MAMBO hadharani! Siku chache baada ya Miss Tanzania 2006/07 ambaye pia ni supastaa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Abraham Sepetu kujigamba amenunua kwa pesa zake gari jipya aina ya Range Rover Evoque 504 lenye thamani ya dola za Kimarekani elfu 90 (karibia shilingi milioni 200), siri kubwa imevuja kuhusu gari hilo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kiliomba kuhifadhiwa jina ili kisionekane kimbeya, gari hilo la kifahari halijanunuliwa na Wema bali amepewa na mwanaume mmoja Mkongo ambaye awali, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa mwingine wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper Massawe.

MSIKIE HUYU
“Jamani nataka kuwapa umbeya lakini naomba msinitaje! Sawa?”
Amani:“Sawa, lete habari ya huo umbeya wako.”
Chanzo:“Mliandika kwamba, Wema amenunua gari la Range sijui. Mkasema amelinunua kwa shilingi kama milioni mia mbili.”
Amani:“Sawasawa kabisa. Lete maneno.”
Chanzo:“Sasa mimi nina habari kwamba, lile gari Wema amepewa na yule mwanaume aliyewahi kuwa mpenzi wa Jack Wolper.”
KACHEZEWA KAMA WOLPER?
“Lakini mimi naogopa sana kwani kuna habari zinasambaa kwa kasi kwamba, ndani ya miezi miwili, Wema hatakuwa tena na hilo gari. Litarudishwa kwa mhusika.
“Nasikia lile gari, kwanza ni kweli ni jipya. Lakini liko kwa dalali sokoni. Sasa watu wanaojua habari za mjini wanasema kuwa, Mkongo aliongea na dalali, wakaelewana kwa kumpa pesa kidogo, ikatengenezwa dokyumenti ambazo zinamwonesha Wema ni mmiliki halali wa gari.
“Nadhani wanaposema Wema hatakuwa na lile gari kwa miezi miwili mbele, huenda watamchezea kama alivyochezewa Wolper mwaka ule na lile gari alilohongwa na yule jamaa yake, Dallas (Abdallah Mtoro). Wolper alipewa gari na dokyumenti zake, kumbe lilikuwa mazabe,” kilisema chanzo hicho.

Kama kilivyosema chanzo kuwa, kisitajwe ili kisije kikaonekana ni kimbeya au kinasema uongo, ili kuweka sawa mizani ya habari hii, Amani lilimsaka Wema kwa njia ya simu na kumuuliza.
Wema alisomewa mashtaka yote mpaka mwisho kwa kuambiwa hajanunua yeye lile gari bali lina nguvu ya mkono wa mwanaume ambapo naye alifunguka kidogo kwa kusema:
“Ni kweli, inawezekana kuna mkono wa mtu mwingine lakini mimi nitakupigia baadaye kidogo ili tuongee vizuri,” alisema Wema kwa kifupi kisha akakata simu.
SIKU ZAKATIKA
Hiyo ilikuwa ni Jumatano ya Novemba 4, 2014. Ilipofika Jumatatu ya Novemba 9, mwaka huu, mwandishi aliamua kumpigia simu Wema, hakupokea.
Jumanne, juzi, mwandishi alimpigia simu tena lakini si tu kwamba hakupokea, bali zaidi sana hakuwa hewani kabisa mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni.
WOLPER SASA
Amani liliamua kumsaka Wolper kwa njia ya simu na kumuuliza kama ana habari za Mkongomani wake kumpa gari Wema ambapo alisema:
“Mimi nitajulia wapi jamani! Sijui lolote lile. Kwanza huyo Mkongo mnayemsema sijui yuko wapi siku hizi. Ana maisha yake na mimi nina maisha yangu. Teh...tehe...teheee...”
TURUDI NYUMA
Novemba Mosi, mwaka huu, Wema aliangusha bethidei ya nguvu iliyofanyika kwenye ukumbi mmojawapo ndani ya Jengo la Millennium Tower jijini Dar.
Katika hafla hiyo, Wema alishika kipaza sauti na kusema: “This is my new brand car, yaani ni jipya la mwaka 2015. Hakuna kenge yeyote anayeweza kufuata nyendo zangu. Na yule ambaye alikuwa akijigamba eti alinipa zawadi ya gari la elfu 30 nini na nini na hili aseme sasa, maana mimi si wa kuhongwa kila kitu.”
Akaendelea: “Naomba niwaambie kuwa, hadi nalifikisha hapa, hili gari nimetumia zaidi ya dola elfu 90 za Kimarekani. Sijahongwa na mtu, ni pesa zangu kwa nguvu zangu mwenyewe. Nawaomba mpande ndani mshuhudie ziro kilometa (halijatumika).”
Kauli hiyo ilionesha wazi kumlenga Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye aliwahi kumzawadia Wema gari (Nissan Murano) lenye thamani ya shilingi milioni 30 miaka miwili iliyopita.
CHANZO: GPL