Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all articles
Browse latest Browse all 12768

Mlima Kilimanjaro watunukiwa zawadi ya kivutio kikuu

$
0
0

Mlima Kilimanjaro.
MLIMA Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi barani Afrika, umetangazwa kuwa kivutio kikuu cha utalii katika bara katika mwaka 2016.
Hili lilitangazwa katika hafla ya taasisi ya masuala ya utalii Afrika na eneo la Bahari ya Hindi ijulikanayo kama World Travel Awards Africa and Indian Ocean  iliyofanyika Zanzibar wiki iliyopita.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) jana ilisema hafla hiyo ilihudhuriwa na mamia ya viongozi wa masuala la utalii iliyoandaliwa na kampuni ya Diamonds La Gemma Dell’est na kufanyika huko  Nungwi, Zanzibar, Jumamosi iliyopita.
“Bodi ya Utalii ya Tanzania, imepokea kwa heshima kutangazwa Mlima Kilimanjaro kuwa ndiyo kivutio kikuu cha utalii barani Afrika.  Uteuzi huu ni dhahiri utachangia juhudi zetu za kuendeleza utalii nchini Tanzania, hususani kwa kuufanya ulimwengu ufahamu kwamba Tanzania ndiyo mmiliki wa Mlima Kilimanjaro ambalo ni kivutio kikuu barani Afrika,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.
Source:Allafrica.com

Viewing all articles
Browse latest Browse all 12768

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>