Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

Wajue nyota Samatta aliocheza nao Simba SC

$
0
0


Mbwana Samatta.
Na Said Ally
GUMZO hapa nchini ni juu ya mshambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana Samatta kutwaa tuzo ya mchezaji Bora wa Afrika kwa upande wa wachezaji waonacheza soka la ndani. Tuzo ambayo ni ya kwanza kwa hapa nchini.
Lakini mashabiki wengi wanamjua Samatta akiwa na kikosi hicho lakini hawatambui nyota ambao waliwahi kucheza na mshambuliaji huyo akiwa Simba. Makala haya yanakuchambulia nyota waliocheza nae akiwa ndani ya kikosi hicho na sasa wapo wapi.
kaseja
Juma Kaseja.
Makipa 
Juma Kaseja – Mbeya City
Mkongwe huyu alicheza na Samatta kwa kipindi kifupi mno ingawa kwa sasa amepungua umaarufu lakini bado yumo kwenye pilikapilika za soka, kwa sasa anaitumikia Mbeya City. Kwa inavyoonyesha, kawaida ya soka ilivyo, alipofikia Kaseja ni ndoto kutwaa tuzo kama ya Samatta.
Ally Mustapha ‘Barthez’ – Yanga
Kama ilivyo kwa Kaseja, baada ya kukaa Simba kwa muda, naye amesepa, yupo Yanga sasa ambapo amekuwa kipa wa kuaminika katika timu hiyo, naye kufikia mafanikio haya ya Samatta ni kazi ngumu kutokana na timu aliyepo.
Salum Kanoni – Kagera Sugar
Alikuwa anacheza beki ya kulia ambapo baada ya mambo kumuendea kombo akaihama Simba na kutua Kagera Sugar ambayo ndiyo anaitumikia mpaka sasa, anaingia katika mkumbo wa Kaseja na Barthez wa inavyoonyesha kufikia mafanikio ya Samatta ni ndoto.
Juma Jabu – Kagera Sugar
Alikuwa maarufu kama ‘JJ’ ambapo alifanya vyema akiitumikia nafasi ya beki wa kushoto ambapo naye baadaye alifungashiwa virago vyake na kujiunga Kagera Sugar. Ni ndoto kwake kuchukua tuzo hii
Nyosso1
Juma Nyosso.
Juma Nyosso – Mbeya City
Anatumikia kifungo cha miaka miwili ya kuwa nje ya soka kutokana na kumdhalilisha nahodha wa Azam, John Bocco. Kwake pia itakuwa ngumu kuona beki huyu siku moja akitwaa tuzo hii ya Samatta ingawa alikuwa moto enzi hizo.
Meshack Abel – Bandari
Aliwahi kwenda Kenya kucheza soka la kulipwa katika timu ya Bandari lakini akarudi nchini msimu uliopita na kujiunga na Polisi Moro kabla ya mwaka huu kupotea na kusikujulikana .
Kelvin Yondani – Yanga
Beki kisiki anayeendelea kudunda akiwa na kikosi cha Yanga, licha ya uimara wake lakini itakuwa jambo la kusshangaza kuona ananyakua tuzo hii ya Samatta kwani umri nao siyo rafiki tena kwake.
Jerry Santo- Posta Rangers
Yupo kwao Kenya ambapo pia aliwahi kuichezea Coastal Union baada ya kuondoka Simba, hana matumaini yoyote kwa kuwa timu yake haiwezi pia kumbeba.
Abdulhalim Humud – Coastal Union
Bado anaendelea kucheza soka lake maridadi akiwa na Coastal Union ya Tanga ingawa aliwahi kuichezea timu ya Sofapaka baada ya kuondoka Simba. Kwa mambo yanavyoonyesha ndiyo ameshamaliza soka lake na kufikia mafanikio ya Samatta ni ‘Impossible’.
Mohamed Banka – Friends Rangers
Amebadili upepo sasa kwani yupo Friends Rangers ya daraja la kwanza baada ya kurejea akitokea Kenya alipokuwa na kikosi cha Bandari, alikuwa kiunga mahiri enzi hizo, maisha yamebadilika umri umemtupa mkono kufikia kwa Samatta.
Nico Nyagawa – Amestaafu
Aliwahi kuwa meneja katika klabu hiyo baada ya kuachana na soka ambapo sasa anashugulika na kikosi cha pili.
Hillary Echessa – Chemelil Sugar
Kama ilivyo kwa Santo, Echessa naye amerejea kwao na sasa anaitumikia timu ya Chemelil Sugar.
Amri Kiemba – Stand United
Yeye naye bado anakomaa kwenye soka ambapo yupo na kikosi cha Mfaransa, Patrick Liewig cha Stand United ya Shinyanga, hawezi tena kuwa bora na kufikia mafanikio haya.
Rashid Gumbo – Hajulikani
Aliwahi kwenda kucheza soka la kulipwa katika visiwa vya Shelisheli lakini kwa sasa hasikiki na haijulikani kama amepata timu ya kuichezea au la.
Patrick Ochan – URA
Ndiye aliyekwenda na Samatta katika klabu ya Mazembe lakini yeye hakuwa na nafasi sana ndani ya kikosi hicho na kujikuta akitimkia katika klabu ya URA ya Uganda, naye kwa hali inavyoonyesha kufikia mafanikio ya Samatta ni ngumu na haitawezekana.
Emmanuel Okwi – Sonderjyske
Kipenzi cha mashabiki wa Simba ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Sonderjyske ya Denmark, Mganda huyu labda akirudi Afrika kuna siku anaweza kutwaa tuzo hii.
Mussa Mgosi – Simba
Ndiye nahodha wa Simba kwa sasa lakini amekuwa akikosa nafasi ya kuanza ndani ya kikosi cha kwanza ingawa alikuwa bora sana wakati Samatta anacheza, kufikia levo za Samatta kwa kipindi hiki ni ngumu kwake.
Ahmed Shiboli – Coastal Union
Amejiunga katika kikosi hicho msimu huu baada ya kutamba na African Sports alipokuwa nayo daraja la kwanza, haitawezekana tena kufikia kwa Samatta.
Amir Maftah – Friends Rangers
Yupo daraja la kwanza na timu ya Friends Rangers, taswira ya kuchukua tuzo imefifia mno.
Uhuru Suleiman – Royal Eagle
Anacheza soka la kulipwa katika timu ya Jomo Cosmos ya Afrika Kusini lakini ametolewa kwa mkopo kwenye timu ya Royal Eagles, labda kwa maajabu ya Mungu lakini kwa sasa ni ndoto kufikia kwa Samatta.
Joseph Owino – Uganda
Alitimka ndani ya kikosi hicho na kurejea kwao katika timu ya Tusker. Hana misimu mingi sana ya kucheza soka, hivyo kufikia kwa Samatta ni ndoto.

Mzee Samatta: Nilimzuia Samatta kwenda Yanga

$
0
0


Mzee Samatta.
USIKU wa kuamkia Ijumaa ya wiki iliyopita, nahodha mpya wa Taifa Stars na straika wa TP Mazembe, Mbwana Samatta, alifanikiwa kunyakua Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wanaocheza ndani baada ya kuwabwaga, Mcongo, Robert Kidiaba na Mualgeria, Baghdad Bounedjah.
Kutokana na mafanikio aliyoyapata straika huyo anayetajwa kujiunga na Genk ya Ubelgiji, Championi lilimsaka baba yake, Ally Samatta kutaka kufahamu maisha ya Mbwana na yaliyojiri baada ya kutangazwa kuwa mshindi.
Unajisikiaje mwanao kuchukua tuzo?
“Kiukweli najisikia raha sana, namshukuru mwenyezi Mungu kwa sababu furaha niliyokuwa nayo mpaka nililia machozi maana sikutegemea kitu kama hiki kutokea sasa hivi.

IMG_3516 
Ulishawahi kuhisi kuhusu hilo?
“Nilishawahi lakini siyo kwa wakati huu kwa sababu alipokuwa ana umri wa miaka saba, kuna kocha mmoja alikuwa anafundisha timu za vijana Simba anaitwa Maka Mwalwisi, aliwahi kunieleza kuwa kijana wangu atafika mbali.

“Unajua alikuwa hakosei kabisa katika kutoa pasi zake kitu ambacho kilimvutia Mwalwisi, naona anafuata nyayo zangu.
Nini kilichobadilika kwa Samatta?
“Kwanza amekuwa mkubwa na ameongeza umakini uwanjani tofauti na zamani alipokuwa bado kijana, hata hivyo, kuna vitu nilikuwa namuongezea kwa sababu mimi mwenyewe ni kocha, kiukweli vipo vitu vingi nilivyokuwa nampatia kijana wangu kama suala la nidhamu na uvumilivu ndani na nje ya uwanja.

“Kimsingi nilikuwa namjenga katika misingi ya kupambana asiwe mtu wa kukata tamaa au kulalamika uwanjani iwapo inatokea amechezewa vibaya, zaidi nilimtaka kuchukulia ni hali ya kawaida katika mchezo kwa mtu uliyemshinda lazima atakuwa anakuchezea vibaya ili kukudhoofisha,” anasema mzee Samatta.
Kabla ya Samatta kutimikia TP Mazembe akitokea Simba mwaka 2011, aliwahi kucheza na kaka yake, Mohammed Samata katika timu ya Mbagala Market ambayo baadaye ilikuja kuitwa African Lyon, kwa sasa Mohammed anakipiga Mgambo JKT inayoshiriki Ligi Kuu Bara.
Championi lilimuuliza mzee Samatta kwa upande wa Mohammed kama anaweza kufikia mafanikio kama ya mdogo wake?
“Mmh! Mohammed, sidhani kama ataweza kufikia huko kwa sababu ana kitu kimoja kinachomponza siku zote licha ya mara nyingi kumuambia, kiukweli anaujua mpira na nimekuwa nikimwambia siku zote kwamba hana nguvu halafu anapenda kucheza soka la Kibrazili.
“Unajua siku zote makocha wanapenda kuwa na mchezaji ambaye akishapunguza watu tayari anaelewa nini cha kufanya, lakini yeye ni tofauti, anapokuwa na mpira ndiyo anazidi kupoa kitu ambacho ni tofauti na Mbwana ambaye akiwa na mpira akili yake inakuwa katika kushambulia tu na hata akikutana na kikwazo atajitahidi ili afikie lengo lake la kwenda kushambulia.
“Lakini Mohammed yeye hapendi kucheza soka la aina hiyo na ndiyo kitu kinachomgharimu lakini kama anashindwa kuelewa ninachomwambia basi hawezi kufanikiwa na kufikia mafanikio ya mdogo wake au zaidi ya hapo, ingawa huwezi jua mipango ya Mungu ipoje.
Unashabikia timu gani hapa nchini?
“Kwa hapa nyumbani ni shabiki wa Simba, lakini nje ya Tanzania naishabikia Manchester United.

Baba alimgomea kwenda Yanga
“Wakati Mbwana akiwa mdogo, viongozi wa Yanga walinifuata na kutaka kumchukua ili akajiunge na timu yao, lakini niliwakataliwa kutokana na timu hiyo kuwa na historia ya kuwazuia wachezaji kwenda kucheza soka nje ya nchi. Nikaona kama angejiunga nayo basi angeweza kuishia hapahapa tu na kukatisha ndoto zake za kucheza nje.

Vipi kwa upande wa mama Samatta, anapenda soka?
“Kwa ufupi mke wangu anapenda michezo kwa sababu alipokuwa shule alikuwa akicheza netiboli, halafu mimi nilikuwa namsumbua kila ninapotoka mazoezini aniwekee maji ya moto ya kuoga na hata nilipokuwa nikicheza alikuwa anakuja kuniangalia.

“Tena jambo zuri, amekuwa akimuunga mkono Mbwana.”
Mzee Samatta amefunguka juu ya mtoto wa Mbwana anayeitwa Kareem, alipoulizwa kama anaweza kufuata nyayo za baba yake

“Naamini lazima atafuata nyayo za baba yake kwa sababu wajukuu zangu wote wanacheza mpira na ukizingatia muda wote tunaye hapa kwa kuwa nilimkataza asiende na familia yake DR Congo ili apunguze majukumu na afanye kazi yake vizuri kwani tulimueleza tutamaliza kila kitu kitakachotokea huku,” alisema mzee Samatta ambaye alikuwa polisi enzi zake.

Kwa Hili la Samatta, Serikali Inafanya Double Standards...Mbona Diamond Hajawahi Fanyiwa Sherehe wala Kupewa Zawadi na Serikali?

$
0
0
Wapendwa wanajukwaa na watanzania kwa ujumla, ni dhahiri kwamba sote tunapenda kuona nchi yetu ikisonga mbele kitaifa na kimataifa katika michezo na sanaa mbalimbali. Tumeshuhudia baadhi ya vijana wetu wakifanya vinzuri kimataifa na kuiletea heshima tele nchi yetu.

Sasa pamoja na heshima hii nina jambo ambalo naliona hakika halijakaa sawa na pengine linaleta picha mbaya kwa wananchi kuanza kudhani labda ni michezo au sanaa za aina fulani tu ndizo ambazo serikali inazithamini. Ni wiki iliyopita ambapo tumeshuhudia mchezaji wa soka Mbwana Samatta akitangazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika. Tumeshuhudia namna serikali ilivyomtembeza mtaani kama kumpongeza kwa tuzo aliyopata. Leo hii muda huu Vodacom na serikali wameandaa hafla ya kumpongeza kwenye Hotel ya Hyat Regend. Kwa mujibu wa posts zinazowekwa na Vodacom katika mtandao wa instagram ni kwamba Samatta amepewa zawadi na serikali pesa taslim na kiwanja huko Kigamboni. Napongeza kwa hilo ni jambo jema hasa katika kutia moyo.

Sasa hoja yangu inakuja hapa, je serikali inayatambua mafanikio ya mpira wa miguu peke yake na si sanaa zingine pia? Nasema hivi nikichukulia mfano Diamond Platinumz. Hakuna mtu asiyetambua mafanikio aliyopata Diamond katika muziki kiasi cha kuiletea heshima kubwa nchi yetu katika Afrika na dunia nzima kwa ujumla. Mbali na tunzo nyingi alizopata Diamond katika Afrika hii, ameweka historia ya kuwa msanii wa kwanza Afrika kushinda tunzo ya dunia inayotolewa na MTV. Ni msanii aliyewafanya waafrika na dunia kwa ujumla waanze kujifunza na kukielewa kiswahili hasa kutoka na nyimbo zake kutumia kiswahili na hata katika nyimbo anazoshirikishwa nazo anaimba kwa kiswahili. Ni msanii aliyefanya soko la mziki wa Tanzania likabadilika hasa katika suala la malipo wanayopewa wasanii katika matamasha na shoo wanazoalikwa. Ni mwanamuziki pekee wa Tanzania aliweza kuzivuta media za kimataifa kama BBC, Aljazeera na CNN kuweza kufanya naye interview.

Pamoja na mafanikio yote hayo hakuna hata kiongozi mmoja aliyediriki kumpa hongera Diamond kwa tunzo kubwa ya Dunia aliyoipata. Nimejiuliza sana na kudhani labda michezo na sanaa zinazothaminika na serikali ni mpira wa miguu tu.

KOMBE LA MAPINDUZI LAGOMA KUBAKI TANZANIA, WATOTO WA MUSEVENI WAONDOKA NALO KWAO

$
0
0
 
Wachezaji wa URA FC wakishangilia ubingwa wao
Unaweza ukasema kisicho riziki hakiliki, hiyo ni baada ya timu ya Mtibwa Sugar kulikosa tena kombe la Mapinduzi Cup kwa mwaka 2016 kufuatia kupoteza mchezo wa fainali kwa magoli 3-1 dhidi ya URA ya Uganda kwenye mchezo uliochezwa usiku wa Jumatano January 14, 2016 kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.
URA walianza kupata bao la kwanza dakika ya 16 kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Julius Ntambi bao ambalo lilidumu kwa dakika zote 45 za kipindi cha kwanza.
Kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime akivalishwa medali yake
Kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime akivalishwa medali yake
Kipindi cha pili Mtibwa waliongeza mashambulizi kwenye lango la URA lakini umahiri wa safu ya ulinzi ya timu hiyo ikiongezwa na nahodha wao Simeon Massa na golikpa wa timu hiyo Bwete Brian.
Peter Lwasa aliyetokea benchi ndiye aliyezima ndoto za Mtibwa kuibuka mashujaa wa kombe la mapinduzi mwaka huu baada ya kutupia bao mbili kambani na kuihakikishia timu yake ushindi na kubeba ndoo ya Mapinduzi. Lwasa alipachika wavuni magoli yake dakika ya 85 na 88 kipindi cha pili.
Nahoha wa URA FC Simeon Massa akipokea kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Mtibwa Sudgar
Nahoha wa URA FC Simeon Massa akipokea kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Mtibwa Sudgar
Jafar Salum aliipatia Mtibwa bao la kufutia machozi dakika ya 90 na kuifanya timu yake imalize mchezo huo ikiwa ya pili kwa mara nyingine tena baada ya mwaka 2015 kumaliza ikiwa nyuma Simba ambao ndiyo walitwaa kombe hilo.
Mtibwa fainali 4
Mshindi wa Mapinduzi Cup ametwaa kitita cha shilingi milioni kumi taslimu wakati mshindi wa pili amejinyakulia shilingi milioni tano.
Mtibwa fainali
Kesho Mtibwa watarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mwendelezo wa mechi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ambapo Jumamosi watakutana na Simba SC ambao waliwatupa nje ya mashindano ya Mapinduzi kwenye hatua ya nusu fainali.
Mtibwa fainali 2

Pato la Taifa laendelea kukua

$
0
0

Pato la Taifa katika kipindi cha Robo tatu ya mwaka 2015 limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 6.3 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.4 katika kipindi cha mwaka 2014.
 
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.
 
Dkt. Albina amesema kuwa kutokana na ongezeko hilo Serikali imeendelea kutoa huduma za kijamii zikiwemo umeme, afya na maji.
 
“ Pato la Taifa kwa robo tatu ya mwaka 2015 limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 6.3 ukilinganisha na asilimia 5.4 katika robo tatu ya mwaka 2014” Alisema Dkt. Albina.
 
Dkt. Albina ameongeza kuwa kuongezeka kwa Pato la Taifa kumeenda sanjari na kuongezeka kwa thamani ya bidhaa na huduma nje ya nchi kwa takribani asilimia 3.3 ambapo bidhaa na huduma zilizochangia ongezeko hilo ni pamoja na dhahabu, Almasi, madini mengine na Utalii.
 
Aliongeza kuwa utangazwaji wa Takwimu za Pato la Taifa unazingatia matakwa ya Sheria ya Takwimu na 9 ya mwaka 2015 inayotoa mamlaka kwa Tume ya Taifa ya Takwimu kukusanya, kuchambua na kutangaza takwimu za Pato la Taifa.
 
Aidha alitaja baadhi ya shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi kubwa katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2015 kuwa ni pamoja na Ujenzi (17.6%), Uchukuzi na Uhifadhi (10.6%), Uendeshaji Serikali na Ulinzi (10.6%) na Uchimbaji Madini na Kokoto (8.0%)
 
Dkt. Albina amesema kuwa jumla ya thamani ya Pato la Taifa kwa bei za miaka husika katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba 2015 ni takribani shilingi tilioni 71.7 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 6.9.

Magazeti ya Tanzania, January 14 2016 Tanzania

$
0
0
January 14 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti 22 ya Tanzania kuanzia kwenye Udaku, Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea mtu wangu.. usiache kukaa karibu yangu kwenye facebook, twitter na instagram @millardayo ili niwe nakutumia kila kinachonifikia.
DSC00948DSC00949DSC00950DSC00951DSC00952DSC00953DSC00954DSC00955DSC00956DSC00957DSC00958DSC00959DSC00960DSC00961DSC00962DSC00963DSC00964DSC00965DSC00966DSC00967DSC00968DSC00969DSC00970DSC00971DSC00972DSC00973DSC00974DSC00975DSC00976DSC00977DSC00978DSC00979DSC00980DSC00981DSC00982DSC00983DSC00984DSC00985DSC00986DSC00987DSC00988DSC00989DSC00990DSC00991
Unataka kutumiwa MSGza habari zote kubwa kutoka kwa Mi

Davina akanusha kuchepuka

$
0
0


Staa kutoka Bongo Muvi, Halima Yahaya ‘Davina’.

STAA kutoka Bongo Muvi, Halima Yahaya ‘Davina’ amekanusha tetesi zinazozagaa kuwa, kwa vile hayuko kwenye ndoa basi atakuwa anachepuka na kuwajibu wanaozieneza kuwa hayupo hivyo na kwamba anaweza kuishi bila kufikiria mapenzi na watoto wake wanamtosha.

Linah: Mastaa Afrika wananitaka kimapenzi

$
0
0
 
Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Estalina Sanga ‘Linah’.
Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Estalina Sanga ‘Linah’ aachane na mchumba wake, amekiri kutakwa kimapenzi na mastaa wa muziki nje ya nchi (Afrika).
Akichonga na Amani Linah amesema, mara nyingi amekuwa akisumbuliwa kimapenzi na mastaa wengi wa muziki Afrika lakini hakuwa tayari kuwaweka wazi na wala kutaja kama alishawahi kubanjuka na mmoja wapo kati ya hao.
“Ni kweli wapo wengi walionitaka kimapenzi, lakini itabaki kuwa siri yangu kujua ni wangapi na nilimkubalia nani kati ya hao,” alisema Linah.

Liverpool yawatambia Arsenal Ligi Kuu watoka bao 3-3

$
0
0
Appropriately, Anfield appeared to be leaking through every crack and cranny by the end of this game. 
The main stand, now one giant building site, was letting in water, perhaps in solidarity with the two defences. There were hurried evacuations, electrical shutdowns, torrents cascading from the sky. As a physical metaphor for the 90 minutes that preceded the downpour, it was close to perfect.
This being a league that nobody wants to win, here was a match played in similar spirit. Liverpool led, twice, in the first-half and surrendered both times. Arsenal finally got in front after 55 minutes and held on until the final attack of the match, when they too, failed to maintain supremacy. It was a brilliant, thrilling game, but strewn with errors and defensive lapses.
Liverpool midfielder Joe Allen (second left) hauls his side level in the final minute of the game to earn his team a point against Arsenal
Liverpool midfielder Joe Allen (second left) hauls his side level in the final minute of the game to earn his team a point against Arsenal
Allen is mobbed by his team-mates after having the final word in a gripping encounter between Liverpool and Arsenal
Allen is mobbed by his team-mates after having the final word in a gripping encounter between Liverpool and Arsenal
Jurgen Klopp celebrates wildly as Allen's shot hits the back of the net to salvage a point against Arsenal at Anfield
Jurgen Klopp celebrates wildly as Allen's shot hits the back of the net to salvage a point against Arsenal at Anfield
Arsene Wenger looked frustrated by his side's failure to hold on to their lead in the final minutes of the game at Anfield
Arsene Wenger looked frustrated by his side's failure to hold on to their lead in the final minutes of the game at Anfield
Klopp takes to the Anfield pitch to applaud the Liverpool supporters as snow falls at Anfield at the end of the game at Anfield
Klopp takes to the Anfield pitch to applaud the Liverpool supporters as snow falls at Anfield at the end of the game at Anfield
Liverpool striker Roberto Firmino (centre) rifles his side into the lead against Arsenal in the 10th minute at Anfield on Wednesday
Liverpool striker Roberto Firmino (centre) rifles his side into the lead against Arsenal in the 10th minute at Anfield on Wednesday
The Liverpool squad gather together in celebration after Firmino (second left) had given the team the lead against Arsenal
The Liverpool squad gather together in celebration after Firmino (second left) had given the team the lead against Arsenal

MATCH FACTS, PREMIER LEAGUE TABLE AND MATCH ZONE 

LIVERPOOL (4-1-4-1): Mignolet 4; Clyne 6.5, Toure 6, Sakho 4.5, Moreno 5.5; Can 6 (Allen, 82); Ibe 5.5, Lallana 6 (Caulker, 88), Henderson 7, Milner 6.5 (Benteke, 66); Firmino 8. Subs not used: Lucas, Smith, Ward, Teixeira.
Scorers: Firmino, 10, 19, Allen 90.
Booked: Clyne, Firmino. 
Arsenal: Cech 6, Bellerin 7, Mertesacker 6.5, Koscielny 7.5, Monreal 7; Ramsey 7.5, Flamini 7; Campbell 7.5 (Oxlade-Chamberlain, 75), Ozil 6 (Arteta, 87), Walcott 6.5 (Gibbs, 79); Giroud 8.5. 
Subs not used: Gabriel, Chambers, Iwobi, Macey.
Scorers: Ramsey, 14, Giroud, 25, 55. 
MOTM: Giroud 
Referee: Mike Jones 7
Never shirked a decision and let the game flow. Got all the major calls correct and was always in the right place to make them.
Att: 44,109
In the end, Liverpool earned a point with a bit of Jurgen Klopp’s heavy metal. A big old wallop into the box, a big old walloper of a centre-forward on the end of it and a loose ball leathered into the net to conclude. It wasn’t total football, but Klopp and his Kop adored it anyway. By then, snow was falling, which soon turned to rain and the roof fell in. Arsene Wenger will know that feeling, too.
At one point in the evening, Leicester were drawing at Tottenham and Arsenal were leading here. In that moment, Wenger’s team were four points clear at the top. After Joe Allen had scored the game’s sixth goal, and Robert Huth Leicester’s winner, that gap was goal difference alone. Arsenal might have settled for a point before kick-off; at the final whistle it must have felt like a blade between the shoulder blades.
It was their own fault, though, failing to defend some fairly agricultural routes to goal, once Klopp had introduced his battering ram Christian Benteke after 66 minutes.
By the end, even emergency signing Steven Caulker, a centre-half by trade and of late not a particularly reliable one, was up in the box and hoping to cause carnage. The ploy worked. 
Jordan Henderson lumped the ball in from deep, Benteke rose high, a chest higher than any other player in the vicinity, and his header looped across the area as Arsenal scrambled to clear. Substitute Joe Allen, no doubt ignoring a nosebleed, arrived first, Frank Lampard style, and defeated Petr Cech at his near post. In an instant, Klopp was off. 
Down the touchline, as is his jubilant style when Liverpool keep going to the bitter end. It is really all he has to cling to right now, but it kept him warm on a wet and snowy night. 
But Aaron Ramsey swiftly hauled Arsenal level at Anfield, drilling low past Simon Mignolet in the 14th minute of the encounter
But Aaron Ramsey swiftly hauled Arsenal level at Anfield, drilling low past Simon Mignolet in the 14th minute of the encounter
Five minutes later, Liverpool had the lead again, this time through a stunning strike from long range by Firmino
Five minutes later, Liverpool had the lead again, this time through a stunning strike from long range by Firmino
Firmino (centre) is mobbed by Liverpool team-mates Jordon Ibe (left) and Adam Lallana after putting the side 2-1 ahead at Anfield
Firmino (centre) is mobbed by Liverpool team-mates Jordon Ibe (left) and Adam Lallana after putting the side 2-1 ahead at Anfield
But Arsenal were soon level once again, when France international striker Giroud (left) got a light touch onto an inswinging corner
But Arsenal were soon level once again, when France international striker Giroud (left) got a light touch onto an inswinging corner
Giroud watches on as his touch helps the ball get beyond the Liverpool goalkeeper Simon Mignolet in the 25th minute of the game
Giroud watches on as his touch helps the ball get beyond the Liverpool goalkeeper Simon Mignolet in the 25th minute of the game
Giroud (third left) put Arsenal into the lead for the first time with a stunning turn and strike in the 55th minute at Anfield
Giroud (third left) put Arsenal into the lead for the first time with a stunning turn and strike in the 55th minute at Anfield
Giroud celebrates in front of the travelling Arsenal supporters after giving his side the lead against Liverpool
Giroud celebrates in front of the travelling Arsenal supporters after giving his side the lead against Liverpool
Giroud scored twice but Arsenal were unable to hold on for victory against Liverpool in an entertaining match at Anfield
Giroud scored twice but Arsenal were unable to hold on for victory against Liverpool in an entertaining match at Anfield

Giroud missed an excellent opportunity to give Arsenal the lead for the first time in the first half, failing to convert from inside six yards
Firmino (right) then saw his left-footed shot hit the crossbar, with the Brazil international almost completing his hat-trick in the first half
Firmino (right) then saw his left-footed shot hit the crossbar, with the Brazil international almost completing his hat-trick in the first half
Liverpool manager Klopp shouts instructions to his players as they try to find an equaliser against Arsenal
Liverpool manager Klopp shouts instructions to his players as they try to find an equaliser against Arsenal
Steven Caulker came on to make his Liverpool debut, replacing Adam Lallana in the 88th minute against Arsenal
Steven Caulker came on to make his Liverpool debut, replacing Adam Lallana in the 88th minute against Arsenal
Former Liverpool manager Rafa Benitez, recently dismissed by Real Madrid, was at Anfield to watch the game against Arsenal
Former Liverpool manager Rafa Benitez, recently dismissed by Real Madrid, was at Anfield to watch the game against Arsenal
A pity that he never really got the chance to enjoy such a splendid display. Just six minutes after giving Liverpool the lead a second time, Firmino was reined in again. 
Ramsey benefitted from a lovely clipped pass over the top of Liverpool’s back line and lobbed Mignolet, before Sakho headed over with the ball goalbound. 
From the resulting corner, however, a flick by Giroud struck the inside of the goalkeeper’s standing leg and diverted the ball over his line. Giroud claimed it, Mignolet didn’t, but the dubious goals panel is likely to make his contribution plain, even if little else is these days. 

Video: Liverpool vs Arsenal 3-3 All Goals and Highlights (Premier League)

$
0
0
Liverpool vs Arsenal 3-3 All Goals and Highlights (Premier League 2015/2016)
Goals : Roberto Firmino 10', 19', J. Allen 90', A. Ramsey 14', O. Giroud 25', 55' Liverpool vs Arsenal 3-3,

Karrueche Tran, Christina Milian wadaiwa kuwa wapenzi wa jinsia moja

$
0
0
Socialites Karrueche Tran and Christina Milian locked lips while partying at The Nice Guy Club in West Hollywood on Tuesday. KUONA PICHA ZAO ZIPO HAPA ===>bit.ly/1ZlPeQu

Zari aokoka, abatizwa kwenye kanisa moja la kiroho mjini Kampala, Uganda

$
0
0

Mzazi mwenzake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’
MUSA MATEJA, AMANI
DAR ES SALAAM: Siri nzito imefichuka baada ya kusitiriwa tangu mwaka juzi kwamba, mzazi mwenzake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ au mama Tiffah (35), mwaka huo aliokoka na akabatizwa kwenye kanisa moja la kiroho mjini Kampala, Uganda kisha kuwa muumini wa Kikristo, Amani limeinyaka. ILIKUAJE MPAKA AKAOKOKA? Kwa mujibu wa chanzo makini, Zari alifikia uamuzi wa kuokoka katika kipindi hicho mara tu baada ya kugombana na mumewe wa kwanza, Ivan Ssemwanga aliyezaa naye watoto watatu, Pinto, Didy na Quincy.
ALIBATIZWAJE?
“Nawapa ishu, mwaka juzi Zari aliokoka kabisa na kuwa Mkristo. Tena ili kuwapa uhakika, baada ya kukata shauri la kuokoka, alibatizwa kwenye maji mengi ya bwawa la kutengeneza. Maandiko ya Biblia yanasema mtu akiokoka lazima abatizwe kwenye maji mengi, yawe ya bwawa, kisima, mto, ziwa hata baharini, sawa tu,” kilinyetisha chanzo
chetu.

zari-
Zari akibatizwa.
ALIANDIKWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI?
Baada ya kuchukua hatua hiyo, mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari vya kielektroniki na magazeti nchini humo viliripoti kwa vichwa vya habari; I AM NOW BORN AGAIN- SAYS ZARI (Zari: Sasa nimeokoka), ZARI IS NOW BORN AGAIN(Zari sasa ameokoka).

MWENYEWE ALISEMA NENO?
Kwa upande wake, kwa mujibu wa chanzo chetu, Zari baada ya kuchukua uamuzi huo, alitupia maneno na picha kwenye mitandao yake ya Twitter na Facebook akisema: “Ni rasmi sasa nimeokolewa.” Zari alionesha ni jinsi gani anampenda Yesu Kristo kwa vile alimuweka kwenye mwanga mpya. Alisema: “Mwenyezi Mungu kama siku moja nitapoteza matumaini, nipe ujasiri ambao hatima yangu ipo mikononi mwako. Sasa nayaona maisha katika mwanga mpya.”

ALIANZA KUYAJUA MAANDIKO?
Mama Tiffah ambaye pia huimba nyimbo za Kizazi Kipya na pia mama wa watoto wanne, Pinto, Didy, Quincy na Tiffah aliyezaa na Diamond alionesha uwezo wake wa kiimani kwa kutupia maandiko kutoka ndani ya Biblia kwenye Twitter yake huku akiendelea kumsifu Mungu na Yesu Kristo kwa kumuokoa.

CHA KUSHANGAZA SASA
Chanzo kilisema kuwa, baadaye Zari aliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo kuwa, anatoka kimapenzi na Diamond, wengi walihoji alikouacha ulokole wake na ‘kurejea’ duniani.

“Mbaya zaidi, nasikia hata wachungaji wake waliposikia walishangaa sana. Walijaribu kumtafuta ili wamwelekeze namna ya kuukulia wokovu lakini bila mafanikio. Zari akawa amegandana na Diamond mpaka mimba na hatimaye kujifungua,” kilisema chanzo.
ANGETANGAZA KUACHA ULOKOLE NA KUWA NA DIAMOND?
Chanzo kikaendelea: “Nadhani walichotaka wachungaji wake ni kumrejesha Zari kundini, lakini si kutangaza kwamba ameamua kurejea maisha ya zamani. Ni vigumu sana. Hakuna anayeokoka kisha akatangaza akiacha.” Hata hivyo, chanzo hicho hakikujua jina la kanisa alilopatia wokovu Zari licha ya kusema waliombatiza ni watumishi wa Mungi Wazungu wa mjini Kampala.

HISTORIA FUPI YA UZAZI WA ZARI
Mpaka anabatizwa, Zari alikuwa akijulikana kwa jina la Zarinah Zaituni Hassan Tiale na aliendelea kutumia jina la Zari. Ana mchanganyiko wa kimataifa. Babu yake mzaa mama yake (Halima) ni Mhindi, bibi Mganda. Babu yake mzaa baba ni Msomali, bibi Mrundi.

DIAMOND AAMBIWA, ATOA TAMKO
Kufuatia Zari mwenyewe kuwa Uganda na kutopatikana hewani, gazeti hili lilizungumza na Diamond kuhusu ishu hiyo ambapo aliamua kulitolea tamko: “Najua lakini sina pingamizi na hilo. Mimi siangalii imani ya mtu, kinachotakiwa ni mapenzi ya dhati tu.”

CHANZO: GPL

Maalim Seif Sharif Hamad Amwandikia Barua Papa Francis Kumwomba Aingilie Kati Mzozo wa Zazibar

$
0
0

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, amemwangukia Papa Francis kwa kumwandikia barua, akimuomba kutumia ushawishi wake na Tanzania kumaliza mzozo wa kisiasa kisiwani humo kabla hali haijawa mbaya.

Kwa mujibu wa barua yake ya Novemba 25, mwaka jana, Maalim Seif alimwomba Papa kutumia ushawishi alionao kwa serikali ya Tanzania ili kuhakikisha haki inatendeka na kuepusha vurugu zinazoweza kutokea.

“Ni wiki tatu sasa tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu na hali hii imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli za kuichumi kutokana na wananchi wengi kuwa na hofu kuhusu mustakabali wa hali hii….watu wanashindwa kujua nini kitatokea maana wana hofu kwamba hali hii inaweza kuharibu umoja wa kitaifa kwa watu kuishi kwa upendo bila kujali dini wala kabila,” ilisema barua hiyo.

Barua hiyo ya Maalim Seif ilisema, Zanzibar ina mchanganyiko wa Waislamu na Wakristo, hivyo hakuna mgawanyiko kwa misingi ya udini lakini hatua ya wananchi kukosa haki yao ya kidemokrasia kupitia sanduku la kura baada ya miaka 20 ya chaguzi visiwani humo kunaweza kusababisha vijana ambao hawafurahishwi na mwenendo huo kutumia njia mbaya kutafuta haki yao.

“Badala ya kuchukua hatua za pamoja kuzuia uovu huu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo chama chake kilishinda kwenye uchaguzi mkuu uliopita, imekuwa ikisaidia serikali ya Zanzibar kwa kutumia askari na majeshi yake  kutishia watu wa upinzani,” ilisema.

“Wakati mmishenari wa kikristu alipomuomba Sultan  wa Zanzibar  mwaka  1840  kibali cha  kujenga asasi ya kusaidia jamii kwenye eneo lake, Sultani yule ambaye alikuwa Muislamu alimtambua kama mtumishi wa Mungu aliyekuwa na lengo la kuendeleza neno la Mungu” ilisema sehemu ya barua hiyo kwenda kwa Papa.

Iliongeza kuwa, Zanzibar  ilipopata Uhuru wake mwaka 1963, kwa kiwango kikubwa watu wake waliishi kwa amani na ushirikiano baina ya watu wa madhehebu yote ya Katoliki, Anglikana, Sunni, Shia  na Hindu na hakukuwahi kuwa na mgogoro wala hofu ya watu hao kuhitilafiana kwa misingi ya tofauti ya dini.

Ilisema Chama cha Wananchi CUF kimekuwa kikishinda chaguzi zote tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, lakini haijawahi kupewa ushindi wake hata muhula mmoja.

Milipuko ya Mabomu Yaua Watu Zaidi ya Saba Indonesia

$
0
0
Jakarta-bombs
Jengo la mgahawa wa Starbucks Coffee lililopo Mji Mkuu wa Indonesia, Jakarta ambapo mabomu hayo yamelipuliwa mapema leo.
Milipuko ya mabomu takribani sita imetokea katika Mji Mkuu wa Indonesia, Jakarta na baadaye ufyatulianaji mkali wa risasi na watu zaidi ya saba wameripotiwa kuuawa japo polisi wanasema huenda kuna idadi kubwa zaidi ya waliouawa.
Kati ya hao waliouawa ni maofisa watatu wa polisi, raia wawili akiwemo Mreno mmoja pamoja na washambuliaji watano.
Jakarta-bombs (1)
Polisi wa Indonesia wakijihami
Milipuko imetokea maeneo kadha, ikiwa ni pamoja na mgahawani katika duka la kibiashara lililoko karibu na Ikulu ya rais wa nchio hiyo na ofisi za Umoja wa Mataifa (UN).
Indonesian-capital-explosions
Kuna ripoti za maafisa wa polisi kuonekana kwenye majengo na barabara za mji huo karibu na kituo hicho cha kibiashara.
Eneo hilo limezingirwa na maafisa wa usalama.
Rais Joko Widodo amehimiza raia wawe na utulivu na kushutumu “kitendo hicho cha ugaidi”.
Indonesian-capital-explosions (3)“Tunaomboleza watu waliofariki kwa sababu ya kisa hiki, lakini pia tunakilaani. Kimevuruga utulivu na amani na kuingiza wasiwasi miongoni mwa raia,” amesema.
Msemaji wa polisi, Anton Charliyan ameambia wanahabari kuwa maafisa wa polisi na raia ni miongoni mwa waliofariki.
Indonesian-capital-explosions (1)
Bado haijabainika ni nani huenda amehusika katika shambulio hilo.
Indonesia, taifa lenye Waislamu wengi zaidi duniani, imeshambuliwa na makundi ya wapiganaji wa Kiislamu awali.
Indonesian-capital-explosions (2)
Majuzi, imekuwa kwenye hali ya juu ya tahadhari kutokana na tishio kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State.
Hili ndilo shambulio la kwanza kubwa kutokea Jakarta tangu mashambulio kwenye hoteli za Marriot na Ritz mwaka 2009.
Jakarta suicide (1)Jakarta suicide (2)Jakarta suicide (3)Hali ilivyokuwa baada ya tukio hiloJakarta suicide (4)Jakarta suicide (5)Eneo ambapo moja ya bomu limelipuliwa.Jakarta suicide (6)Hali ya taharuki wakati mabomu yakiripukaJakarta suicide (7)Polisi wakifanya juhudi za kupambana na taharuki hiyoJakarta suicide (8)Jakarta suicide (9)Jakarta suicide (10)…Miili ya waliouawaJakarta suicide (11)Jakarta suicide (12)Polisi akiimarisha ulinziJakarta suicide (13)Miili ya waliouawa ikifunikwaJakarta suicide (14)Jeshi la Usalama la Indonesia wakipambana na walipuaji wa mabomu hayoJakarta suicide (15)Kikosi chaJeshi la Usalama la Indonesia wakiwa katika hekaheka ya kupambana na adha hiyo.
Jakarta suicide (17)Jakarta suicide (18)Majeruhi wakipewa msaada.Jakarta suicide (19)Jakarta suicide (20)Mmoja wa ofisa wa polisi aliyejeruhiwa kwa bomu akiokolewa.
Jakarta suicide (21)Jakarta suicide (22)Jakarta suicide (23)Anayedhaniwa kuwa mtuhumiwa akiwanyooshea bastola raiaJakarta suicide (24)Jakarta suicide (25)Jakarta suicide (26)Jakarta suicide (27)Polisi wakizidi kuimarisha ulinzi.Jakarta suicide (28)Eneo la tukio.Jakarta suicide (29)Polisi akijihami.Jakarta suicide (30)Anayedhaniwa kuwa mmoja wa watuhumiwa akikatiza na bunduki mkononi.
Jakarta suicide (31)Ofisa wa Polisi akiamurisha kikosi chake kupambana na walipuaji.Jakarta suicide (32)Mbwa wa polisi akipelekwa eneo la tukio ili kufanya utafiti wa kubaini walipuaji wa mabomu hayo.Jakarta suicide (33)
Polisi wakichukua tahadhari.
PICHA NA DAILY MAIL

Karrueche Tran anaswa akidendeka na Christina Milian

$
0
0


2
Karrueche Tran (kushoto) akibusiana na Christina Milian baada ya kukutana katika Klabu ya The Nice Guy iliyopo magharibi mwa Hollywood nchini Marekani jana.
1
Karrueche Tran na Christina Milian wakionyeshana mahaba.
3
4
Christina Milian wakati akiwasili kwenye Klabu ya The Nice Guy jana.
56
Karrueche Tran akiwa katika vazi la sweta kwenye eneo la Klabu ya The Nice Guy jana.
Mwigizaji na mwanamitindo wa nchini Marekani, Karrueche Tran jana jioni alinaswa akidendeka na mpenzi wake wa kike Christina Milian katika Klabu ya The Nice Guy iliyopo magharibi mwa Hollywood nchini Marekani.
Warembo hao waliweka wazi mahusiano yao mwaka jana baada ya Karrueche kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, mwanamuziki Chris Brown huku Christina akiwa tayari amembwaga mpenzi wake wa zamani mwanamuziki Lil Wayne.
Mbali na mahusiano hayo, lakini inaonyesha Karrueche mwenye umri wa miaka 27 bado anapambana na changamoto za maisha ya mapenzi ya jinsia moja kitendo kilichopelekea jana aandike katika ukurasa wake wa Twitter kuwa kwa sasa amefungua milango ya mahusiano mapya na kwamba yupo tayari kumpokea mpenzi baada ya kukaa mpweke kwa muda mrefu japo alidai itakuwa vigumu kumpata mpenzi wa kweli ambaye ataweza kumpa penzi ya dhati.

Airtel yazindua Duka la kisasa jijini Dar es Saalam‏

$
0
0


pic 1Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald,(wakwanza kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani jinsi ya kupata taarifa kuhusu huduma mbalimbali za Airtel kupitia komputa zilizoweka katika duka jipya la Airtel Expo wakati wa uzinduzi rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso (nyuma katikati) na Meneja huduma kwa wateja Bi. Zakia Omarypic 2
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani akiongea wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kisasa la Airtel Expo lililopo katika makao makuu ya Airtel Morocco, jijini Dar es Saalam. Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasilino wa Airtel Bi. Beatrice Singano Mallya.pic 2 b
Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald (kulia) akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng. Edwin Ngonyani juu ya huduma zinazopatikana katika duka jipya wakati wa uzinduzi wa duka hilo. Wakishuhudia (kutoka kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Prof. Faustine Kamuzora, Naibu Katibu Mkuu Dr Mary Sasabo na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw. Sunil Colaso.
pic 3
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kisasa la Airtel Expo lililopo katika makao makuu ya Airtel Morocco,jijini Dar es Saalam.
pic 4
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng. Edwin Ngonyani pamoja na mkurugenzi mkuu wa Airtel kwa pamoja wakibonyesha kitufe kuashiria uzinduzi wa duka la Airtel Expo lililopo makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
pic 5
Shamrashamra za uzinduzi wa duka la Airtel Expo Morocco, jijini Dar es Saalam
pic 6
Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald,(kwanza kushoto) akimuonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani vifaa na simu mbalimbali vinavyopatikana katika duka jipya la Airtel Expo wakati wa uzinduzi rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel Morocco, jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw. Sunil Colaso (wa kwanza kulia) akifatiwa na Meneja huduma kwa wateja bi, Zakia Omary.
Adrina pic
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani akimsikiliza Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel, Bi Adriana Lyamba na meneja huduma kwa wateja Zakia Omary (katikati) wakati wa uzinduzi rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel Morocco, jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso.

Lowassa Akutana na Wafanyabiashara wa Team Mabadiliko Kutoka Soko la Kariakoo

$
0
0

Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akizungumza na Ujumbe wa Wafanyabiashara wa Team Mabadiliko kutoka soko kuu la Kariakoo, Jijini Dar es salaam waliomtembelea Ofisini kwake jana Januari 14, 2016.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Team Mabadiriko kutoka soko kuu la Kariakoo, Severin Mushi, akizungumza wakati akiutambulisha ujumbe wake kwa Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, walipokwenye kumuona jana Januari 14, 2016.

Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyabiashara wa Team Mabadiriko kutoka soko kuu la Kariakoo, mara baada ya kuzungumza nao jana, Jijini Dar es salaam

Agizo la Serikali la Kukamatwa Waliomuozesha Binti wa Miaka 13

$
0
0

(PRESS RELEASE).
WIZARA YAAGIZA KUKAMATAWA KWA WALIOMWOZESHA MTOTO WA MIAKA 13 WILAYA YA KISHAPU, MKOA WA SHINYANGA
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea kwa masikitiko makubwa na inataka hatua kali zichukuliwe dhidi ya wazazi wawili tofauti wanaotuhumiwa kuwaozesha watoto wao wa umri wa miaka 13 na kuwakatisha masomo katika mkoa wa Shinyanga na Dodoma.
Imeelezwa kuwa, wakati mtoto mmoja mwanafunzi wa shule ya msingi Wishiteleja wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga ameozeshwa kwa nguvu kwa mahari ya ngombe 13 na kumkatisha masomo yake akiwa darasa la sita, mtoto mwingine wa mtaa wa Chikole, Kata ya Msalato Manispaa ya Dodoma anasemekana kuozeshwa kwa mahali ya shilingi 600,000. Kufuatia kuwepo kwa matukio haya mawili Wizara inataka vyombo vya dola kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi wa Mtoto katika mikoa yote kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanachukuliwa hatua kali.
Tukio la kuwaoza watoto katika umri mdogo siyo tu linakinzana na haki za msingi za mtoto bali pia linamkosesha mtoto haki ya kuendelezwa ikiwa ni pamoja na kuhatarisha uhai wake kwa kupatiwa majukumu ya mtu mzima katika umri mdogo.
Wizara inawataka wazazi na walezi kubadilika na kuachana na tabia ya kuwaoza watoto wao katika umri mdogo maana vitendo hivyo ni vya kikatili. Jamii inatakiwa kutambua kuwa, vitendo vya kikatili kama hivyo vinapofanywa katika familia vinarudisha nyuma juhudi za Serikali za kupambana na ukatili maana kwa kiasi kikubwa familia inatakiwa kuwa mahala salama panapofaa watoto kuishi na kulindwa.
Aidha, Wizara inakumbusha wazazi, walezi na wadau wengine kuwa, ndoa za utotoni ni kinyume na Sheria ya Mtoto (2009) na Mikataba ya Kimataifa kuhusu Haki na Ustawi wa Mtoto. NIwajibu wa kila mtu kuhakikisha kuwa watoto wanaishi katika usalama na kuhakikishiwa haki zao zote za msingi ikiwemo kulindwa, kuendelezwa, kuishi na kushirikishwa katika maisha ya kila siku ili kujenga Taifa linaloheshimu maslahi ya watoto.
Erasto T. Ching’oro
Kny: KATIBU MKUU
MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZAZI NA WATOTO.

Kesi ya Kafulila: Mahakama Yatupilia Mbali Pingamizi la Wakili wa Serikali

$
0
0

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tabora Chini ya Jaji Sam Rumanyika jana Januari 14, 2016 imetupilia mbali mapingamizi ya Wakili wa serikali yaliyowasilishwa na kujadiliwa Januari 11, 2015 katika mahakama hiyo.

Katika mapingamizi ya serikali Wakili wa serikali kwa niaba ya msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria wa serikali aliweka mapingamizi na kutaka mahakama itupilie mbali kesi ya Kafulila David kwa madai kwamba;

  1.  Hati ya mashtaka haina vifungu vya sheria vinavyoipa mahakama mamlaka ya kusikiliza kesi hii
  2.  Ombi la Kafulila kutangazwa mshindi halimo ndani ya uwezo Wa mahakama kwakuwa mamlaka hayo ni ya Tume ya uchaguzi
  3.  Kwamba ombi la Kafulila kwamba mahakama ipitie fomu za matokeo haitambuliki kisheria

Katika uamuzi wa MAHAKAMA, Jaji Rumanyika amesema baada ya kusikiliza na kuchambua mapingamizi na utetezi wa Wakili wa Kafulila imeamua kuwa;

  1.  Hoja kwamba hati ya mashtaka haina au haijaweka sheria I nayoipa mamlaka mahakama kusikiliza na kuamua KESI hii haina msingi kwakuwa kwanza kesi ya uchaguzi sio sawa na maombi ya kawaida na zaidi sheria ya uchaguzi ya 2015, kifungu110 kimesisitiza wazi kuwa mahakama kuu ndio yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za uchaguzi na hivyo haikuwa na ulazima kutaja ukweli ulio hayana.
  2.  Hoja kwamba mahakama haina uwezo wa kutangaza mshindi haina msingi kwasababu sheria ya uchaguzi ya 2015 kifungu112 kimeweka wazi mamlaka ya mahakama kuwa ni pamoja na kutangaza mshindi alochaguliwa na hivyo Kafulila Ana haki kuomba ombi hilo.
  3.  Kuhusu pingamizi kuwa ombi la Kafulila la kuomba kupitiwa fomu 21B za kila kituo, MAHAKAMA imelekeza kuwa dhana ya ombi hilo inamezwa na ombi la kutangazwa mshindi hivyo halina sababu kuwepo

Baada ya maelekezo na maelezo hayo, Mahakama haioni sababu ya kufuta kesi ya Kafulila David Kama ilivyombwa na wakili wa serikali na badala yake Kesi itaendelea Januari 28, 2015.

Wastara atengwa Bongo Muvi

$
0
0
Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma.

DAR ES SALAAM: Baada ya staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma kufunga ndoa na mheshimiwa Sadifa Juma, anadaiwa kutengwa na wasanii wenzake wa Bongo Muvi hasa wale waliokuwa karibu naye katika zoezi la kumchangishia fedha za matibabu aliyokuwa akitarajia kwenda kuyafanyiwa nchini India.

Sosi wa ndani ya Bongo Muvi alilinyetishia Ijumaa kwamba, baadhi ya mastaa walifikia uamuzi kufuatia kukasirishwa na kitendo cha Wastara kuolewa ghafla bila kuwashirikisha wao.
“Wasanii wamemkasirikia sana Wastara na ninavyokwambia kwa sasa kimenuka kwani hawataki hata kumsikia.
12509891_1406480552699692_7771509362345070065_n 
“Wanamshangaa kuolewa wakati anaumwa na alikuwa akiomba msaada hivyo wamemtenga na wamesitisha michango yake,” kilifunguka chanzo hicho.
Ilielezwa kwamba, aliyekuwa akiongoza ishu ya kumchangishia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba aliyejitolea kuandika barua na kuipeleka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa ajili ya kuomba msaada wa matibabu ya mguu wake nchini India lakini walisitisha mara moja zoezi hilo baada ya ndoa hiyo.
Mwakifwamba alipoendewa hewani na kufikishiwa ishu hiyo alisema: “Nilifuatwa na kaka wa Wastara, akaniomba kuwa dada yake anaumwa sana, anahitaji kwenda kwenye matibabu India, nikaamua kumuandikia barua ya kumuombea msaada wizarani.
“Barua hiyo niliipeleka kwa katibu mkuu wa wizara hiyo, Profesa Elisante Ole Gabrielleo. Alipoipokea aliniambia kuwa ataishughulikia iende Wizara ya Afya kwa ajili ya matibabu hayo haraka na mchakato ulikuwa unaenda vizuri.
“Ilipofika jioni nikashangaa kuona mitandaoni kuwa Wastara anaolewa, nikaona nimpigie haraka katibu mkuu kwani barua yangu ilisema kuwa Wastara ni mgonjwa sana ambaye anahitaji matibabu ya haraka kwa hiyo kitendo cha kufunga ndoa kilinishtua kwani sikulitambua.
“Baada ya kumweleza katibu mkuu huyo alisema kuwa kwa sababu ameolewa na mbunge kuna taratibu zao azifuate hivyo tukaishia hapo.”
Kwa upande wake Wastara alifunguka mambo mazito ya kusikitisha: “Nikiongea sasa nitaonekana najitetea lakini wasanii wenzangu wajue kuwa niliamriwa na mume wangu, niliwatumia ujumbe kwenye makundi yetu na kuwaeleza kuwa naolewa.
“Hata hivyo, ndoa haikuwa imepangwa kwa siku hiyo kama wanavyodhani ila baada ya mimi kuwa na hali mbaya, Sadifa aliwaomba ndugu zangu na kuwaambia kuwa anataka anioe hivyohivyo ili anihudumie kwa sababu tulipanga ndoa baada ya mimi kutoka kwenye matibabu.
“Wasanii ni watu wa kulaumu tu, ila mimi naumwa sana, Mungu akipenda nitakuwa India ‘soon’, nitafanyiwa matibabu na anayetaka kunichangia nitamshukuru.”
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>