Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

MUSOTI: OKWI HAKUSTAHILI KUKAA BENCHI YANGA

$
0
0
BEKI makini wa Simba raia wa Kenya, Donald Musoti, amesema kocha wa Yanga, Ernie Brandts, alifanya kosa kumweka mshambuliaji Emmanuel Okwi benchi.
Yanga ilicheza na Simba, Jumamosi iliyopita kwenye mchezo wa kirafiki wa ‘Nani Mtani Jembe’ na kulala kwa mabao 3-1.

Okwi ambaye ndiye alifunga bao pekee la Yanga aliwekwa benchi na kuingia mwanzoni kabisa mwa kipindi cha pili na ndiye aliyeisumbua safu ya ulinzi ya Simba.

Akizungumza  Musoti  alisema Okwi ni mchezaji hatari na anahitaji muda ili aweze kufanya vizuri zaidi kwenye timu yake kwani anamfahamu vizuri na kudai hakupaswa kuanzia benchi.

“Yanga ni timu nzuri, lakini ilikuwa ikicheza kwa kujiamini, walikuwa wakicheza polepole sana, sisi tulikuwa na mbinu yetu ambayo tulikuwa tukiitumia kwa kurudi nyuma kulinda bao letu na kutafuta nafasi jinsi ya kufunga, hali ambayo tulikuwa tukiwachanganya wapinzani wetu.

“Okwi ndiye alikuwa mchezaji pekee aliyecheza katika kiwango kizuri kwa kuwa alivyoingia alijitahidi kuubadili mchezo na kutufanya tushambuliwe na matokeo yake ametufunga.

“Kocha amefanya makosa makubwa sana kwa kumweka benchi kwani naamini angefunga zaidi ya bao moja iwapo kocha angemuanzisha, anaonekana ni mchezaji mzuri sana kwani amekaa muda mfupi tu na timu lakini ameweza kuelewana na wenzake,” alisema  beki huyo.

YANGA: SIMBA WAMETUBEBA KLABU BINGWA AFRIKA

$
0
0
KLABU ya Yanga imesema kichapo cha mabao 3-1 toka kwa Simba kwenye mchezo wa ‘Nani Mkali Jembe’ kimewafungua macho ya kufanya vizuri kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Uongozi wa timu hiyo umesema ungepata aibu ya mwaka kama wasingecheza mchezo huo dhidi ya Simba kwa kuwa wangejiona wana timu nzuri.

Yanga inatarajiwa kufungua dimba kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Komorozine ya Comoro, Februari, mwakani jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb, alisema kama wasingecheza na Simba na kupata matokeo kama hayo basi wangeathirika zaidi kwenye michuano ya kimataifa.

Alisema wamewapa changamoto kubwa na mikakati mipya ya kukiunda kikosi chao kwa kuwa tayari wameshajua upungufu wao mapema.

“Ni vyema tulivyoona upungufu wetu kupitia mechi yetu ya kirafiki na Simba vinginevyo si ajabu ingekuwa aibu sana kwenye Michuano ya Klabu Bingwa tunayotarajia kushiriki.
“Yaani tungeathirika zaidi lakini sasa tumejijua tupo kwenye hali gani,” alisema Bin Kleb.
Kama wakifanikiwa kuitoa timu hiyo ya Comoro Yanga itavaana na Al Ahly ya nchini Misri kwenye hatua itakayofuata

2JIACHIE.COM WISH YOU MERRY CHRISTMAS

PICHA:VODACOM YAFUNIKA VIWANJA VYA COCO BEACH SIKU YA JANA

$
0
0
Vodacom siku ya jana wamezindua simu zao za HUAWEI watu walijitokeza kwa wingi katika viwanja vya Coco beach.
PICHA ZOTE NA 2JIACHIE, DAR

PICHA KATIKA MATUKIO:TAMASHA LA KRISMASI LILIVYOFANA DAR

TAMASHA LA KRISMASI LAFANA UWANJA WA JAMHURI, MOROGORO‏

$
0
0
Mwimbaji Edson Mwasabwite akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wake wakati akitumbuiza kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana jioni.
 3
Boniface Mwaitege naye akawanyanyua kwenye viti mashabiki waliojitokeza kushuhudia tamasha hilo.
4
Mwanamama mwenye sauti ya mirindimo Upendo Nkone akikonga nyoyo za mashabiki wake.
1a
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba katika tamasha la Krismasi lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro likishirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki huo hapa nchini na mwimbaji wa kimataifa kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti ambao kwa ujumla walisuuza mioyo ya mashabiki baada ya kushusha burudani ya nguvu katika tamasha hilo. Tamasha hilo liliandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini D es Salaam. (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MOROGORO)
 5
Mwanamama mwingine Upendo Kirahiro akiwaimbisha mashabiki wake.
 6
Hapa akiimba kwa furaha kumtukuza Mungu wake mbele ya mashabiki kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
 7
Vijana wa kazi kutoka kundi la Kitimtim la Rose Muhando wakionyesha umahiri wao katika kucheza.
8
Mwimbaji Edson Mwasabwite akiimba na mmoja wa mashabiki wake katika tamasha hilo.
 9
Mwimbaji wa kimataifa kutoka Zambia, Ephraim Sekereti, akiimba jukwaani katika tamasha hilo.
 10
Hapa akiimba na mashabiki wake.
 11
Upendo Nkone akicheza na vijana wake.

MASHAUZI CLASSIC YATIMIZA MIAKA MITATU

$
0
0
Keki iliyoandaliwa kwa ajili ya sherehe hiyo ya kutimiza miaka mitatu.
 Ndugu pamoja na marafiki wa Isha wakikata keki kwa pamoja.
 Wanenguaji hao wakifanya yao jukwaani kama wanavyoonekana.
BENDI ya muziki wa taarabu Mashauzi Classic inayoongozwa na mwanadada Aisha Ramadhani Makongo 'Isha Mashauzi' usiku wa kuamkia leo (Ijumaa) imetimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi mtendaji wa bendi hiyo Isha Mashauzi alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumfikisha miaka mitatu tangu kuanzisha bendi yake hiyo.
"Kiukweli napenda kuchukuwa fursa hii kumshukuru Mungu, mama yangu mzazi mdogo wangu Saida Ramadhani 'Sungura mjanja' kwa kuwa pamoja kulisukuma gurudumu hili la kuisimamia bendi ya Mashauzi kikamilifu hadi leo kufikia hatua ya kutimiza miaka mitatu" alisema Isha.

DIAMOND ATANGAZA NDOA NA WEMA...YAMETIMIA SASA

$
0
0
Tukio hilo lilitokea rasmi juzi kati  kwenye show ya Diamond pale leaders Club ambapo Diamond aliuliza msahabiki wake kuwa ''Mnataka kumjua mchumba wangu?'' na ndipo baada ya muda mfupi alipanda stejini mwanadada Wema Sepetu na kuanza kucheza na Diamond na kukumbatiana naye kuonesha ishara ya penzi lao jipya hilo lililorudi kwa kasi.
 Wema na Diamond wakiajiachia jukwaani jionee kwa piacha.
 Hali haikuwa ya kawaida jukwaani kwani kilichofuata hapo ni Wema kuonesha kwa vitendo mambo yaliyoashiria kuwa, wawili hao sasa ni mwendo mdundo.

 Wema alishuhudiwa akimzungushia mikono Diamond kwenye kiuno jambo ambalo liliwafanya baadhi ya mashabiki wa mastaa hao kutoa machozi ya furaha kuona penzi la wawili hao limerudi upya, wengine walimwambia Diamond amuoe Wema.
 Diamond muoe Wema, mnapendezana sana,” walisikika mashabiki.Diamond nataka kumuoa Wema Sepetu  na nataka kuzaa na staa,” alisema Diamond huku Wema akiwa hapingi.
HABARI NA 2JIACHIE.COM

MNENGUAJI WA BENDI YA AFRICAN STARS ALILIA PENZI.

$
0
0


Mnenguaji wa bendi ya African Stars Mandela juzi usiku alitoa mpya ya mwaka baada ya kulazimisha penzi kutoka kwa dada nnoja aliyefahamika kwa jina moja la Zainab
 Tukio hilo lilitokea nje ya ukumbi wa Mango Garden ambako bendi ya Afican Stars ilikuwa ikifanya onyesho la sikukuu ya Krismas.
 Mara baada ya bendi hiyo kumaliza kufanya onyesho hilo majira ya saa tisa na nusu mnenguaji huyo alienda katika baa ya Uhuru Pic ambapo alimwita msichana huyo ili waondoke  lakini kulitokea kama mtafaruku kwani msichana huyo alikataa katakata kuondoka na mnenguaji huyo.

Baada ya kuona hivyo mnenguaji huyo ili mbidi atumie nguvu kumvutia ndani ya bajaji dada huyo ambayo haikuwa kazi laisi ndipo mtafakuru ukazuka.
Hata hivyo dada huyo baada ya kupata upenyo alichurupuka na kutoka mbio na kudandia bajaji ingine na kuondoka kwa kasi.                       

WARAKA WA ABSALOM KIBANDA KWA JK

$
0
0
 Absalom Kibanda.
Rais Jakaya Kikwete alipofika Kumjulia Hali Absalom Kibanda nchini Afrika ya kusini Mwezi tarehe 8-2013.
MHESHIMIWA Rais wangu, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Nakusalimu kwa salamu ya utii inayotambua na kuheshimu kwa dhati mamlaka makubwa na ya juu uliyonayo kama mkuu wa taifa letu ambalo mazingira yake ya leo yanapaswa yawe wenye mwelekeo wa kushangilia kama si kujivunia uhuru ambao tuliupata mwaka 1961 na 1964 kwa kutegemea upande tulipo katika muungano wetu.
 
Mheshimiwa Rais, najisikia faraja iliyojaa majonzi moyoni kupata fursa hii adhimu kukuandikia waraka ambao msukumo wake unasukwasukwa na dhamira njema kabisa ambayo aghalabu kiini chake si kingine bali mapenzi mema kwa nchi na viongozi wetu wote.
 
Ni faraja kwa kuwa nimepata fursa ghali na adimu ya kuteta na kiongozi wetu mkuu kwa upendo, uhuru na kwa kujiamini, huku nikiwa na uchungu pia kwa sababu ujumbe ambao unabebwa na waraka huu ni wa kuumiza sana nafsi, roho, akili na mwili.
 
Mheshimiwa Rais, wewe ni kiongozi wa Watanzania wote tukiwamo sisi ambao baadhi ya wateule wako wameamua kwa sababu wanazozijua wao na wakati mwingine wakidai kwa maelekezo ya wakuu wao kutujengea taswira zinazotufanya tuonekane tu watu wa ovyo na kada ya wanajamii waliokosa utu na eti tunaopaswa kufundishwa hekima na somo la uzalendo ambalo limekuwa sehemu ya makuzi yetu nyumbani, shuleni, jeshini na ndani ya jamii.
 
Kabla sijafikisha ujumbe ambao nimeubeba kwa mfano wa mzigo mzito moyoni, napenda kwanza kupitia fursa hii kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema na neema kwa kuniwezesha kuuona mwanga wa siku hii njema ya leo ambayo kama si kwa kudra na mapenzi yake, yumkini ingeongeza hesabu za siku ambazo kiwiliwili changu kingekuwa katika kaburi la sahau ambalo kila kukicha linameza roho za makumi kama si mamia ya Watanzania wasio na hatia wanaopoteza maisha kutokana na kazi za mikono ya majahili, miungu watu waliojitwalia haki ya kuchagua aina ya maisha na vifo vya watu wengine. 
 
Baada ya hilo, kwa niaba ya mamilioni ya Watanzania wenzangu ambao hawana fursa ya kuwasiliana nawe kwa njia kama hii ya waraka niliyoitumia, napenda kutumia pia wasaa huu kukushukuru wewe binafsi kwa namna ulivyojitoa usiku na mchana pasipo kuchoka kuliongoza taifa hili katika mazingira magumu yaliyojaa changamoto za kila namna ambazo wakati mwingine sina shaka hata kidogo kwamba zimekuwa zikikunyima raha na kukosa usingizi.
 
Wakati nikikuandikia ujumbe huu, picha na taswira yako inayonijia ni ile ya Machi 8, mwaka huu siku uliponitembelea kando ya kitanda nilichokuwa nimelazwa katika Hospitali ya Milpark, Johanesburg kule Afrika Kusini ikiwa ni siku mbili tangu nilipovamiwa, nikajeruhiwa na kupewa ulemavu na majahili ambao hadi leo hii wameweza kuukwepa mkono mrefu wa vyombo vya dola unavyoviongoza.
 
Mheshimiwa Rais, japo nilikuwa nina maumivu makali na machungu ya kupoteza jicho, kidole na kupasuliwa kwa mifupa ipatayo minane katika paji langu la uso, ukiacha taya lililoachanishwa kikatili na watesi wangu wale, bado ninaweza kukumbuka kwa ufasaha namna ulivyozungumza nami ukionyesha jinsi ulivyokuwa ukiguswa na kuumizwa sana na tukio lile. 
 
Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, tangu niliporejea nchini miezi sita iliyopita sijapata kukutana nawe ana kwa ana ingawa nilipata fursa ya kukutumia salamu zangu za shukrani kupitia kwa marafiki zako kadhaa akiwamo msaidizi na mshauri wako nambari moja, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal ambaye siku zote wakati nikiwa katika matibabu nchini Afrika Kusini na hata baada ya kurejea nchini, alionekana kuwa mtu wa kukosa amani kabisa pasipo kunijulia hali kwa njia ama ya simu, wasaidizi wake na mwisho kwa kuonana nami ana kwa ana. 
 
Nayarejea haya yote huku nikitambua kwamba, wakati ninapoandika waraka huu ndiyo kwanza umerejea kutoka nchini Marekani ambako ulikwenda kuchunguzwa afya yako ambayo nina matumaini makubwa ni njema hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa, ulikwenda huko siku chache tu baada ya kuiwakilisha vyema nchi yetu katika msiba mzito wa shujaa wa mapambano ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, mzee wetu, Nelson Mandela.
 
Ninapoyatafakari matibabu ghali niliyopata nchini Afrika Kusini kwa msaada wa mwajiri wangu na safari yako nchini Marekani, vinanikumbusha swali la mmoja wa wasaidizi wangu hapa ofisini aliyetaka kujua ni sababu gani hasa ambazo zimekuwa zikisababisha wasomi na viongozi wetu kuchunguzwa na kutibiwa katika hospitali za nje, tofauti na ilivyokuwa kwa Madiba ambaye kwa nyakati zote tangu afya yake ianze kumtatiza alikuwa akipata matibabu huko huko kwao Afrika Kusini?
 
Niseme kweli, japo nilikuwa na jibu au majibu ya swali lake, sikuwa na maelezo ya kutosheleza yaliyokuwa na mwelekeo wa kukata kiu ya swali lake, ingawa kwa kupapasa nilifanya kila juhudi kuutetea utaifa wangu na viongozi wake ilhali miye mwenyewe nikiendelea kukosa raha kwa namna nilivyokuwa nikitoa majibu ambayo yalikuwa yakionyesha hali ya kuukubali unyonge, kukiri ufukara, kuficha udhaifu wetu kama taifa na kutetea makosa ambayo aghalab ninyi viongozi wetu na wale wa kabla yenu mngeweza kuwa watu mliostahili kuwa na majibu halisi.
 
Rais wangu, swali na majibu vilisababisha kimoyomoyo, nijiulize maswali mengi mengine na moja ya maswali hayo yakiwa ni wapi tulipopotea njia hata tukafikia hatua ya kusababisha kuwa na kundi kubwa la watu waliokata tamaa, wanaoteswa na ufukara, ukosefu wa ajira na kila aina ya kero na karaha zinazozonga maisha yao ya kila siku.
 
Mheshimiwa Rais, hali hiyo ilinipeleka moja kwa moja nchini Afrika Kusini na hususan katika Hospitali ya Milpark ambako huko ndiko miye mwenyewe na Watanzania wenzangu wengine tulikonusuru maisha yetu, huku baadhi kama ilivyo kwa Dk. Sengondo Mvungi wakipoteza maisha yao baada ya kukimbizwa huko. 
 
Mheshimiwa Rais, naomba unisamehe kwa kulisema hili nitakaloliandika hapa kwamba, jibu nililolipata haraka haraka kuwa moja ya chagizo la matukio ya namna hii kutokea, halikuwa jingine bali ni kushindwa kuwajibika ipasavyo kwa viongozi wetu hususan wale tuliowapa dhamana ya kuongoza sekta kadhaa nyeti kama ya afya na ustawi wa jamii.
 
Ushahidi wa kupwaya huko kwa viongozi hususan wale walio chini yako, ndiko huko huko ambako kumedhihirika pia wiki iliyopita bungeni Dodoma, ambako tulishuhudia zahama nyingine iliyowang’oa madarakani mawaziri wako muhimu wanne kwa sababu kama hizo hizo za mkwamo wao au watendaji wa chini yao katika kusimamia ipasavyo na kuchukua hatua kwa wakati, kila yatokeapo matatizo yanayogusa maeneo wanayoyaongoza.
 
Nitakuwa sijaitendea haki nafsi yangu, mheshimiwa Rais iwapo nitaficha shauku ya moyo wangu ambayo ilikwenda sambamba na tukio lile la Dodoma lililowagusa baadhi ya mawaziri ambao anguko lao linaweza likaelezwa kuwa ni ‘ajali ya kisiasa’ nikitumia msamiati ulioutumia wewe mwenyewe kwa mara ya kwanza ulipozungumzia tukio la kujiuzulu kwa waziri wako mkuu wa kwanza, Edward Lowassa.
 
Haja ya moyo wangu, nikiwa mhariri, mwanahabari, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na mdadisi wa kawaida tu wa mambo, ilikuwa kuona anguko la namna hiyo hiyo likimfika Waziri wa Habari ambaye amethibitisha pasipo na shaka kuwa pamoja na kuwa msomi wa Shahada ya Falsafa (Phd), ni kiongozi asiyejua anachofanya kwa kiwango cha kuwa mtu ambaye vichwa vya watu wengine ndivyo vinavyofikiri kwa niaba yake. 
 
Nilitamani afikwe na zahama hiyo si kwa sababu ya kuwa na hasira au kumchuria mabaya, bali kwa kuzingatia ukweli kwamba yeye ni mtu ambaye bado anasongwa na matongotongo ya mfumo wa kibabe wa zama za magazeti ya Serikali na yale ya chama tawala, ambayo yanalazimika kuandika yale tu yanayofurahisha nyoyo na akili za watawala.
 
Mheshimiwa Rais, ingawa natambua na kuheshimu ukweli mchungu kwamba, suala la nani awe waziri na nani asiwe ni jambo la wewe mwenyewe kupenda na kuchagua na kwamba ulishasema mapema kabisa mbele yetu kwamba urais wako hauna ubia, bado naamini pia kwamba, wewe ni mtu msikivu na mkweli uliye tayari kusikia na kustahimili mambo mengi machungu unayokabiliana nayo kila siku.
 
Kwa sababu hiyo, basi napenda kukueleza kwa kuweka kumbukumbu sahihi ili mbele ya safari kabla na baada ya kumaliza urais wako uje kuyatafakari na kuukumbuka ushauri huu kwako kwamba, waziri uliyempa dhamana ya kulea na kuendeleza vyombo vya habari, ni mtu wa kuhofiwa, jeuri, mwenye kiburi, asiyeshaurika na dikteta asiyekutakia mema wewe binafsi, vyombo vya habari, serikali yako na taifa kwa ujumla. 
 
Mheshimiwa rais sijui kama unajua kwamba tangu umteue amefanya kazi na vyombo vya habari vya umma na hata baada ya sisi kufanya juhudi kubwa ya kuwa karibu naye kikazi kwa makusudi na kwa ujeuri mkubwa, amekataa wito na kupuuza maoni na ushauri wetu na kwa namna ya kusikitisha amesikika akitamba waziwazi kwamba anao uwezo wa kulifungia au kulifutia usajili gazeti lolote ambalo ataliona linakwenda kinyume cha maadili ya uandishi wa habari. 
 
Waziri huyu ambaye alitarajiwa kuwa na silika za kuwa mlezi bora kutokana na jinsia yake na historia yake ya kupata kuwa mwanaharakati kabla ya kuingia serikalini, ndiye ambaye mamlaka makubwa uliyomtwisha, ameyageuza na kuwa mwavuli wa kuvisulubisha vyombo vya habari vyenye uthubutu wa kukosoa serikali na kuandika ukweli mchungu ambao asingependa kuona ukiripotiwa.
 
Mheshimiwa Rais, pengine baya zaidi kwa tasnia hii ni kwamba waziri huyo ana bahati mbaya ya kuwa na mmoja wa wasaidizi na washauri wake katika sekta yetu ya habari ambaye naye, hulka zake tangu aingie katika tasnia ya habari amekuwa ni mtu wa kujipendekeza, kupenda makuu, kuzusha na kutokuwa na mawazo huru. Huyu si mwingine bali Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO). 
 
Ni jambo la bahati mbaya kwamba waziri huyu msomi pengine kwa sababu ya kutojua vyema rekodi na historia ya msaidizi wake huyo, ambaye japokuwa naye pia ni mteule wako, amejikuta akiwa mhanga wa fikra pandikizi zinazopenyezwa wizarani chini ya uratibu mahususi unaofanywa na baadhi ya wateule wako ambao wameshaanza kujipanga kusaka urais baada ya wewe kustaafu.
 
Mheshimiwa Rais, nimelazimika kuyasema yote haya baada ya kula kiapo cha moyoni huku nikirejea mafunzo tuliyokuwa tukikaririshwa utotoni chini ya imani ya wana TANU, ambayo hata sisi ambao hatukuwa wanachama wa chama hicho tulilazimika kuikariri kwa kuitamka kila kukicha; ‘Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.’
 
Rais wangu, gazeti la MTANZANIA limerejea tena mitaani. Japokuwa ni rahisi kuhesabu miezi, napenda kukueleza kwamba, ilikuwa ni miezi mitatu michungu sana kwetu kihisia na katika hali halisi.
 
Nitakuwa mzushi sawa sawa na hao ninaowashangaa leo, iwapo nitasema kulikuwa hakuna hitilafu au makosa ya kiuandishi ambayo yaliwapa kisingizio cha mikakati waliyoipanga mapema kabisa, wasaidizi wako hao kwa kulifungia gazeti letu hili.
 
Mheshimiwa Rais, nasema haya kwa sababu ni ukweli ulio bayana kabisa kwamba, habari zilizoandikwa na kutoa mwanya kwa serikali yako kutuadhibu gazeti hili, hazikulenga kuchochea na wala hazikuchochea kabisa chuki yoyote dhidi ya yeyote na mamlaka unazoziongoza kwa namna na kwa njia yoyote ile.
 
Siyo siri hata kidogo, mkurugenzi aliyetangaza uamuzi huo alifanya hivyo akijua watu wengi hawajui mapito na dhamira yake. Tunajua yeye alimshauri vibaya waziri na serikali huku akijua vyema kwamba, yuko hapo alipo kwa maelekezo mahususi ya kundi la watu wenye malengo binafsi ambao mheshimiwa rais, niko tayari wakati wowote na mahali popote kukueleza kwa kina na kwa undani ili wakati utakapotaka kuchukua maamuzi ya haki na kweli ujue undani halisi wa mambo haya. 
 
Leo hii wakati tukirejea tena sokoni, tayari tumeshasikia kuendelea kuwapo kwa mikakati ile ile ya kuhakikisha gazeti hili na jingine ambalo halipendwi na watu hao hao kwa sababu binafsi yakiinaingizwa tena mtegoni na kufungiwa kifungo kingine kama hiki tulichomaliza au kinachofanana na kile kilichoifika MwanaHalisi. 
 
Mheshimiwa Rais, naandika waraka huu nikikumbuka semi zako mbili unazotumia; ‘tunajenga nyumba moja kwanini tugombee fito?’ na ile ya ‘akili za kuambiwa changanya na zako’ ambazo kwa muktadha wa waraka wangu huu kwako zinaweza zikawa za msaada sana kwako na pengine kwetu sisi wa MTANZANIA ambao tunashangilia kurejea mtaani kwa gazeti letu lililodhulumiwa fursa ya kuchapwa kwa muda wa siku 90.
 
Nimelazimika kukutumia wewe Rais si kwa lengo la kuchosha akili zako au kukupotezea muda, isipokuwa kwa kutambua hadhi, heshima na mamlaka makubwa uliyonayo juu ya wateule wako hao ambao wameamua kwa sababu ya jeuri za kimamlaka walizonazo kuumiza watu na kutupa sifa na majina mabaya tusiyostahili. Hakika wazungu walikuwa sahihi waliposema ‘power currupts’. 
 
Mheshimiwa Rais, lingekuwa ni jambo la kheri kwa Serikali na kwa taifa letu zima iwapo kusudi la kufungia magazeti linalopangwa na wateule wako kuwa utamaduni wa kudumu, lingekuwa ni kujenga mustakabali mwema kwako wewe binafsi, chama chako, Serikali unayoiongoza na nchi yetu kuliko hili la sasa lenye dhamira ya kufunga watu midomo, kutesa, kuzusha na kuharibu taswira yetu kama watu binafsi, taasisi na taifa.
 
Ni kwa sababu hizo, mheshimiwa Rais ndiyo maana baada ya kusukwasukwa na moyo na kuumizwa mno kifikra nikaona nitakuwa sijaitendea haki nafsi yangu na haki za maelfu ya Watanzania ambao tunaamini wanahitaji huduma ya magazeti haya katika kukidhi mahitaji yao muhimu ya kimaisha, kielimu na kiufahamu kila kukicha na kuacha dhamira hizi za kishetani zikiendelea kuongoza sekta yetu.
 
Mheshimiwa Rais, siyo siri hata kidogo kwamba, ingawa mawazo hasi dhidi ya uhuru wa kikazi na kiwajibikaji wa vyombo vya habari na wanahabari yanaonekana kutawala kauli na maamuzi ya baadhi ya viongozi na washauri wako kwa kiwango cha kukushawishi hata wewe binafsi kukubaliana nayo, ukweli ni kwamba, nyuma ya maneno matamu wanayotumia kutupaka matope, kutujeruhi na kutupa kila aina ya sifa mbaya kuna ajenda za kutuharibia sisi, kukuharibia wewe, kukomoa, kuumiza na zaidi kulikwamisha taifa.
 
Nitakuwa mhariri nisiyewajibika, iwapo nitakaa kimya ilhali nikijua fika kwamba, leo hii ndani ya wizara iliyopewa dhamana ya kulea vyombo vya habari, baadhi ya wateule wako na watendaji wake wamekalia viti walivyonavyo si kwa sababu ya kuwa kwao na uwezo kustahimili ukosoaji, au upeo wao wa kuchochea maendeleo ya kitaaluma, bali kwa kuendeleza na kuyatumikia matakwa ya utarishi wa kifikra na kimatendo. 
 
Kwa waraka huu mheshimiwa Rais, wakati tukikuahidi kwa dhati kabisa wewe binafsi na Watanzania wenzetu kwamba, tutaendelea na kazi kwa kuzingatia miiko na maadili ya uandishi wa habari, sambamba na kuheshimu sheria zilizopo, tunapenda kuliweka hili bayana kwamba, tutakuwa wa mwisho kuwatii viongozi dhalimu, madikteta, waliokosa utu na ambao kwao hila ndiyo msingi mama wa kupotosha na kupindisha mambo kwa sababu tu ya kulinda maslahi na malengo yao binafsi au yale ya makundi yenye hila.
 
Rais wangu, nimeona nitakuwa mtu nisiyekutakia mema wewe binafsi na taifa kwa ujumla, iwapo nitakaa kimya na kuruhusu fikra za kikaburu zikijijenga vichwani mwa viongozi wetu. 
 
Mheshimiwa Rais, tutakuwa tumeshindwa kutimiza wajibu wetu kama wanahabari, wahariri na viongozi iwapo tutahalalisha kwa sababu ya ukimya wetu majina mabaya tunayoitwa leo na wateule wako kama wasaliti, wachochezi na wazushi.
 
Miye binafsi naamini kwa dhati kabisa kwamba iwapo wewe utaamua kwa moyo na nia njema kulinusuru taifa letu na majahili hao walio ndani ya Serikali yako, basi siku moja historia itakuja kuandika kwa usahihi na ufasaha jina lako na letu..
 
Mungu ibariki Tanzania.

MAKAMBA AWASIHI BODABODA WA MWANZA: URAHISI NA UHARAKA WA UPATIKANAJI LESENI USIWE TIKETI YA VIFO VYA WANANCHI

$
0
0

NAIBU wa Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia January Makamba ametaka ujio wake Jiji la Mwanza usihusishwe na Kampeni za chini kwa chini za Urais bali ni kutekeleza ombi la Umoja wa waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza kuwasaidia kupata Bima ya Afya baada ya kuwawezesha kupata pikipiki 1745 za FEKON na si vinginevyo.



Kauli hiyo ya Makamba ameitoa leo wakati wa kufungua kongamano kubwa la siku moja la Umoja wa Madereva wa pikipiki Mwanza lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Nyamagana Jijini hapa, alisema kwamba kuna baadhi ya watu wameanza kuhoji ujio wangu Mwanza “Niko hapa kwa ajili ya shughuli hii mliyonialika bali kuja kushiriki Kampeni muhimu ya Bima ya Afya kwa ajili ya Usalama wa badae” na si vinginevyo.




Makamba amesema kwamba upatikanaji wa Leseni kwa urahisi na uharaka usiwe tiketi ya Kifo  kwa wananchi.
Awali kabla ya kongamano hilo madereva hao wa bodaboda walifanya maandamano toka makao makuu ya ofisi zao yaliyopo mtaa wa malango mmoja wilayani Nyamagana jijini Mwanza hadi katika uwanja wa historia wa Nyamagana.

Wadau wa Bodaboda wakiingia uwanja wa Nyamagana.

Ndani ya uwanja wa Nyamagana madereva wa Bodaboda wamejitokeza kiasi cha kutosha.

Huku wengine wakizidi kumiminika viwanjani hapa kuhudhuria kongamano lao.

Naibu wa Sayansi na Teknolijia ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli mhe. January Makamba akiingia katika uwanja wa Nyamagana kushiriki kongamano la Bima ya Afya kwa waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda wa mkoa wa Mwanza.

Kila mmoja viwanjani hapa alikuwa na kiu ya kusalimiana ana kwa ana na Naibu waziri huyo.

Licha ya kutoa elimu ya uelimishaji kujitambua kwa Bodaboda wa jiji la Mwanza ili kuepukana na maisha magumu uzeeni kwa wadau hao wa usafiri, Mkuu wa mkoa waMwanza Evarist Ndikilo ndiye aliye mkaribisha Mhe. Naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia kuhutubia maelfu ya wadau hao. 

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evaris Ndikilo kabla ya kumkalibisha mgeni rasmi aliwaasa bodaboda kufuata sheria na kanuni ikiwa ni pamoja na kuhakikisha shughuli zao zinafanyika kwa umakini na kwa amani na utulivu huku wakihakikisha usalama kwanza katika kazi zao kwa kuwa wanatumia vyombo vya moto.

Injinia Ndikilo aliwataka pia kufuata sheria za barabarani kutokana na kuwepo watumiaji wengine, kuwa waangalifu na abiria wengine wanaowachukua kutokana na baadhi yao kuwateka na kuwafanyia ukatili, kuwauwa na kuwanyanganya pikipiki zao nyakati za usiku na kuwataka kukataa kushiriki katika shughuli za uhalifu na badala yake wawabaini na kuwatolea taarifa kwa viongozi na jeshi la polisi.


Makamba alisema kuwa kupatikana kwa Bima za Afya kutatawezesha wanaopata ajali kupatiwa matibabu na kupata fidia pindi wanapopata ajali na kupata ulemavu na kifo jambo ambalo ni hakika lazima wakubali kukata bima kutoka Kampuni ya Ndege Insurance na Shirika la Bima la Taifa (NIC) yaliyokubali kuingia mkataba na wa waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza. 

Ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kuachana na tabia ya manyanyaso kwa waendesha pikipiki ya kuwabambikia kesi na makosa bali washirikiane nao kuwabaini walio wachache wanaojipenyeza kujifanya ni bodaboda kumbe ni wanaofanya vitendo vya kihuni, uhalifu na wizi kwa kivuli cha bodaboda jambo ambalo litasaidia pia kuwabaini wanaovunja sheria taritibu zilizopo.

“Mimi leo nimekubali kuwa Mlezi wenu lakini kila kijana lazima amiliki pikipiki yake mwenyewe badala ya kuwa mtu wa kuajiliwa tunahitaji kila mmoja ajiajili kwa kuwa na chombo chake, kazi ya pikipiki iwe ya usalama isiwe leseni ya kifo na ulemavu, msije mkadanganywa na baadhi ya watu kuwa watawatetea bali sisi wa viongozi wa Serikali Taifa, Mkoa, Wilaya na Jiji na kuweni makini kwa kufuata sheria za usalama” alisisitiza

Tangu kuingia mkataba na Kampuni ya Tanzania China Dev Ltd wamefanikiwa kuwakopesha 1745 na awamu ya kwanza umoja umlikopesha pikipiki 265, awamu ya pili 450 na awamu ya tatu pikipiki 1000 na wanachama wapatao 1745 wamenufaika na kupata ajira .

Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula alikuwa ni mmoja kati ya viongozi walioshiriki zoezi la kuendesha bahati nasibu ya waendesha bodaboda 100 waliobahatika kuandikishwa Bima ya Afya bure katika kongamano hilo.

Zoezi la bahati nasibu ya Bima ya Afya linaendelea na waliobahatika ndiyo hawa waliokuwa wakifika mbele katika mstari.

Mwakilishi toka jeshi la polisi na bahati nasibu ya Bima ya Afya.


Kongamano hilo limelenga kutoa elimu kwa waendesha pikipiki juu ya kufuata sheria za usalama barabarani, kusoma na kupata cheti na hatimaye leseni, kuhimiza kuvaa kofia ngumu, kuhimiza kuacha kujichukulia sheria mkononi na kuhimiza waendesha pikipiki kufuata taratibu zote zilizowekwa na serikali kwa wanachama wa wilaya za Sengerema, Nyamagana, Ilemela , Kwimba, Ukerewe, Magu na Misungwi.

Ndikilo kusanyikoni.



Burudani ndani ya Kongamano hazikukosekana.

Wadau walikuja na vyombo vyao.

No Parking.

NEYMAR NOUMAAAA, APIGA TANO PEKE YAKE MECHI LA HISANI LA MASTAA BRAZIL

$
0
0
 Kitu kipya: Neymar ameonyesha tattoo yake mpya wakati wa mechi ya hisani mjini Goiania, Brazil

WAKATI La Liga ikiwa mapumzikoni, nyota wa Barcelona, Neymar alitumia nafasi hiyo kurejea Brazil kushiriki mchezo maalum wa hisani dhidi ya mchezaji wa zamani wa Paris Saint-Germain na AC Milan, Leonardo.

Marafiki wa Neymar waliwafunga Marafiki wa Leonardo mabao8-6 huku Neymar akifunga mabao matano na kuonyesha uwezo mkubwa sana wa kandanda pamoja na kuonyesha tattoo yake mpya.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 atarejea Hispania mapema Januari akidhamiria kuiongoza Barca katika mashindano ya nyumbani na Ulaya kwa mafanikio, kabla ya kwenda kwenye Fainali za Kombe la Dunia nyumbani kwao, Julai mwakani.

Wachezaji Mtibwa Sugar wagoma

$
0
0
WACHEZAJI wa timu ya Mtibwa Sugar wametangaza kugomea mazoezi ya timu hiyo ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu baada ya kukaa miezi miwili bila ya kulipwa mishahara.

Kutokana na hali hiyo wachezaji hao wamesema kuwa hawatafanya mazoezi hayo na wataendelea kukaa nyumbani hadi siku ambayo uongozi wa timu hiyo utakapowalipa madai yao.

“Wote hatujalipwa mishahara ya miezi miwili, ukweli tumekubaliana kuwa hatuwezi kwenda mazoezini mpaka tutakapolipwa, kama hatupewi basi hatutakwenda,” alisema mchezaji mmoja aliyeomba asitajwe jina.
“Itabidi nilifuatilie ili nijue ukweli wake lakini hivi sasa sina chochote ninachofahamu juu ya suala hilo alisema kocha wa Mtibwa Mecky Maxime.

Yanga yatamba kurudisha heshima Mapinduzi Cup

$
0
0
TIMU ya Yanga SC imeahidi kutoa kipigo kwa timu walizopangiwa, ikiwemo timu ya Tusker ya Kenya wanayotarajia kuanza nayo kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup yaliyopangwa kuanza Januari 2, mwakani Visiwani Zanzibar.

 Yanga inatarajiwa kuondoka jijini Dar Januari Mosi kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mashindano hayo siku ambayo wapinzani wao Simba watashuka dimbani kuvaana na timu ya AFC Leopards ya Kenya.

Akizungumza Kocha Msaidizi wa Yanga, Fredy Minziro, alisema kikosi kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo na wanaamini kuwa mazoezi hayo yatawafanya waibuke na ushindi kwenye kila mchezo.

“Tumewaandaa vizuri wachezaji wetu kwa ajili ya mashindano ya Mapinduzi Cup na kurudisha heshima tuliyoipoteza kwenye mchezo wa Nani Mtani Jembe.

 “Kwa sasa wachezaji wako makini wanajituma kwenye mazoezi ili kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mashindano hayo, hawatakiwi kufanya makosa waliyoyafanya kwenye mechi iliyopita,” alisema Minziro.




Zitto kufukuzwa CHADEMA siku chache zijazo

$
0
0
Ni wazi kuwa huu msuguano ndani ya CHADEMA kuhusu kuvuliwa nyadhifa zote Bw. Zitto Kabwe ndani ya chama zitakoma.

Taarifa za kuaminika ni kwamba kikao kijacho cha Kamati Kuu (CC), pamoja na mambo mengine kitakuwa na agenda ya kumvua uanachama mwanasiasa huyo ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.

                         Source: Gazeti la Raia Tanzania.

Audio:Snura - UKO NYUMA SANA

WAZIRI MKUU MHE. PINDA AHUDHURIA JUBILEI YA KANISA KATOLIKI ARUSHA

$
0
0
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Maaskofu wa Kaisa Katoliki baada ya Ibada ya Jubilei ya miaka 50 ya  Kanisa Kuu  la jimbo la Arusha  iliyofanyika mjini Arusha  Desemba 30,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)IMG_0134

AMANDA: MWAKA 2013 ULIKUWA MAJANGA KWANGU

$
0
0
 MWANADADA kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa mwaka 2013 ulikuwa majanga kwake kwani ulikuwa mgumu sana na mambo yake hayakumwendea vizuri.
 
Akichonga Amanda alisema bora mwaka huu upite, kwani ulikuwa mgumu sana kwa upande wake  katika mambo f’lani ambayo hakutaka kuyataja ila anaamini kuwa mwaka ujao utakuwa mzuri kwake kwani ameshaanza kuona dalili za mafanikio mapema.

“Mwaka 2013 ulikuwa mgumu kwangu, ila nashukuru unaisha, ninaamini huo ujao utakuwa mzuri na wa mafanikio kwangu kwani nimeshaanza kuona dalili nzuri, suala la kuolewa halipo kichwani kwani hata sina mwanaume kwa sasa, ninawaza tu jinsi ya kupata fedha kwa kufanya kazi kwa bidii,” alisema Amanda.


AMANDA POSHY KATIKA POZI

TMA PRESS CONFERENCE 31-DESEMBA 2014, JUMANNE SAA TANO ASUBUHI‏

$
0
0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: TAARIFA YA MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA MWEZI JANUARI NA FEBRUARI 2014
Tafadhali husika na somo tajwa hapo juu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania atatoa taarifa ya mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Januari na Februari 2014. Taarifa hiyo itatolewa kwa vyombo vya habari Jumanne tarehe 31 Desemba 2013, saa 5 (tano) asubuhi, katika ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania zilizopo kwenye jengo la Ubungo Plaza, Barabara ya Morogoro, kwenye ukumbi wa mikutano, ghorofa ya tatu. Tafadhali usikose kuhudhuria ukiwa kama mdau mkubwa wa hali ya hewa nchini.

RAIS KIKWETE AMTEUA ERNEST MANGU KUWA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI

$
0
0
Kamishna wa Polisi Ernest Mangu aliyeteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.
Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence)katika Jeshi hilo la Polisi.
Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.
Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).
Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne,  Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>