Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all articles
Browse latest Browse all 12768

Kanga Moja Kiunoni... MBENGEMBEGE - 24

$
0
0
 
ILIPOISHIA: “Haa! Haa!” mzee Hewa alianza kuonesha uchu wake kabisa. Alimfuata na kumkumbatia kwa kumuweka kifuani mzimamzima. Mama Mei hakutaka kuonesha kwamba, hajakubali kukumbatiwa, akatoa ushirikiano kwa yeye naye kumkumbatia. “We mama Mei,” sauti ya baba Mei iliita kwa nguvi mlangoni... kwake akiwa amesimama... JIACHIE MWENYEWE SASA...
MAMA Mei aliruka kutoka sehemu aliyosimama na kwenda kusimama sehemu nyingine na kusema... “Mungu wangu.” Mzee Hewa yeye alichoka kabisa, miguu ilianza kunyong’onyea yenyewe kwani alijua kuna kosa amelifanya... “Ilitakiwa nisubiri mpaka masaa yapite mengi ndiyo ningemuita ndani huyu mwanamke, nimefanya makosa sana,” alisema moyoni mzee huyo. Baba Mei aliendelea kuita akiwa ndani kwake sasa. Alishangaa kutomwona mkewe ndani, hadi chumbani. Mlio wa milango ilisikika ikifunguliwa ndani hali ambayo ilizidi kumuumiza mama Mei. “Sasa mzee Hewa itakuaje? Maana sijui kwa nini baba Mei amerudi?” alisema mama Mei akitetemeka. Hali ilizidi kuwa tete baada ya Mfaume naye kurudi muda huohuo na kukutana na baba Mei akitoka ndani kwake huku akiendelea kuita akienda uani... “Za saa hizi kaka?” alisalimia Mfaume... “Njema bwana...huyu sijui ameenda wapi? Kuna maagizo nataka kumpa nilisahau,” baba Mei alisikika akisema... “Au kaenda dukani...maana mimi nilimuacha wakati natoka kwenda kazini na nimerudi mara moja kuna kitu nimesahau,” alisema Mfaume akiwa hana shaka kwamba, mama Mei anaweza kuingia ndani kwa mzee Hewa. Ni kweli, kurudi kwa baba Mei muda huo ambao ni dakika chache baada ya kuondoka hakuingiliani na mpango wake wa kumuweka mtegoni mkewe huyo. Alitoka hadi nje akasimama akishikashika simu yake. Hakumpigia simu mkewe kwani aliikuta chumbani. Lakini kwa mbali, baba Mei
alihisi jambo. Ni baada ya dakika tano kupita bila mama Mei kurudi. Alirejea tukio la mwenye nyumba wake huyo na kwenda kugonga mlango wake jana yake usiku... “Au...mh! Inawezekana kweli? Kwamba awe ameingia ndani kwa mzee mwenye nyumba?!” aliwaza mwenyewe baba Mei akiwa bado amesimama pale nje. Aliamua kurudi na kukaa sebuleni mahali ambapo, mkewe hata kama angekuwa amekwenda mkoani, ili arudi ilikuwa lazima apitie pale! Mfaume aliondoka zake akiwa hana hili wale lile kwake aliamini mama Mei alikwenda dukani au gengeni ambako angerudi na kumkuta mumewe amesharudi. “Mzee Hewa, itakuaje sasa? Mimi nahisi kuna mambo mazito sana,” alisema mama Mei kwa sauti ya chini kabisa wakiwa chumbani sasa maana pale sebuleni walipokuwa awali pasingewezekana. “Naona mimi nitokee nikaangalie mazingira, maana kama kuna ukimya au wewe unasemaje?” alishauri mzee
Hewa... “Mh! Mkionana hawezi kujua kitu kweli?” mama Mei aliingia shaka kidogo... “Hawezi! Ataingiaje shaka wakati hajui kama upo kwangu?” “Haya nenda basi.” Mzee Hewa alitoka na wakati akifungua mlango wake, baba Mei alisikia, akatoka haraka kumchugulia... “Kumbe wewe mzee, namtafuta mama Mei, kuna maagizo nataka kumpa. Sijui kaenda wapi?” aliuliza baba Mei... “Labda kaenda shamba...Eh! Sorry kwani na yeye alikuwa hasafiri? Aah! Mimi naye, siku mbili hizi sijui nikoje! Nilitaka kukwambia huenda amekwenda dukani baba Mei.” “Mh!” Baba Mei aliguna kwanza, hakujua ni kwa nini mzee Hewa huchanganyikiwaga akiongea na yeye. Mzee huyo alipitiliza  mpaka nje, lakini hakuchukua muda, akarudi mpaka ndani kwake. Akafunga mlango kwa woga, akaenda mpaka chumbani kwake huku akihema... “Vipi mzee Hewa?” mama Mei alimuuliza... “Yaani mambo ni mazito sana binti...” “Kivipi?” “Nimejichanganya tena...” “Kivipi mzee Hewa jamani?”“Nimekutana na mumeo, akaniuliza wewe umekwenda wapi, kuna maagizo anataka kukupa, alisahau, nikamwambia labda umeenda shamba... akaguna!” “Jamani jamani mzee Hewa... sasa mimi tangu lini nikaenda shamba hapa mjini. Hata kama lingekuwepo kweli hilo shamba, ningeenda muda huuhuu wakati yeye ametoka?” “Nisamehe sana binti.” Mama Mei alianza kulia. Mumewe kule sebuleni, alibaki amekaza macho akiwaza hili na lile. Shaka kuhusu mzee Hewa iliongezeka mara dufu. Aliamini kwa asilimia tisini na tano kwamba, mkewe alikuwa ndani kwa mzee huyo kwa alivyomsoma. Hata kama angeambiwa aweke pesa ya mshahara kupingana na mtu kwamba, mkewe hakuwemo ndani kwa mzee Hewa, angekubali kuweka akijua yeye angeibuka mshindi... “Lakini tabu yote ya nini wakati sasa ukweli umejiweka wenyewe kuhusu mke wangu. Kwa nini nisiende kumgongea yule kikongwe nimwambie nina wasiwasi mke wangu yumo chumbani mwake? Akigoma nimlazimishe kuingia hata kwa mabavu, maana hana nguvu za kinizuia!” alisema moyoni baba Mei na kusimama kwenda. Alifika mlangoni, akagonga na kuita... “Ngo ngo ngo! Wenyewe!”
ITAENDELEA

Viewing all articles
Browse latest Browse all 12768

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>