Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

Hamisa Mobeto: Ndoa yangu itazinduliwa mitandaoni

$
0
0


Mwanamitindo Hamisa Hassan ‘Mobeto’ amefunguka kuwa siku atakayofunga ndoa atafanya siri na watu wataiona kwa mara ya kwanza kupitia mitandao ya kijamii.
Akizungumza hivi karibuni, Hamisa alisema kuwa ndoa yake itakuwa ya siri kwa maana atafunga na mumewe Kiislamu bila kuita watu na picha za ndoa hiyo zitazinduliwa mtandaoni.
“Watu wakishaziona picha hizo kupitia mitandao ya kijamii ndiyo nitafanya pati ya kusherehekea, nataka kwangu kiwe kitu cha tofauti kidogo,” alisema Hamisa ambaye ni mama wa mtoto mmoja.

NEC yatoa mwongozo utangazaji matokeo urais

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imetoa mwongozo ikisema kuwa matokeo ya udiwani, ubunge na urais yanayobandikwa kwenye vituo mbalimbali nchini ni ruksa kutangazwa na vyombo vya habari, lakini havina mamlaka ya kumtangaza mshindi wa nafasi yoyote.
 
Kamishna wa Nec, Prof. Amon Chaligha, alitoa mwongozo huo wakati akijibu maswali ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliotaka kujua kama vyombo vyao vitaruhusiwa kutangaza matokeo ya urais kadiri yatakavyokuwa yakipokelewa kutoka kwenye vituo mbalimbali nchini.
 
Alisema awali, matokeo ya urais yalikuwa hayabandikwi wala mawakala kusomewa, lakini sasa imeamuliwa yasomwe, yabandikwe na kila mmoja kupewa nakala kwa lengo la kuongeza uwazi.
 
“Matokeo ya vituo yanaruhusiwa kujumlishwa na kutangazwa... waandishi wa habari wanaweza kutangaza matokeo ya vituo, lakini siyo kutangaza mshindi,” alisema Profesa Chaligha na kuongeza:
 
“Tunafanya hivi ili kuondoa hisia mbaya na kuziba mianya ya kuibwa kwa kura au kubadilishwa matokeo. Tume haina matokeo yake kama inavyosemwa, bali ni yale yatokanayo na kura zinazopigwa na wananchi,” alisema.
“Tangazeni matokeo, lakini msiandike huyu ni mshindi kwa sababu hiyo si kazi yetu,” alisema.
 
Kwa mujibu wa kifungu cha 80 cha sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 na kifungu cha 81 cha sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa, sura ya 292, Nec ndiyo yenye mamlaka kisheria kujumlisha na kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais. 
 
Wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo husika ndiyo wenye mamlaka kisheria kujumlisha na kutangaza matokeo ya uchaguzi ya ubunge na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ndiyo wenye mamlaka ya kujumlisha na kutangaza matokeo ya udiwani.
 
JAJI LUBUVA ATOA NENO
Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva, alivitaka vyombo vya habari kuzingatia maadili ya kazi yao kwa kuendelea kuandika ukweli bila kuegemea upande wowote.
 
“Tunaomba mtumie kalamu zenu kuelimisha wapigakura wajitokeze kushiriki uchaguzi mkuu,” alisema.
 
Kamishna wa Nec, Jaji mstaafu John Mkwawa, pia alifafanua juu ya wapigakura ambao walirekebisha taarifa zao, lakini hadi siku ya uchaguzi majina yakakosekana katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, akisema kuwa kitakachotumika kuwaruhusu kupiga kura ni hekima na burasa ya msimamizi wa kituo baada ya kujiridhisha na kitambulisho kitakachoonyeshwa na mpigakura.
 
Mkurugenzi wa Nec, Ramadhani Kailima, alisema hadi kufikia Oktoba 15, vifaa vyote vya uchaguzi vitakuwa vimeshawasili katika majimbo yote nchini isipokuwa karatasi za kupigia kura ambazo alisema zitawasili baadaye.
CHANZO: NIPASHE

Mama Lowassa afichua atakavyokuwa 'first lady'.

$
0
0
Mke wa Edward Lowassa ambaye ni mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Regina Lowassa, amesema ana uhakika mumewe atashinda katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu kutokana na muitikio mkubwa anaoupata katika mikutano yake na pia kiu ya wazi ya wananchi katika kufanya mabadiliko.
 
Kadhalika, ametaja vipaumbele vinne alivyojiwekea katika kumshauri mumewe ili mwishowe aliongoze taifa kwa mafanikio makubwa katika kipindi chake cha kuwa madarakani.
 
Mbali na Chadema, Lowassa anawakilisha pia muungano wa vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya NLD, NCCR-Mageuzi na Chama cha Wananchi (CUF).
 
Mama Lowassa alielezea mambo hayo jijni Dar es Salaam jana katika mkutano wake na wanawake walio katika Baraza la Wanawake wa Chadema( Bawacha), Wilaya ya Kinondoni.
 
Akizungumza katika mkutano huo kuitikia shangwe zilizokuwa zikimtaja Lowassa kama rais ajaye, Mama Lowassa alisema amejawa na imani kuwa mumewe atashinda kwa sababu ameshuhudia mwenyewe muitikio wa wananchi katika mikoa mbalimbali waliyopita katika harakati za kampeni zinazoendelea nchini kote.
 
“Awali, nilikuwa ninafahamu kwamba Watanzania wengi wana matatizo. Lakini baada ya kutembea zaidi katika kila pembe ya nchi, sasa nikiri kugundua kwamba nilichokuwa nakifahamu juu ya matatizo ya Watanzania kilikuwa kidogo sana kulinganisha na ukweli uliopo... sasa nimejionea, ni matatizo makubwa na ndiyo maana wana kila sababu ya kuamua kufanya mabadiliko,” alisema Mama Lowassa.
 
ATAKAVYOKUWA 'FIRST-LADY' 
Akieleza zaidi, Mama Lowassa ambaye atakuwa 'first lady' kama mumewe atashinda na kuwa rais baada ya Oktoba 25, mwaka huu, alisema atajielekeza katika kushauri na kupigania vipaumbele vinne kwa ajili ya wanawake nchini. Alivitaja vipaumbele vyake hivyo pindi atakapokuwa mke wa rais kuwa ni katiba, elimu, afya na uchumi.
 
Akifafanua, Mama Lowassa alisema ataendeleza mapambano kuhakikisha kuwa ukombozi wa mwanamke unapatikana kwa dhati kupitia Katiba ya nchi, ambayo serikali itakayoundwa na Ukawa imeeleza wazi kuwa itaisimamia ili iandikwe upya kwa maslahi ya Watanzania.
 
Alisema yeye kama Mke wa Rais mtarajiwa, atahakikisha elimu kwa wanawake inapewa kipaumbele na kuingizwa kwenye katiba kwani huo ndiyo ufunguo wa ukombozi wa kweli.
 
Akielezea kuhusu afya, alisema ni dhamira yake pia kuona eneo hilo linaboreshwa kwani waathirika wakubwa wa huduma duni ya hospitali ni pamoja na wanawake. Alizungumzia pia umuhimu wa kuwainua wanawake kiuchumi ili hatimaye waondokane na umaskini.
 
Alisema hapendi kuona wanawake wanakuwa tegemezi na kwamba atahakikisha mara zote anamshauri Rais ili kuhakikisha wanawake nao wanajitegemea kiuchumi kwa kuhakikisha wanapata fursa za kujipatia mikopo, elimu bora na afya bora  tofauti na ilivyo sasa.
 
Aliwataka wanawake wajitokeze kwa wingi Oktoba 25 na kumpigia Lowassa kura nyingi za ndiyo ili aingie madarakani na kuleta mabadiliko kwa manufaa ya taifa.
 
Alisema mabadiliko na kuijenga Tanzania mpya yanawezekana, wala si kwa kutumia gharama kubwa na nguvu kubwa isipokuwa kwa kuweka mikakati mizuri, thabiti na kuitekeleza kwa vitendo. 
 
“Ninaomba wanawake mniamini katika hili...kwa sasa siwezi kusema mengi, ila ninanawahakikishia kuwa baada ya Lowassa kuchaguliwa, nitarudi kwenu na tutapanga kwa pamoja mikakati zaidi ya kuishauri serikali ya Ukawa katika kutimiza dhamira ya kuwakomboa wanawake na Watanzania wote,” alisema.
 
Naibu Katibu Mkuu wa Bawacha, Kunti Yusuph, alisema katika vipindi vyote vya uchaguzi, wanawake wamekuwa wakirubuniwa na chama tawala kwa vizawadi vidogo kama khanga na kisha kutelekezwa baada ya uchaguzi, lakini sasa hawapaswi kukubali hali hiyo bali washiriki kwa dhati ya kuleta mabadiliko ya kweli kupitia Ukawa.
 
CHANZO: NIPASHE

MBEYA CITY, MSITAKE KULIFANYA SUALA LA NYOSSO KAMA SEHEMU YA UTANI

$
0
0
Na Saleh Ally
SAKATA la beki Said Juma Nyosso limekuwa maarufu hata kuliko matokeo ya mechi ya watani, Simba na Yanga iliyochezwa jijini Dar es Salaam, Jumamosi.

Nyosso alimtomasa makalio nahodha wa Azam FC, John Bocco, baada ya kuwa wamejibizana na Bocco akarusha mguu kumpiga teke, alipomkosa, Nyosso akatumia mwanya huo kufanya alichotaka.
Tayari Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza adhabu ambayo hakika ni kali, maana miaka miwili bila kucheza soka na faini ya Sh milioni mbili, si adhabu ndogo.
Wapo ambao wanaona adhabu hiyo inatosha, wapo wanaoona ni ndogo, wanataka Nyosso afungiwe maisha lakini wapo pia wanaoona Nyosso ameonewa, wanataka ipunguzwe. Maoni, kila mtu ana yake, kikubwa ni kuangalia kanuni.
Watu wengi wameonekana kuchukizwa na tukio hilo maradufu kwa kuwa Nyosso amerudia. Aliwahi kufanya hivyo kwa Elius Maguli, mwanzoni mwa mwaka huu, nakumbuka ilikuwa Januari.
Mwisho akaomba radhi, akasisitiza kwamba ameidhalilisha familia yake, ya Maguli, pia ya Mbeya City. Hata mwaka haujapita, karudia tena baada ya kuwa amekumbana na adhabu ya kufungiwa mechi nane.
Mjadala ni mpana, lakini jana nimeona viongozi wa Mbeya City pamoja na Kocha Juma Mwambusi kila mmoja akitoa maoni yake wakati akilizungumzia suala hilo.
Wamezungumzia suala la kuunda kamati, suala la kusubiri mkanda wa video kwamba kama Nyosso atakuwa amefanya watamchukulia hatua, kama hakufanya watakata rufaa.
Mwambusi amekaririwa akisema ameuona mkanda wa video Nyosso hajafanya lolote! Nyosso mwenyewe, amesema hakumbuki kumfanyia hivyo Bocco na watu wanamhukumu kutokana na mazoea. Maana yake alichokifanya huko nyuma!
Hakika inashangaza sana, kila mmoja anajua namna Nyosso alivyo muhimu sana katika kikosi cha Mbeya City. kwa alichokifanya si suala la kujaribu kukwepesha au kutaka kuonyesha mnamjali kwa kutaka kupotosha mambo.
Suala la kusema TFF wamekurupuka, hoja nyingine zimezuka mbona fulani hakuadhibiwa, sawa. Kuna haki ya kuhoji, lakini adhabu aliyopewa Nyosso ni sahihi iwe fundisho hasa kwa wale wanaotenda maovu, wanaidanganya jamii kwa kuomba radhi halafu wanafanya tena. Haya ni maovu kujumlisha dharau.
Kumtetea Nyosso kweli ni haki ya viongozi wa Mbeya City, lakini si wakati huu na mnapaswa kuwa makini sana kuingiza vichekesho (comedy) katika suala hili. Acheni watu wa mtaani wataniane halafu nyie fanyeni kazi kuhakikisha mnalikomesha kabisa.
Video zipo lundo, hazidanganyi, hazifichi na hakuna haja ya kulazimisha eti Nyosso anaonewa. Eti kuna watu walitengeneza picha ili Nyosso aadhibiwe, vichekesho vya namna hii ni propaganda za kisiasa ndani ya mchezo wa soka.
Mwacheni Nyosso atumikie au apate anachostahili kutokana na upuuzi aliouanzisha kwa mikono yake mwenyewe. Mbeya City itakuwa haina cha kulaumiwa kama itatenda haki kwa kuwa viongozi wakumbuke, siku nyingine atatendwa mchezaji wao, halafu watashindwa hata kuinua midomo kulalamika kwa kuwa leo wanaingia kwenye njia ya kusifia maovu.
Hakuna haja ya kuzungusha, Nyosso amefanya ujinga na ameharibu heshima ya Mbeya City ambayo sasa bado ni changa sana. Huu ndiyo msimu wa tatu Ligi Kuu Bara. Lazima viongozi wanaonyesha timu hiyo ni ya Wanambeya, inahudumiwa na fedha za wananchi pia wadhamini.
Hawa wote wanapaswa kuombwa radhi, wanapaswa kuona haki inatendeka na suala la nidhamu ndiyo msingi linapewa kipaumbele.
Ninaamini viongozi wa Mbeya City hawatakubali kuuingia mkenge wa kuwa watetezi wa Nyosso kwa maana ya kwamba hakufanya lolote. Kama wana hoja ya ziada, wanaweza kuiinua lakini sasa, kilicho mezani ni Nyosso amefanya ujinga, tena akiwa na kitambaa cha unahodha cha Mbeya City.
Hii ni mara ya pili ndani ya mwaka mmoja, adhabu haikwepeki kama kweli klabu inataka kuwaonyesha watu inaamini nidhamu ndiyo msingi wa mafanikio.

Lowassa ataja vipaumbe vyake 13 ndani ya siku 100

$
0
0
Mgombea urais aliyesimamishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chadema, Edward Lowassa, ametaja vipaumbele vyake 13 ambavyo atavitekeleza ndani ya siku 100 akichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania Oktoba 25, mwaka huu.
 
Lowassa alitaja vipaumbele hivyo wakati akizungumza katika mikutano mbalimbali ya kampeni jijini Dar es Salaam jana.
 
Alivitaja vipaumbele atakavyovitekeleza ndani ya siku 100 kuwa ni, upatikanaji wa dawa na vifaa vya uzazi kwa kina mama, umeme wa uhakika nchi nzima, kupunguza foleni jijini Dar es Salaam, kuondoa kero kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na bodaboda na kutengeneza mkakati wa kumaliza tatizo la maji nchini ikiwamo Dar es Salaam.
 
Vingine ni kutengeneza mfumo bora na rafiki wa wafanyabiashara wakubwa na wadogo, kufuta ada na michango kwa wanafunzi, kupunguza kodi ya mshahara kwa wafanyakazi, kufuta kodi zote za mazao ya wakulima, mkakati kabambe wa kukuza michezo na sanaa, kuunda tume ya kutatua migogoro ya wafugaji na wakulima, kuanzisha kituo kila wilaya kwa ajili ya kutoa huduma za serikali na kuboresha maslahi ya polisi, wanajeshi na walimu.
 
Aidha, Lowassa alisema akichaguliwa kuingia Ikulu, kuanzia Januari, mwakani hakuna Mtanzania atakayelipa ada ya shule wala mchango wa aina yoyote.
 
Alisema zipo fedha nyingi na za kutosha kwa ajili ya kuwasomesha Watanzania bure na kwamba akiingia Ikulu pia atafuta utaratibu wa serikali kununua magari ya kifahari ili fedha hizo zitumike kuboresha elimu nchini.
 
Kuhusu kuondoa umaskini, Lowassa alisema anauchukia, hivyo atahakikisha anauondoa na kuwataka vijana kuhakikisha wanampigia kura ili kumuingiza ikulu Oktoba 25, mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE

M/kiti wa Tume ya Uchaguzi, shemeji yake Lowassa

$
0
0
Mwenyekiti wa Nec, Jaji mstaafu Damian Lubuva
Na Waandishi Wetu
Wakati Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) chini ya Mwenyekiti Mwenza, Freeman Mbowe wakilalamikia uteuzi wa makamishna wapya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nao wamelalamika kuwa Mwenyekiti wa Nec, Jaji mstaafu Damian Lubuva ni shemeji wa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa.
mama reginaMke wa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa, mama Regina Lowassa.
Hali hiyo imezua sintofahamu baina ya vyama hivyo viwili vinavyoonekana kuwa vikuu katika kampeni za urais za mwaka huu ambazo zimebakiza siku 23 tu kabla ya Watanzania kupiga kura kumchagua rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Chanzo chetu makini kimelieleza gazeti hili hivi karibuni kuwa Jaji Lubuva ni shemeji wa Lowassa kwa sababu mkewe Regina, ni motto wa damu wa ndugu yake na mwenyekiti huyo wa Nec.
lowassa na mkewe
Lowassa akiambatana na mkewe.
“Hawa ni ndugu na tuna wasiwasi kwamba anaweza kuweka undugu mbele na kusababisha CCM kukosa ushindi, hili ni jambo linalowezekana,” kilisema chanzo ndani ya CCM.
Wakati chanzo chetu ndani ya makada wa CCM kikidai hivyo, Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila alipohojiwa juzi kama anafahamu kuhusu uhusiano wa watu hao, alipigilia msumari na kudai kuwa anamfahamu Jaji Lubuva na kwamba Regina ni mtoto wa kaka yake, hivyo Lowassa ni mkwewe.
“Hii siyo siri na siyo dhambi, Regina na Lubuva ni mtu na mwanaye, yule ni mtoto wa kaka yake, hivyo Lowassa ni mkwe wake,” alidai Mtikila.
Wakati chanzo hicho
kikilalamikia udugu wa Jaji Lubuva na mke wa Lowassa, Ukawa wamelalamika kuwa uteuzi mpya wa makamishna wa NEC una walakini kwani Rais Jakaya Kikwete ameufanya zikiwa zimebaki siku chache kufanyika uchaguzi mkuu.
Walioteuliwa kushika nyadhifa hizo ni Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mary Longway na Wakili wa Kujitegemea, Asina A. Omari, uteuzi huo ulifanyika siku 52 tangu amteue Mkurugenzi Mpya wa NEC, Kailima Ramadhan Kobwey, Julai 25, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe alitoa tuhuma nzito akimhusisha Rais Kikwete na kile alichoita hujuma zinazoendelea ndani ya Nec.
Mbowe alimtuhumu Rais Kikwete kwa kuwaengua kwa kimizengwe watendaji wakuu wa tume hiyo na kuwapachika wanajeshi pamoja na watu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuwa watendaji wakuu.
Alidai kuwa ndani ya miezi miwili iliyopita, Rais Kikwete amevuruga utendaji wa tume hiyo kwa kupachika watu wa kuilinda CCM na wizi wa kura.
“Kwa maana hiyo, Chadema
na Ukawa hawatathubutu kukubaliana na mizengwe yoyote ile itakayotokea kipindi cha uchaguzi na hatutakubali matokeo yanayotia shaka ya aina yoyote ile,” alisema Mbowe hivi karibuni.
Katika mahojiano na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kikao baina ya NEC na wahariri wa vyombo vya habari, Jaji mstaafu Damian Lubuva alisema kwamba yeye na Regina Lowassa wanatoka sehemu moja, Kondoa mkoani Dodoma lakini akashindwa kukubali wala kukanusha kuhusu taarifa hizo kwamba wana undugu.
Hata hivyo, alisema hata kama wangekuwa na nasaba, kamwe undugu wao hauwezi kumshawishi akakiuka sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi ili ampendelee Lowassa.
“Wote tunatoka Kondoa lakini nataka niwaambie hawa wanasiasa wenye hofu kwamba hata angekuwa ndugu yangu, kamwe siwezi kupindisha sheria ili nimpendelee mumewe… Tume hii ni huru, kwanza inawezekana vipi niwashawishi makamishna wote hawa eti wafanye upendeleo kwa ajili ya ndugu yangu? Kwa faida ya nani?” alihoji Jaji Lubuva.
Jaji Lubuva alionya kwamba, tuhuma kama hizo ni mbaya katika kipindi hiki cha uchaguzi kwa kuwa zinaweza kujenga chuki kwa jamii kwa kuwa hata kama hazina ukweli, baadhi ya wananchi wanaweza kuziamini, jambo ambalo ni la hatari.
Alisema uchaguzi unaofanyika ni wa Watanzania wote na hauwezi kuharibiwa kwa namna yoyote, ama kwa shinikizo la udugu.
Akizungumza wakati wa mkutano baina ya NEC na wahariri kuhusu tuhuma zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kwamba tume hiyo imejaa maofisa Usalama wa Taifa walioteuliwa hivi karibuni na Rais Kikwete maalum kwa kuchakachua matokeo, Jaji Lubuva alisema tuhuma hizo hazina msingi na ni za kupuuzwa kwa sababu uteuzi uliofanywa ni wa kawaida na hauhusishi agenda zozote kama wanavyodai wapinzani.
Jaji Lubuva alisema, Rais Kikwete alifanya mabadiliko ya kawaida ikiwemo kujaza baadhi ya nafasi kwenye tume, huku akimtaja aliyekuwa Mkurugenzi wa Tume, Jaji Julius Benedicto Mallaba, kwamba uteuzi wake kama Jaji wa Mahakama Kuu ulikuwa umefika na isingekuwa busara kuiacha nafasi hiyo ambayo hutokea mara chache.
Aliwataka wanasiasa kunadi sera zao na kama wameishiwa sera, hawalazimishwi kuendelea na kampeni, bali wasubiri Oktoba 25, wakapige kura kuliko kuchochea.
Aidha, aliwataka Watanzania wapuuze kauli zilizotolewa na wanasiasa kwamba kuna chama ambacho kimeapa kuingia madarakani hata kwa kutumia ‘goli la mkono’.
“Hakuna goli la mkono wala hakuna short-cut (njia ya mkato). Sisi hatulijui goli la mkono, lazima wanasiasa walielewe hili na wasiwapotoshe wananchi,” alionya.
Jaji huyo mstaafu alisema kwamba, taarifa zinazotolewa na wanasiasa, hasa wapinzani, kwamba kuna njama za kuiba kura ni za upotoshaji na zinaashiria kujenga chuki kwa wananchi ambao wanaweza kuamini yanayosemwa na wanasiasa hao na kuamua kususa kupiga kura.
“Wao wanadhani wanajenga, lakini wanajiharibia hata wenyewe kwa sababu wapo wananchi ambao wanaweza kuamini maneno yao na kuamua kutokwenda kupiga kura kwa kuona hakuna haja tena ikiwa kura zinaibiwa, jambo ambalo linaweza kuwaathiri hata wao wenyewe,” alisema.
Hata hivyo, amewataka wanasiasa hao wanaodai kuna wizi wa kura kwenye tume waende wakaonesha dirisha linalotumika kuibia kura na wao wataliziba kwa nondo na saruji.
CHANZO: UWAZI MIZENGWE/GPL

Yona, Mramba kwenda jela miaka 2 bila faini

$
0
0
Kutoka kushoto ni Basil Mramba,  Daniel Yona na Gray Mgonja wakiteta jambo mahakamani. (Picha na Maktaba Yetu)
MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam leo imetoa hukumu ya rufaa dhidi ya mawaziri wa zamani, Bazil Mramba na Daniel Yona waliohukumiwa kifungo cha miaka mitatu na faini ya milioni tano baada ya kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Projest Rugazia ametupilia mbali rufaa yao ila wamepunguziwa adhabu kutoka miaka mtatu hadi miwili na kwa sasa hawatalipa faini.
Mapema Agosti 5, mwaka huu mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Rugazia iliagiza pande zote mbili kuwasilisha hoja za kusikiliza rufaa hizo kwa njia ya maandishi.
Upande wa Jamhuri ulikata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumwachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja, kwamba ushahidi uliotolewa haukuthibitisha makosa dhidi ya tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.
Kadhalika, Mramba na Yona walikata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa dhidi yao ya kifungo cha miaka mitatu na faini ya milioni tano

Singidani (A Story From My Heart) - 10

$
0
0


 

MACHO ya mshangao yalimtoka. Woga ukamjaa moyoni mwake. Alibaki akiingalia ile simu bila kuipokea. Mara simu ikakatika. Hapo sasa akapata nafasi ya kuangalia simu yake vizuri.
Alikuta meseji nne, zote zilitoka kwa Laura. Alipoifungua ya kwanza tu, simu ikaanza kuita tena. Chris akazidi kuogopa. Akili yake ilimtuma kwamba, huenda aliyekuwa akipiga alikuwa ni mume wa Laura au walikuwa pamoja na alilazimishwa kufanya hivyo ili aingie mtegoni.
Hakuwa tayari!
Simu ilipokatika, mara moja akaanza kusoma ile meseji. Maneno aliyoyasoma yalimchanganya sana. Hakuamini alichokiona. Meseji ile iliandikwa: “Kwa muda mfupi sana umeuteka moyo wangu, tafadhali Chris usinitese. Mbona hujanitafuta wakati tulikubaliana tukutane klabu?”
Inawezekana vipi mwanamke ambaye aliambiwa ni mke wa mtu ampigie simu usiku ule tena akimwambia kuwa anatakiwa kwenda kukutana naye klabu? Jambo hilo lilimchanganya sana kichwa chake.
Akaendelea kusoma nyingine mfululizo: “Baba vipi jamani? Mbona kimya? Acha kunitesa.”
“Chris nimekuwa tayari kukukabidhi moyo wangu wote kwako, mbona sasa huonyeshi kuwa upo tayari?”
“Sikia, tayari mimi nipo klabu hapa, kama huji niambie nirudi zangu hosteli nikapumzike. Nimekuja hapa kwa ajili yako Chris.”
Meseji ya mwisho ndiyo iliyomchanganya zaidi. Anamwambia anataka kwenda hosteli? Ni hosteli gani wakati alishaambiwa kuwa ni mke wa mtu?
Kwa hakika usingizi wote ulipotea. Pamoja na yote hayo, alijua alikuwa mtegoni na kama angejibu chochote angeweza kukamatwa mara moja. Kwa mtu mkubwa kama mkuu wa kituo cha polisi, maana yake ni kwamba, kama angeamua kumfanyia chochote kwa kosa la kutembea na mke wake, angeweza!
Wazo moja la haraka likamvamia kichwani mwake; alitakiwa kuvunja kabisa line yake. Hakutakiwa kupatikana tena kwa namba ile. Hilo ndilo wazo lililomwingia kwa kasi sana. Hakutaka kufikiria sana kuhusu hilo.
Akavunja ile line na kuitupilia mbali!
“Shiiit! Tuone sasa, watanipata wapi! Kwanza mimi sijafumaniwa. Najua wakiamua kunitafuta watanipata, lakini natakiwa kuwa mjanja sana kwenye eneo hilo. Hawawezi kunikamata asilani.”
Hasira ilimjaa moyoni. Alishindwa kuelewa ni kwa nini Laura aliamua kumdanganya kuwa hajaolewa wakati alikuwa mke wa mtu, tena wa askari kabisa. Jambo hilo lilimuumiza sana.
Akajilazimisha kulala.
***
Nani asiyemjua Dk. Chris, msanii wa filamu za Kibongo? Kila kona alijulikana. Hilo lilimaanisha kuwa, kama polisi mkoani Singida wangeamua kumtafuta kwa dhati kabisa, wangemkamata mapema sana asubuhi hiyo.
Chris alilijua hilo. Mara baada ya kuamka, alikwenda moja kwa moja mapokezi na kumuomba mhudumu akamnunulie kofia ya kapero. Yule mhudumu hakuwa na maswali mengi, alichukua fedha kwa Chris kisha akaenda kununua kofia na kumpelekea.
Chris akaichukua na kuivaa baada ya kujiandaa kikamilifu. Alitoka nje ya gesti hiyo na kutembea kwa mwendo wenye tahadhari zote. Taratibu akiwa ameuficha uso wake kwa kapero, alikodi teksi na kumtaka dereva ampeleke stendi kuu ya mabasi mkoani Singida, Misuna.
Dakika tano tu zilitosha kumfikisha kituoni hapo. Alishuka na kumlipa dereva kisha akatembea hadi katika ofisi za basi la Beffe, linalofanya safari zake kutoka mjini kwenda wilayani Mkalama kupitia Iguguno na Nduguti.
“Gari linaondoka saa ngapi?” Chris akamwuliza dada aliyekuwa akimkatia tiketi.
“Saa tano kamili, kwa sababu leo tunapita hadi Meatu.”
“Sawa, nipatie tiketi lakini kuna shughuli zangu nazifanya hapa mjini, sitapandia hapa. Mtanikuta kwenye mizani huo muda.”
“Tafadhali usije kulalamika umeachwa, saa tano juu ya alama uwe pale, sisi tutakukuta hapo.”
“Haina shida dada.”
Chris akalipa kisha akaondoka zake na kwenda kuchukua teksi nyingine iliyompeleka Kibaoni, ambapo ndipo gesti iliyokuwa na begi lake na vitu vyake vingine. Gari liliingia eneo hilo na kuegesha mbele ya geti.
“Naomba ukaniitie mhudumu tafadhali,” Chris akamwomba yule dereva ambaye alitii.
Sekunde chache sana, Mwanjaa alitokea, akakutana na swali kutoka kwa Chris: “Vipi, jamaa walirudi tena jana?”
Chris alisubiria jibu la Mwanjaa akiwa mwenye wasiwasi mwingi sana. Bado hakuijua hatma yake.
Itaendelea wiki ijayo.

MBEYA CITY: TAARIFA KWA UMMA JUU YA SUALA LA JUMA NYOSO

$
0
0


Bodi ya klabu ya Mbeya City ilikutana tarehe 29.09.2015 kwa dharula kulijadili suala ambalo hivi sasa linaendelea kujadiliwa katika Umma wa wanamichezo nchini likimuhusisha mchezaji wa timu yetu Juma Said maarufu kama “Nyoso” baada ya mchezo kati ya timu yetu na Azam Fc uliochezwa tarehe 27.9.2015 katika uwanja wa chamazi.
Katika kikao hicho yafuatayo yaliamuliwa:
1. Klabu iliunda kikosi kazi kuliangalia suala zima na kikosi kazi hicho kilipewa masaa 86 na kilifanya kazi kwa adidu za rejea zifuatazo:
(a) Kupitia rejea za mchezo husika na kuangalia Mazingira na Asili ya suala zima lililojitokeza.
(b) Kupata Maelezo ya awali ya mchezaji wetu juu ya suala lenyewe.
(c) Kufanya uchambuzi wa kisayansi wa mzizi wa suala analohusishwa mchezaji kwa kushirikisha watalaam wa Ushauri Nasihi na Saikolojia kisha kuishauri Bodi.
Wakati kazi hiyo ikiendelea, Klabu ilipokea nakala ya barua ya adhabu ya mchezaji wetu Juma Said maarufu kama “Nyoso” yenye Kumb:TPLB/VPL/766/15 ya tarehe 30.09.2015.
Kwa Mukhtasari ifuatayo ni taarifa ya klabu baada ya kikosi kazi hicho kuwasilisha taarifa yake.
Klabu inapenda umma wa wanamichezo nchini ukajua kuwa inasononeka sana na matukio yoyote yenye kuupunguzia ladha mchezo wa mpira wa miguu kunakofanywa na mdau yoyote wa mchezo huo.

Mara zote klabu imekuwa ikisisitiza na kusimamia nidhamu ya wachezaji na viongozi muda wote wanapotekeleza majukumu yao.
Katika mchezo wetu wa ligi kuu namba 32 uliochezwa katika uwanja wa Chamazi tarehe 27.09.2015 inadaiwa mchezaji wetu tajwa hapo juu alifanya kitendo cha udhalilishaji dhidi ya mchezaji wa Azam Fc John Bocco.
Tarehe 29.09.2015 kamati ya masaa 72 inayoisimamia shughuli za bodi ya ligi ilikutana na kutoa uamuzi wa kumfungia mchezaji Juma Saidi Nyoso kutocheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili kwa kufuata kanuni namba 37(24) za ligi kuu toleo la 2015(Kwa mujibu wa barua TPLB/VPL/766/15 ya tarehe 30.09.2015).
Ufuatao ni uchambuzi wa adhabu iliyotolewa
1. (a) Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa bodi ya ligi ( Masaa sabini mbili) pamoja na mambo mengine inashughulikia kufanya maamuzi kwa masuala yote ambayo maamuzi yake hayakatiwi rufaa kama yalivyoainishwa katika kanuni namba 74 ya ligi kuu. Kanuni iliyotumika kutoa adhabu 37(24) si miongoni mwa kanuni ambazo hazikatiwi rufaa ni kanuni inayopaswa kutumika na kamati ya Maadili au Nidhamu ambayo kulingana na aina ya kosa linahitaji kuthibitishwa pasipo shaka na pande zote zinazohusika.
(b) Hata kama kanuni waliyoitumia ingekuwa ni sahihi lakini tafsiri ya kanuni hasa maneno AU, NA hayakutumika ipasavyo kwa kuwa walikuwa na uchaguzi wa adhabu lakini adhabu hizo haziendi pamoja kama kamati ilivyo tafsiri. Adhabu imeangalia upande mmoja wa hisia , hivyo kutoa adhabu kubwa bila kuangalia upande wa mchezaji husika. Pia Kamati imeunganisha adhabu zote kwa pamoja wakati kanuni inatoa nafasi ya adhabu moja kwa wakati mmoja.
“37(24) Mchezaji yeyote atakayepatikana na hatia ya kufanya makosa makubwa ya kimaadili au kinidhamu, au ya kibaguzi au yakidhalilishaji au yatakayotafsiriwa kuwa ni ukiukaji mkubwa wa taratibu za mchezo na ubinaadamu atatozwa faini kati ya shilingi milioni moja mpaka milioni tatu au/na kusimamishwa kushiriki michezo mitatu mpaka kumi ya klabu yake yoyote atakayoitumikia katika Ligi Kuu na mashindano mengine rasmi ya TFF  au kufungiwa kipindi cha kati ya mwaka mmoja na miwili.”
2. (a) Klabu inapata shaka juu ya maamuzi ya kamati husika kutokana na kikao kilichotoa maamuzi kiliongozwa na Mwenyekiti wa kamati hii ni Ndugu Said Mohamed ambaye pia ni Mwenyekiti wa Azam Fc. Sisi tuna amini kwamba kwa kuwa yeye ni kiongozi wa Timu ya Azam aliwajibika kujitoa kusikiliza shauri.Lakini hakujitoa na aliendelea kuongoza kikao hicho huku akijua kwamba yeye ni mjumbe mwenye maslahi na upande mmoja (AZAM FC).
(b) Mchezaji anayetuhumiwa (Juma Said Nyoso) hakupewa nafasi ya kusikilizwa na kamati kama misingi ya utendaji haki inavyohitaji (Principle of natural justice), Klabu inaona mchakato mzima wa usikilizaji wa shauri hili umeingia dosari hivyo maamuzi na adhabu iliyotolewa inakosa sifa kisheria.
3 Mazingira ya tukio lenyewe:
(a) Klabu inatilia shaka ushahidi uliotumika na kutafsiriwa na kamati kufanya uamuzi uliotolewa,kuna uwezekano mkubwa kuwa kamati iliangalia picha ya mnato(Still Picture)iliyosambaa punde baada ya mchezo huo na kuzua mjadala miongoni mwa jamii bila kuangalia mazingira mengine ya tukio hilo.
(b) Katika kipande cha picha mwendo(Video) kinachoonesha chanzo cha tukio hilo ni baada ya mchezaji wa Azam Fc mwenye jezi namba 20 iliyoandikwa Mudathir kumfanyia madhambi mchezaji wa Mbeya City mwenye jezi namba 10,hii ilikuwa faulo yake ya tatu kwa mchezaji huyohuyo bila kuonywa na mwamuzi,Juma Said Nyoso akiwa kiongozi wa wachezaji wa Mbeya City alimfuata Mwamuzi wa mchezo huo kumueleza kuwa Mudathir amekuwa akimchezea sivyo mchezaji huyo bila kuonywa,ndipo John Bocco alipofika eneo ambalo alikuwepo Mwamuzi,Juma Said Nyoso na mchezaji Mwingine wa Mbeya City Fc aliyevaa jezi namba 15 (Christian Sembuli),John Bocco alimpiga kibao usoni Christian Sembuli(Jezi 15) mbele ya muamuzi, wakati John Bocco akifanya hivyo Mudathir(Jezi 20)alizunguka mgongoni kwa John Bocco na kumvuta sehemu za siri(korodani) za Juma Said Nyoso na akarudi upande wa kulia kwa mwamuzi, wakati Mudathir (20) akifanya hivyo John Bocco alimkanyaga na kumpiga teke Juma Said Nyoso.
Klabu inaamini wanaopaswa kuathibiwa ni wachezaji wa AZam Fc John Bocco na Mudathir(20) waliotengeneza mazingira ya kuharibu taswira ya mchezo wa mpira wa miguu mbele ya macho ya watu waungwana.
Mapungufu ya Jumla ya adhabu iliyotolewa:
1. Kamati badala ya kutumia Kanuni ya 37.7(F) ambayo haikatiwi Rufaa wakaitumia Kanuni ya 37(24) ambayo inakatiwa Rufaa.
2. Kamati hawakumpa nafasi ya kujitetea mchezaji husika kwa mujibu wa kanuni ya 37(24).
3. Mwenyekiti wa kamati hii ni Ndugu Said Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa Azam Fc hakusitahili kuongoza wala kuwemo katika kikao hicho kwa kuwa alikuwa na maslahi na timu ya Azam Fc ambao ndio walio mlalamikia mchezaji Juma Said Nyoso.

Umma wa wanamichezo ujifunze nini kutokana na suala hili?
1. Mamlaka zinazosimamia mchezo wa mpira wa miguu ni vizuri sasa kutafsiri kwa upana dhana ya “udhalilishaji” katika mpira wa miguu.
Hii inatokana na namna ambavyo suala hili limeripotiwa na wadau mbalimbali wa mpira wa miguu na wanaharakati,picha za tukio hilo zilisambaa kila uchao.

Klabu inaamini kwa namna wadau walivyolijadili na kulichambua suala hili,lilimdhalilisha zaidi muhusika,kuwekwe utaratibu na chombo ambacho kipewe jukumu la kupitia mashauri na ushahidi wa matukio yanayotafsiriwa kuwa ni ya “udhalilishaji” ili kuendelea kulinda heshima za wahusika katika jamii.
Klabu imewasilisha Tff maelezo ya kutoridhishwa na adhabu aliyopewa Juma Said Nyoso.
Imetolewa na
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC

2/10/2015


Mgombea urais wa Chadema kupitia UKAWA amepata mapokezi makubwa Monduli

$
0
0

Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa ameingia mjini Monduli na kupata mapokezi makubwa huku akiahidi kuendelea kushughulikia changamoto za kimaendeleo ndani ya jimbo hilo.
Tofauti na mawazo ya wengi, akiwa monduli kazi yake ya kwanza aliyoifanya ni kumtangaza Bw Julius Kalanga kuwa mrithi wake wa kiti cha ubunge jimbo la Monduli.
Mgombea huyo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Monduli kwa kipindi cha miaka 20, amewashukuru wakazi wa jimbo hilo kwa ushirikiano waliompatia uliowezesha kupatiakana kwa maendeleo ndani ya jimbo hilo huku akiahidi kuendelea kutekeleza ahadi ambazo bado hajazikamilisha.
Edwrad Lowassa ametumia jukwaa la mto wa mbu wilayani Monduli kuwaomba watanzania kuhakikisha wanampigia kura nyingi zaidi kwani uwezo, nia na sababu ya kuwa mshindi wa kiti cha urais anao.
Fredrick Sumaye amewataka wanamonduli na watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanaunga mkono kauli mbiu ya mabadiliko kwani umasikini wa watanzania umechochewa na uongozi mbovu wa CCM kwani rasilimali nyingi za nchi zimeshindwa kuwanufaisha watanzania.
Katika siku yake ya kwanza ya kampeni kanda ya kaskazini huku akitumia usafiri wa chopa alifanikiwa kuhutubia maeneo ya, Mangora, Mburu na mto wa mbu wilayani Monduli kabla ya kuhutubia maelfa ya wakazi wa mjini Babati mkoani Manyara katika uwanja wa Kwaraa.




MABAO 500 YA CRISTIANO RONALDO, HATA WEWE YANAKUHUSU

$
0
0
Na Saleh Ally 
MSHAMBULIAJI nyota duniani, Cristiano Ronaldo, amefikisha mabao 500 aliyoyafunga akiwa na timu tatu pamoja na timu yake ya taifa.


Ronaldo amefikisha mabao 500 katika kipindi ambacho ametimiza miaka 30, jambo ambalo si dogo au si la kuliacha lipite tu.

 Hakika Ronaldo ambaye amekuwa mwanasoka bora duniani mara mbili, ana kipaji cha juu kabisa.

 Mabao hayo na mfano utaona amefikisha mabao 323 sawa na gwiji wa Real Madrid, Raul Gonzalez si jambo dogo. Sasa ana nafasi ya kuwa gwiji kwa kufunga mabao mengi zaidi.

 Tayari Ronaldo ana rekodi ya wastani wa juu zaidi katika ufungaji kwenye Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’. Ana wastani wa 1.05 ya mabao. Maana yake amefunga bao katika kila mechi kama mabao yake yatagawanywa.

 Mafanikio ya mabao 500 tangu alipofunga bao lake la kwanza akiichezea Sporting Lisbon ya Ureno Oktoba 7, 2002.
Ndani ya miaka 13, Ronaldo ameweza kufunga mabao hayo 500 tena akicheza katika timu kubwa tatu ambazo hakika zinakuwa na ushindani wa juu na wachezaji wake hupambana na upinzani wa juu kabisa.

Ameshinda kila kombe kwa ngazi ya klabu akiwa na Manchester United na Real Madrid ambazo ni moja ya timu kubwa tatu zaidi duniani.

 Wakati anatua Real Madrid, msimu wa kwanza aliweza kuweka wastani wa mabao 20 kwa msimu. Baada ya hapo akapanda kwenda hadi mabao 53, kitu ambacho si mzaha hata kidogo.
Msimu wake wa kwanza na Madrid ambao ulikuwa ule wa 2009/10, alifunga mabao 21, uliofuata wa 2010/11 akatandika kimiani mabao 50.

Msimu wa 2011/12, akafunga mabao 66, msimu wa 2012/13 akashuka kwa kufunga mabao 51, ule wa 2013/14 akafunga mabao 56 na 2014/15 akafunga mabao 66.

Angalia ushindani wa La Liga au michuano ya Ulaya, lakini huyu mtu ana uwezo wa kufunga hadi mabao 50 kwa zaidi ya misimu miwili au mitatu anafanya hivyo.

Katika hali ya kawaida unaamini kweli ni kipaji pekee? Ndiyo maana nikaamua kukumbusha kwamba mafanikio ya watu hawa hayapatikani ukiwa umelala na kufumba macho.
Lazima kujituma, lazima kujipambanua na kuamini mtafutaji hachoki. Historia ya Ronaldo inajielezea, kwa kuwa wazazi wake walikuwa ni watu wa maisha ya chini kabisa.

Baba yake alikuwa ni mtunza bustani tu huko kwao katika Kisiwa cha Madeira, Ureno. Ronaldo alionyesha anataka kufanikiwa na utaona wakati akiwa Manchester United wachezaji wengi walimshangaa kwamba anaishi vipi, kweli anaweza kula raha na maisha yake. Kwamba hakuwa akijipa nafasi ya kula maisha?

Maana alikuwa akifika mazoezini saa moja au mbili kabla ya wenzake, aliondoka mazoezini saa moja baada ya wenzake. Muda wote aliokuwa pale aliendelea kujifua zaidi.

Hata walipokwenda gym, yeye ndiye alibaki muda mwingi zaidi ya wengine. Kuna wakati hadi Kocha Sir Alex Ferguson aliwahi kumuonya kufanya hivyo, kwamba apunguze mazoezi.

Wakati anatokea Manchester United kwenda Madrid, wengi walichambua na kusema angefunikwa kabisa na Lionel Messi na kupotea. Lakini leo amebaki pekee anayechuana vikali na mshambuliaji huyo wa Barcelona mwenye kipaji cha juu kabisa.

Ronaldo si mashine, ni binadamu kama wewe lakini ameamua kuishi tofauti, ameamua kutaka kufanikiwa. Amepania kutimiza ndoto zake bila ya kusikiliza maneno mengi ya pembeni ambayo hukatisha tamaa.

Hii inakuhusu wewe mchezaji wa soka wa Tanzania katika daraja lolote, achana na woga na kusikiliza sana maneno ya watu hasa yale yanayosisitiza ‘hauwezi’.

Unaweza zaidi ya wanavyofikiri, unaweza kufika zaidi ya ulipo. Lakini usifumbe macho ukalala. Hauwezi kuwa kama Ronaldo, lakini unaweza kupata mafanikio ya juu yanayoweza kuwashangaza wengi kama Mreno huyo anavyoshangaza kwa mabao yake hayo 500.

Kwa Tanzania hata kufunga mabao 50 kwa misimu minne nayo ni shida kubwa. Bado wewe unaweza kuwa wa kwanza kama utaachana na woga, kukubali kukatishwa tamaa.

Ronaldo si mashine, ni binadamu lakini anafanikiwa. Lakini lazima ukubali kuumia zaidi na kujituma zaidi ili kufikia mafanikio.

Usiyaache mafanikio yake ya mabao 500 yapite tu kama kitu cha kukushangaza, badala yake yafanyie kazi siku nyingine yakusaidie hata katika maisha ya kawaida. Panga ndoto, iote ukipambana na mwisho ufanikiwe.
BAO LA KWANZA AKIWA….
SPORTING LISBON
Oktoba 7, 2002 vs Real Betis.
MAN UNITED
Novemba  Mosi, 2003 vs Portsmouth.
REAL MADRID
Agosti 29, 2009 vs Deportivo.
TIMU YA TAIFA URENO
Juni 12, 2004 vs Ugiriki.
MABAO:
NDANI YA BOKSI: 417
NJE YA BOKSI: 83
PENALTI: 81
ADHABU:  45
ALIFUNGAJE?
Mguu wa Kulia: 326
Mguu wa kushoto: 89
Kichwa: 83
TIMU ALIZOZIFUNGA LA LIGA:
Sevila-21, Getafe-18, Barcelona-15, Atletico Madrid-15, Malaga-14
WALIOMPA ‘ASISTI’ NYINGI:
Karim Benzema 31, Mesut Ozil 28, Angel di Maria 20, Gareth Bale 15, Ryan Giggs 16, Gonzalo Higuain 15.
SOURCE: CHAMPIONI

Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania bara, Uingereza na Hispania LEO NA KESHO

$
0
0
Najua mtu wangu wa nguvu ungependa kufahamu ratiba ya mechi za Ligi Kuu mbalimbali ambazo zitachezwa siku ya Jumamosi ya October 3 na Jumapili ya October 4. Naomba nikusogezee karibu yako ratiba ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara, Uingereza na Hispania, hii ni ratiba ya mechi za Ligi hizo zitakazochezwa  Jumamosi na Jumapili.
5
Hii ni ratiba ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara weekend hii ila zilizoandikwa kwa wino wa rangi nyekundu zimehairishwa
Hii ni ratiba ya Ligi Kuu Uingereza October 3
1
Hii ni ratiba ya Ligi Kuu Uingereza October 3 kwa saa za Afrika Mashariki
  • Crystal Palace Vs West Brom saa 14:45
  • Aston Villa Vs Stoke saa 17:00
  • Bournemouth Vs Watford saa 17:00
  • Man City Vs Newcastle saa 17:00
  • Norwich Vs Leicester saa 17:00
  • Sunderland Vs West Ham saa 17:00
  • Chelsea Vs Southampton saa 19:30
Hii ni ratiba ya mechi za Jumapili ya October 4
2
Hii ni ratiba ya mechi za Jumapili ya October 4 kwa saa za Afrika Mashariki
  • Everton Vs Liverpool saa 15:30
  • Arsenal Vs Man Utd saa 18:00
  • Swansea Vs Tottenham saa18:00
Hii ni ratiba ya Ligi Kuu Hispania ya mechi za Jumamosi ya October 3
3
Hii ni ratiba ya Ligi Kuu Hispania ya mechi za Jumamosi ya October 3 Saa za Afrika Mashariki
  • Sevilla Vs Barcelona saa 17:00
  • Granada CF Vs Deportivo de La Coruña Saa 19:15
  • Espanyol Vs Sporting de Gijón Saa 21:30
  • Las Palmas Vs Eibar Saa 23:00
  • Málaga Vs Real Sociedad Saa 23:05
Hii ni ratiba ya mechi za Jumapili ya October 4
4
Hii ni ratiba ya mechi za Jumapili ya October 4 kwa saa za Afrika Mashariki
  • Rayo Vallecano Vs Real Betis 13:00
  • Ath Bilbao Vs Valencia 17:00
  • Levante Vs Villarreal Saa 19:15
  • Atl Madrid Vs Real Madrid Saa 21:30

Wolper kufunga ndoa ya siri

$
0
0

BAADA ya kuvishwa pete na mwanaume aliyedaiwa kuwa na mume wa mtu, raia wa Kongo, mwigizaji Jacqueline Walper ‘Wolper’ amesema kamwe watu hawatajua siku atakayofunga ndoa kwani amegundua watu wengi wana husda.
Wolper alisema anaamini kuwa siyo kila mtu ana mapenzi ya dhati kwake hivyo atafunga ndoa ya kimyakimya ndipo baadaye atafanya sherehe.“Siku hizi wanga wengi watu watashtukia nimeshafunga ndoa sherehe baadaye kwa wale ndugu na marafiki maana najua siyo wote wanaopenda jambo hili litimie,” alisema Wolper.

Mjengo wa Lulu yadaiwa kigoma sokoni

$
0
0
ULE mjengo wa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambao alimzawadia mama yake Lucresia Karugila, imedaiwa umeshindikana kuuzika baada ya kutangaza kuupiga bei ya shilingi milioni hamsini.
Mjengo wa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Lulu na mama yake walifikia uamuzi wa kuupiga bei mjengo huo uliopo maeneo ya Kimara Saranga jijini Dar baada ya kuona mazingira ya eneo hilo si mazuri hususan kipindi cha mvua kutofikika kwa urahisi.
“Wamedhamiria kuipiga bei nyumba hiyo lakini wanashindwana na wateja kutokana na pesa hiyo ndefu anayoitaka wakati kiuhalisia nyumba haina hadhi.
“Isitoshe ile nyumba ndani inapasukapasuka sakafu huenda kwa sababu ilianza kujengwa siku nyingi, hivyo wateja wengi wanakwamia shilingi milioni 35 wengine milioni 40, pesa ambayo Lulu na mama’ke hawapo tayari kuipokea,” alisema mpashaji huyo.
 Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kutokana na ishu hiyo paparazi wetu alimtafuta Lulu ambaye simu yake iliita bila kupokelewa lakini mama Lulu alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo alisema:
“Hii nyumba ni yetu hata kama tukiiuza kwani kuna tatizo gani sioni kama kuna cha ajabu hapo mpaka mkae mnatufuatilia kiasi hicho, nimeshasema hayo ni mambo yetu binafsi hayawahusu sababu hamkutusaidia kujenga, nimetoka msibani bado nina majonzi sitaki kuongelea tena hayo mamboº.”

Magazeti ya Tanzania leo Octoba 3, 2015 yapo hapa

$
0
0

.
.
Kutoka Dar es Salaam Tanzania leo Jumamosi Octoba 3, 2015 tayari nimeyakusanya Magazeti yote na stori zake kubwakubwa kukusogezea hapa, headlines baada ya headlines kwenye Magazeti ya Udaku, Michezo na Hardnews, zote ziko hapa
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC01001
.
.

Penny, Siza wanaswa kimahaba

$
0
0

WATANGAZAJI wa Shindano la Bongo Star Search, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Siza Daniel wamenaswa wakioneshana mahaba hadharani kama mtu na ‘bebi’ wake.
Tukio hilo lililopigwa chabo na paparazi wetu lilijiri wikiendi iliyopita maeneo ya Kawe Beach, Dar wakati wawili hao walipokuwa wakijiandaa kurekodi kipindi cha shindano hilo ambapo walionekana kushea juisi ambayo kuna wakati Siza alimnywesha Penny huku wakati mwingine, Penny akijibu mapigo.
Wawili hao baada ya kupigwa picha na paparazi wetu na kuwauliza kama ni wapenzi, Siza alishindwa kuzungumza lolote lakini Penny alipoulizwa kama jamaa huyo ndiye mrithi wa Diamond (Nasibu Abdul), alijibu kwa kifupi:
“Jamani kusoma hujui hata picha huoni?”

Kiba,Hasheem wagongana kumuoa Jokate! Mkasa upo hapa

$
0
0
Mgongano! Mastaa katika category tofauti, Ali Saleh Kiba na Mtanzania anayecheza mpira wa kikapu nchini Marekani (NBA), Hasheem Thabit Manka, wanadaiwa kuchuana vikali kila mmoja akiwania kumuoa mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ huku mama mzazi wa mrembo huyo akitia ngumu, Risasi Jumamosi linaweza kuripoti.
TAARIFA ZA AWALI
Habari za awali, zilizovujishwa na mtoa taarifa wetu ambaye ni rafiki wa karibu na familia ya Jokate, juzi Jumatano zilieleza kwamba, kwa sasa kuna vita baridi kati ya Hasheem na Kiba kwa kila mmoja kutumia njia mbadala ili kuhakikisha anamuweka kibindoni mrembo huyo.
MPASUKO NDANI YA FAMILIA
“Lakini wakati hilo likiendelea, kuna taarifa kwamba kuna mpasuko kwenye familia ya Jojo (Kidoti). Inasemekana mama wa mrembo huyo anampa nafasi kubwa Hasheem.
“Lakini kwa upande wake, Jokate amekuwa akimnadi Kiba, jambo linalozua mpasuko mkubwa kwa familia hiyo,” kilinyetisha chanzo hicho.
Chanzo hicho kilishusha madai mazito kwamba, hivi karibuni baada ya Hasheem kusikia tetesi za kushamiri kwa penzi la Kiba na Jokate, alidaiwa kukwea pipa kutoka Marekani kisha akatua Bongo kimyakimya ambapo alifika nyumbani kwa akina Jokate, Oysterbay jijini Dar ili kujua mbivu na mbichi.
“Baada ya kuona hivyo, mama Kidoti aliitisha kikao cha dharura na kumtaka Jokate akubali kuolewa na Hasheem ili waishi maisha mazuri lakini bidada (Jokate) alilipinga vibaya na kushikilia alichokiita uhuru wa mapenzi na kwamba chaguo lake ni Kiba.
“Kiukweli hali mbaya sana kati ya Jokate na bimkubwa wake, mama anataka binti aolewe na Hasheem lakini Jokate anashikilia msimamo wa kuwa na Kiba,” kilinyetisha ‘kikulacho’ hicho.
Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
RISASI HADI KWA JOKATE
Ili kung’amua lipi ni tui na yapi ni maziwa juu ya madai hayo, mwanahabari wetu alisaga lami hadi ushuani, Oysterbay, Dar nyumbani kwa akina Jokate ambapo aliwakuta watumishi wawili ambao walimwambia mwandishi wetu kuwa Jokate na mama yake hawakuwepo, walitoka kwenda kwenye mihangaiko yao ya kila siku.
UDADISI WAANZA
Ili kupata chembechembe ya madai hayo, paparazi wetu alidodosa na kubaini kuwepo kwa sintofahamu kati ya Jokate na mama yake huku jina la Hasheem likitajwa kuwa alionekana maeneo hayo kama wiki mbili zilizopita.
JOKATE ‘BIZE’ MUDA WOTE
Baada ya kupata ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alimtafuta Jokate kupitia simu yake ya mkononi ambapo hakupokea licha ya kuita mfululizo.Hata alipotumiwa meseji kwa njia ya WhatsApp hakujibu licha ya kusomewa kila kitu.
Kwa upande wake, Kiba simu yake haikupatikana hewani huku Hasheem akielezwa amesharejea nchini Marekani.
TUMEFIKAJE HAPA?
Kabla ya kudaiwa kuwa mikononi mwa Mbongo-Fleva, Kiba, Jokate aliwahi kunasa kwenye penzi la mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akitokea kwa Hasheem ambaye ilidaiwa kwamba mrembo huyo alikufa kwake kiasi cha kutaka kujiua baada ya kuachana naye.
CHANZO:GPL

Mjengo wa Lulu yadaiwa kigoma sokoni

$
0
0

ULE mjengo wa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambao alimzawadia mama yake Lucresia Karugila, imedaiwa umeshindikana kuuzika baada ya kutangaza kuupiga bei ya shilingi milioni hamsini.
Mjengo wa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Lulu na mama yake walifikia uamuzi wa kuupiga bei mjengo huo uliopo maeneo ya Kimara Saranga jijini Dar baada ya kuona mazingira ya eneo hilo si mazuri hususan kipindi cha mvua kutofikika kwa urahisi.
“Wamedhamiria kuipiga bei nyumba hiyo lakini wanashindwana na wateja kutokana na pesa hiyo ndefu anayoitaka wakati kiuhalisia nyumba haina hadhi.
“Isitoshe ile nyumba ndani inapasukapasuka sakafu huenda kwa sababu ilianza kujengwa siku nyingi, hivyo wateja wengi wanakwamia shilingi milioni 35 wengine milioni 40, pesa ambayo Lulu na mama’ke hawapo tayari kuipokea,” alisema mpashaji huyo.
 Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kutokana na ishu hiyo paparazi wetu alimtafuta Lulu ambaye simu yake iliita bila kupokelewa lakini mama Lulu alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo alisema:
“Hii nyumba ni yetu hata kama tukiiuza kwani kuna tatizo gani sioni kama kuna cha ajabu hapo mpaka mkae mnatufuatilia kiasi hicho, nimeshasema hayo ni mambo yetu binafsi hayawahusu sababu hamkutusaidia kujenga, nimetoka msibani bado nina majonzi sitaki kuongelea tena hayo mamboº.”

BETHDEI YA DIAMOND YAFANA USIKU WA KUAMKIA LEO JIJINI DAR

$
0
0

1Diamond akikata keki na baadhi ya ndugu na marafiki zake waliojitokeza mahali hapo.2Wadau wakimmwagia maji na vinywaji mbalimbali kama ishara ya kumpongeza siku yake ya kuzaliwa.3
Shilole akionyesha furaha yake na Tudi Thomas.
4
Queen Doreen (kushoto), akiwa kwenye pozi na Halima Kimwana.
5
Diamond akigonga msosi na meneja wake Babu Tale.
6
Mkubwa Said Fella akiwa kwenye pozi na baadhi ya marafiki wa Diamond.
7
Baadhi ya wadau wakijichukulia msosi.
8
Babu Tale akimsulubu Diamond kwa kummwagia soda.
9
Diamond akiwa katika pozi na marafiki zake.
10
Baadhi ya marafiki wa Diamond wakiwa kwenye pozi.
USIKU wa kuamkia leo staa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’, alifanikisha sherehe ya kuzaliwa kwake ambayo ilifana vilivyo nyumbani kwake Tegeta Madale jijini Dar es Salaam, ambapo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali. Katika sherehe hiyo Diamond alipata fursa ya kukata keki na kunywa na baadhi ya ndugu jamaa na marafiki zake waliohudhuria mahali hapo, huku kivutio kikubwa kikibaki kuwa wingi wa vinywaji vilivyokuwepo. Habari/Picha: Musa Mateja/GPL

Daah!! Kisiwani Pemba Tayari Muda Huu Wakiwasubiri Lowassa & Seif. Hali Si Kawaida

Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>