Quantcast
Channel: Rogers Linky - Sports Home
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live

Wanafunzi 7,000 Watimuliwa UDOM

$
0
0

Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kimewasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi 7,000 wa kozi maalumu ya ualimu wa sayansi kwa ngazi ya stashahada na kuwataka waondoke chuoni hapo mara moja.

Jana, lilitolewa tangazo chuoni hapo likiwataka wanafunzi hao kuondoka kati ya jana hadi leo saa 12 jioni. Tangazo hilo lilieleza kuwa kutokana na matatizo yaliyopo katika ufundishaji wa stashahada hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imeamua wanafunzi hao kurejea majumbani na wataelezwa mustakabali wao “mapema iwezekanavyo”.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula alipotakiwa kufafanua suala hilo, alisema kwa ufupi kuwa suala hilo lipo lakini akaelekeza apigiwe simu Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Beatrice Baltazal kwa maelezo zaidi.

Baltazal alipotafutwa alisema kusimamishwa kwa wanafunzi hao kulitokana na agizo la Serikali na wametakiwa kulitekeleza.

Kuhusu lini na nini hatima ya wanafunzi hao, alisema bado hawajui hadi hapo watakapoelekezwa vinginevyo.

Hata hivyo, kulikuwa na malalamiko kwa wanafunzi hao juu ya namna walivyopewa taarifa za kusimamishwa masomo yao kwa ghafla na kutakiwa kuondoka.

Kozi ya stashahada ya ualimu wa sayansi, ilianzishwa maalumu kwa agizo la Rais Jakaya Kikwete kwa lengo la kuziba pengo la walimu wa sayansi na ilikuwa inatolewa UDOM pekee.

Waliokuwa na sifa za kujiunga na kupewa mikopo ni wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na kufaulu vizuri masomo ya sayansi. 
Wanafunzi hao waliokuwa wamekopeshwa na Serikali wamesimamishwa siku mbili baada ya wenzao zaidi ya 480 wa Chuo Kikuu cha St. Joseph kusimamishwa baada ya kubainika hawakuwa na sifa za kudahiliwa. 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya May 29, 2016

Makamu Mkuu wa Shule Atiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kumlawiti Mwanafunzi Wake

$
0
0


MAKAMU Mkuu wa Shule ya Sekondari Usevya katika Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele , Makonda Ng’oka “Membele” (34) amefikishwa katika Mahakama ya mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake.

Mshtakiwa huyo alifikishwa juzi mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Chiganga Tengwa ambapo alikana shitaka lake na yupo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kulipa kiasi cha Sh 3,000,000 mahakamani.

Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali, Gregory Mhangwa alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo katika shule ya sekondari Usevya kati ya Novemba 2015 na Aprili 2016.

Alieleza mahakamani hapo kwamba katika kipindi hicho mshtakiwa alimuingilia mwanafunzi wake huyo kinyume cha maumbile. Hakimu Tengwa aliahirisha shauri hilo hadi Juni 26 , mwaka huu litakapotajwa tena.

Inadaiwa kuwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Makamu Mkuu huyo wa shule hiyo kunafuatia wanafunzi wa kiume wanaosoma Kidato cha Tano katika shule hiyo kumkataa na kutishia kuandamana kupinga vitendo vyake vya kuwalawiti wanafunzi wake.

Kufuatia msimamo wa wanafunzi hao iliwalazimu Ofisa Elimu mkoa wa Katavi, Everest Hunji na Mkurugenzi Mtendaji Halmashari ya Mpimbwe wilayani Mlele, Evaristo Kiwale kufika shuleni hapo Jumatatu jioni na kuzungumza na wanafunzi hao.

Wanafunzi hao walidai kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwalawiti baadhi yao ikiwa ni adhabu mbadala wanapobainika kufanya makosa shuleni hapo. 
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe, Kiwale alisema vitendo vya ushoga havikubaliki na kwamba tayari hatua stahiki zimeshachukuliwa za kumpeleka katika vyombo vya kisheria. 
“Msitaharuki mnapomuona mwalimu huyo mitaani msidhani hajachukuliwa hatua yoyote ile,” alisisitiza.

Maalim Seif Atikisa Zanzibar, Mabomu Yarindima Kuwatawanya Wafuasi Wake

$
0
0

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad jana aliitikisa Zanzibar pale alipoanza ziara yake ya siku sita katika Wilaya ya Kaskazini A na kusababisha polisi kuwatawanya wafuasi wake kwa mabomu na risasi huku baadhi wakijeruhiwa.

Wakati wa ziara hiyo, shughuli za biashara zilisimama kwa muda ili kupisha ziara ya Maalim Seif na mamia ya wananchi wake kwa waume walimpokea na kumfuata kila alipoelekea.

Ulinzi uliimarishwa katika maeneo yote ya Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati wote wa ziara hiyo na vikosi vya ulinzi na usalama vilionekana vikipiga doria kila mahali.

Akiwa Kinyasini, Jimbo la Chaani ambako alifanya kikao cha ndani, wakazi wa eneo la Kivunge kwa mamia walianza kujikusanya katika maeneo ambako Maalim Seif alitarajiwa kutembelea huku wakijipanga barabarani kumsubiri kiongozi huyo. Hata hivyo, askari wenye silaha waliwatawanya.

Katika kuwatawanya, polisi walitumia mabomu ya machozi na risasi hali iliyosababisha kizaazaa kwa takriban dakika 30 katika eneo la Kivunge kabla ya kurudi hali ya kawaida.

Baada ya hapo baadhi ya askari waliokuwa na silaha waliwazuia waandishi kusogelea eneo hilo wala kuwapiga picha majeruhi.

Mkazi wa Kivunge ambaye alidai ni miongoni mwa watu waliopatwa na mkasa huo, Omari Makame (32) alisema, “Sisi tumejipanga kwa heshima zote kumsubiri kiongozi wetu kipenzi cha Wazanzibari, tukiimba kwa furaha lakini ghafla tumepata kipigo na mabomu ya machozi, nini hiki kama siyo chuki na choyo kibaya.”

Mkazi mwingine, Haji Omar (27) alisema hata baada ya kuwajeruhi wenzao, polisi wali wakatalia kuwapa fomu za kwenda kupata matibabu na hata walipopelekwa hospitali ya Kivunge, polisi walifika na kuwachukua kwa nguvu.

“Wamekataa ushauri wa madaktari wa hapa kwamba wawapeleke Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja, lakini wamewachukua kwa nguvu wamekwenda nao Kituo cha Polisi Mkokotoni,” alisema Omar.

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msangi alikiri kuwapo kwa tukio hilo akibainisha kuwa yote hayo yanatokea kwa sababu kuna watu hawataki kufuata sheria, lakini akasema Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Hassina Tawfik ndiye mwenye nafasi ya kufafanua zaidi.

Juhudi za kumpata Tawfik hazikufanikiwa ikielezwa na baadhi ya watendaji wa ofisi yake kuwa bosi wao hapatikani na hawakuwa na mawasiliano na yeye.

Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu wa CUF, Pavu Juma Abdalla alifika katika Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja na kushuhudia majeruhi hao wakiwa mikononi mwa polisi.

Waliojeruhiwa ni Makame Abdalla Makame (28), mkazi wa Kivunge Bondeni na Shaame Juma Haji (45) mkazi wa Tumbatu Chwaka.

“Tunapigwa kwa sababu ya umma kuonyesha mapenzi kwa Maalim Seif, wangelikuja watu wa vyama vingine wasingelipigwa lakini ipo siku hawa jamaa wataheshimu haki zetu,” alisema mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Haji akisema baadhi ya majeruhi ni ndugu zake.

Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Salim Bimani ambaye alifika hospitali kuwaona majeruhi alisema:“Wenye mabomu na risasi wamewahujumu watu bure kwa sababu za chuki lakini yote hayo yana mwisho.”. 
Bimani alisema Chama chake kinalaani kwa nguvu zote uonevu na hujuma hizo walizo tendewa wananchi wasiokuwa na hatia.

“Tunatumia pia kumbukumbu za hujuma hizi za leo kuongeza ushahidi wa kesi yetu tutakaouwasilisha ICC,” alisema Bimani.

Ziara yenyewe 
Maalim Seif alianza ziara hiyo ya kwanza Unguja tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio aliosusa kushiriki katika eneo la Kinyasini, Chaani na kupokewa na mamia ya wafuasi wake ambao walikuwa wakiimba “rais! rais! rais!

Aliambatana na viongozi na watendaji wa CUF, akiwamo Naibu Katibu Mkuu, Nassor Ahmed Mazrui; Bimani; Pavu Abdalla na Mkurugenzi wa Mipango na Chaguzi, Omar Ali Shehe.

Aliondoka Kinyansini kuelekea Gamba, Mkwajuni ambako mamia ya wananchi waliokuwa wakimshangilia walijipanga barabarani na walionekana kuongezeka kadri alivyoelekea Kaskazini na kukaribia Jimbo la Mkwajuni.

Baadaye Maalim Seif aliwahutubia wajumbe wa kamati mbalimbali za wilaya na majimbo akieleza kile alichosema ni mwelekeo wa kisiasa wa chama chake, Zanzibar na Tanzania kwa jumla.

Alisema dunia ilishuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki na demokrasia visiwani humo, akidai kwamba pamoja na maonyo ya jamii mbalimbali za kitaifa na kimataifa, watawala waliamua kupora uamuzi wa mamlaka halali ya wananchi kupitia masanduku ya kura ya Oktoba 25, 2015.

“Angalieni watu hawa walivyokosa aibu, umma uliwakataa, mataifa yaliwakataa hata kuwanyima misaada lakini bado hawakuonyesha dalili za kujali kutokana na dhulma waliyotenda.

“Nasema hali hii haitupeleki pema sisi na Taifa kwa ujumla maana iliyoporwa ni haki ya umma na haiwezekani kuisamehe dhambi hii, hivyo mwishowe si mwema na dhuluma haiwezi kudumu kwa muda mrefu asilani, sasa kusema hivyo kuna ubaya gani?”

Hata hivyo, Mwangalizi Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU – EOM) kwa Tanzania, Judith Sargentini amesema atawasilisha ripoti kamili na mapendekezo ya umoja huo, kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana Alhamisi ijayo.

Maalim Seif aliwataka wananchi wote, kama walivyoikataa CCM kabla ya uchaguzi, wakati na baada ya kupiga kura Oktoba mwaka jana, kuunga mkono juhudi na mikakati ya CUF, ili kuhakikisha haki inapatikana, uamuzi wao unaheshimiwa, kwa masilahi ya nchi na Taifa kwa jumla.

Viongozi wa chama hicho Wilaya ya Kaskazini A, walimhakikishia Maalim Seif; “sisi tuko tayari kwa lolote, na naona siyo sisi pekee, kwa sasa kila mtu anaisoma namba, tutakuwa bega kwa bega mpaka haki yetu ipatikane,” alisema Makame Bakari, mmoja wa makatibu wa CUF.

PICHA 10: Miss Arusha 2016 alivyopatikana na burudani kutoka kwa Navy Kenzo

$
0
0

Usiku wa May 28 2016 ilikuwa ni siku ya kumtafuta Miss Arusha 2016 ambaye amerithi Taji lililokuwa likishikiliwa na Miss Arusha 2014 Lilian Kamanzima ambaye pia ndiye Miss Tanzania kwa sasa, mchuacho ulianza kwa washiriki 17 hatimaye washiriki wakabaki watano ambapo Maurine Ayubu amenyakua taji hilo la Miss Arusha 2016/2017, Usiku huo burudani ya nguvu ilidondoshwa na wakali kutoka kundi la Navy Kenzo.
.
Miss Tanzania 2014, Lilian Kamanzima
.
Navy Kenzo Back Stage
.
.
.
Navy Kenzo
.
Miss Tanzania 2014, Lilian Kamanzima
.
Miss Tanzania 2014 Lilian Kamanzima
.
.
.
Mshindi wa taji la Miss Arusha 2016, Murine Ayubu
.
.
.

Video: Miss IFM kwa mwaka 2016 alivyopatikana na burudani kutoka kwa Navy Kenzo

$
0
0
Usiku wa May 27 2016 ndio ilikuwa siku ya chuo cha usimamizi wa fedha (Institute of Financial Management) kumtafuta mrembo atakayerithi taji la umiss lililokuwa linashikiliwa na Miss IFM 2015 Sophia Basil Macha, mchujo ulifanyika na kupatikana TOP 5 na hatimae Glory Gideon akafanikiwa kushinda taji hilo.

Wema aweka wazi kuhusu mimba, alivyojigundua mpaka ilivyoharibika ‘nikaona donge la damu likidondoka’

$
0
0
Inaonekana somo la uzalendo limewaingia vyema mastaa wetu licha ya tofauti zao. Baada ya hivi karibuni Alikiba kuwaomba watanzania wampigie kura Diamond anayewania tuzo za BET, Wema Sepetu naye amefanya hivyo.

Wema ametumia Instagram kuwaambia mashabiki wake wampigie kura ex wake huyo aliyetajwa kuwania kipengele cha Best International Act: Africa.

“Uzalendo ndo unaotakiwa… Tanzania Kwanza Vingine Baadae… Ama nene…? Vote Vote Vote….,” ameandika Wema kwenye picha ya BET Awards aliyoiweka Instagram.

Mashabiki wengi wamempongeza kwa uzalendo huo aliounesha licha ya yeye na Diamond kuwa mbali kwa sasa kutokana na kila mmoja kuwa na maisha yake. Wema na mpenzi wa sasa wa Diamond ni paka na panya.

Diamond anachuana na mastaa wengine wa Afrika wakiwemo Wizkid, Yemi Alade, AKA, Cassper Nyovest na wengine wawili.

Hii ni mara ya pili kwa muimbaji huyo wa Make Me Sing kutajwa kuwania tuzo hizo kubwa duniani.

Wema aweka wazi kuhusu mimba, alivyojigundua mpaka ilivyoharibika ‘nikaona donge la damu likidondoka’

$
0
0
Mashabiki wa malkia wa filamu, Wema Sepetu pamoja na wadau wa burudani walikuwa bado wanamaswali mengi kuhusu mimba ya Wema Sepetu huku wengine wakihisi labda zilikuwa ni kiki, lakini Jumamosi hii staa huyo amefunguka kinagaubaga kuhusu sakata hilo.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Wema alikiri kwamba ni kweli alikuwa ni mjamzito.

“Nilikuwa na ujamzito kweli,” alisema Wema. “Mwezi wa 12 mwaka jana, nilikuwa najihisi kuongezeka uzito, hivyo nikaenda kwa daktari kwa lengo la kusafisha kizazi. Nilipofika kwa dokta nilimwambia hata hivyo nimemisi period, akaniambia ya Mungu mengi pengine nime-concive, nilimkatalia katakata.”

Wema anaendelea kwamba daktari alimshauri akanunue kipimo cha ujauzito ajipime haja ndogo atakapoamka asubuhi na asile kitu chochote kwa ajili ya zoezi la kusafisha kizazi.

“Nilipokuwa narudi nyumbani nilipitia dukani na kununua kipimo hicho na asubuhi nikafanya hivyo, nilishtuka sana, nilikuwa kama nimewehuka nilipoona mistari miwili katika kipimo, siku zote nilizoea kuona mstari mmoja. Nikawauliza rafiki zangu nikiwa katika hali ya furaha baadaye nikampigia daktari nikamwambia nimepima lakini sielewi ninachokiona maana kuna mistari miwili, aliniambia niende na kipimo hicho na akanihakikishia kwamba nilikuwa na ujauzito, sikutaka kumwamini, nikamtaka anipime, hapo ndipo nilipothibitisha, nilisema sasa watanikoma,” anasema.

Baada ya fuhara ya muda mchache akisubiria kupata mtoto, aliona dalili mbaya katika mwili wake.

“Siku ambayo sipendi kuikumbuka ni ile niliyokwenda msalani kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo kisha nikaona donge la damu likidondoka, nilichanganyikiwa kwa kuwa daktari aliniambia sikutakiwa kuona damu. Nilipompigia mama yangu naye alinilaumu sana badala ya kunipa pole aliniambia, ‘Wema nilikuambia mimba haitangazwi!, unaona sasa kilichotokea, niliyajua madhara ya kufanya hivyo!”

Wema alisema alikwenda kwa daktari akiwa na Idris kuthibitisha ni kweli ujauzito ulikuwa umetoka na ulikuwa na wiki 13.

Wema anasema, daktari alimwambia ndugu yake mwingine aliyeambatana naye kwamba ujauzito huo ulikuwa ni wa watoto wawili, yaani pacha.

Source: Mwanaspoti

Serikali yatangaza kuisafisha Sekta ya Elimu na Watumishi wa umma wenye vyeti bandia

$
0
0
Serikali imetangaza rasmi kuanza kwa kampeni ya kuwashughulikia na kuwaondoa katika utumishi wa umma watumishi wote walioajiriwa katika  sekta hiyo  wakitumia vyeti bandia .

Aidha, imewataka watumishi hao waanze kujitathmini na kuanza kujiondoa wenyewe kabla ya kufikiwa na mabadiliko makubwa ya kusafisha sekta ya elimu na utumishi wa umma yanayokuja nchini.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof.Joyce Ndalichako wakati wa majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Amesema Serikali ya awamu ya tano imejipanga kufanya mabadiliko makubwa katika Sekta ya Elimu nchini ili kuhakikisha kuwa Elimu inayotolewa katika shule, vyuo na taasisi mbalimbali inazalisha wahitimu wenye sifa na ubora kwa maslahi ya Taifa .

Amesema katika kulitimiza hilo Serikali itawachukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria watendaji wote walioshiriki na wale wanaoendelea kushiriki kwa namna moja au nyingine kukwamisha maendeleo ya elimu nchini ikiwa ni pamoja na wale waliohusika katika udahili wa wanafunzi wasio na sifa katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Songea.

"Serikali ya awamu ya tano imedhamilia kwa dhati kabisa kuboresha kiwango cha elimu yetu kwa kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa elimu, naomba niwahakikishie kwamba pale panapohitajika kufanyika mabadiliko tutayafanya bila woga" Amesisitiza.

Amesema katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za elimu hapa nchini, serikali imejipanga kubadilisha mfumo wa elimu ambao umekuwa ukilalamikiwa kwa muda mrefu na kwamba mabadiliko hayo yatafanyika kwa kuwashirikisha wadau wote wa sekta hiyo.

" Tunapotaka kufanya mabadiliko kwenye mfumo wetu wa elimu tumekubali kwamba tuna changamoto,  katika changamoto hizi lazima tuwe na mahali pa kuanzia hivyo tunapochukua hatua tunaomba Watanzania mtuunge mkono"Amesisitiza Prof.Ndalichako.

Prof.Ndalichako Amesema lengo la Serikali kupitia Wizara yake ni kuhakikisha sekta ya elimu inaboreshwa hapa nchini kwa kuendelea kutoa wahitimu bora wanaokidhi vigezo na viwango katika soko la ajira.

Amesisitiza kuwa mkakati wa Serikali ni kuanza kuwafuatilia wahitimu wote wasio na viwango ambao wako katika maeneo mbalimbali ya ajira huku akisisitiza kwamba elimu ya Tanzania ni sawa na kiwanda kinahitaji malighafi nzuri ili kitoe bidhaa bora.

Ameeleza kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kuvikagua vyuo vyote vinavyotoa elimu ya juu kuona kama vinakidhi sifa na vigezo vya kiutendaji ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wale wote wanaowadanganya wananchi  na kuwapotezea muda vijana wanaowadahili bila kuzingatia sifa.

"Wizara yangu tunaendelea kufanya mawasiliano na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili tuchukue hatua kwa wote walioichezea sekta hii muhimu, tulichofanya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph kinaendelea kwa vyuo vingine"

Kuhusu ujenzi wa maabara amesema kuwa Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 12 kwa ajili ya kununulia vifaa vya maabara kwa shule zote 1536 ambazo zimekamilisha ujenzi wa majengo ya maabara kote nchini.

Katika hatua nyingine amesema kuwa Serikali katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 itafanya ukaguzi wa vyuo vyote vya Maendeleo ya Jamii kote nchini ili majengo ya vyuo hivyo yaweze  kutumika kuanzishia vyuo vya Ufundi Stadi VETA katika wilaya na mikoa ili kuwapatia stadi za kazi vijana waweze kujitegemea kwa kujiajiri wenyewe.

Kwa upande wao baadhi ya Wabunge waliopata nafasi ya kuchangia wakati wa Kupitisha Bajeti ya wizara hiyo wameiomba Serikali kuweka mkazo katika usimamizi wa Sekta ya Elimu nchini ili shule, Taasisi na vyuo vya Tanzania vitoe wahitimu wenye ubora kwa maslahi ya Taifa.

Aidha, wameiomba Serikali kupitia Bajeti hiyo itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kuimarisha shughuli za ukaguzi wa shule, kuboresha maslahi na kulipa madai ya walimu pamoja na kuziimarisha Mamlaka za Udhibiti wa Elimu ili ziweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Basi Jingine la Mwendo kasi Lapata ajali Eneo la Magomeni Usalama

$
0
0
Basi jingine la mwendo kasi limepata ajali mabaya eneo la Magomeni Usalama. Ni baada ya gari dogo kukatisha kwenye barabara ya magari ya mwendo kasi.

TANCDA YAPIMA AFYA ZA WABUNGE DODOMA

$
0
0
 Mbunge wa Viti Maalum, Bupe Mwakang'ata (CCM) Mkoa wa Rukwa, akipimwa mapigo ya moyo wakati wa programu maalumu ya wabunge kupimwa afya zao. Programu hiyo ilifanywa bure na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza katika Zahanati ya Bunge, Dodoma Mei 28, 2016.
 Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Leonidas Gama akipimwa afya na Muuguzi Asha Shao bungeni Dodoma
 Mbunge wa Viti Maalum, Joyce Sokombi akipimwa afaya na Muuguzi kutoka Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Asha Shao. Katikati ni muuguzi mwingine Christina Chamwela
 Mhudumu wa Afya wa Hospitali ya Dodoma akimpima kimo Mbunge
 Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Costantine Kanyasu akipimwa mapigo ya moyo
 Mbunge Kanyasu akipimwa kimo
 Mbunge wa Jimbo la Nachingwe, Hassan Masala akipimwa kimo
 Mbunge wa Jimbo la Makambaku, Deo Sanga akipimwa afya
Baadhi ya wabunge wakipata ushauri nasaha.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

MABINGWA MADRID WATUA NYUMBANI MADRID NA KUPATA BONGE YA MAPOKEZI

$
0
0


Mabingwa wa Uefa Champions League kwa mara ya 11, Real Madrid wamerejea kwao Hispania na kupokelewa kwa shangwe ile kinoma.

Madrid wamerejea katika jiji la Madrid saa chache baada ya kubeba ubingwa huo kwa mikwaju 5-3 ya penalti dhidi ya wapinzani wao wakubwa Atletico Madrid.

Mechi ya fainali ilichezwa katika jiji la Milan, kwenye Uwanja maarufu wa San Siro na mechi hiyo kutazamwa na zaidi ya watu milioni 200 duniani kote.






















Katibu Mkuu Mambo Ya Ndani Ya Nchi Afanya Ziara NIDA, Atoa Habari Njema Kwa Watumishi 597 Walioachishwa Kazi

$
0
0
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amesema fedha za kuwalipa watumishi 597 waliositishiwa mikataba yao katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) zipo na watalipwa hivi karibuni.

Rwegasira alisema kiasi cha shilingi bilioni 2.3 zimetengwa kwa ajili ya malipo ya Watumishi hao waliaochishwa kazi Machi 7, 2016 ambapo wanaidai Mamlaka mishahara ya miezi mitatu nyuma, malimbikizo ya fedha katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na makato ya fedha za Bima ya Afya.

Akuzungumza na watumishi wa Makao Makuu ya NIDA pamoja na Maafisa Wasajili wa Vitambulisho vya Taifa, jijini Dar es Salaam jana, Rwegasira aliwataka watumishi hao waliositishiwa mikataba yao, wasipotoshwe na mtu yeyote kuhusu kutokulipwa haki zao kwani wapo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha taratibu ndogo ndogo kabla ya kuanza kuwalipa.

“Naomba muwaambie waondoe wasiwasi wowote, waache maneno, watulie kwani Serikali ipo makini na fedha tunazo na tutaanza kuwalipa mara tumalizapo taratibu ndogo ndogo zilizobaki.” Alisema Rwegasira.

Aidha, Rwegasira aliwataka watumishi wa Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha ifikapo Desemba 31 mwaka huu Watanzania Milioni 23 wanatakiwa watambuliwe na kupata namba kabla ya kuanza kupewa Vitambulisho vya Taifa.

Hata hivyo, watumishi hao walimuakikishia Katibu Mkuu huyo, kuwa kazi hiyo ya utambuzi itakamilika kama ilivyopangwa na itafanyika kwa umakini mkubwa kama inavyotarajiwa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kuwatembelea na kuwatia hamasa katika kukamilisha kazi pamoja na kufikisha lengo lao la kukamilisha utambuzi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

“Tunakuahidi Katibu Mkuu kuwa tutatimiza lengo letu na tunakuakikishia tutafanya kazi kadiri ya uwezo wetu tukiongozwa na kauli mbiu ya ‘hapa kazi tu’", alisema Dk. Kipilimba.

Katibu Mkuu Rwegasira alifanya ziara hiyo kwa lengo la kujifunza zaidi shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka, hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji. 
Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Ansigar Chilemba akitoa maelezo jinsi taarifa za muombaji wa Kitambulisho cha Taifa zinavyohakikiwa, kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba. Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam jana.
Afisa Usajili Kitengo cha Ubora wa Kadi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Jemima Mulokozi (kushoto) akimuonyesha vitambulisho vilivyokamilika vikiwa na ubora unaohitajika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba. Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam jana.

Chura ya Snur yauzwa kama njugu, CD yake yazagaa kila kona, wajanja wavuna mamilioni!

$
0
0
 Majanga! Wimbo wa Chura wa msanii anayekuja juu kwa kasi, Snura Mushi licha ya kusitishwa matumizi yake kwa kupigwa marufuku kusikilizwa hadharani au kuonesha video yake, sasa wajanja wametoa CD yake na inauzwa mfano wa njugu mitaani, kwa Sh. 4,000, Wikienda limeinasa. Mei 4, mwaka huu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliifungia video ya wimbo huo kwa madai kwamba haiendani na maandili ya Kibongo huku Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) likimtaka msanii huyo kuurekebisha wimbo huo na yeye mwenyewe kujisajili kwenye baraza hilo ili aweze kutambuliwa.
 
WIKIENDA LATONYWA 
Wiki mbili zilizopita, baadhi ya wasomaji wa Wikienda walipiga simu chumba cha habari na kuuliza kama video ya Wimbo wa Chura imeruhusiwa kuuzwa au kuoneshwa madukani, kwani kumbukumbu zao, ulizuiwa na hakuna maamuzi ya kinyume na zuio hilo. Wikienda: “Ile video bado ipo ndani ya zuio, kwani vipi kaka?” “Sasa mbona CD (VCD) inauzwa mitaani, tena mbaya zaidi si mtaani tu hata kwenye baadhi ya maduka ya Kariakoo pia inauzwa,” alisema msomaji huyo aliyesema anaishi Kimara Suka, Dar. Siku tatu nyuma, msomaji mwingine alipiga simu na kusema makazi yake ni Mabatini jijini Mbeya naye alisema habari kama hizo, kwamba, Video ya Chura ameiona ikiuzwa kwa siri mitaani.

WIKIENDA LAFANYA UTAFITI

 Kufuatia taarifa hivyo, timu ya Wikienda ilizama mitaani na
madukani kujiridhisha na madai hayo mazito. Kweli, katika baadhi ya maduka ya kuuza tv Kariakoo, Wikienda lilishuhudia video hiyo ikioneshwa kwenye ‘flat screen’ kubwa huku baadhi ya wapiti njia wakiwa wamepiga kambi kuiangalia huku wakizozana juu ya wimbo wenyewe. Wapo waliotaka itolewe kwa kuwa ilishapigwa marufuku. Baadhi ya watu waliokuwa wakitoka kwenye duka moja Kariakoo walisikika wakilaani kuoneshwa kwa wimbo huo wakisema kuwa, kama ilipigwa marufuku hakukuwa na sababu ya msingi ya wauza CD hao kuionesha video hiyo kwani ni kukaidi agizo la serikali.

CD YAPATIKANA SINZA
 Wikienda liliendelea kufanya uchunguzi wake ambapo liliweza kuipata CD hiyo kwa muuzaji mmoja aliyekuwa akipitisha bidhaa zake nje ya Baa ya Way Side.

WIKIENDA NYUMBANI KWA SNURA 

Ili kumsikia Snura mwenyewe anasema nini kuhusu ishu hiyo, Wikienda lilifunga safari hadi nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar na kuzungumza naye kwa kina kuhusu kuwepo kwa biashara hiyo na kama kuna mkono wake. Kwanza, Snura alionekana kushangazwa sana na kitendo hicho ambapo alisema hakuwa anajua, lakini akaanika anachokijua yeye. “Mimi nilitii agizo la Basata na ndiyo maana hata kwenye YouTube niliifuta, ila wajanja waliiwahi kuichukua na kupiga pesa kupitia mgongo wangu.
“Watu wakikamatwa huko na polisi mimi simo, maana Chura nimeshamfungia ndani, sasa wao wanaendelea kumuhangaisha awape majanga, naomba nisiunganishwe maana sijui lolote. “Najua wengi walibani (kuchoma) CD hivyo wanapiga pesa kupitia kazi yangu na hao wanaoitana Chura waache mara moja maana nimesikia wengine wamekamatwa na polisi kwa kuitana Chura,” alisema Snura. 

KIONGOZI WA BASATA 
Kufuatia sekeseke hilo, juzi gazeti hili lilimtafuta Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mungereza ambaye simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. 

YALIYOTOKANA NA YATOKANAYO 
Kufuatia wimbo huo kuzua sintofahamu kutokana na wanenguaji wake wanavyocheza na maumbo yao, baadhi ya vijana wa kiume wakaanzisha utani wa kumwita mwanamke yeyote Chura jambo ambalo si la kiungwana hivyo, Mei 26, mwaka huu, Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala liliwataka wanawake kutoa taarifa vituo vya polisi wanapoitwa Chura na vijana pale wanapopita kwenye mitaa yao. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Lukas Mkondya alisema jijini Dar hivi karibuni kuwa, jeshi lake halijapokea malalamiko lakini kama kweli mambo hayo yapo basi aliwataka vijana kuacha mara moja tabia ya kuwaita wanawake Chura na wale watakaoitwa kutoa taarifa. Imeandaliwa: Hamida Hassan, Mayasa Mariwata na Gladness Mallya. 

CHANZO: GPL

Davina: Filamu za mapenzi wanazocheza wasanii wengi zimeua soko Bongo

$
0
0
 
MUIGIZA wa long time Bongo, Halima Yahya ‘Davina’ ameibuka na kueleza kwamba filamu za mapenzi wanazocheza wasanii
wengi zimeua soko ndiyo maana kwa sasa ni kama sanaa hiyo haipo. Akichonga na paparazi wetu hivi karibuni, Davina alisema
kutokana na soko la filamu kuwa gumu wasanii wengi wameamua kugeukia biashara kwani wakikaa na kusubiria sanaa
hiyo watakufa njaa. “Tunapigana ili tulirudishe soko la filamu liwe kama zamani maana limekufa kutokana na filamu za
mapenzi tunazocheza mara kwa mara. Kuna kila sababu ya kubadilika kama kweli tunataka kulishika soko,” alisema Davina.

Kanga Moja Kiunoni...Mbengembenge - 01

$
0
0
 
“Kwani lazima ...kwani lazima mama Mei uvae hivyo? Kwa nini usivae gauni au sketi? Basi si bora hata ungevaa ile suruali yako kubwakubwa...mara hii umesahau kwa nini tupo hapa hapa ee!” alisema kwa kufoka baba Mei huku akimwangalia mke wake kwa macho yenye hasira... “Baba Mei kwani tatizo liko wapi? Mbona unakuwa na wivu wa kijinga... mimi ndiye ninayeweza kujichunga mwenyewe, nikitaka kuharibu nitaharibu mwenyewe,” alisema mama Mei huku akitoka, mkononi alishika mfuko wenye chupa tupu za bia... “Basi afadhali juu ungevaa blauzi kubwa kuliko hicho kidude,” baba Mei aliongeza kushauri... “Baba Mei bwana... kwani wewe hulisikii hili joto la Dar?” mama Mei aliongeza akiwa ameshafika hatua zaidi ya tano kutoka nyumbani hapo. Baba Mei alitoka na kusimama nje akimwangalia mke wake anavyotembea kwenda dukani na jinsi alivyogoma kusikia ushauri wake... “Hivi mama Mei ni lini atajitambua lakini? Ina maana mpaka sasa hajajijua kwamba ana umbo tata! Hajui kama hapa ni mjini?” alisema moyoni akiwa amejishika kiuno. *** “Nilikwambia ndugu yangu Sudi, mimi mkali wa drafti
lakini sijui ni kwa nini hutaki kuamini wewe,” alisema Jombi huku mlio wa kete ukitawala. Wengine waliokuwa wakushuhudia mchezo huo ni Mfaransa na Jumbe. Ilikuwa Jumamosi kwa hiyo hakuna aliyekwenda kazini na muda huo walishakula na kufika kwenye kijiwe hicho ambacho kina michezo mingine kama pool na bao. Mara kikapita kimya kama vile waliamrishwa kutulia... “Jamani yule mwanamke vipi?” alihoji Mfaransa... “Yule kahamia juzi pale kwa mzee Hewa...ana mume na mtoto mmoja...nasikia mume wake anafanya kazi Halmashauri ya Jiji,” alisema Jombi. Sudi yeye alibaki ametoa macho tu... “Tena mume wake dakika kumi nyuma alipita hapa na gari dogo jeupe,” aliongeza Mfaransa. Mama Mei alikuwa kama kituko, kwani mchana huo wa jua kali, yeye alivaa kanga kwa kuizungushia kiunoni, juu alivaa kitop ambacho kwa chini kilikuwa hakifiki usawa wa alipopitisha kanga. Hilo moja, pili, maumbile yake ya nyuma, yaani wowowo ni kama alikuwa anatumia dawa za Mchina ingawa ukweli ni kwamba, hakuwa mtumiaji wa dawa hizo zaidi ya Mungu kumjalia tu. Kama angepita mbele yako
akitokea upande mmoja kwenda mwingine, ungeweza kusema anataka kuinama ili aokote kitu kwa jinsi alivyokuwa amefungashia. Watu walikuwa wakisema umri wake wa miaka 31 na umbo lake ni vitu viwili tofauti. Kifuani alibanwa sana na kumfanya aonekane mwembamba. Mama Mei alijijua kuwa ana macho ya gololi hivyo alipomwangalia mtu yakiwa kama yanataka kusinzia kama siyo kulala, yalimzidishia urembo. Wakati anachumbiwa na baba Mei, karibia wanaume wengine wanne walikuwa wakimfukuzia, wawili walitaka kumuoa kabisa, wawili walitaka kupita tu ili kuchezea lakini msimamo wake ulibaki kwa baba Mei au Kitwana. Mara zote anapokwenda mahali akiwa amevaa suruali au sketi za kimini, watu huachana na shughuli zao kwa muda ili kumfaidi anavyopita mpaka kupotea. Hali hiyo imekuwa ikimfanya mumewe kupata gharama bila sababu kwani anaposema anakwenda mahali, au ampe pesa ya Bajaj au ya teksi kama hatampeleka yeye, lengo
likiwa kumkimbiza na macho ya watu. *** “Jamani! Jamani! Sasa kwa nini avae kanga vile wakati anajijua ana mzigo mkubwa?” alihoji Sudi sasa... “Ha! Yale ni maamuzi yao ndani ya familia bwana. Mtu umeambiwa ana mume na ametoka nyumbani halafu wewe unashauri asingevaa vile, sasa angevaaje kwa mfano?” alisema Mfaransa. “Angejistahi bwana...ona sasa... oneni wenyewe,” alisema Jumbe huku akimfuatilia mama Mei anavyotembea na kulitingisha wowowo lake. Vicheko vya kike kutoka kwenye baadhi ya nyumba za jirani vilisikika lakini ni hakika kwamba, waliokuwa wakicheka wote walikuwa wakimwangalia mama Mei kwa kupitia madirisha au milango. *** Siku iliyofuata ni Jumapili, Jombi aliamua kupita nje ya nyumba ya mzee Hewa ili kuona kama angeweza kumwona mama Mei... “Shikamoo mzee Hewa,” alisalimia Jombi...
“Marhaba Jombi, za siku nyingi bwana?” “Nzuri, upo mzee wangu?” alijibu Jombi huku akikaa kwenye kiti hapo nje... “Nipo bwana, karibu sana,” mzee Hewa alimkaribisha Jombi ambaye naye alikaa huku macho yakiwa mlango mkubwa wa kuingilia ndani. Ni muda huohuo, mama Mei alitoka akiwa ameshika mfuko wa rambo wenye uchafu kwenda kutupa kwenye pipa pembeni ya nyumba. Siku hiyo pia alipiga kanga moja  tena nyepesi huku ndani akionekana kusindikizwa na skintaiti. Juu alivaa kiblauzi cha njano, kata mikono... “Habari yaka anko?” alimsalimia Jombi huku akipita karibu yake na kulitingisha wowowo kisawasawa kabisa... “Nzu...nzu...nzuri sista... mi...wewe vi...” alibabaika kujibu salamu Jombi. Mzee Hewa alimkazia macho mama Mei mpaka anavyotupa ule mfuko na kusema kwa sauti ya chini akimwambia Jombi...

Kanga Moja Kiunoni...Mbengembenge - 2

$
0
0




ILIPOISHIA “Nzu...nzu...nzuri sista...mi... wewe vi...” alibabaika kujibu salamu Jombi. Mzee Hewa alimkazia macho mama Mei mpaka anavyotupa ule mfuko na kusema kwa sauti ya chini akimwambia Jombi... SASA SHUKA NAYO MWENYEWE... “YAANI Jombi mwanangu sijawahi kupata majaribu kwenye nyumba hii kama mwaka huu...” “Kwa nini mzee Hewa?” Jombi aliuliza kwa sauti ya chini sana ili mama Mei asisikie kwani sasa alikuwa akirudi ndani. Na hata alipokuwa akirudi, vibastola vilitokeza kwa pembeni na kumfanya aonekane namna alivyojazia hata kwa mbele... “Loo! Kumbe si kwa nyuma tu, hata front,” Jombi alijisemea moyoni huku akimwangalia mwanamke huyo kwa jicho la wizi, akazama ndani... “We Jombi unavyoona unaweza kuishi na mwanamke wa hivi kwenye nyumba moja?” mzee Hewa aliuliza... “Kazi sana mzee Hewa...mimi hata kuishi nyumba jirani siwezi achilia kuishi naye nyumba
moja,” alisema Jombi akikiri uzuri wa mwanamke huyo. Baada ya dakika kama tano, baba Mei alitoka akionekana ana kasafari... “Wapi bwana?” mzee Hewa alimuuliza baada ya kumwona mkononi ameshika funguo za gari... “Nafika mjini mara moja... huyu nani mzee wangu?” aliuza baba Mei akitaka kumjua Jombi... “Huyu kijana wangu... anaishi mtaa wa pili kule... sasa amepita hapa akaona anisalimie kidogo mzee wake,” alijibu mzee Hewa... “Ahaa! Oke...halafu anaondoka zake?” baba Mei alitaka kujua zaidi... “Anaondoka...kwani vipi?” “Nimeuliza tu mzee wangu...” “Ataondoka...ataondoka.” Baba Mei alirudi kwanza ndani kisha baada ya kama dakika tano akatoka huku akisikika akisema... “Ole...ndiyo utanitambua mimi nani?!” Baada ya baba Mei kuondoka, mzee Hewa na Jombi walijadili lile swali... “Huyu bwana inaonekana amekutilia wasiwasi...maana kijana kama wewe kuja hapa
na mke mwenyewe kama huyu ni tatizo,” alisema mzee Hewa... “Hata mimi nimemshangaa hivyohivyo mzee Hewa kwani asingeweza kusema maneno yale mbele yangu huku nasikia...afadhali angekuuliza nikiwa sipo,” alisema Jombi huku moyoni yeye akiijua dhamira iliyompeleka pale... “Jana nilisoma gazeti moja linasema hizi nyumba zetu hapa zitabomolewa, we unazo habari hizi?” mzee Hewa alikata maongezi ya awali na kumuuliza Jombi hivyo... “Hapana mzee Hewa, ni kweli?” “Ngoja nikalilete na wewe upitie habari hizo,” alisema mzee Hewa huku akisimama kwenda ndani akiimba nyimbo za dini kama ilivyo kawaida yake. Mara, mama Mei alitoka. Safari hii alikuwa amejifunga kitenge, mkononi alishika kipochi kidogo, ilionekana alikuwa akienda dukani au gengeni. Licha ya kuvaa kitenge ambacho kilikaribia kuburuza chini lakini mzigo ulionekana kama kawa... “Anti naona unafuata bidhaa dukani sasa!” alisema Jombi. Mama Mei alimwangalia
kwa jicho la uchokozi kisha akasema... “Ni kweli lakini leo jua kali kama nini Mungu wangu, sijui niende na mwamvuli...” “Hata mimi nashauri hivyo maana...au nitume mimi.” Mama Mei alicheka huku akimkazia macho Jombi... “Yaani nikutume wewe anko si itakuwa dharau kubwa... nakwenda pale buchani na kwenye lile soko la pale kona...” “Nitume tu anti,” Jombi aling’ang’ania kutumwa. “Kweli?” mama Mei alitaka kujua ya moyoni... “Kweli kabisa anti,” alisema Jombi huku akisimama tayari kwa kutumwa... “Basi asante, nataka nyama kilo tano maana huwa naiweka kwenye friji kwa wiki nzima. Halafu nataka kabeji tatu... nazi sita...viazi mviringo kisado na mchele kilo tano,” alisema mama Mei... “Mh!” Jombi aliguna  moyoni baada ya kupata picha ya ukubwa wa mzigo atakaobeba. *** Jombi, licha ya kufanya kazi serikalini tena ya maana, pia ni mume wa mtu, bidhaa alizojituma kununua na maeneo zinakopatikana na nyumbani kwake ni jirani tu,
hivyo alikwenda kwa mahesabu sana. Alipokuwa kwenye soko alikumbana na maneno haya... “Baba Hawa leo umekuja mwenyewe? Mama vipi..?” “Leo baba Hawa nakuona umeamua kufuatilia mahesabu mwenyewe.” Mpaka mwisho anaondoka akiwa amebeba mfuko mkubwa kabisa, hivyo aliamua kuchukua Bajaj japokuwa alikokuwa anakwenda si mbali sana. *** Mzee Hewa alishangaa kukuta Jombi hayupo nje alikomwacha... “Kha! Huyu bwana vipi tena?” alijiuliza bila kupata majibu kwani hakumkuta mama Mei, aliingia ndani akijua anko huyo akirudi na mizigo atamwita. *** “Baba Hawa hiyo mizigo unaipeleka wapi mume wangu? Sikuelewi,” sauti ya mkewe, mama Hawa ilimshtua kwa nyuma akiwa anapanda Bajaj...
Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma  Ijumaa ijayo.

Lulu Diva amgeukia Belle 9 Baada ya Nay kuchepuka...

$
0
0
 
SIYO siri tena! Baada ya mkali wa Muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuchepuka kwa msichana wa Kihabeshi mwenye asili ya Ethiopia, aliyekuwa mpenzi wake Lulu Abass ‘Lulu Diva’ naye ameamua kugeukia kwa staa wa muziki, Abedinego Damian ‘Belle 9’. Akizungumza na Over Ze Weekend Lulu ambaye ni muuza nyago kwenye video za Kibongo alidai kuwa, Nay hajatulia na badala yake anahitaji kuwa na mtu asiye na skendo za kutembea na wanawake ovyo na Belle 9 ndiye tulizo lake. “Ni ukweli Nay nilikuwa naye kwenye uhusiano nikifahamu alishawahi kuwa na msururu wa wanawake lakini siyo siri yamenishinda na sasa nahitaji kujiweka kando. Sasa hivi feelings zangu zote zipo kwa Belle na analijua hilo,” alisema Lulu

Prezzo amfuata Gigy Bongo!

$
0
0
 IMEVUJA! Kumbe rapa mwenye jina kubwa Afrika Mashariki, Jackson Makini ‘Prezzo’moja ya ishu zilizomleta Bongo ni pamoja na kukutana na muuza nyago kwenye Video za Kibongo, Gift Stanford  ‘Gigy Money’. 

Akichonga na Over Ze Weekend Prezzo aliyewahi kubamba na Ngoma ya Nipe Nikupe akimshirikisha staa wa Bongo Fleva, Ambwene Yessaya ‘AY’ alisema kuwa, Gigy ni
msichana ambaye amekuwa akimsikia siku za hivi karibuni Wakenya wakimzungumzia hasa juu ya vituko vyake jambo lililomfanya kuvutiwa kuonana naye.


 “Gigy yuko hot mazee, nimemsikia sana Wakenya wakimzungumzia so nipo katika mpango wa kuonana naye, si unajua mimi nina mambo mengi, reality show na vitu vingine private,” alisema Prezzo. Gigy Money aliponyetishiwa ishu hiyo na Over Ze Weekend alifurahia jina lake kupaa hadi Kenya.

 Muuza nyago kwenye Video za Kibongo, Gift Stanford  ‘Gigy Money’.




 

Shilole na Vanessa walipokutana kwenye Stage Usiku wa May 29 2016 Club Billcanas

$
0
0
Huenda wewe ulikuwa ni moja kati ya watu waliokuwa wameshtushwa na taarifazilizokuwa zimeenea wiki mbili zilizopita kuwa Vanessa Mdee na Shilolewana bifu, ukweli umejulikana usiku wa May 29 2016, kuwa haikuwa bifu bali ni promo ya show yao ya pamoja waliofanya usiku huo.
3X6A9861
Dakika chache kabla ya Show Vanessa Mdee akiwa backstage alinukuliwa akisema“Kiukweli haukuwa ugomvi bali tulijaribu kuwaonesha watu kuwa usiamini kila unachokiona kwenye mitandao, namuheshimu sana Shilole katika kazi zake, lakini baada ya sisi kufanya vile watu walionekana kama wanataka kuona sisi tukigombana”
3X6A9862
3X6A9876
3X6A9878
3X6A9879
3X6A9893
3X6A9894
3X6A9897
3X6A9898
3X6A9906
Vanessa alimsurprise Shilole On Stage kwa kumletea zawadi ya ugali kwenye stage
3X6A9914
3X6A9915
3X6A9919
Viewing all 12768 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>