakutana na wananchi katika mikutano ya hadhara ambapo atazungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa na eneo husika, kisha atafanya vikao vya ndani vya kichama.
Ziara hiyo itaanzia mkoani Shinyanga ambapo siku ya Jumatano Desemba 4, mwaka huu, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Wilaya ya Kahama, siku inayofuata Desemba 5, atakuwa Wilaya ya Kakonko, Jimbo la Buyungu na Desemba 6, atakuwa Jimbo la Muhambwe.
Ratiba ya siku zinazofuata itaendelea kutolewa kwa vyombo vya habari.
Imetolewa Jumanne, Desemba 3, 2013, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA

KAJALA APETA

$
0
0


Kajala Masanja.
Mahakama ya Rufaa Kanda ya Dar imeridhia hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya faini ya Sh. Milioni 13 na kumwachia huru staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja.

Kajala sasa anapeta katika rufaa hiyo iliyofunguliwa na mumewe, Faraji Agostino, ambaye anatumikia kifungo cha miaka mitano katika hukumu ya kesi ya kutakatisha fedha haramu iliyotolewa mapema mwaka huu. CREDIT GPL

BABY MADAHA: DIAMOND FUSKA!..SOMA HAPA

$
0
0
ACHANA na mabifu yaliyotangulia, hili ni jipya kabisaa! Msanii wa sinema na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ameingia kwenye bifu zito na Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na kudai staa huyo wa Wimbo wa Number One ni mzinzi ‘fuska’, Amani lina mkanda mzima.
Diamond Platnumz na Wema Sepetu.
Bila kumung’unya maneno, mapema wiki hii, Baby Madaha alimvaa Diamond ambaye ni Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB) akimtuhumu kuwa na tabia za kifuska.
Baby Madaha alidai hata muziki anaoufanya Diamond kamwe hauwezi kulingana na mafanikio makubwa ya jina lake zaidi ya kubebwa na skendo tu.

CHOKOCHOKO ZILIVYOANZA
Kupitia mitandao ya kijamii, ilivuja posti ambayo ilidaiwa kutoka kwa Baby Madaha ikimpaka Diamond kuwa siyo mwanamuziki kama ilivyo kwa wasanii wengine wenye uwezo mkubwa, akitolea mfano Elias Barnaba wa THT.
Sehemu ya posti hiyo ilionesha kuwa, Diamond si msanii wa muziki bali ni mzinzi f’lani hivi anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi.
“Siku wanawake maarufu nchini Tanzania watakapojitambua na kuacha kulewa penzi la Diamond, huo ndiyo utakuwa mwisho wa maisha yake kimuziki kwa sababu hatakuwa na jipya na hivyo soko lake litaporomoka,” ilisomeka posti hiyo.

UKWELI NI UPI?
Baada ya ishu hiyo kugeuka habari ya mjini na kuibuka kwa makundi mawili yanayokinzana, Amani lilimtafuta Baby Madaha ili kujua ukweli wa posti hiyo ndipo akatiririka aya za kuthibitisha kuwa picha haziivi, hamkubali Diamond na kudai hata kimuziki hamkubali kwani anaamini wapo wanamuziki wanaofanya vema katika gemu kuliko yeye.
“…tuseme ukweli, Diamond ni mfanyabiashara siyo mwanamuziki. Kuhusu hiyo posti iwe ni mimi nimeandika au si mimi lakini kimsingi hayo maneno yanamstahili kabisa. Mzinzi tu.
“Diamond anabebwa na media (vyombo vya habari). Kuna wanamuziki wengi wazuri sembuse yeye? Ana nini haswa?” alihoji Baby.
AMANI LAMGEUKIA DIAMOND
Baada ya kusikia maelezo ya Baby kwa kifupi, Amani lilimuweka ‘pending’ kwa muda na kumwendea hewani Diamond ili liweze kujua upande wake analizungumziaje bifu hilo ambalo lilikuwa likienea mitandaoni kama moto wa kifuu.
Tofauti na matarajio ya mapaparazi wetu kwamba huenda angejibu mashambulizi makali kwa Madaha, Diamond au ‘Sukari ya Warembo’ aling’aka huku akimponda mwanadada huyo na kumshangaa:

BOFYA HAPA KUMSIKIA
“Daaah! Huko ni kunishusha…mimi na huyo (Baby) wapi kwa wapi kamwe huwezi kunilinganisha na mtu ambaye yupo chini yangu sana, nikijibizana naye nitajishusha tu. Ingekuwa ni mtu mkubwa mwenye levo yangu hapo ningesema natakiwa kusema neno.
“Hana lolote huyo anatafuta ‘kiki’ tu kupitia mimi, nipo na dili zangu za maana nipoteze muda kwake? Atafute wa levo yake na wala si mimi.”
UZINZI VIPI?
Alipoulizwa kuhusu suala la uzinzi ambalo Baby Madaha aliumaanisha katika posti yake, Diamond aliendelea kukazia kuwa hana muda wa kupoteza kwa mtu kama Baby Madaha ambaye kimsingi ni kama ardhi na mbingu.
“Huyo anatafuta kiki tu, aachane na mimi…mbona hatufanani kabisa mimi na yeye wapi kwa wapi?” alikazia Diamond a.k.a Weka Mbali na Watoto Wazuri wa Kike.

BABY AREJEA HEWANI
Wakati mapaparazi wetu wakimalizana na Diamond, kilongalonga kimoja cha paparazi wetu kilikuwa kikionesha kinaita, ilivyokatika ya Diamond, Baby akapanda hewani kwa mara nyingine.
Safari hii alimchana laivu: “Nimeisoma upya posti yenyewe, kilichopo humu ni ukweli mtupu. Hakuna hata tone la uongo, wewe utamlinganisha Diamond na mtu kama Barnaba? Huyu ni mfanyabiashara tu, hajui kuimba kwa kutumia vyombo kama mimi.
“Diamond hawezi kupiga chombo hata kimoja cha muziki atajiitaje mwanamuziki? Anastahili kabisa ujumbe huu.”

UFUSKA
Mapaparazi wetu walilazimika kumtwanga swali Baby Madaha kuhusiana na ufuska ambao ulikuwa umetajwa katika maelezo ya awali, kama endapo Diamond ni mzinzi au yeye ndiyo mzinzi.
Katika maelezo yake, Baby Madaha aliwashangaza mapaparazi wetu kwa kutaja namna gani anaweza kumuita Diamond mzinzi. Sikia:
Amani: “Umesema Diamond si mwanamuziki, je, suala la uzinzi ni nani analo kati yako na yeye?”
Baby: “Mimi si mzinzi. Diamond ndiyo mzinzi tena sana tu.”
Amani: “Uzinzi wake upo wapi?”
Baby: “Kitendo cha kubadilisha wanawake, kufumaniwa na Wema Sepetu akiwa na Jokate Mwegelo ndiyo uzinzi wenyewe huo.”
Amani: “Kwani wewe hujawahi kuwa na wanaume tofauti? Hujawahi kufumaniwa?”
Baby: “Mimi sijawahi, yeye amewahi na hakuwahi kukanusha hivyo inadhihirisha kuwa ni kweli. Kwangu mimi kila aliyetajwa kutoka na mimi kama haikuwa kweli, nilikanusha mara moja yeye mbona hakanushi?”
Amani: “Kwani Diamond alifumaniwa na nani?”
Baby: “Acha hizo, kwani hukumbuki kipindi cha Wema? Mara alinaswa na Aunt mara na… yule ndiyo mzinzi sasa.”

KWANI WALITONGOZANA?
Kuhusu suala la kutongozwa, Baby alisema Diamond hajawahi. Cha kushangaza zaidi, alisema hata kama ikitokea siku staa huyo akamtongoza kamwe hawezi kumkubalia kwani hawaendani hata kidogo.
Alisema yeye ni mtu wa kutembea na vigogo na si vitoto kama Diamond.
“Hana hela, kamwe siwezi kumkubalia. Ni mtu ambaye ana vihela mbuzi sasa mtu kama yeye mimi wa nini? Ndiyo maana aliwahi kukimbiwa na mwanamke kwa kuwa hana hela.
“Tena yule mwanamke akaenda kwa kigogo mwenye hela, mimi na yeye ni mbalimbali kabisa. Hata muziki ninaofanya hauwezi, mimi ninaimba RnB yeye anafanya Pop, tuko tofauti kabisa,” alisema Baby pasipo kumtaja mwanamke aliyemkimbia Diamond.

TUJIKUMBUSHE PANDE ZOTE
Diamond aliwahi kuripotiwa kutoka kimapenzi na ‘totoz’ kibao wakiwemo yule wa mwanzo aliyemzingua aitwaye Sarah, Rehema Fabian, Jacqueline Wolper, Upendo Mushi ‘Pendo wa Maisha Plus’, Wema Sepetu, Natasha (Video Queen wa Wimbo wa Moyo Wangu), Najma (aliwahi kuwa mpenzi wa Mr. Blue), Jokate Mwegelo, yule demu wa Kenya na aliyekuwa mwigizaji aliyefulia ambaye ni mke wa mtu.
Kwa upande wake Baby Madaha anayekimbiza na ngoma yake ya Summer Holiday naye si haba kwani aliwahi kuripotiwa kuminya kimapenzi na yule mtoto wa mwanasiasa maarufu Bongo (jina lipo), Mwisho Mwampamba, Dokta Pakir, Juma Nature na Joe Kairuki aliye naye sasa ambaye ni mume wa mtu.
CREDIT: GPL

NCHIMBI ABEBESHWA ZIGO LA PROF KAPUYA

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi ameingia lawamani kwa kudaiwa kumlinda Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), anayedaiwa kumbaka na kumtishia kumuua binti wa miaka 16.

Akizungumza kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi wa simu (sms) na Tanzania Daima jana, binti anayelalamika kutishiwa maisha na Profesa Kapuya, amemtuhumu Waziri Nchimbi kushindwa kulishughulikia suala hilo mapema licha ya kuwa na taarifa za tukio hilo muda mrefu.

Binti huyo alisema kuwa Dk. Nchimbi ni miongoni mwa mawaziri na viongozi wa CCM waliokuwa wakifahamu kila kinachoendelea dhidi ya malalamiko husika.

Alibainisha kuwa makada hao wa CCM walikuwa wakifanya jitihada za kuhakikisha manyanyaso na vitisho kutoka kwa Profesa Kapuya haviwekwi hadharani.

Katika kile kinachoonekana ni kukata tamaa juu ya usalama wake pamoja na dada yake, binti huyo alisema amewasiliana na Waziri Nchimbi asubuhi ya jana na kwamba waziri huyo hakuonyesha dalili yoyote ya kujali madhila yao.

Alisema kutokana na Waziri Nchimbi kutokutilia uzito malalamiko yao, waliamua kumuandikia ujumbe mfupi wa maandishi wakimshutumu kuendelea kumlinda Profesa Kapuya.

“Nimemwambia katika ujumbe mfupi wa maneno (sms) kuwa jukumu la polisi iliyo chini ya wizara yake ni kuhakikisha wananchi wanalindwa dhidi ya manyanyaso na vitisho vya aina yoyote, na kwamba katika kadhia hii ya Kapuya Jeshi la Polisi limekuwa kimya.

“Matukio mbalimbali ya kihalifu yenye kutatanisha yametokea nchini, lakini serikali inasema haiwajui wahusika na kwamba hata hili la kutishiwa maisha pia serikali inasubiri nife,” alisema binti huyo.

Binti huyo alisema katika ujumbe huo aliomtumia Waziri Nchimbi, pia amemdokezea kuwa haogopi kitakachompata ilimradi yupo katika msitari wa kutafuta haki yake.

Amedai kuwa hivi sasa bado kuna jitihada kubwa za watu walio karibu na Kapuya kuwataka waachane na suala hilo.

“Juzi mtu aliye karibu na Kapuya ametuhoji tunataka nini ili tuachane na jambo hili… sisi tumemjibu tunataka haki si kingine chochote,” alisema.

Jitihada za Tanzania Daima kumpata Waziri Nchimbi ziligonga mwamba baada ya simu yake ya mkononi kuita bila majibu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) haukujibiwa.

Wanaharakati walia na polisi
Wakati sakata hilo la Kapuya likiwa kwenye hali ya kutoeleweka, baadhi ya wanaharakati na watetezi wa masuala ya jinsia wamelitaja Jeshi la Polisi kwa kuchangia vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwenye viwanja vya Mtandao wa Jinsia (TGNP).
Joseph Mathias, alisema vitendo hivyo vya ukatili vinaongezeka kutokana na polisi kuwalea na kuwalinda baadhi ya vigogo wanaovitenda.

Bila kumtaja jina, Mathias alisema hivi karibuni kiongozi mmoja anahusishwa na ubakaji na kutishia kuua, lakini hadi sasa hajafikishwa mahakamani.
Mathias, alisema pamoja na dawati la kupinga ukatili wa kijinsia kupata taarifa hiyo, lakini hadi leo halijamchukulia hatua yoyote ile kama inavyofanya kwa watu wengine waliofanya makosa kama hayo.

Aliongeza kuwa polisi bado ni tatizo katika mapambano hayo, na kama hawatabadilika kiutendaji kuna uwezekano tatizo hilo likazidi kushamiri.
“Kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria watu kama hawa, kumekuwa chanzo cha baadhi ya watu kuyachukulia matendo haya ya ukatili wa kijinsia kuwa ni haki yao,” alisema Mathias.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TGNP, Anna Sangai, alisema changamoto kubwa inayochangia vitendo hivyo katika jamii ni mila potofu.

“Sisi TGNP tunalichukulia kuwa ni la kirasilimali, hivyo tunaishauri serikali ijaribu kutenga fedha za kutosha na kuzielekeza kwenye Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi na Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ili zifikishe elimu bila vikwazo kwa jamii,” alisema.
Anna alisema endapo jamii itapatiwa elimu kuhusu ukatili huo, anaamini kuwa vitendo hivyo kwa kiasi kikubwa vitapungua.

Aidha, jamii nayo imetakiwa kuondokana na mila potofu kwa kuwaona wanawake si lolote katika kuchangia masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Mwakilishi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Judith Kizenga, alisema serikali imejipanga kukamilisha sheria zote ambazo zitaweza kupambana na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.

Kuruthumu Mikidadi, ambaye ni mwakilishi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, alikiri 
kuwa dawati la jinsia linakabiliwa na changamoto mbalimbali, lakini hali hiyo inatokana na uchanga wake.

Awali kwa nyakati tofauti, washiriki zaidi ya wanne kutoka mikoa ya Mbeya, Morogoro na Dar es Salaam, walilishambulia dawati hilo kuwa watendaji wake wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa na kushindwa kutoa haki.
Walisema wakati mwingine mhalifu anamfikishwa kwenye dawati hilo, lakini cha kushangaza kesho unamkuta ameachiwa katika mazingira tata.
CREDIT TANZANIA DAIMA
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>