Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

PICHA: WEMA SEPETU KATIKA MAPOZI TATA


PICHA ZA MKOKO MPYA WA BARNABA..CHEKI PICHA HAPA

$
0
0
 Mkoko mpya wa Mwana muziki Mkali wa Bongo Fleva Elias Barnaba aina ya Mark x wenye thamani zaidi ya mil 25.

SIKINDE YAJICHIMBIA BAGAMOYO KUKABILI MSONDO KRISMASI

$
0
0


HOMA ya pambano la watani wa jadi katika muziki wa dansi nchini kati ya Mlimani Park 'Wana Sikinde' na Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' litakalofanyika siku ya Krismasi imeanza kupanda kwa bendi hizo kujificha kambini na huku wakipigana vijembe.

Bendi hizo kongwe nchini zinatarajiwa kuonyeshana kazi katika onyesho litakalofanyika kwenye viwanja wa TCC Club Chang'ombe, Temeke Dar es Salaam katika kunogesha sikukuu hiyo ya Krismasi.

Katika kuonyesha wamelipania pambano hilo bendi ya Sikinde tayari imeiendea Msondo wilayani Bagamoyo kwa ajili ya kuweka kambi yao na wamewatahadharisha 'mahasimu' wao hao wasije wakatoa visingizio baada ya kugaragazwa kwenye onyesho hilo.

"Sisi tumeamua kuweka kambi yetu mjini Bagamoyo ambako tutatua viwanja vya TCC kutokea huko ili kuisambaratisha Msondo, na tunataka wajipange sawasawa ili wasije wakatoa visingizio tena kwa maana kama vyombo vipya bendi zote imepewa na Konyagi," Katibu wa Sikinde, Hamis Milambo alisema.

Milambo alisema mashabiki wa dansi wajitokeze kwa wingi kushuhudia namna gani wanavyowachachafya wapinzani wao hao, ikizingatiwa hawajakutana kwa muda tangu mwaka jana.

Upande wa Msondo kupitia Meneja wao, Said Kibiriti, alisema hawana haja ya kutaja mahali kambi yao ilipo isipokuwa wamejiandaa kuwatoa nishai wapinzani wao siku ya onyesho hilo litakaloanza saa nane mchana.

 
 "Sisi hatuna mchecheto wowote na mpambano huo, tunaendelea kujifua kimya kimya mahali ambapo siwezi kupataja kwa sasa," alisema Kibiriti.

Naye muimbaji anayekuja juu wa bendi hiyo ya Msondo alitokea Sikinde, Athuman Kambi, alisema amejipanga kuonyesha umahiri wake katika mpambano huo baada ya kufanya hivyo wakati akiwa Sikinde dhidi ya Msondo kwenye ukumbi wa Diamond na kuwawehusha mashabiki wa muziki wa dansi nchini.

"Najua watu watataka kuona nafanya kitu gani dhidi ya bendi yangu ya zamani iliyonitangaza vyema, wasiwe na hofu waje Desemba 25 waone nini nitakachofanya TCC Club Chang'ombe," alisema Kambi.

Mpambano huo wa Sikinde na Msondo umeandaliwa na kampuni ya Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi, gazeti la NIPASHE, Integrated Communications, CXC Africa na Salute5.

MANJI AWAOMBA WANACHAMA WA YANGA WASIVUNJIKE MOYO

$
0
0
Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya juzi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, kushoto ni makamu mwenyekiti Clement Sanga

Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa wa
Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.

"Mechi ya juzi ilikuwa ni bonanza, ndio maana hapakuwa na timu iliyopata pointi katika mchezo huo zaidi ya kusherehekea, sisi tumepata zawadi ya milion 98 wakati wenzetu Simba SC wamepata milion 1, hivyo zaidi sisi tumeendelea kuimarika kiuchumi zaidi wenzetu wameishia kusherehekea" alisema Manji. 

Aidha amesema wachezaji zaidi ya tisa wa Yanga hawajapata muda wa kupumzika tangu mwezi Novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kwani walijiungana timu za

Taifa na wamekua huko kwa takribani mwezi mzima bila kupumzika tofauti na wenzetu Simba SC ambao hawana wachezaji wengi timu ya Taifa.

Manji pia alisema anawapa hongera timu ya Simba SC kwa kushinda bonanza la jana, amesema mchezo wa jana walicheza vizuri hivyo wanastahili pongezi kwa hilo.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyojitokez katika mchezo wa jana, amesema kamati husika inayafanyia kazi na kwa kuwa yeye anasafiri leo kwenda nje ya nchi  majukumu yote amemkabidhi makamu mwenyekiti Clement Sanga mpaka yeye atakaporejea.

MH. LOWASSA AZUNGUMZA NA WAENDESHA BODABODA MKOA WA DAR ES SALAAM

HOTUBA YA ZITTO KABWE NA MAPOKEZI YAKE - KIGOMA, 21 DESEMBA 2013‏

$
0
0
Zitto Kabwe akihutubia wananchi wa Kigoma jana.
Wananchi wakiwa na mabango ya kumpokea Zitto.
HOTUBA YA MH ZITTO Z. KABWE - KIGOMA – 21 DESEMBA 2013
Leo nina furaha kubwa sana kwani baada ya safari ndefu na yenye changamoto nimerudi nyumbani kuwasalimu wananchi wenzangu! Na hii si salamu za kawaida bali nawasalimu kwa salaam za demokrasia, uadilifu, uzalendo na uwajibikaji. Nawasalimu si kama mbunge bali kama mwana wenu wa Kigoma! Na popote niendapo najivunia kujitambulisha kama Mtanzania; kama mwenyeji wa mkoa wa Kigoma na zao la Ujiji.
Tuna mengi ya kujivunia kama taifa lakini Ujiji na watu wake mna nafasi ya pekee katika historia. Watu wa Ujiji mlipokea harakati za kudai uhuru wa nchi yetu mapema kabisa mapambano ya uhuru yalipoanza. Watu wa Ujiji mlikuwa wa kwanza kabisa kupokea mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Na Jimbo la Kigoma Mjini ilikuwa miongoni mwa majimbo ya mwanzo kabisa kutoa mbunge wa CHADEMA mwaka 1995. Kabla ya hapo mlitoa madiwani wengi mwaka 1994.
Wakati Watanzania wengine wakiwa wanajiuliza mara mbili mbili kuhusu kujiunga na vyama vipya vilivyoanzishwa, watu wa Ujiji, watu wa Kigoma hamkusita kupokea mabadiliko. Wengi wamepoteza maisha yao, wengine kazi zao na wengine hata ndoa zao katika kupata mbegu ya mabadiliko katika nchi yetu. Nawataka msichoke. Wekeni nguvu mpya katika kusimika mabadiliko kwani bado kazi ya kuimarisha demokrasia katika nchi yetu haijaisha na inahitaji uvumilivu, kusameheana na kuaminiana.
Na nchi yetu Tanzania ni nchi inayoonyesha uwezo mkubwa katika kupendana, kuaminiana, kuvumiliana na hata kusameheana. Na haya si maneno tu ambayo ninayazungumza kama mwanasiasa. Hii ni hali halisi na maisha niliyoyaishi kwa mifano nilipokuwa ninakua na kusoma katika shule ya Msingi Kigoma na baadaye Shule ya Sekondari Kigoma. Malezi yangu yalikuwa yanaongozwa na jamii nzima ya Kigoma.
Nimekuwa nikiwaeleza rafiki zangu niliokutana nao kwenye masomo na kwenye siasa kwamba nimeanza kuvaa viatu kwa mara ya kwanza nikiwa darasa la tatu. Viatu hivyo viliitwa 'asante Salim' vilivyokuwa vinatengenezwa na Kampuni ya Bora Shoes. Vililinunuliwa na mama Coretha Furugunya ambaye tulikuwa tunakaa mtaa mmoja wa Kisangani Mwanga. Mama Coretha hakuninunulia viatu kwa sababu alikuwa ana uwezo mkubwa, la hasha! Alifurahishwa na matokeo yangu ya mitihani ya darasa la pili kwenda la tatu.
Ninaamini kitendo cha mama huyu ni ushahidi wa uungwana, upendo na hata uwajibikaji ambao tunao sisi watanzania. Uwajibikaji kwani alichukua jukumu kunilea ingawa hakuwa mzazi wangu, lakini aliona kuwa kama mwanajamii ana nafasi kubwa katika kuwaendeleza watoto wote. Jamii hii ya watu wa Kigoma ilinifunza kuwa nikijitahidi na kukazana kwa bidii kwenye masomo na majukumu, nitafanikiwa. Siwezi kusahau somo hili katika maisha yangu na ni somo hili ndilo limenifanya nijitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kuwatumikia kwa uadilifu na mafanikio ya hali ya juu sana.
Nikiwa nimejaa matumaini haya kuhusu wananchi wenzangu, leo nataka niwakumbushe kwa nini kama jamii tulichagua kufuata njia ya demokrasia. Demokrasia ina maana pale ambapo inatumika kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha ya wananchi. Maisha yanayotakiwa ni yale yanayomwezesha mwananchi kupata huduma zake stahili kama Elimu, Afya, Maji na miundombinu. Demokrasia haina maana pale wananchi wanakufa njaa kwa kukosa ajira na kukuza umasikini.
Demokrasia inahusu maendeleo. Tumejitahidi kwa upande wetu kuondoa mkoa wa Kigoma kutoka mikoa isiyo na miundombinu kabisa ya maendeleo mpaka kuwa mkoa unaotumika kama mfano kwa miradi mingi ya Maendeleo ikiwemo Daraja la Malagarasi, Uwanja wa ndege wa Gombe-Mahale, barabara za lami na upanuzi wa Bandari, ujenzi wa bandari ndogo mpya na ujenzi wa kituo cha Usafirishaji Mwandiga.
Asije mtu akasema yeye ndio kafanya haya. Haya ni matunda ya nyinyi watu wa Kigoma kupokea demokrasia na bila woga kuchagua viongozi wenu bila kujali vyama bali kwa kuangalia uwezo. Haya ni matunda ya viongozi wenu kupaza sauti yenu kwenye baraza la Taifa, Bunge. Haya ni matunda ya uvumilivu wenu na uamuzi wenu wa kutaka maendeleo. Juhudi hizi lazima ziendelezwe kwa nguvu zote ili kuhakikisha kuwa nafasi ya mkoa wa Kigoma katika uchumi wa Tanzania inaonekana dhahiri na hivyo kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwa kituo cha biashara katika nchi za maziwa makuu.
Lakini tukumbuke pia kuwa Demokrasia ni Uwajibikaji. Katika kipindi cha utumishi wangu kwenu,kutokana na malezi niliyoyapata kutoka kwenu,nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa Serikali inawajibika kwa Wananchi. Nakumbuka wakati napambana kuhusu sheria mbovu ya madini kuna watu hapa nyumbani walisema 'sasa huyu kawa mbunge wa Taifa' lakini watu wengi zaidi wakasema tumemtuma Dodoma kusemea Watanzania wote na sio Kigoma tu.
Tuliweza ndani ya miaka mitano kufanya mabadiliko makubwa sana kwenye sera ya Madini na sheria ya madini ambapo baadhi ya mambo ambayo yalikuwa hayafikiriki sasa yametungiwa sheria ikiwemo Serikali kuwa na hisa kwenye migodi, Tanzanite kumilikiwa na Watanzania sio chini ya asilimia 50 na kuzuia kabisa wageni kuchimba vito vya thamani.
Uwajibikaji ulipelekea kumshinikiza Rais kufanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri kwa kuwafukuza mawaziri wanane mwaka jana. Hii ilitokana sio tu na hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu bali pia ushiriki mkubwa wa wananchi kupitia simu na mitandao ya kijamii ambapo wabunge walishinikizwa kuweka saini kwenye karatasi za kumtoa Waziri Mkuu.
Toka wakati huo kumekuwa na utaratibu sasa ambapo wabunge hawaoni taabu kutaka uwajibikaji waziwazi ili kuzuia ubadhirifu wa fedha za Umma. Ni hivi jana tumeshuhudia mawaziri wanne wamejiuzulu na kufukuzwa kazi kutokana na kashfa ya operesheni Tokomeza ujangili iliyoibuliwa na ripoti ya kamati ya bunge. Mabadiliko haya ni hatua muhimu katika kuimarisha demokrasia yetu.
Pamoja na matunda haya mengi mazuri lakini bado kuna changamoto katika juhudi zetu.
Changamoto kubwa tuliyonayo wananchi ni kukosekana kwa imani katika demokrasia yetu.
Kutoaminiana. Ni dhahiri kuwa kutoaminiana katika nchi yetu kumekuwa kwa kiasi kikubwa. Taarifa za kitafiti zinaonyesha kuwa katika kila Watanzania kumi, wanane hawaaminiani. Ni changamoto kubwa sana. Wananchi wameacha kutuamini wanasiasa na wanasiasa wameacha kuaminiana wenyewe kwa wenyewe.
Hivi sasa uongo umegeuzwa kuwa ukweli na ukweli umekuwa ni uongo. Hivi sasa ukitaka kuwa mwanasiasa maarufu inabidi ujue kudanganya na ukitaka kuitwa mwanasiasa msaliti inabidi uwe msema kweli. Kukosekana kwa uaminifu na kuaminiana imekuwa ni kansa katika siasa zetu. Itachukua muda mrefu sana kujenga demokrasia imara katika nchi yetu kama hatutapata jibu la changamoto hii ya kutoaminiana na kugeuza uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo. Hivi sasa ukweli umekuwa unatengenezwa badala ya kutafutwa.
Ni majanga! Juzi bungeni Mwanasheria Mkuu wa Serikali alielekeza shutuma kwangu kwamba sikushirikiana na kamati maalum iliyoundwa na Bunge kufuatilia mabilioni ya uswisi na kwamba chini ya kiapo nilisema sina majina ya watu wenye akaunti huko Uswisi. Huu ulikuwa ni uongo. Ni uongo kwa sababu niliitika wito wa kamati hata nilipokuwa katika mafunzo ya mgambo huko Tanga na nilikutana nao mara nne.
Ni uongo kwa sababu niliwapa wajumbe wa Kamati Maalaum maelezo na taarifa nyingi sana kuhusu utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na umiliki wa mali nje ya nchi kinyumecha sheria. Ni uongo kwa sababu mimi kutotaja majina haya haina maana sina majina, bali ni kwamba ninaheshimu utaratibu na nimeachia vyombo husika vikamilishe uchunguzi. Kwani mimi kama mtu binafsi nikianza kuchukua majukumu ya taasisi ninaweza kutia dosari harakati hizi muhimu na hata kupelekea mchakato mzima kuvurugika. Sitaingia mtego huu! Lakini hatua hii ya Mwanasheria Mkuu imenipelekea kujiuliza maswali mengi kwa mfano uongo kama huu ulifanywa kwa malengo gani? Na ninajikuta hata mimi ninaingia katika hali ninayoilalamikia ya KUTOAMINIANA.
Lakini mtambue pia kuwa kutoaminiana kunaleta kutovumiliana. Hivi sasa kuwa na mawazo tofauti katika vyama vya siasa au hata asasi za kijamii ni uhaini. Lakini bila kuenzi tofauti za mawazo hatuwezi kujenga vyama imara wala Taifa imara. Demokrasia imara ni zao la tofauti za mawazo na uhuru wa mawazo.
Kama hatuwezi kujenga vyama vinavyorutubisha uhuru wa mawazo na tofauti za mawazo, tutajenga Taifa lenye watu wenye kuogopa na waliojaa woga. Wanachama wanapoogopa uongozi ni udikteta, lakini uongozi unapoogopa wanachama ni demokrasia. Bila demokrasia ya uwazi na kuvumiliana tutakuwa Taifa la kidikteta. Lazima vyama vya siasa, viongozwe kwa namna ile ile ambayo Taifa litaongozwa.
Demokrasia bila kuaminiana, demokrasia bila kuvumiliana sio demokrasia ya kweli.
Juzi nilipoingia Bungeni kwa mara ya kwanza baada ya matukio kadhaa yanayoendelea ndani ya chama chetu nilikaa pamoja na mbunge Tundu Lissu. Wabunge wengine walidhani tutarushiana ngumi na badala yake ikawa ni vicheko na mazungumzo. Hii ni kwa sababu sina chuki na mtu yeyote yule.
Mmenifunza kutojenga chuki na watu na badala yake kuchukua kila tukio kama changamoto ya maisha. Siasa ni kupambanisha mawazo tofauti na hatimaye kutafuta suluhu ya pamoja. Na siasa ina misingi yake ambayo sisi wanasiasa huwa tunasahau kwa maksudi. Msingi wa siasa ni kuwa inapaswa kuleta unafuu wa maisha ya wananchi na sio malumbano tu ya kurushiana maneno na kuzushiana ili kujijengea umaarufu wa kisiasa. Siasa si kuwekeana chuki na kuonyeshana ubabe.
Na hapo ni muhimu muelewa wanaKigoma mnapoambiwa kuwa eti ninapofuatilia mabilioni ya Uswisi ninatafuta umaarufu, ni uongo! Mnaposikia eti kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki na kujitafutia umaarufu, ni uongo! Kinachonisukuma kufanya vyote hivi ni ninyi. Ninasukuwa kila ninapowaona watoto bado wanatembea bila viatu;kila ninapoona akina mama wanapoteza maisha yao katika uzazi;kila ninapoona vijana ambao hawana uhakika wa kupata hata mlo moja kwa siku kwa kukosa kazi; ninapoona wazee wa Kigoma kukosa hata shilingi mia moja kununua chai asubuhi.
Ninawaona si wanaKigoma bali mamilioni ya watanzania wakiishi katika hali hii. Alafu nalinganisha na taarifa tunazozipata kuhusu ufujaji na utoroshwaji wa pesa zetu. Hebu sasa linganisheni na ukweli kuwa ripoti ya kimataifa iliyotolewa hivi karibuni imeonyesha kuwa mwaka 2010 pekee, jumla ya dola za kimarekani milioni 1315 (bilioni 1.3), yaani shilingi trilioni  2,113,930,000,000 (sh trilioni 2.1) zilitoroshwa kutoka nchini Tanzania. Mwaka 2011 kiasi cha dola za kimarekani milioni 817 yani shilingi za kitanzania zipatazo trilioni 1,315,370,000,000 (trilioni 1.3) zilitoroshwa.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa jumla ya fedha za Watanzania zilizotoroshwa nje ya nchi katika miaka kumi iliyopita zilifikia dola za kimarekani milioni 4526 (bilioni 4.5) sawa na shilingi za kitanzania trilioni 7,286,860,000,000 (trilioni 7.3).  Nimewatajia hapa namba chungu nzima na matrilioni na mabilioni hayaleti maana. Lakini hii ina maana kwamba kiasi cha pesa zilizotoroshwa katika miaka 10 pesa - robo yake tuingeweza kujenga barabara ya lami ya kiwango cha juu kabisa kutoka Kigoma mpaka Dar-es-salaam! Pesa hizi zingeweza kuajiri na kuwalipa vizuri walimu, madaktari na wafanyakazi wengine ili kuhakikisha tunapata huduma bora na kutengeneza ajira bora kwa vijana wetu.
Pesa hizi zingeweza kununua madawa muhimu na kuokoa maisha ya maelfu ya akina mama tunaowapoteza kila mwaka wakati wa uzazi. Pesa hizi zingeweza kuwanunulia watanzania wote si watoto tu angalau pea 10 ya viatu. Sasa nikitafakari haya siwezi kuchapa usingizi mnono na kufumbia macho utoroshwaji wa fedha au matumizi mabaya ya fedha za umma kwa njia ya sisi wabunge kujilipia posho! Hapana! Nafsi yangu hainiruhusu kukaa kimya kwa kuogopa kuitwa mbinafsi au msaliti!
Lakini naomba niwasihi kuwa katika nyakati kama hizi za changamoto za kisiasa jambo la msingi kuliko yote ni kutulia maana hakuna linalotokea bila sababu. Licha ya kwamba kuna watu wengi wanapaza sauti zao katika mambo haya lakini pia kuna wengi zaidi ambao wapo kimya lakini wana mawazo yao, ndani na nje ya chama chetu;ndani na nje ya Serikali na ndani nanje ya nchi yetu. Ndio maana lazima kuibadili nchi yetu ili kuweza kuhakikisha kila raia anakuwa na fursa ya kutoa mawazo na fikra zake zinakuwa huru.
Maisha ni mabadiliko; mabadiliko hayana ukomo; mabadiliko hayazuiliki kwa sababu bila mabadiliko hakuna ukuaji, bila mabadiliko hakuna maendeleo. Mabadiliko ni kiu kikubwa cha Tanzania kwa sababu mabadiliko huleta matumaini. Na kiu hii ni kubwa zaidi kwetu sisi vijana wa kizazi hiki kipya. Siasa za kizazi kipya cha viongozi ni siasa za majawabu ya kero za wananchi. Siasa za mabadiliko ni siasa za kujenga na kuimarisha; ni siasa za kuaminiana na kuheshimiana hata pale mnapopingana kimawazo. Ninataka tujenge siasa mpya Tanzania;siasa za mabadiliko; siasa zinazojenga matumaini ya kweli;siasa zinazowajali na kuwajengea uwezo wananchi wa Tanzania. Mungu ibariki Tanzania.

TOP 10 VINARA WA SKENDO 2013

$
0
0
KATIKA ulimwengu wa mastaa kuna ambao wamekuwa wakitikisa kwa skendo mbalimbali kwa mwaka 2013 ambazo ziliwachefua mashabiki wao, Ijumaa Wikienda linakupa Top 10 ya skendo hizo.
AGNES GERALD ‘MASOGANGE’
Video Queen huyo alitikisa mwaka 2013 kwa skendo ya kukamatwa na dawa za kulevya huko Afrika Kusini na kuwekwa rumande kwa siku kadhaa.
Baadaye alifikishwa mahakamani ambapo iligundulika kuwa mzigo aliokuwa amebeba siyo dawa za kulevya ila ni unga unaotumika kama dawa za binadamu na kesi ikaishia hapo.
Pia Masongange alikuwa kinara wa kupiga picha za nusu utupu ambazo alizitundika mtandaoni na kugeuka gumzo kubwa.
WEMA SEPETU
Wema alitikisa kwa ishu ya kurudiana na mwanamuziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ikiwa ni baada ya kukutana nchini China na kupiga picha za kimahaba, hali iliyozua gumzo kila kona na mitandaoni.
Wema alirudiana na Diamond huku akijua kwamba mwanamuziki huyo alikuwa na mpenzi mwingine ambaye ni mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Ukiachilia mbali misala midogomidogo, Wema alitikisa na ile kesi yake ya kumtandika makofi meneja wa hoteli ambapo alisota mahakani hadi alipohukumiwa akalipa faini ya Sh. laki moja.
JACQUELINE WOLPER
Skendo iliyotikisa kwa mwanadada Wolper ni ile ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Ramadhan Mtoro ‘Dallas’ ambayo ilitokea tangu mwaka jana akavuka nayo mpaka mwaka huu.
Pia alitikisa kwa ishu ya kupigania nyumba ya kupanga na Baby Madaha. Baby alidai aliilipia nyumba hiyo Sh. milioni milioni 3.6 na kufanya usafi kwa ajili ya kuhamia lakini siku ya kuhamia alimkuta Wolper ameshahamia na kupanga vitu vyake hali ambayo ilizua mtafaruku kwa wawili hao na kuwa na bifu kali hadi leo.
BABY MADAHA
Mwaka 2013 alitikisa kwa ishu ya kugombea nyumba ya kupanga na Wolper.
Baada ya hapo alitikisa na skendo ya kumuiba mume wa mtu ambaye pia ni meneja wake, raia wa Kenya, Joe Kairuki ambaye yupo naye hadi sasa.
JACQUELINE PATRICK
Mwaka 2013 alitikisa kwa skendo ya kuachana na mumewe, Abdulatif Fundikira ambaye ndoa yao haikudumu kwa muda mrefu na alipewa talaka mahakamani kabla ya kudaiwa kutoka na msanii Jux.

JACQUELINE PENTZEL ‘JACK CHUZ’
Yeye alitikisa kwa skendo ya kunasa kwenye mtego wa kujiuza ambapo alinaswa na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) inayoendeshwa na Global Publishers katika hoteli moja iliyopo Ubungo Dar, baada ya kuelewana na mwanaume aliyekutwa naye kwamba atamlipa kwa dola.
Siku chache baada ya kunaswa na mtego huo Jack Chuz aliolewa na Gadna Dibibi ambaye naye alidaiwa kuwa ni mume wa mtu.
 
LULU SEMAGONGO ‘AUNTY LULU’
Ikiwa ni siku chache tangu Jack Chuz kunaswa na mtego wa OFM, Aunty Lulu naye aliingia kwenye mtego huo ambapo alinaswa katika hoteli moja iliyopo Sinza, Dar.
KAJALA MASANJA
Mwaka 2013 haukuwa mzuri kwa upande wake kwani aliswekwa jela kwa kosa la utakatishaji wa fedha haramu uliofanywa na mumewe, Faraji Agustino.
Kajala alihukumiwa kwenda jela miaka mitano lakini Wema Sepetu akamlipia faini ya Sh. milioni 13.
Baada ya kutoka gerezani, aliripotiwa kutoka kimapenzi na Petit Man huku akiwa bado ni mke wa mtu.
BLANDINA CHAGULA ‘JOHARI’
Yeye alipamba kwenye vyombo vya habari kutokana na skendo yao ya kumgombea msanii mwenzao, Vincent Kigosi ‘Ray’ ambapo alifikia hatua ya kupigana na Chuchu Hans ambaye alidaiwa kuingilia penzi hilo.
CHUCHU HANS
Mwaka 2013, Chuchu alitikisa kwa skendo ya kudaiwa kutoka na mpenzi wa Ruth Suka ‘Mainda’, Ray hali iliyosababisha mtafaruku mkubwa baina yake na Mainda pamoja na Johari ambaye alimpiga ikiwa ni baada ya tetesi kuzagaa kuwa wawili hao walifumaniwa.
CREDIT:GPL

Brandts atimuliwa Yanga

$
0
0

Habari na Championi Jumatatu

KOCHA Ernie Brandts hana chake tena Yanga na ndani ya siku mbili, uongozi wa klabu hiyo utatangaza kumtimua.

Taarifa za uhakika ambazo Championi Jumatatu limezipata kutoka ndani ya Yanga, zimeeleza Brandts ameshafukuzwa kazi.

“Kweli Brandts ameonekana hafai na wakubwa walikaa jana kikao mara tu baada ya mechi ya Simba na Yanga, wamefikia hatua ya kumuachisha kazi.

“Mimi ninavyojua tayari mawasiliano na makocha kadhaa yameanza na Brandts atapewa muda kidogo tu ili akusanye virago vyake na kurejea kwao Uholanzi,” kilieleza chanzo cha uhakika.

Lakini viongozi wa Yanga walikuwa wagumu kulizungumzia suala hilo, ingawa mtu mwingine wa karibu na uongozi wa Yanga, alisema huenda leo Yanga wakatangaza.

“Wanaweza kutangaza kesho (leo), nimeelezwa kuwa wamefikia uamuzi huo na kuna bosi mmoja atatangaza leo au kesho,” alisema na kuongeza: “Kama mtaandika wanaweza wasitangaze.”

Brandts amejikuta katika wakati mgumu baada ya kikosi chake kulambwa na Simba kwa mabao 3-1 katika mechi ya Nani Mtani Jembe iliyopigwa juzi jijini Dar.

Inaelezwa baada ya mechi hiyo, kocha huyo aliyeipa Yanga ubingwa msimu uliopita, alishindwa kuwaridhisha mabosi wake baada ya kuulizwa sababu za kufungwa.

Mbali na Brandts, inadaiwa kuwa uongozi wa timu hiyo una mpango wa kutimua benchi zima la timu hiyo, akiwemo Kocha Msaidizi, Fred Felix Minziro.

Kocha wa sasa wa Mbeya City, Juma Mwambusi, ndiye anapewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya Minziro kwenye kikosi hicho cha Jangwani.

Yanga inatarajia kwenda kuweka kambi na inaelezwa zitakuwa nchi kati ya Hispania, Uturuki au Ureno na taarifa zinasema kuwa inataka kwenda na benchi zima la ufundi.

Brandts awataja walioiua Yanga SC

$
0
0

KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts,  amewataja waliochangia kuimaliza Yanga dhidi ya wapinzani wao Simba katika mchezo wa Nani Mtani Jembe uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, juzi.

Yanga ilishindwa kutamba juzi mbele ya Simba baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1.

Akizungumza  Brandts alisema kosa alilolifanya kipa Juma Kaseja la kufanya mbwembwe karibu na lango, kisha kusababisha bao la tatu, lilichangia timu hiyo kufanya vibaya.

Ukiachana na hilo, Brandts alisema wachezaji wake katika mchezo ule, walicheza kama siyo wa timu moja, kitu ambacho kilichangia kufanya vibaya.

“Wachezaji hawakucheza kama timu na maprofesheno ninao wengi katika kikosi changu lakini walishindwa kuonyesha uwezo wao katika mchezo, japo kipa naye alifanya kosa ambalo lilisababisha kuwapa nafasi Simba kupata bao rahisi sana.
“Japo hata mfumo tuliotumia nao ulisumbua kidogo ila wachezaji wanapaswa kutambua nini wanachofanya wanapokuwa uwanjani, ingawa kipindi cha pili walijitahidi,” alisema Brandts.

KOCHA WA SIMBA, TAMBWE NI KIBOKO

$
0
0
KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic,  amefurahishwa  na uwezo wa mshambuliaji wake, Amissi Tambwe na akasisitiza Mrundi huyo ni kiboko.
Tambwe alikuwa amemuudhi kocha huyo raia wa Croatia kutokana na kuchelewa kufika kambini, hali iliyosababisha uhusiano wa wawili hao kuyumba, lakini baada ya Mrundi huyo kuibeba Simba Taifa, Logarusic amechekelea na kusahau tofauti zao zote.

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, Tambwe alitupia mabao mawili, moja likafungwa na Awadh Juma.

Akizungumza kocha huyo alisema katika mchezo huo, safu ya ushambuliaji iliweza kumtendea haki.
 “Safu ya ushambuliaji iliyoongozwa na Tambwe ilikuwa nzuri, yenye uwezo na kiwango kinachovutia,” alisema Logarusic.

PICHA:MASHABIKI WA SIMBA WATOA BURUDANI TAIFA, SIKU YA WATANI..

YANGA YASITISHA MKATABA NA BRANDTS

$
0
0

Uongozi wa klabu ya Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.

Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.

Hatua ya Young Africans SC kusitisha huduma na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili.

Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.

Young Africans SC imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.

Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.

Ikiwa Brandts ataondoka mapema timu itaendelea na mazoezi kama kawaida katika kila siku asubuhi katika uwanja wa bora kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Fred Felix “Minziro”.

Ili kuhakikisha timu inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa uongozi unakamilisha maandalizi ya safari ya kambi nje ya nchi na taratibu zote zitakapokamilika tutawajulisha.

Aidha uongozi upo katika mchakato wa kumapata mrithi wa Brandts ambaye ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na Mashindano ya klabu Bingwa Afrika.

Mwisho tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wasivunjike moyo kufuatia matokeo ya bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga kuhakikisha timu inaimarika kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha katika mzunguko wa pili wa VPL.
Abdallah Bin Kleb
Mwenyekiti - Kamati ya Mashindano
Young Africans Sports Club.
DAR ES SALAAM
23 Disemba, 2013

MECHI YA MTANI JEMBE YAINGIZA MIL 422/-

$
0
0

                                                            Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu TFF
MECHI YA MTANI JEMBE YAINGIZA MIL 422/-
Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Desemba 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 422,611,000.
Mapato hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.
Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh. 7,488,000.
Mgawo mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh. 28,052,553.22.
MALINZI, MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Desemba 24 mwaka huu).
Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
 Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MWENYEKITI WA CHADEMA JIMBO LA BUMBULI ASIMAMISHWA UONGOZI

$
0
0
TAARIFA KWA UMMA
KUKOMA/KUSIMAMISHWA KUWA KIONGOZI KWA MWENYEKITI WA JIMBO YA BUMBULI ABDI SHEKIMWAGA
CHADEMA Kanda ya Kaskazini, inawatangazia umma wote kuwa, Ndugu ABDI SHEKIMWAGA amesimamishwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Bumbuli kuanzia 21 Desemba 2013.
Ofisi ya kanda, ilipokea nakala ya taarifa na miniti ya kikao kilichoketi tarehe 22 septemba 2013 kutoka kamati tendaji ya wilaya/jimbo pamoja na nakala ya barua ya tuhuma alizoandikiwa ndugu ABDI SHEKIMWAGA ili ajieleze na kujibu, ikiwemo na barua ya tarehe 12 Desemba 2013 aliyoandikiwa katibu wa mkoa kujulishwa mapendekezo na hatua za kunusuru chama dhidi ya hila mbaya zilizokuwa zinafanywa na ABDI SHEKIMWAGA. Kwa bahati mbaya sana ndugu SHEKIMWAGA alitoa maneno ya kashfa na dharau pamoja na kutumia lugha isiyofaa kwa viongozi na kuamua kugoma kujibu barua ya tuhama hizo.
Uongozi wa Kanda baada ya kupitia taarifa hizi na baada ya kufanya kikao cha pamoja na viongozi wa wilaya tarehe 21 Desemba 2013 huko wilaya lushoto mkoani Tanga, unamtangaza ndugu SHEKIMWAGA kuwa kwa kukinisuru chama dhidi ya tuhuma dhidi yake, kwa ajili ya kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kwa ajili ya hofu na kutokuwa na imani kulikoonyeshwa na viongozi na wanachama wenzake AMESIMAMISHWA KUWA MWENYEKITI WA CHAMA KUANZIA TAREHE 21 DESEMBA 2013. Hatua hii ni ya kuzingatia pendekezo la kamati tendaji ya wilaya/jimbo kwa mujibu wa ibara ya 6.3.4 (c), “amekoma kuwa kiongozi kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa masharti ya katiba, kanuni na maadili ua chama”.
Aidha uongozi wa kanda, unaliagiza baraza la uongozi la mkoa ambayo ndio mamlaka ya nidhamu kwa wilaya/jmbo kwa mujibu wa katiba ya chama ibara ya 6.3.6 (a) sehemu (iV) kuwa ndugu ABDI SHEKIMWAGA APEWE FURSA NYINGINE TENA akiwa katika hali ya kusimamishwa uongozi kwa kuandikiwa barua tena ya tuhuma dhidi yake na apewe muda wa kikatiba kujibu ama sivyo hatua kali zichukuliwe dhidi yake.
Tuhuma hizo ni;
        1. Kuamua kwa makusudi kuzuia na kukwamisha kazi za CHAMA, programu ya CHADEMA ni msingi. Ndugu SHEKIMWAGA ametoa maneno ya uzushi na upotoshaji kwa uwazi mbele ya viongozi wenzake na maafisa wa kanda kuwa hayuko tayari kufanya kazi ambayo yeyé aliitafsiri kuwa ina lengo la kumjengea mtu fulani mtandao ndani ya chama. Hii ni kinyume na kanuni ya maadili ya kiongozi na uendeshaji wa kazi za chama sura ya 10.1 (viii)
        2. Ametoa lugha na matamshi yenye kuonyesha udini na ukabila mbele ya viongozi wenzake na mbele ya maafisa wa kanda kuwa kaimu katibu wa CHADEMA mkoa wa Tanga ndugu Jonathan Leonard Baweje kuwa ni Mkristo na ametokea mkoa wa Kigoma hivyo hawezi kuwa katibu wa mkoa wa Tanga kwa sababu sio muislam. Hii ni dhambi mbaya sana na ni kinyume na kanuni ya maadili ya kiongozi na uendeshaji wa kazi za chama sura ya 10.1 (iv), “Kiongozi yoyote asijihusishe na vikundi vyovyote vyenye misingi ya ukabila, udini, au ukanda ambavyo vina makusudi ya kubaguana ndani ya chama au miongozi mwa jamii kisiasa au kijamii”.
        3. Amejitambulisha wazi mbele ya viongozi wenzake na mbele ya maafisa wa kanda kuwa yeyé yupo kundi la Zito Kabwe na atahakikisha CHADEMA inakufa Bumbuli iwapo maamuzi ya kamati kuu ya kumvua uongozi Zito Kabwe hayatabadilishwa. Kitendo hiki cha kujitengenezea makundi na upotoshaji ni kinyume na kanuni ya maadili ya kiongozi na uendeshaji wa kazi za chama sura ya 10.1. (iv), “Ni mwiko kwa kiongozi kujihusisha na upotoshaji wa maamuzi halali ya vikao vya chama”.
        4. Amezuia kwa makusudi kazi za chama na amekuwa akifanya hujuma dhidi ya viongozi wengine ambao wamekuwa wakifanya kazi za chama. Sambamba na hili ametuhumiwa kuwa anashirikiana na wapinzani wetu CCM katika kuhujumu chama na kwa kumwaga sumu na maneno ya uongo. Kitendo hiki kimekuwa sababu ya kuzuka kwa migogoro isiyokwisha katika jimbo la bumbuli na imeendelea kuvunja moyo na kuleta mifarakano inayorudisha nyuma kazi za chama. Jambo hili ni kinyume na kununi ya maadili ya uongozi na uendeshaji wa kazi za chama sura ya 10.1 (ix), “Kiongozi asijihusishe au kushiriki na vikundi au vitendo vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama au wanachama wake”.
    Taarifa hii inaenda sambamba na ndugu ABDI SHEKIMWAGA kukabidhi vifaa vyote vya chama, ikiwemo kadi za chama mpya zipatazo 400 zenye thamani ya Tshs 600,000 ndani ya siku TATU kuanzia tarehe ya taarifa hii kwa KATIBU WA CHADEMA MKOA WA TANGA.
    CHADEMA Kanda ya Kaskazini inaendelea kuonya kuwa haitavulia kabisa kuona CHAMA CHETU ambacho ni tumaini kwa Watanzania wengi kikivurugwa na watu wachache wenye hila mbaya na chafu. Aidha nitoe rai kwa WanaCHADEMA wote wa kanda ya kaskazini na Watanzania wapenda haki na kweli wasiwe na hofu yoyote na matukio haya ya kukisafisha chama maana hatuna budi kusafisha na kufukuza bundi wote waondoke.

    Imetolewa leo tarehe 23 Desemba 2013
    Amani Golugwa
    Katibu wa CHADEMA – KANDA YA KASKAZINI.
    Makao Makuu ya Kanda – Arusha, Tanzania:
    Simu: +255 754 912 914

UMEME BEI JUU JANUARI MOSI

$
0
0

Taarifa ya EWURA YA bei mpya za umeme zitakazoanza kutumika Januari, Mosi,2013.

Tarehe 11 Oktoba 2013, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liliwasilisha maombi ya kurekebisha bei ya umeme kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). TANESCO ilipendekeza kuongeza bei kwa asilimia 67.87 kuanzia tarehe 1 Oktoba 2013, asilimia 12.74 kuanzia tarehe 1 Januari 2014 na asilimia 9.17 kuanzia tarehe 1 Januari 2015.

Vilevile TANESCO waliomba kuidhinishwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya kitanzania. Aidha, TANESCO iliomba kuidhinishwa viwango vya gharama za kuunganisha umeme vinavyozingatia ruzuku inaliyotolewa na Serikali, na kuidhinishwa tozo mbalimbali kwa huduma zitolewazo na TANESCO.

Kwa mujibu wa TANESCO, kupitishwa kwa maombi haya kutaliwezesha Shirika (a) kupata fedha za uendeshaji na uwekezaji wa miundombinu, (b) kulifanya Shirika liweze kukopesheka na hivyo kuwezesha kupata mikopo yenye masharti nafuu, (c) kuliwezesha Shirika kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme kwenye Gridi ya Taifa, na (d) kuongeza uwezo wa 
kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya miundombinu iliyopo ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa huduma za umeme wa uhakika kwa wateja.

Itakumbukwa kwamba bei za umeme zinazotumika hivi sasa ziliidhinishwa mwezi Januari 2012. Bei hizo zilipanda kwa asilimia 40.29 ikilinganishwa na maombi ya TANESCO ambapo ilipendekeza bei zipande kwa wastani wa asilimia 155. Sababu ilikuwa ni kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kulikosababishwa na hali ya ukame katika maeneo yanayotiririsha maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme, toka mwaka 2011. 

Hali hiyo ilipelekea TANESCO kulazimika kununua umeme kwa gharama kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers). Hali ya maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme bado sio nzuri na hivyo TANESCO itaendelea kununua umeme kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers).


USHIRIKISHWAJI WA WADAU
Kulingana na Kifungu Na. 19(2) (h) cha Sheria ya EWURA, Mamlaka ilifanya Taftishi ili kupata maoni juu ya ombi la kurekebisha bei za umeme. Ukusanyaji wa maoni ulihusisha pia mikutano minne (4) iliyofanyika Iringa na Shinyanga tarehe 15 Novemba 2013, Bagamoyo tarehe 20 Novemba na kuhitimishwa Dar es Salaam tarehe 22 Novemba 2013. Aidha, tarehe 6 Desemba 2013, EWURA iliitisha mkutano wa mwisho wa wadau wakiwemo wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini(MEM), TANESCO, Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO), Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania, Baraza la Watumiaji na Baraza la Ushauri la Serikali, Umoja wa Wazalishaji wa Saruji wa Afrika Mashariki, na kiwanda cha ALAF. Katika mkutano huo EWURA iliwasilisha mwelekeo wa maamuzi kuhusu maombi ya TANESCO na namna zilivyokokotolewa. Wadau walipewa fursa ya kutoa maoni yao kuhusu mwelekeo wa bei na maoni yao yamezingatiwa katika kufikia maamuzi ya mwisho.
UCHAMBUZI NA UAMUZI
Kwa kufuata sheria na kanuni zinazoelekeza kuhusu uchambuzi wa bei ya umeme, EWURA ilifanya uchambuzi wa kifedha na kiufundi ili kubaini uwezo wa TANESCO katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku. Uchambuzi uliangalia utendaji wa Shirika la TANESCO katika miaka iliyopita na pia iliangalia majukumu yanayoikabili TANESCO katika miaka mitatu ijayo. EWURA imebaini kwamba hali ya kifedha ya Shirika la Umeme sio nzuri. Shirika limeendelea kupata hasara, ambayo iliongezeka kutoka shilingi bilioni 47.3 katika mwaka 2010 na kufikia shilingi bilioni 223.4 mwishoni mwa mwaka 2012. Pamoja na mapungufu ya kiufanisi, sababu kubwa ya ongezeko la hasara ni kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wa umeme ambao TANESCO inanunua kutoka kwa wazalishaji binafsi. Hali hii imelifanya shirika kushindwa kulipa madeni yake ya muda mfupi na ya muda mrefu, ambayo yamelibikizwa na kufikia TZS 456.8 bilioni tarehe 22 Novemba 2013, hali ambayo inatishia uendelevu wa huduma ya umeme hapa nchini.
Mamlaka imetumia Kanuni ya Ukokotoaji wa Bei kama ilivyopendekezwa na AF-MERCADOS wakati wa kukokotoa mahitaji ya mapato ya TANESCO. Kanuni hiyo inawezesha kukokotoa bei zinazolandana na gharama halisi kwenye mfumo wa umeme na kuzigawa kwenye makundi ya watumiaji umeme, kadiri kila kundi linavyosababisha gharama kwenye mfumo wa umeme kwa mujibu wa mahitaji ya Sheria ya Umeme ya 2008 Kifungu cha 23(2)(f).
EWURA imejiridhisha kwamba, ufumbuzi wa matatizo ya kifedha ya TANESCO, unahitaji njia/mikakati miwili itekelezwe kwa pamoja:
kuongeza bei ya umeme ili kufikia bei inayokidhi gharama halisi (Cost Reflective Tariff); na
TANESCO kupata mkopo wa gharama nafuu ama ruzuku kutoka Serikalini ili kulipa limbikizo la madeni ya Shirika.
Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, katika kikao chake cha tarehe 10 Desemba 2013 pamoja na mambo mengine, ilitoa maamuzi ya ongezeko la bei za umeme kwa viwango mbalimbali kwa makundi mbalimbali ya wateja, kama ifuatavyo:
Kundi D1: Hili ni kundi la wateja wadogo wa majumbani, hasa vijijini, ambao hutumia wastani usiozidi wa Uniti 75 kwa mwezi. EWURA imeongeza wigo wa mahitaji ya umeme na kufikia uniti 75 kwa mwezi, lengo likiwa ni kuongeza idadi ya wateja wa TANESCO wanaoweza kulipa kidogo kwa matumizi ya umeme kwa kiwango hicho, na pia kuwahamasisha kutumie zaidi umeme. Awali kundi hili lilikuwa linatunia wastani wa matumizi ya uniti 50 kwa mwezi. Bei mpya ni shilingi 100 kwa uniti moja, kutoka shilingi 60 za sasa, sawa na ongezeko la shilingi 40.
Kundi T1: Hili ni kundi la watumiaji wakubwa wa umeme majumbani, biashara ndogondogo, mashine za kukoboa na kusaga nafaka, taa za barabarani, mabango n.k. Bei iliyoidhinishwa ni shilingi 306 kwa uniti moja, ikiwa ni ongezeko la Shilingi 85 ya bei ya sasa. TANESCO ilipendekeza ongezeko la shilingi 131.
Kundi T2: Hili ni kundi la watumiaji umeme wa kawaida ambao hupimwa katika msongo wa volti 400, na ambao matumizi yao ya wastani kwa mwezi ni zaidi ya uniti 7,500 wateja wafanyabiashara kubwa, viwanda vya kati. Bei ya nishati iliyoridhiwa ni shilingi 205 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 73 ya bei ya sasa. TANESCO walipendekeza ongezeko la shilingi 145 ya bei ya sasa.
Kundi T3-MV: Hili ni kundi la wateja wakubwa kama viwanda vikubwa waliounganishwa katika msongo wa kati (Medium Voltage). EWURA imeidhinisha bei ya nishati kwa kiwango cha shilingi 166 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 45 ya bei ya sasa. TANESCO walipendekeza ongezeko la shilingi 148 kwa uniti moja.
Kundi T3-HV: Hili ni kundi la wateja wakubwa waliounganishwa katika msongo wa juu (High Voltage – Voti 66,000 na zaidi) ikiwa ni pamoja na ZECO, Bulyanhulu, na Twiga Cement. Bei iliyoidhinishwa ni shilingi 159 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 53 la bei ya sasa. TANESCO waliomba ongezeko la shilingi 80 kwa uniti moja.
Bei ya umeme itakuwa inarekebishwa kila baada ya miezi mitatu kulingana na mabadiliko ya kiwango na bei za mafuta; mfumuko wa bei, mabadiliko ya thamani ya fedha, na upatikanaji wa ruzuku toka Serikalini.
Vilevile, TANESCO inatakiwa kutekeleza miradi ya uwekezaji iliyoainishwa kwa kutumia fedha zitakazokusanywa kutokana na bei zilizoidhinishwa. EWURA inaweza kurekebisha bei ya umeme ya TANESCO kila mwisho wa mwaka 2014 na/au mwaka 2015 endapo TANESCO itashindwa kutekeleza miradi iliyotajwa katika Jedwali husika. Marekebisho hayo yatatokana na makadirio ya gharama za miradi ambayo haikutekelezwa.
Kutokana na matazamio ya kuwa na mabadiliko makubwa katika uzalishaji wa umeme (generation mix) katika mwaka 2015 na kuendelea, kutokana na matarajio ya kuongezeka kwa kwa upatikanaji wa gesi asilia, EWURA itafanya utafiti kubaini gharama halisi (Cost of Service Study) ya huduma ya umeme kwa wakati huo. Hivyo, bei zilizoidhinishwa zitatumika mpaka mwaka 2016, kama utafiti unaotazamiwa kufanywa hautakamilika kabla ya mwisho wa mwaka 2015.
EWURA ililinganisha bei za umeme kwa kila Uniti, katika nchi za Afrika ya Mashariki, na kuona kuwa bado bei za umeme za Tanzania zipo chini ukilinganisha na bei za katika nchi jirani kama inavyoonyeshwa hapa chini, kwa makundi mbalimbali ya watumiaji umeme.
Pamoja na maamuzi hayo, Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, pia iliagiza TANESCO kutekeleza yafuatayo:
  • kuzalisha umeme kwa kutumia mitambo yenye gharama nafuu ("least cost merit order") na kuwasilisha ripoti kwa Mamlaka katika kila mwezi ikionyesha uzalishaji halisi na mpango wa uzalishaji kama ilivyoidhinishwa na EWURA;

  • kuhakikisha kuwa zabuni za miradi ya uzalishaji umeme zinatolewa kulingana na mahitaji kama ilivyoidhinishwa kwenye Mpango wa Umeme wa Taifa (Power System Master Plan). Miradi yote mipya lazima ipatikane kwa njia ya ushindani kwa kufuata Sheria ya Umeme, "Public Private Partnership Act", Sheria ya Manunuzi ya Umma na Kanuni husika;

  • kuwasilisha ripoti kila baada ya miezi mitatu kuhusu viashiria vya takwimu za ubora na uhakika wa umeme (supply and reliability) katika misongo ya 11kV, 33 kV, 66 kV, 132 kV, na 220 kV kwa kila mkoa kwa ajili ya uhakiki. Takwimu husika zinatakiwa kuonyesha jumla ya masaa mteja aliyokosa umeme kwa kila njia ya umeme ("feeder"), kukosekana kwa umeme kulikopangwa (planned outages), na ambao haukupangwa (unplanned outages), idadi ya matukio ya kukosa umeme katika kila "feeder", idadi ya wateja wanaohudumiwa na kila "feeder", idadi ya wateja walioathirika na katizo la umeme katika kila "feeder" na kiasi cha umeme kilichokosekana kutokana na katizo hilo (total unserved energy in kWh);

  • kuwasilisha kwa Mamlaka, katika kipindi cha miezi mitatu baada kuanza kwa Agizo hilo la Mamlaka, mpango wa utekelezaji wa "Demand Side Management Programme" ili uidhinishwe;

  • kupunguza kiwango cha upotevu wa umeme (technical and non-technical losses) katika mtandao wa usambazaji kutoka asilimia 19 ya mwaka 2012 hadi asilimia 15.1 ifikapo mwisho wa mwaka 2015;

  • kubuni mikakati ya kupambana wizi wa umeme utokanao na uunganishaji umeme usio halali, na kuondoa ucheleweshaji usio wa lazima katika kutunganisha wateja wapya;

  • kuhamisha wateja walio katika kundi la D1 kwenda T1 endapo matumizi yao ya mwezi yatazidi uniti 75 kwa miezi mitatu mfululizo;

  • kuwasilisha kwa Mamlaka, kabla au tarehe 31 Machi, 2014, Mpango wa kuwawekea wateja wake mita za LUKU na AMR ili kupunguza wateja wanaotumia mita za zamani (conventional meters);

  • kuwasilisha kwa Mamlaka, kila baada ya miezi mitatu, taarifa/ripoti ya ukusanyaji wa madeni kutoka kwa wateja wake ili kuongeza mapato ya Shirika;

  • kutoa elimu kwa wateja wake kuhusu haki na wajibu wa wateja kwa mujibu wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja na kushughulikia kero za wateja kama inavyoelekezwa katika Mkataba husika na Kanuni za Umeme;

  • kuwasilisha kwa Mamlaka, maombi ya marekebisho ya bei yatokanayo na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na ubadilikaji wa thamani ya fedha; Ukokotoaji wa marekebisho hayo utakuwa kama ulivyoainishwa katika Kanuni za Kupanga Bei za Umeme za mwaka 2013 (Electricity (Tariff Setting) Rules, 2013);

  • kuendelea kutoa taarifa kwa Mamlaka kuhusu hali ya kifedha na kiundeshaji. Taarifa hizi zitatumiwa na Mamlaka katika kutathmini utendaji wa TANESCO ikilinganishwa na mashirika mengine ya umeme katika nchi jirani ili kuboresha utendaji wake. Tathmini hii pia itatumiwa na Mamlaka katika kubaini uhalali wa maombi ya baadae ya kurekebisha bei;

  • kuwasilisha kwa Mamlaka, kabla au tarehe 31 Machi 2014, mpango wa utekelezaji wa kila sharti katika Agizo la EWURA.

Bei mpya za umeme zitaanza kutumika tarehe 1 Januari 2014. Ni matarajio ya EWURA kwamba TANESCO watatumia fursa hii kutoa huduma bora zaidi za umeme na kuhakikisha kuwa wanashughulikia malalamiko ya wateja kila yanapojitokeza ili kurejesha imani kwa Shirika la Umeme la TANESCO.

TANZANIA,DIWANI WA KATA YA NYIDA SHINYANGA (CCM) AMEFARIKI KWA AJALI YA PIKIPIKI

$
0
0
SHINYANGA, Tanzania 
DIWANI wa Kata ya Nyida wilayani Shinyanga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Shindiko Masele(40) amekufa papo hapo baada ya kupinduka na pikipiki aliyokuwa akiendesha.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Mjini hapa, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Sosteness Ngassa alisema diwani huyo alipata ajali hiyo jumamosi saa 2.30 usiku wakati alipojaribu kumkwepa mwendesha baiskeli na kusababisha pikipiki yake kupoteza mwelekeo na ikagonga mti uliokuwa kando ya barabara.
 
Ngassa alisema baada ya pikipiki hiyo kugonga mti diwani huyo alianguka chini na kufa papo hapo huku abiria aliyekuwa amebebwa aliyetambuliwa kwa jina la Silasi Ngoni alijeruhiwa kidogo kwa kupata michubuko ambapo hata hivyo alikimbizwa katika hospitali ya serikali mkoani Shinyanga alikotibiwa na kuruhusiwa.
 
Makamu mwenyekiti huyo alisema kifo hcho  kilichotokea ghafla  kimewasikitisha na kwamba halmashauri yake imepoteza mmoja wa viongozi muhimu na ameacha pengo ambalo halitokuwa kuwa rahisi kuzibika kwa siku za hivi karibuni.
 
Alisema hivi sasa wanaendelea na maandalizi ya shughuli za mazishi ambapo mwili wa marehemu ulikuwa umehifadhiwa katika hospitali ya serikali mkoani Shinyanga na kwamba iwapo mipango itakwenda kama ilivyopangwa mazishi yake yalitarajiwa kufanyika leo mchana kijijini kwake Nyida.
 
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Annarose Nyamubi alisema amepokea kwa majonzi makubwa taarifa za kifo cha diwani huyo na kwamba alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa mstari wa mbele katika suala zima la uhimizaji wa maendeleo katika kata yake na usimamiaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
 
“Nimeshitushwa na taarifa za kifo cha diwani wetu wa kata ya Nyida, kwa kweli inasikitisha sana, maana ametutoka ghafla, ameacha pengo ndani ya halmashauri yetu na katika kata yake, alikuwa mstari wa mbele katika suala zima la uhimizaji wa maendeleo katika eneo lake ni wazi tutamkumbuka daima,” alisema Nyamubi.
 
Marehemu Masele alizaliwa mwaka 1973 wilayani Shinyanga na ameacha mjane mmoja na watoto watatu a ambapo wakati akipata ajali hiyo alikuwa akitokea Kata ya Isaka wilayani Kahama akirejea kijijini kwake Nyida.

LULU: MIMI NIMPE PENZI DIAMOND..!

$
0
0
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Stori:  Mayasa Mariwata
STAA kiwango katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekanusha uvumi uliozagaa mitaani kuhusu kutoka kimapenzi na mbabe wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Imekuwepo minong’ono ya muda mrefu kitaani kuwa, Diamond analilia penzi la Lulu lakini Diamond au Sukari ya Warembo alipoulizwa kuhusu hilo, alisema siyo kwamba analilia tu bali waliwahi kutoka (haijulikani kwenda wapi) naye, madai yaliyotupiliwa mbali na Lulu.

MADAI YA AWALI
Habari zilizotua katika meza zinasema kwamba, wawili hao wanafanya kazi za kisanii pamoja (haikuwekwa wazi ni kazi gani kati ya filamu au muziki) lakini tatizo lililopo kati yao ni Diamond kumtaka Lulu.

Chanzo kilichoomba hifadhi ya jina lake, kilifunguka: “Diamond anashindwa kuelewa, tatizo yeye kila mwanamke anataka kutoka naye. Mwenzake anajua yupo kazini, yeye anataka penzi, ndiyo mzozo uliopo kati yao.”
Wema Sepetu.
KAZI KWA DIAMOND
Paparazi wetu alimvutia waya Diamond ili kutaka kupata ufafanuzi kwa upande wake, ambapo aliposomewa maelezo yote alicheka sana kisha akasema: “Nililie penzi la Lulu? Acheni hizo... ngoja nikuambie kitu, siyo kulilia, mimi nimeshawahi kutoka naye. Nilitembea naye kishkaji tu kisha kila mmoja akaendelea na yake.

“Hayo mambo yalishapita na sikutaka kuyaongelea lakini kwa sababu naona kama yanakuzwa, ndiyo maana nimeamua kuweka wazi. Kwa sasa tunaheshimiana kama kaka na dada. Kuna ugumu gani mimi kuwa naye wakati nimeshampitia?”
Risasi: Unasema kweli Diamond?
Diamond: Wa asilimia mia moja.
Penny.
Risasi: Una ushahidi gani?
Diamond: Watu wanaojua hii ishu ni wawili tu; Wema (Sepetu) na Penny (Penniel Mungilwa). Niliwaeleza kwa uwazi kabisa hawa ili tusielewane vibaya. Kama huamini waulize. Hawa ndiyo niliowapa siri hii.
Paparazi wetu alijaribu kuwatafuta Penny na Wema kupitia simu zao za mkononi lakini hawakupokea.

TURUDI KWA LULU SASA
Akizungumza kwa sauti ya kujiamini, Lulu alimshangaa Diamond na kusema kwamba, si kutoka naye tu bali hana hata kazi anayofanya naye pamoja.

“Nawashangaa sana eti mimi nifanye kazi na Diamond, kazi gani sasa wakati mimi na yeye tupo kwenye fani tofauti? Muziki na  filamu wapi na wapi? Kifupi hayo madai hayana ukweli wowote na kila mtu yupo na yake,” alisema Lulu na kuongeza:
 
Lulu.
“Kwanza mimi siwezi kutoka na Diamond... levo zetu ni tofauti kabisa, wala hazilingani. Mimi nilianza kutoka kabla yake, nimeanza kujulikana toka kitambo hicho nina miaka mitano sijui hata kujifuta kamasi vizuri.... hakuna ukweli wowote.”

TUJIKUMBUSHE
Diamond amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na mastaa mbalimbali, huku madai hayo yeye mwenyewe akiyakubali, jambo lililosababisha aitwe Sukari ya Warembo.
Mbali na orodha ndefu aliyotoka nayo Diamond, kinachovuta hisia za wengi ni uhusiano wake wa sasa, ambapo haijulikana kama yupo na Penny, Wema au wote kwa wakati mmoja!

SHAMSA FORD AGOMA KUOLEWA

$
0
0
STAA wa filamu Bongo ‘Shamsa Ford’ amegoma kuolewa siku chache baada ya tarehe ya harusi yake kufika kwa madai kuwa mambo yalivyopangwa sivyo alivyotarajia.
 Shamsa Ford.
Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika, zinasema kuwa harusi ya Shamsa ilikuwa ifanyike kati ya Desemba 24 na 25, mwaka huu lakini aligoma kwa vile walikwenda kinyume na makubaliano ya tarehe husika.

“Unajua mwanzoni tarehe ilipangwa nyingine na Shamsa alijiandaa kwa siku hiyo, lakini wanafamilia ya mumewe mtarajiwa wakataka tarehe ibadilishwe ili wafunge siku moja na kaka wa mumewe mtarajiwa yaani shemeji yake ambaye naye pia alikuwa anaoa.

“Ndoa ya shemeji yake ilitakiwa kuharakishwa kwa sababu mchumba wake ana mimba tayari. Kwa hiyo sasa wanafamilia wakaona ni bora kufanya shughuli ya pamoja kwa kuwa wote ni ndugu.. Shamsa akagoma, akataka tarehe ileile waliyokubaliana,” kilieleza chanzo chetu.

Shamsa alipatikana kwenye simu na kufafanua ambapo alisema: “Mimi sikutaka mambo ya kuchanganya harusi mbili kwa wakati mmoja.

Ukizingatia hii ni ndoa yangu ya kwanza halafu leo hii eti tukafanyiwe shughuli pamoja, nitakosa uhuru na sherehe yangu. Mimi nina marafiki wengi ambao wameipania siku hiyo, ndiyo maana niliomba wao waoane kwanza siku hiyo sisi tupange tu mwakani.”

MESSI WA SIMBA AZAWADIWA GARI

$
0
0
KIUNGO nyota wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’ amepata baraka baada ya kupewa zawadi ya gari na mwanachama wa klabu hiyo.
Mwanachama wa siku nyingi wa Simba, Musley Luwah ambaye amekuwa karibu na klabu ya Simba tokea akiwa mtoto mwaka 1977, ndiye aliyetoa zawadi hiyo.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba zinaeleza mwanachama huyo amempa Messi gari aina ya Suzuki Carry 4WD ambalo kiungo huyo mwenye miaka 21 analitumia kumuingizia fedha.
 
“Unajua Muslah ni mtu anayependa sana maendeleo ya Simba, hivyo alivyoona Messi anajituma na ana nidhamu, akajitolea kumpa gari.

“Aliulizwa anataka gari ya aina gani, yeye Messi akachagua gari hiyo kwa ajili ya kubebea mizigo ili awe anaingiza fedha. Ameonyesha ana akili sana maana angekuwa mtu mwingine angechagua gari la kutembelea,” kilieleza chanzo cha uhakika.

Alipotafutwa Messi kuhusiana na hilo, alitoa ushirikiano ingawa hakutaka kulizungumzia sana suala hilo katika vyombo vya habari.
 
“Ulichosema ni kweli, Muslah ni mtu anayependa maendeleo ya Simba, pia amewasaidia watu wengi tu, ila mimi niliposikia gari ndiyo nikaamua kuchagua hilo la kubeba mizigo badala ya lile la kutembelea.

“Awali niliona kama utani, kweli imekuwa hivyo na ninamshukuru Mungu maana linaniingizia fedha kiasi. Lakini kwa kuwa sipendi makuu, wengi hawajui hata kama nina gari, hivyo sipendi kuzungumza sana suala hili hapa,” alisema.
Juhudi za kumpata Muslah hazikuzaa matunda kwa kuwa ilielezwa yuko nchini Oman ambako hufanya kazi zake na kuendesha maisha yake lakini pia hapa nchini ana kampuni zake hivyo atarejea hivi karibuni.

Messi alionyesha uwezo mkubwa katika mechi ya Jumamosi iliyopita wakati Simba ilipoivaa Yanga katika mechi ya Nani Mtani Jembe na kushinda kwa mabao 3-1, kiungo huyo akiwa kati ya waliong’ara.
Alisababisha penalti baada ya kunyanyasa beki David Luhende lakini akasababisha Kelvin Yondani apewa kadi nyekundu baada ya kumtoka naye akamfanyia faulo na kupewa kadi ya pili ya njano iliyozaa nyekundu.

YANGA YAKAA KIKAO NA KASEJA KWA SAA TATU

$
0
0
BAADA ya kutua Yanga KOCHA wa makipa wa Yanga, Razack Siwa, amesema alitumia zaidi ya saa tatu kumweka sawa kisaikolojia kipa Juma Kaseja siku moja baada ya mechi dhidi ya Simba.
 Kipa mpya wa Yanga, Juma Kaseja.
Kaseja alitupiwa lawama kibao kutoka kwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kutokana na kuruhusu bao jepesi kwenye mechi dhidi ya watani wao, Simba, Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na matokeo kumalizika kwa Simba kushinda 3-1.

Akizungumza Siwa, raia wa Kenya, alisema baada ya mechi hiyo kumalizika siku iliyofuata alimuita
Juma na kukaa naye kujadili hasa kuhusiana na bao la tatu ambalo lililalamikiwa na kila mtu.

“Nilikaa na Juma baada ya mechi kwa saa tatu nikamwambia ni sehemu ya mchezo na anatakiwa kuwa sawa lakini pia kama kocha niliumizwa sana na lile bao la tatu alilofungwa na sasa namfanyisha mazoezi ya mtindo kama wa bao hilo tulilofungwa,” alisema Siwa.

Kaseja alifungwa bao hilo baada ya kugeuka na mpira aliokuwa amepasiwa langoni mwake na ndipo kiungo mshambuliaji wa Simba, Awadhi Juma, alipounasa na kufunga bao safi kwenye mchezo huo wa kirafiki maarufu kama ‘Nani Mtani Jembe’.
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live