Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

MKALI WA SONGI LA 'AMARULA' ROBERTO TOKA ZAMBIA AWASILI NCHINI TANZANIA,

$
0
0

MKALI WA SONGI LA 'AMARULA' ROBERTO TOKA ZAMBIA AWASILI NCHINI TANZANIA, ATUA MWANZA PATA MAHOJIANO ALIYOFANYA NA JEMBA FM 93.7

Mtangazaji wa Jembe FM host wa kipindi cha HIT ZONE kinachoruka hewani siku za Jumatatu hadi Ijumaa saa saba mchana hadi saa kumi jioni Timoth Ngalula aka 'Mbaba' akifanya mahojiano na mwanamuziki toka nchini Zambia Roberto ambaye ni mkali wa songi linalokwenda kwa jina la Amarula, ikiwa ni maandalizi ya show yake kali itakayofanyika kesho Jumamosi ya tarehe 3 oct 2015 Jembe Beach Resort Malimbe jijini Mwanza, Kiingilio ni shilingi 10,000/= Kawaida na VIP ni shilingi 50,000/=.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA SEHEMU YA KWANZA.  
Mwanamuziki toka nchini Zambia Roberto ambaye ni mkali wa songi linalokwenda kwa jina la Amarula, hapa akisikiliza kwa umakiini moja kati ya maswali yaliyoulizwa na HIT ZONE ya JEMBE FM Mwanza 
ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA SEHEMU YA PILI.

 

Mtangazaji wa Jembe Fm Bonzy kwenye mic.
Mwanamuziki toka nchini Zambia Roberto ambaye ni mkali wa songi linalokwenda kwa jina la Amarula, (C) akipata picha ya pamoja na moja kati ya watangazaji wa Jembe FM 93.7 Mwanza hii leo mara baada ya kufanya mahojiano.
Mtangazaji wa Jembe Fm Kipindi cha majira ya jioni Jacquline Shuma aka Curry Barry Coco (L) akipata picha na Rais wa Team Maua Classic ambaye ni balozi wa kitaa wa  Jembe Fm, Bobb White Pamba (R).
Mapicha kwa Instagram na Facebook yalihusishwa.
Mwanamuziki toka nchini Zambia, Roberto ambaye ni mkali wa songi linalokwenda kwa jina la Amarula, akionyesha ishara ya kidole kimoja kuashiria kauli mbiu ya Jembe Fm 'PAMOJA SANA'
PAMOJA SANA kutoka kushoto ni Bob White Pamba toka Team Maua Classic, DJ Hq wa Groove Entertainment, Roberto 'Amarula' , Producer Oxy na Dreva wetu Ramadhan Suka.
We...Peace.
Kutoka kushoto Chriss The Dj, Roberto, DJ HQ, Bob White Pamba na nyuma ni Baraka.
Balozi wa Habari toka Jembe Media Group Mr. Albert G. Sengo akifanya mazungumzo na Barmedaz Tv jinsi team yake ilivyojipanga kwa mashambulizi hiyo jumamosi ya tarehe 3October 2015 Jembe Beach Resort.
PAMOJA XANA.

AUNT EZEKEL AKANUSHA TUHUMA ZAKE NA NAPE

$
0
0




Naomba niwakumbushe jambo moja kubwa na la msingi ambalo labda mmelisahau. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na inaruhusu kila mtanzania kuwa na imani yake ya kisiasa, kwani ni haki yake ya msingi.Kiukweli nasikitishwa sana na hii tabia ya watu kuamini kwamba vijana wanaokiunga mkono chama tawala wamenunuliwa, wanatukanwa kila siku na kudhalilishwa kana kwamba hawana haki kwenye nchi yao.Mbaya zaidi sasa tunaelekea kwenye kupandikizwa ugomvi na viongozi wetu wa chama, najiuliza ili iweje?
Ndio demokrasia hiyo?
Jioni ya leo kuna clip ya kutengenezwa, imewekwa, eti mimi nagombana na Katibu Mwenezi wa CCM, hicho kitu hakijawahi kutokea, sisi hatuna tofauti, najiuliza sasa haya yote yanatoka wapi?
Kwa nini tusiongee sera tukabaki kwenye kuamua kumpigia tunayemtaka?
Kuna wakati kaka yetu ambaye ni Mwandishi wa muda mrefu Mdimuz aliwahi kuandika twitter kwamba kuna demokrasia ya mihemko, nikawa sijamuelewa leo ndio nimemuelewa, tuongee hoja za msingi, tujibu kwa hoja matusi tusiyape nafasi wala kuchafuana.
Kuna maisha baada ya uchaguzi, tusije kushindwa kuangaliana usoni na hii mihemko yetu na jazba tunazozipa nafasi mpaka tunapandikizana mauongo.
Mungu atubariki sana sisi watanzania na amani yetu iliyo katika hatari ya kuchafuliwa na wasiojielewa", Aunt Ezekiel ameandika kwenye ukursa wake wa Instagram

Toka jana clip yenye sauti inayodaiwa ni kuwa ya Aunt Ezekiel ikimtolea maneno machafu Nape imekuwa ikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii hususani Whatsapp

KAYIRA, IDD SEIF WAACHA KAZI BBC

$
0
0

              Aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza BBC, Kassim Kayira.
vlcsnap-322919
Aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza BBC, Idd Seif.
vlcsnap-323676
Kassim Kayira na Idd Seif wakiwa katika studio ya BBC.
vlcsnap-327856
vlcsnap-327492
Idd Seif na Kassim Kayira wakiagana.
vlcsnap-327568vlcsnap-327929
Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza BBC wakiwaaga watangazi hao.
WATANGAZAJI bora kabisa wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza BBC, katika kipindi cha Dira ya dunia, Kassim Kayira na Idd Seif wameacha kazi katika kituo hicho kikubwa duniani.
Kwa mujibu wa watangazaji hao wawili waliokuwa pamoja studio katika kipindi cha Dira ya Dunia kwa mara ya mwisho jana, walisema wameamua kuacha kazi na kurudi nyumbani Afrika ili kuendeleza miradi yao.
Idd Seif, ambaye alijiunga na BBC mwaka 1997 akitokea Kampala, Uganda, alisema ameamua kurejea Uganda ili aweze kusimamia miradi yake, baada ya kazi ya utangazaji kwa miaka 40. Alielezea huzuni yake kwa kuwaacha watu waliompokea vizuri na kufanya nao kazi kwa miaka 20.
Kwa upande wake, Salim Kayira, alisema alijiunga na shirika hilo akitokea kituo cha televisheni cha Rwanda miaka kumi iliyopita akiwa Mhariri. Alisema naye atarejea Afrika ambako atajishughulisha na kilimo pamoja na ufugaji na sehemu aliyoamua kuishi ni Uganda.
Watangazaji hao wameondoka miezi michache baada ya mtangazaji mwingine mahiri wa Kiswahili, Charles Hilary wa Tanzania kuacha kazi na kujiunga na kituo cha televisheni cha Azam. Taarifa ambazo hazijathibitishwa, zinasema wawili hao nao huenda wakajiunga na Azam tv.

Kada wa CCM agongwa na gari afia hospitali Dodoma

$
0
0


 

Kwa ufupi

Tukio hilo lilitokea saa tisa alasiri katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe A kabla ya Duni kuwasili kuhutubia mkutano wa kampeni.
By Sharon Sauwa
Dodoma. Kada wa CCM, Fatuma Isaka anayedaiwa kugongwa na gari kwenye vurugu zilizotokea juzi baada ya wafuasi wa chama hicho kuvamia mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji, amefariki dunia.
Tukio hilo lilitokea saa tisa alasiri katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe A kabla ya Duni kuwasili kuhutubia mkutano wa kampeni.
Inadaiwa Fatuma aligongwa na gari la CCM baada ya kuteleza wakati likiondoka kwenye uwanja huo.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Jenifa John alisema wakiwa katika viwanja hivyo, walifika makada sita wa CCM na kuwaamuru wanachama wa Chadema kuondoka kwa madai kuwa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ilionyesha hawakupangiwa kufanya mkutano kwenye eneo hilo kwa siku hiyo.
“Walituambia Serikali ni yao na shule ni yao, kwa hiyo hakuna chama chochote kinachoweza kuwazuia kufanya kampeni mahali hapo na kututaka tuondoke,” alidai Jenifa.
Alisema baada ya mabishano hayo, makada hao wa CCM waliokuwa na gari, waliamua kuondoka.
Alisema wakati gari linaondoka, kada mmoja wa chama hicho (hakumtaja jina) alikuwa hajapanda, hivyo alivyokuwa akitaka kulirukia kwa bahati mbaya aliteleza, akaanguka na kukanyagwa na magurudumu ya nyuma.
“Wenzake waliondoka na kumuacha majeruhi huyo akiwa chini. Wakazi wa eneo hili walikodi gari na kumpeleka hospitali,” alidai Jenifa.
Akizungumzia tukio hilo, Katibu wa Chadema Mkoa wa Dodoma, Kennedy Kimario alisema CCM ilifanya makusudi kuvamia mkutano huo. “Walifanya fujo bila sababu, walikuwa wanajua kuwa anapokuja mgombea urais au mgombea mwenza kisheria mikutano yote midogo ya kampeni inapaswa kusimama,” alisema Kimario.
Katibu Msaidizi wa CCM Mkoa wa Dodoma, Othman Dunga alivilaumu vyombo vya dola kwa madai kuwa vilishindwa kuchukua hatua mapema. “Sisi tulikuwa na barua halali kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi ya kufanya mkutano mahali hapo, lakini walipokuja polisi waliwaruhusu Chadema waendelee na mkutano wao wa kampeni,” alidai Dunga.
Hata hivyo, Dunga alidai kuwa kada huyo aligongwa na gari la Chadema na kuchomwa mwilini na vitu vyenye ncha kali.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Mnyambuga alithibitisha kutokea kwa mgongano wa ratiba kati ya vyama hivyo na kumalizwa na msimamizi wa uchaguzi wa Manispaa ya Dodoma Mjini.
“Ratiba ilileta shida baada ya kufanyiwa marekebisho kwa sababu siku hiyo aliyekuwa ahutubie mkutano ule wa kampeni alikuwa mgombea mwenza wa Chadema, kwa mujibu wa utaratibu, ililazimu kupangua ratiba suala hilo lilimalizwa na mkurugenzi ambaye ni msimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Dodoma Mjini),” alisema.

Chanzo: Mwananchi

Tatizo la umeme nchini lawa kizungumkuti

$
0
0





By Bakari Kiango
Tanga. Uwezo wa kuzalisha umeme kwenye vituo vya Nyumba ya Mungu, Hale na New Pangani Falls nchini umeshuka kutoka asilimia 100 hadi kufikia 15 kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya baadhi ya wananchi kuchepusha mkondo wa maji wa Mto Pangani ambao ni tegemeo kubwa kwa uzalishaji wa vituo hivyo.
Hayo yalisemwa jana na Mhandisi, John Skauki katika eneo la Mto Pangani kunakodaiwa mkondo wake wa maji kuchepushwa katika Kijiji cha Buiko, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.
Mhandisi Skauki alisema hali hiyo imesababisha umeme kuzalishwa chini ya kiwango tofauti na matarajio ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Alisema kituo cha Nyumba ya Mungu huzalisha umeme mita za ujazo 10 kwa sekunde chini ya kiwango cha ujazo wa mita 25 za kawaida. Kiwango kinachohitajika ni mita za ujazo 45.
“Suala hili la kuchepusha mkondo wa maji linashughulikiwa na mamlaka husika,” alisema Skauki.
Alisema kwa kawaida, maji hayo husafiri kwa ujazo wa mita 42 kwa sekunde kuelekea Bwawa la Nyumba ya Mungu linalotiririsha maji vituo vya New Pangani Falls na Hale kwa ajili ya kuzalisha umeme.
“Kwa sasa Bwawa la Nyumba ya Mungu linazalisha megawati tano badala ya saba, New Pangani 17 badala ya 68 za kawaida na Hale megawati nne kati ya 10 zinazotakiwa ,” alisema Mhandisi Skauki.
Mtaalamu wa Bonde la Maji la Mto Pangani, Vendelin Basso alisema ofisi yake imeendelea kulishughulikia tatizo hilo.
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Buiko, Idd Seng’onyi alisema kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, wakazi wa eneo hilo wanapata hasara ya mazao yao kutokana na maji ya mto huo kutuama sehemu moja badala ya kutembea.

Vicent Nyerere: Tutamchagua Lowassa hivyohivyo

$
0
0




By Anthony Mayunga
Serengeti. Mwenyekiti wa Chadema Musoma Mjini, Vicent Nyerere amesema Mkoa wa Mara utamchagua Edward Lowassa kuwa rais licha ya madai kwamba ni mgonjwa ili aweze kushughulikia masuala ya hospitali na kumwambia mgombea huyo kuwa: “Wanasema wewe mwizi, sisi huku tumesema tutamchagua mwizi na kumfungia Ikulu miaka 10 atumikie wananchi.”
Nyerere alisema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine, Serengeti mkoani Mara.
“Lowassa wamekutukana sana na wengine wanasema wewe mgonjwa, sasa sisi tumesema Mkoa wa Mara tunamchagua mgonjwa ili ashughulikie masuala ya hospitali zetu kwa kuwa hilo ndilo tatizo kubwa.
“Rais ambaye akiweka sahihi mtu ananyongwa, sahihi yake inaruhusu nchi kuingia vitani, anazungumza kuwa atajenga Mahakama za kufunga wezi na mafisadi, wakati ukienda magereza waliojaa ni walala hoi… sisi watu wa Mkoa wa Mara tunasema hatuhitaji mahakama za mafisadi, tunahitaji hospitali bora,” alisema Nyerere.
Huku akishangiliwa na umati wa waliofika kumsikiliza, Nyerere alisema pia kuwa baba yake mkubwa, hayati Mwalimu Julius Nyerere alitawala kwa miaka 23 lakini hakuwahi kutoa kauli za kibabe.
Lowassa
Akihutubia mkutano huo wa kampeni, Lowassa aliahidi kujenga barabara ya lami kuanzia Makutano hadi Mto wa Mbu kupitia Mugumu iwapo atachaguliwa na kusema anakusudia kumaliza matatizo yanayoisumbua wilaya hiyo ikiwamo barabara, chujio la maji, migogoro ya wanyama na wananchi na hospitali ili kuhakikisha wananchi wa wilaya hiyo wanafaidi matunda ya nchi.
“Wingi wenu ni ishara kubwa kuwa mnataka mabadiliko ya kweli, natambua mnayo matatizo mengi hapa, ninaombeni mtumie wingi wenu huu kunipigia kura, mbunge na madiwani ili tuweze kuleta mabadiliko, nasisitiza nipeni mgombea ubunge ili tushirikiane kukamilisha matatizo hayo ikiwamo barabara,” alisema.
Hivi karibuni, akiwahutubia wakazi wa Mji wa Mugumu, mgombea mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan alisema wakichaguliwa, watahakikisha barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami.
Lowassa alisema anakerwa na mfumo ambao umeanza kujengeka wa wanyama kuthaminiwa kuliko wananchi, pamoja na kurejea kauli yake kuwa serikali yake itachunguza upya suala la Operesheni Tokomeza ili waliopata madhara wafidiwe huku akisisitiza kurudisha heshima ya wananchi kuthaminiwa badala ya wanyama.
Kuhusu bodaboda, aliahidi kuwa serikali atakayounda itawatafutia benki ili wakopeshwe.
“Katika nchi zilizoendelea kundi kama hili la bodaboda, serikali inawajibika kuwalipa kwa kuwa hawana ajira… hapa pamoja na kushindwa kuwatafutia mitaji, wamebaki kuwafukuza na kuwapiga, lazima hayo yakomeshwe na watakuwa marafiki zangu,” alisema.
Akimnadi mgombea ubunge jimbo hilo, Marwa Ryoba na madiwani wa kata 30, Lowassa aliwataka wananchi kutobweteka, bali wahakikishe wanajitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura na kwamba hiyo ndiyo itakuwa silaha pekee ya kuiondoa CCM na kuiweka ya Ukawa ili iwaletee mabadiliko ambayo yameshindikana kwa muda mrefu.
Sumaye
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye aliwataka wananchi wasimchague mgombea wa urais wa CCM kwa kuwa hana sifa za kuwa kiongozi mkuu, haambiliki na hapokei ushauri wa wengine.
“Nimekuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10, Lowassa na Magufuli walikuwa mawaziri chini yangu, najua utendaji wao, Lowassa ni mtu wa kutafakari kwanza kabla ya kuchukua hatua, lakini huyu Magufuli anahitaji kuwa chini ya mtu... kauli zake za sasa hata ninyi mmesikia huyu alipaswa kuwa waziri chini ya mtu,” alisema.
Sumaye alisema wananchi wanatakiwa kumpima kwa kauli zake ambazo anatoa kwa sasa ikiwa ni pamoja na kushughulikia mafisadi na wala rushwa ndani ya Serikali ya sasa ambayo na yeye ni miongoni mwao.
“Wao wanapita na kututukana lakini sisi tunaeleza ukweli mtupu, kama ufisadi umemshinda ndani ya wizara yake anawezaje ngazi ya urais? Amelazimisha kununua meli mbovu iliyotumika kwa zaidi ya miaka 30 ambayo walitarajia iwe inafanya safari zake kwenda Bagamoyo, sasa wameipeleka Kusini, nawaambia Watanzania mtajuta,” alisema.
Alisema miongoni mwa matatizo yatakayoikuta serikali itakayoundwa na Lowassa endapo atachaguliwa ni kulipa madeni makubwa ya nje ambayo yamefikia zaidi ya Sh35trilioni. Alisema wakati hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kutokana na matumizi mabaya ya CCM ikiwamo safari zaidi ya 412 za Rais zilizotumia zaidi ya Sh4trilioni kwa kipindi cha miaka 10, Dk Magufuli amezisifia kuwa zimetusaidia na kuongeza kuwa hiyo inaashiria kuwa wakimchagua huenda akatembea zaidi ya mtangulizi wake.
Alibainisha kuwa mfumo ndani ya CCM ni mbovu ndiyo maana watu wengi wanakimbia, kwa kuwa fedha za umma zinachotwa na watu na kuanzisha kampuni kubwa ambazo huandika majina ya watoto wadogo hata wa miaka mitatu, huku watoto wengine wakikosa madawati na dawa hospitalini hakuna.
Kabla ya mkutano
Shughuli nyingi mjini Mugumu zilisimama na watu walijaa uwanjani hapo kuanzia saa mbili asubuhi, eneo hilo likipambwa kwa bendera na mabango ya mgombea huyo. Aliwasili saa sita mchana na kuhutubia na baadaye kuelekea Nyamongo wilayani Tarime.
Chanzo: Mwananchi

MWAMBUSI RASMI YANGA, AWAAMGA MBEYA CITY, KUANZA KAZI YANGA RASMI JUMATATU

$
0
0


Baada ya uficho wa siku kadhaa, sasa mambo hadharani kuwa Kocha Juma Mwambusi, amechukua nafasi ya Charles Boniface Mkwasa.

Mwambusi aliyekuwa Kocha wa Mbeya City, amechukua nafasi ya kocha msaidizi wa Yanga iliyoachwa na Mkwasa ambaye sasa ni Kocha Mkuu wa Taifa Stars.
Mwambusi tayari amewaaga Mbeya City na rasmi amesajiunga na Yanga kwa mkataba wa  miaka miwili, huku akitarajia kutambulishwa kesho.

Kocha huyo ataanza kazi rasmi keshokutwa Jumatatu chini ya Kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm.

SIMBA YAMJUMUISHA KIIZA SAFARI YA MBEYA, APISHANA NA MWAMBUSI

$
0
0


Mshambuliaji Hamisi Kiiza ambaye alikuwa majeruhi anaungana na Simba katika safari ya Mbeya.

Simba inafunga safari kwenda kuivaa Mbeya City katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayipigwa Jumatano.

Kiiza ni kati ya wachezaji 22 wa Simba watakaosadiri hadi Mbeya kwa ajili ya mechi hiyo.
Mbeya City itakuwa ikicheza kwa mara ya kwanza bila ya kocha wake mkuu, Juma Mwambusi.


Mwambusi amejiunga na Yanga na sasa atakuwa Kocha Msaidizi akichukua nafasi ya Charles Boniface Mkwasa ambaye sasa ni Kocha Mkuu wa Taifa Stars.

Tamasha la Jokate latikisa Sekondari ya Jangwani, Dar

$
0
0
IMG-20151010-WA0007IMG-20151010-WA0012Staa wa Bongo fleva, Ally Kiba na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ wakikamua jukwaani.IMG-20151010-WA0008Kiba na madenti wakishambulia jukwaa.
IMG-20151010-WA0009 Wanafunzi wa shule mbalimbali za wasichana jijini Dar, wakifuatilia kwa makini tamasha hilo.IMG-20151010-WA0010Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ akimpandisha stejini msanii chipukizi wa bongo fleva, Rubby jukwaani hapo.
IMG-20151010-WA0013 Rubby akifanya yake jukwaani.IMG-20151010-WA0014 Mbunifu wa mavazi, Martin kadinda akitoa neno kwa wanafunzi waliojumuika na wenzao wa Sekondari ya Jangwani kwenye tamasha la Jokate.IMG-20151010-WA0015 Kadinda na Jokate wakiteta jambo.IMG-20151010-WA0016IMG-20151010-WA0017 Mwanadada mkali wa wimbo wa Nimempata, Pamera Daffa ‘Pam D’ akitoa burudani wakati wa tamasha hilo.IMG-20151010-WA0020 Jokate akitoa neno kwa washiriki wa tamasha hilo (hawapo pichani).IMG-20151010-WA0021
Mo Music akifanya yake jukwaani wakati watamasha hilo.
MWANAMITINDO maarufu nchini na mmiliki wa kampuni ya Kidoti Foundation, Jokate Mwegelo maarufu kwa jina la Kidoti amefanya tamasha kubwa katika shule ya sekondari Jangwani, jijini Dar es Salaam, tamasha ambalo limehudhuriwa na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam ikiwemo Jangwani, Azania, Makongo na nyingine.
Lengo kuu la tamasha hilo ilikuwa ni kuhamasisha wanafunzi katika vipaji mbalimbali ambapo walipewa fursa ya kuonesha vipaji vyao kwa kufanya shoo ya kuimba, kucheza na michezo mbalimbali na kuonesha mitindo.
Wasanii waliotumbuiza kwenye tmasha hilo ni Ally Kiba, Niki wa Pili, Pamera Daffa ‘Pam D’, Mo Music na Ruby.
Mbunifu wa mavazi, Martin Kadinda alipata fursa ya kuwazawadia wanafunzi walioweza kuonesha vipaji vyao, kiasi cha Tsh. 50,000/= kila mmoja kwa niaba yaw engine.
Pesa zilizopatikana kutokana na kiingilio kwenye ntamasha hilo zitaingizwa kwenye mfuko wa Kidoti Foundation kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wasichana wanaosoma katika mazingira magumu sehemu mbalimbali nchini.
PICHA NA MAYASA MARIWATA/GPL

Diamond Platnumz,Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee wang’ara kwenye tuzo za AFRIMMA,orodha ya washindi iko hapa

$
0
0
Tuzo za mwaka 2015 za African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) zimefanyika Dallas, Texas nchini Marekani
Diamond Platnumz ndio msanii aliyeshinda tuzo nyingi zaidi,kashinda tatu, rapa kutoka Africa kusini alifata kwa kushinda mbili.
Hii ni orodha ya washindi.
Best Male (South Africa) – AKA
Best Male (East Africa) – Diamond Platnumz
Best Male (Central Africa) – Yuri Da Cunha
Best Male (West Africa) – Davido
Best Female (East Africa) – Vanessa Mdee
Best Female (West Africa) – Yemi Alade
AFRIMMA Inspirational Song – Bracket feat. Tiwa Savage and Diamond Platnumz for ‘Alive’
Best DJ (US) – DJ Simplesimon
Best Newcomer – Ommy Dimpoz
Best Collaboration – AKA feat. Da Les and Burna Boy for ‘All Eyes on Me’
Best Dance Video – Diamond Platnumz for ‘Nana’
Best Video – Wizkid for ‘Ojuelegba’
Artist of the Year – Diamond Platnumz
Legendary Award – Yossou N’Dou

Roberto & PatoranKing-Amarula Remix

Video mpya ya Kcee Ft Uhuru na Dj Buckz ‘Talk & Do’

$
0
0
Five Star Music award winning artist collaborates with South African hit makers Uhuru on the high banging tune Talk & Do. Enjoy

Mh.Lowassa aahidi kuboresha miundombinu ya maji afya na elimu Musoma

$
0
0

Mji wa Musoma na viunga vyake vyote umelazimika kusimama kwa muda kupisha mkutanop mkubwa wa kampeni nuliokuwa ukiongozwa na mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Mh.Edwrad Lowassa,
Hatimaye ameivunja rekodi mjini Musoma.
Ilikuwa ni siku iliyoulazimu mji huu wa Musoma kusitisha kudhughuli zake huku barabara zikipigwa deki kwa ajili ya Edwrad Lowassa.
 
Katika siku yake ya pili ya kampeni akitumia chopa alimehutubia mikutano mikubwa sita tofauti iliyohudhuliwa na idadi kubwa zaidi wananchi huku akiahidi kuboresha miundombinu ya maji, afya, elimu, kuukarabati uwanja wa ndege wa mji huo, ikiwa ni pamoja na kufufua matumani ya ujenzi wa chuo kikuu ndani ya mji wa Musoma.
 
Fredrick Sumaye waziri mkuu mstaafu licha ya kutoa ya kutosha ya namna watanzania wanavyoweza kumpa ushindi Edward Lowassa, amesema siri kubwa ya maendeleo ya Tanzania ni kukinyofoa madarakani chama cha CCM.





BSS 2015: Kilichoficwa nyuma ya pazia chafichuka, Mshindi aibua gumzo

$
0
0

Musa Mateja na Imelda Mtema
MASHINDANO ya Bongo Star Search (BSS) 2015, wikiendi iliyopita yalifikia tamati huku historia ya kwanza ikiwekwa na kijana mwenye umri wa miaka 19 tu, Kayumba Juma aliyeibuka kidedea kwa kuwatupa wenzake 6 waliofaulu kuingia fainali na licha ya shughuli hiyo kumalizika salama, lakini kilichojificha nyuma ya pazia kimefichuka.
Fainali hizo zilifanyika Oktoba 9, mwaka huu kwenye Ukumbi wa King Solomon uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar huku zikishuhudiwa na maelfu ya wakazi wa jiji, burudani zilikuwa kibao siku hiyo ambapo zilianza saa 3: 30 usiku zikifunguliwa na mkali wa miondoko ya R&B, Bongo, Bernard Paul ‘Ben Pol’.
WASHIRIKI WAANZA
Baada ya Ben Pol kufungua ukurasa huo, kete ya kwanza kwa washiriki ilianza kwa kumdondokea mshiriki kutoka Mwanza, Angel Mary Kato aliyeonesha manjonjo yake akimpisha Kayumba Juma ambaye aliingia na Wimbo wa Christian Bella huku akipata shangwe nyingi kutoka kwa mashabiki waliomtunza fedha.
Baadaye, Nasibu Fonabo akichukua nafasi ya tatu kwa kufungua jukwaa hilo, tena akitumia gitaa huku Kelvin Geryson akiingia kwa makeke mengi na kumpisha Frida Amani ambaye alikuwa mshiriki kutoka Kaskazini.
Jackline Kakengi kutoka Bukoba alitoka na kuacha washiriki wenzake wakisonga mbele na kuunda Tano Bora.
LAKINI SASA
Hata hivyo, ukiachana na ushindi huo wa Kayumba, kuna mambo ambayo yalizua gumzo ukumbini hapo ambapo u-team wa majaji. Wasanii waligawanywa katika makundi ya Madam Ritha, Salama Jabir na Master J na kuonekana wazi hasa pale mshiriki wa jaji mmojawapo alipokuwa akipongezwa tofauti na ilivyokuwa kwa yule ambaye si wa timu yake, jambo lililolalamikiwa na mashabiki.
Mashabiki wengi walisema, siku ya fainali, majaji hao ‘wanaojua kusema’ wangekuwa kimya kama inavyokuwa kwenye shindano la Miss Tanzania.
MFANO NI SALAMA
Katika kipengele hicho cha u-team, jaji Salama Jabir alionesha mapenzi yake waziwazi kwa Kayumba baada ya kumsifia kutokana na kupafomu Wimbo wa Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ katika raundi ya mwisho.
Salama alisema: “Bwana wee gitaa kitu gani? Sisi watu wa uswahilini bwana, tuna mambo yetu na hayo mambo ya gitaa kwanza hatujayazoea, hongera Kayumba.” (akimaanisha kuwa, Nasibu Fonabo hakufanya kitu baada ya kupafomu na gitaa).
MASHABIKI WASEMA KAYUMBA ALIANDALIWA
Baada ya ushindi huo wa Kayumba, gumzo kubwa liliibuka mashabiki ukumbini hapo wakidai kuwa aliandaliwa mapema kutwaa taji hilo kwa msimu huu kwani baadhi ya kura zilionesha mapema.
“Bwana wee, yaani hapa ni kama tumeliwa. Inaonesha kuwa nyuma ya pazia Kayumba aliandaliwa toka kitambo awe mshindi kwani utaona hata majaji wenyewe, kama Salama alionesha wazi mapenzi yake kwa mshiriki huyo,” alisema mmoja wa wahudhuriaji.
KUNA UPENDELEO WA WANAUME?
Katika hatua nyingine, baadhi ya mashabiki walisema mashindano hayo yametawaliwa na uchaguzi wa wanaume tu licha ya muandaaji wake kuwa mwanamke.Walisema mpaka juzi, BSS imetimiza misimu nane huku sita ikitwaliwa na wanaume tu, jambo lililotafsiriwa kuwa huenda waandaaji wake hawazingatii usawa.
KUMBUKUMBU YA WIKIENDA
Ilibidi gazeti hili lifukue kwenye kumbukumbu zake za nyuma na kubaini kwamba, washiriki waliowahi kutwaa taji hilo tangu kuanzishwa mwaka 2006 ni Jumanne Idd (mwanaume), Pascal Casian (mwanaume), Emmanuel Msuya (mwanaume), Misoji Nkwabi (mwanamke), Walter Chilambo (mwanaume), Mariam Ramadhan (mwanamke), Haji Ramadhan (mwanaume) na sasa Kayumba Juma (mwanaume).
UKUMBI PIA WAZUA MANENO
Baadhi ya mashabiki walisema kutokana na mashindano hayo kuwa makubwa, yangefanyiwa kwenye ukumbi mkubwa zaidi kama ilivyozoeleka kuliko kupeleka sehemu ngeni.
MADAM NA GAUNI LA BEI MBAYA
Lingine lililozua gumzo ukumbini, ni Madam Ritha kuvaa gauni ambalo lilikadiriwa kuuzwa dukani kwa shilingi laki tano.
Ijumaa Wikienda lililazimika kumfuata Madam kwa lengo la kujua bei ambapo alisema alilitungua dukani kwa shilingi milioni moja na laki nane (1,800,000).

1
Mshindi wa Shindano la Bongo Star Search 2015 (BSS), Kayumba Juma (katika), akiwa ameshikilia fedha zake muda mfupi baada ya kuibuka kidedea kwenye fainali hizo zilizokuwa zikifanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa King Solomoni uliopo Namanga jijini Dar es Salaa.2Jaji Mkuu wa mashindano hayo, Madam Rita (wa pili kutoka kushoto), akimtangaza mshindi huyo.3Washiriki waliongia kwenye 6 bora ya mashindano hayo wakiwa jukwaani kabla ya mchujo huo kuanza.
4Mmoja wa Majaji wa shindano hilo (kulia), Master Jay akiingia ukumbini hapo huku akiwa ameongozana na mpenzi wake ambaye ni msanii wa Bongo fleva Shaa.
5Majaji wakiwa kwenye meza yao ya kuratibia mashindano hayo.
6Peter Msechu akiwa katika pozi kwenye Red Carpet.
7Wasnii wanaounga kundi la Navy Kenzo wakipagawisha jukwaani hapo.
8Msanii kutoka nchini Nigeria, Run Town anayetamba na kibao chake cha Gallardo, akipagawisha jukwaani hapo.
9Mmoja wa washiriki waliokuwa wakichuana jukwaani hapo, Angel Marykato akisaka milioni 50.
10Vijana wanaounda kundi la Yamoto Bendi wakitoa burudani kwenye fainali hizo.
11Msanii wa Dansi Christiani Bella akitunza na mashabiki wake wakati akitumbuiza kwenye fainali hizo.
12Bosi anayesimamia lebo ya Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akishuhudia kwa makini fainali hizo.
13Mshiriki wa Shindano hilo kutoka Arusha, Frida Amani akipagawisha jukwaani hapo kuwania kitita cha shilingi milioni 50.14Kala Jeremiah akikumbushia enzi zake katika mashindano hayo.
15Msanii wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ akiwa katika pozi kwenye red Carpet ya mashindano hayo.16Ben Poul akiwa katika pozi na mmoja wa mashabiki zake.
17Baadhi ya washiriki waliyotolewa mapema kwenye kinyang’anyiro hicho wakihojiwa muda mfupi baada ya kuwasili ukumbini hapo.
18Msanii wa Filamu, Muna Alphonce akiwa katika ubora wake kwenye tamasha hilo.
19Kayumba akitunzwa na mashabiki wake kabla ya kutangazwa kuwa mshindi.
20Madam Rita akifuta machozi muda mfupi baada ya kumkabidhi mshindi kitita cha shilingi milioni 50.
21Madam Rita akiwa kwenye pozi.
22Mmoja ya kikundi cha kudansi kikitumbuiza jukwaani hapo.
23Mpiga picha wa Mtandao huu, Musa Mateja (kushoto), akihojiwa mara baada ya kuingia ukumbini hapo.
24Baadhi ya mashabiki waliohudhuria ukumbini hapo wakifuatilia burudani hizo kwa makini.

KIM KARDASHIAN KUKUMBWA NA KISUKARI CHA UZAZI

$
0
0

 Mwanamitindo maarufu wa Marekani, Kim Kardashian.kim11
Kim Kardashian akifanyiwa uchunguzi kwa njia ya Ultra Sound.kim2
...Akiwa na mwanaye North.
MWANAMITINDO maarufu wa Marekani, Kim Kardashian, amefichua kwamba anaweza kukumbwa na kisukari cha uzazi wakati akisubiri kujifungua mtoto wake wa pili.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34 na anayeelekea mwishoni mwa kipindi chake cha ujauzito aliyasema hayo akiwa na familia yake katika matayarisho ya msimu wa kipindi kinachorushwa na vyombo vya habari cha Keeping Up With The Kardashians.
Kipindi hicho kinatayarishwa kurushwa mwezi ujao. Kim anayetegemea kujifungua mtoto wa kiume mwezi Desemba mwaka huu, alionekana akipimwa na daktari ambaye alimwambia: “Ukishakuwa na dalili za matatizo yanayoanzisha shinikizo la damu, matatizo ya kibofu na figo (reeclampsia) utakuwa unakabiliwa na tatizo la kukumbwa na kisukari cha wakati wa uzazi. Mwanamitindo huyo alikwepa tishio hilo alipokuwa na ujauzito wa binti yake, North, ambapo alibidi apelekwe kujifungua kabla ya wakati wake.
Ugonjwa huo huwapata wanawake katika kipindi chao cha mwishoni cha ujauzito, lakini huwa unapotea mara tu wanapojifungua. Wanawake wajawazito hubidi kufuatiliwa kwa karibu viwango vya sukari mwilini mwao ambapo wengine hupewa matibabu ya kuzuia kutokea kwake.
Kitu kingine ambacho kinampa wasiwasi mke huyo wa mwanamuziki maarufu wa Marekani, Kanye West,  ni pale ambapo Kim alimwambia mama yake, Kris Jenner na dada yake,  Kourtney Kardashian, kwamba: “Madaktari waliona majimaji mengi katika kondo, hali ambayo inamaanisha ninaweza kupatwa na kisukari.” Hivi majuzi, Kim alikiri kwamba huwa hafurahii kuwa mjamzito kwani huwa hapendi jinsi mwili wake unavyopanuka na kujikuta anashindwa kuvaa nguo zake.

Mkakati wa Lowassa kuongeza Mapato...upo hapa

UKIIJADILI AKILI YA MWAMBUSI ITAKUCHANGANYA, LAKINI KUNA FAIDA NA HASARA

$
0
0

GUMZO sasa katika soka nchini ni Kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi kukubali kuchukua nafasi ya Kocha Msaidizi ndani ya Yanga timu ambazo zinacheza ligi moja!

Mwambusi sasa anakuwa msaidizi wa Kocha Hans van Der Pluijm, ambaye alikuwa kocha wa zamani wa Berekum Chelsea ya Ghana na kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi.

Kila mmoja anazungumza lake analoliamini, wengine wakitoa mifano ya Ulaya kwamba haiwezekani, jambo ambalo ni sahihi. Lakini wamesahau namna ambavyo Tanzania inavyowezekana kutokana na mambo kadhaa kama haya yafuatayo.
Maslahi:
Ndiyo, suala la maslahi ni muhimu sana ingekuwa Ulaya, Mwambusi asingekubali kweli kwenda Yanga kwa kuwa ni kocha mkuu.

Lakini hapa Tanzania, hii si mara ya kwanza na huenda likawa funzo kubwa.

Kwamba kocha msaidizi wa Yanga, ana mshahara mara mbili na ushee wa kocha wa timu nyingine mfano Mbeya City, Coastal Union au nyingine.

Mwambusi ana familia kama sisi, ana majukumu na huenda angependa kuona familia yake inaishi kwa raha zaidi.
Hivyo huo ni moja ya msukumo. Maslahi ya Yanga, pia huduma kama nyumba bora, usafiri ni kati ya mambo yaliyomvuta. Lazima tukubali naye ni mwanadamu.
Kila kitu City:
Mwambusi anajua mengi sana kuhusiana na Mbeya City. Mwenendo wa kikosi, wanakwenda wapi na nini kitafuata.

Ana uwezo wa kujua njia wanayopita na mwisho wao kutokana na hali ilivyo. Lazima tukubali ndani ya klabu hizi kuna mengi yanapita chini kwa chini yawe ni ya furaha au karaha, lakini walio ndani kama vile Mwambusi, wanajua mengi zaidi.
Ndiye aliyeipandisha daraja, akaipa nafasi ya tatu, sasa anajua msimu huu utakuwa vipi.

Kama ni hivyo, bado angeweza kubaki kweli na kuisaidia, lakini si vibaya kuondoka kama umepata nafasi ya kujifunza zaidi kwa kuwa Yanga kutakuwa na changamoto kubwa zaidi kutokana na ukubwa wa timu yenyewe ambayo pia inashiriki michuano ya kimataifa.
Ligi ya Mabingwa:
Kama nilivyoeleza mwanzo, Mwambusi anaujua undani zaidi wa Mbeya City kuliko mimi na wewe. Lazima anajua nini kinafuata na hali ikoje, pia nafasi ya kikosi chake kubeba ubingwa.

Kama hawezi, basi anahitaji nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa iliyo chini ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf). Yanga watashiriki, yeye akiwa kocha msaidizi atapata nafasi ya kujifunza mengi.

Hii itamsaidia hapo baadaye kwa Yanga, Simba au timu nyingine yoyote kumuamini kama inashiriki michuano ya kimataifa kwa kutumia rekodi zake, wakati akiwa Yanga.
Uhusiano:
Uhusiano kati ya Mwambusi na Mbeya City, tayari ulikuwa na doa. Walisigana hadi kocha huyo akajitoa katika kikosi.

Juhudi zikafanyika kumrudisha, akarejea. Pamoja na hivyo, hauwezi kujua alifanya hivyo yaani kurudi huenda kwa heshima ya baadhi ya watu au kuonyesha yameisha tu akisubiri ikifika siku, ataondoka zake.

Ana haki ya kufanya hivyo, kufanya kwake kazi ya juhudi haikuwa pekee anataka kuonekana au sura yake iwe maarufu sana. Alitaka afanikiwe kweli na maslahi au kufundisha timu kubwa kama Yanga ni sehemu ya ndoto zake.
Jikoni:
Kujiunga na Yanga kama kocha msaidizi ni sehemu ya kusogea jikoni. Siku Yanga imeamua kumwamini kocha Mzalendo, huenda Mwambusi akawa wa kwanza kwa kuwa atakuwa yuko tayari kikosini. Kwa rekodi zake za Mbeya City na Moro United, zitamsaidia kupewa nafasi hiyo na huenda akafanya vizuri zaidi.

Inashangaza wengi kuona Mwambusi akiwa kocha mkuu anayeiacha Mbeya City na kuwa kocha msaidizi Yanga.
Lakini hakuna anayeshangaa aliyekuwa kocha msaidizi Yanga, amepewa timu ya taifa na kuwaacha makocha wakuu 16 wa Ligi Kuu Bara wakiwa hawana nafasi ya kuifundisha timu ya taifa.

Kocha msaidizi, ndiye kocha mkuu pia. Maana ndiye msaidizi wa bosi mwenye nafasi ya kuwa kocha mkuu wakati wowote.

Mwambusi anaweza kuwa amekosea kwa maana ya mtazamo, lakini uamuzi wake ukawa umemtengenezea ushujaa wa baadaye na huenda wengine watakuwa wamesahau kabisa.

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi, atambulisha kampeni ya Amani kuelekea uchaguzi Mkuu

$
0
0


HOTUBA YA UFUNGUZI YA MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KATIKA MKUTANO WA TUME NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KATIKA UKUMBI WA NEW AFRICA HOTEL TAREHE

12/10/2015.


Viongozi wa Vyama vya Siasa, Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa Ya Uchaguzi, Waheshimiwa Makamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Inspekta Jenerali wa Polisi, Msajili wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa Serikali, Watendaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Demokrasia (DEP), Watendaji wa Tume, Waandishi wa Habari, Mabibi na Mabwana.

Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisheni wote katika Mkutano huu wa kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya Uchaguzi pia kupeana taarifa kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015. Pamoja na kwamba mna majukumu mengi na ya muhimu mmetambua umuhimu wa mkutano wetu na mmekuja kuhudhuria mkutano huu kama ilivyotarajiwa. Tume imefarijika sana kukutana nanyi siku ya leo na tunawashukuru kwa moyo mliyoonyesha katika mchakato huu wa maandalizi ya Uchaguzi na wa kututhamini na kuja kuhudhuria Mkutano wetu.

Viongozi wa Vyama vya Siasa,Pamoja na changamoto mbalimbali mnazokabiliana nazo katika kutekeleza majukumu yenu kisiasa ni ukweli ulio dhahiri, kuwa Viongozi wa Vyama vya Siasa ni Wadau muhimu wa Uchaguzi ambapo mkishirikiana kutekeleza majukumu yenu kwa ufasaha mtaleta mafanikio katika uendeshaji wa Uchaguzi.Viongozi wa Vyama vya Siasa,Vyama vya Siasa vina nafasi kubwa katika kuelimisha na kuhamasisha jamii, Tume inaamini kwamba ili Mpiga Kura aweze kufanya maamuzi sahihi ni muhimu kwake kupate Elimu sahihi. hivyo basi, Tume inatarajia kuona mkitumia majukwaa yenu vyema katika kuhamasishaji na kuelimishaji si tu wanachama wenu bali jamii nzima ya watanzaniaViongozi wa Vyama Vya SiasaKuelekea Uchaguzi Mkuu, Tume imeaandaa vituo vya kupigia kura 64,736, ambapo, Tanzania Bara ni Vituo 63, 156 na Zanzibar ni Vituo 1,580.

Kila kituo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia Wapiga Kura 450 na wasiozidi 500. Hata hivyo Kituo kinapokuwa na wapiga Kura zaidi ya 500 kinabidi kigawanywe ili viwe viwili yaani Kituo “A” na Kituo “B” na namba ya Wapiga Kura itakuwa nusu kwa nusu.

Wapiga Kura wanashauriwa kwenda katika vituo walivyojiandikishia kupiga kura siku nane (8) kabla ya siku ya kupiga kura ili kuweza kujua Vituo vyao halisi vya kupigia kura. Sambamba na hilo wananchi wataweza kupata taarifa zao zilizoko kwenye kanzidata (Database) kwa kutumia simu zao za kiganjani kupitia ujumbe mfupi wa maneno ‘sms’ bila wao kulazimika kufika vituoni, namba hiyo ni *152*00# na kufuata maelekezo. Au kupitia Tovuti ya Tume ambayo ni (www.nec.go.tz) Viongozi wa Vyama Vya Siasa,Tume imekuwa ikifuatilia kampeni za Vyama vyenu vya Siasa, hata hivyo Tume inasikitika kuona kuwa baadhi ya Vyama vya Siasa vimekuwa vikitumia majukwaa yao vibaya. Tume kwa namna ya pekee inawaomba katika kipindi hiki kifupi kilichobaki kutumia nafasi zenu majukwaani kuelezea sera za Vyama Vyenu ili kuweza kuwasaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi baada ya kuwa na taarifa sahihi.

Viongozi wa Vyama Vya Siasa,Tume imekuwa ikisikia katika vyombo vya Habari malalamiko mengi kuhusu uvunjifu wa maadili ya Uchaguzi katika kipindi hiki cha kampeni, naomba nitumie nafasi hii kuwaasa viongozi wa vyama vya siasa kupeleka malalamiko yenu katika kamati za maadili na si kukimbilia katika Vyombo vya Habari kama ambavyo baadhi ya Vyama vya Siasa na Wagombea mmekuwa mkifanya.Viongozi wa Vyama Vya SiasaTume inawaomba kuepuka kutoa taarifa na shutuma sisizo sahihi kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi badala yake mjikite katika kufikisha taarifa zilizo sahihi na zilizokusudiwa kwa Wafuasi wenu na wananchi wote kwa jumla, na pia kuwahamasisha wananchi kujitokeza kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba 2015.Viongozi wa Vyama Vya Siasa,Tume imejipanga kuhakikisha kila Mpiga kura mwenye sifa za Kupiga Kura anapiga Kura yake pasipo kubughudhiwa.

Ili kuhakikisha jambo hili linafanyika kwa ufanisi, Tume imetoa maelekezo kwa Makarani waongozaji vituoni kutoa upendeleo kwa watu wanaoishi na Ulemavu ili kuwasaidia waweze kupiga kura. Kwa wale wasioona Tume imeandaa kifaa maalumu cha nukta nundu ‘Tactile Ballot Folder’ ambayo itawasaidia katika upigaji kura kwa urahisi. Viongozi wa Vyama Vya SiasaBaadhi ya wagombea wamekuwa wakiwashawawishi Wapiga Kura wao kutoondoka katika Vituo vya Kupigia Kura baada ya kumaliza zoezi la Upigaji Kura, naomba nichukue nafasi hii kuwakumbusha kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kinasema nanukuu“Hakuna mtu atakayefanya Mkutano siku ya kupiga kura katika au ndani ya jengo lolote ambamo upigaji kura katika Uchaguzi unaendelea, au mahali popote ndani ya eneo la mita 200 ya jengo hilo, kuvaa au kuonyesha kadi ya picha yoyote, upendeleo au nembo nyingine inayoonyesha kuunga mkono mgombea Fulani katika Uchaguzi.“ mwisho wa kunukuu.

Aidha, kifungu cha 103 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 kinasema, nanukuu:“Hakuna mtu atakayeruhusiwa, katika jengo lolote ambalo upigaji kura katika Uchaguzi unaendelea, au njia yoyote inayotumiwa na umma ndani ya umbali wa mita tatu ya mlango wowote wa kuingilia katika jengo atavaa au kuonyesha au kuonyesha kadi, upendeo au nembo yoyote inayoashiria kumuunga mkono mgombea Fulani katika Uchaguzi” mwisho wa kunukuu. Kifungu cha 5 cha Sheria ya Adhabu, Sura Na. 16 kinaeleza maana ya njia ya Umma. Nanukuu:“Public way includes any highway, market place, square, street, bridge or other way which is lawfully used by the public” Mwisho wa kunukuu.

Vifungu vya Sheria zote kwa pamoja havisemi wala kutoa fursa au nafasi kwa wananchi kukusanyika, zinapiga marufuku na kukataza uvaaji wa sare, au nembo au alama za Vyama vya Siasa siku ya kupiga kura kwa umbali kati ya mita 200 na 300.Hivyo basi ieleweke kwamba umbali huo wa mita 200 mpaka 300 sio umbali unaowaruhusu watu kukusanyika kwa kisingizio cha kulinda kura.Hivyo niwaase Wanasiasa kuzingatia Sheria na taratibu za uendeshaji wa Uchaguzi, kuepuka lugha zozote za uchochezi zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani na kuhatarisha maisha ya Watanzania.

Aidha uzoefu unaonyesha kwamba, katika Kampeni zinazoendelea, pale ambapo wafuasi wa Vyama tofauti wanapokutana uwezekano wa kutokea vurugu ni mkubwa na sehemu nyingine vurugu zimetokea na kusababisha maafa, majeruhi na uharibifu wa mali.Hivyo, endapo kila chama kitaamua kuwaelekeza wafuasi wake kubaki kwenye Vituo vya Kupigia Kura uwezekano wa kutokea vurugu ambazo zinaweza kupelekea kuwatisha, kuwabughudhi, kuwatia hofu na kuwasumbua Wapiga Kura ni mkubwa hivyo kuhujumu zoezi la Upigaji Kura,Zaidi ya hayo, maelekezo yaliyotolewa chini ya kifungu cha 126 na kifungu cha 63(2) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 63(2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura 292 na kifungu2.1 cha Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015 yanasistiza kwamba kiongozi yeyote wa Chama cha Siasa anapaswa kuheshimu na kufuata maagizo yote ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Viongozi wa Vyama Vya SiasaKwa kumalizia ninapenda tena kuwashukuru wote kwa kuhudhuria Mkutano huu na Tume inaahidi kuyachukua mawazo yenu na kuyafanyia kazi yale yaliyomo ndani ya uwezo wetu ili kuweza kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa amani na utulivu.

Baada ya kusema hayo kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, natamka kuwa Mkutano huu umefunguliwa rasmi.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

Mgombea urais wa Chadema kupitia UKAWA apokelewa kwa kishindo Mwanza

$
0
0
Jiji la kibiashara la Mwanza limejikuta likisimamisha shughuli zake zote kupisha mkutano mkubwa wa hadhara uliokuwa ukiongozwa na mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa huku zaidi ya wananchi 130 wakizimia.
Swali jepesi kabisa ambalo kwa sasa kila mtanzania anaweza kulijibu, lakini kwa jiji la Mwanza sauti imepaa zaidi.
 
Kishindo cha mgombea huyo wa nafasi ya urais Edward Lowassa ndani ya uwanja wa Furahisha kikatikisa afya za wakazi wa jiji la Mwanza kwa mujibu wa chama cha msalaba mwekundu.
 
Akiwa jiji Mwanza alikuwa na kazi rahisi zaidi ya kuomba kupigiwa kura ya ushindi wa kishindo kwakuwa anania, ari na nguvu za kuhakikisha Tanzania inapata uchumi imara huku akiwataka watanzania kujiandaa vema na Oct 25 mwaka huu.
 
Wakati tume ya uchaguzi ikiwa tayari imekwisha weka bayana idadi ya vituo vya kupigia kura, umoja wa katiba ya wananchi UKAWA umekwisha kubaini tatizo ndani ya tume hiyo na kutoa rai kwa watanzania.
 
Baada ya kutumia muda wake wa miaka 61 ndani ya tanu na CCM, kabla ya kukitosa chama chake cha CCM hivi karibuni, amemwagia sifa lukuki mgombea urais Edward Lowassa kwani ni kiongozi imara mwenye ndoto na Tanzania mpya, huku akitoa neno kwa watanzania.
.


Name:  2.jpg Views: 3823 Size:  67.8 KB
Name:  4.jpg Views: 3800 Size:  78.0 KB
Name:  1.jpg Views: 3819 Size:  80.9 KB
Name:  3.jpg Views: 3773 Size:  90.8 KB

Name:  5.jpg Views: 4043 Size:  199.1 KB


Singidani (A Story From My Heart) - 19

$
0
0



ILIPOISHIA...
“Mh! Kweli hapa nimepata mke,” akajisemea moyoni mwake Chris.
SASA ENDELEA...
HISIA za kuwa ndani ya ndoa zilimvamia Chris kwa kasi sana, ni kweli alikuwa anakimbia kuoa muda mrefu kwa sababu hakupata mwanamke ambaye amempenda kwa dhati ya moyo wake, lakini safari hii alikiri kuwa kweli Laura alikidhi vigezo vyote.
“Kama sijawahi kukuambia, naomba nikuambie leo kutoka moyoni mwangu, nakupenda sana Laura,” akasema Chris.
Laura akacheka sana!
“Mbona unacheka?”
“Ni mara ngapi baby umeniambia kuwa unanipenda? Mara nyingi tu... hata jana usiku uliniambia neno hilo.”
“Basi kama ndivyo, naomba nibadilishe maneno, leo utambue kuwa ninasema kwa kumaanisha kuliko siku zote; nakupenda sana Laura, sijajuta kuwa na wewe na kamwe sitajuta mpenzi wangu.”
“Ahsante sana mpenzi wangu kwa maneno yako mazuri.”
Kimya kifupi kilipita, wote wakiendelea kula. Kila mmoja kichwani mwake alikuwa na mawazo yake. Laura alikuwa akiota ndoa na Chris. Kijana mtanashati kama yule, maarufu anayejulikana ndani na nje ya Tanzania kwa kazi yake ya sanaa lakini zaidi ya yote daktari!
Chris yeye alikuwa akifikiria zaidi kuhusu baba yake, ni kweli amempenda sana Laura, lakini maelekezo ya baba yake ilikuwa lazima mkewe atokee kijijini kwao. Tayari alimshamdanganya kuwa mchumba amepatikana kijijini.
“Itakuwaje? Mbona naanza kuona dalili mbaya za kumkosa Laura?” akawaza Chris.
“Lakini nitajua cha kufanya, hawezi kunisumbua. Kichwa changu kinafanya kazi sawasawa,” akajiliwaza kwa maneno hayo.
Ukimya huo wa mawazo ya ndani kwa ndani huku kila mmoja akiwaza lake, ulivunjwa na Laura: “Halafu dear, kuna jambo nataka kukuuliza.”
“Uliza tu mama.”
“Imekuwaje wewe daktari mzima, ukaingia kwenye mambo ya filamu?”
“Kwanza kwa nini umesema daktari mzima? Inamaana hupendi mimi kuwa msanii?”
“Sina maana hiyo mpenzi wangu. Ninavyojua mimi, wengi wanaoingia kwenye sanaa huwa hawana elimu ya kutosha lakini wewe kitaaluma uko vizuri kabisa. Kwa nini sasa ukaingia kwenye filamu?”
“Ni habari ndefu Laura lakini jambo kubwa ambalo nataka kukuambia ujue, napenda sana sanaa na siku zote ndiyo imekuwa chanzo cha ugomvi kati yangu na mzee wangu. Baba alitaka sana niwe daktari, ndiyo maana alinilazimilisha nikazanie masomo ya Sayansi.
“Alijua kunishawishi, kweli nikajikuta taratibu nimeanza kupenda masomo ya Sayansi na nikayamudu vizuri. Baada ya kumaliza kidato cha sita, mzee alinipeleka Uingereza kusomea udaktari. Nimeishi huko kwa miaka saba.
“Pamoja na hayo, bado ndani yangu kulikuwa na chembechembe za sanaa, ndiyo maana nikaamua kurudi nchini kwa lengo hilo, lakini kwa sababu kiu ya mzee ni kutaka kusikia nikiitwa daktari tena nikiwatibu watu, nikaamua kuomba kazi Hospitali ya Kinondoni.
“Mpaka sasa nafanya kazi hapo, lakini nikiendelea na sanaa kama kawaida. Bosi wangu hana tatizo na hilo, maana nilimweleza hali halisi kabla ya kuanza kazi.  Naijua vizuri taaluma yangu lakini napenda sana sanaa, vyote vinanipa fedha na ninafanya vyote kwa wakati mmoja,” alisema Chris.
“Hongera yako.”
“Ahsante.”
Walipomaliza kula, wote walitoka kwa pamoja na kuingia kwenye gari la Chris, wakaenda moja kwa moja kazini kwa Chris, akamtambulisha kwa baadhi ya wafanyakazi wenzake kisha akamruhusu aendelee na mizunguko yake mingine.
Laura hakuwa na mambo mengi sana siku hiyo, kikubwa hasa ilikuwa ni kwenda Kariakoo kufanya manunuzi ya mavazi na vitu vingine vya kwenda navyo Singida.
***
Laura alikaa Dar kwa wiki nzima akipoteza vipindi vyote kwa muda huo. Siku ya kurejea Singida ilikuwa ya huzuni sana kwake. Chris alimsindikiza mpaka kituoni, Ubungo ambapo alikuwa ameshamkatia tiketi kwenye basi la ABC.
Laura aliagana na Chris wakiwa wamekumbatiana kwa muda mrefu sana. Ilikuwa ni kama hawakuwa na mpango wa kuachiana. Mwili wa Laura ulisisimka sana, alitamani kuendelea kubaki Dar lakini haikuwezekana, alipaswa awahi masomo Singida.
Muda wa safari ulipowadia, hakuwa na jinsi – aliingia garini na kumwacha Chris akiwa anamtazama kupitia dirishani. Saa 12:00 asubuhi, gari lilianza kuondoka. Laura akampungia Chris mkono huku akitoa machozi, ni kama walikuwa wanarekodi filamu lakini ilikuwa kweli.
Waliendelea kupungiana mikono mpaka gari lilipofika mbali. Chris akaenda kwenye maegesho, akaingia kwenye gari lake, akaondoka. Ilikuwa safari ya kuelekea kazini kwake. Saa 3:00 asubuhi hiyo alikuwa na kazi ngumu sana ya kumfanyia mtu upasuaji mkubwa!
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>