Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

Pam D achomoa dili la kuuza unga

$
0
0

MSANII wa muziki Bongo, Pamella Daffa ‘Pam D’ amefunguka kuwa hivi karibuni kuna jamaa alimfuata na na kutaka amuingize kwenye dili la kuuza unga lakini akamchomolea. Akipiga Pam D alisema: “Yule “Yule jamaa alinifuata akaniambia eti kwa kuwa nakutana na mastaa wengi, anipe
mchongo huo. Kwanza nilimshangaa sana, nikajiuliza kwa nini anifuate mimi. “Kwa kuwa ni
biashara ambayo sitaki hata kuisikia, nilimjia juu sana, nilifanya hivyo kwa kuwa nilijua anataka kuniingiza
kwenye matatizo, mimi na unga wapi na wapi bwana.”

Magazeti Ya Tanzania Leo Ijumaa Ya Januari 8, 2015

Kadja: Rubby ‘cha mtoto’ sana kwangu

$
0
0
Mwanamuziki Kadijanito au ukipenda muite Kadja amefunguka kuwa, anawashangaa sana wanaomfananisha uwezo wake wa kuimba na alio nao mwenzake kutoka THT, Rubby.

 Mwanamuziki Kadijanito

Kadja aliiambia safu hii kuwa, anajua uwezo wake wa kimuziki uko juu, hivyo wanaomlinganisha na Rubby wamekosa kazi ya kufanya.

“Unajua mimi najijua niko levo gani, sijisifii ila mimi siyo levo za akina Rubby, yule ni cha mtoto kabisa kwangu hivyo najisikia vibaya sana pale mtu anapofikia hatua ya kunifananisha naye.

Kadja sasa anafanya poa na wimbo wake wa Sina Maringo ambao ameshaufanyia kichupa.

Mkongo awamaliza Mastaa Bongo, Hofu ya Kuambukizana Ukimwi yatanda

$
0
0
 
PEDESHEE Mkongo anayefahamika kwa jina la Rajab Mwami, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwenye maskani jijini Dar, amegandwa na madai ya kutaka kuwamaliza mastaa wa kike Bongo kutokana na kuwa na uhusiano nao kwa nyakati tofauti. Madai hayo yanakuja kufuatia jamaa huyo awali kuripotiwa kuwa na uhusiano na staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe kabla ya baadaye kuhamia kwa Video Queen, Husna Maulid. 

AMTAKA LULU
 Habari ya mjini ni kwamba, baada ya kutokea hali ya kutokuelewana kati ya Wolper na Husna, jamaa huyo aliamua kuachana nao na baadaye akatangaza kuwa, yuko tayari kupoteza kiasi chochote cha fedha ilimradi amnase staa mwingine wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’. Hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja kama alifanikiwa kutimiza azma yake hiyo kwani kilipita kimya kidogo bila kujulikana anatoka na staa gani.
 
 Husna.

ADAIWA KUMNASA WEMA
 Baada ya kupita kimya
kirefu, yaliibuka madai kuwa, Mkongo huyo amejiweka kwa mwigizaji Wema Sepetu na kwamba kufuru alizokuwa akifanya mwandada huyo mjini, zilitokana na jeuri ya fedha za Mwami.


 ATUA KWA TUNDA Kana kwamba jamaa huyo hatulii kwa demu mmoja, kuna kipindi yaliibuka tena madai kuwa amejiweka kwa Video Queen wa Bongo, Tunda Sabasita hali iliyosababisha watu kuhoji sababu ya mabinti hao kumpapatikia.

 SHAMSA ADAI KUTOKEWA Naye staa mwingine wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford aliwahi kunukuliwa na gazeti hili akidai kuwa, Mkongo aliyewahi kuwa na Wema na Wolper, amemtokea. Hata hivyo, hakukuwa na ushahidi kama aliyemtokea ni Mwami au Mkongo mwingine ambaye huenda aliwahi kuwatokea Wema na Wolper.
 
 Wolper

 MASOGANGE NAYE KABANG 
Wakati watu wakihisi jamaa huyo katulia zake Kongo, juzikati Mkongo huyo akanaswa akiwa na Video Queen mwingine wa Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ wakiwa hotelini na akadai wapo kibiashara zaidi. Hata baada ya pedeshee huyo kujitetea, wengi walidai kuwa, licha ya uwezekano
wa kuwepo kwa biashara kati ya wawili hao, kwa jinsi anavyopenda watoto wazuri, hawezi kumuacha. 

 
HOFU YA KUAMBUKIZANA UKIMWI YATANDA Kufuatia mastaa hao kupishana kwa pedeshee huyo, wengi waliozungumza na Ijumaa walionesha hofu yao ya kuambukizana ugonjwa hatari wa Ukimwi. “Yaani huyu jamaa sijui pesa zake ndiyo zinampa kiburi, maana kila staa anayemtaka anamtokea, lakini hofu yangu ni kwamba kama anatembea nao wote bila kinga si watakuwa wanaambukizana?” alihoji Husna Juma wa Kinondoni huku akiomba ikiwezekana jamaa huyo arudishwe kwao kwani atawamaliza mastaa hao.
 
 MWAMI ANASEMAJE? Baada ya kuwepo kwa msururu ‘mtungo’ huo wa mastaa wakiwepo aliowapitia na aliopanga kuwapitia, mwandishi wetu alimtafuta Mwami kupitia simu yake ya mkononi ambapo katika kujitetea alisema kuwa, yeye ni mtu na familia yake na hao mastaa wengi wao wanajigonga kwake. “Hao bwana wanajigonga kutokana na tamaa zao, mimi siwezi kuwa nao kwa kuwa nina mke wangu na nampenda sana,” alisema Mwami.
CHANZO: GPL

Tazama picha ya Samatta akiwa na tuzo yake Kitandani

Serikali Yatoa Picha Rasmi ya Rais wa Awamu ya Tano, Dkt John Pombe Magufuli

$
0
0
Picha Rasmi ya Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli itaanza kuuzwa Januari 08, 2015, katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) Mtaa wa Samora.
Kila nakala ya picha hiyo itauzwa shilingi Elfu Kumi na Tano tu bila fremu.  Picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere itauzwa shilingi Elfu Tano tu.  Aidha, Picha hizo zitauzwa katika Ofisi za Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).
 

Picha hizo zinatakiwa kutundikwa katika ofisi zote za Serikali, Taasisi za Umma, Mashirika na Ofisi binafsi.  Kila ofisi inatakiwa iwe na picha ya Mhe. Rais pamoja na Baba wa Taifa.
Serikali inatoa onyo kwa wale wote wanaosambaza  picha isiyo rasmi pamoja na Serikali kutoa taarifa kusitisha matumizi ya picha hiyo na wanaotengeneza picha ukubwa ambao siyo rasmi.

Hatua za kisheria  zitachukuliwa dhidi yao.  Idara ya Habari(MAELEZO) ndio yenye Haki miliki ya picha hiyo.

Rais Magufuli Ampongeza Mbwana Ally Samatta Kwa Kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salam za pongezi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na  Michezo Mhe. Nape Nnauye kufuatia mchezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu  Mbwana Ally Samatta kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Barani Afrika; iliyotolewa katika mji wa Abuja nchini Nigeria jana usiku..
Mhe. Rais Magufuli amemtaka Waziri Nape Nnauye amfikishie salam zake za pongezi kwa mchezaji huyo ambaye pia ni mchezaji wa kulipwa wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Amesema tuzo hiyo imemjengea heshima na kuleta sifa kwa Mbwana Samatta mwenyewe, wanasoka hapa nchini na Tanzania kwa ujumla katika medali ya Soka Kimataifa.
Aidha, Rais Magufuli amewasihi wachezaji wa soka wote na wadau wa mchezo huo kuongeza juhudi za kuundeleza mchezo huo ili upige hatua zaidi za kimaendeleo.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
08 Januari, 2016

Askofu Pengo Kutoka Hospitali Leo

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi amesema afya ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo imeimarika na leo ataruhusiwa.

Kardinali Pengo alifikishwa katika hospitali hiyo Desemba 31, mwaka jana kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Profesa Janabi alisema Pengo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo. Hata hivyo, hakueleza kwa undani.

Jana, kwa mara ya kwanza tangu afikishwe katika hospitali hiyo, Pengo alijitokeza hadharani na kuzungumza na wafanyakazi wa taasisi hiyo na waandishi wa habari, huku akishukuru kwa huduma alizopata.

Alisema amepatiwa huduma nzuri na kumfanya afute kichwani mwake habari za watu mbalimbali wanaodai kuwa MNH haiwahudumii vizuri wagonjwa.

“Nataka niwashukuru wahudumu wote walionifikisha katika hali hii, hasa Profesa Janabi na Mkuu wa Kitengo cha Dharura na Ajali, Dk Juma Mfinanga,” alisema.

Akiwa hospitalini hapo jana, Kardinali Pengo alitembelewa na maaskofu wasaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Titus Mdoe na Eusebius Nzigilwa pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea, Damian Dallu.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu alisema Serikali imejipanga kuhakikisha wagonjwa wa moyo hawapelekwi nje ya nchi kutibiwa.

Alisema tangu kuanza kwa mpango wa kuwatibu wagonjwa hao nchini Taifa limeokoa takribani Sh5 bilioni.

“Tutatoa vibali kwa wagonjwa kutibiwa nje ya nchi ikiwa itathibitishwa na madaktari kuwa huduma husika haiwezi kutolewa nchini,” alisema.

 Jana, Profesa Janabi alisema waliwahudumia wagonjwa 500 na mwaka huu wanatarajia kupokea kundi la madaktari bingwa kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kutoa mafunzo.     

Waziri Kitwanga: Hatua Kali Kuchukuliwa Kwa Yeyote Atakaye Kaidi Kulipisha Gari La Zimamoto Wakati Linaenda Katika Tukio

$
0
0

Katika kuhakikisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linafanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika kupambana na majanga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ameliagiza jeshi hilo kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote atakayekaidi kulipisha gari la Zimamoto na Uokoaji pindi linapokuwa linawahi  eneo la tukio ili kuweza kuzima moto na kuokoa maisha ya watu  pamoja na mali zao.

Waziri Kitwanga ametoa agizo hilo alipokuwa anamaliza ziara yake katika Makao Makuu ya Jeshi hilo Kanda ya Ilala, Dar es Salaam mara baada ya Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kamisha Jenerali, Pius Nyambacha kubainisha kuwa mojawapo ya changamoto zinazolikumba jeshi hilo ni ukaidi wa baadhi ya wananchi kutotaka kupisha gari la Zimamoto pindi linapokuwa katika harakati za kuwahi eneo la tukio.

 “Hivi hamjui hata msafara wa Rais unalazimika kupisha gari la Zimamoto au wagonjwa? Iweje leo wananchi wasipishe magari hayo? Simamieni sheria hii” Alisisitiza Mhe. Waziri. 

Aidha Mhe. Waziri aliahidi kushughulikia changamoto zote zinazolikabili Jeshi hilo changamoto hizo ni ukosefu wa vifaa, ufinyu wa bajeti pamoja na idadi ndogo ya Askari. 

Waziri Kitwanga: Hatua Kali Kuchukuliwa Kwa Yeyote Atakaye Kaidi Kulipisha Gari La Zimamoto Wakati Linaenda Katika Tukio

$
0
0

Katika kuhakikisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linafanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika kupambana na majanga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ameliagiza jeshi hilo kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote atakayekaidi kulipisha gari la Zimamoto na Uokoaji pindi linapokuwa linawahi  eneo la tukio ili kuweza kuzima moto na kuokoa maisha ya watu  pamoja na mali zao.

Waziri Kitwanga ametoa agizo hilo alipokuwa anamaliza ziara yake katika Makao Makuu ya Jeshi hilo Kanda ya Ilala, Dar es Salaam mara baada ya Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kamisha Jenerali, Pius Nyambacha kubainisha kuwa mojawapo ya changamoto zinazolikumba jeshi hilo ni ukaidi wa baadhi ya wananchi kutotaka kupisha gari la Zimamoto pindi linapokuwa katika harakati za kuwahi eneo la tukio.

 “Hivi hamjui hata msafara wa Rais unalazimika kupisha gari la Zimamoto au wagonjwa? Iweje leo wananchi wasipishe magari hayo? Simamieni sheria hii” Alisisitiza Mhe. Waziri. 

Aidha Mhe. Waziri aliahidi kushughulikia changamoto zote zinazolikabili Jeshi hilo changamoto hizo ni ukosefu wa vifaa, ufinyu wa bajeti pamoja na idadi ndogo ya Askari. 

Sikuuu Za Kitaifa - 2016

BomoaBomoa Yaipasua Kichwa Serikali....Mwanasheria Wa Nemc Aliyehalalisha Jumba La Mchungaji Rwakatare Afukuzwa Kazi

$
0
0

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU ZOEZI LA KUHAMISHA WAKAZI WA MABONDENI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

Utangulizi
Nchi yetu ina kingo za mito na mabonde na maeneo mengi hatarishi ambamo watu wanaishi kinyume cha sheria, huku wakiharibu mazingira na kuhatarisha maisha yao.  Kutokana na uhaba wa makazi, hali ni mbaya zaidi katika mabonde ya Jiji la Dar es Salaam, hasa bonde la Mto Msimbazi.
 
Serikali za awamu zote, zimekuwa zikifanya jitihada za kuwaondoa wakazi wa maeneo ya mabondeni wanaoishi katika maeneo hayo kinyume cha sheria lakini mafanikio yamekuwa si ya kuridhisha.

Serikali ya Awamu ya Tano, ambayo moja ya misingi yake mikuu ni utii wa sheria za nchi, imeanza jitihada za kuwaondoa wakazi hawa. 
Tuliamua kuanza na Bonde la Mto Msimbazi kwasababu ndiko kwenye watu wengi na athari kubwa.Sababu zetu kuu za kufanya zoezi hili ni kusafisha mabonde na mito katika jiji la Dar es Salaam na mazingira yanayozunguka ni:-

Kunusuru maisha ya wananchi wanaoishi katika mazingira hatarishi. Eneo la Bonde la Mto Msimbazi lilitangazwa kuwa ni eneo hatarishi kuishi binadamu tangu mwaka 1949 na baadaye 1979.

Kupanua uwezo wa mito ya Dar es Salaam ili kupitisha maji ya mvua kwa kasi kubwa, hivyo kupunguza uwezekano wa kutokea mafuriko na maafa wakati wa mvua nyingi;Kuzuia milipuko ya magonjwa, hasa ya kipindupindu, hasa wakati wa mvua;

Kuzuia eneo hilo kuendelea kutumika kama maficho ya wahalifu na uhalifu;

Kutoa nafasi kwa Serikali kuandaa na kuendeleza eneo hilo kwa mujibu wa sheria za nchi na mipango miji;

Utaratibu wa Zoezi
Kabla ya nyumba kubomolewa, taasisi hizi zinashirikiana kuhakiki iwapo nyumba anayokaa mkazi ina nyaraka za umiliki na vibali vya ujenzi na iwapo nyaraka hizo zina uhalali wowote. 
 
Nyumba ambazo zimethibitika kuwepo katika maeneo yasiyostahili ndio zinawekwa alama X kuashiria kwamba wakazi wanapaswa kuhama au kubomoa. Baada ya hapo, mkazi hupewa muda wa kubomoa na kuhama mwenyewe.

Kutokana na utaratibu huu, sehemu kubwa ya nyumba zinazobomolewa ni zile ambazo watu wamekwishaamua kubomoa wenyewe. 
 
Baada ya hapo, alama huwekwa kuonyesha mpaka wa bonde. Katika zoezi hili, imebainika kwamba sehemu kubwa ya wakazi wa maeneo ya mabondeni ni wapangaji huku wamiliki wakikaa sehemu nyingine salama.
 Serikali pia imeweka Dawati la Malalamiko katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Tathmini ya Zoezi
Jana, terehe 7 Januari 2016, Mawaziri watatu (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI; na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais; pamoja na Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii), walifanya mkutano wa kutathmini zoezi la kuhamisha wakazi wa mabondeni katika Jiji la Dar es Salaam. 

Mkutano huo ulipokea ripoti ya timu ya wataalam wa Wizara mbalimbali, inayoongozwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, ambayo, pamoja na mambo mengine ilibainisha kwamba sehemu kubwa ya kubaini makazi yaliyojengwa kinyume cha Sheria katika Bonde la Mto Msimbazi imekamilika. 
Ripoti ilieleza kwamba, hadi sasa, wananchi katika nyumba 774  wamehama na nyumba hizo kubomolewa. Ilielezwa pia kwamba kabla ya mkazi kuombwa  kuhama, uhakiki kuhusu uhalali wa makazi anayoishi hufanywa. 
Kutokana na uhakiki huo, jumla ya wakazi 20 walikuwa na hati halali za makazi na wakazi 119 walikuwa na leseni za makazi za muda mfupi. 
Hawa watu hawakuhamishwa. Mawaziri walipokea maelezo kuhusu changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika zoezi hilo.  
Baada ya tafakuri na mjadala, Mawaziri hao walitoka na msimamo ufuatao, kama uamuzi wa Serikali: -

1.Zoezi la kuwaondoa wananchi waishio katika bonde la Mto Msimbazi (eneo hatarishi) litaendelea kwa utaratibu ambao hautaleta mateso na usumbufu kwa wananchi;

2.Katika awamu hii, zoezi litajikita katika Bonde la Mto Msimbazi tu.

3.Kwa wakati huu, watakaohitajika kuhama ni wale tu ambao makazi yao yamo NDANI kabisa ya bonde, kwenye miteremko ya kuingia bondeni na kwenye KINGO za mto;

4.Wale watakaokuwa na nyaraka halali walizopewa na mamlaka za umma, zilizowamilikisha na kuwaruhusu kujenga katika bonde hilo, hawatahamishwa bila kupewa sehemu nyingine za kujenga. Na watumishi wa umma waliowamilikisha maeneo hayo watachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria;

5.Serikali, ndani ya siku tatu zijazo, itaanza zoezi la kuzoa kifusi na kusafisha maeneo ambapo ubomoaji umefanyika.

6.Serikali itaheshimu amri za mahakama kuhusu mapingamizi yaliyowekwa na baadhi ya wakazi wa mabondeni lakini pia itafuatilia kesi hizi ziishe haraka ili taratibu zinazofuatia zifanyike;

7.Serikali itawachukulia hatua za kinidhamu watumishi wake wanaoendesha zoezi hili kinyume na misingi ya sheria zinazotekelezwa, na kinyume na misingi ya haki na uwazi, ikiwemo wanaoweka alama za X zaidi ya mita zilizowekwa kisheria. Limeanzishwa dawati la malalamiko katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kupokea malalamiko au maswali kuhusu zoezi hili.

8.Nyumba na majengo ya miaka mingi, yaliyokuwepo miaka mingi kabla ya kutungwa kwa Sheria zinazotekelezwa kwa zoezi hili, hayatabomolewa isipokuwa tu pale maisha ya wakazi yapo hatarini. Wanaoishi katika makazi hayo watapewa miongozo ya hatua za kuhifadhi mazingira na kujiokoa na maafa;

9.Serikali haina dhamira ya kubomoa mahoteli makubwa ya siku nyingi yaliyo karibu na fukwe katika maeneo ya Masaki. Wamiliki wa mahoteli haya watapewa masharti na miongozo ya kuhifadhi mazingira kwa mujibu wa Sheria.

10.Serikali inaweka uratibu wa karibu zaidi miongoni mwa taasisi zake ili hatua za utekelezaji wa sheria za nchi zisiwe chanzo cha taharuki katika jamii.

11.Serikali haina dhamira ya kuwatesa wananchi wake kwa kuwalazimisha kuhama katika makazi yao bila sababu za msingi. Lakini pia Serikali haiwezi kuruhusu wananchi waendelee kukaa katika maeneo ambayo ikinyesha mvua kubwa maisha yao yapo hatarini.
 Itakumbukwa kwamba katika mafuriko ya mwaka 2011, wananchi 49 waishio mabondeni walipoteza maisha. Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Hali ya Hewa, mwaka huu zinatarajiwa kunyesha mvua kubwa kuliko zilizowahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.

12.  Serikali inafuatilia kwa karibu kwa mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya taarifa za wananchi wanaohitaji msaada maalum wa kibinadamu.

Suala la Mchungaji Getrude Rwakatare
Mkutano ulipokea taarifa kuhusu suala linaloongelewa sana la nyumba ya Mchungaji Rwakatare.  Ilielezwa kwamba Mchungaji Rwakatare amejenga nyumba yake pahali ambapo amezuia mtiririko wa mto kwa kujaza kifusi ili kupata eneo zaidi katika eneo la miti ya mikoko, kinyume kabisa na Sheria tatu muhimu.  
Pia ilielezwa kwamba tangu wakati ujenzi unaanza jitihada za kumsimamisha zilifanyika na mamlaka za Serikali za Mitaa lakini ikashindikana kutokana na sababu mbalimbali. Pale Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira lilipoingilia kati na kutaka kuibomoa nyumba hiyo, Baraza lilishtakiwa mahakamani. 
Wakati kesi inataka kuanza kusikilizwa, mwanasheria mdogo wa Baraza, yeye mwenyewe bila kuagizwa wala kuwaarifu wakubwa zake, mnamo tarehe 11 Mei 2015, aliingia makubaliano na mawakili wa Mchungaji Rwakatare kwa niaba ya Baraza ya kuondoa kesi hiyo mahakamani na kukubali, kwa niaba ya Baraza, kutombughudhi kabisa Mchungaji Rwakatare.  
Makubaliano hayo yalisajiliwa na Mahakama kama hukumu tarehe 13 Mei 2015. Mwanasheria huyo alificha makubaliano hayo kwa miezi mitano hadi Oktoba 2015, yalipogundulika na mtumishi mwingine wa Baraza. Mkutano ulielezwa kwamba Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa kufuata taratibu zote, alishaagiza kufukuzwa kazi, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa mwanasheria huyo. 
Mwanasheria huyo alifukuzwa kazi siku ya juzi tarehe 6 Januari 2016 na taarifa zake zimekwishafikishwa TAKUKURU. 
Vilevile, Ofisi ya Makamu wa Rais, iliiagiza Baraza kufungua shauri mahakamani la kuomba “makubaliano” kati yake na Mchungaji Rwakatare yawekwe pembeni kwasababu yalipatikana na njia ya udanganyifu. Shauri hilo lilifunguliwa tarehe 29 Disemba 2015.

Kuhusu Karakana ya Mradi wa Mabasi Yaendayo kwa Kasi (DART)
Mkutano pia ulijulishwa kuhusu hoja inayozungumzwa kwamba wananchi wanaondolewa katika maeneo ya kuishi mabondeni lakini mradi wa DART umeachwa.
 Mkutano ulielezwa kwamba Sheria ya Mazingira (kifungu 57 (2)) inatoa nafasi ya kutolewa ruhusa kwa miradi/shughuli zenye maslahi ya taifa kufanyika katika maeneo ya mabondeni, na kwamba Waziri mwenye dhamana ya mazingira anaruhusiwa kutoa miongozo ya namna ya shughuli hizo zinavyoweza kufanyika bila kuathiri mazingira.
 Mradi wa DART ulipata kibali hicho na una mkataba na Baraza la Mazingira kuhusu hatua za hifadhi ya mazingira zinazopaswa kutekelezwa katika mradi huo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
08.01.2016

Magazeti Ya Tanzania Leo Jumamosi Ya Januari 9, 2016

Mbwana Samatta alivyotua Airport Dar na tuzo yake Usiku wa kuamkia leo

$
0
0















 Jan 9 2016 mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika Mbwana Samatta alitua Dar na kupokewa na mashabiki zake kutokea maeneo mbalimbali ya jiji.


Jide, Nameless wazua gumzo wadaiwa kuwa wapenzi

$
0
0
Mbongo Fleva, Judith Wambura ‘Jide’ na msanii wa muziki wa kizazi kipya toka nchini Kenya, David Mathenge ‘Nameless’ wakikumbatiana.
Mwandishi Wetu
PICHA yenye pozi la kimahaba kati ya Mbongo Fleva, Judith Wambura ‘Jide’ na msanii wa muziki wa kizazi kipya toka nchini Kenya, David Mathenge ‘Nameless’ imezua gumzo kubwa kiasi cha wadau wao kusema wana wasiwasi wawili hao wako kimapenzi huku kesi ya talaka ya Jide ikishika kasi mahakamani, tembea na Risasi Jumamosi.
Kwa mujibu wa picha hiyo ambayo licha ya gazeti hili kurushiwa na chanzo chake lakini pia ipo kwenye mitandao ya kijamii, Jide na Nameless wamegandana utadhani ni sehemu ya kazi yao!
Jide (2)Jide.
MWONEKANO WA JIDE
Picha inamwonesha Jide kwa nyuma akiwa ‘vere klozi’ na jamaa huyo. Mikono ya Jide, wa kulia umemshika jamaa hadi shingoni na wa kushoto umeshika ukuta kwa mbele kuonesha kwamba, alikuwa akijizuia la sivyo wangeanguka. Kidevu cha Jide kimelalia bega la kulia la Nameless.
nameless-kenya-5Nameless
MWONEKANO WA NAMELESS
Kwa upande wa Nameless, yeye amemkumbatia Jide kwa mikono yote iliyokutanikia kwenye mgongo wa Jide na kumfanya aonekana amemmiliki vilivyo msanii huyo. Kidevu chake kinaonekana kikiwa sambamba na bega la kulia la Jide.
JideWALIVYOFANYA WADAU
Baada ya kusambaa kwa picha hiyo, baadhi ya wadau wa Jide au kwa lugha nyingine mashabiki, waliisukuma kwenye Mtandao wa WhatsApp wa mume waliyetangana naye, Gardner G. Habash kwa lengo la kumwonesha picha hiyo ili kumrusha roho.
MITANDAONI GUMZO
Saa chache baada ya kuingia mitandaoni, picha hiyo ilizua gumzo kubwa huku kila mtu akizungumza lake. Kuna ambao walimtakia heri kama ni kweli wana uhusiano huku wengine wakisema si rahisi kwani Nameless ana mke wake (Wahu, mwanamuziki).
RISASI JUMAMOSI LASAKA UKWELI
Juzi, gazeti hili lilimtafuta kwa njia ya simu Jide mwenyewe kwa lengo la kumuuliza kama kuna kitu zaidi kati yake na Nameless lakini hakuwa hewani. Hata hivyo, watu wake wa karibu walisema mwanamuziki huyo yupo nchini Kenya kikazi.
Gazeti hili likajiongeza kwa kumtafuta mmoja wa viongozi wa Jide kwa sasa ambaye aliomba hifadhi ya jina lake na kumuuliza kama anajua chochote kuhusu picha hiyo ambapo alisema:
“Ninavyojua mimi Jide alikuwa Kenya kikazi na huyo jamaa (Nameless). Jide, si Nameless tu, pia amefanya kazi na Morgan Heritage na wamefanya na Sauti Sol. Haiwezi kuwa kweli maana Nameless ana mke.
Risasi Jumamosi: “Kama kweli ni kazi, ni ngoma gani wamefanya Jide na Nameless?”
Kiongozi: “Details hizo (maelezo) hatuwezi kutoa kwa sasa lakini ndiyo wamefanya kazi na wote katika Studio ya Bruce Othiambo ya Sauti Sol.
“Hata mimi mwenyewe nilikuwa Kenya na Jide lakini tumerudi. Kama humpati kwa simu labda amezima, hajaamka kwa uchovu wa safari.”
GARDNER SASA
Risasi Jumamosi juzi lilimtwangia simu Gardner kwa lengo la kumsikia anasemaje kuhusu ‘mtalaka’ wake huyo na Nameless lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Hata alipotumiwa meseji kwa simu na kuambiwa kila kitu, hakujibu.
MADAI YA TALAKA
Wakati hali ikiwa hivyo, gazeti hili lina taarifa ya ile kesi yao ya talaka ambapo habari zinasema kuwa, Jide ameshinda kesi hiyo baada ya Mahakama ya Mwanzo Manzese/Sinza kukubali ombi lake.
Inadaiwa kuwa mahakama hiyo ilitoa hukumu hiyo mwishoni mwa mwaka jana.
Hata hivyo, wiki iliyopita, Gardner alitafutwa na kuulizwa kuhusu ishu ya talaka ambapo alisema: “Hakuna talaka iliyotoka. Kama ingetoka kweli, lazima mimi ningeitwa mahakamani. Sasa mbona sijaitwa?”
Lakini pamoja na utetezi huo wa Gardner, kiongozi mmoja wa Jide alipoulizwa, alikiri kutolewa kwa talaka hiyo mahakamani akisema, anachotakiwa kufanya Gardner ni kufuata kopi yake kwa makarani wa mahakama hiyo.
HABARI NYINGINE
Pamoja na yote, kuna habari kwamba, Jide yuko huru kwa sasa kufuatia shauri lake na mtalaka huyo kuhusu mgawanyo wa mali kumalizika kwenye Ofisi za Ustawi wa Jamii, Kinondoni jijini Dar.
Ilidaiwa kuwa, katika shauri hilo, Gardner aliamua Jide ndiyo agawanye mali kwa kadiri atakavyoona yeye, hata kama hatampa angalau meza ya chakula. Hata hivyo baada ya kauli hiyo, ilipaswa wanandoa hao wakutane ili kuhitimisha safari yao ya ndoa jambo ambalo bado halijafanyika.

CHANZO: GPL

Video: Alichosema Samatta Uwanja wa Ndege Dar

Hawa Ndiyo ‘Maadui Wakubwa’ wa Diamond Kesho!

$
0
0


Diamond platinumz (11) 
Staa wa ngoma ya Utanipenda, Nasbu Abdul ‘Diamond’.
…’nayosema yana maana, sababu hakuna anayejua kesho, anayepanga ni Rabana, ila ameificha ni confidential, ukisali omba sana, mumeo nisije kuwa kichekesho, Maana rafiki wa jana, ndiye adui mkubwa keshoo!!!”
Ni mojawapo ya verse (ubeti) uliyomo kwenye hit single ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ’Diamond’ iitwayo Utanipenda? Wimbo ambao ndani ya takriban siku 30 tangu kuachiwa kwa video yake kwenye Mtandao wa YouTube umetizamwa karibu mara milioni 2!
Diamond platinumz (6)Moja ya vipande katika video mpya ya wimbo wa Diamond, Utanipenda
Katika wimbo huo, Diamond amejaribu kuvuta hisia na kujiweka katika nafasi ya msanii maarufu atakayefulia siku moja.
Amejaribu kuvuta picha na namna ambavyo mambo yanavyoweza kutokea kwake binafsi na kwa familia yake.
Ameenda mbele zaidi kuwazungumzia wadau wake wakubwa, au ‘marafiki zake’ katika mafanikio yake ya sasa namna ambavyo wanaweza kumgeuka, kwa sababu anatambua kwamba ‘rafiki wa jana, ndiye adui mkubwa kesho’
Katika Showbiz ya leo, nakuletea listi kamili ya ‘marafiki’ hao wanaoweza kuja kuwa ‘maadui wakubwa’ kesho ambao amewataja kwa majina mmojammoja na nguvu au mchango walionao katika maisha yake ya sasa na ya baadaye, japo hatuombei wala hatutarajii yamkute aliyoyawaza, lakini kama alivyosema mwenywewe ‘ Anayepanga ni Rabana, ila ameificha (kesho), ni confidential;
MENEJA TALE
Ametajwa kwenye vesi ya kwanza tu ya wimbo huo. Anajulikana kama , Hamis Tale ‘Babu Tale’ au Meneja Tale. Unaweza kusema ndiye Meneja Mkuu wa Diamond Platnumz.
Ni miongoni mwa wadau wakubwa vijana wa muziki nchini Tanzania, anasimamia na kuratibu karibu shoo zote za msanii huyu, ndani na nje ya Tanzania. Ndiye anayepokea michongo yote ya shoo za Daimond na kundi zima la Wasafi Classic Baby (WCB).
Katika wimbo huo, Diamond amemuweka katika kundi la meneja ambaye mambo yakiharibika, atakuwa hamtaki tena kiasi kwamba hata akimuona kwa mbali, atakuwa ana lala mbele (anamkimbia ni sheedah! Ameimba; Redio nyimbo wamezima, TV ndiyo hatari, meneja umebaki jina, hanitaki hata Tale…).
KIMWANA
Huyu ni dada wa hiyari wa Diamond, anajulikana zaidi kwa majina ya Halima Kimwana, ambaye amekuwa mtu wa karibu sana wa msanii huyo kiasi cha wengine kusema ni mpenzi wake ama dada yake damdam. Kutokana na ukaribu huo, bila shaka anajua mambo mengi ya Diamond na anaweza kuwa na athari katika maisha yake.
Diamond platinumz (9)Kutoka kushoto ni Sallam, Jackline Wolper, Babu Tale na God Father .
Kimwana ametajwa katika wimbo wa Utanipenda katika mstari mmoja wapo, pale Diamond anaposema “Kimwana sidadaangu, eti naye hanifahamu…” akimaanisha kwamba siku atakapofulia, Kimwana atajifanya hamfahamu licha ya ukaribu walionao sasa!
harmonizeHarmonize
HARMONIZE
Ni msanii chipukizi anayetamba na ‘hit singo’ ya Aiyola, majina yake ya kwenye paspoti ni Rajabu Abdulkhali a.k.a Harmonize. Kama Harmonize ana mtu anayemheshimu na kumthamini sana katika mafanikio aliyoyapata hadi sasa, basi ni Diamond, kwani ndiye msanii aliyetambua kipaji chake na kuamua kumsaidia kwa kumuweka chini ya lebo yake (WCB) na kuwa msanii wa kwanza kutolewa na kujulikana ndani ya muda mfupi.
Katika mabadiliko ya kimaisha anayoyatabiri Diamond katika Utanipenda, amemtaja msanii huyu kwa kusema;
“..Hata Harmonize nikimpigia ananifokea kama Sallam…..” akimaanisha kwamba hata huyu dogo atasahau wema wote aliomtendea mpaka kufanikiwa na kuanza kumletea nyodo kiasi cha kumfokea pale anapopigiwa simu ili amsaidie..dah!
SALLAM
Ni meneja wa Diamond akishirikiana na Babu Tale. Anajulikana kwa majina ya Sallam Sharaff ambaye ni mfanyabiashara, promota wa wasanii na mtendaji mkuu wa SK Entertainment. Ni kijana ambaye anamuongoza na kuendesha mambo mengi ya Diamond na ndiyo maana kwenye wimbo wake anamwambia Harmonise atakuwa akimfokea kama Sallam, kwani sasa hivi ndiye kama bosi wake pia.
Diamond platinumz (12)Kipande cha video hiyo kinachoonesha Mama Diamond akitimuliwa nyumbani kwa ‘JK’.
JK
Ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye Diamond anamuelezea kama ni mtu mwenye mchango mkubwa katika mafanikio yake, mbali ya kuwa ni kiongozi wa nchi, lakini kwake amekuwa mshauri na rafiki.
Hivyo katika hali ya kawaida, iwapo ikitokea Diamond akakwama, JK atakuwa mtu wa kwanza kumkimbilia kuomba msaada,lakini anaweza pia akajikuta anaishia getini na kufukuzwa.
Kwenye Video ya Wimbo wa Utanipenda, Diamond amemuonesha mama yake (Sandra) akiwa amembeba mgongoni mwanaye, Tiffah akienda kwa Jakaya kuomba msaada lakini anakataliwa na mlinzi hata kuingia ndani, anaishia getini.
FELLA
Jina lake kamili ni Said Fella, a.k.a Mkubwa Fella, ambaye hivi karibuni ameukwaa Udiwani wa Kata ya Mbagala jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ni Meneja wa Yamoto Band, mvumbuaji na muendelezaji wa vipaji vya wasanii wa Bongo hasa vijana, ana kituo cha kuendeleza vipaji vya muziki wilayani Temeke.
Fella, Tale na Diamond wana masilahi ya pamoja katika Yamoto Band.
Fella naye ana ‘play part’ kubwa ya mafanikio ya Diamond na ndiyo maana ametajwa katika wimbo huo kuwa naye anaweza kuja kumgeuka baada ya kufulia ambapo mama yake anaonekana kweye video akienda kuomba msaada nyumbani kwa Mkubwa Fella lakini naye anaishia getini.
TIFFAH-DIAMOND.jpgDiamond akimbeba mwanaye, Tiffah
ROHO YAKE (TIFFAH)
Katika wimbo huu, Diamond anamtaja mtoto wake pekee, Princess Tiffah kama ndiye roho yake iwapo mambo  yataharibika.
Diamond anatuonesha namna ambavyo binti yake atahangaika. Tiffah ndiye mtoto wake wa kwanza na wa pekee hadi sasa, kwani tangu aanze uhusiano wa kimapenzi miaka kadhaa iliyopita na wanawake kadhaa, hakuwahi kupata mtoto.
Diamond platinumz (2)Diamond katika pozi na kimwana wake, Zari.
ZARI
Diamond ndiye ameshafulia, usupastaa hakuna tena, hapati shoo tena kama zamani na hata akipata hazijazi watu, kwake ni mikosi tu, sawa na jahazi kuzama. Swali linakwenda kwa mpenzi wake wa sasa, ambaye ni matawi ya juu na bila shaka amempenda
Diamond na kuamua kumzalia mtoto si kwa sababu ya pesa zake, bali pengine kwa umaarufu wake, kwa sababu ukilinganisha utajiri wa Diamond na wa Zari unaonesha Zari ni zaidi.
Katika wimbo huu, Diamond anamtupia swali mama watoto wake; Je, nawe utanipendaga au nawe ndiyo utanimwaga? (pindi atakapofulia).
MAADUI WENGINE
‘Maadui’ wengine watarajiwa wa Diamond ambao amewatajani pamoja na mashabiki zake, vyombo vya habari kama redio, TV na magazeti, amekwenda mbele zaidi kwa kuonesha ni magazeti gani ambayo atakapofulia na kumwagwa na Zari hayatasita kumuandika.
Kwenye video yake amelionesha gazeti hili la Ijumaa, gazeti namba moja la kuandika habari za mastaa nchini Tanzania, kuwa litakuwa na habari zake ukurasa wa mbele.
ANAUPENDA SANA
Kwa mujibu wa Diamond mwenyewe, wimbo huu wa Utanipenda ni wimbo ambao ametokea kuupenda zaidi kuliko nyimbo zake zingine kwa mwaka huu.
Sehemu au vesi anayoipenda zaidi ni hii inayosema: “…ooo bado nimewaza sana, zile tunzo, mashauzi ya airport, je itakapofika tamati, utadiriki hata japo kunipost?
Pindi shows zimekwama, nikipata sijazi ni mikosi, ooh jahazi limezama, Mola ninusuru baba.
“Kama namuona mwanangu, roho yangu, Tiffah Dangote, Anakwenda na Mama’ngu kwa Jakaya Kikwete wanafukuzwa watoke, usilie Sandra wangu, mboni yangu, jikaze usichoke….”
Nadiriki kusema Utanipenda ni miongoni mwa nyimbo zinazofundisha jamii na umewasilisha ipasavyo dhima ya msanii kwa jamii. Ni vyema kujua kuna maisha mengine kesho ambayo hatuyajui na tunatakiwa kujitambua katika hilo kadiri tunavyopata mafanikio.

Mbwana Samatta alivyopokelewa na serikali Uwanja wa Ndege Dar

Isabela asaula live hotelini jijini Dar

$
0
0



Miss Ruvuma 2006 ambaye pia ni msanii wa filamu za Kibongo na muziki wa kizazi kipya, Isabela Mpanda ‘Bella’, ametoa kali ya kufungulia mwaka baada ya hivi karibuni kusaula nguo zote alizokuwa amevaa mbele za watu.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lisilo na staha, lilitokea ndani ya hoteli moja maarufu iliyopo maeneo ya Oyster Bay jijini Dar ambapo inaelezwa kuwa msanii huyo na wenzake, walikuwa wakirekodi video mpya ya mwanadada huyo ‘chakaramu’.
“Unajua mnapokuwa ‘location’, mkimaliza kucheza ‘scene’ moja mnaingia vyumbani kubadilisha nguo kwa ajili ya kuendelea na zoezi la kurekodi. Sasa Bella badala ya kuingia chumbani, yeye aliamua kuvua nguo mbele za wasanii, madairekta na wapiga picha waliokuwa wakishuti video yake.

“Alivua moja baada ya nyingine, tukabaki tumepigwa na butwaa,” kilisema chanzo chetu na kuongeza kuwa kitendo hicho kilisababisha wasanii wenzake aliokuwa nao hotelini hapo kuingilia kati ambapo walimponda kwa kukosa staha.

Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Isabella ambapo alipopatikana alisema:
“Mimi naishi maisha yangu, hakuna mtu wa kunipangia nini cha kufanya. Nilikuwa nashuti video ya wimbo wangu wa Nimekumisi, we elewa tu hivyo,” alisema Isabela.


CHANZO: GPL

Samatta apewa uraia wa DR Congo

$
0
0
Samatta apewa uraia wa DR Congo

GUMZO ni Mtanzania Mbwana Samatta kutwaa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa wanaocheza soka Afrika. Mitandao mbalimbali na vyombo vya habari jana Ijumaa viliripoti tofauti kwa kumvika uraia wa nchi nyingine Samatta.
Mtandao maarufu wa Wikipedia uliandika Samatta ni raia wa DR Congo inapotokea timu ya TP Mazembe anayochezea straika huyo.
Mtandao wa NBC wa Marekani ukaandika mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba ni raia wa Tunisia.
Hali hiyo ilizua sintofahamu kwa watu wengi lakini baadaye Wikipedia walibadili na kuandika Samatta ni raia wa Tanzania.
Samatta hadi anatwaa tuzo hiyo, katika fainali aliwapiku Robert Kidiaba anayecheza naye TP Mazembe raia wa DR Congo. Pia alimzidi raia wa Algeria, Bounedjah Baghdad anayechezea Etoile du Sahel.
Kwa upande mwingine, mastraika wa Yanga, Donald Ngoma na Amissi Tambwe wote walimpongeza Samatta na kusema ameonyesha kweli yeye ni mchezaji bora Afrika.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Tambwe raia wa Burundi, akiwa na Ngoma ambaye ni raia wa Zimbabwe, walimtumia Samatta meseji za kumpongeza kutokana na kutwaa tuzo hiyo.
“Tulimpongeza kwa kutwaa tuzo ya uanasoka bora Afrika, hii inadhihirisha yeye ni bora na sisi tunakubali uwezo wake. Samatta ametutoa kifua mbele watu wa Afrika Mashariki,” alisema Tambwe ambaye nchi yake Burundi inaunda Umoja wa Afrika Mashariki.
“Samatta ana uwezo mkubwa sasa, ameisaidia Mazembe kutwaa ubingwa wa Afrika, kweli huyu ni bora Afrika na tunampongeza kwa kweli.
“Hii ni nafasi ya wachezaji wengine siyo wa Tanzania tu bali wote tunaotoka Afrika Mashariki kujituma na kufanya vizuri zaidi.”
Samatta alitarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo akitokea Lagos, Nigeria kulikofanyika sherehe za utoaji wa tuzo hizo zinazoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>