Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

TASWIRA ZA SKYLIGHT BAND NDANI YA THAI VILLAGE

$
0
0
DSC_0012
Divas wa Skylight Band wakiongozwa na Meneja wa Bendi Aneth Kushaba AK47 (katikati) kutoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar ambapo leo pia watakuwa pale pale kwenye uwanja wao wa nyumbani. Kulia ni Digna Mbepera na kushoto ni Winfrida Richard.
DSC_0028
Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo (kulia) akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band huku akisindikizwa na Hashim Donode.
DSC_0058
Mashabiki wa Skylight Band wakiburudika na muziki muziri ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0008
Mary Lucos na Digna Mpebera wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0105
Rappa Joniko Flower akifanya yake jukwaani huku Digna Mbepera na Sony Masamba wakionyesha umahiri wao wa kusebeneka.
DSC_0081
Muziki mzuri na watu wastarabu si pengine ni Skylight Band ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar kila siku za Ijumaa kuanzia saa usiku na kuendelea.
DSC_0113
Palitapikaje.....Pata picha usiku wa leo sasa na hivi kitu cha Salary kishatoka..!! Mara moja kwa mwezi sio mbaya.
DSC_0111
DSC_0145
Winfrida Richard akifanya yake jukwaani huku akipewa sapoti na Digna Mbepera.
DSC_0155
Mheshimiwa Bundala kama kawaida yake ndani ya Vest.
DSC_0170
Kuwafundisha tuwafundishe sie halafu mtuzidi????.... Vijana wa Skylight Band wakitikisa jukwaaa.
 Mwenye mamcho haambiwi ona... Skylight Band ndio habari ya mujini 2014. SKELEWU ......SKELEWU.......!!
DSC_0178
Sam Mapenzi a.k.a Sukari ya warembo akipagawisha mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0189
Sam Mapenzi a.k.a Sukari ya warembo akililiwa asipande jukwaani na mashabiki wake.
DSC_0085
Mpiga Solo wa Skylight Band Joshua akiling'uta vilivyoo gitaa lake.
DSC_0130
Kijana mtanashati kutoka kundi la Wadananda akiwa amestarehe kwenye kiti kutegeshea mrembo wa kucheza naye mdaura hapo kati..!
DSC_0139
Mdau Gerald Kilimo akiwa na mfanyakazi mwenzake walikuja kupunguza stress za kazi na burudani ya Skylight Band.
DSC_0120
Back stage ya wasanii wa Skylight Band: Pichani juu Kulia ni Winfrida Richard na Digna Mbepera, Picha ya Chini ni Kulia ni Hashim Donode na Mary Lucos.
DSC_0123
DSC_0097
Wadau wa Skylight Band na Ukodak.
DSC_0100
Wadau na Ukodak Moment.
DSC_0206
Wadau wa Skylight Band na Msanii Hashim Donode katika picha ya ukumbusho.
DSC_0182
Mary Lucos akipata Ukodak na Mama Kisso Mundende.
DSC_0184
Mama Kisso wakipata Ukodak na Aneth Kushaba AK 47 a.k.a Mjasiriamali mpango mzima wa kupendeza kichwani unaweza kumwona yeye...!
DSC_0197
Aneth Kushaba akibadilishana mawazo na Mtangazaji wa kipindi cha Mama land Benny Kinyaiya wa Clouds fm.

WOLPER AKATAA SHOBO KWA MCHUMBA ‘AKE

$
0
0
Jacqueline Wolper amesema kuwa, ana imani kubwa na mpenzi wake wa sasa aliyemtambulisha kwa jina la G Modo akiamini atampoza machungu aliyoyapata kutoka kwa mpenzi wake wa zamani, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ huku akiwatahadharisha mashosti zake kutoleta shobo (kuwa mbali naye).
Jacqueline Wolper.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Wolper alisema anafikia hatua ya kusema hayo kwa kuwa muda mfupi aliokuwa naye amegundua ni mwanaume anayejitambua na anayeheshimu mapenzi ila akawataka mashosti zake kutomsogelea.
“Tangu niwe na huyu kijana nimekuwa ni mwenye furaha kubwa, nasahau hata yale machungu niliyopata kwa mpenzi wangu wa zamani. Lakini najua wapo wanaomtolea macho, tusitafutane ubaya, kila mtu na maisha yake,” alisema Wolper.

SIMBA SC YAIANGUSHIA KICHAPO CHA BAO 4-0 JKT OLJORO

$
0
0

Mshambuliaji wa Simba SC, Amissi Tambwe aliyetupia 'hat trick' dhidi ya JKT Oljoro.
TIMU ya Simba SC imeishushia kichapo cha bao 4-0 timu ya maafande ya JKT Oljoro siku ya jana katika mtanannge uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yamewekwa kimiani na Amissi Tambwe aliyetupia 'hat trick'wakati lingine likifungwa na Jonas Mkude.

Kwa matokeo ya siku ya jana Simba imefikisha pointi 30 baada ya kucheza michezo 15 ikiwa nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu ya Bara.

KIKOSI SIMBA KILICHOPELEKA KILIO KWA MAAFANDE WA JKT OLJORO:
Ivo Mapunda, William Lucian, Baba Ubaya, Joseph Owino, Donald Musoti, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Awadhi Juma, Amri Kiemba, Amissi Tambwe na Ramadhan Singano 'Messi'.

BARCA YAKALISHWA NA VALENCIA, MESSI NDANI

$
0
0
REKODI ya kutofungwa ya Barcelona usiku huu imekomea kwenye mechi ya 31, baada ya kufungwa mabao 3-2 na Valencia. 

Mabao ya Barca yalifungwa na Alexis dakika ya saba na Messi kwa penalti dakika ya 51, wakati mabao ya Valencia yalifungwa na Parejo dakika ya 44, Piatti dakika ya 46 na Alcacer dakika ya 58.

Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini bila shaka aliuangalia mchezo huo kabla ya timu hizo kukutana Februaryi 18 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Matokeo hayo yanatoa nafasi kwa Barca kuipisha Real Madrid kileleni, kwani inabaki na pointi zake 54 sawa na Atletico Madrid, ikiwa imecheza mechi moja zaidi. Real ina pointi 53 na imecheza mechi 21, wakati Barca 22.   





Ushindi wa kushitua: Wachezaji wa Valencia wakishangilia baada ya kupata bao la tatu kupitia kwa Alcacer dakika ya 58





Imekwisha: Lionel Messi akisikitika baada ya Barcelona kufungwa

LIBYA MABINGWA CHAN 2014, GHANA CHALI CAPE TOWN

$
0
0
TIMU ya taifa ya Libya imetwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2014  baada ya kuifunga Ghana kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya bila kufungana Jumamosi ya jana Uwanja wa Cape Town. 


Ushindi huo ni sawa na Libya kulipa kisasi kwa Ghana baada ya kufungwa kwa penalti 7-6 miaka 32 iliyopita kwenye fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
 
Kipa wa Ghana, Stephen Adams aliokoa penalti mbili za Mohamed Elgadi na Abdelsalam Omar na kufanya mikwaju mitano mitano ya awali imizike kwa sare ya 3-3. 


Ahmed El Trbi aliifungia penalti ya sita Libya kabla ya Joshua Tijani kukoa upande wa Ghana na kuamsha shamrashamra za wafalme wa Mediterranean Knights wa Libya.
 
Katika mchezo uliotangulia kusaka mshindi wa tatu, Nigeria iliifunga Zimbabwe 1-0 na kushinda Medali ya Shaba ya michuano hiyo ya tatu. 
 
Libya inakuwa bingwa wa tatu tangu kuanzishwa CHAN, michuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, wakifuata nyayo za DRC 2009 nchini Ivory Coast na Tunisia 2011 nchini Sudan.

ZAHA ALIYEONEKANA WA KAZI GANI MAN UNITED AIPA USHINDI CARDIFF CITY

$
0
0
WACHZAJI wapya wa Cardiff wameanza vizuri baada ya Wilfried Zaha na Kenwyne Jones kuiwezesha timu hiyo kushinda mabao 2-1 dhidi ya Norwich.
 Raha tupu: Kenwyne Jones (katikati) akishangilia kuifungia Cardiff City bao la pili dhidi ya Norwich City
 
Robert Snodgrass aliifungia Norwich bao la kuongoza dakika ya tano Uwanja wa Cardiff City, lakini Zaha aliyetua timu hiyo kwa mkopo kutoka Manchester United, aliyetokea benchi alimtengenezea nafasi Craig Bellamy kufunga bao la kusawazisha kipindi cha pili, na Jones akafunga la ushindi dakika kadhaa baadaye.

MAN UTD KAMA KAWAIDA YAO, WALALA 2-1 KWA STOKE CITY

$
0
0
MABAO mawili ya Charlie Adam yameipa Stoke City ushindi wa kwanza kabisa kihistoria dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Britannia.
Adam alifunga mabao hayo dakika ya 38 na 52, wakati bao pekee la United lililofungwa dakika ya 47 na Robin van Persie.
Kiungo mpya wa United, Juan Mata alicheza kwa dakika zote 90 na hakuweza kuwaepusha Mashetani hao Wekundu na kipigo. United sasa inabaki na pointi 40 baada ya kucheza mechi 24 na inaporomoka hadi nafasi ya saba kutoka ya sita.
Raha ya ushindi: Charlie Adam (katikati) akishangilia na Mark Hughes baada ya kufunga mabao mawili yaliyoifanya Stoke imalize ukame wa ushindi ndani ya mechi sita
Misery: David Moyes' team lost their eighth league match of the season and he saw both Phil Jones and Jonny Evans pick up injuries
Mikosi: Kocha David Moyes ameendelea kuwa katika wakati mgumu Man United.

JIDE AOMBA TALAKA

$
0
0
UNAWEZA ukakataa lakini ndivyo ilivyotokea, ndoa ya mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteini’ na Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ iliyofungwa miaka 9 iliyopita inadaiwa kuingia kidudu kufuatia mke huyo kuomba aandikiwe talaka.
Jide akiwa na jumewe Gardner.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Jide au Lady Jaydee alifikia uamuzi huo baada ya Gardner kupata kazi ya kutangazia redio moja nchini Kenya.
HABARI KAMILI
Mnyetishaji wa kisanga hiki, aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa mara baada ya mume huyo kupata mchongo mzima alirudi nyumbani akiwa na furaha na kumwambia mkewe kuhusu bahati hiyo.
“Baada ya Gardner kupata mchongo wote wa kazi alikwenda mbio nyumbani kwake Kimara (Dar) ili akamwambie mkewe.
“Pia katika safari ya kwenda Kenya kupiga mzigo ilikuwa aende na mkewe huyo kwa sababu lilikuwa suala la kuhamisha makazi yao Tanzania,” kilisema chanzo hicho.
 
Jide na Gardner siku ya ndoa yao.
JIDE AHAMAKI
Chanzo kikatoboa kwamba Gardner alipofika nyumbani kwake na kumweleza mkewe, alikumbana na kitu ambacho hakukitarajia.
“Komando (Jide) alihamaki na kumjia juu akisema yeye hawezi kuondoka Tanzania kwenda kuishi Kenya, kama Gardner analiona jambo hilo ni heri kwake, amuandikie talaka yake na kuachana ili kila mmoja achukue hamsini zake,” chanzo kilizidi kuporomosha maneno.
KWA NINI JIDE HAKUPENDA?
Habari zilizidi kuanikwa kwamba Jide au Binti Machozi alifikia uamuzi huo baada ya kugundua kuwa kitendo cha kwenda kuishi Kenya kitaua bendi yake ya Machozi na sehemu ya biashara ya Nyumbani Lounge iliyopo Ada-Estate, Kinondoni, Dar.
MBAYA ZAIDI
Taarifa zikazidi kumiminika kwamba, mbali na Jide au Anakonda kuhofia biashara zake kufa, lakini pia hakupenda Gardner aondoke hata peke yake kwa sababu yeye ndiye meneja wa miradi hiyo miwili.
“Mimi nilipopata habari hizo nilikutana na Jide nikamuuliza, akanijibu ameamua iwe hivyo tu, kikubwa mumewe (Gardner) aamue moja kati ya hayo mawili kwani yeye ana haki akiwa kama mkewe wa ndoa,” kilisema chanzo kikimkariri Jide.
GARDNER AISHIWA NGUVU
Kufuatia majibu ya mkewe, taarifa zinasema mtangazaji huyo ambaye alishawahi kupiga mzigo kwenye kituo cha Radio Clouds FM cha jijini Dar alijikuta akiishiwa nguvu na kuachana na dili hilo mara moja.
“Gardner alisalimu amri kwa mkewe, akaamua kuachana na dili la kwenda kutangaza Kenya. Lakini alifikiri sana akasema ni kweli kuhamia Kenya kungeua miradi yao ya Tanzania maana ingekosa msimamizi wa kuaminika,” chanzo kiliweka wazi.
KAMA ANGEKWENDA KENYA
Siri hiyo iliyovujia mikononi mwa Ijumaa Wikienda haikuishia hapo, ilizidi kuanikwa kwamba kama Kapteini angekwenda Kenya na kuanza kazi, ilikuwa alipwe mshahara wa shilingi za Kenya laki 3 kwa mwezi (kama milioni 6 za Tanzania).

NAFASI YAKE BADO IPO
Mpashaji wetu alisema kwamba nafasi ya Gardner kwenye kituo hicho cha redio ambacho hakikutajwa, bado ipo lakini tamko la Jide nalo li hai, kwa vile hakubatilisha, endapo mumewe atataka kwenda hata kesho (Jumanne) aandike talaka.

WIKIENDA NA GARDNER
Baada ya kunyetishiwa taarifa nzima, juzi gazeti hili lilimsaka Gardner. Kwa njia ya simu lilimkosa, likamfuata Nyumbani Lounge. Lilipomkuta lilimsimulia kisanga chote cha ndoa yake kutikiswa na kitendo cha yeye kupata kazi Kenya ambapo alijibu hivi:
“Ndoa ni nzuri, ni kweli ilikuwa niende Kenya, nilipata kazi kule lakini kama familia ilikuwa lazima tukae na kupanga, mwenzangu hakuafiki.”
Wikienda: “Ni kweli shemeji ameomba uchague mawili, umwandikike talaka au uende Kenya?”
Gardner: “Ndiyo maana nimesema ndoa nzuri, lazima makubaliano yawepo, mke anaweza kuonesha msimamo wake na mume kama utakaa chini na kuufikiria ukapata jibu unakubaliana na mke wako wala hakuna ubaya.”

Wikienda: “Kule mshahara wako ungekuwa shilingi ngapi?”
Gardner: “Hiyo sasa ni siri ya makubaliano.”
Wikienda: “Kwa nini usiamue kwenda tu?”
Gardner: “Nimekwambia ndoa nzuri.”

JIDE BIZE
Juhudi za kumpata Jide ziligonga mwamba baada ya muda wote kuwa bize na shoo ya kukata na shoka aliyokuwa akiifanya siku hiyo kwenye ukumbi huo akikimbiza na nyimbo zake kali za zamani na hizi mbili zilizogeuka nyimbo za taifa, Joto Hasira na Yahaya.

RAFIKI WA GADNER AMCHAMBUA JIDE
Rafiki wa karibu na Gardner (jina tunalo) ambaye alisikia mahojiano ya mtangazaji huyo na Ijumaa Wikienda, alisubiri jamaa aondoke ambapo alianza kumchambua Jide.
“Nataka kuwaambia kitu, Jide ni mwanamke jasiri sana. Ana msimamo na anaposhikilia msimamo wake hatengui hasa kama atabaini kuwa yupo sahihi.
“Ni kweli jamaa (Gardner) alipata kazi Kenya tena mshahara mzuri tu, lakini mama (Jide) akaweka ngumu hakuna kwenda,” alisema rafiki huyo.
CHANZO NI IJUMAA WIKIENDA

WEMA: NIKIFA NIAGWE UWANJA WA TAIFA

$
0
0
Kazi ipo! Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ambaye huwa haishiwi habari, ameibuka na jipya akidai kuwa akifa leo au kesho basi aagwe Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Wema Isaac Sepetu.
Miss Tanzania huyo wa 2006/07 ambaye anakimbiza kwenye sinema za Kibongo alifunguka hayo wikiendi iliyopita wakati akiwa safarini kuelekea jijini Arusha ambapo msanii anayemilikiwa na kampuni ya Wema ya Endless Fame Production aliyetajwa kwa jina moja la Mirrow alikwenda kuangusha shoo pande hizo.

Wema aliyasema hayo alipokuwa akichangia mada ya utabiri wa mtoto wa aliyekuwa mtabiri bingwa, marehemu Sheikh Yahya Hussein, Maalim Hassan Hussein aliyetabiri kwamba wasanii wengi wenye majina makubwa watakufa mwaka 2014.
Mwanadada huyo alisema mastaa wengi wameaga dunia na kuagwa kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni lakini yeye itakuwa Uwanja wa Taifa.

Alitolea mifano ya waliokuwa mastaa kama Steven Kanumba, Albert Mangweha ‘Ngwea’, Julius Nyaisangah ‘Anko J’ na wengine kuwa waliagwa Leaders lakini kwa namna ambavyo jina lake ni kubwa ndani na nje ya Bongo viwanja hivyo havitatosha.

“Mimi nakwambia kabisa, pale Leaders hapatatosha. Kama nikifa leo au kesho, niagwe Uwanja wa Taifa ili kila mtu apate nafasi. Naamini watu watakuwa wengi sana so Leaders hapatatosha,” alisema staa huyo mkubwa anayeminya kilamalavidavi na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Marafiki zake wa karibu lilitonywa kwamba tayari jambo hilo alishawaeleza na kwamba aliomba iwe hivyo.

Mbali na wasanii, Maalim Hassan alitabiri pia kuwa mwaka huu kuna mwanasiasa mkubwa atakufa na utakuwa msiba wa kitaifa, vifo vya wanahabari na malumbano makubwa juu ya serikali tatu.

Wiki iliyopita ilijaa simanzi baada ya kufariki dunia kwa watu maarufu kama mchekeshaji wa Futuhi ya Star TV, Omary Majuto ‘Mzee Dude’, mpiga ngoma wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Soud Mohamed ‘MCD’, mwigizaji wa Bongo Movies, Victor Peter na mtangazaji wa East Africa Radio, Kenneth Kidago Lyanga.

YANGA NA MBEYA CITY YAINGIZA MILIONI 175

$
0
0
MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji Yanga na Mbeya City iliyofanyika jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 175,285,000.

Watazamaji 30,411 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Yanga ndiyo iliyoibuka na ushindi wa bao 1-0. 
Mgawanyo wa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 26,738,389.83, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,919,200 wakati kila klabu ilipata sh. 42,960,086.50. Uwanja sh. 21,844,111.53, gharama za mechi sh. 13,106,466.92, Bodi ya Ligi sh. 13,106,466.92, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 6,553,233.46 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 5,096,959.36. 
Nayo mechi ya Simba na Oljoro JKT iliyochezwa Februari 1 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 47,705,000 ambapo kila timu imepata sh. 11,254,122 kutokana na watazamaji 8,267. 
Mgawanyo mwingine katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Simba kushinda mabao 4-0 ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 7,277,033.90 na gharama za kuchapa tiketi sh. 2,278,400.Uwanja sh. 5,722,434.92, gharama za mechi sh. 3,433,460.95, Bodi ya Ligi sh. 3,433,460.95, 

Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,716,730.47 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,335,234.81. 
Wakati huo huo: Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepata hati ya kiwanja chake kilichopo eneo la Mnyanjani katika Jiji la Tanga. 
Hati hiyo ya miaka 99 ya kiwanja hicho namba 75 Block D chenye ukubwa wa ekari 7.6 ilikabidhiwa kwa TFF, Januari 13 mwaka huu.Kiwanja hicho kitaendelezwa kwa matumizi mbalimbali, kubwa ikiwa ni uwanja wa mpira wa miguu. 
Katika hatua nyingine, TFF itaadhimisha miaka 50 tangu lipate uanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (TFF) kwa shughuli mbalimbili ikiwemo michezo na makongamano. 
Kamati maalumu itaundwa kwa ajili ya kupanga na kuratibu shughuli hiyo ambayo TFF imepanga kuadhimisha nchini nzima kwa kutumia wanachama wake.TFF wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) ilijiunga na FIFA Oktoba 8, 1964.

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAJENGO YA BUNGE DODOMA

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua sehemu ya kukalia katuka  Bunge jijini Dodoma alikotembea kukagua inayokarabati na kufanyiwa marekebisho  tayari tayari kwa kupokea wajumbe wa Bunge la katiba baadaye mwezi huu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali za majengo ya Bunge jijini Dodoma alikotembea kukagua inayokarabati na kufanyiwa marekebisho  tayari tayari kwa kupokea wajumbe wa Bunge la katiba baadaye mwezi huu.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi inayokarabati na kufanyia marekebisho ukumbi wa bunge mjini Dodoma tayari tayari kwa kupokea wajumbe wa Bunge la katiba baadaye mwezi huu.Picha na Ikulu

MATEMBEZI YA MSHIKAMANO YA MIAKA 37 YA CCM YAFANA MBEYA SIKU YA JANA

$
0
0






Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete akiwa na baadhi ya viongozi tayari kwa kuanza matembezi ya mshikamano




























Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi walioshiriki matembezi ya mshikamano 


Na Mbeya yetu

SIKU WEMA, KAJALA NA AUNT WALIPOTUATRIPLE A ARUSHA NA VIVAZI TATA!!

CHELSEA WAIKALISHA MAN CITY ETIHAD

$
0
0
UCHAMBUZI wa haraka ni kwamba, Chelsea imeziweka wazi mno mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England, kufuatia ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Manchester City, Uwanja wa Etihad usiku wa kuamkia leo.
Mfungaji wa bao hilo pekee Ivanovic dakika ya 32 na sasa Chelsea inatimiza pointi 53 sawa na Manchester City iliyo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi kwa wastani wake mzuri wa mabao.
Matokeo hayo yanakuwa faraja zaidi kwa Arsenal ambayo sasa inatuliza roho kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi zake 55, baada ya timu zote hizo kucheza mechi 24.
Tumewashikisha adabu: Ivanovic akishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao pekee la ushindi usiku huu
Park the bus? Not me: Mourinho looks happy with his team's effort as Manuel Pellegrini shouts orders
Kupaki basi? Siyo mimi: Mourinho akionekana mwenye furaha na matokeo ya timu yake,huku Manuel Pellegrini akifoka
Eyes wide shut: Manchester City's Edin Dzeko and Chelsea's Nemanja Matic fight for the ball
Edin Dzeko wa City na Nemanja Matic wa Chelsea
Boot it away: Petr Cech and Gary Cahill try and clear the ball before Alvaro Negredo can get to it
Kipa Petr Cech na beki wake Gary Cahill wakijaribu kuondosha mpira hatarini kabla Alvaro Negredo hajaupata
Fight for the ball: City's Martin Demichelis competes with Eden Hazard for the ball

Martin Demichelis na Eden Hazard 
Close, but not close enough: David Silva sees his effort go agonisingly wide
David Silva alipiga nje hapa
Close ball control: Hazard gets the better of both Pablo Zabaleta and Demichelis

Hazard akiwatoka Pablo Zabaleta na Demichelis
Winding runs: Hazard was a threat for Chelsea all evening
Hazard aliwasumbua mno City

BLUE MARK REAL ESTATE: YOUR DESTINATION FOR APARTMENTS NEEDS IN DAR!

$
0
0










FOR your apartments requirement in Msasani Beach (Mwalimu Nyerere area, Behind Regency Park Hotel – Dar es salaam) and Mikocheni area - off Garden Road), please contact Blue Mark:
+255 290 167 or +255 784  888982.
We have Three, Two and One Bedroom Apartments. Fully furnished, with Standby Generator, 24hr Security, Car Parking, reliable water supply and a Swimming Pool. Our rates ranges from 2000 USD to 500 USD per month.

KUMBE LOWASSA NI TISHIO CCM

$
0
0
PATASHIKA nguo kuchanika ni kauli ya kibabe inayoweza kutumika kuelezea sakata la siasa za makundi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)  linaloshika kasi huku baadhi ya wanachama wakitupiana lawama kwa kuunga mkono upande fulani kuelekea mbio za urais hapo mwakani.
 Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa hajawahi kutoa tamko lolote juu ya kugombea urais mwakani lakini shutuma kwamba anautaka zimekuwa zikiibuka kila kukicha.

Hali hiyo inatafsiriwa na wengi kuwa, Lowassa ni tishio kwani wote waliowahi kumshambulia wanaambulia kutokwa jasho huku wakijibiwa hoja zao na watu wengine.
Hivi karibuni Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Paul Makonda aliibuka na kudai Lowassa anakivuruga chama kwa kuanza mbio za urais kabla ya muda wake.
Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Paul Makonda.
Naye Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela aliunga mkono hoja ya Makonda na kumtupia lawama mwanachama mwenzake huyo kwamba amechapisha fulana zilizoandikwa ‘Friends of Lowassa’ (marafiki wa Lowassa), akadai hazina nia nzuri ndani ya chama hicho.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, Jumamosi iliyopita aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar kuwa, Makonda na mzee Malecela wawaombe radhi viongozi wa dini kwa kudai kwamba wanapokea mamilioni ya fedha kutoka kwa kiongozi huyo ambaye ni Mbunge wa Monduli.
 
Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela.
Mgeja alisema anashangaa kuona panya akimfukuza paka huku taarifa hizo zikimpa uzito Lowassa ambaye licha ya kwamba hajawahi kutoa tamko la kugombea urais mwaka 2015 lakini jina lake liko vinywani mwa wanasiasa kila kukicha.
Naye Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula wiki iliyopita alisema anafurahishwa kuona wanachama wake wakionesha ukomavu wa demokrasia ndani ya chama huku akiwataka wazingatie taratibu, kanuni na misingi waliyojiwekea.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula.
“Tunafurahi kuona wanachama wetu wakionesha ukomavu wa demokrasia ndani ya chama lakini tuzingatie misingi, kanuni  na taratibu tulizojiwekea kulinda chama chetu,” alisema Mangula.

REDIO 5 WAFUNGUA MWAKA KWA KUFANYA TAMASHA

$
0
0

DSCF2600Timu ya AJTC ikiwa katika picha ya pamoja baada ya kunyakuwa ushindi katika tamasha la fungua mwaka na redio 5 lililoandaliwa na kampuni ya Tan media jijini Arusha katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid
DSCF2553Muonekano wa wachezaji wakiwa uwanjani
DSCF2593Kulia ni meneja mbunifu wa redio 5 Vicky Mwokoyo akiwa na MC Victoria wakijadili jambo
DSCF2562Mtangazaji maarufu wa kituo cha redio 5 Semio Sonyo akijadili jambo na baadhi ya wachezaji
DSCF2552Nyama choma pia ilikuwepo
DSCF2556 
DJ akifanya yake kuwapa burudani wakazi wa Arusha
DSCF2557Mashabiki wakiangalia burudani kutoka kwa wasanii wa Arusha
DSCF2564Timu ya Highridge ikipokea zawadi ya saa kutoka kwa mtangazaji Semio Sonyo baada ya kushika nafasi ya pili
DSCF2577 
Mmiliki wa jamiiblog akishow love na kikundi cha kck spark katika tamasha la fungua mwaka na Redio 5
DSCF2569
DSCF2589
DSCF2634K-vant gin nao walikuwa wadhamini wa tamasha hilo
DSCF2629Jambo squard wakiwapa burudani wakazi wa Arusha
DSCF2584 
Kulia Mtangazaji maarufu wa redio 5 Linus Kilembu kushoto producer BR tukishow love
DSCF2587Miondoko ya archuga pia ilichezwa
DSCF2632Mashabiki wakiangalia burudani
DSCF2627
DSCF2619 
Wadau muhimu pia walikuwepo kwenye tamasha
DSCF2629

HAPPY BIRTHDAY RONALDO, NEYMAR, TEVEZ NA BROWN

$
0
0
Cristiano Ronaldo.
MASTAA wa soka duniani Cristiano Ronaldo,  Neymar da Silva, Carlos Tevez pamoja na mwanamuziki Bobby Brown leo wanasherehekea sikukuu za kuzaliwa kwao.
Cristiano Ronaldo
Mwanasoka Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro mwenye umri wa miaka 28, alizaliwa Februari 5, 1985 Santo António, Ureno. Ronaldo ni mshambuliaji wa Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno. Hivi karibuni alitwaa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia ya Ballon d'Or. Ronaldo anavaa jezi namba 7 akiwa Real Madrid na Ureno.
Neymar da Silva
Mchezaji machachari Neymar da Silva Santos ana umri wa miaka 21, alizaliwa Februari 5, 1992 huko Sao Paulo, Brazil. Neymar ni kiungo na mshambuliaji wa timu ya  FC Barcelona na timu ya taifa ya Brazil. Neymar anavaa jezi namba 11 akiwa na Barcelona na 10 akiwa na timu yake ya taifa ya Brazil.
Carlos Tevez
Mshambuliaji Carlos Alberto Martínez Tevez ana miaka 29, alizaliwa Februari 5, 1984 huko Ciudadela,  Argentina. Tevez ni mshambuliaji wa timu ya Italia, Juventus na timu ya taifa ya Argentina. Tevez aliyewahi kutamba na klabu za Manchester City, Boca Juniors, Corinthians, West Ham United and Manchester United anavaa jezi namba 10 akiwa Juventus wakati akivaa namba 32 akiwa na Argentina.
Bobby  Brown
Mwimbaji wa R&B, mtunzi wa nyimbo, rapa na dansa, Robert Barisford "Bobby" Brown ana umri wa miaka 44, alizaliwa Februari 5, 1969 huko Massachusetts, Marekani.
Brown alikuwa mume wa marehemu Whitney Houston na alianza safari yake ya muziki akiwa mmoja wa watu muhimu katika Kundi la The Bricks mwaka 1978 mpaka mwaka 1986 alipoondoka katika kundi hilo kutokana na utovu wa nidhamu.
Baada ya hapo aliamua kuwa msanii wa kujitegemea ambapo alipata mafaniko kwa albamu yake ya pili ya mwaka 1988 iitwayo Don't Be Cruel.

AJIRA: UTARATIBU WA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI WAHITIMU KIDATO CHA SITA

$
0
0
KAOHSIUNG NA JESHI LA POLISI KWA WAHITIMU WATARAJIWA WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014
Katika mwaka wa fedha 2014/2015 Jeshi la Polisi linatarajia kuajiri wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014 na kidato cha nne mwaka 2013. Ili kutekeleza azma hii tumeweka fomu kwenye tovuti ambayo wahitimu watarajiwa wa kidato cha sita wa mwaka 2014 watajaza kabla ya kufanya mitihani yao ya kumaliza kidato cha sita.

Baada ya kujazwa kikamilifu wakabidhi fomu kwa wakuu wa shule ambao watazirejeshe kwa Makamada wa Polisi wa mikoa kabla ya tarehe 17.03.2014. Wahitimu wa kidato cha nne wasijaze fomu hizi walishajaza kupitia “selform” walizojaza walipokuwa shuleni.

MASHARTI KWA MWOMBAJI:
1.Mwombaji anatakiwa ajaze fomu hii kikamilifu na abandike picha yake “Passport Size” kwenye fomu kisha akabidhi kwa Mkuu wa Shule kwa hatua zaidi.
2.Kila mwombaji aandike namba ya simu kwa usahihi na anuani yake ya kudumu ambayo itatumika wakati wa kuitwa kwenye usaili.
3.Pakua:Fomu ya Chaguo hapa...
Imetolewa na:
Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
DAR ES SALAAM.
Chanzo: Jeshi la Polisi Tanzania

BIFU LAO KWA DIAMOND...JOKATE AMWANGUKIA WEMA

$
0
0
Stori:  Imelda Mtema, Arusha
WERAWERAA! Staa wa Bongo anayesumbua kwenye mitindo na sinema, Jokate Mwegelo amekubali kushindwa baada ya kumwangukia Wema Sepetu waliyekuwa kwenye bifu la kimyakimya wakigombea penzi la Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

 Jokate akiwa sambamba na Wema.
Tukio hilo la kufungulia mwaka lilijiri wikiendi iliyopita jijini Arusha, katika kiwanja cha kulia bata, Triple A Club ambapo Wema alikuwa akimtambulisha mwanamuziki Miraji Hussein ‘Mirror’ kutoka Lebo ya Endless Fame Production.
Wema aikumbatiana na Jokate.
BONGE LA SAPRAIZI
Mwandishi wetu ambaye alikuwa katika msafara wa Wema na mashosti zake, Kajala Masanja na Aunt Ezekiel waliokuwa wakimpa kampani, hakumuona Jokate, hivyo alifika pale kwa kushtukiza.
Jokate akionekana mwenye furaha, alipanda jukwaani na kuomba kuzungumza machache ambapo alimkumbatia Wema kwa furaha huku akionekana hana kinyongo.

Jokate baada ya kupanda stejini na kumfuata Wema.
AKIRI WEMA NDIYE MKE MKUBWA
“Wema ni rafiki yangu na ninampenda kwa dhati... yaliyopita yamepita. Nipo hapa kwa ajili ya kumpa sapoti kutokana na upendo nilionao juu yake. Nakiri  yeye ni mke mkubwa. Nimeamua kumshtukiza ili aone thamani yake kwangu.”
Maneno hayo ya Jokate yalisababisha ukumbi mzima ulipuke kwa kelele za shangwe.

Jokate akianza kummwagia manoti Wema.
AMWAGA MINOTI
Kama vile haitoshi, huku shangwe zikiendelea, bidada huyo alitoa burungutu la fedha na kuanza kumtuza Wema.

Mamaa Kidoti akizidi kutoa 'misimbazi' kwa Wema.
Pia aliwatuza Kajala na Aunt ambao wote kwa pamoja walikuwa wamevaa sare kama kinogesho cha shughuli hiyo.
Wapambe wakikusanya minoti iliyomwagwa na Jokate.
JOKATE ABANWA
Risasi Mchanganyiko halikuishia kufotoa picha na kuweka gazetini pekee, lilimfuata Jokate na kumwuliza sababu ya kufanya tukio hilo ambapo alijibu kifupi: “Ni upendo tu dadangu.”

Minoti iliyotapakaa stejini ikizidi kukusanywa.
Alipobanwa zaidi alisema: “Mimi niliona nikifika kumpa kampani mwenzangu itapendeza sana na sikutaka ajue mapema ili ujio wangu umshangaze. Nimefurahi imekuwa hivyo.”
Jokate akiendelea kuonyesha jeuri ya fedha kwa kumtunza shosti wake Wema.
WEMA SASA!
“Yaani nimefurahi sana kuona Jokate anajua kuwa mimi ni mke mkubwa na ndiyo kila kitu,  nimefurahi kuacha kazi zote kuja kuungana nami, kitu ambacho nimekiona tofauti kwani hatukuwahi kukaa hivyo na Jokate tangu tulivyoingia kwenye mgogoro (wa kumgombea Diamond),” alisema Wema.

Ilikuwa 'misimbazi' tupu!
WEMA / JOKATE
Upinzani wa Wema na Jokate ulianza kitambo kwani mwaka 2006, Wema ndiye aliyeibuka Miss Tanzania akifuatiwa na Jokate aliyeshika namba mbili huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Lisa Jensen.

Jokate akishangiliwa na mashabiki.
CHANZO NI GPL
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>